Categories
Zekaria

Zekaria Utangulizi

Utangulizi

Maana ya jina Zekaria ni “

Bwana

amekumbuka.” Yaonekana kama alikuwa kijana wakati alipoanza huduma yake. Zekaria aliwaonya watu waliokuwa wameanza kujenga upya Hekalu kwamba iliwapasa kusikiliza ujumbe wa Mungu kupitia kwa manabii. Aliwahimiza kudumisha uhusiano wa muhimu na Mungu ili wasiiharakishe hukumu ya Mungu. Mfululizo wa maono yalikuwa ya kuwatia moyo wajenzi katika wakati mgumu. Mtazamo wa jumla wa mafunzo wa maono haya manane yaliwahakikishia wajenzi kwamba Mungu alikuwa na mpango wa muda mrefu kwa ajili ya Israeli.

Sehemu ya mwisho wa huduma yake, Zekaria alikazia mpango wa maendeleo wa muda mrefu akionyesha kusimamishwa kwa ufalme wa mwisho. Mfalme anatambulishwa kama anayekuja kwa unyenyekevu akileta wokovu lakini akikataliwa na watu wake mwenyewe, yaani, Waisraeli, ambao baadaye wanaachwa kwenye hukumu ya mataifa. Mataifa yatakapokusanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Yerusalemu, Waisraeli watamtambua Masiya na wataibuka na ushindi, nayo mataifa yote yatakuja Yerusalemu kumwabudu Mfalme.

Mwandishi

Zekaria.

Kusudi

Kuwapa watu wa Mungu matumaini kwa kuwajulisha watu mpango wa Mungu wa baadaye wa ukombozi kupitia kwa Masiya.

Mahali

Yerusalemu.

Tarehe

Sura 1-8 kati ya 520–518 K.K.; sura 9-14 mwaka wa 480 K.K.

Wahusika Wakuu

Zekaria, Zerubabeli, Yoshua na waliorudi kutoka uhamishoni.

Wazo Kuu

Zekaria anaonyesha kwamba Mungu ana mpango wa muda mrefu na Israeli, hivyo anaita watu kwa mwito wa utii. Anaonyesha jinsi watu wanaweza kufanya mambo kwa Roho wa Mungu.

Mambo Muhimu

Zekaria alieleza juu ya hukumu ya Mungu dhidi ya maadui wa Israeli, baraka kwa ajili ya Yerusalemu, na umuhimu wa watu wa Mungu kudumu katika utakatifu. Mungu atawahukumu adui wa Israeli na Mfalme (Masiya) atakuja.

Mgawanyo

Utangulizi (

1:1-6

)

Maono nane ya kinabii (

1:7–6:8

)

Kutawazwa kwa Yoshua kinabii (

6:9-15

)

Jumbe mbali mbali za hukumu na matumaini (

7:1–10:12

)

Kuja kwa Masiya na kukataliwa kwake (

11:1–13:9

)

Ushindi mwishowe wa Masiya (

14:1-21

).

Categories
Zekaria

Zekaria 1

Wito Wa Kumrudia Bwana

1 Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno laBwanalilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia, mwana wa Ido, kusema:

2 “Bwanaaliwakasirikia sana baba zako wa zamani.

3 Kwa hiyo waambie watu: Hivi ndivyoBwanaMwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Nirudieni mimi,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, ‘nami nitawarudia ninyi,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

4 Msiwe kama baba zenu, ambao manabii waliotangulia waliwatangazia: Hivi ndivyoBwanaMwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asemaBwana.

5 Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je, wanaishi milele?

6 Je, maneno yangu na amri zangu nilizowaagiza manabii watumishi wangu, hayakuwapata baba zenu?”

“Kisha walitubu na kusema, ‘BwanaMwenye Nguvu Zote ametutenda sawasawa na njia zetu na matendo yetu yalivyostahili, kama alivyokusudia kufanya.’ ”

Maono Ya Kwanza: Mtu Katikati Ya Miti Ya Mihadasi

7 Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, yaani mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno laBwanalilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia mwana wa Ido.

8 Wakati wa usiku nilipata maono, mbele yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na weupe.

9 Nikauliza, “Hivi ni vitu gani bwana wangu?”

Malaika aliyekuwa akizungumza na mimi akanijibu, “Nitakuonyesha kuwa ni nini.”

10 Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti ya mihadasi akaeleza, “Ni wale ambaoBwanaamewatuma waende duniani kote.”

11 Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika waBwana, aliyekuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi, “Tumepita duniani kote na kukuta ulimwengu wote umepumzika kwa amani.”

12 Kisha malaika waBwanaakasema, “BwanaMwenye Nguvu Zote, utazuia mpaka lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?”

13 Kwa hiyoBwanaakazungumza maneno ya upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza nami.

14 Kisha malaika yule aliyekuwa akizungumza nami akasema, “Tangaza neno hili: Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nina wivu sana kwa ajili ya Yerusalemu na Sayuni,

15 lakini nimeyakasirikia sana mataifa yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa nimewakasirikia Israeli kidogo tu, lakini mataifa hayo yaliwazidishia maafa.’

16 “Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyoBwana: ‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyooshwa Yerusalemu,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

17 “Endelea kutangaza zaidi kwamba: Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote: ‘Miji yangu itafurika tena ustawi naBwanaatamfariji tena Sayuni na kumchagua Yerusalemu.’ ”

Maono Ya Pili: Pembe Nne Na Mafundi Wanne

18 Kisha nikatazama juu, na pale mbele yangu nikaona pembe nne!

19 Nikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini hivi?”

Akanijibu, “Hizi ni zile pembe zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu.”

20 KishaBwanaakanionyesha mafundi wanne.

21 Nikauliza, “Hawa wanakuja kufanya nini?”

Akanijibu, “Hizi ndizo pembe zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/1-820ed10f4b850a2f4b472d51dc147d9d.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 2

Maono Ya Tatu: Mtu Mwenye Kamba Ya Kupimia

1 Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake!

2 Nikamuuliza, “Unakwenda wapi?”

Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.”

3 Kisha malaika aliyekuwa akizungumza nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye

4 na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo.

5 Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka,’ asemaBwana, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’

6 “Njooni! Njooni! Kimbieni mtoke katika nchi ya kaskazini,” asemaBwana, “Kwa kuwa nimewatawanya kwenye pande nne za mbingu,” asemaBwana.

7 “Njoo, ee Sayuni! Kimbia, wewe ukaaye ndani ya Binti Babeli!”

8 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote: “Baada ya yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya mataifa yaliyokuteka nyara, kwa kuwa yeyote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho lake,

9 hakika nitauinua mkono wangu dhidi yao ili watumwa wao wawateke nyara. Ndipo mtakapojua ya kwambaBwanaMwenye Nguvu Zote amenituma.

10 “Piga kelele na ufurahie, ee Binti Sayuni, kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni mwenu,” asemaBwana.

11 “Mataifa mengi yataunganishwa naBwanasiku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu nanyi mtajua kwambaBwanaMwenye Nguvu Zote amenituma kwenu.

12 Bwanaatairithi Yuda kama fungu lake katika nchi takatifu na atachagua tena Yerusalemu.

13 Tulieni mbele zaBwana, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka kutoka makao yake matakatifu.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/2-06be10e5a99c4aa4dc8c4b6f42a72993.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 3

Maono Ya Nne: Mavazi Safi Kwa Ajili Ya Kuhani Mkuu

1 Kisha akanionyesha Yoshua,kuhani mkuu, akiwa amesimama mbele ya malaika waBwana, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshtaki.

2 Bwanaakamwambia Shetani, “Bwanaakukemee Shetani!Bwana, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?”

3 Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika.

4 Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, “Mvueni hizo nguo zake chafu.”

Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.”

5 Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.” Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika waBwanaakiwa amesimama karibu.

6 Malaika waBwanaakamwamuru Yoshua:

7 “Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa.

8 “ ‘Sikiliza, ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu walio ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi.

9 Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja.

10 “ ‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/3-c64274bd8a3b66d89d3b97fa83c4bb8b.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 4

Maono Ya Tano: Kinara Cha Taa Cha Dhahabu Na Mizeituni Miwili

1 Kisha malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka usingizi wake.

2 Akaniuliza, “Unaona nini?”

Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake.

3 Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa bakuli na mwingine upande wa kushoto.”

4 Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami, “Hivi ni vitu gani, bwana wangu?”

5 Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?”

Nikajibu, “Hapana, bwana wangu.”

6 Kisha akaniambia, “Hili ni neno laBwanakwa Zerubabeli: ‘Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

7 “Wewe ni kitu gani, ee mlima mkubwa sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la mwisho na watu wakipiga kelele wakisema, ‘Mungu libariki! Mungu libariki!’ ”

8 Kisha neno laBwanalikanijia:

9 “Mikono ya Zerubabeli iliweka msingi wa Hekalu hili, mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya kuwaBwanaMwenye Nguvu Zote amenituma mimi kwenu.

10 “Ni nani anayeidharau siku ya mambo madogo? Watu watashangilia watakapoona timazi mkononi mwa Zerubabeli.

“(Hizi saba ni macho yaBwanaambayo huzunguka duniani kote.)”

11 Kisha nikamuuliza yule malaika, “Hii mizeituni miwili iliyoko upande wa kuume na wa kushoto wa kinara cha taa ni nini?”

12 Tena nikamuuliza, “Haya matawi mawili ya mizeituni karibu na hiyo mirija miwili ya dhahabu inayomimina mafuta ya dhahabu ni nini?”

13 Akajibu, “Hujui kuwa haya ni nini?”

Nikamjibu, “Hapana, bwana wangu.”

14 Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia Bwana wa dunia yote.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/4-51d0f1bc6012e8fa94020756f8a1cb5a.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 5

Maono Ya Sita: Kitabu Kinachoruka

1 Nikatazama tena: na hapo mbele yangu kulikuwa na kitabu kilichoruka!

2 Akaniuliza, “Unaona nini?”

Nikamjibu, “Naona kitabu kinachoruka chenye, urefu wa dhiraa ishirinina upana wa dhiraa kumi.”

3 Akaniambia, “Hii ni laana inayotoka kwenda juu ya nchi yote, kwa kuwa kufuatana na yale yaliyoandikwa katika upande mmoja, kila mwizi atafukuziwa mbali, pia kufuatana na yaliyo upande wa pili, kila aapaye kwa uongo atafukuziwa mbali.

4 BwanaMwenye Nguvu Zote asema, ‘Nitaituma hiyo laana, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi na nyumba ya huyo aapaye kwa uongo kwa Jina langu. Itabaki katika nyumba yake na kuiharibu, pamoja na mbao zake na mawe yake.’ ”

Maono Ya Saba: Mwanamke Ndani Ya Kikapu

5 Kisha yule malaika aliyekuwa akizungumza nami akanijia na kuniambia, “Tazama juu uone ni nini kile kinachojitokeza.”

6 Nikamuuliza, “Ni kitu gani?”

Akanijibu, “Ni kikapu cha kupimia.” Kisha akaongeza kusema, “Huu ni uovu wa watu katika nchi nzima.”

7 Kisha kifuniko kilichotengenezwa kwa madini ya risasi kilichokuwa kimefunika kile kikapu, kiliinuliwa na ndani ya kile kikapu alikuwako mwanamke ameketi!

8 Akasema, “Huu ni uovu,” tena akamsukumia ndani ya kikapu na kushindilia kifuniko juu ya mdomo wa kikapu.

9 Kisha nikatazama juu: na pale mbele yangu, walikuwepo wanawake wawili, wakiwa na upepo katika mabawa yao! Walikuwa na mabawa kama ya korongo, nao wakainua kile kikapu na kuruka nacho kati ya mbingu na nchi.

10 Nikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Wanakipeleka wapi hicho kikapu?”

11 Akanijibu, “Wanakipeleka katika nchi ya Babeli na kujenga nyumba kwa ajili yake. Itakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa pale mahali pake.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/5-031fb2a0523b1a93f0ac97c4c8da5cd7.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 6

Maono Ya Nane: Magari Manne Ya Vita

1 Nikatazama juu tena: nikaona mbele yangu magari manne ya vita yakija kutoka kati ya milima miwili, milima ya shaba!

2 Gari la kwanza lilivutwa na farasi wekundu, la pili lilivutwa na farasi weusi,

3 la tatu lilivutwa na farasi weupe na gari la nne lilivutwa na farasi wa madoadoa ya kijivu, wote wenye nguvu.

4 Nikamuuliza malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Hawa ni nani bwana wangu?”

5 Malaika akanijibu, “Hizi ni roho nne za mbinguni zisimamazo mbele ya uwepo wa Bwana wa dunia yote, zinatoka kwenda kufanya kazi yake.

6 Gari linalovutwa na farasi weusi linaelekea katika nchi ya kaskazini, la farasi weupe linaelekea magharibi na la farasi wa madoadoa ya kijivu linaelekea kusini.”

7 Wakati hao farasi wenye nguvu walipokuwa wakitoka, walikuwa wakijitahidi kwenda duniani kote. Akasema, “Nenda duniani kote!” Kwa hiyo wakaenda duniani kote.

8 Kisha akaniita, “Tazama, wale wanaokwenda kuelekea nchi ya kaskazini wamepumzisha Roho yangu katika nchi ya kaskazini.”

Taji Kwa Ajili Ya Yoshua

9 Neno laBwanalikanijia kusema:

10 “Chukua fedha na dhahabu kutoka kwa watu waliohamishwa, yaani Heldai, Tobia na Yedaya ambao wamefika kutoka Babeli. Siku iyo hiyo nenda nyumbani kwa Yosia mwana wa Sefania.

11 Chukua fedha na dhahabu utengeneze taji, nawe uiweke kichwani mwa kuhani mkuu Yoshua, mwana wa Yehosadaki.

12 Umwambie, hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: ‘Huyu ndiye mtu ambaye jina lake ni Tawi, naye atachipua kutoka mahali pake na kujenga Hekalu laBwana.

13 Ni yeye atakayejenga Hekalu laBwana, naye atavikwa utukufu na ataketi kumiliki katika kiti cha enzi naye atakuwa kuhani katika kiti chake cha enzi. Hapo patakuwa amani kati ya hao wawili.’

14 Taji itatolewa kwa Heldai, Tobia, Yedaya na Heni mwana wa Sefania kama kumbukumbu ndani ya Hekalu laBwana.

15 Wale walio mbali sana watakuja na kusaidia kulijenga Hekalu laBwana, nanyi mtajua ya kwambaBwanaMwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. Hili litatokea ikiwa mtamtiiBwanaMungu wenu kwa bidii.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/6-37bf2cdc07051c6c342943793dc898da.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 7

Haki Na Rehema, Sio Kufunga

1 Katika mwaka wa nne wa utawala wa Mfalme Dario, neno laBwanalilimjia Zekaria siku ya nne ya mwezi wa tisa, mwezi wa Kisleu.

2 Watu wa Betheli walikuwa wamemtuma Shareza na Regem-Meleki pamoja na watu wao, kumsihiBwana

3 kwa kuwauliza makuhani wa nyumba yaBwanaMwenye Nguvu Zote na manabii, “Je, imempasa kuomboleza na kufunga katika mwezi wa tano, kama ambavyo nimekuwa nikifanya kwa miaka mingi?”

4 Kisha neno laBwanaMwenye Nguvu Zote likanijia kusema:

5 “Waulize watu wote wa nchi na makuhani, ‘Je, mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba kwa miaka sabini iliyopita, mlifunga kweli kwa ajili yangu?

6 Na mlipokuwa mkila na kunywa, je, hamkuwa mnasherehekea kwa ajili ya nafsi zenu?

7 Je, haya sio maneno yaBwanaaliyosema kupitia manabii waliotangulia, wakati Yerusalemu pamoja na miji inayoizunguka ilipokuwa katika hali ya utulivu na ya mafanikio, wakati Negebu na Shefala zikiwa zimekaliwa na watu?’ ”

8 Neno laBwanalikamjia tena Zekaria:

9 “Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote: ‘Fanyeni hukumu za haki, onyesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi.

10 Msimwonee mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’

11 “Lakini wakakataa kusikiliza, wakanipa kisogo kwa ukaidi na kuziba masikio yao.

12 Wakaifanya mioyo yao migumu kama jiwe gumu na hawakuisikiliza sheria au maneno ambayoBwanaMwenye Nguvu Zote aliyatuma kwa njia ya Roho wake kupitia manabii waliotangulia. Kwa hiyoBwanaMwenye Nguvu Zote alikasirika sana.

13 “ ‘Wakati nilipoita, hawakusikiliza, kwa hiyo walipoita, sikusikiliza,’ asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

14 ‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/7-d996fd37dc78e47b0482ee31ac2e93e0.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 8

Bwana Anaahidi Kuibariki Yerusalemu

1 Neno laBwanaMwenye Nguvu Zote likanijia tena.

2 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Nina wivu sana kwa ajili ya Sayuni, ninawaka wivu kwa ajili yake.”

3 Hili ndilo asemaloBwana: “Nitarudi Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha Yerusalemu utaitwa mji wa kweli, mlima waBwanaMwenye Nguvu Zote utaitwa Mlima Mtakatifu.”

4 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Kwa mara nyingine tena wazee wanaume kwa wanawake walioshiba umri wataketi katika barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri wake.

5 Barabara za mji zitajaa wavulana na wasichana wanaocheza humo.”

6 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu kwa mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza kuwa ya ajabu kwangu?” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

7 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Nitawaokoa watu wangu kutoka nchi za mashariki na magharibi.

8 Nitawarudisha waje kuishi Yerusalemu, watakuwa watu wangu nami nitakuwa mwaminifu na wa haki kwao kama Mungu wao.”

9 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Ninyi ambao sasa mnasikia maneno haya yanayozungumzwa na manabii ambao walikuwepo wakati wa kuwekwa kwa msingi wa nyumba yaBwanaMwenye Nguvu Zote, mikono yenu na iwe na nguvu ili Hekalu liweze kujengwa.

10 Kabla ya wakati huo, hapakuwepo na ujira kwa mtu wala mnyama. Hakuna mtu aliyeweza kufanya shughuli yake kwa usalama kwa sababu ya adui yake, kwa kuwa nilikuwa nimemfanya kila mtu adui wa jirani yake.

11 Lakini sasa sitawatendea mabaki ya watu hawa kama nilivyowatenda zamani,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

12 “Mbegu itakua vizuri, mzabibu utazaa matunda yake, ardhi itatoa mazao yake, na mbingu zitadondosha umande wake. Vitu hivi vyote nitawapa mabaki ya watu kama urithi wao.

13 Jinsi mlivyokuwa kitu cha laana katikati ya mataifa, ee Yuda na Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka. Msiogope, bali iacheni mikono yenu iwe na nguvu.”

14 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Kama nilivyokuwa nimekusudia kuleta maangamizi juu yenu, wakati baba zenu waliponikasirisha na sikuonyesha huruma,” asemaBwanaMwenye Nguvu Zote,

15 “hivyo sasa nimeazimia kufanya mema tena kwa Yerusalemu na Yuda. Msiogope.

16 Haya ndiyo mtakayoyafanya: Semeni kweli kila mtu kwa mwenzake, na mtoe hukumu ya kweli na haki kwenye mahakama zenu,

17 usipange mabaya dhidi ya jirani yako, wala msipende kuapa kwa uongo. Nayachukia yote haya,” asemaBwana.

18 Neno laBwanaMwenye Nguvu Zote likanijia tena.

19 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Saumu za miezi ya nne, tano, saba na kumi itakuwa sikukuu za furaha na za shangwe kwa Yuda. Kwa hiyo uipende kweli na amani.”

20 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Mataifa mengi na wakazi wa miji mingi watakuja,

21 na wenyeji wa mji mmoja watakwenda kwenye mji mwingine na kusema, ‘Twende mara moja na tukamsihiBwana, na kumtafutaBwanaMwenye Nguvu Zote. Mimi mwenyewe ninakwenda.’

22 Pia watu wa kabila nyingi na mataifa yenye nguvu yatakuja Yerusalemu kumtafutaBwanaMwenye Nguvu Zote na kumsihi.”

23 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Katika siku hizo watu kumi kutoka lugha zote na mataifa, watangʼangʼania upindo wa joho la Myahudi mmoja na kusema, ‘Twende pamoja nawe kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/8-2a05f3df0113be2add0cbb18079c346b.mp3?version_id=1627—

Categories
Zekaria

Zekaria 9

Hukumu Juu Ya Adui Za Israeli

1 Neno:

Neno laBwanaliko kinyume na nchi ya Hadraki

na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika,

kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote

za Israeli yako kwaBwana,

2 pia juu ya Hamathi inayopakana nayo,

juu ya Tiro na Sidoni,

ingawa wana ujuzi mwingi sana.

3 Tiro amejijengea ngome imara,

amelundika fedha kama mavumbi

na dhahabu kama taka za mitaani.

4 Lakini Bwana atamwondolea mali zake

na kuuangamiza uwezo wake wa baharini,

naye atateketezwa kwa moto.

5 Ashkeloni ataona hili na kuogopa;

Gaza atagaagaa kwa maumivu makali,

pia Ekroni, kwa sababu

matumaini yake yatanyauka.

Gaza atampoteza mfalme wake

na Ashkeloni ataachwa pweke.

6 Wageni watakalia mji wa Ashdodi,

nami nitakatilia mbali kiburi cha Wafilisti.

7 Nitaondoa damu vinywani mwao,

chakula kile walichokatazwa kati ya meno yao.

Mabaki yao yatakuwa mali ya Mungu wetu,

nao watakuwa viongozi katika Yuda,

naye Ekroni atakuwa kama Wayebusi.

8 Lakini nitailinda nyumba yangu

dhidi ya majeshi ya wanyangʼanyi.

Kamwe mdhalimu hatashambulia watu wangu tena,

kwa maana sasa ninawachunga.

Kuja Kwa Mfalme Wa Sayuni

9 Shangilia sana, ee Binti Sayuni!

Piga kelele, Binti Yerusalemu!

Tazama, Mfalme wako anakuja kwako,

ni mwenye haki, naye ana wokovu,

ni mpole, naye amepanda punda,

mwana-punda, mtoto wa punda.

10 Nitaondoa magari ya vita kutoka Efraimu

na farasi wa vita kutoka Yerusalemu,

nao upinde wa vita utavunjwa.

Atatangaza amani kwa mataifa.

Utawala wake utaenea kutoka bahari hadi bahari,

na kutoka Mto Frati hadi mwisho wa dunia.

11 Kwako wewe, kwa sababu ya damu ya Agano langu nawe,

nitawaacha huru wafungwa wako

watoke kwenye shimo lisilo na maji.

12 Rudieni ngome yenu, enyi wafungwa wa tumaini;

hata sasa ninatangaza kwamba

nitawarejesheeni maradufu.

13 Nitampinda Yuda kama nipindavyo upinde wangu,

nitamfanya Efraimu mshale wangu.

Nitawainua wana wako, ee Sayuni,

dhidi ya wana wako, ee Uyunani,

na kukufanya kama upanga wa shujaa wa vita.

Bwana Atatokea

14 KishaBwanaatawatokea;

mshale wake utamulika

kama umeme wa radi.

BwanaMwenyezi atapiga tarumbeta,

naye atatembea katika tufani za kusini,

15 naBwanaMwenye Nguvu Zote atawalinda.

Wataangamiza na kushinda

kwa mawe ya kutupa kwa kombeo.

Watakunywa na kunguruma kama waliolewa mvinyo;

watajaa kama bakuli linalotumika kunyunyizia

kwenye pembe za madhabahu.

16 BwanaMungu wao atawaokoa siku hiyo

kama kundi la watu wake.

Watangʼara katika nchi yake

kama vito vya thamani kwenye taji.

17 Jinsi gani watavutia na kuwa wazuri!

Nafaka itawastawisha vijana wanaume,

nayo divai mpya vijana wanawake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ZEC/9-08089358769e121f8d7a1cfb11bd5758.mp3?version_id=1627—