Categories
Ezekieli

Ezekieli 23

Dada Wawili Makahaba

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, walikuwepo wanawake wawili, binti wa mama mmoja.

3 Wakawa makahaba huko Misri, wakajitia kwenye ukahaba tangu ujana wao. Katika nchi ile vifua vyao vya ubikira vikakumbatiwa huko na wakapoteza ubikira wao.

4 Mkubwa aliitwa Ohola na mdogo wake Oholiba. Walikuwa wangu nao wakazaa wavulana na msichana. Ohola ni Samaria, Oholiba ni Yerusalemu.

5 “Ohola akajitia kwenye ukahaba alipokuwa bado ni wangu, akatamani sana wapenzi wake, mashujaa Waashuru,

6 waliovaa nguo za buluu, watawala na majemadari, wote walikuwa wanaume vijana wa kuvutia, wapandao farasi.

7 Akafanya ukahaba na wasomi wote wa Ashuru, na kujinajisi kwa sanamu zote za kila mwanaume aliyemtamani.

8 Hakuacha ukahaba wake aliouanza huko Misri, wakati ambapo tangu ujana wake wanaume walilala naye, wakikumbatia kifua cha ubikira wake na kumwaga tamaa zao juu yake.

9 “Kwa hiyo nilimtia mikononi mwa wapenzi wake, Waashuru, kwa kuwa ndio aliowatamani.

10 Wakamvua nguo zake wakamwacha uchi, wakawachukua wanawe na binti zake, naye wakamuua kwa upanga. Akawa kitu cha kudharauliwa miongoni mwa wanawake na adhabu ikatolewa dhidi yake.

11 “Oholiba dada yake aliliona jambo hili, lakini kwa tamaa zake na ukahaba wake, akaharibu tabia zake kuliko Ohola dada yake.

12 Yeye naye aliwatamani Waashuru, watawala na majemadari, mashujaa waliovalia sare, wapandao farasi, wanaume vijana wote waliovutia.

13 Nikaona kuwa yeye pia alijinajisi, wote wawili wakaelekea njia moja.

14 “Lakini yeye akazidisha ukahaba wake. Akaona wanaume waliochorwa ukutani, picha za Wakaldayowaliovalia nguo nyekundu,

15 wakiwa na mikanda viunoni mwao na vilemba vichwani mwao, wote walifanana na maafisa wa Babeli wapandao magari ya vita, wenyeji wa Ukaldayo.

16 Mara tu alipowaona, aliwatamani, akatuma wajumbe kwao huko Ukaldayo.

17 Ndipo hao Wababeli wakaja kwake kwenye kitanda cha mapenzi, nao katika tamaa zao wakamtia unajisi. Baada ya kutiwa unajisi, akawaacha kwa kuwachukia.

18 Alipofanya ukahaba wake waziwazi na kuonyesha hadharani uchi wake, nilimwacha kwa kumchukia, kama vile nilivyokuwa nimemwacha dada yake.

19 Lakini akazidisha zaidi ukahaba wake alipozikumbuka siku zake za ujana, alipokuwa kahaba huko Misri.

20 Huko aliwatamani wapenzi wake, ambao viungo vyao vya uzazi ni kama vya punda, na kile kiwatokacho ni kama kiwatokacho farasi.

21 Hivyo ulitamani uasherati wa ujana wako wakati ulipokuwa Misri, kifua chako kilipokumbatiwa, na walipokutomasa kwa sababu ya matiti yako machanga.

22 “Kwa hiyo, Oholiba, hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitawachochea wapenzi wako wawe kinyume na wewe, wale uliowaacha kwa kuchukia, nitawaleta dhidi yako kutoka kila upande:

23 Wababeli na Wakaldayo wote, watu kutoka Pekodi, na Shoa na Koa, wakiwa pamoja na Waashuru wote, vijana wazuri, wote wakiwa watawala na majemadari, maafisa wa magari ya vita na watu wa vyeo vya juu, wote wakiwa wamepanda farasi.

24 Watakuja dhidi yako wakiwa na silaha, magari ya vita, magari ya kukokota, pamoja na umati mkubwa wa watu. Watakuzingira pande zote kwa ngao na vigao na kofia za chuma. Nitakutia mikononi mwao ili wakuadhibu, nao watakuadhibu sawasawa na sheria zao.

25 Nitaelekeza wivu wa hasira yangu dhidi yako, nao watakushughulikia kwa hasira kali. Watakatilia mbali pua yako na masikio yako, na wale watakaosalia miongoni mwako watauawa kwa upanga. Watachukua wana wako na binti zako, na wale watakaosalia miongoni mwenu watateketezwa kwa moto.

26 Watakuvua pia nguo zako na kuchukua mapambo yako yaliyotengenezwa kwa vito na dhahabu.

27 Hivyo ndivyo nitakavyokomesha uasherati wako na ukahaba wako uliouanza huko Misri. Hutatazama vitu hivi kwa kuvitamani tena, wala kukumbuka Misri tena.

28 “Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ninakaribia kukutia mikononi mwa wale unaowachukia, kwa wale uliojitenga nao kwa kuwachukia.

29 Watakushughulikia kwa chuki na kukunyangʼanya kila kitu ulichokifanyia kazi. Watakuacha uchi na mtupu na aibu ya ukahaba wako itafunuliwa. Uasherati wako na uzinzi wako

30 umekuletea haya yote, kwa sababu ulitamani mataifa na kujinajisi kwa sanamu zao.

31 Umeiendea njia ya dada yako, hivyo nitakitia kikombe chake mkononi mwako.

32 “Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“Utakinywea kikombe cha dada yako,

kikombe kikubwa na chenye kina kirefu;

nitaletea juu yako dharau na dhihaka,

kwa kuwa kimejaa sana.

33 Utalewa ulevi na kujawa huzuni,

kikombe cha maangamizo na ukiwa,

kikombe cha dada yako Samaria.

34 Utakinywa chote na kukimaliza;

utakivunja vipande vipande

na kuyararua matiti yako.

Nimenena haya, asemaBwanaMwenyezi.

35 “Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa kuwa tangu uliponisahau mimi na kunitupa nyuma yako, lazima ubebe matokeo ya uasherati wako na ukahaba wako.”

36 Bwanaakaniambia, “Mwanadamu, Je, utawahukumu Ohola na Oholiba? Basi wakabili kwa ajili ya matendo yao ya machukizo,

37 kwa kuwa wamefanya uzinzi na damu imo mikononi mwao. Wamefanya uzinzi na sanamu zao, hata wamewatoa watoto wao walionizalia kuwa kafara, kuwa chakula kwao.

38 Pia wamenifanyia hili: wakati huo huo wamenajisi patakatifu pangu na kuzitangua Sabato zangu.

39 Siku ile ile walitoa watoto wao kuwa kafara kwa sanamu zao, waliingia patakatifu pangu na kupatia unajisi. Hilo ndilo walilolifanya katika nyumba yangu.

40 “Walituma hata wajumbe kuwaita watu kutoka mbali, nao walipowasili ulioga kwa ajili yao, ukapaka macho yako rangi na ukavaa mapambo yako yaliyotengenezwa kwa vito vya dhahabu.

41 Ukaketi kwenye kiti cha anasa, kukiwa na meza iliyoandaliwa mbele yake ambayo juu yake ulikuwa umeweka uvumba na mafuta ambayo yalikuwa yangu.

42 “Kelele za umati wa watu wasiojali zilikuwa zimemzunguka, wakaleta watu wengi waliokuwa wakifanya makelele na walevi kutoka nyikani, ambao walitia bangili kwenye mikono ya yule mwanamke na dada yake na pia taji nzuri za kupendeza kwenye vichwa vyao.

43 Ndipo nikasema kuhusu yule aliyechakazwa na uzinzi, ‘Basi wamtumie kama kahaba, kwa kuwa ndivyo alivyo.’

44 Nao wakazini naye. Kama vile watu wazinivyo na kahaba, ndiyo hivyo walivyozini na hao wanawake waasherati, Ohola na Oholiba.

45 Lakini watu wenye haki, watawahukumia adhabu wanawake wafanyao uzinzi na kumwaga damu, kwa kuwa ni wazinzi na damu iko mikononi mwao.

46 “Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo, Leteni watu wengi wenye makelele dhidi yao na uwaache wapate hofu na watekwe nyara.

47 Hao watu wengi watawapiga kwa mawe na kuwaua kwa panga zao, watawaua wana wao na binti zao na kuzichoma nyumba zao.

48 “Hivyo nitaukomesha uasherati katika nchi, ili wanawake wote wapate onyo nao wasije wakafanya uasherati kama ninyi mlivyofanya.

49 Utapata adhabu kwa ajili ya uasherati wako na kuchukua matokeo ya dhambi zako za uasherati. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimiBwanaMwenyezi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/23-a0ae4a9ec64d4321eeeda23a3ee1a039.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 24

Chungu Cha Kupikia

1 Katika mwaka wa tisa, mwezi wa kumi, siku ya kumi, neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, weka kumbukumbu ya tarehe hii, tarehe hii hasa, kwa kuwa mfalme wa Babeli ameuzingira mji wa Yerusalemu kwa jeshi siku hii ya leo.

3 Iambie nyumba hii ya kuasi fumbo, na uwaambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Teleka sufuria jikoni; iteleke

na umimine maji ndani yake,

4 Weka vipande vya nyama ndani yake,

vipande vyote vizuri,

vya paja na vya bega.

Ijaze hiyo sufuria kwa mifupa hii mizuri;

5 chagua yule aliye bora wa kundi la kondoo.

Panga kuni chini ya sufuria kwa ajili ya mifupa;

chochea mpaka ichemke

na uitokose hiyo mifupa ndani yake.

6 “ ‘Kwa kuwa hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Ole wa mji umwagao damu,

ole wa sufuria ambayo sasa

ina ukoko ndani yake,

ambayo ukoko wake hautoki.

Kipakue kipande baada ya kipande,

bila kuvipigia kura.

7 “ ‘Kwa kuwa damu aliyoimwaga ipo katikati yake:

huyo mwanamke aliimwaga

juu ya mwamba ulio wazi;

hakuimwaga kwenye ardhi,

ambako vumbi lingeifunika.

8 Kuchochea ghadhabu na kulipiza kisasi,

nimemwaga damu yake

juu ya mwamba ulio wazi,

ili isifunikwe.

9 “ ‘Kwa hiyo, hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Ole wa mji umwagao damu!

Mimi nami nitalundikia kuni nyingi.

10 Kwa hiyo lundika kuni

na uwashe moto.

Pika hiyo nyama vizuri,

changanya viungo ndani yake,

na uiache mifupa iungue kwenye moto.

11 Kisha teleka sufuria tupu kwenye makaa

mpaka iwe na moto sana na shaba yake ingʼae,

ili uchafu wake upate kuyeyuka

na ukoko wake upate kuungua na kuondoka.

12 Imezuia juhudi zote,

ukoko wake mwingi haujaondoka,

hata ikiwa ni kwa moto.

13 “ ‘Sasa uchafu wako ni uasherati wako. Kwa sababu nilijaribu kukutakasa lakini haikuwezekana kutakaswa kutoka kwenye huo uchafu wako, hutatakasika tena mpaka ghadhabu yangu dhidi yako iwe imepungua.

14 “ ‘MimiBwananimesema, wakati umewadia wa mimi kutenda. Mimi sitazuia, mimi sitaona huruma wala sitapunguza hasira yangu, Utahukumiwa sawasawa na mwenendo na matendo yako, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

Kifo Cha Mke Wa Ezekieli

15 Neno laBwanalikanijia kusema:

16 “Mwanadamu, kwa pigo moja nakaribia kukuondolea kile kilicho furaha ya macho yako. Lakini usiomboleze au kulia wala kudondosha machozi yoyote.

17 Lia kwa uchungu kimya kimya usimwombolezee mtu aliyekufa. Jifunge kilemba chako na uvae viatu vyako miguuni mwako, usifunike sehemu ya chini ya uso wako, wala usile vyakula vya kawaida vya wakati wa matanga.”

18 Hivyo nikanena na watu asubuhi na jioni mke wangu akafa. Asubuhi yake nilifanya kama nilivyoamriwa.

19 Ndipo watu wakaniuliza, “Je, jambo hili unalofanya linamaanisha nini kwetu?”

20 Kwa hiyo nikawaambia, “Neno laBwanalilinijia kusema:

21 ‘Sema na nyumba ya Israeli. Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ninakaribia kupatia unajisi mahali pangu patakatifu, ngome ambayo ndani yake mnaona fahari, furaha ya macho yenu, kitu mnachokipenda. Wana wenu na binti zenu mliowaacha nyuma wataanguka kwa upanga.

22 Nanyi mtafanya kama nilivyofanya. Hamtafunika sehemu ya chini ya nyuso zenu wala hamtakula vyakula vya kawaida vya waombolezaji.

23 Mtajifunga vilemba vichwani mwenu na kuvaa viatu vyenu miguuni mwenu. Hamtaomboleza au kulia, lakini mtadhoofika kwa sababu ya dhambi zenu na kulia kwa uchungu kila mtu na mwenzake.

24 Ezekieli atakuwa ishara kwenu, mtafanya kama yeye alivyofanya. Wakati jambo hili litakapotokea, mtajua kuwa Mimi ndimiBwanaMwenyezi.’

25 “Nawe, mwanadamu, siku ile nitakapoondoa ngome yao iliyo furaha yao na utukufu wao, kitu cha kupendeza macho yao, kile kilicho shauku ya mioyo yao, wana wao na binti zao vilevile,

26 siku hiyo atakayetoroka atakuja kuwapasha habari.

27 Katika siku ile kinywa chako kitamfumbukia yeye aliyenusurika, nawe utaongea wala hutanyamaza tena. Hivyo wewe utakuwa ishara kwao, nao watajua kuwa Mimi ndimiBwana.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/24-2c9a4dc9b1872b730362d7a788ef928b.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 25

Unabii Dhidi Ya Amoni

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Waamoni utabiri dhidi yao.

3 Waambie, ‘Sikieni neno laBwanaMwenyezi. Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa sababu ulisema, “Aha!” juu ya mahali pangu patakatifu palipotiwa unajisi, na juu ya nchi ya Israeli ilipoangamizwa, na juu ya watu wa Yuda walipokwenda uhamishoni,

4 kwa hiyo nitawatia mikononi mwa watu wa mashariki mkawe mali yao. Watapiga kambi zao katikati yenu na kufanya makazi miongoni mwenu, watakula matunda yenu na kunywa maziwa yenu.

5 Nitaufanya mji wa Raba kuwa malisho ya ngamia na Amoni kuwa mahali pa kondoo pa kupumzikia. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.

6 Kwa kuwa hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa kuwa umepiga makofi yako na kufanya kishindo kwa miguu, mkifurahia kwa mioyo yenu miovu juu ya yale mabaya yaliyoipata nchi ya Israeli,

7 hivyo nitaunyoosha mkono wangu dhidi yako na kukutoa kuwa nyara kwa mataifa. Nitakukatilia mbali kutoka kwenye mataifa na kukungʼoa katika nchi. Nitakuangamiza, nawe utajua ya kuwa Mimi ndimiBwana.’ ”

Unabii Dhidi Ya Moabu

8 “Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: ‘Kwa sababu Moabu na Seiri wamesema, “Tazama, nyumba ya Yuda imekuwa kama mataifa mengine yote,”

9 kwa hiyo nitaiondoa ile miji iliyo kando ya Moabu, kuanzia miji iliyoko mipakani, yaani: Beth-Yeshimothi, Baal-Meoni na Kiriathaimu, iliyo utukufu wa nchi hiyo.

10 Nitaitia Moabu pamoja na Waamoni mikononi mwa watu wa Mashariki kuwa milki yao, ili kwamba Waamoni wasikumbukwe miongoni mwa mataifa,

11 nami nitatoa adhabu kwa Moabu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.’ ”

Unabii Dhidi Ya Edomu

12 “Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: ‘Kwa sababu Edomu ulilipiza kisasi juu ya nyumba ya Yuda na kukosa sana kwa kufanya hivyo,

13 kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitaunyoosha mkono wangu dhidi ya Edomu na kuua watu wake na wanyama wao. Nitaufanya ukiwa, kuanzia Temani hadi Dedani wataanguka kwa upanga.

14 Nitalipiza Edomu kisasi kwa mkono wa watu wangu Israeli, nao watawatendea Edomu sawasawa na hasira yangu na ghadhabu yangu, nao watakijua kisasi changu, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

Unabii Dhidi Ya Ufilisti

15 “Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: ‘Kwa sababu Wafilisti wamewalipiza kisasi kwa uovu wa mioyo yao na kwa uadui wa siku nyingi wakataka kuangamiza Yuda,

16 kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi ninakaribia kuunyoosha mkono wangu dhidi ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi na kuwaangamiza wale waliosalia katika pwani.

17 Nitalipiza kisasi kikubwa juu yao na kuwaadhibu katika ghadhabu yangu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimiBwana, nitakapolipiza kisasi juu yao.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/25-176ab2fb5fd6b2b4751ec6aa48088928.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 26

Unabii Dhidi Ya Tiro

1 Mwaka wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, kwa sababu Tiro amesema kuhusu Yerusalemu, ‘Aha! Lango la kwenda kwa mataifa limevunjika, nayo milango yake iko wazi mbele yangu, sasa kwa kuwa amekuwa magofu nitastawi.’

3 Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi niko kinyume na wewe, ee Tiro, nami nitaleta mataifa mengi dhidi yako, kama bahari inayovurumisha mawimbi yake.

4 Watavunja kuta za Tiro na kuibomoa minara yake, nitakwangua udongo wake na kuufanya mwamba mtupu.

5 Itakuwa huko katikati ya bahari patakuwa mahali pa kutandaza nyavu za kuvulia samaki, kwa maana nimenena, asemaBwanaMwenyezi. Atakuwa nyara kwa mataifa,

6 nayo makao yake huko bara yataangamizwa kwa upanga. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwana.

7 “Kwa maana hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kutoka kaskazini nitamleta dhidi ya Tiro Mfalme Nebukadneza wa Babeli, mfalme wa wafalme, akiwa na farasi na magari ya vita, wapanda farasi na jeshi kubwa.

8 Atayaharibu makao yako huko bara kwa upanga, ataweka jeshi kukuzingira, atakuzingira mpaka kwenye kuta za ngome zako na kuinua ngao zake dhidi yako.

9 Ataelekeza mapigo ya vyombo vyake vya kubomolea dhidi ya kuta zako na kubomoa minara yako kwa silaha zake.

10 Farasi zake zitakuwa nyingi sana kiasi kwamba utafunikwa na mavumbi watakayotimua. Kuta zako zitatikisika kwa mshindo wa farasi wa vita, magari makubwa na magari ya vita wakati aingiapo malango yako kama watu waingiao mji ambao kuta zake zimebomolewa kote.

11 “Kwato za farasi zake zitakanyaga barabara zako zote, atawaua watu wako kwa upanga na nguzo zako zilizo imara zitaanguka chini.

12 Watateka utajiri wako na kuchukua nyara bidhaa zako, watazivunja kuta zako na kuzibomoa nyumba zako nzuri, watatupa baharini mawe yako, mbao zako na kifusi chako.

13 Nitakomesha kelele za nyimbo zako, na uimbaji wako wa kinubi kamwe hautasikika tena.

14 Nitakufanya mwamba mtupu, nawe utakuwa mahali pa kutandazia nyavu za kuvulia samaki. Kamwe hutajengwa tena, kwa maana MimiBwananimenena, asemaBwanaMwenyezi.

15 “Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo kwa Tiro: ‘Je, nchi za pwani hazitatetemeka kwa kishindo cha anguko lako, wakati majeruhi wanapolia kwa maumivu makali na wakati mauaji yanaendelea ndani yako?

16 Ndipo wakuu wote wa mataifa ya pwani watashuka kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kuweka kando majoho yao na kuvua nguo zao zilizotariziwa. Wakiwa wamevikwa hofu kuu, wataketi chini ardhini, wakiwa wanatetemeka kila dakika na wakikustajabia.

17 Ndipo wao watakuombolezea na kukuambia:

“ ‘Tazama jinsi ulivyoharibiwa,

ee mji uliokuwa na sifa,

wewe uliyekaliwa na mabaharia!

Ulikuwa na nguvu kwenye bahari,

wewe na watu wako;

wote walioishi huko,

uliwatia hofu kuu.

18 Sasa nchi za pwani zinatetemeka

katika siku ya anguko lako;

visiwa vilivyomo baharini

vinaogopa kwa kuporomoka kwako.’

19 “Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitakapokufanya uwe mji wa ukiwa, kama miji isiyokaliwa tena na watu, nitakapoleta vilindi vya bahari juu yako na maji yake makuu yatakapokufunika,

20 ndipo nitakapokushusha chini pamoja na wale washukao shimoni, kwa watu wa kale, nami nitakufanya uishi katika pande za chini za nchi kama katika magofu ya kale, pamoja na wale washukao shimoni, nawe hutarudi au kurejea kwenye makao yako katika nchi ya walio hai.

21 Nitakufikisha mwisho wa kutisha wala hutakuwepo tena. Watu watakutafuta, lakini kamwe hutaonekana tena, asemaBwanaMwenyezi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/26-1350b9e2e93ca208ffc6908a28a41cdb.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 27

Maombolezo Kwa Ajili Ya Tiro

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Tiro.

3 Umwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Ee Tiro, wewe umesema,

“Mimi ni mkamilifu katika uzuri.”

4 Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari,

wajenzi wako walikamilisha uzuri wako.

5 Walizifanya mbao zako zote

kwa misunobari itokayo Seniri;

walichukua mierezi kutoka Lebanoni

kukutengenezea mlingoti.

6 Walichukua mialoni toka Bashani

wakakutengenezea makasia yako;

kwa miti ya msanduku

kutoka pwani ya Kitimu

wakatengeneza sitahayako

na kuipamba kwa pembe za ndovu.

7 Kitani safi kilichotariziwa kutoka Misri kilikuwa tanga lako,

nacho kilikuwa bendera yako;

chandarua chako kilikuwa cha rangi ya buluu na ya zambarau

kutoka visiwa vya Elisha.

8 Watu kutoka Sidoni na Arvadi walikuwa wapiga makasia yako;

watu wako wenye ustadi, ee Tiro,

walikuwa ndio mabaharia wako.

9 Wazee wa Gebalipamoja na mafundi stadi

walikuwa mafundi wako melini.

Meli zote za baharini na mabaharia wao

walikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako.

10 “ ‘Watu wa Uajemi, Ludi na Putu

walikuwa askari katika jeshi lako.

Walitundika ngao zao na chapeo zao kwenye kuta zako,

wakileta fahari yako.

11 Watu wa Arvadi na wa Heleki

walikuwa juu ya kuta zako pande zote;

watu wa Gamadi

walikuwa kwenye minara yako.

Walitundika ngao zao kuzizunguka kuta zako;

wakaukamilisha uzuri wako.

12 “ ‘Tarshishi walifanya biashara nawe kwa sababu ya utajiri wako mkubwa wa bidhaa, walibadilisha fedha, chuma, bati na risasi kwa mali zako.

13 “ ‘Uyunani, Tubali na Mesheki, walifanya biashara nawe, walibadilisha watumwa na vyombo vya shaba kwa bidhaa zako.

14 “ ‘Watu wa Beth-Togarma walibadilisha farasi wa mizigo, farasi wa vita na nyumbu kwa mali zako.

15 “ ‘Watu wa Dedaniwalifanya biashara nawe, watu wengi wa nchi za pwani walikuwa wachuuzi wako, walikulipa kwa pembe za ndovu na mpingo.

16 “ ‘Watu wa Aramu walifanya biashara nawe kwa ajili ya wingi wa kazi za mikono yako, wakibadilishana kwa almasi, vitambaa vya rangi ya zambarau, vitambaa vilivyotariziwa, kitani safi, matumbawena akiki nyekundu.

17 “ ‘Yuda na Israeli walifanya biashara nawe, walibadilishana kwa ngano kutoka Minithi, mtama, asali, mafuta na zeri ya kuponyeshea.

18 “ ‘Dameski, kwa sababu ya wingi wa kazi za mikono yako na ukuu wa utajiri wa mali, walifanya biashara nawe wakibadilishana mvinyo kutoka Helboni na sufu kutoka Zahari.

19 “ ‘Wadani na Wayunani kutoka Uzali, walikuletea mali za biashara, nao wakabadilishana nawe chuma kilichofuliwa, mdalasini na mchaichai.

20 “ ‘Dedani alifanya biashara nawe kwa matandiko ya farasi.

21 “ ‘Arabuni na wakuu wote wa Kedari walikuwa wanunuzi wako waliobadilishana bidhaa zako na wana-kondoo, kondoo dume na mbuzi.

22 “ ‘Wafanyabiashara wa Sheba na wa Raama walifanya biashara nawe, wakabadilishana bidhaa zako na aina zote za vikolezi, vito vya thamani na dhahabu.

23 “ ‘Harani, Kane na Edeni na wafanyabiashara wa Sheba, Ashuru na Kilmadi walifanya biashara nawe.

24 Kwenye soko lako, walifanya biashara nawe kwa mavazi mazuri, vitambaa vya buluu, nguo za kutariziwa na mazulia ya rangi mbalimbali yenye kamba zilizosokotwa na kuwekwa mafundo imara.

25 “ ‘Merikebu za Tarshishi ndizo

zinazokusafirishia bidhaa zako.

Umejazwa shehena kubwa

katika moyo wa bahari.

26 Wapiga makasia wako wanakupeleka

mpaka kwenye maji makavu.

Lakini upepo wa mashariki umekuvunja vipande vipande

katika moyo wa bahari.

27 Utajiri wako, bidhaa zako na mali zako,

mabaharia wako, manahodha wako,

mafundi wako wa meli,

wafanyabiashara wako na askari wako wote,

na kila mmoja aliyeko melini

atazama kwenye moyo wa bahari

siku ile ya kuvunjika kwa meli yako.

28 Nchi za pwani zitatetemeka

wakati mabaharia wako watakapopiga kelele.

29 Wote wapigao makasia

wataacha meli zao,

mabaharia wote na wanamaji wote

watasimama pwani.

30 Watapaza sauti zao

na kulia sana kwa ajili yako;

watajitupia mavumbi juu ya vichwa vyao

na kujivingirisha kwenye majivu.

31 Watanyoa nywele zao kwa ajili yako,

nao watavaa nguo za magunia.

Watakulilia kwa uchungu wa moyo

na kwa maombolezo makuu.

32 Watakapokuwa wanalia na kuomboleza juu yako,

watafanya maombolezo kukuhusu wakisema:

“Ni nani aliyepata kuangamizwa kama Tiro,

katika moyo wa bahari?”

33 Wakati bidhaa zako zilipotoka baharini,

ulitosheleza mataifa mengi;

kwa wingi wa utajiri wako na bidhaa zako

ulitajirisha wafalme wa dunia.

34 Sasa umevunjavunjwa na bahari,

katika vilindi vya maji,

bidhaa zako na kundi lako lote

vimezama pamoja nawe.

35 Wote waishio katika nchi za pwani

wanakustaajabia;

wafalme wao wanatetemeka kwa hofu kuu,

nazo nyuso zao zimekunjamana kwa woga.

36 Wafanyabiashara miongoni mwa mataifa wanakucheka;

umefikia mwisho wa kutisha

nawe hutakuwepo tena.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/27-5e0174060ef0a4ccecab004d567f1dce.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 28

Unabii Dhidi Ya Mfalme Wa Tiro

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, mwambie mfalme wa Tiro, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Kwa sababu moyo wako umejivuna

na umesema, “Mimi ni mungu;

nami ninaketi katika kiti cha enzi cha mungu

katika moyo wa bahari.”

Lakini wewe ni mwanadamu, wala si mungu,

ingawa unafikiri kuwa una hekima kama mungu.

3 Je, wewe una hekima kuliko Danieli?

Je, hakuna siri iliyofichika kwako?

4 Kwa hekima yako na ufahamu wako,

umejipatia utajiri,

nawe umejikusanyia dhahabu

na fedha katika hazina zako.

5 Kwa werevu wako mwingi katika biashara,

umeongeza utajiri wako

na kwa sababu ya utajiri wako

moyo wako umekuwa na kiburi.

6 “ ‘Kwa hiyo, hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Kwa sababu unafikiri una hekima,

mwenye hekima kama mungu,

7 mimi nitawaleta wageni dhidi yako,

taifa katili kuliko yote;

watafuta panga zao dhidi ya uzuri wa hekima yako,

na kuchafua fahari yako inayongʼaa.

8 Watakushusha chini shimoni,

nawe utakufa kifo cha kikatili

katika moyo wa bahari.

9 Je, wakati huo utasema, “Mimi ni mungu,”

mbele ya wale wanaokuua?

Utakuwa mwanadamu tu, wala si mungu,

mikononi mwa hao wanaokuua.

10 Utakufa kifo cha wasiotahiriwa

kwa mkono wa wageni.

Kwa kuwa mimi nimenena, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

11 Neno laBwanalikanijia kusema:

12 “Mwanadamu, mfanyie maombolezo mfalme wa Tiro, nawe umwambie: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Ulikuwa kipeo cha ukamilifu,

ukiwa umejaa hekima

na mkamilifu katika uzuri.

13 Ulikuwa ndani ya Edeni,

bustani ya Mungu;

kila kito cha thamani kilikupamba:

akiki nyekundu, yakuti manjano na zumaridi,

krisolitho, shohamu na yaspi,

yakuti samawi, almasi na zabarajadi.

Kuwekwa kwa hayo mapambo na kushikizwa kwake

kulifanywa kwa dhahabu;

siku ile ulipoumbwa yaliandaliwa tayari.

14 Ulitiwa mafuta kuwa kerubi mlinzi,

kwa kuwa hivyo ndivyo nilivyokuweka wakfu.

Ulikuwa kwenye mlima mtakatifu wa Mungu;

ulitembea katikati ya vito vya moto.

15 Ulikuwa mnyofu katika njia zako

tangu siku ile ya kuumbwa kwako,

hadi uovu ulipoonekana ndani yako.

16 Kutokana na biashara yako iliyoenea,

ulijazwa na dhuluma,

nawe ukatenda dhambi.

Hivyo nilikuondoa kwa aibu kutoka mlima wa Mungu,

nami nikakufukuza, ee kerubi mlinzi,

kutoka katikati ya vito vya moto.

17 Moyo wako ukawa na kiburi

kwa ajili ya uzuri wako,

nawe ukaiharibu hekima yako

kwa sababu ya fahari yako.

Kwa hiyo nikakutupa chini;

nimekufanya kioja mbele ya wafalme.

18 Kwa dhambi zako nyingi na biashara yako ya dhuluma,

umenajisi mahali pako patakatifu.

Kwa hiyo nilifanya moto utoke ndani yako,

nao ukakuteketeza,

nami nikakufanya majivu juu ya nchi,

machoni pa wote waliokuwa wakitazama.

19 Mataifa yote yaliyokujua

yanakustajabia;

umefikia mwisho wa kutisha

na hutakuwepo tena milele.’ ”

Unabii Dhidi Ya Sidoni

20 Neno laBwanalikanijia kusema:

21 “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Sidoni, ukatabiri dhidi yake,

22 nawe useme: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Mimi ni kinyume chako, ee Sidoni,

nami nitapata utukufu ndani yako.

Nao watajua kwamba Mimi ndimiBwana,

nitakapotekeleza hukumu zangu

na kuonyesha utakatifu wangu ndani yake.

23 Nitapeleka tauni ndani yake

na kufanya damu itiririke katika barabara zake.

Waliochinjwa wataanguka ndani yake,

kwa upanga dhidi yake kila upande.

Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwana.

24 “ ‘Nyumba ya Israeli hawatakuwa tena na majirani wenye nia ya kuwadhuru wanaoumiza kama michongoma na miiba mikali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwanaMwenyezi.

25 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitakapoikusanya nyumba ya Israeli kutoka mataifa ambako wametawanyika, nitajionyesha kuwa mtakatifu miongoni mwao machoni pa mataifa. Ndipo watakapoishi katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu Yakobo.

26 Wataishi humo kwa salama na watajenga nyumba na kupanda mashamba ya mizabibu, wataishi kwa salama nitakapowaadhibu majirani zao wote ambao waliwafanyia uovu. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwana, Mungu wao.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/28-c103ccfad913a2740d4a2fb7d66b7a6b.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 29

Unabii Dhidi Ya Misri

1 Katika mwaka wa kumi, mwezi wa kumi, siku ya kumi na mbili, neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Farao mfalme wa Misri na utabiri dhidi yake na dhidi ya Misri yote.

3 Nena, nawe useme: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Mimi ni kinyume nawe, Farao, mfalme wa Misri,

joka kubwa ulalaye katikati ya vijito vyako.

Unasema, “Mto Naili ni wangu mwenyewe;

niliufanya kwa ajili yangu mwenyewe.”

4 Lakini nitatia ndoana katika mataya yako

nami nitawafanya samaki wa vijito vyako

washikamane na magamba yako.

Nitakutoa katikati ya vijito vyako,

pamoja na samaki wote

walioshikamana na magamba yako.

5 Nitakutupa jangwani,

wewe pamoja na samaki wote wa vijito vyako.

Utaanguka uwanjani,

nawe hutakusanywa au kuchukuliwa.

Nitakutoa uwe chakula

kwa wanyama wa nchi

na ndege wa angani.

6 Ndipo wale wote waishio Misri watakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.

“ ‘Umekuwa fimbo ya tete kwa nyumba ya Israeli.

7 Walipokushika kwa mikono yao, ulivunjika na kuchana mabega yao; walipokuegemea, ulivunjika na migongo yao ikateguka.

8 “ ‘Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitaleta upanga juu yako na kuua watu wako na wanyama wao.

9 Misri itakuwa ukiwa na isiyolimwa wala kukaliwa na watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.

“ ‘Kwa sababu ulisema, “Mto Naili ni wangu; mimi niliufanya,”

10 kwa hiyo mimi ni kinyume nawe na kinyume na vijito vyako, nami nitaifanya nchi ya Misri kuwa magofu na ukiwa isiyolimwa wala kukaliwa na watu kuanzia Migdoli hadi Aswani, hata kufikia mpakani wa Ethiopia.

11 Hakuna unyayo wa mtu au mnyama utakaopita ndani yake, wala hakuna yeyote atakayeishi humo kwa muda wa miaka arobaini.

12 Nitaifanya nchi ya Misri ukiwa, miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yake itabaki ukiwa miaka arobaini miongoni mwa miji iliyo magofu. Nami nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi nyingine.

13 “ ‘Lakini hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mwishoni mwa hiyo miaka arobaini, nitawakusanya Wamisri kutoka mataifa walikotawanywa.

14 Nitawarudisha hao Wamisri kutoka kwenye kutekwa kwao na kuwaweka katika Pathrosi,nchi ya baba zao. Huko watakuwa na ufalme usiokuwa na nguvu.

15 Utakuwa ufalme dhaifu kuliko zote na kamwe Misri haitajikweza tena juu ya mataifa mengine. Nitaufanya ufalme wake dhaifu sana kiasi kwamba kamwe hautatawala tena juu ya mataifa mengine.

16 Misri haitakuwa tena tumaini la watu wa Israeli bali itakuwa kumbukumbu ya dhambi yao kwa kuigeukia kuomba msaada. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimiBwanaMwenyezi.’ ”

17 Katika mwaka wa ishirini na saba, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza, neno laBwanalikanijia, kusema:

18 “Mwanadamu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliongoza jeshi lake kufanya kazi ngumu dhidi ya Tiro; kila kichwa kilipata upaa na kila bega likachunika. Lakini yeye na jeshi lake hawakupata malipo yoyote kutokana na muda wote aliongoza hiyo vita dhidi ya Tiro.

19 Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitaitia Misri mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye atachukua utajiri wa Misri. Atateka mateka na kuchukua nyara mali za Misri kama ujira kwa ajili ya jeshi lake.

20 Nimempa mfalme wa Babeli nchi ya Misri kuwa ujira kwa juhudi zake kwa sababu yeye na jeshi lake walifanya kwa ajili yangu, asemaBwanaMwenyezi.

21 “Katika siku hiyo nitaifanya nyumba ya Israeli iwe na nguvu nami nitakifungua kinywa chako miongoni mwao. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwana.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/29-5437dd410916fae9f64647825480fa5b.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 30

Maombolezo Kwa Ajili Ya Misri

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Ombolezeni ninyi na mseme,

“Ole wa siku ile!”

3 Kwa kuwa siku ile imekaribia,

siku yaBwanaimekaribia,

siku ya mawingu,

siku ya maangamizi kwa mataifa.

4 Upanga utakuja dhidi ya Misri,

nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia.

Mauaji yatakapoangukia Misri,

utajiri wake utachukuliwa

na misingi yake itabomolewa.

5 Kushina Putu, Ludi na Arabia yote, Libyana watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.

6 “ ‘Hili ndiloBwanaasemalo:

“ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka

na kiburi cha nguvu zake kitashindwa.

Kutoka Migdoli hadi Aswani,

watauawa ndani yake kwa upanga,

asemaBwanaMwenyezi.

7 “ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa

miongoni mwa nchi zilizo ukiwa,

nayo miji yao itakuwa magofu

miongoni mwa miji iliyo magofu.

8 Ndipo watakapojua kwamba mimi ndimiBwana,

nitakapoiwasha Misri moto

na wote wamsaidiao watapondwa.

9 “ ‘Siku hiyo wajumbe watatoka kwangu kwa merikebu, ili kuwatia hofu Ethiopia, wakiwa katika hali yao ya kuridhika. Maumivu makali yatawapata siku ya maangamizi ya Misri, kwa kuwa hakika itakuja.

10 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Nitakomesha makundi ya wajeuri ya Misri

kwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli.

11 Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote,

litaletwa ili kuangamiza nchi.

Watafuta panga zao dhidi ya Misri

na kuijaza nchi kwa waliouawa.

12 Nitakausha vijito vya Naili

na nitaiuza nchi kwa watu waovu,

kwa mkono wa wageni,

nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu

kilichomo ndani yake.

MimiBwananimenena haya.

13 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Nitaangamiza sanamu

na kukomesha vinyago katika Memfisi

Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri,

nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.

14 Nitaifanya Pathrosikuwa ukiwa

na kuitia moto Soani,

nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi

15 Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,

ngome ya Misri,

nami nitakatilia mbali

makundi ya wajeuri wa Thebesi.

16 Nitaitia moto nchi ya Misri;

Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu.

Thebesi itachukuliwa na tufani,

Memfisi itakuwa katika taabu daima.

17 Wanaume vijana wa Onina wa Pi-Besethi

wataanguka kwa upanga

nayo hiyo miji itatekwa.

18 Huko Tahpanhesi mchana utatiwa giza

nitakapovunja kongwa la Misri;

hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma.

Atafunikwa na mawingu

na vijiji vyake vitatekwa.

19 Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu,

nao watajua kuwa Mimi ndimiBwana.’ ”

20 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa kwanza, siku ya saba, neno laBwanalikanijia kusema:

21 “Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga.

22 Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na Farao mfalme wa Misri. Nitavunja mikono yake yote miwili, ule mkono ulio mzima pia na ule uliovunjika na kuufanya upanga uanguke toka mkononi mwake.

23 Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi zote.

24 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli na kuutia upanga wangu mkononi mwake, lakini nitavunja mikono ya Farao, naye atalia kwa huzuni mbele yake kama mtu aliyetiwa jeraha la kumfisha.

25 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, lakini mikono ya Farao italegea. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwana, nitakapoutia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye ataunyoosha dhidi ya Misri.

26 Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi mbalimbali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwana.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/30-1df7d03bab06f06833e454751ecfd504.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 31

Mwerezi Katika Lebanoni

1 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa tatu, siku ya kwanza, neno laBwanalikanijia, kusema:

2 “Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri na makundi yake ya wajeuri:

“ ‘Je, ni nani awezaye kulinganishwa

na wewe katika fahari.

3 Angalia Ashuru, wakati fulani ilikuwa mwerezi huko Lebanoni,

ukiwa na matawi mazuri ukitia msitu kivuli;

ulikuwa mrefu sana,

kilele chake kilipita majani ya miti yote.

4 Maji mengi yaliustawisha,

chemchemi zenye maji mengi ziliufanya urefuke;

vijito vyake vilitiririka pale

ulipoota pande zote

na kupeleka mifereji yake

kwenye miti yote ya shambani.

5 Hivyo ukarefuka

kupita miti yote ya shambani;

vitawi vyake viliongezeka

na matawi yake yakawa marefu,

yakitanda kwa sababu ya wingi wa maji.

6 Ndege wote wa angani

wakaweka viota kwenye vitawi vyake,

wanyama wote wa shambani

wakazaana chini ya matawi yake,

mataifa makubwa yote

yaliishi chini ya kivuli chake.

7 Ulikuwa na fahari katika uzuri,

ukiwa na matawi yaliyotanda,

kwa kuwa mizizi yake ilikwenda chini

mpaka kwenye maji mengi.

8 Mierezi katika bustani ya Mungu

haikuweza kushindana nao,

wala misunobari haikuweza

kulingana na vitawi vyake,

wala miaramoni

haikulinganishwa na matawi yake,

wala hakukuwa na mti katika bustani ya Mungu

wa kulinganisha na uzuri wake.

9 Niliufanya kuwa mzuri

ukiwa na matawi mengi,

ulionewa wivu na miti yote ya Edeni

katika bustani ya Mungu.

10 “ ‘Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa sababu ulikuwa mrefu sana, kilele chake kikiwa juu ya majani manene ya miti na kwa sababu ulikuwa na kiburi cha urefu wake,

11 niliutia mikononi mwa mtawala wa mataifa, ili yeye aushughulikie sawasawa na uovu wake. Nikaukatilia mbali,

12 nayo mataifa mageni yaliyo makatili sana yaliukata huo mti na kuuacha. Matawi yake yalianguka juu ya milima na kwenye mabonde yote, vitawi vyake vikavunjika na kusambaa katika makorongo yote ya nchi. Mataifa yote ya duniani yakaondoka kutoka kwenye kivuli chake na kuuacha.

13 Ndege wote wa angani wakakaa kwenye ule mti ulioanguka na wanyama pori wote wakakaa katikati ya vitawi vyake.

14 Kamwe hakutakuwa na miti mingine kando ya hayo maji itakayorefuka zaidi ya huo, vilele vyake vikiwa juu ya majani yote ya miti. Hakuna miti mingine, hata kama imekunywa maji vizuri namna gani, itakayofikia urefu huo. Yote mwisho wake ni kifo, na kuingia ardhini, kama vile ilivyo kwa wanadamu, pamoja na wale waendao shimoni.

15 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Katika siku ile mwerezi uliposhushwa chini kaburininilizifunika chemchemi zenye maji mengi kwa maombolezo: Nilivizuia vijito vyake na wingi wa maji yake nikauzuia. Kwa sababu yake niliivika Lebanoni huzuni, nayo miti yote ya shambani ikanyauka.

16 Niliyafanya mataifa yatetemeke kwa kishindo cha kuanguka kwake wakati nilipoushusha chini kaburini pamoja na wale washukao shimoni. Ndipo miti yote ya Edeni, miti iliyo bora kuliko yote na iliyo mizuri sana ya Lebanoni, miti yote ile iliyokunywa maji vizuri, ilifarijika hapa duniani.

17 Wale walioishi katika kivuli chake, wale walioungana naye miongoni mwa mataifa, nao pia walikuwa wamezikwa pamoja naye, wakiungana na wale waliouawa kwa upanga.

18 “ ‘Ni miti ipi ya Edeni inayoweza kulinganishwa nawe kwa fahari na utukufu? Hata hivyo, wewe pia, utashushwa chini pamoja na miti ya Edeni mpaka kuzimu, utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.

“ ‘Huyu ni Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/31-2981f288694f100387272388ec45df59.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 32

Maombolezo Kwa Ajili Ya Farao

1 Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, neno laBwanalikanijia, kusema:

2 “Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie:

“ ‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa,

wewe ni kama joka kubwa baharini,

unayevuruga maji kwa miguu yako

na kuchafua vijito.

3 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Nikiwa pamoja na wingi mkubwa wa watu

nitautupa wavu wangu juu yako,

nao watakukokota katika wavu wangu.

4 Nitakutupa nchi kavu

na kukuvurumisha uwanjani.

Nitawafanya ndege wote wa angani watue juu yako

na wanyama wote wa nchi

watajishibisha nyama yako.

5 Nitatawanya nyama yako juu ya milima

na kujaza mabonde kwa mabaki yako.

6 Nitailowanisha nchi kwa damu yako inayotiririka

njia yote hadi milimani,

nayo mabonde yatajazwa na nyama yako.

7 Nitakapokuzimisha, nitafunika mbingu

na kuzitia nyota zake giza;

nitalifunika jua kwa wingu,

nao mwezi hautatoa nuru yake.

8 Mianga yote itoayo nuru angani

nitaitia giza juu yako;

nitaleta giza juu ya nchi yako,

asemaBwanaMwenyezi.

9 Nitaifadhaisha mioyo ya mataifa mengi

nitakapokuangamiza miongoni mwa mataifa,

nikikuleta uhamishoni miongoni mwa nchi

ambazo haujapata kuzijua.

10 Nitayafanya mataifa mengi wakustaajabie,

wafalme wao watatetemeka

kwa hofu kwa ajili yako

nitakapotikisa upanga wangu mbele yao.

Siku ya anguko lako

kila mmoja wao atatetemeka

kila dakika kwa ajili ya maisha yake.

11 “ ‘Kwa kuwa hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Upanga wa mfalme wa Babeli

utakuja dhidi yako.

12 Nitafanya makundi yako ya wajeuri kuanguka

kwa panga za watu mashujaa,

taifa katili kuliko mataifa yote.

Watakivunjavunja kiburi cha Misri,

nayo makundi yake yote

ya wajeuri yatashindwa.

13 Nitaangamiza mifugo yake yote

wanaojilisha kando ya maji mengi,

hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamu

wala kwato za mnyama

hazitayachafua tena.

14 Kisha nitafanya maji yake yatulie

na kufanya vijito vyake

vitiririke kama mafuta,

asemaBwanaMwenyezi.

15 Nitakapoifanya Misri kuwa ukiwa

na kuiondolea nchi kila kitu

kilichomo ndani yake,

nitakapowapiga wote waishio humo,

ndipo watakapojua kuwa

Mimi ndimiBwana.’

16 “Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote ya wajeuri wataliimba, asemaBwanaMwenyezi.”

17 Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi, neno laBwanalikanijia kusema:

18 “Mwanadamu, omboleza kwa ajili ya makundi ya wajeuri wa Misri na uwatupe kuzimu yeye na binti za mataifa yenye nguvu, waende huko pamoja nao washukao shimoni.

19 Je, ninyi mnamzidi nani kwa uzuri? Shukeni chini! Nanyi mkalazwe pamoja na hao wasiotahiriwa!

20 Wataanguka miongoni mwa wale waliouawa kwa upanga. Upanga umefutwa, mwache aburutwe mbali pamoja na hao wajeuri wake wote.

21 Kutoka kuzimu viongozi hodari watanena kuhusu Misri pamoja na wale walioungana nao, ‘Wameshuka chini, nao wamelala kimya pamoja na hao wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.’

22 “Ashuru yuko huko pamoja na jeshi lake lote, amezungukwa na makaburi ya watu wake wote waliouawa, wale wote walioanguka kwa upanga.

23 Makaburi yao yako kwenye kina cha chini cha shimo na jeshi lake limelala kulizunguka kaburi lake. Wote waliokuwa wameeneza hofu kuu katika nchi ya walio hai wameuawa, wameanguka kwa upanga.

24 “Elamu yuko huko, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote wameuawa, wameanguka kwa upanga. Wote waliokuwa wameeneza hofu katika nchi ya walio hai walishuka kuzimu bila kutahiriwa. Wanaichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni.

25 Kitanda kimetandikwa kwa ajili yake miongoni mwa waliouawa, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote ni watu wasiotahiriwa, wameuawa kwa upanga. Kwa sababu vitisho vyao vilienea katika nchi ya walio hai, wameichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni, nao wamewekwa miongoni mwa waliouawa.

26 “Mesheki na Tubali wako humo, pamoja na makundi yao ya wajeuri wakiwa wameyazunguka makaburi yao. Wote hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga kwa sababu walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai.

27 Je, hawakulala na mashujaa wengine wasiotahiriwa waliouawa, ambao wameshuka kaburini wakiwa na silaha zao za vita, ambao panga zao ziliwekwa chini ya vichwa vyao na uovu wao juu ya mifupa yao? Adhabu kwa ajili ya dhambi zao ilikuwa juu ya mifupa yao, ingawa vitisho vya mashujaa hawa vilikuwa vimeenea hadi kwenye nchi ya walio hai.

28 “Wewe pia, ee Farao, utavunjwa nawe utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.

29 “Edomu yuko humo, wafalme wake wote na wakuu wake wote, ambao ijapokuwa wana nguvu, wamelazwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga. Wamelala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale washukao shimoni.

30 “Wakuu wote wa kaskazini na Wasidoni wote wako huko, wameshuka chini pamoja na waliouawa kwa aibu ijapokuwa kuna vitisho vilivyosababishwa na nguvu zao. Wamelala bila kutahiriwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga na kuchukua aibu yao pamoja na wale washukao chini shimoni.

31 “Farao, yeye pamoja na jeshi lake lote, atakapowaona atafarijiwa kwa ajili ya makundi yake yote ya wajeuri, wale waliouawa kwa upanga, asemaBwanaMwenyezi.

32 Ingawa nilimfanya Farao aeneze vitisho vyake katika nchi ya walio hai, Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri watalazwa miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga, asemaBwanaMwenyezi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/32-f004430cd7113fc65cb6929eca50cbac.mp3?version_id=1627—