Categories
Zekaria

Zekaria 10

Bwana Ataitunza Yuda

1 MwombeniBwanamvua wakati wa vuli;

ndiyeBwanaatengenezaye mawingu ya tufani.

Huwapa watu manyunyu ya mvua,

pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.

2 Sanamu huzungumza udanganyifu,

waaguzi huona maono ya uongo;

husimulia ndoto ambazo si za kweli,

wanatoa faraja batili.

Kwa hiyo watu wanatangatanga kama kondoo

walioonewa kwa kukosa mchungaji.

3 “Hasira yangu inawaka dhidi ya wachungaji,

nami nitawaadhibu viongozi;

kwa kuwaBwanaMwenye Nguvu Zote

atalichunga kundi lake,

nyumba ya Yuda,

naye atawafanya kuwa kama farasi

mwenye kiburi akiwa vitani.

4 Kutoka Yuda litatokea Jiwe la pembeni,

kutoka kwake vitatoka vigingi vya hema,

kutoka kwake utatoka upinde wa vita,

kutoka kwake atatoka kila mtawala.

5 Kwa pamoja watakuwa kama mashujaa

wanaokanyaga barabara za matope

wakati wa vita.

Kwa sababuBwanayu pamoja nao,

watapigana na kuwashinda wapanda farasi.

6 “Nitaiimarisha nyumba ya Yuda

na kuiokoa nyumba ya Yosefu.

Nitawarejesha kwa sababu

nina huruma juu yao.

Watakuwa kama watu ambao

sijawahi kuwakataa

kwa sababu mimi ndimiBwanaMungu wao,

nami nitawajibu.

7 Waefraimu watakuwa kama mashujaa,

mioyo yao itafurahi kana kwamba ni kwa divai.

Watoto wao wataona na kufurahi,

mioyo yao itashangilia katikaBwana.

8 Nitawaashiria na kuwakusanya ndani.

Hakika nitawakomboa,

nao watakuwa wengi

kama walivyokuwa mwanzoni.

9 Ijapokuwa niliwatawanya miongoni mwa mataifa,

hata hivyo wakiwa katika nchi za mbali

watanikumbuka mimi.

Wao na watoto wao watanusurika katika hatari

nao watarudi.

10 Nitawarudisha kutoka Misri

na kuwakusanya toka Ashuru.

Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni,

na hapo hapatakuwa na nafasi ya kuwatosha.

11 Watapita katika bahari ya mateso;

bahari iliyochafuka itatulizwa

na vilindi vyote vya Mto Naili vitakauka.

Kiburi cha Ashuru kitashushwa,

nayo fimbo ya utawala ya Misri itatoweka.

12 Nitawaimarisha katikaBwana,

na katika jina lake watatembea,”

asemaBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/10-7ec337ae9edf5ebc6d71d1068febb350.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 11

1 Fungua milango yako, ee Lebanoni,

ili moto uteketeze mierezi yako!

2 Piga yowe, ee mti wa msunobari,

kwa kuwa mwerezi umeanguka;

miti ya fahari imeharibiwa!

Piga yowe, enyi mialoni ya Bashani,

msitu mnene umefyekwa!

3 Sikiliza yowe la wachungaji;

malisho yao manono yameangamizwa!

Sikia ngurumo za simba;

kichaka kilichostawi sana

cha Yordani kimeharibiwa!

Wachungaji Wawili Wa Kondoo

4 Hili ndilo asemaloBwanaMungu wangu: “Lilishe kundi lililokusudiwa kuchinjwa.

5 Wanunuzi wake huwachinja na kuondoka pasipo kuadhibiwa. Wale wanaowauza husema, ‘Bwanaasifiwe, mimi ni tajiri!’ Wachungaji wao wenyewe hawawahurumii.

6 Kwa kuwa sitawahurumia tena watu wa nchi,” asemaBwana. “Nitawakabidhi kila mtu mkononi mwa jirani yake na mfalme wake. Wataitenda jeuri nchi, nami sitawaokoa kutoka mikononi mwao.”

7 Kwa hiyo nikalilisha kundi lililotiwa alama kwa kuchinjwa, hasa kundi lililoonewa sana. Kisha nikachukua fimbo mbili, moja nikaiita Fadhili na nyingine Umoja, nami nikalilisha kundi.

8 Katika mwezi mmoja nikawaondoa wachungaji watatu.

Kundi la kondoo likanichukia, nami nikachoshwa nao,

9 nikasema, “Sitakuwa mchungaji wenu. Waache wanaokufa wafe na wanaoangamia waangamie. Wale waliobakia kila mmoja na ale nyama ya mwenzake.”

10 Kisha nikachukua fimbo yangu inayoitwa Fadhili nikaivunja, kutangua Agano nililofanya na mataifa yote.

11 Likatanguka siku hiyo, kwa hiyo wale waliodhurika katika kundi, waliokuwa wakiniangalia wakajua kuwa hilo lilikuwa neno laBwana.

12 Nikawaambia, “Mkiona kuwa ni vyema, nipeni ujira wangu, la sivyo, basi msinipe.” Kwa hiyo wakanilipa vipande thelathini vya fedha.

13 NayeBwanaakaniambia, “Mtupie mfinyanzi,” hiyo bei nzuri waliyonithaminia! Kwa hiyo nikachukua hivyo vipande thelathini vya fedha na kumtupia huyo mfinyanzi katika nyumba yaBwana.

14 Kisha nikaivunja fimbo yangu ya pili iitwayo Umoja, kuvunja undugu kati ya Yuda na Israeli!

15 KishaBwanaakaniambia, “Vitwae tena vifaa vya mchungaji mpumbavu.

16 Kwa maana ninakwenda kumwinua mchungaji juu ya nchi ambaye hatamjali aliyepotea, wala kuwatafuta wale wachanga au kuwaponya waliojeruhiwa, wala kuwalisha wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo wanono na kuzirarua kwato zao.

17 “Ole wa mchungaji asiyefaa,

anayeliacha kundi!

Upanga na uupige mkono wake na jicho lake la kuume!

Mkono wake na unyauke kabisa,

jicho lake la kuume lipofuke kabisa!”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/11-0b5e697f06c9d0abe484dd4a4beb0ab5.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 12

Maadui Wa Yerusalemu Kuangamizwa

1 Hili ni neno laBwanakuhusu Israeli.Bwana, yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema:

2 “Nitakwenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbisha mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia.

3 Katika siku hiyo, wakati mataifa yote ya dunia yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya Yerusalemu kuwa jabali lisilosogezwa kwa mataifa yote. Wote watakaojaribu kulisogeza watajiumiza wenyewe.

4 Katika siku hiyo nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye ampandaye nitampiga kwa uwazimu,” asemaBwana. “Nitalielekeza jicho langu la ulinzi juu ya nyumba ya Yuda, nami nitawapofusha farasi wote wa mataifa.

5 Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababuBwanaMwenye Nguvu Zote ni Mungu wao.’

6 “Katika siku hiyo nitawafanya viongozi wa Yuda kuwa kama kigae cha moto ndani ya lundo la kuni, kama mwenge uwakao kati ya miganda. Watateketeza kulia na kushoto mataifa yote yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki salama mahali pake.

7 “Bwanaatayaokoa makao ya Yuda kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa zaidi kuliko ile ya Yuda.

8 Katika siku hiyo,Bwanaatawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika waBwanaakiwatangulia.

9 Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu.

Kumwombolezea Yule Aliyechomwa Mkuki

10 “Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neemana maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.

11 Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido.

12 Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi na wake zao, ukoo wa nyumba ya Nathani na wake zao,

13 ukoo wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao,

14 na koo zote zilizobaki na wake zao.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/12-45113d9771af5d9b045bd9d1bcff06e4.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 13

Kutakaswa Dhambi

1 “Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi.

2 “Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi.

3 Ikiwa yupo yeyote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina laBwana.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo.

4 “Katika siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la kinabii la nywele ili apate kudanganya watu.

5 Atasema, ‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima; ardhi imekuwa kazi yangu tangu ujana wangu.’

6 Ikiwa mtu atamuuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni majeraha niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu.’

Mchungaji Apigwa, Nao Kondoo Watawanyika

7 “Amka, ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu,

dhidi ya mtu aliye karibu nami!”

asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

“Mpige mchungaji,

nao kondoo watatawanyika,

nami nitageuza mkono wangu

dhidi ya walio wadogo,

8 katika nchi yote,” asemaBwana,

“theluthi mbili watapigwa na kuangamia;

hata hivyo theluthi moja watabaki ndani yake.

9 Hii theluthi moja nitaileta katika moto;

nitawasafisha kama fedha isafishwavyo

na kuwajaribu kama dhahabu.

Wataliitia Jina langu

nami nitawajibu;

nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’

nao watasema, ‘Bwanani Mungu wetu.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/13-e23899078fb1e45117b740bf03ba066c.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 14

Bwana Yuaja Kutawala

1 Siku yaBwanainakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu.

2 Nitayakusanya mataifa yote huko Yerusalemu kupigana dhidi yake, mji utatekwa, nyumba zitavamiwa na kuporwa na wanawake watanajisiwa. Nusu ya mji watakwenda uhamishoni, lakini watakaobaki hawataondolewa kutoka mjini.

3 KishaBwanaatatoka na kupigana dhidi ya watu wa yale mataifa, kama apiganavyo siku ya vita.

4 Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini.

5 Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. KishaBwanaMungu wangu atakuja na watakatifu wote pamoja naye.

6 Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji.

7 Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo naBwana. Jioni inapofika nuru itakuwepo.

8 Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki,na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibiwakati wa kiangazi na wakati wa masika.

9 Bwanaatakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepoBwanammoja na jina lake litakuwa jina pekee.

10 Nchi yote kuanzia Geba, kaskazini mwa Yuda, hadi Rimoni, kusini mwa Yerusalemu, itakuwa kama Araba.Lakini Yerusalemu utainuliwa juu na kubaki mahali pake, toka Lango la Benyamini hadi mahali pa Lango la Kwanza, mpaka kwenye Lango la Pembeni na kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye mashinikizo ya divai ya mfalme.

11 Utakaliwa na watu, kamwe hautaharibiwa tena, Yerusalemu utakaa salama.

12 Hii ndiyo tauni ambayoBwanaatapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao.

13 Katika siku hiyoBwanaatawatia wanaume hofu kuu. Kila mwanaume atakamata mkono wa mwenzake nao watashambuliana.

14 Yuda pia atapigana katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka Yerusalemu utakusanywa, wingi wa dhahabu, fedha na nguo.

15 Tauni ya aina iyo hiyo itapiga farasi na nyumbu, ngamia na punda, nao wanyama wote walioko kwenye kambi za adui.

16 Kisha walionusurika katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme,BwanaMwenye Nguvu Zote na kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.

17 Ikiwa taifa lolote la dunia hawatakwenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme,BwanaMwenye Nguvu Zote, mvua haitanyesha kwao.

18 Ikiwa watu wa Misri nao hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua.Bwanaataleta juu yao tauni ile ambayo itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.

19 Hii itakuwa adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale ambayo hayatakwenda Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.

20 Katika siku hiyo, kengele zilizofungwa kwenye farasi zitaandikwa maneno haya:Takatifu kwa Bwana, navyo vyungu vya kupikia katika nyumba yaBwanavitakuwa kama bakuli takatifu mbele ya madhabahu.

21 Kila chungu kilichoko Yerusalemu na Yuda kitakuwa kitakatifu kwaBwanaMwenye Nguvu Zote na wote wanaokuja kutoa dhabihu watachukua baadhi ya vyungu hivyo na kupikia. Katika siku hiyo hatakuwepo tena mfanyabiashara katika nyumba yaBwanaMwenye Nguvu Zote.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/14-698a795a95f1f16342cf6326c69ea23d.mp3?version_id=1627—