Categories
Yona

Yona Utangulizi

Utangulizi

Yona maana yake ni “Hua.” Kitabu hiki kinaelezea yale yaliyomtukia kama mjumbe wa Mungu. Yona alikuwa ameagizwa na Mungu aende akawaonye watu wa Ninawi juu ya hukumu iliyokuwa inakuja. Alijaribu kumkimbia Mungu na kuelekea Tarshishi, upande wa magharibi wa Israeli ilhali Ninawi ilikuwa kaskazini mashariki. Yona alipotupwa baharini alimezwa na nyangumi ambaye alimrudisha mpaka pwani ya mashariki ya Bahari ya Kati (Mediterania). Hatimaye alikwenda Ninawi na kuwaonya watu kuhusu hukumu ya Mungu. Alivunjika moyo watu wa Ninawi walipotubu na Mungu akaonyesha rehema zake kwa kughairi na kuahirisha siku ya hukumu.

Mwandishi

Yona mwana wa Amitai.

Kusudi

Kuonyesha ukubwa wa neema ya Mungu, na kuwa wokovu ni kwa watu wote.

Mahali

Israeli, Bahari ya Kati (Mediterania) na Ninawi.

Tarehe

Kati ya 785–760 K.K.

Wahusika Wakuu

Yona, nahodha wa meli na mabaharia, mfalme wa Ninawi, na Waninawi wote.

Wazo Kuu

Watu wanaposikia neno la Mungu, wanapoamini na kutubu, Mungu huonyesha rehema na kufuta hukumu iliyokuwa inawakabili. Mungu hapendi mtu yeyote aangamie, bali wafikie toba.

Mambo Muhimu

Rehema za Mungu na upendo wa Mungu kwa watu wote.

Mgawanyo

Yona anamtoroka Mungu (

1:1-17

)

Sala ya Yona na kuokolewa (

2:1-10

).

Yona aenda Ninawi (

3:1-10

)

Yona amkasirikia Mungu kwa sababu ya rehema zake (

4:1-11

).

Categories
Yona

Yona 1

Yona Anamkimbia Bwana

1 Neno laBwanalilimjia Yona mwana wa Amitai:

2 “Nenda katika mji mkubwa wa Ninawi ukahubiri juu yake, kwa sababu uovu wake umekuja juu mbele zangu.”

3 Lakini Yona alimkimbiaBwanana kuelekea Tarshishi. Alishuka mpaka Yafa, ambapo alikuta meli iliyokuwa imepangwa kuelekea bandari ile. Baada ya kulipa nauli, akapanda melini na kuelekea Tarshishi ili kumkimbiaBwana.

4 NdipoBwanaakatuma upepo mkali baharini, nayo dhoruba kali sana ikavuma hata meli ikawa hatarini kuvunjika.

5 Mabaharia wote waliogopa na kila mmoja akamlilia mungu wake mwenyewe. Nao wakatupa mizigo baharini ili meli ipungue uzito.

Lakini Yona alikuwa ameteremkia chumba cha ndani ya meli, mahali ambapo alilala na kupatwa na usingizi mzito.

6 Nahodha akamwendea na kusema, “Wewe unawezaje kulala? Amka ukamwite mungu wako! Huenda akatuangalia, tusiangamie.”

7 Kisha mabaharia wakasemezana wao kwa wao, “Njooni, tupige kura tumtafute anayehusika na maafa haya.” Wakapiga kura, kura ikamwangukia Yona.

8 Kwa hiyo walimuuliza, “Tuambie, ni nani anayehusika kwa kutuletea tatizo hili lote? Unafanya kazi gani? Umetoka wapi? Nchi yako ni ipi? Wewe ni kutoka taifa lipi?”

9 Akajibu, “Mimi ni Mwebrania, nami namwabuduBwana, Mungu wa Mbinguni, aliyeumba bahari na nchi kavu.”

10 Hili liliwaogopesha nao wakamuuliza,

“Umefanya nini?” (Walijua alikuwa anamkimbiaBwana, kwa sababu alishawaambia hivyo.)

11 Bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Kwa hiyo walimuuliza, “Tukutendee nini ili kufanya bahari itulie kwa ajili yetu?”

12 Akawajibu, “Niinueni mnitupe baharini, nayo itakuwa shwari. Ninajua mawimbi haya makubwa yamewatokea kwa ajili ya kosa langu.”

13 Badala yake, wale watu walijitahidi kupiga makasia wawezavyo ili wapate kurudi pwani. Lakini hawakuweza, kwa kuwa bahari ilizidi kuchafuka kuliko mwanzo.

14 Ndipo wakamliliaBwana, “EeBwana, tafadhali usituue kwa kuondoa uhai wa mtu huyu. Usituhesabie hatia kwa kuutoa uhai wa mtu asiyekuwa na hatia, kwa kuwa wewe, EeBwana, umefanya kama ilivyokupendeza.”

15 Kisha walimchukua Yona, wakamtupa baharini nayo bahari iliyokuwa imechafuka ikatulia.

16 Katika jambo hili watu wakamwogopaBwanasana, wakamtoleaBwanadhabihu na kumwekea nadhiri.

17 LakiniBwanaakamwandaa nyangumikummeza Yona, naye Yona alikuwa ndani ya tumbo la nyangumi kwa siku tatu, usiku na mchana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JON/1-88d9c5090d23b0666bf1c2f3f721558c.mp3?version_id=1627—

Categories
Yona

Yona 2

Maombi Ya Yona Katika Tumbo La Nyangumi

1 Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwombaBwanaMungu wake.

2 Akasema:

“Katika shida yangu nalimwitaBwana,

naye akanijibu.

Kutoka kina cha kaburiniliomba msaada,

nawe ukasikiliza kilio changu.

3 Ulinitupa kwenye kilindi,

ndani kabisa ya moyo wa bahari,

mikondo ya maji ilinizunguka,

mawimbi yako yote na viwimbi

vilipita juu yangu.

4 Nikasema, ‘Nimefukuziwa

mbali na uso wako,

hata hivyo nitatazama tena

kuelekea Hekalu lako takatifu.’

5 Maji yaliyonimeza yalinitisha,

kilindi kilinizunguka;

mwaniulijisokota kichwani pangu.

6 Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima,

makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele.

Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni,

EeBwanaMungu wangu.

7 “Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka,

nilikukumbuka wewe,Bwana,

nayo maombi yangu yalikufikia wewe,

katika Hekalu lako takatifu.

8 “Wale watu wanaongʼangʼana na sanamu zisizofaa

hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao.

9 Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,

nitakutolea dhabihu.

Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza.

Wokovu watoka kwaBwana.”

10 BasiBwanaakamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JON/2-1ef80839c1ff5f108dbc49b6c823801f.mp3?version_id=1627—

Categories
Yona

Yona 3

Yona Aenda Ninawi

1 Ndipo neno laBwanalikamjia Yona mara ya pili:

2 “Ondoka uende katika mji mkubwa wa Ninawi, ukautangazie ujumbe ninaokupa.”

3 Yona akalitii neno laBwananaye akaenda Ninawi. Basi Ninawi ulikuwa mji maarufu sana, ilichukua siku tatu kuuzunguka.

4 Siku ya kwanza, Yona aliingia mjini. Akatangaza: “Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.”

5 Watu wa Ninawi wakamwamini Mungu, wakatangaza kufunga, watu wote kuanzia mkubwa sana hadi yule mdogo kabisa, wakavaa nguo za gunia.

6 Habari zilipomfikia mfalme wa Ninawi, aliondoka kwenye kiti chake cha enzi, akavua majoho yake ya kifalme, akajifunika nguo ya gunia kisha akaketi chini mavumbini.

7 Ndipo akatoa tangazo katika Ninawi yote:

“Kwa amri ya mfalme na wakuu wake:

“Msiruhusu mtu yeyote au mnyama, makundi ya ngʼombe au wanyama wengine wafugwao, kuonja kitu chochote, msiwaruhusu kula wala kunywa.

8 Bali wanadamu na wanyama wafunikwe kwa nguo za gunia. Kila mmoja afanye hima kumwomba Mungu. Waziache njia zao mbaya na udhalimu ulio mikononi mwao.

9 Ni nani ajuaye? Huenda Mungu akaghairi kwa huruma yake akaacha hasira yake kali ili tusiangamie.”

10 Mungu alipoona walivyofanya na jinsi walivyogeuka kutoka njia zao mbaya, akawa na huruma wala hakuleta maangamizi juu yao kama alivyokuwa ameonya.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JON/3-dab15e2b36e80b076aaf45c9f9cf3e67.mp3?version_id=1627—

Categories
Yona

Yona 4

Hasira Ya Yona Kwa Ajili Ya Huruma Ya Bwana.

1 Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika.

2 AkamwombaBwana, “EeBwana, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharikisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa.

3 Sasa, EeBwana, niondolee uhai wangu, kwa kuwa ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”

4 LakiniBwanaakamjibu, “Je unayo haki yoyote kukasirika?”

5 Yona akatoka nje akaketi mahali upande wa mashariki wa mji. Hapo akajitengenezea kibanda, akaketi kwenye kivuli chake na kungojea ni nini kitakachotokea katika mji.

6 NdipoBwana, Mungu akaweka tayari mzabibu na kuufanya uote, kumpa Yona kivuli kilichomfunika kichwa ili kuondoa taabu yake, naye Yona akafurahi sana kwa ajili ya ule mzabibu.

7 Lakini kesho yake asubuhi na mapema Mungu akaamuru buu, autafune mzabibu huo nao ukanyauka.

8 Wakati jua lilipochomoza, Mungu akautuma upepo wa hari wa mashariki, nalo jua likawaka juu ya kichwa cha Yona mpaka akazimia. Akatamani kufa, naye akasema, “Ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”

9 Lakini Mungu alimwambia Yona, “Je, unayo haki kukasirika kuhusu mzabibu huo?”

Akasema, “Ndiyo, ninayo haki. Nimekasirika kiasi cha kufa.”

10 LakiniBwanaakamwambia, “Wewe unakasirika kwa ajili ya mzabibu huu, nawe hukuusababisha kuota wala kuutunza. Uliota usiku mmoja, nao ukafa usiku mmoja.

11 Lakini Ninawi ina zaidi ya watu 120,000 ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto, pamoja na ngʼombe wengi. Je, hainipasi kufikiri juu ya mji ule mkubwa?”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JON/4-da616231ce885d25d27bec5b3a1c64da.mp3?version_id=1627—

Categories
Mika

Mika Utangulizi

Utangulizi

Jina Mika maana yake ni “Ni nani aliye kama

Bwana

.” Mika aliishi wakati mmoja na Isaya na Hosea. Aliona Waashuru wakiendelea kustawi wakati Israeli ilikuwa ikididimia hadi ikawa jimbo la Ashuru baada ya kuanguka kwa Israeli mwaka wa 722 K.K. Yuda mara kwa mara ilipata vitisho kutoka kwa wafalme wa Ashuru waliofanikiwa. Mika alionya juu ya hukumu ya Mungu dhidi ya falme zote mbili za Yuda na Israeli. Alitabiri kuwa miji hiyo ingeangamizwa kwa sababu ya watawala wake waovu, manabii wa uongo, makuhani waovu, wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu, na mahakimu waliopokea rushwa na kwa hivyo walishindwa kuonyesha hali ya uchaji na hofu ya Mungu katika wajibu wao.

Kinyume na hayo, Mika alitoa ahadi ya kufanywa upya kwa Sayuni na utawala wa amani kwa wale waliomwamini na kumtumaini Mungu. Alitabiri kwamba Sayuni iliyofanywa upya itakuwa kitovu cha utawala wa ulimwengu wote, mahali ambapo amani halisi na haki vitatawala. “Mtawala katika Israeli” ambaye angelizaliwa Bethlehemu, angesimamisha utawala ambao ungedumu milele.

Mwandishi

Mika, mwenyeji wa Moreshethi, karibu na Gathi.

Kusudi

Kuwaonya watu wa Mungu kuhusu hukumu iliyokuwa inakaribia, na kuwasamehe wote waliotubu.

Mahali

Samaria na Yerusalemu.

Tarehe

Kati ya 742–687 K.K.

Wahusika Wakuu

Watu wa Samaria na Yerusalemu.

Wazo Kuu

Kuwaonya watu juu ya dhambi za udhalimu, uchoyo, ufisadi na ibada za sanamu, vitu ambavyo vingesababisha hukumu iwapo watu wasingetubu na kuacha njia zao mbaya.

Mambo Muhimu

Huu ni mfano mzuri wa ushairi wa Kiebrania. Ziko sehemu tatu, kila moja ikianza na “Sikia” au “Sikiliza” (

1:2

3:1

6:1

) na kufunga na ahadi.

Mgawanyo

Hukumu dhidi ya Samaria na Yerusalemu (

1:1-16

)

Uonevu wa viongozi (

2:1–3:12

)

Urejesho wa Mungu (

4:1–5:15

)

Hukumu na huruma (

6:1–7:20

).

Categories
Mika

Mika 1

1 Neno laBwanalilimjia Mika, Mmoreshethi, wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda; ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu.

2 Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote,

sikilizeni, ee dunia na wote mliomo ndani yake,

iliBwanaMwenyezi ashuhudie dhidi yenu,

Bwana kutoka Hekalu lake takatifu.

Hukumu Dhidi Ya Samaria Na Yerusalemu

3 Tazama!Bwanaanakuja kutoka mahali pake;

anashuka na kukanyaga

mahali palipoinuka juu pa dunia.

4 Milima inayeyuka chini yake

na mabonde yanagawanyika

kama nta mbele ya moto,

kama maji yatiririkayo kasi

kwenye mteremko.

5 Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo,

ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli.

Kosa la Yakobo ni lipi?

Je, sio Samaria?

Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini?

Je, sio Yerusalemu?

6 “Kwa hiyo nitaufanya Samaria kuwa lundo la kokoto,

mahali pa kuotesha mizabibu.

Nitayamwaga mawe yake katika bonde

na kuacha wazi misingi yake.

7 Sanamu zake zote

zitavunjwa vipande vipande;

zawadi zake zote za Hekalu

zitachomwa kwa moto;

nitaharibu vinyago vyake vyote.

Kwa kuwa alikusanya zawadi zake

kutokana na ujira wa kahaba,

nazo zitatumika tena

kulipa mishahara ya kahaba.”

Kulia Na Kuomboleza

8 Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza;

nitatembea bila viatu na tena uchi.

Nitabweka kama mbweha

na kuomboleza kama bundi.

9 Kwa sababu jeraha lake halitibiki;

limekuja Yuda.

Limefika hasa kwenye lango la watu wangu,

hata Yerusalemu kwenyewe.

10 Usiliseme hili huko Gathi;

usilie hata kidogo.

Huko Beth-le-Afra

gaagaa mavumbini.

11 Piteni mkiwa uchi na wenye aibu,

ninyi mkaao Shafiri.

Wale waishio Saanani

hawatatoka nje.

Beth-Eseli iko katika maombolezo;

kinga yake imeondolewa kwako.

12 Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu

wakingoja msaada,

kwa sababu maangamizi yamekuja

kutoka kwaBwana,

hata katika lango la Yerusalemu.

13 Enyi mkaao Lakishi,

fungeni farasi kwenye magari ya vita.

Mlikuwa chanzo cha dhambi

kwa Binti Sayuni,

kwa kuwa makosa ya Israeli

yalikutwa kwako.

14 Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi

zawadi za kuagana.

Mji wa Akzibu utaonyesha wazi udanganyifu

kwa wafalme wa Israeli.

15 Nitawaleteeni atakayewashinda

ninyi mnaoishi Maresha.

Yeye aliye utukufu wa Israeli

atakuja Adulamu.

16 Nyoeni nywele zenu katika kuomboleza

kwa ajili ya watoto wenu mnaowafurahia;

jifanyieni upara kama tai,

kwa kuwa watawaacha

na kwenda uhamishoni.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/MIC/1-c497a0b0b0e802008686ab0250d6b152.mp3?version_id=1627—

Categories
Mika

Mika 2

Mipango Ya Mwanadamu Na Ya Mungu

1 Ole kwa wale wapangao uovu,

kwa wale wafanyao shauri la hila vitandani mwao!

Kunapopambazuka wanalitimiza

kwa sababu uko katika uwezo wao kutekeleza.

2 Wanatamani mashamba na kuyakamata,

pia nyumba na kuzichukua.

Wanamlaghai mwanaume nyumba yake,

mwanadamu mwenzake urithi wake.

3 Kwa hiyo,Bwanaasema:

“Ninapanga maangamizi dhidi ya watu hawa,

ambayo hamwezi kujiokoa wenyewe.

Hamtatembea tena kwa majivuno,

kwa kuwa utakuwa ni wakati wa maafa.

4 Siku hiyo watu watawadhihaki,

watawafanyia mzaha

kwa wimbo huu wa maombolezo:

‘Tumeangamizwa kabisa;

mali ya watu wangu imegawanywa.

Ameninyangʼanya!

Ametoa mashamba yetu kwa wasaliti.’ ”

5 Kwa hiyo hutakuwa na yeyote katika kusanyiko laBwana

wa kugawanya mashamba kwa kura.

Manabii Wa Uongo

6 Manabii wao husema, “Usitabiri.

Usitabiri kuhusu vitu hivi;

aibu haitatupata.”

7 Je, ingesemwa, ee nyumba ya Yakobo:

“Je, Roho waBwanaamekasirika?

Je, yeye hufanya vitu kama hivyo?”

“Je, maneno yangu hayamfanyii mema

yeye ambaye njia zake ni nyofu?

8 Siku hizi watu wangu wameinuka

kama adui.

Unawavua joho la kitajiri wale wanaopita

pasipo kujali,

kama watu warudio kutoka vitani.

9 Unawahamisha wanawake wa watu wangu

kutoka kwenye nyumba zao za kupendeza.

Unaondoa baraka yangu

kwa watoto wao milele.

10 Inuka, nenda zako!

Kwa maana hapa sio mahali pako pa kupumzikia,

kwa sababu pametiwa unajisi,

pameharibiwa, wala hapatengenezeki tena.

11 Ikiwa mwongo na mdanganyifu atakuja na kusema,

‘Nitawatabiria divai na pombe kwa wingi,’

angekuwa ndiye nabii

anayekubalika na watu hawa!

Ahadi Ya Ukombozi

12 “Hakika nitawakusanya ninyi nyote, ee Yakobo,

Hakika nitawaleta pamoja mabaki ya Israeli.

Nitawaleta pamoja kama kondoo ndani ya zizi,

kama kundi kwenye malisho yake,

mahali hapa patakuwa na msongamano wa watu.

13 Yeye afunguaye njia atawatangulia;

watapita kwenye lango na kutoka nje.

Mfalme wao atawatangulia,

Bwanaatakuwa kiongozi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/MIC/2-61aa4bb2bd6125b458447424fc120017.mp3?version_id=1627—

Categories
Mika

Mika 3

Viongozi Na Manabii Wakemewa

1 Kisha nikasema,

“Sikilizeni enyi viongozi wa Yakobo,

enyi watawala wa nyumba ya Israeli.

Je, hampaswi kujua hukumu,

2 ninyi mnaochukia mema

na kupenda maovu;

ninyi mnaowachuna watu wangu ngozi

na kuondoa nyama kwenye mifupa yao;

3 ninyi mnaokula nyama ya watu wangu,

mnaowachuna ngozi

na kuvunja mifupa yao vipande vipande;

mnaowakatakata kama nyama

ya kuwekwa kwenye sufuria

na kama nyama

ya kuwekwa kwenye chungu?”

4 Kisha watamliliaBwana,

lakini hatawajibu.

Wakati huo atawaficha uso wake

kwa sababu ya uovu waliotenda.

5 Hili ndilo asemaloBwana:

“Kuhusu manabii wanaowapotosha watu wangu,

mtu akiwalisha,

wanatangaza ‘amani’;

kama hakufanya hivyo,

wanaandaa kupigana vita dhidi yake.

6 Kwa hiyo usiku utawajieni, msiweze kuwa na maono,

na giza, msiweze kubashiri.

Jua litawachwea manabii hao,

nao mchana utakuwa giza kwao.

7 Waonaji wataaibika

na waaguzi watafedheheka.

Wote watafunika nyuso zao

kwa sababu hakuna jibu litokalo kwa Mungu.”

8 Lakini kuhusu mimi, nimejazwa nguvu,

nimejazwa Roho waBwana,

haki na uweza,

kumtangazia Yakobo kosa lake,

na Israeli dhambi yake.

9 Sikieni hili, enyi viongozi wa nyumba ya Yakobo,

enyi watawala wa nyumba ya Israeli,

mnaodharau haki

na kupotosha kila lililo sawa;

10 mnaojenga Sayuni kwa kumwaga damu

na Yerusalemu kwa uovu.

11 Viongozi wake wanahukumu kwa rushwa,

na makuhani wake wanafundisha kwa malipo,

nao manabii wake wanatabiri kwa fedha.

Hata hivyo wanamwegemeaBwanana kusema,

“Je,Bwanasi yumo miongoni mwetu?

Hakuna maafa yatakayotupata.”

12 Kwa hiyo kwa sababu yenu,

Sayuni italimwa kama shamba,

Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto,

na kilima cha Hekalu

kitakuwa kichuguu

kilichofunikwa na vichaka.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/MIC/3-ab13fe7fa79e1ebce9ede403a655dfa0.mp3?version_id=1627—

Categories
Mika

Mika 4

Mlima Wa Bwana

1 Katika siku za mwisho

mlima wa Hekalu laBwanautaimarishwa

kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote;

utainuliwa juu ya vilima,

na watu wa mataifa watamiminika humo.

2 Mataifa mengi yatakuja na kusema,

“Njooni, twendeni mlimani mwaBwana,

kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo.

Atatufundisha njia zake,

ili tuweze kuenenda katika mapito yake.”

Sheria itatoka Sayuni,

neno laBwanalitatoka Yerusalemu.

3 Atahukumu kati ya mataifa mengi,

na ataamua migogoro ya mataifa

yenye nguvu na yaliyo mbali.

Watafua panga zao ziwe majembe,

na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi.

Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine,

wala hawatajifunza vita tena.

4 Kila mtu ataketi chini ya mzabibu wake

na chini ya mtini wake,

wala hakuna mtu atakayewaogopesha,

kwa kuwaBwanaMwenye Nguvu Zote amesema.

5 Mataifa yote yanaweza kutembea

katika jina la miungu yao;

sisi tutatembea katika jina laBwana

Mungu wetu milele na milele.

Mpango Wa Bwana

6 “Katika siku hiyo,” asemaBwana,

“nitawakusanya walemavu;

nitawakusanya walio uhamishoni

na wale niliowahuzunisha.

7 Nitawafanya walemavu kuwa mabaki,

wale waliofukuzwa kuwa taifa lenye nguvu.

Bwanaatatawala juu yao katika Mlima Sayuni

kuanzia siku hiyo na hata milele.

8 Lakini kuhusu wewe, ee mnara wa ulinzi wa kundi,

ee ngome ya Binti Sayuni,

milki ya awali itarudishwa kwako,

ufalme utakuja kwa Binti Yerusalemu.”

9 Kwa nini sasa unalia kwa nguvu:

kwani huna mfalme?

Je, mshauri wako amekufa, hata maumivu yakukamate

kama ya mwanamke

aliye na utungu wa kuzaa?

10 Gaagaa kwa utungu, ee Binti Sayuni,

kama mwanamke mwenye utungu wa kuzaa,

kwa kuwa sasa ni lazima uuache mji

ukapige kambi uwanjani.

Utakwenda Babeli;

huko utaokolewa.

HukoBwanaatakukomboa

kutoka mikononi mwa adui zako.

11 Lakini sasa mataifa mengi

yamekusanyika dhidi yako.

Wanasema, “Mwache anajisiwe,

macho yetu na yatazame Sayuni kwa furaha!”

12 Lakini hawayajui

mawazo yaBwana;

hawauelewi mpango wake,

yeye awakusanyaye kama miganda

kwenye sakafu ya kupuria.

13 “Inuka upure, ee Binti Sayuni,

kwa kuwa nitakupa pembe za chuma;

nitakupa kwato za shaba

na utavunja vipande vipande mataifa mengi.”

Utatoa mapato yao waliopata kwa udanganyifu kwaBwana,

utajiri wao kwa Bwana wa dunia yote.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/MIC/4-afe6010954f60b8538d4c7d5d9bcb9dc.mp3?version_id=1627—