Categories
Yoshua

Yoshua 20

Miji Ya Makimbilio

1 NdipoBwanaakamwambia Yoshua,

2 “Waambie Waisraeli, watenge miji mikubwa ya kukimbilia, kama nilivyokuagiza kupitia Mose,

3 ili mtu yeyote atakayemuua mtu kwa bahati mbaya na pasipo kukusudia aweze kukimbilia huko na kujiepusha na mlipiza kisasi wa damu.

4 “Anapokimbilia mojawapo ya hii miji mikubwa atasimama kwenye maingilio ya lango la mji mkuu na kueleza wazee wa mji kuhusu shauri lake. Kisha watampokea katika mji wao na kumpa mahali pa kuishi nao.

5 Kama mlipiza kisasi wa damu akimfuatilia, wasimkabidhi yule mshtakiwa, kwa sababu alimuua jirani yake bila kukusudia, na bila kuwa na nia ya kudhuru.

6 Huyu aliyeua atakaa kwenye mji mkubwa huo mpaka awe amesimama kukabili mashtaka yake mbele ya kusanyiko na mpaka kuhani mkuu anayehudumu kwa wakati huo atakapokufa. Ndipo atakapoweza kurudi nyumbani kwake katika mji ambao aliukimbia.”

7 Basi wakatenga Kedeshi katika Galilaya kwenye nchi ya vilima ya Naftali, Shekemu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na Kiriath-Arba (yaani Hebroni) kwenye nchi ya vilima ya Yuda.

8 Katika upande wa mashariki mwa Yordani ya Yeriko wakatenga Bezeri katika jangwa katika uwanda wa juu katika kabila la Reubeni, Ramothi katika Gileadi katika kabila la Gadi, na Golani huko Bashani katika kabila la Manase.

9 Mwisraeli yeyote au mgeni yeyote aishiye miongoni mwao aliyemuua mtu kwa bahati mbaya, angeweza kukimbilia katika miji mikubwa hiyo iliyotengwa na asiuawe na mlipiza kisasi wa damu kabla hajasimama kukabili mashtaka mbele ya kusanyiko.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOS/20-c7cceb20f5e46f9c32b9499b2e677e89.mp3?version_id=1627—

Categories
Yoshua

Yoshua 21

Miji Kwa Walawi

1 Basi viongozi wa jamaa ya Walawi, wakamwendea kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa nyingine za makabila ya Israeli

2 huko Shilo katika Kanaani na kuwaambia, “Bwanaaliamuru kupitia Mose kuwa mtupe miji ya kuishi yenye sehemu za malisho kwa mifugo yetu.”

3 Hivyo kama vileBwanaalivyoamuru, Waisraeli wakawapa Walawi miji ifuatayo pamoja na sehemu zake za malisho kutoka urithi wao wenyewe.

4 Kura ya kwanza ikaangukia Wakohathi, ukoo kwa ukoo. Walawi waliokuwa wazao wa kuhani Aroni walipewa miji kumi na mitatu kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini.

5 Wazao wengine waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za makabila ya Efraimu, Dani na nusu ya Manase.

6 Wazao wa Gershoni walipewa miji kumi na mitatu kutoka koo za makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na nusu ya Manase huko Bashani.

7 Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

8 Kwa hiyo Waisraeli wakawapa Walawi miji hii pamoja na sehemu zake za malisho, kama vileBwanaalivyokuwa ameamuru kupitia kwa Mose.

9 Kutoka makabila ya Yuda na Simeoni waligawa miji ifuatayo kwa majina

10 (miji hii walipewa wazao wa Aroni ambao walitokana na koo za Wakohathi wa Walawi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):

11 Waliwapa Kiriath-Arba (yaani Hebroni), pamoja na sehemu zake za malisho zilizoizunguka, katika nchi ya vilima ya Yuda. (Arba alikuwa baba wa Anaki.)

12 Lakini mashamba na vijiji vilivyozunguka mji mkubwa walikuwa wamempa Kalebu mwana wa Yefune kuwa milki yake.

13 Kwa hiyo wazao wa kuhani Aroni wakapewa Hebroni (mji mkuu wa makimbilio kwa ajili ya yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji), Libna,

14 Yatiri, Eshtemoa,

15 Holoni, Debiri,

16 Aini, Yuta na Beth-Shemeshi, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji tisa kutoka kwa makabila haya mawili.

17 Kutoka kabila la Benyamini wakawapa Gibeoni, Geba,

18 Anathothi na Almoni, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.

19 Miji yote waliyopewa makuhani, wazao wa Aroni, ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho.

20 Koo nyingine za Wakohathi, ambao pia ni Walawi, walipewa miji kutoka kabila la Efraimu:

21 Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji mkubwa wa makimbilio kwa yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji) na Gezeri,

22 Kibsaimu na Beth-Horoni, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.

23 Pia kutoka kabila la Dani wakapokea Elteke, Gibethoni,

24 Aiyaloni na Gath-Rimoni pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne

25 Kutoka nusu ya kabila la Manase, wakapokea Taanaki na Gath-Rimoni pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili.

26 Miji yote hii kumi pamoja na sehemu zake za malisho ilipewa koo za Wakohathi zilizobaki.

27 Koo za Walawi za Wagershoni walipewa:

kutoka nusu ya kabila la Manase,

Golani katika Bashani (mji mkuu wa makimbilio kwa yeyote aliyeshtakiwa kwa mauaji) na Beeshtera, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji miwili;

28 kutoka kabila la Isakari walipewa,

Kishioni, Daberathi,

29 Yarmuthi na En-Ganimu, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne

30 kutoka kabila la Asheri walipewa,

Mishali, Abdoni,

31 Helkathi na Rehobu, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.

32 Kutoka kabila la Naftali walipewa,

Kedeshi katika Galilaya (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa mauaji), Hamoth-Dori na Kartani, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji mitano.

33 Miji yote ya koo za Wagershoni ilikuwa kumi na mitatu, pamoja na sehemu zake za malisho.

34 Koo za Wamerari (Walawi waliobaki) walipewa:

kutoka kabila la Zabuloni,

Yokneamu, Karta,

35 Dimna na Nahalali, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne;

36 kutoka kabila la Reubeni walipewa

Bezeri, Yahasa,

37 Kedemothi na Mefaathi, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne;

38 kutoka kabila la Gadi walipewa,

Ramothi katika Gileadi (mji wa makimbilio kwa ajili ya yeyote anayeshtakiwa kwa ajili ya mauaji), Mahanaimu,

39 Heshboni na Yazeri, pamoja na sehemu zake za malisho, ilikuwa miji minne.

40 Miji yote waliyopewa koo za Wamerari, waliokuwa mabaki ya Walawi, ilikuwa ni kumi na miwili.

41 Miji yote ya Walawi katika eneo lililoshikwa na Waisraeli lilikuwa arobaini na minane, pamoja na sehemu zake za malisho.

42 Kila mmoja wa miji hii ulikuwa na sehemu ya malisho kuuzunguka; ndivyo ilivyokuwa kwa miji hii yote.

43 Kwa hiyoBwanaakawapa Israeli nchi yote aliyokuwa ameapa kuwapa baba zao, nao wakaimiliki na kukaa humo.

44 Bwanaakawapa pumziko kila upande, kama vile alivyokuwa amewaapia baba zao, hakuna hata mmoja wa adui zao aliyeweza kusimama mbele yao,Bwanaakawatia adui zao wote mikononi mwao.

45 Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri yaBwanakwa nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOS/21-3289d313f3c32f8264ff0432930a553c.mp3?version_id=1627—

Categories
Yoshua

Yoshua 22

Makabila Ya Mashariki Yarudi Nyumbani

1 Ndipo Yoshua akawaita Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase,

2 naye akawaambia, “Mmeshafanya yale yote Mose mtumishi waBwanaaliyowaamuru, nanyi mmenitii kwa kila jambo nililowaamuru.

3 Kwa muda mrefu sasa, hadi siku hii ya leo, hamkuwaacha ndugu zenu, bali ninyi mmetimiza ile kaziBwanaMungu wenu aliyowapa.

4 Sasa kwa kuwaBwanaMungu wenu amewapa ndugu zenu pumziko kama alivyoahidi, rudini nyumbani mwenu katika nchi ile ambayo Mose mtumishi waBwanaaliwapa ngʼambo ya Yordani.

5 Lakini mwe waangalifu sana kushika amri na sheria zile Mose mtumishi waBwanaalizowapa: yaani kumpendaBwanaMungu wenu na kuenenda katika njia zake zote, kutii amri zake, kushikamana naye kwa uthabiti na kumtumikia kwa moyo wenu wote na roho yenu yote.”

6 Ndipo Yoshua akawabariki na kuwaaga waende zao, nao wakaenda nyumbani mwao.

7 (Kwa nusu ya kabila la Manase Mose alikuwa amewapa eneo katika Bashani na ile nusu nyingine ya hilo kabila Yoshua aliwapa eneo upande wa magharibi ya Yordani pamoja na ndugu zao). Yoshua alipowaaga waende zao nyumbani, aliwabariki,

8 akisema, “Rudini nyumbani mwenu na utajiri wenu mwingi, yaani makundi makubwa ya mifugo, mkiwa na fedha, dhahabu, shaba na chuma, pia wingi wa nguo, nanyi mkagawane na ndugu zenu hizo nyara zilizotoka kwa adui zenu.”

9 Kwa hiyo Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase wakawaacha Waisraeli huko Shilo katika nchi ya Kanaani ili kurudi Gileadi, nchi yao wenyewe waliyoipata sawasawa na agizo laBwanakupitia Mose.

10 Walipofika Gelilothi karibu na Yordani, katika nchi ya Kanaani, Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase wakajenga madhabahu ya fahari kubwa huko kando ya Yordani.

11 Waisraeli wengine waliposikia kwamba Wareubeni, Wagadi na ile nusu ya kabila la Manase walikuwa wamejenga madhabahu kwenye mpaka wa Kanaani huko Gelilothi karibu na Yordani kwenye upande wa Israeli,

12 kusanyiko lote la Israeli wakakusanyika huko Shilo ili wakapigane vita dhidi yao.

13 Kwa hiyo Waisraeli wengine wakamtuma Finehasi mwana wa kuhani Eleazari katika nchi ya Gileadi, kwa Wareubeni, Wagadi na hiyo nusu ya kabila la Manase.

14 Wakatuma pamoja naye watu kumi ambao ni viongozi, mmoja kwa kila kabila la Israeli, kila mmoja aliyekuwa kiongozi katika mgawanyiko wa jamaa miongoni mwa koo za Israeli.

15 Walipofika Gileadi, kwa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, wakawaambia:

16 “Kusanyiko lote laBwanalasema: ‘Je, mmewezaje kuacha kumwamini Mungu wa Israeli jinsi hii? Mmewezaje kumwachaBwanana kujijengea madhabahu dhidi yake na kumwasi?

17 Je, dhambi ya Peori haikutosha? Hata ingawa kulikuja tauni juu ya kusanyiko laBwana, mpaka leo hii hatujatakasika kutokana na dhambi hiyo!

18 Je, sasa ndiyo mnamwachaBwana?

“ ‘Kama mkimwasiBwanaleo, kesho atalikasirikia kusanyiko lote la Israeli.

19 Kama nchi mnayomiliki imenajisika, vukeni mje katika nchi yaBwana, mahali Maskani yaBwanailipo, nanyi mkajitwalie sehemu miongoni mwetu, lakini msije mkaasi dhidi yaBwanawala dhidi yetu sisi kwa kujijengea madhabahu, zaidi ya madhabahu yaBwanaMungu wetu.

20 Wakati Akani mwana wa Zera alipokosa uaminifu kwa vitu vilivyowekwa wakfu, je, ghadhabu haikulipata kusanyiko lote la Israeli? Hakuwa yeye peke yake aliyekufa kwa ajili ya dhambi yake.’ ”

21 Ndipo Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walipowajibu viongozi wa koo za Israeli, wakisema:

22 “Yeye Mwenye Nguvu, Mungu,Bwana! Yeye Mwenye Nguvu, Mungu,Bwana! Yeye anajua! Israeli na wajue! Kama huu umekuwa ni uasi au kukosa utii kwaBwana, msituache hai siku hii ya leo.

23 Kama tumejijengea madhabahu yetu wenyewe ili kumwachaBwanana kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, au kutoa sadaka za amani juu yake,Bwanamwenyewe na atupatilize leo.

24 “Sivyo! Tulifanya hivyo kwa hofu kwamba siku zijazo wazao wenu wanaweza wakawaambia wazao wetu, ‘Mna uhusiano gani naBwana, Mungu wa Israeli?

25 Bwanaameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi, ninyi Wareubeni na Wagadi! Hamna fungu kwaBwana.’ Kwa hiyo wazao wenu wanaweza wakawasababisha wazao wetu wakaacha kumchaBwana.

26 “Hii ndiyo sababu tulisema, ‘Tujiweke tayari na tujenge madhabahu, lakini si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa au dhabihu.’

27 Badala yake, itakuwa ni ushahidi kati yetu na ninyi na vizazi vijavyo, kwamba tutamwabuduBwanakatika mahali patakatifu pake pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa, dhabihu na sadaka za amani. Ndipo katika siku zijazo, wazao wenu hawataweza kuwaambia wazao wetu, ‘Ninyi hamna fungu katikaBwana.’

28 “Nasi tulisema, ‘Ikiwa wakati wowote watatuambia hilo, au kuwaambia uzao wetu, tutawajibu hivi: Angalieni nakala hii ya madhabahu yaBwana, ambayo baba zetu waliijenga, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu, bali kama ushahidi kati yetu na ninyi.’

29 “Hili jambo la kumwasiBwanana kumwacha siku hii ya leo kwa kujenga madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na dhabihu, zaidi ya madhabahu yaBwanaMungu wetu iliyo mbele ya maskani yake na liwe mbali nasi.”

30 Wakati kuhani Finehasi na viongozi wa kusanyiko na wakuu wa koo za Israeli, waliposikia hayo waliyosema Wareubeni, Wagadi na Manase, wakaridhika.

31 Naye Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, akawaambia Wareubeni, Wagadi na Manase, “Leo tunajua kwambaBwanayuko pamoja nasi, kwa sababu hamkukosa uaminifu kwaBwanakatika jambo hili. Sasa mmewaokoa Waisraeli na mkono waBwana.”

32 Ndipo Finehasi, mwana wa kuhani Eleazari na viongozi wakarudi Kanaani kutoka kwenye kukutana kwao na Wareubeni na Wagadi huko Gileadi nao wakatoa taarifa kwa Waisraeli.

33 Walifurahi kusikia taarifa hiyo, na wakamhimidi Mungu. Wala hawakuzungumza tena habari za kupigana vita dhidi yao ili kuharibu nchi ambayo Wareubeni na Wagadi waliishi.

34 Nao Wareubeni na Wagadi wakayaita yale madhabahu Edi, yaani Shahidi: kwa kuwa itakuwa shahidi kati yetu na ninyi kwambaBwanandiye Mungu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOS/22-28b4efe4dc43b505ff70d12f79c11a8d.mp3?version_id=1627—

Categories
Yoshua

Yoshua 23

Yoshua Anawaaga Viongozi

1 Baada ya muda mrefu kupita, nayeBwanaakawa amewapa Israeli pumziko mbele ya adui zao wote waliowazunguka, Yoshua, wakati huo akiwa mzee na umri ukiwa umeendelea sana,

2 akawaita Israeli wote, wazee wao, viongozi, waamuzi na maafisa Yoshua akawaambia: “Mimi ni mzee na umri wangu umeendelea sana.

3 Ninyi wenyewe mmeona kila kituBwanaMungu wenu, alichowatendea mataifa haya yote kwa ajili yenu. Ilikuwa niBwanaMungu wenu aliyewapigania.

4 Kumbukeni jinsi nilivyowagawia kama urithi kwa makabila yenu yote nchi ya mataifa yaliyobaki, yaani mataifa niliyowashinda, kati ya Mto Yordani na Bahari kuu upande wa magharibi.

5 BwanaMungu wenu mwenyewe atawaondoa watoke mbele yenu. Atawafukuza mbele yenu, nanyi mtamiliki nchi yao, kama vileBwanaMungu wenu alivyowaahidi.

6 “Kuweni hodari sana, kuweni waangalifu kutii yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Sheria ya Mose, pasipo kugeuka upande wa kuume au kushoto.

7 Msishirikiane na mataifa yaliyobakia katikati yenu, wala msiombe kwa majina ya miungu yao au kuapa kwayo. Msiitumikie wala kuisujudia.

8 Bali mtashikamana kwa uthabiti naBwana, Mungu wenu, kama vile ambavyo mmefanya mpaka sasa.

9 “Bwanaamewafukuza mbele yenu mataifa makubwa na yenye nguvu, mpaka siku ya leo hakuna yeyote aliyeweza kusimama mbele yenu.

10 Mtu mmoja miongoni mwenu anafukuza watu elfu, kwa kuwaBwanaMungu wenu anawapigania, kama alivyoahidi.

11 Kwa hiyo kuweni waangalifu sana kumpendaBwanaMungu wenu.

12 “Lakini ikiwa mtageuka na kushikamana na mabaki ya mataifa haya yaliyosalia katikati yenu na kama mtaoana na kushirikiana nao,

13 basi mwe na hakika kuwaBwanaMungu wenu hatawafukuza tena mataifa hayo mbele yenu. Badala yake, watakuwa tanzi na mitego kwenu, mijeledi migongoni mwenu, na miiba machoni mwenu, mpaka mwangamie kutoka nchi hii nzuri, ambayoBwanaMungu wenu amewapa.

14 “Sasa mimi ninakaribia kwenda katika njia ya watu wote wa dunia. Mnajua kwa mioyo yenu na roho zenu kwamba hakuna ahadi zozote njemaBwanaMungu wenu alizowaahidia, ambazo hazikutimia. Kila ahadi imetimizwa, hakuna hata moja ambayo haikutimia.

15 Lakini kama vile kila ahadi njema yaBwanaMungu wenu imekuwa kweli, vivyo hivyoBwanaataleta maovu yote kama alivyo onya, mpaka awe amewaangamiza kutoka nchi hii nzuri aliyowapa.

16 Kama mkilivunja agano laBwanaMungu wenu, ambalo aliwaamuru ninyi, mkaenda na kuitumikia miungu mingine na kuisujudia, hasira yaBwanaitawaka dhidi yenu, nanyi mtaangamia kutoka nchi nzuri aliyowapa ninyi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOS/23-66bad3d200ae96492b40ac9253ae7665.mp3?version_id=1627—

Categories
Yoshua

Yoshua 24

Agano Lafanywa Upya Huko Shekemu

1 Ndipo Yoshua akaita pamoja makabila yote ya Israeli huko Shekemu. Akawaita wazee, viongozi, waamuzi na maafisa wa Israeli, nao wakaja mbele za Mungu.

2 Yoshua akawaambia watu wote, “Hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Hapo zamani baba zenu, pamoja na Tera baba yake Abrahamu na Nahori, waliishi ngʼambo ya Mto nao waliiabudu miungu mingine.

3 Lakini nilimwondoa baba yenu Abrahamu kutoka nchi hiyo ngʼambo ya Mto, nami nikamwongoza katika nchi yote ya Kanaani, nikampa wazao wengi. Nikampa Isaki,

4 naye Isaki nikampa Yakobo na Esau. Esau nikampa nchi ya vilima ya Seiri, lakini Yakobo pamoja na wanawe wakashuka Misri.

5 “ ‘Kisha nikawatuma Mose na Aroni, nami nikawapiga Wamisri kwa kile nilichokitenda huko, tena nikawatoa ninyi huko.

6 Nilipowatoa baba zenu Misri, mlifika kwenye bahari, nao Wamisri wakawafuatia baba zenu kwa magari na wapanda farasi mpaka kwenye Bahari ya Shamu.

7 Lakini wakamliliaBwanawakitaka msaada, naye akaweka giza kati yenu na Wamisri, akaileta bahari juu yao ikawafunika. Ninyi mliona kwa macho yenu wenyewe kile nilichowatendea Wamisri. Kisha mliishi jangwani kwa muda mrefu.

8 “ ‘Nikawaleta katika nchi ya Waamori ambao waliishi mashariki mwa Yordani. Wakapigana nanyi, lakini nikawatia mikononi mwenu. Nikawaangamiza mbele yenu nanyi mkaimiliki nchi yao.

9 Wakati Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, alipojiandaa kupigana dhidi ya Israeli, alimwita Balaamu mwana wa Beori apate kuwalaani.

10 Lakini sikumkubali Balaamu, kwa hiyo aliwabariki tena na tena, nami niliwaokoa toka mkononi mwake.

11 “ ‘Ndipo mlipovuka Yordani mkafika Yeriko. Raiya wa Yeriko wakapigana nanyi, kama walivyofanya Waamori, Waperizi, Wakanaani, Wahiti, Wagirgashi, Wahivi na Wayebusi, lakini niliwatia mikononi mwenu.

12 Nikatuma manyigu mbele yenu, ambao pia waliwafukuza mbele yenu, hao wafalme wawili wa Waamori. Siyo upanga au upinde wenu wenyewe vilivyowapatia ushindi.

13 Hivyo nikawapa ninyi nchi ambayo hamkuitaabikia na miji ambayo hamkuijenga na mnaishi ndani yake na kula toka kwa mashamba ya mizabibu na mizeituni msiyoipanda.’

14 “Sasa basi mcheniBwanana kumtumikia kwa uaminifu wote. Itupeni mbali miungu ambayo baba zenu waliiabudu huko ngʼambo ya Mto Frati na huko Misri, nanyi mtumikieniBwana.

15 Lakini msipoona vyema kumtumikiaBwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ngʼambo Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikiaBwana.”

16 Ndipo hao watu wakajibu, “Hili jambo liwe mbali nasi la kumsahauBwanana kuitumikia miungu mingine!

17 BwanaMungu wetu mwenyewe ndiye alitutoa sisi na baba zetu akatupandisha kutoka Misri, kutoka nchi ile ya utumwa, na kutenda zile ishara kubwa mbele ya macho yetu. Ndiye aliyetulinda katika safari yetu yote na kutokana na mataifa yote ambayo tulipita katikati yao.

18 Bwanaakayafukuza mbele yetu mataifa yote pamoja na Waamori, walioishi katika nchi hii. Hivyo sisi nasi tutamtumikiaBwanakwa kuwa yeye ndiye Mungu wetu.”

19 Yoshua akawaambia watu, “Hamwezi kumtumikiaBwana. Yeye ni Mungu Mtakatifu, ni Mungu mwenye wivu. Hatasamehe uasi wenu na dhambi zenu.

20 Ikiwa mkimwachaBwanana kuitumikia miungu migeni, atageuka na kuwaleteeni maafa na kuwaangamiza, baada ya kuwa mwema kwenu.”

21 Lakini watu wakamwambia Yoshua, “Sivyo! Sisi tutamtumikiaBwana.”

22 Ndipo Yoshua akawaambia, “Ninyi mmekuwa mashahidi juu yenu wenyewe kuwa mmechagua kumtumikiaBwana.”

Nao wakajibu, “Ndiyo, tu mashahidi.”

23 Yoshua akawaambia, “Sasa basi, itupeni mbali hiyo miungu migeni iliyo katikati yenu, nanyi mtoleeniBwana, Mungu wa Israeli, mioyo yenu.”

24 Nao watu wakamwambia Yoshua, “TutamtumikiaBwanaMungu wetu na kumtii yeye.”

25 Siku ile Yoshua akafanya agano kwa ajili ya watu na hapo Shekemu ndipo alipowaandikia amri na sheria.

26 Naye Yoshua akayaandika mambo haya katika Kitabu cha Sheria ya Mungu. Ndipo akalitwaa jiwe kubwa, akalisimamisha huko chini ya mwaloni, karibu na mahali patakatifu paBwana.

27 Yoshua akawaambia watu wote, “Angalieni! Jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu. Limesikia maneno yoteBwanaaliyotuambia. Litakuwa shahidi juu yenu kama mtakuwa waongo kwa Mungu wenu.”

Kuzikwa Katika Nchi Ya Ahadi

28 Basi Yoshua akawatuma watu kila mmoja aende katika urithi wake mwenyewe.

29 Baada ya mambo haya, Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi waBwanaakafa akiwa na umri wa miaka mia moja na kumi.

30 Nao wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-Serakatika nchi ya vilima ya Efraimu, kaskazini ya Mlima wa Gaashi.

31 Israeli wakamtumikiaBwanasiku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, ambao waliona kila kituBwanaalichowatendea Israeli.

32 Nayo ile mifupa ya Yosefu, ambayo Waisraeli waliipandisha kutoka huko Misri, wakaizika huko Shekemu kwenye eneo, ambalo Yakobo alilinunua kwa wana wa Hamori baba yake Shekemu, kwa vipande mia vya fedha. Eneo hili likawa ni urithi wa uzao wa Yosefu.

33 Naye Eleazari mwana wa Aroni akafariki akazikwa huko Gibea, mlima aliokuwa amepewa mtoto wake Finehasi, kwenye nchi ya vilima ya Efraimu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOS/24-60870f2732749295a19fb15578d5f092.mp3?version_id=1627—