Categories
Zaburi

Zaburi 110

Bwana Na Mfalme Wake Mteule

Zaburi ya Daudi.

1 Bwanaamwambia Bwana wangu:

“Keti mkono wangu wa kuume,

mpaka nitakapowafanya adui zako

kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”

2 Bwanaataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;

utatawala katikati ya adui zako.

3 Askari wako watajitolea kwa hiari

katika siku yako ya vita.

Ukiwa umevikwa fahari takatifu,

kutoka tumbo la mapambazuko

utapokea umande wa ujana wako.

4 Bwanaameapa,

naye hatabadilisha mawazo yake:

“Wewe ni kuhani milele,

kwa mfano wa Melkizedeki.”

5 Bwana yuko mkono wako wa kuume,

atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.

6 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga

na kuwaponda watawala wa dunia nzima.

7 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia,

kwa hiyo atainua kichwa chake juu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/110-8f324b599490c012590b4eb9baf7390b.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 111

Sifa Za Bwana Kwa Matendo Ya Ajabu

1 MsifuniBwana.

NitamtukuzaBwanakwa moyo wangu wote,

katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.

2 Kazi zaBwanani kuu,

wote wanaopendezwa nazo huzitafakari.

3 Kazi zake zimejaa fahari na utukufu,

haki yake hudumu daima.

4 Amefanya maajabu yake yakumbukwe,

Bwanani mwenye neema na huruma.

5 Huwapa chakula wale wanaomcha,

hulikumbuka agano lake milele.

6 Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake,

akiwapa nchi za mataifa mengine.

7 Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki,

mausia yake yote ni ya kuaminika.

8 Zinadumu milele na milele,

zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.

9 Aliwapa watu wake ukombozi,

aliamuru agano lake milele:

jina lake ni takatifu na la kuogopwa.

10 KumchaBwanandicho chanzo cha hekima,

wote wanaozifuata amri zake wana busara.

Sifa zake zadumu milele.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/111-fcbaf92f4ba0a7f3ecc7034f23b9cdb2.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 112

Baraka Za Mwenye Haki

1 MsifuniBwana.

Heri mtu yule amchayeBwana,

mtu yule apendezwaye sana na amri zake.

2 Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi,

kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.

3 Nyumbani mwake kuna mali na utajiri,

haki yake hudumu milele.

4 Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu,

yule mwenye rehema, huruma na haki.

5 Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba,

anayefanya mambo yake kwa haki.

6 Hakika hatatikisika kamwe,

mtu mwenye haki atakumbukwa milele.

7 Hataogopa habari mbaya,

moyo wake ni thabiti, ukimtegemeaBwana.

8 Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu,

mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake.

9 Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini;

haki yake hudumu milele;

pembe yake itatukuzwa kwa heshima.

10 Mtu mwovu ataona na kuchukizwa,

atasaga meno yake na kutoweka,

kutamani kwa mtu mwovu kutaishia patupu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/112-9a9d1bf374d655d84427efbeb9eed1f0.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 113

Kumsifu Bwana Kwa Wema Wake

1 MsifuniBwana.

Enyi watumishi waBwanamsifuni,

lisifuni jina laBwana.

2 Jina laBwanana lisifiwe,

sasa na hata milele.

3 Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake,

jina laBwanalinapaswa kusifiwa.

4 Bwanaametukuka juu ya mataifa yote,

utukufu wake juu ya mbingu.

5 Ni nani aliye kamaBwanaMungu wetu,

Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi,

6 ambaye huinama atazame chini

aone mbingu na nchi?

7 Huwainua maskini kutoka mavumbini,

na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala,

8 huwaketisha pamoja na wakuu,

pamoja na wakuu wa watu wake.

9 Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake,

akiwa mama watoto mwenye furaha.

MsifuniBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/113-53c3869e1e1a9355715e21b5247d5f73.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 114

Maajabu Ya Mungu Wakati Israeli Walipotoka Misri

1 Wakati Israeli walipotoka Misri,

nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni,

2 Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu,

Israeli akawa milki yake.

3 Bahari ilitazama ikakimbia,

Yordani ulirudi nyuma,

4 milima ilirukaruka kama kondoo dume,

vilima kama wana-kondoo.

5 Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia,

nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma,

6 enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume,

enyi vilima, kama wana-kondoo?

7 Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana,

mbele za Mungu wa Yakobo,

8 aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji,

mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/114-a52b5ed5bf63e707f5cbb4eefbbfdc14.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 115

Mungu Mmoja Wa Kweli

1 Sio kwetu sisi, EeBwana, sio kwetu sisi,

bali utukufu ni kwa jina lako,

kwa sababu ya upendo

na uaminifu wako.

2 Kwa nini mataifa waseme,

“Yuko wapi Mungu wao?”

3 Mungu wetu yuko mbinguni,

naye hufanya lolote limpendezalo.

4 Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu,

zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.

5 Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,

zina macho, lakini haziwezi kuona;

6 zina masikio, lakini haziwezi kusikia,

zina pua, lakini haziwezi kunusa;

7 zina mikono, lakini haziwezi kupapasa,

zina miguu, lakini haziwezi kutembea;

wala koo zao haziwezi kutoa sauti.

8 Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,

vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.

9 Ee nyumba ya Israeli, mtumaininiBwana,

yeye ni msaada na ngao yao.

10 Ee nyumba ya Aroni, mtumaininiBwana,

yeye ni msaada na ngao yao.

11 Ninyi mnaomcha, mtumaininiBwana,

yeye ni msaada na ngao yao.

12 Bwanaanatukumbuka na atatubariki:

ataibariki nyumba ya Israeli,

ataibariki nyumba ya Aroni,

13 atawabariki wale wanaomchaBwana,

wadogo kwa wakubwa.

14 Bwanana awawezeshe kuongezeka,

ninyi na watoto wenu.

15 Mbarikiwe naBwana

Muumba wa mbingu na dunia.

16 Mbingu zilizo juu sana ni mali yaBwana,

lakini dunia amempa mwanadamu.

17 Sio wafu wanaomsifuBwana,

wale washukao mahali pa kimya,

18 bali ni sisi tunaomtukuzaBwana,

sasa na hata milele.

MsifuniBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/115-0d3279443497f8791dd5f7b28dc7850f.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 116

Shukrani Kwa Kuokolewa Kutoka Mauti

1 NinampendaBwanakwa maana amesikia sauti yangu;

amesikia kilio changu ili anihurumie.

2 Kwa sababu amenitegea sikio lake,

nitamwita siku zote za maisha yangu.

3 Kamba za mauti zilinizunguka,

maumivu makuu ya kuzimu yalinipata,

nikalemewa na taabu na huzuni.

4 Ndipo nikaliitia jina laBwana:

“EeBwana, niokoe!”

5 Bwanani mwenye neema na haki,

Mungu wetu ni mwingi wa huruma.

6 Bwanahuwalinda wanyenyekevu,

nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa.

7 Ee nafsi yangu, tulia tena,

kwa kuwaBwanaamekuwa mwema kwako.

8 Kwa kuwa wewe, EeBwana,

umeniokoa nafsi yangu na mauti,

macho yangu kutokana na machozi,

miguu yangu kutokana na kujikwaa,

9 ili niweze kutembea mbele zaBwana,

katika nchi ya walio hai.

10 Niliamini, kwa hiyo nilisema,

“Mimi nimeteseka sana.”

11 Katika taabu yangu nilisema,

“Wanadamu wote ni waongo.”

12 NimrudishieBwananini

kwa wema wake wote alionitendea?

13 Nitakiinua kikombe cha wokovu

na kulitangaza jina laBwana.

14 Nitazitimiza nadhiri zangu kwaBwana

mbele za watu wake wote.

15 Kifo cha watakatifu kina thamani

machoni paBwana.

16 EeBwana, hakika mimi ni mtumishi wako,

mimi ni mtumishi wako,

mwana wa mjakazi wako;

umeniweka huru

toka katika minyororo yangu.

17 Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru

na kuliita jina laBwana.

18 Nitazitimiza nadhiri zangu kwaBwana

mbele za watu wake wote,

19 katika nyua za nyumba yaBwana,

katikati yako, ee Yerusalemu.

MsifuniBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/116-426552c15b8abe3ec7a3067ce28fab59.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 117

Sifa Za Bwana

1 MsifuniBwana, enyi mataifa yote;

mtukuzeni yeye, enyi watu wote.

2 Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu,

uaminifu waBwanaunadumu milele.

MsifuniBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/117-530b30e55d947946e2b942776ec8e206.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 118

Shukrani Kwa Ajili Ya Ushindi

1 MshukuruniBwana, kwa kuwa ni mwema;

upendo wake wadumu milele.

2 Israeli na aseme sasa:

“Upendo wake wadumu milele.”

3 Nyumba ya Aroni na iseme sasa:

“Upendo wake wadumu milele.”

4 Wote wamchaoBwanana waseme sasa:

“Upendo wake wadumu milele.”

5 Wakati wa maumivu yangu makuu nilimliliaBwana,

naye akanijibu kwa kuniweka huru.

6 Bwanayuko pamoja nami, sitaogopa.

Mwanadamu anaweza kunitenda nini?

7 Bwanayuko pamoja nami,

yeye ni msaidizi wangu.

Nitawatazama adui zangu

wakiwa wameshindwa.

8 Ni bora kumkimbiliaBwana

kuliko kumtumainia mwanadamu.

9 Ni bora kumkimbiliaBwana

kuliko kuwatumainia wakuu.

10 Mataifa yote yalinizunguka,

lakini kwa jina laBwananaliwakatilia mbali.

11 Walinizunguka pande zote,

lakini kwa jina laBwananaliwakatilia mbali.

12 Walinizunguka kama kundi la nyuki,

lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo;

kwa jina laBwananaliwakatilia mbali.

13 Nilisukumwa nyuma karibu kuanguka,

lakiniBwanaalinisaidia.

14 Bwanani nguvu yangu na wimbo wangu,

yeye amefanyika wokovu wangu.

15 Sauti za shangwe na ushindi

zinavuma hemani mwa wenye haki:

“Mkono wa kuume waBwana

umetenda mambo makuu!

16 Mkono wa kuume waBwana

umeinuliwa juu,

mkono wa kuume waBwana

umetenda mambo makuu!”

17 Sitakufa, bali nitaishi,

nami nitatangaza yaleBwanaaliyoyatenda.

18 Bwanaameniadhibu vikali,

lakini hakuniacha nife.

19 Nifungulie malango ya haki,

nami nitaingia na kumshukuruBwana.

20 Hili ni lango laBwana

ambalo wenye haki wanaweza kuliingia.

21 Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu,

umekuwa wokovu wangu.

22 Jiwe walilolikataa waashi,

limekuwa jiwe kuu la pembeni.

23 Bwanaametenda hili,

nalo ni la kushangaza machoni petu.

24 Hii ndiyo sikuBwanaaliyoifanya,

tushangilie na kufurahi ndani yake.

25 EeBwana, tuokoe,

EeBwana, utujalie mafanikio.

26 Heri yule ajaye kwa jina laBwana.

Kutoka nyumba yaBwanatunakubariki.

27 Bwanandiye Mungu,

naye ametuangazia nuru yake.

Mkiwa na matawi mkononi,

unganeni kwenye maandamano ya sikukuu

hadi kwenye pembe za madhabahu.

28 Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru,

wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza.

29 MshukuruniBwanakwa kuwa ni mwema;

upendo wake wadumu milele.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/118-be933dac5034ae0b06fc0dc59d5bc913.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 119

Sifa Za Sheria Ya Bwana

Kujifunza Sheria Ya Bwana

1 Heri wale walio waadilifu katika njia zao,

wanaoenenda katika sheria yaBwana.

2 Heri wale wanaozishika shuhuda zake,

wamtafutao kwa moyo wao wote.

3 Wasiofanya lolote lililo baya,

wanaoenenda katika njia zake.

4 Umetoa maagizo yako

ili tuyatii kwa ukamilifu.

5 Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara

katika kuyatii maagizo yako!

6 Hivyo mimi sitaaibishwa

ninapozingatia amri zako zote.

7 Nitakusifu kwa moyo mnyofu

ninapojifunza sheria zako za haki.

8 Nitayatii maagizo yako;

usiniache kabisa.

Kutii Sheria Ya Bwana

9 Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani?

Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.

10 Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,

usiniache niende mbali na amri zako.

11 Nimelificha neno lako moyoni mwangu

ili nisikutende dhambi.

12 Sifa ni zako, EeBwana,

nifundishe maagizo yako.

13 Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote

zinazotoka katika kinywa chako.

14 Ninafurahia kufuata sheria zako

kama mtu afurahiaye mali nyingi.

15 Ninatafakari maagizo yako

na kuziangalia njia zako.

16 Ninafurahia maagizo yako,

wala sitalipuuza neno lako.

Furaha Katika Sheria Ya Bwana

17 Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi;

nitalitii neno lako.

18 Yafungue macho yangu nipate kuona

mambo ya ajabu katika sheria yako.

19 Mimi ni mgeni duniani,

usinifiche amri zako.

20 Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa

juu ya sheria zako wakati wote.

21 Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa

waendao mbali na amri zako.

22 Niondolee dharau na dhihaka,

kwa kuwa ninazishika sheria zako.

23 Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia,

mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako.

24 Sheria zako ni furaha yangu,

nazo ni washauri wangu.

Kuamua Kuitii Sheria Ya Bwana

25 Nimelazwa chini mavumbini,

yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.

26 Nilikueleza njia zangu ukanijibu,

nifundishe sheria zako.

27 Nijulishe mafundisho ya mausia yako,

nami nitatafakari maajabu yako.

28 Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni,

uniimarishe sawasawa na neno lako.

29 Niepushe na njia za udanganyifu,

kwa neema unifundishe sheria zako.

30 Nimechagua njia ya kweli,

nimekaza moyo wangu katika sheria zako.

31 Nimengʼangʼania sheria zako, EeBwana,

usiniache niaibishwe.

32 Nakimbilia katika njia ya maagizo yako,

kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru.

Maombi Ili Kupata Ufahamu Wa Sheria

33 EeBwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako,

nami nitayashika mpaka mwisho.

34 Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako

na kuitii kwa moyo wangu wote.

35 Niongoze kwenye njia ya amri zako,

kwa kuwa huko napata furaha.

36 Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako,

na siyo kwenye mambo ya ubinafsi.

37 Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa,

uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.

38 Mtimizie mtumishi wako ahadi yako,

ili upate kuogopwa.

39 Niondolee aibu ninayoiogopa,

kwa kuwa sheria zako ni njema.

40 Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako!

Hifadhi maisha yangu katika haki yako.

Kuitumainia Sheria Ya Bwana

41 EeBwana, upendo wako usiokoma unijie,

wokovu wako sawasawa na ahadi yako,

42 ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki,

kwa kuwa ninalitumainia neno lako.

43 Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu,

kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako.

44 Nitaitii amri yako daima,

naam, milele na milele.

45 Nitatembea nikiwa huru,

kwa kuwa nimejifunza mausia yako.

46 Nitasema sheria zako mbele za wafalme

wala sitaaibishwa,

47 kwa kuwa ninazifurahia amri zako

kwa sababu ninazipenda.

48 Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu,

nami ninatafakari juu ya maagizo yako.

Matumaini Katika Sheria Ya Bwana

49 Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako,

kwa sababu umenipa tumaini.

50 Faraja yangu katika mateso yangu ni hii:

Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.

51 Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka,

hata hivyo sitaiacha sheria yako.

52 EeBwana, ninazikumbuka sheria zako za zamani,

nazo zinanifariji.

53 Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu,

ambao wameacha sheria yako.

54 Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu

popote ninapoishi.

55 EeBwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako,

nami nitatii sheria yako.

56 Hili limekuwa zoezi langu:

nami ninayatii mausia yako.

Kujitolea Katika Sheria Ya Bwana

57 EeBwana, wewe ni fungu langu,

nimeahidi kuyatii maneno yako.

58 Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote,

nihurumie sawasawa na ahadi yako.

59 Nimezifikiri njia zangu

na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako.

60 Nitafanya haraka bila kuchelewa

kuzitii amri zako.

61 Hata waovu wanifunge kwa kamba,

sitasahau sheria yako.

62 Usiku wa manane ninaamka kukushukuru

kwa sababu ya sheria zako za haki.

63 Mimi ni rafiki kwa wale wote wakuchao,

kwa wote wanaofuata mausia yako.

64 EeBwana, dunia imejaa upendo wako,

nifundishe maagizo yako.

Thamani Ya Sheria Ya Bwana

65 Mtendee wema mtumishi wako

EeBwana, sawasawa na neno lako.

66 Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri,

kwa kuwa ninaamini amri zako.

67 Kabla sijapata shida nilipotea njia,

lakini sasa ninalitii neno lako.

68 Wewe ni mwema, unalotenda ni jema,

nifundishe maagizo yako.

69 Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo,

nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote.

70 Mioyo yao ni katili na migumu,

bali mimi napendezwa na sheria yako.

71 Ilikuwa vyema mimi kupata shida

ili nipate kujifunza maagizo yako.

72 Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu

kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.

Haki Ya Sheria Ya Bwana

73 Mikono yako ilinifanya na kuniumba,

nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako.

74 Wakuchao wafurahie wanaponiona,

kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako.

75 EeBwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki,

katika uaminifu wako umeniadhibu.

76 Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu,

sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.

77 Huruma yako na inijie ili nipate kuishi,

kwa kuwa naifurahia sheria yako.

78 Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu,

lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako.

79 Wale wakuchao na wanigeukie mimi,

hao ambao wanazielewa sheria zako.

80 Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako,

ili nisiaibishwe.

Maombi Kwa Ajili Ya Kuokolewa

81 Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako,

lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako.

82 Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako;

ninasema, “Utanifajiri lini?”

83 Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi,

bado sijasahau maagizo yako.

84 Mtumishi wako itampasa angoje mpaka lini?

Ni lini utawaadhibu washtaki wangu?

85 Wenye majivuno wananichimbia mashimo,

kinyume na sheria yako.

86 Amri zako zote ni za kuaminika;

unisaidie, kwa sababu watu wananishtaki bila sababu.

87 Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia,

lakini sijaacha mausia yako.

88 Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako,

nami nitatii sheria za kinywa chako.

Imani Katika Sheria Ya Bwana

89 EeBwana, neno lako ni la milele,

linasimama imara mbinguni.

90 Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote,

umeiumba dunia, nayo inadumu.

91 Sheria zako zinadumu hadi leo,

kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia.

92 Kama nisingefurahia sheria yako,

ningeangamia katika taabu zangu.

93 Sitasahau mausia yako kamwe,

kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu.

94 Uniokoe, kwa maana mimi ni wako,

kwa kuwa nimetafuta mausia yako.

95 Waovu wanangojea kuniangamiza,

bali mimi ninatafakari sheria zako.

96 Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo,

lakini amri zako hazina mpaka.

Kuipenda Sheria Ya Bwana

97 Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.

Ninaitafakari mchana kutwa.

98 Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu,

kwa kuwa nimezishika daima.

99 Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote,

kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako.

100 Nina ufahamu zaidi kuliko wazee,

kwa kuwa ninayatii mausia yako.

101 Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya,

ili niweze kutii neno lako.

102 Sijaziacha sheria zako,

kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe.

103 Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu,

matamu kuliko asali katika kinywa changu!

104 Ninapata ufahamu kutoka mausia yako,

kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.

Nuru Kutoka Kwenye Sheria Ya Bwana

105 Neno lako ni taa ya miguu yangu

na mwanga katika njia yangu.

106 Nimeapa na nimethibitisha,

kwamba nitafuata sheria zako za haki.

107 Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, EeBwana,

sawasawa na neno lako.

108 EeBwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu,

nifundishe sheria zako.

109 Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote,

sitasahau sheria yako.

110 Waovu wamenitegea mtego,

lakini sijayakiuka maagizo yako.

111 Sheria zako ni urithi wangu milele,

naam ni furaha ya moyo wangu.

112 Nimekusudia moyoni mwangu

kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho.

Usalama Ndani Ya Sheria Ya Bwana

113 Ninachukia watu wa nia mbili,

lakini ninapenda sheria yako.

114 Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu,

nimeweka tumaini langu katika neno lako.

115 Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya,

ili niweze kushika amri za Mungu wangu!

116 Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi;

usiache matumaini yangu yakavunjwa.

117 Nitegemeze, nami nitaokolewa,

nami daima nitayaheshimu maagizo yako.

118 Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako,

kwa maana udanganyifu wao ni bure.

119 Waovu wa nchi unawatupa kama takataka,

kwa hivyo nazipenda sheria zako.

120 Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe,

ninaziogopa sheria zako.

Kuitii Sheria Ya Bwana

121 Nimetenda yaliyo haki na sawa,

usiniache mikononi mwa watesi wangu.

122 Mhakikishie mtumishi wako usalama,

usiache wenye kiburi wanionee.

123 Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako,

na kuitazamia ahadi yako ya kweli.

124 Mfanyie mtumishi wako kulingana na upendo wako

na unifundishe maagizo yako.

125 Mimi ni mtumishi wako; nipe ufahamu

ili niweze kuelewa sheria zako.

126 EeBwana, wakati wako wa kutenda umewadia,

kwa kuwa sheria yako inavunjwa.

127 Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu,

naam, zaidi ya dhahabu safi,

128 na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili,

nachukia kila njia potovu.

Shauku Ya Kuitii Sheria Ya Bwana

129 Sheria zako ni za ajabu,

hivyo ninazitii.

130 Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru,

kunampa mjinga ufahamu.

131 Nimefungua kinywa changu na kuhema,

nikitamani amri zako.

132 Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote

wale wanaolipenda jina lako.

133 Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako,

usiache dhambi yoyote initawale.

134 Niokoe na uonevu wa wanadamu,

ili niweze kutii mausia yako.

135 Mwangazie mtumishi wako uso wako

na unifundishe amri zako.

136 Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni yangu,

kwa kuwa sheria yako haifuatwi.

Haki Ya Sheria Ya Bwana

137 EeBwana, wewe ni mwenye haki,

sheria zako ni sahihi.

138 Sheria ulizoziweka ni za haki,

ni za kuaminika kikamilifu.

139 Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu

wanayapuuza maneno yako.

140 Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu,

mtumishi wako anazipenda.

141 Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa,

sisahau mausia yako.

142 Haki yako ni ya milele,

na sheria yako ni kweli.

143 Shida na dhiki zimenipata,

lakini amri zako ni furaha yangu.

144 Sheria zako ni sahihi milele,

hunipa ufahamu ili nipate kuishi.

Maombi Kwa Ajili Ya Kuokolewa

145 EeBwana, ninakuita kwa moyo wangu wote,

nami nitayatii maagizo yako.

146 Ninakuita; niokoe

nami nitazishika sheria zako.

147 Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada;

nimeweka tumaini langu katika neno lako.

148 Sikufumba macho yangu usiku kucha,

ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako.

149 Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako,

EeBwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako.

150 Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami,

lakini wako mbali na sheria yako.

151 EeBwana, hata hivyo wewe u karibu,

na amri zako zote ni za kweli.

152 Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako

kwamba umezithibitisha ili zidumu milele.

Maombi Kwa Ajili Ya Msaada

153 Yaangalie mateso yangu, uniokoe,

kwa kuwa sijasahau sheria yako.

154 Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe,

uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako.

155 Wokovu uko mbali na waovu,

kwa kuwa hawatafuti maagizo yako.

156 EeBwana, huruma zako ni kuu,

uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako.

157 Adui wanaonitesa ni wengi,

lakini mimi sitaziacha sheria zako.

158 Ninawatazama wasioamini kwa chuki,

kwa kuwa hawalitii neno lako.

159 Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako;

EeBwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako.

160 Maneno yako yote ni kweli,

sheria zako zote za haki ni za milele.

Kujiweka Wakfu Kwa Sheria Ya Bwana

161 Watawala wamenitesa bila sababu,

lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako.

162 Nafurahia ahadi zako

kama mtu aliyepata mateka mengi.

163 Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo,

lakini napenda sheria yako.

164 Ninakusifu mara saba kwa siku,

kwa ajili ya sheria zako za haki.

165 Wanaopenda sheria yako wana amani tele,

wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza.

166 EeBwana, ninangojea wokovu wako,

nami ninafuata amri zako,

167 Ninazitii sheria zako,

kwa sababu ninazipenda mno.

168 Nimetii mausia yako na sheria zako,

kwa kuwa njia zangu zote zinajulikana kwako.

Kuomba Msaada

169 EeBwana, kilio changu na kifike mbele zako,

nipe ufahamu sawasawa na neno lako.

170 Maombi yangu na yafike mbele zako,

niokoe sawasawa na ahadi yako.

171 Midomo yangu na ibubujike sifa,

kwa kuwa unanifundisha maagizo yako.

172 Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako,

kwa kuwa amri zako zote ni za haki.

173 Mkono wako uwe tayari kunisaidia,

kwa kuwa nimechagua mausia yako.

174 EeBwana, ninatamani wokovu wako,

na sheria yako ni furaha yangu.

175 Nijalie kuishi ili nipate kukusifu,

na sheria zako zinitegemeze.

176 Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea.

Mtafute mtumishi wako,

kwa kuwa sijasahau amri zako.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/119-0c58850b10e27952fc249f71e7c597c6.mp3?version_id=1627—