Categories
Isaya

Isaya 59

Dhambi, Toba Na Ukombozi

1 Hakika mkono waBwanasi mfupi hata usiweze kuokoa,

wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia.

2 Lakini maovu yenu yamewatenga

ninyi na Mungu wenu,

dhambi zenu zimewaficha ninyi uso wake,

ili asisikie.

3 Kwa maana mikono yenu imetiwa mawaa kwa damu

na vidole vyenu kwa hatia.

Midomo yenu imenena uongo,

nazo ndimi zenu zimenongʼona mambo maovu.

4 Hakuna hata mmoja anayedai kwa haki;

hakuna hata mmoja anayetetea shauri lake kwa haki.

Wanategemea mabishano matupu na kusema uongo,

huchukua mimba ya magomvi na kuzaa uovu.

5 Huangua mayai ya nyoka wenye sumu kali

na kutanda wavu wa buibui.

Yeyote alaye mayai yao atakufa,

na wakati moja lianguliwapo, nyoka hutoka humo.

6 Utando wao wa buibui haufai kwa nguo;

hawawezi kujifunika kwa kile walichokitengeneza.

Matendo yao ni matendo maovu,

vitendo vya jeuri vipo mikononi mwao.

7 Miguu yao hukimbilia kwenye dhambi,

ni myepesi kumwaga damu isiyo na hatia.

Mawazo yao ni mawazo maovu;

uharibifu na maangamizi huonekana katika njia zao.

8 Hawajui njia ya amani,

hakuna haki katika mapito yao.

Wameyageuza kuwa njia za upotovu,

hakuna apitaye njia hizo atakayeifahamu amani.

9 Hivyo uadilifu uko mbali nasi,

nayo haki haitufikii.

Tunatazamia nuru, kumbe! Yote ni giza,

tunatazamia mwanga, lakini tunatembea katika giza kuu.

10 Tunapapasa ukuta kama kipofu,

tunapapasa katika njia zetu kama watu wasio na macho.

Adhuhuri tunajikwaa kama wakati wa gizagiza;

katikati ya wenye nguvu, tuko kama wafu.

11 Wote tunanguruma kama dubu;

tunalia kwa maombolezo kama hua.

Tunatafuta haki, kumbe hakuna kabisa;

tunatafuta wokovu, lakini uko mbali.

12 Kwa sababu makosa yetu ni mengi machoni pako,

na dhambi zetu zinashuhudia dhidi yetu.

Makosa yetu yako pamoja nasi daima,

nasi tunayatambua maovu yetu:

13 Uasi na udanganyifu dhidi yaBwana,

kumgeuzia Mungu wetu kisogo,

tukichochea udhalimu na maasi,

tukinena uongo ambao mioyo yetu imeuhifadhi.

14 Hivyo uadilifu umerudishwa nyuma,

nayo haki inasimama mbali,

kweli imejikwaa njiani,

uaminifu hauwezi kuingia.

15 Kweli haipatikani popote,

na yeyote aepukaye uovu huwa mawindo.

Bwanaalitazama naye akachukizwa

kwamba hapakuwepo haki.

16 Aliona kuwa hakuwepo hata mtu mmoja,

akashangaa kwamba hakuwepo hata mmoja wa kuingilia kati;

hivyo mkono wake mwenyewe

ndio uliomfanyia wokovu,

nayo haki yake mwenyewe

ndiyo iliyomtegemeza.

17 Alivaa haki kama dirii kifuani mwake,

na chapeo ya wokovu kichwani mwake,

alivaa mavazi ya kisasi

naye akajifunga wivu kama joho.

18 Kulingana na kile walichokuwa wametenda,

ndivyo atakavyolipa

ghadhabu kwa watesi wake

na kisasi kwa adui zake,

atavilipa visiwa sawa na wanavyostahili.

19 Kuanzia magharibi, watu wataliogopa jina laBwana

na kuanzia mawio ya jua, watauheshimu utukufu wake.

Wakati adui atakapokuja kama mafuriko,

Roho waBwanaatainua kiwango dhidi yake na kumshinda.

20 “Mkombozi atakuja Sayuni,

kwa wale wa Yakobo

wanaozitubu dhambi zao,”

asemaBwana.

21 “Kwa habari yangu mimi, hili ndilo agano langu nao,” asemaBwana. “Roho wangu, aliye juu yenu, na maneno yangu ambayo nimeyaweka katika vinywa vyenu, havitaondoka vinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwa watoto wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao, kuanzia sasa na hata milele,” asemaBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/59-ecfce4b395d865a4f791bddcefdd149a.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 60

Utukufu Wa Sayuni

1 “Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja

na utukufu waBwanaumezuka juu yako.

2 Tazama, giza litaifunika dunia

na giza kuu litayafunika mataifa,

lakiniBwanaatazuka juu yako

na utukufu wake utaonekana juu yako.

3 Mataifa watakuja kwenye nuru yako

na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako.

4 “Inua macho yako na utazame pande zote:

Wote wanakusanyika na kukujia,

wana wako wanakuja toka mbali,

nao binti zako wanabebwa mikononi.

5 Ndipo utatazama na kutiwa nuru,

moyo wako utasisimka na kujaa furaha,

mali zilizo baharini zitaletwa kwako,

utajiri wa mataifa utakujilia.

6 Makundi ya ngamia yatajaa katika nchi yako,

ngamia vijana wa Midiani na Efa.

Nao wote watokao Sheba watakuja,

wakichukua dhahabu na uvumba

na kutangaza sifa zaBwana.

7 Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako,

kondoo dume wa Nebayothi watakutumikia,

watakubalika kama sadaka juu ya madhabahu yangu,

nami nitalipamba Hekalu langu tukufu.

8 “Ni nani hawa warukao kama mawingu,

kama hua kuelekea kwenye viota vyao?

9 Hakika visiwa vinanitazama,

merikebu za Tarshishindizo zinazotangulia,

zikiwaleta wana wenu kutoka mbali,

wakiwa na fedha na dhahabu zao,

kwa heshima yaBwana, Mungu wenu,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,

kwa maana amekujalia utukufu.

10 “Wageni watazijenga upya kuta zako,

na wafalme wao watakutumikia.

Ingawa katika hasira nilikupiga,

lakini katika upendeleo wangu

nitakuonyesha huruma.

11 Malango yako yatakuwa wazi siku zote,

kamwe hayatafungwa, mchana wala usiku,

ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa:

wafalme wao wakiongoza maandamano ya ushindi.

12 Kwa maana taifa au ufalme ule ambao hautakutumikia utaangamia;

utaharibiwa kabisa.

13 “Utukufu wa Lebanoni utakujilia,

msunobari, mvinje pamoja na mteashuri,

ili kupapamba mahali pangu patakatifu,

nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu.

14 Wana wa wale waliokuonea watakuja wakisujudu mbele yako,

wote wanaokudharau watasujudu kwenye miguu yako,

nao watakuita Mji waBwana,

Sayuni ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.

15 “Ingawa umeachwa na kuchukiwa,

bila yeyote anayesafiri ndani yako,

nitakufanya kuwa fahari ya milele,

na furaha ya vizazi vyote.

16 Utanyonya maziwa ya mataifa,

na kunyonyeshwa matiti ya wafalme.

Ndipo utakapojua kwamba Mimi,Bwana, ni Mwokozi wako,

Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.

17 Badala ya shaba nitakuletea dhahabu,

na fedha badala ya chuma.

Badala ya mti nitakuletea shaba,

na chuma badala ya mawe.

Nitafanya amani kuwa mtawala wako,

na haki kuwa mfalme wako.

18 Jeuri hazitasikika tena katika nchi yako,

wala maangamizi au uharibifu ndani ya mipaka yako,

lakini utaita kuta zako Wokovu,

na malango yako Sifa.

19 Jua halitakuwa tena nuru yako mchana,

wala mwangaza wa mwezi hautakuangazia,

kwa maanaBwanaatakuwa nuru yako ya milele,

naye Mungu wako atakuwa utukufu wako.

20 Jua lako halitazama tena,

nao mwezi wako hautafifia tena;

Bwanaatakuwa nuru yako milele,

nazo siku zako za huzuni zitakoma.

21 Ndipo watu wako wote watakuwa waadilifu,

nao wataimiliki nchi milele.

Wao ni chipukizi nililolipanda,

kazi ya mikono yangu,

ili kuonyesha utukufu wangu.

22 Aliye mdogo kwenu atakuwa elfu,

mdogo kuliko wote atakuwa taifa lenye nguvu.

Mimi ndimiBwana;

katika wakati wake nitayatimiza haya upesi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/60-adb772b686a020b5ab89ef6afd31c9f6.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 61

Mwaka Wa Upendeleo Wa Bwana

1 Roho waBwanaMwenyezi yu juu yangu,

kwa sababuBwanaamenitia mafuta

kuwahubiria maskini habari njema.

Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo,

kuwatangazia mateka uhuru wao,

na hao waliofungwa

habari za kufunguliwa kwao;

2 kutangaza mwaka waBwanauliokubaliwa,

na siku ya kisasi ya Mungu wetu,

kuwafariji wote waombolezao,

3 na kuwapa mahitaji

wale wanaohuzunika katika Sayuni,

ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu,

mafuta ya furaha badala ya maombolezo,

vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa.

Nao wataitwa mialoni ya haki,

pando laBwana,

ili kuonyesha utukufu wake.

4 Watajenga upya magofu ya zamani

na kupatengeneza mahali palipoachwa ukiwa zamani;

watafanya upya miji iliyoharibiwa,

iliyoachwa ukiwa kwa vizazi vingi.

5 Wageni watayachunga makundi yenu,

wageni watafanya kazi katika mashamba yenu,

na kutunza mashamba yenu ya mizabibu.

6 Nanyi mtaitwa makuhani waBwana,

mtaitwa watumishi wa Mungu wetu.

Mtakula utajiri wa mataifa,

nanyi katika utajiri wao mtajisifu.

7 Badala ya aibu yao

watu wangu watapokea sehemu maradufu,

na badala ya fedheha

watafurahia katika urithi wao;

hivyo watarithi sehemu maradufu katika nchi yao,

nayo furaha ya milele itakuwa yao.

8 “Kwa maana Mimi,Bwana, napenda haki,

na ninachukia unyangʼanyi na uovu.

Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao

na kufanya agano la milele nao.

9 Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa,

na uzao wao miongoni mwa kabila za watu.

Wale wote watakaowaona watatambua

kuwa ni taifa ambaloBwanaamelibariki.”

10 Ninafurahia sana katikaBwana,

nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu.

Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu,

na kunipamba kwa joho la haki,

kama vile bwana arusi apambavyo

kichwa chake kama kuhani,

na kama bibi arusi ajipambavyo

kwa vito vyake vya thamani.

11 Kwa maana kama vile ardhi ifanyavyo chipukizi kuota,

na bustani isababishavyo mbegu kuota,

ndivyoBwanaMwenyezi atafanya haki na sifa

zichipuke mbele ya mataifa yote.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/61-97beb3b5258f8abd70a3e59639a345a3.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 62

Jina Jipya La Sayuni

1 Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza,

kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia,

mpaka haki yake itakapoangaza kama mapambazuko,

wokovu wake kama mwanga wa moto.

2 Mataifa wataona haki yako,

nao wafalme wote wataona utukufu wako;

wewe utaitwa kwa jina jipya

lile ambalo kinywa chaBwanakitatamka.

3 Utakuwa taji ya fahari mkononi mwaBwana,

taji ya kifalme mkononi mwa Mungu wako.

4 Hawatakuita tena Aliyeachwa,

wala nchi yako kuiita Ukiwa.

Bali utaitwa Hefsiba,

nayo nchi yako itaitwa Beula,

kwa maanaBwanaatakufurahia,

nayo nchi yako itaolewa.

5 Kama vile kijana aoavyo mwanamwali,

ndivyo wanaowatakavyokuoa wewe;

kama bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi wake,

ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe.

6 Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, ee Yerusalemu,

hawatanyamaza mchana wala usiku.

Ninyi wenye kumwitaBwana,

msitulie,

7 msimwache apumzike hadi atakapoufanya imara Yerusalemu

na kuufanya uwe sifa ya dunia.

8 Bwanaameapa kwa mkono wake wa kuume

na kwa mkono wake wenye nguvu:

“Kamwe sitawapa tena adui zenu

nafaka zenu kama chakula chao;

kamwe wageni hawatakunywa tena

divai mpya ambayo mmeitaabikia,

9 lakini wale waivunao nafaka wataila

na kumsifuBwana,

nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yake

katika nyua za patakatifu pangu.”

10 Piteni, piteni katika malango!

Tengenezeni njia kwa ajili ya watu.

Jengeni, jengeni njia kuu!

Ondoeni mawe.

Inueni bendera kwa ajili ya mataifa.

11 Bwanaametoa tangazo

mpaka miisho ya dunia:

“Mwambie Binti Sayuni,

‘Tazama, mwokozi wako anakuja!

Tazama ujira wake uko pamoja naye,

na malipo yake yanafuatana naye!’ ”

12 Wataitwa Watu Watakatifu,

Waliokombolewa naBwana;

nawe utaitwa Aliyetafutwa,

Mji Usioachwa Tena.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/62-7cb6a6fcfd003392984c732ae7925927.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 63

Siku Ya Mungu Ya Kisasi Na Ukombozi

1 Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu,

kutoka Bosra, mwenye mavazi yaliyotiwa madoa mekundu?

Ni nani huyu, aliyevikwa joho la kifahari,

anayetembea kwa ukuu wa nguvu zake?

“Mimi ndimi, nisemaye katika haki,

mwenye nguvu wa kuokoa.”

2 Kwa nini mavazi yako ni mekundu,

kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu?

3 “Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu;

kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami.

Nimewaponda kwa miguu katika hasira yangu

na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu;

damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu,

na kutia madoa nguo zangu zote.

4 Kwa kuwa siku ya kisasi ilikuwa moyoni mwangu,

mwaka wa ukombozi wangu umefika.

5 Nilitazama, lakini hakuwepo yeyote wa kunisaidia,

nilishangaa kwa kuwa hakuwepo yeyote aliyetoa msaada;

hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu,

na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza.

6 Nilikanyaga mataifa kwa miguu katika hasira yangu,

katika ghadhabu yangu niliwalewesha,

na kumwaga damu yao juu ya ardhi.”

Kusifu Na Kuomba

7 Nitasimulia juu ya wema waBwana,

kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa,

sawasawa na yote ambayoBwana

ametenda kwa ajili yetu:

naam, mambo mengi mema aliyoyatenda

kwa ajili ya nyumba ya Israeli,

sawasawa na huruma zake

na wema wake mwingi.

8 Alisema, “Hakika wao ni watu wangu,

wana ambao hawatanidanganya”;

hivyo akawa Mwokozi wao.

9 Katika taabu zao zote naye alitaabika,

na malaika wa uso wake akawaokoa.

Katika upendo wake na rehema zake aliwakomboa,

akawainua na kuwachukua siku zote zilizopita.

10 Lakini waliasi,

na kumhuzunisha Roho Mtakatifu wake.

Hivyo aligeuka na kuwa adui yao,

na yeye mwenyewe akapigana dhidi yao.

11 Ndipo watu wake wakazikumbuka siku zilizopita,

siku za Mose na watu wake:

yuko wapi yeye aliyewaleta kupitia katikati ya bahari,

pamoja na wachungaji wa kundi lake?

Yuko wapi yule aliyeweka

Roho wake Mtakatifu katikati yao,

12 aliyetuma mkono wake uliotukuka wenye nguvu

kuwa katika mkono wa kuume wa Mose,

aliyegawa maji ya bahari mbele yao,

ili kujipatia jina milele,

13 aliyewaongoza kupitia kwenye vilindi?

Kama farasi katika nchi iliyo wazi,

wao hawakujikwaa,

14 kama ngʼombe washukao bondeni kwenye malisho,

walipewa pumziko na Roho waBwana.

Hivi ndivyo ulivyowaongoza watu wako

ili kujipatia mwenyewe jina tukufu.

15 Tazama chini kutoka mbinguni ukaone

kutoka kiti chako cha enzi

kilichoinuliwa juu, kitakatifu na kitukufu.

Uko wapi wivu wako na uweza wako?

Umetuzuilia wema wako na huruma zako.

16 Lakini wewe ni Baba yetu,

ingawa Abrahamu hatufahamu sisi

wala Israeli hatutambui;

wewe, EeBwana, ndiwe Baba yetu,

Mkombozi wetu tangu zamani za kale ndilo jina lako.

17 EeBwana, kwa nini unatuacha twende mbali na njia zako,

na kuifanya mioyo yetu migumu hata hatukukuheshimu?

Rudi kwa ajili ya watumishi wako,

yale makabila ambayo ni urithi wako.

18 Kwa maana kwa muda mfupi watu wako walimiliki mahali pako patakatifu,

lakini sasa adui zetu wamepakanyaga mahali patakatifu pako.

19 Sisi tumekuwa kama wale ambao hujawatawala kamwe,

kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/63-f03a29f94e7239bcc6f2674f5b9a1265.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 64

1 Laiti ungelipasua mbingu na kushuka chini,

ili milima ingelitetemeka mbele zako!

2 Kama vile moto uteketezavyo vijiti

na kusababisha maji kuchemka,

shuka ukafanye jina lako lijulikane kwa adui zako,

na kusababisha mataifa yatetemeke mbele zako!

3 Kwa maana ulipofanya mambo ya kutisha ambayo hatukuyatazamia,

ulishuka, nayo milima ikatetemeka mbele zako.

4 Tangu nyakati za zamani hakuna yeyote aliyesikia,

hakuna sikio lililotambua,

hakuna jicho lililomwona Mungu mwingine ila wewe,

anayetenda mambo kwa ajili ya wale wamngojeao.

5 Uliwasaidia watu wale watendao yaliyo haki kwa furaha,

wale wazikumbukao njia zako.

Lakini wakati tulipoendelea kutenda dhambi kinyume na njia zako,

ulikasirika.

Tutawezaje basi kuokolewa?

6 Sisi sote tumekuwa kama mtu aliye najisi,

nayo matendo yetu yote ya uadilifu ni kama matambaa machafu;

sisi sote tunasinyaa kama jani,

na kama upepo maovu yetu hutupeperusha.

7 Hakuna yeyote anayeliitia jina lako

wala anayejitahidi kukushika,

kwa kuwa umetuficha uso wako

na kutuacha tudhoofike kwa sababu ya dhambi zetu.

8 Lakini, EeBwana, wewe ndiwe Baba yetu.

Sisi ni udongo, wewe ndiye mfinyanzi;

sisi sote tu kazi ya mkono wako.

9 EeBwana, usikasirike kupita kiasi,

usizikumbuke dhambi zetu milele.

Ee Bwana, utuangalie, twakuomba,

kwa kuwa sisi sote tu watu wako.

10 Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa;

hata Sayuni ni jangwa, Yerusalemu ni ukiwa.

11 Hekalu letu takatifu na tukufu, mahali ambapo baba zetu walikusifu wewe,

limechomwa kwa moto,

navyo vitu vyote tulivyovithamini vimeharibika.

12 EeBwana, baada ya haya yote, utajizuia?

Je, utanyamaza kimya na kutuadhibu kupita kiasi?

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/64-c505bafdc93ede5028d0667993427f8b.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 65

Hukumu Na Wokovu

1 “Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia.

Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta.

Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu,

nilisema, ‘Niko hapa, niko hapa.’

2 Mchana kutwa nimeinyoosha mikono yangu

kwa watu wakaidi,

wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri,

wafuatao mawazo yao wenyewe:

3 taifa ambalo daima hunikasirisha

machoni pangu,

wakitoa dhabihu katika bustani

na kufukiza uvumba juu ya madhabahu za matofali;

4 watu waketio katikati ya makaburi

na kukesha mahali pa siri,

walao nyama za nguruwe,

nazo sufuria zao zina mchuzi wa nyama zilizo najisi,

5 wasemao, ‘Kaa mbali; usinikaribie,

kwa maana mimi ni mtakatifu mno kwako!’

Watu wa aina hiyo ni moshi katika pua zangu,

ni moto uwakao mchana kutwa.

6 “Tazama, jambo hili hubakia limeandikwa mbele zangu:

sitanyamaza, bali nitalipiza kwa ukamilifu;

nitalipiza mapajani mwao:

7 dhambi zenu na dhambi za baba zenu,”

asemaBwana.

“Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima

na kunichokoza mimi juu ya vilima,

nitawapimia mapajani mwao

malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.”

8 Hili ndilo asemaloBwana:

“Kama vile divai mpya ingali bado inapatikana

katika kishada cha zabibu,

nao watu husema, ‘Usikiharibu,

kwa kuwa bado kuna kitu kizuri ndani yake,’

hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu;

sitawaangamiza wote.

9 Nitawaleta wazao kutoka kwa Yakobo,

na kutoka kwa Yuda wale watakaomiliki milima yangu,

nao watu wangu wateule watairithi,

nako huko wataishi watumishi wangu.

10 Sharoni itakuwa malisho

kwa ajili ya makundi ya kondoo,

na Bonde la Akori mahali pa kupumzikia

kwa makundi ya ngʼombe,

kwa ajili ya watu wangu wanaonitafuta.

11 “Bali kwenu ninyi mnaomwachaBwana

na kuusahau mlima wangu mtakatifu,

ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati,

na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywa

kwa ajili ya Ajali,

12 nitawaagiza mfe kwa upanga,

nanyi nyote mtainama chini ili kuchinjwa;

kwa kuwa niliwaita lakini hamkuitika,

nilisema lakini hamkusikiliza.

Mlitenda maovu machoni pangu,

nanyi mkachagua mambo yale yanayonichukiza.”

13 Kwa hiyo hili ndilo asemaloBwanaMwenyezi:

“Watumishi wangu watakula,

lakini ninyi mtaona njaa;

watumishi wangu watakunywa

lakini ninyi mtaona kiu;

watumishi wangu watafurahi,

lakini ninyi mtaona haya.

14 Watumishi wangu wataimba

kwa furaha ya mioyo yao,

lakini ninyi mtalia

kutokana na uchungu wa moyoni,

na kupiga yowe kwa sababu

ya uchungu wa roho zenu.

15 Mtaliacha jina lenu

kuwa laana kwa watu wangu waliochaguliwa;

BwanaMwenyezi atawaua ninyi,

lakini watumishi wake atawapa jina jingine.

16 Yeye aombaye baraka katika nchi

atafanya hivyo kwa Mungu wa kweli;

yeye aapaye katika nchi

ataapa kwa Mungu wa kweli.

Kwa kuwa taabu za zamani zitasahaulika

na kufichwa kutoka machoni pangu.

Mbingu Mpya Na Dunia Mpya

17 “Tazama, nitaumba

mbingu mpya na dunia mpya.

Mambo ya zamani hayatakumbukwa,

wala hayatakuja akilini.

18 Lakini furahini na kushangilia daima

katika hivi nitakavyoumba,

kwa kuwa nitaumba Yerusalemu uwe wa kupendeza,

nao watu wake wawe furaha.

19 Nami nitaifurahia Yerusalemu

na kuwafurahia watu wangu;

sauti ya maombolezo na ya kilio

haitasikika humo tena.

20 “Kamwe hatakuwepo tena ndani yake

mtoto mchanga atakayeishi siku chache tu,

au mzee ambaye hataishi akatimiza miaka yake.

Yeye atakayekufa akiwa na umri wa miaka mia moja

atahesabiwa kwamba ni kijana tu,

yeye ambaye hatafika miaka mia moja,

atahesabiwa kuwa amelaaniwa.

21 Watajenga nyumba na kuishi ndani yake;

watapanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake.

22 Hawatajenga nyumba, nao watu wengine waishi ndani yake,

au kupanda mazao na wengine wale.

Kwa kuwa kama zilivyo siku za mti,

ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu,

wateule wangu watafurahia kwa siku nyingi

kazi za mikono yao.

23 Hawatajitaabisha kwa kazi bure,

wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga,

kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa naBwana,

wao na wazao wao pamoja nao.

24 Kabla hawajaita, nitajibu,

nao wakiwa katika kunena, nitasikia.

25 Mbwa mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja,

naye simba atakula nyasi kama maksai,

lakini mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka.

Hawatadhuru wala kuharibu

katika mlima wangu mtakatifu wote,”

asemaBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/65-b96d6a2c779da3ede40e458f972ec0be.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 66

Hukumu Na Matumaini

1 Hili ndilo asemaloBwana,

“Mbingu ni kiti changu cha enzi,

nayo dunia ni mahali pa kuweka miguu yangu.

Iko wapi nyumba mtakayoijenga kwa ajili yangu?

Mahali pangu pa kupumzikia patakuwa wapi?

2 Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote,

hivyo vikapata kuwepo?”

asemaBwana.

“Mtu huyu ndiye ninayemthamini:

yeye ambaye ni mnyenyekevu

na mwenye roho yenye toba,

atetemekaye asikiapo neno langu.

3 Lakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali

ni kama yeye auaye mtu,

na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo,

ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa.

Yeyote atoaye sadaka ya nafaka,

ni kama yule aletaye damu ya nguruwe,

na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu,

ni kama yule aabuduye sanamu.

Wamejichagulia njia zao wenyewe,

nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao.

4 Hivyo, mimi pia nitawachagulia mapigo makali,

nami nitaleta juu yao kile wanachokiogopa.

Kwa maana nilipoita, hakuna yeyote aliyejibu,

niliposema, hakuna yeyote aliyesikiliza.

Walifanya maovu machoni pangu

na kuchagua lile linalonichukiza.”

5 Sikieni neno laBwana,

ninyi mtetemekao kwa neno lake:

“Ndugu zenu wanaowachukia ninyi

na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema,

‘Bwanana atukuzwe,

ili tupate kuona furaha yenu!’

Hata sasa wataaibika.

6 Sikieni hizo ghasia kutoka mjini,

sikieni hizo kelele kutoka hekaluni!

Ni sauti yaBwanaikiwalipa adui zake

yote wanayostahili.

7 “Kabla hajasikia utungu, alizaa;

kabla hajapata maumivu,

alizaa mtoto mwanaume.

8 Ni nani amepata kusikia jambo kama hili?

Ni nani amepata kuona mambo kama haya?

Je, nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja,

au taifa laweza kutokea mara?

Mara Sayuni alipoona utungu,

alizaa watoto wake.

9 Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwa

na nisizalishe?” asemaBwana.

“Je, nifunge tumbo la uzazi

wakati mimi ndiye nizalishaye?”

asema Mungu wako.

10 “Shangilieni pamoja na Yerusalemu na mfurahi kwa ajili yake,

ninyi nyote mnaompenda,

shangilieni kwa nguvu pamoja naye,

ninyi nyote mnaoomboleza juu yake.

11 Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka

katika faraja ya matiti yake;

mtakunywa sana,

na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.”

12 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwana:

“Nitamwongezea amani kama mto,

nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho;

utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwake

na kubembelezwa magotini pake.

13 Kama mama anavyomfariji mtoto wake,

ndivyo nitakavyokufariji wewe,

nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.”

14 Wakati mtakapoona jambo hili, mioyo yenu itashangilia,

nanyi mtastawi kama majani;

mkono waBwanautajulikana kwa watumishi wake,

bali ghadhabu yake kali

itaonyeshwa kwa adui zake.

15 Tazama,Bwanaanakuja na moto,

magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli,

atateremsha hasira yake kwa ghadhabu kali,

na karipio lake pamoja na miali ya moto.

16 Kwa maana kwa moto na kwa upanga wake

Bwanaatatekeleza hukumu juu ya watu wote,

nao wengi watakuwa ni wale

waliouawa naBwana.

17 “Watu wote wanaojiweka wakfu na kujitakasa wenyewe ili kwenda bustanini, wakimfuata aliye katikati ya wale ambao hula nyama za nguruwe na panya pamoja na vitu vingine vilivyo machukizo, watafikia mwisho wao pamoja,” asemaBwana.

18 “Nami, kwa sababu ya matendo yao na mawazo yao, niko karibu kuja na kukusanya mataifa yote na lugha zote, nao watakuja na kuuona utukufu wangu.

19 “Nitaweka ishara katikati yao, nami nitapeleka baadhi ya hao walionusurika kwa mataifa, hadi Tarshishi, kwa Pulina Waludi (wanaojulikana kama wapiga upinde), kwa Tubali na Uyunani, hadi visiwa vya mbali ambavyo havijasikia juu ya sifa zangu au kuuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa.

20 Nao watawaleta ndugu zenu wote, kutoka mataifa yote, mpaka kwenye mlima wangu mtakatifu katika Yerusalemu kama sadaka kwaBwana, juu ya farasi, katika magari ya vita na magari makubwa, juu ya nyumbu na ngamia,” asemaBwana. “Watawaleta, kama Waisraeli waletavyo sadaka zao za nafaka, katika Hekalu laBwana, katika vyombo safi kwa kufuata desturi za ibada.

21 Nami nitachagua baadhi yao pia wawe makuhani na Walawi,” asemaBwana.

22 “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya ninazozifanya zitakavyodumu mbele zangu,” asemaBwana, “ndivyo jina lenu na wazao wenu watakavyodumu.

23 Kutoka Mwezi Mpya hata mwingine, na kutoka Sabato hadi nyingine, wanadamu wote watakuja na kusujudu mbele zangu,” asemaBwana.

24 “Nao watatoka nje na kuona maiti za wale walioniasi mimi. Funza wao hawatakufa, wala moto wao hautazimika, nao watakuwa kitu cha kuchukiza sana kwa wanadamu wote.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/66-d36be496ce49a45a4cc727d8e05ba436.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia Utangulizi

Utangulizi

Kitabu hiki kimepewa jina la Yeremia, mwana wa kuhani, aliyezaliwa katika kijiji cha Anathothi. Kitabu hiki kinatoa taarifa kwa kina na mtazamo wa kidini, na hali ya kisiasa katika Yuda kwenye kipindi cha miaka arobaini kabla ya kuharibiwa kwa Yerusalemu. Mengi yanajulikana kuhusu historia binafsi ya Yeremia kuliko nabii mwingine yeyote katika Agano la Kale. Yeremia, kama Isaya, alikuwa kijana ambaye aliitwa na Mungu kuionya Yuda juu ya uovu wake.

Kwa miaka 21 ya mwanzo ya huduma ya Yeremia, Yuda, chini ya utawala wa Yosia, walipata mwamko wa kisiasa na uamsho wa kiroho; wakati huo dola ya Waashuru ilikuwa inadidimia. Yeremia alipoanza huduma yake ya unabii 627 K.K., alipata miaka mizuri ya huduma yake hadi Yosia alipouawa mnamo 609 K.K.

Baada ya Yosia kufa, Yeremia alikuwa katika hatari kubwa kutoka kwa viongozi wa dini na wa kisiasa ambao walikasirishwa na ujumbe wake. Ingawa Yeremia alishauri Wayahudi wajitolee kwa Wababeli, wao waliasi. Hivyo mnamo mwaka wa 586 K.K., mji wa Yerusalemu pamoja na Hekalu lake vikaharibiwa, naye Yeremia akachukuliwa kwa nguvu na watu wa Yuda, wakaenda naye Misri.

Mwandishi

Nabii Yeremia.

Kusudi

Yeremia anawaita watu wa Mungu kugeuka kutoka dhambi zao na kumrudia Mungu.

Mahali

Yerusalemu.

Tarehe

627–586 K.K.

Wahusika Wakuu

Wafalme wa Yuda: Yosia, Yehoahazi, Yehoyakimu, Yehoyakini na Sedekia; Yeremia, Baruku, Ebed-Meleki, Mfalme Nebukadneza, Warekabi.

Wazo Kuu

Uovu usipotubiwa husababisha taifa, jamii, au mtu binafsi kuangamia.

Mambo Muhimu

Yeremia aliorodhesha dhambi za Yuda zote na kutoa unabii wa hukumu ya Mungu, na pia kuwaita watu watubu. Lakini watu waliendelea na maisha yao ya ubinafsi na kuabudu sanamu. Pia viongozi wote walikataa sheria ya Mungu, wakakubaliana na manabii wa uongo. Yerusalemu iliharibiwa, Hekalu likaachwa likiwa magofu, nao watu wakatekwa na kupelekwa uhamishoni Babeli. Ilipasa watu waajibike kwa ajili ya uharibifu na utekwaji huu uliosababishwa na wao kutosikia na kutotii ujumbe wa Mungu.

Mgawanyo

Wito wa Yeremia (

1:1-9

)

Hali ya dhambi ya Yuda (

2:1–6:30

)

Hekalu, sheria na agano (

7:1–12:17

)

Uhakika wa kutekwa (

13:1–18:23

)

Yeremia anakumbana na viongozi (

19:1–29:32

)

Ahadi ya kufanywa upya (

30:1–33:26

)

Ufalme unasambaratika (

34:1–39:18

)

Safari ya kwenda Misri (

40:1–45:5

)

Jumbe kuhusu mataifa ya kigeni (

46:1–51:64

)

Kuanguka kwa Yerusalemu (

52:1-34

).

Categories
Yeremia

Yeremia 1

1 Maneno ya Yeremia mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani katika mji wa Anathothi, katika nchi ya Benyamini.

2 Neno laBwanalilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda,

3 na pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa uhamishoni.

Wito Wa Yeremia

4 Neno laBwanalilinijia, kusema,

5 “Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua;

kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum;

nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.”

6 Nami nikasema, “Aa,BwanaMwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.”

7 LakiniBwanaakaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza.

8 Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asemaBwana.

9 KishaBwanaakaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako.

10 Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.”

11 Neno laBwanalikanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?”

Nami nikajibu, “Naona tawi la mti wa mlozi.”

12 Bwanaakaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba limetimizwa.”

13 Neno laBwanalikanijia tena, “Unaona nini?”

Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.”

14 Bwanaakaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote waishio katika nchi.

15 Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asemaBwana.

“Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya enzi

katika maingilio ya malango ya Yerusalemu,

watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka,

na dhidi ya miji yote ya Yuda.

16 Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu

kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi,

kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine

na kuabudu kile ambacho mikono yao imekitengeneza.

17 “Jiandae! Simama useme chochote nitakachokuamuru. Usiwaogope, la sivyo nitakufanya uwaogope wao.

18 Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma, na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo.

19 Watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa kuwa niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,” asemaBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/1-95955986344391729205a4da72b0ed63.mp3?version_id=1627—