Categories
Zekaria

Zekaria 12

Maadui Wa Yerusalemu Kuangamizwa

1 Hili ni neno laBwanakuhusu Israeli.Bwana, yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema:

2 “Nitakwenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbisha mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia.

3 Katika siku hiyo, wakati mataifa yote ya dunia yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya Yerusalemu kuwa jabali lisilosogezwa kwa mataifa yote. Wote watakaojaribu kulisogeza watajiumiza wenyewe.

4 Katika siku hiyo nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye ampandaye nitampiga kwa uwazimu,” asemaBwana. “Nitalielekeza jicho langu la ulinzi juu ya nyumba ya Yuda, nami nitawapofusha farasi wote wa mataifa.

5 Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababuBwanaMwenye Nguvu Zote ni Mungu wao.’

6 “Katika siku hiyo nitawafanya viongozi wa Yuda kuwa kama kigae cha moto ndani ya lundo la kuni, kama mwenge uwakao kati ya miganda. Watateketeza kulia na kushoto mataifa yote yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki salama mahali pake.

7 “Bwanaatayaokoa makao ya Yuda kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa zaidi kuliko ile ya Yuda.

8 Katika siku hiyo,Bwanaatawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika waBwanaakiwatangulia.

9 Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu.

Kumwombolezea Yule Aliyechomwa Mkuki

10 “Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neemana maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.

11 Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido.

12 Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi na wake zao, ukoo wa nyumba ya Nathani na wake zao,

13 ukoo wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao,

14 na koo zote zilizobaki na wake zao.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/12-45113d9771af5d9b045bd9d1bcff06e4.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 13

Kutakaswa Dhambi

1 “Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi.

2 “Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi.

3 Ikiwa yupo yeyote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina laBwana.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo.

4 “Katika siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la kinabii la nywele ili apate kudanganya watu.

5 Atasema, ‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima; ardhi imekuwa kazi yangu tangu ujana wangu.’

6 Ikiwa mtu atamuuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni majeraha niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu.’

Mchungaji Apigwa, Nao Kondoo Watawanyika

7 “Amka, ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu,

dhidi ya mtu aliye karibu nami!”

asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

“Mpige mchungaji,

nao kondoo watatawanyika,

nami nitageuza mkono wangu

dhidi ya walio wadogo,

8 katika nchi yote,” asemaBwana,

“theluthi mbili watapigwa na kuangamia;

hata hivyo theluthi moja watabaki ndani yake.

9 Hii theluthi moja nitaileta katika moto;

nitawasafisha kama fedha isafishwavyo

na kuwajaribu kama dhahabu.

Wataliitia Jina langu

nami nitawajibu;

nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’

nao watasema, ‘Bwanani Mungu wetu.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/13-e23899078fb1e45117b740bf03ba066c.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 14

Bwana Yuaja Kutawala

1 Siku yaBwanainakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu.

2 Nitayakusanya mataifa yote huko Yerusalemu kupigana dhidi yake, mji utatekwa, nyumba zitavamiwa na kuporwa na wanawake watanajisiwa. Nusu ya mji watakwenda uhamishoni, lakini watakaobaki hawataondolewa kutoka mjini.

3 KishaBwanaatatoka na kupigana dhidi ya watu wa yale mataifa, kama apiganavyo siku ya vita.

4 Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini.

5 Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. KishaBwanaMungu wangu atakuja na watakatifu wote pamoja naye.

6 Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji.

7 Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo naBwana. Jioni inapofika nuru itakuwepo.

8 Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki,na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibiwakati wa kiangazi na wakati wa masika.

9 Bwanaatakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepoBwanammoja na jina lake litakuwa jina pekee.

10 Nchi yote kuanzia Geba, kaskazini mwa Yuda, hadi Rimoni, kusini mwa Yerusalemu, itakuwa kama Araba.Lakini Yerusalemu utainuliwa juu na kubaki mahali pake, toka Lango la Benyamini hadi mahali pa Lango la Kwanza, mpaka kwenye Lango la Pembeni na kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye mashinikizo ya divai ya mfalme.

11 Utakaliwa na watu, kamwe hautaharibiwa tena, Yerusalemu utakaa salama.

12 Hii ndiyo tauni ambayoBwanaatapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao.

13 Katika siku hiyoBwanaatawatia wanaume hofu kuu. Kila mwanaume atakamata mkono wa mwenzake nao watashambuliana.

14 Yuda pia atapigana katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka Yerusalemu utakusanywa, wingi wa dhahabu, fedha na nguo.

15 Tauni ya aina iyo hiyo itapiga farasi na nyumbu, ngamia na punda, nao wanyama wote walioko kwenye kambi za adui.

16 Kisha walionusurika katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme,BwanaMwenye Nguvu Zote na kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.

17 Ikiwa taifa lolote la dunia hawatakwenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme,BwanaMwenye Nguvu Zote, mvua haitanyesha kwao.

18 Ikiwa watu wa Misri nao hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua.Bwanaataleta juu yao tauni ile ambayo itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.

19 Hii itakuwa adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale ambayo hayatakwenda Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.

20 Katika siku hiyo, kengele zilizofungwa kwenye farasi zitaandikwa maneno haya:Takatifu kwa Bwana, navyo vyungu vya kupikia katika nyumba yaBwanavitakuwa kama bakuli takatifu mbele ya madhabahu.

21 Kila chungu kilichoko Yerusalemu na Yuda kitakuwa kitakatifu kwaBwanaMwenye Nguvu Zote na wote wanaokuja kutoa dhabihu watachukua baadhi ya vyungu hivyo na kupikia. Katika siku hiyo hatakuwepo tena mfanyabiashara katika nyumba yaBwanaMwenye Nguvu Zote.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/14-698a795a95f1f16342cf6326c69ea23d.mp3?version_id=1627—

Categories
Malaki

Malaki Utangulizi

Utangulizi

Malaki maana yake ni “Mjumbe Wangu” au “Mjumbe wa

Bwana

.” Malaki aliishi baada ya ujenzi wa Hekalu la pili kumalizika. Maisha ya uchaji wa Mungu ya Wayahudi yalikuwa mabaya. Walikuwa wamekengeuka, wakawaoa wanawake wa mataifa mengine, wakaacha kutoa zaka na dhabihu ambayo ni sehemu ya Mungu, hata wakawa wamemwacha Mungu, hali ambayo ilifanana sana na ile iliyokuwepo wakati wa Nehemia.

Mwandishi

Malaki.

Kusudi

Kuwahimiza watu wafanye mabadiliko thabiti ya kimsingi katika maisha yao kwa kuziacha dhambi zao ili kurejeza uhusiano wao na Mungu na kuwakumbusha upendo wa Mungu.

Mahali

Yerusalemu na Hekaluni.

Tarehe

Kama 430 K.K.

Wahusika Wakuu

Malaki, makuhani, na watu wa Yuda.

Wazo Kuu

Mungu anawapenda watu wake hata wakati wanapomwacha na kutomtii. Ana baraka nyingi anazowapa wale walio waaminifu kwake. Upendo wake hauna mwisho.

Mambo Muhimu

Kitabu hiki kinaonyesha kuwa Hekalu lilijengwa tena, na dhabihu na sikukuu zikarudishwa. Ufahamu wa jumla wa Sheria ulirudishwa tena na Ezra, na kurudi kwao nyuma kimaadili kulikofuatia kulitokea zaidi miongoni mwa makuhani.

Mgawanyo

Upendo wa Mungu kwa Israeli (

1:1-5

)

Israeli wamtukana Mungu (

1:6–2:16

)

Hukumu ya Mungu na ahadi yake (

2:17–4:6

).

Categories
Malaki

Malaki 1

1 Ujumbe: Neno laBwanakwa Israeli kupitia kwa Malaki.

Yakobo Alipendwa, Esau Alichukiwa

2 Bwanaasema, “Nimewapenda ninyi.”

“Lakini ninyi mnauliza, ‘Wewe umetupendaje?’ ”

Bwanaasema, “Je, Esau hakuwa ndugu yake Yakobo? Hata hivyo nimempenda Yakobo,

3 lakini nikamchukia Esau, nami nimeifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa jangwani.”

4 Edomu anaweza kusema, “Ingawa tumepondapondwa, tutajenga upya magofu.”

Lakini hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo: “Wanaweza kujenga, lakini nitabomoa. Wataitwa Nchi Ovu, watu ambao siku zote wapo chini ya ghadhabu yaBwana.

5 Mtayaona kwa macho yenu wenyewe na kusema, ‘Bwanani mkuu, hata nje ya mipaka ya Israeli!’

Dhabihu Zilizo Na Mawaa

6 “Mwana humheshimu baba yake, naye mtumishi humheshimu bwana wake. Kama mimi ni baba, iko wapi heshima ninayostahili? Kama mimi ni bwana, iko wapi heshima ninayostahili?” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Ni ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau Jina langu.

“Lakini mnauliza, ‘Tumelidharau Jina lako kwa namna gani?’

7 “Mnatoa sadaka chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu.

“Lakini ninyi mnauliza, ‘Tumekutia unajisi kwa namna gani?’

“Kwa kusema kuwa meza yaBwanani ya kudharauliwa.

8 Wakati mletapo dhabihu za wanyama walio vipofu, je, hilo si kosa? Mnapoleta dhabihu zilizo vilema au wanyama wagonjwa, je, hilo si kosa? Jaribuni kuvitoa kwa mtawala wenu! Je, angefurahishwa nanyi? Je, atawakubalia?” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

9 “Basi mwombeni Mungu awe na neema kwetu. Je, kwa sadaka kama hizo kutoka mikononi mwenu, atawapokea?” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

10 “Laiti mmoja wenu angalifunga milango ya Hekalu, ili msije mkawasha moto usiokuwa na faida juu ya madhabahu yangu! Sina furaha nanyi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, “nami sitaikubali sadaka toka mikononi mwenu.

11 Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa, kuanzia mawio ya jua hata machweo yake. Kila mahali uvumba na sadaka safi zitaletwa kwa Jina langu, kwa sababu Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

12 “Lakini mnalinajisi Jina langu kwa kusema kuhusu meza ya Bwana, ‘Imetiwa unajisi pamoja na chakula chake. Ni ya kudharauliwa.’

13 Nanyi mnasema, ‘Mzigo gani huu!’ Nanyi mnaidharau kwa kiburi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

“Wakati mnapowaleta wanyama mliopokonya kwa nguvu, walio vilema au walio wagonjwa na kuwatoa kama dhabihu, je, niwakubali kutoka mikononi mwenu?” asemaBwana.

14 “Amelaaniwa yeye adanganyaye, aliye na mnyama wa kiume anayekubalika katika kundi lake na kuweka nadhiri ya kumtoa, lakini akatoa dhabihu ya mnyama aliye na dosari kwaBwana. Kwa kuwa mimi ni Mfalme Mkuu, nalo Jina langu linapaswa kuogopwa miongoni mwa mataifa,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/MAL/1-2d81f459cdbe68056fa3c5106d0e3452.mp3?version_id=1627—

Categories
Malaki

Malaki 2

Onyo Kwa Makuhani

1 “Sasa onyo hili ni kwa ajili yenu, enyi makuhani.

2 Kama hamtasikiliza, na kama hamtaki kuielekeza mioyo yenu kuheshimu Jina langu, nitatuma laana juu yenu, nami nitalaani baraka zenu. Naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamkuielekeza mioyo yenu kuniheshimu mimi,” AsemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

3 “Kwa sababu yenu nitawakatilia mbali wazao wenu. Nitazipaka nyuso zenu mavi, mavi ya dhabihu zenu. Nanyi mtafukuzwa pamoja nazo mtoke mbele zangu.

4 Nanyi mtajua kuwa nimewapelekea onyo hili ili kwamba Agano langu na Lawi lipate kuendelea,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

5 “Agano langu lilikuwa pamoja naye, agano la uhai na amani, nami nilimpa yote, ili aniche na kuniheshimu, naye akaniheshimu na kusimama akilicha Jina langu.

6 Fundisho la kweli lilikuwa kinywani mwake, wala hakuna uongo wowote uliopatikana katika midomo yake. Alitembea nami katika amani na unyofu, naye akawageuza wengi kutoka dhambini.

7 “Kwa maana yapasa midomo ya kuhani kuhifadhi maarifa. Tena kutoka kinywani mwake watu wangepaswa kutafuta mafundisho, kwa sababu yeye ni mjumbe waBwanaMwenye Nguvu Zote.

8 Lakini mmegeuka mkaiacha njia, na kwa mafundisho yenu mmesababisha wengi kujikwaa. Mmevunja agano na Lawi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

9 “Kwa hiyo nimewasababisha ninyi kudharauliwa na kufedheheshwa mbele ya watu wote, kwa sababu hamkufuata njia zangu, bali mmeonyesha upendeleo katika mambo ya sheria.”

Yuda Si Mwaminifu

10 Je, sote hatuna Baba mmoja? Hatukuumbwa na Mungu mmoja? Kwa nini basi tunalinajisi Agano la baba zetu kwa kukosa uaminifu kila mmoja kwa mwenzake?

11 Yuda amevunja uaminifu. Jambo la kuchukiza limetendeka katika Israeli na katika Yerusalemu: Yuda amepanajisi mahali patakatifu apendapoBwana, kwa kuoa binti wa mungu mgeni.

12 Kwa maana kwa mtu yeyote atendaye jambo hili,Bwanana amkatilie mbali kutoka hema za Yakobo, hata kama huwa anamleteaBwanaMwenye Nguvu Zote sadaka.

13 Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu yaBwanakwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu.

14 Mnauliza, “Kwa nini?” Ni kwa sababuBwanani shahidi kati yako na mke wa ujana wako, kwa sababu umevunja uaminifu naye, ingawa yeye ni mwenzako, mke wa agano lako la ndoa.

15 Je,Bwanahakuwafanya wao kuwa mmoja? Katika mwili na katika roho wao ni wa Mungu. Kwa nini wawe mmoja? Kwa sababu Mungu alikuwa akitafuta mzao mwenye kumcha Mungu. Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, mtu asivunje uaminifu kwa mke wa ujana wake.

16 “Ninachukia kuachana,” asemaBwana, Mungu wa Israeli, “pia nachukia mtu anayejivika jeuri kama vazi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, wala msije mkavunja uaminifu.

Siku Ya Hukumu

17 MmemchoshaBwanakwa maneno yenu.

Nanyi mnauliza, “Tumemchosha kwa namna gani?”

Mmemchosha kwa kusema, “Wote watendao mabaya ni wema machoni paBwana, naye anapendezwa nao” au “Mungu wa haki yuko wapi?”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/MAL/2-c418f954b47c68ff590265794d4cdda5.mp3?version_id=1627—

Categories
Malaki

Malaki 3

1 “Angalieni, nitamtuma mjumbe wangu, atakayeiandaa njia mbele yangu. Ndipo ghafula Bwana mnayemtafuta atakuja hekaluni mwake. Mjumbe wa Agano, ambaye mnamwonea shauku, atakuja,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

2 Lakini ni nani atakayeweza kustahimili hiyo siku ya kuja kwake? Ni nani awezaye kusimama atakapotokea? Kwa kuwa atakuwa kama moto wa mfua fedha au kama sabuni ya afuaye nguo.

3 Ataketi kama mfuaji na asafishaye fedha. Atawatakasa Walawi, naye atawasafisha kama dhahabu na fedha. KishaBwanaatakuwa na watu watakaoleta sadaka katika haki,

4 nazo sadaka za Yuda na Yerusalemu zitakubalika kwaBwana, kama katika siku zilizopita, kama katika miaka ya zamani.

5 “Basi nitakuja karibu nanyi ili kuhukumu. Nami nitakuwa mwepesi kushuhudia dhidi ya wachawi, wazinzi, waapao kwa uongo, wanaopunja vibarua malipo yao, wanaowaonea wajane na yatima, na wanaowanyima wageni haki, lakini hawaniogopi mimi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

Kumwibia Mungu

6 “MimiBwanasibadiliki. Kwa hiyo ninyi, enyi uzao wa Yakobo, hamjaangamizwa.

7 Tangu wakati wa baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu nanyi hamkuzishika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

“Lakini mnauliza, ‘Tutarudi kwa namna gani?’

8 “Je, mwanadamu atamwibia Mungu? Hata hivyo mnaniibia mimi.

“Lakini mnauliza, ‘Tunakuibia kwa namna gani?’

“Mnaniibia zaka na dhabihu.

9 Mko chini ya laana, ninyi taifa lote, kwa sababu mnaniibia mimi.

10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kuwe na chakula katika nyumba yangu. Nijaribuni katika hili,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, “nanyi mwone kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka nyingi mpaka mkose nafasi ya kutosha.

11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu, wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

12 “Ndipo mataifa yote yatawaita mliobarikiwa, kwa maana nchi yenu itakuwa ya kupendeza sana,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

13 “Mmesema vitu vigumu dhidi yangu,” asemaBwana.

“Hata hivyo mnauliza, ‘Tumesema nini dhidi yako?’

14 “Mmesema, ‘Ni bure kumtumikia Mungu. Tumepata faida gani kwa kushika maagizo yake na kwenda kama waombolezaji mbele zaBwanaMwenye Nguvu Zote?

15 Lakini sasa wenye kiburi wanabarikiwa. Hakika watenda mabaya wanastawi, pia hata wale wanaoshindana na Mungu ndio wanaosalimika.’ ”

16 Ndipo wale waliomchaBwanawakasemezana wao kwa wao, nayeBwanaakasikiliza na akasikia. Kitabu cha kumbukumbu kikaandikwa mbele yake kuhusu wale ambao walimchaBwanana kuliheshimu jina lake.

17 “Nao watakuwa watu wangu,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, “katika siku ile nitakapowafanya watu kuwa hazina yangu. Nitawahurumia, kama vile kwa huruma mtu amhurumiavyo mwanawe anayemtumikia.

18 Kwa mara nyingine tena utaona tofauti kati ya wenye haki na waovu, kati ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/MAL/3-e12e85093aad32613aefd604cc373f9f.mp3?version_id=1627—

Categories
Malaki

Malaki 4

Siku Ya Bwana

1 “Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu, na siku ile inayokuja itawawasha moto,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao.

2 Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini.

3 Kisha ninyi mtawakanyaga waovu, nao watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu siku ile nitakayofanya mambo haya,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

4 “Kumbukeni sheria ya mtumishi wangu Mose, amri na sheria nilizompa huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote.

5 “Tazama, nitawapelekea nabii Eliya kabla ya kuja siku ile iliyo kuu na ya kutisha yaBwana.

6 Ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, la sivyo nitakuja na kuipiga nchi kwa laana.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/MAL/4-5240a62128de639eb6ba1d9251f8fc90.mp3?version_id=1627—

Categories
Mathayo

Mathayo Utangulizi

Utangulizi

Mathayo alikuwa mtoza ushuru ambaye Bwana Yesu alimwita awe mwanafunzi wake hapo mwanzoni mwa huduma yake ya hadharani. Mathayo alianza Injili yake kwa kueleza kwa kirefu kuhusu Yesu alivyozaliwa na bikira Maria, alivyobatizwa, na kujaribiwa nyikani. Yesu alikuja akihubiri kuhusu Ufalme wa Mungu, ambao ni wa kila mtu anayetaka kupata uzima wa milele. Mtu anaingia katika Ufalme huu kwa kutubu dhambi na kumwamini Yesu. Mathayo aliyagawa mafundisho ya Yesu katika sehemu kuu tano: Maadili, Kueneza Habari Njema, Mifano, Ushirika, na Kuja kwa Ufalme wa Mungu. Sehemu ya Mwisho ya Injili ya Mathayo inaeleza juu ya kufa na kufufuka kwa Yesu, na agizo alilolitoa kwa wote wanaomwamini kueneza Habari Njema ulimwenguni kote.

Mwandishi

Mathayo aitwaye Lawi.

Kusudi

Kumtambulisha Yesu kwa Wayahudi kuwa ndiye Masiya, na pia Mfalme wa milele.

Mahali

Palestina.

Tarehe

Kati ya 60-65 B.K.

Wahusika Wakuu

Yesu na wanafunzi wake, Maria, Yohana Mbatizaji na wanafunzi wake, viongozi wa dini ya Kiyahudi, na Pilato.

Wazo Kuu

Kudhibitisha kwamba Bwana Yesu alikamilisha ahadi ambazo Mungu alitoa katika Agano la Kale.

Mambo Muhimu

Kitabu hiki kinaelezea matukio manne ya utoto wa Yesu. Pia kinapeana mifano kumi aliyoitoa Yesu, na miujiza miwili aliyoifanya. Ina midahalo tisa ambayo Yesu alihojiana na baadhi ya watu. Kinamalizia na hisia sita zilizoandamana na kusulubiwa kwake, na maagizo kwa wanafunzi wake kueneza Habari Njema duniani kote.

Mgawanyo

Maisha na huduma ya Bwana Yesu (

1:1–4:25

)

Mahubiri ya Mlimani (

5:1–7:29

)

Mafundisho ya mifano na mazungumzo (

8:1–18:35

)

Safari ya kwenda Yerusalemu, na maonyo ya mwisho (

19:1–23:39

)

Unabii kuhusu mambo yajayo (

24:1–25:46

)

Kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu (

26:1–28:20

).

Categories
Mathayo

Mathayo 1

Kumbukumbu Za Ukoo Wa Yesu Kristo

1 Habari za ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu:

2 Abrahamu akamzaa Isaki,

Isaki akamzaa Yakobo,

Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake,

3 Yuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari,

Peresi akamzaa Hesroni,

Hesroni akamzaa Aramu,

4 Aramu akamzaa Aminadabu,

Aminadabu akamzaa Nashoni,

Nashoni akamzaa Salmoni,

5 Salmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu,

Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu,

Obedi akamzaa Yese,

6 Yese akamzaa Daudi ambaye alikuwa mfalme.

Daudi akamzaa Solomoni, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.

7 Solomoni akamzaa Rehoboamu,

Rehoboamu akamzaa Abiya,

Abiya akamzaa Asa,

8 Asa akamzaa Yehoshafati,

Yehoshafati akamzaa Yoramu,

Yoramu akamzaa Uzia,

9 Uzia akamzaa Yothamu,

Yothamu akamzaa Ahazi,

Ahazi akamzaa Hezekia,

10 Hezekia akamzaa Manase,

Manase akamzaa Amoni,

Amoni akamzaa Yosia,

11 wakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.

12 Baada ya uhamisho wa Babeli:

Yekonia alimzaa Shealtieli,

Shealtieli akamzaa Zerubabeli,

13 Zerubabeli akamzaa Abiudi,

Abiudi akamzaa Eliakimu,

Eliakimu akamzaa Azori,

14 Azori akamzaa Sadoki,

Sadoki akamzaa Akimu,

Akimu akamzaa Eliudi,

15 Eliudi akamzaa Eleazari,

Eleazari akamzaa Matani,

Matani akamzaa Yakobo,

16 naye Yakobo akamzaa Yosefu ambaye alikuwa mumewe Maria, mama yake Yesu, aitwaye Kristo.

17 Hivyo, kulikuwepo na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli hadi Kristo.

Kuzaliwa Kwa Yesu Kristo

18 Basi Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake alikuwa ameposwa na Yosefu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Maria alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

19 Kwa kuwa Yosefu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Maria hadharani, aliazimu kumwacha kwa siri.

20 Lakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yosefu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

21 Naye atamzaa mwana, nawe utamwita Jina lake Yesu,kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”

22 Haya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilokuwa amenena kupitia nabii, akisema:

23 “Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita Jina lake Imanueli”: maana yake, “Mungu pamoja nasi.”

24 Yosefu alipoamka kutoka usingizini, akafanya kama vile alivyoagizwa na malaika wa Bwana, akamchukua Maria kuwa mke wake.

25 Lakini hawakukutana kimwili mpaka Maria alipojifungua mwanawe kifungua mimba akamwita Jina lake Yesu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/MAT/1-9229e9c077322285084c45783ed18d7a.mp3?version_id=1627—