Categories
Yeremia

Yeremia 40

Yeremia Aachiwa Huru

1 Neno likamjia Yeremia kutoka kwaBwanabaada ya Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme kumfungua huko Rama. Alikuwa amemkuta Yeremia akiwa amefungwa kwa minyororo miongoni mwa mateka wote kutoka Yerusalemu na Yuda waliokuwa wakipelekwa uhamishoni Babeli.

2 Kiongozi wa walinzi alipomwona Yeremia, akamwambia, “BwanaMungu wako aliamuru maafa haya kwa mahali hapa.

3 SasaBwanaameyaleta haya, amefanya sawasawa na vile alivyosema angefanya. Yote haya yametokea kwa sababu ninyi mlifanya dhambi dhidi yaBwanana hamkumtii.

4 Lakini leo ninakufungua minyororo iliyo kwenye viwiko vya mikono yako. Twende pamoja mpaka Babeli ikiwa unataka, nami nitakutunza. Lakini kama hutaki, basi usije. Tazama, nchi yote iko mbele yako, nenda kokote unakotaka.”

5 Lakini kabla Yeremia hajageuka kuondoka, Nebuzaradani akaongeza kusema, “Rudi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemchagua awe juu ya miji ya Yuda, ukaishi naye miongoni mwa watu, au uende popote panapokupendeza.”

Kisha huyo kiongozi akampa posho yake na zawadi, akamwacha aende zake.

6 Kwa hiyo Yeremia akaenda kwa Gedalia mwana wa Ahikamu huko Mispa, na kuishi naye miongoni mwa watu walioachwa katika nchi.

Gedalia Auawa

7 Maafisa wote wa jeshi na watu wao waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemteua Gedalia mwana wa Ahikamu kuwa mtawala wa nchi, na amemweka kuwa kiongozi wa wanaume, wanawake na watoto waliokuwa maskini zaidi katika nchi ambao hawakuchukuliwa kwenda uhamishoni Babeli,

8 wakamjia Gedalia huko Mispa. Hawa walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani na Yonathani wana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi, wana wa Efai Mnetofathi, na Yezania mwana wa Mmaaka, pamoja na watu wao.

9 Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani akaapa ili kuwatia moyo wao na watu wao. Akasema: “Msiogope kuwatumikia Wakaldayo. Kaeni katika nchi na kumtumikia mfalme wa Babeli, na itakuwa vyema kwenu.

10 Mimi mwenyewe nitakaa Mispa ili kuwawakilisha mbele ya Wakaldayo wanaotujia, lakini ninyi mtavuna divai, matunda ya kiangazi na mafuta, nanyi mtaweka katika vyombo vyenu vya kuhifadhia, na kuishi katika miji mliyojitwalia.”

11 Wayahudi wote waliokuwa Moabu, Amoni, Edomu na nchi nyingine zote waliposikia kwamba mfalme wa Babeli ameacha mabaki ya watu katika Yuda na amemweka Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kuwa mtawala wao,

12 wakarudi wote katika nchi ya Yuda kwa Gedalia huko Mispa, kutoka nchi zote ambazo walikuwa wametawanywa. Nao wakavuna divai na matunda tele wakati wa kiangazi.

13 Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi wakamjia Gedalia huko Mispa

14 na kumwambia, “Je, hujui kwamba Baalisi mfalme wa Waamoni amemtuma Ishmaeli mwana wa Nethania akuue?” Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu hakuwaamini.

15 Kisha Yohanani mwana wa Karea akamwambia Gedalia kwa siri huko Mispa, “Acha niende nikamuue Ishmaeli mwana wa Nethania, wala hakuna atakayejua. Kwa nini akuue na kusababisha Wayahudi wote waliokuzunguka watawanyike, na mabaki wa Yuda waangamie?”

16 Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu akamwambia Yohanani mwana wa Karea, “Usifanye jambo kama hilo! Unalosema kuhusu Ishmaeli si kweli.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/40-2b41241e28fda5b61839539c135b76e0.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 41

1 Katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, aliyekuwa wa uzao wa mfalme na pia alikuwa mmoja wa maafisa wa mfalme, akaja pamoja na watu kumi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu huko Mispa. Walipokuwa wakila pamoja huko,

2 Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi waliokuwa pamoja naye waliinuka na kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kwa upanga, wakamuua yule ambaye mfalme wa Babeli alikuwa amemteua awe mtawala wa nchi.

3 Ishmaeli akawaua pia Wayahudi wote waliokuwa na Gedalia huko Mispa, pamoja na askari wa Kikaldayo waliokuwa huko.

4 Siku moja baada ya kuuawa kwa siri kwa Gedalia, kabla mtu yeyote hajafahamu jambo hilo,

5 watu themanini waliokuwa wamenyoa ndevu zao, waliorarua nguo zao na kujikatakata walikuja kutoka Shekemu, Shilo na Samaria wakileta sadaka za nafaka na uvumba katika nyumba yaBwana.

6 Ishmaeli mwana wa Nethania akaondoka Mispa ili kwenda kuwalaki, huku akilia alipokuwa akienda. Alipokutana nao, akasema, “Karibuni kwa Gedalia mwana wa Ahikamu.”

7 Walipoingia mjini, Ishmaeli mwana wa Nethania na wale watu waliokuwa pamoja naye wakawachinja na kuwatupa ndani ya kisima.

8 Lakini watu kumi miongoni mwao wakamwambia Ishmaeli, “Sisi usituue! Tuna ngano na shayiri, mafuta na asali, vilivyofichwa katika shamba.” Kwa hiyo akawaacha na hakuwaua pamoja na wale wengine.

9 Basi kile kisima ambacho alitupa zile maiti za watu aliowaua pamoja na Gedalia kilikuwa ni kile kisima ambacho Mfalme Asa alikifanya sehemu ya ulinzi wake dhidi ya Baasha mfalme wa Israeli. Ishmaeli mwana wa Nethania akakijaza kisima hicho kwa maiti.

10 Ishmaeli akawafanya mateka watu wote ambao Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme alikuwa amewaacha huko Mispa na kumweka Gedalia mwana wa Ahikamu juu yao: walikuwa binti za mfalme pamoja na watu wote aliokuwa amewaacha huko. Ishmaeli mwana wa Nethania akawachukua mateka na kuondoka nao, akavuka kwenda kwa Waamoni.

11 Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye waliposikia juu ya uhalifu wote ambao Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa ameufanya,

12 waliwachukua watu wao wote kwenda kupigana na Ishmaeli mwana wa Nethania. Wakakutana naye karibu na bwawa kubwa huko Gibeoni.

13 Ikawa watu wote waliokuwa na Ishmaeli walipomwona Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wa jeshi waliokuwa pamoja naye, wakafurahi.

14 Watu wote ambao Ishmaeli alikuwa amewachukua mateka huko Mispa wakageuka na kumfuata Yohanani mwana wa Karea.

15 Lakini Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na watu wake wanane wakamtoroka Yohanani na kukimbilia kwa Waamoni.

Kukimbilia Misri

16 Ndipo Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye wakawaongoza wote walionusurika kutoka Mispa, ambao walipona kutoka mikononi mwa Ishmaeli mwana wa Nethania baada yake kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu: walikuwa askari, wanawake, watoto na matowashi aliowaleta kutoka Gibeoni.

17 Kisha wakaenda mbele na kutua Geruth-Kimhamu karibu na Bethlehemu wakiwa njiani kwenda Misri

18 ili kuwatoroka Wakaldayo. Waliwaogopa kwa sababu Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa amemuua Gedalia mwana wa Ahikamu, ambaye alikuwa amewekwa na mfalme wa Babeli kuwa mtawala wa nchi.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/41-ccd8f5f9bab8a17c7046626013160691.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 42

Yeremia Ashauri Walionusurika Wasihame Yuda

1 Ndipo maafisa wote wa jeshi, pamoja na Yohanani mwana wa Karea, na Yezania mwana wa Hoshaya, na watu wote kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana wakamjia

2 Yeremia nabii na kumwambia, “Tafadhali sikia maombi yetu na umwombeBwanaMungu wako kwa ajili ya watu hawa wote waliosalia. Kwa kuwa kama unavyoona sasa, ingawa wakati fulani tulikuwa wengi, sasa tumesalia wachache tu.

3 Omba iliBwanaMungu wako atuambie twende wapi na tufanye nini.”

4 Nabii Yeremia akajibu, “Nimewasikia. Kwa hakika nitamwombaBwanaMungu wenu kama mlivyoomba. Nitawaambia kila kitu asemachoBwana, wala sitawaficha chochote.”

5 Kisha wakamwambia Yeremia, “Bwanana awe shahidi wa kweli na mwaminifu kati yetu kama hatutafanya sawasawa na kila kituBwanaMungu wako atakachokutuma utuambie.

6 Likiwa jema au likiwa baya, tutamtiiBwanaMungu wetu, ambaye tunakutuma kwake, ili mambo yote yawe mema kwetu, kwa maana tutamtiiBwanaMungu wetu.”

7 Baada ya siku kumi, neno laBwanalikamjia Yeremia.

8 Kwa hiyo akawaita pamoja Yohanani mwana wa Karea, na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye na watu wote kuanzia mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana.

9 Akawaambia, “Hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa Israeli, ambaye mlinituma kuwasilisha maombi yenu:

10 ‘Kama mkikaa katika nchi hii, nitawajenga wala sitawabomoa, nitawapanda wala sitawangʼoa, kwani ninahuzunishwa na maafa niliyowapiga nayo.

11 Msimwogope mfalme wa Babeli, ambaye sasa mnamwogopa. Msimwogope, asemaBwana, kwa kuwa niko pamoja nanyi, nami nitawaokoa na kuwaponya kutoka mikononi mwake.

12 Nitawaonea huruma ili naye awe na huruma nanyi na kuwarudisha katika nchi yenu.’

13 “Hata hivyo, kama mkisema, ‘Hatutakaa katika nchi hii,’ hivyo mkaacha kumtiiBwanaMungu wenu,

14 nanyi kama mkisema, ‘Hapana, tutakwenda kuishi Misri, mahali ambapo hatutaona vita au kusikia sauti ya tarumbeta au kuwa na njaa ya chakula,’

15 basi sikieni neno laBwana, enyi mabaki ya Yuda. Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Ikiwa mmekusudia kwenda Misri na kufanya makazi huko,

16 basi ule upanga mnaouogopa utawapata huko, na njaa mnayoihofia itawafuata huko Misri, nanyi mtafia huko.

17 Naam, wote waliokusudia kwenda kuishi Misri watakufa kwa upanga, njaa na tauni; hakuna hata mmoja wao atakayenusurika au kuokoka maafa nitakayoyaleta juu yao.’

18 Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kama vile hasira yangu na ghadhabu yangu ilivyomwagwa juu ya wale walioishi Yerusalemu, ndivyo ghadhabu yangu itakavyomwagwa juu yenu mtakapokwenda Misri. Mtakuwa kitu cha kulaania na cha kutisha, cha kulaumia na cha kushutumia, nanyi kamwe hamtaona mahali hapa tena.’

19 “Enyi mabaki ya Yuda,Bwanaamewaambia, ‘Msiende Misri.’ Hakikisheni jambo hili: Ninawaonya leo

20 kwamba mmefanya kosa kubwa mioyoni mwenu mliponituma kwaBwanaMungu wenu na kusema, ‘MwombeBwanaMungu wetu kwa ajili yetu, nawe utuambie kila kitu atakachosema, nasi tutafanya.’

21 Nimewaambieni leo, lakini bado ninyi hamtaki kumtiiBwanaMungu wenu katika yote aliyonituma niwaambie.

22 Basi sasa, hakikisheni jambo hili: Mtakufa kwa upanga, njaa na tauni mahali ambapo mnataka kwenda kuishi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/42-cbf1b9b5829e6b57663bebfd3101cb3a.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 43

Yeremia Apelekwa Misri

1 Yeremia alipomaliza kuwaambia watu maneno yote yaBwanaMungu wao, yaani kila kituBwanaalichokuwa amemtuma kuwaambia,

2 Azaria mwana wa Hoshaya, na Yohanani mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakamwambia Yeremia, “Wewe unasema uongo!BwanaMungu wetu hajakutuma kusema, ‘Kamwe msiende Misri kukaa huko.’

3 Lakini Baruku mwana wa Neria anakuchochea dhidi yetu ili ututie mikononi mwa Wakaldayo, ili watuue au watuchukue uhamishoni Babeli.”

4 Basi Yohanani mwana wa Karea, na maafisa wote wa jeshi, na watu wote wakakataa kutii amri yaBwanaya kukaa katika nchi ya Yuda.

5 Badala yake, Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi wakawaongoza mabaki yote ya Yuda waliokuwa wamerudi kuishi katika nchi ya Yuda kutoka mataifa yote ambayo walikuwa wametawanywa.

6 Pia wakawaongoza wanaume wote, wanawake na watoto, na binti za mfalme ambao Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme alikuwa amewaacha na Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani, na nabii Yeremia, na Baruku mwana wa Neria.

7 Kwa hiyo wakaingia Misri kwa kutokumtiiBwana, wakaenda mpaka Tahpanhesi.

8 Huko Tahpanhesi neno laBwanalikamjia Yeremia kusema:

9 “Wayahudi wakiwa wanaona, chukua baadhi ya mawe makubwa na kuyazika katika udongo wa mfinyanzi katika njia iliyojengwa kwa matofali katika ingilio la jumba la kifalme la Farao huko Tahpanhesi.

10 Kisha uwaambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Nitamtumania mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, nami nitakiweka kiti chake cha enzi juu ya haya mawe niliyoyazika hapa, naye atatandaza hema yake ya ufalme juu yake.

11 Atakuja na kuishambulia Misri, akiwaua wale waliokusudiwa kuuawa, awateke mateka wale waliokusudiwa kutekwa, na upanga kwa wale waliokusudiwa upanga.

12 Atachoma moto mahekalu yao ya miungu ya Misri, atachoma mahekalu yao na kuteka miungu yao. Kama vile mchungaji ajizungushiavyo vazi lake ndivyo atakavyojizungushia Misri na kuondoka mahali hapo bila kudhurika.

13 Humo ndani ya hekalu la juanchini ya Misri atabomoa nguzo za ibada, na kuteketeza kwa moto mahekalu ya miungu wa Misri.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/43-88d879b29483712a980b15c7665d6430.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 44

Maafa Kwa Sababu Ya Ibada Za Sanamu

1 Neno hili lilimjia Yeremia kuhusu Wayahudi wote waishio Misri, huko Migdoli, Tahpanhesi na Memfisi,katika nchi ya Pathrosikusema:

2 “Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Mliona maangamizi makubwa niliyoyaleta juu ya Yerusalemu na juu ya miji yote ya Yuda. Leo imeachwa ukiwa na magofu

3 kwa sababu ya uovu waliokuwa wameufanya. Walinikasirisha kwa kufukiza uvumba na kwa kuabudu miungu mingine ambayo kamwe wao, wala ninyi, wala baba zenu hawakuifahamu.

4 Tena na tena, niliwatuma watumishi wangu manabii ambao walisema, ‘Msifanye jambo hili la kuchukiza ambalo nalichukia!’

5 Lakini hawakusikiliza wala hawakujali, hawakugeuka ili kuuacha uovu wao, wala hawakuacha kufukiza uvumba kwa miungu mingine.

6 Kwa hiyo hasira yangu kali ilimwagika, ikawaka dhidi ya miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu, na kuifanya ukiwa na magofu kama ilivyo leo.

7 “Basi hili ndiloBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Kwa nini kujiletea maafa makubwa kama haya juu yenu kwa kujikatilia mbali kutoka Yuda wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, hata kujiacha bila mabaki?

8 Kwa nini kuichochea hasira yangu kwa kile ambacho mikono yenu imekitengeneza, mkaifukizia uvumba miungu mingine huko Misri, mahali mlipokuja kuishi? Mtajiangamiza wenyewe na kujifanya kitu cha kulaania na shutumu miongoni mwa mataifa yote duniani.

9 Je, mmesahau uovu uliotendwa na baba zenu, na wafalme na malkia wa Yuda, na uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na barabara za Yerusalemu?

10 Mpaka leo hawajajinyenyekeza au kuonyesha heshima, wala hawajafuata sheria yangu na amri nilizoweka mbele yenu na baba zenu.

11 “Kwa hiyo, hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Mimi nimekusudia kuleta maafa juu yenu, na kuiangamiza Yuda yote.

12 Nitawaondoa mabaki ya Yuda waliokusudia kwenda Misri kukaa humo. Wote wataangamia huko Misri, wataanguka kwa upanga au kufa kwa njaa. Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana, watakufa kwa upanga au njaa. Watakuwa kitu cha kulaania na cha kutisha, cha laumu na shutumu.

13 Nitawaadhibu wale waishio Misri kwa upanga, njaa na tauni kama nilivyoiadhibu Yerusalemu.

14 Hakuna hata mmoja wa mabaki ya Yuda ambaye amekwenda kuishi Misri atakayeepuka au kunusurika ili kurudi katika nchi ya Yuda, ambayo wanaitamani sana kurudi na kuishi ndani yake, hakuna hata mmoja atakayerudi isipokuwa wakimbizi wachache.”

15 Kisha wanaume wote ambao walijua kwamba wake zao walikuwa wakifukiza uvumba kwa miungu mingine, pamoja na wanawake wote waliokuwako, yaani, kusanyiko kubwa na watu wote walioishi nchi ya Misri na Pathrosi, wakamwambia Yeremia,

16 “Hatutausikiliza ujumbe uliotuambia katika jina laBwana!

17 Hakika tutafanya kila kitu tulichosema tutakifanya: Tutafukiza uvumba kwa Malkia wa Mbinguni na tutammiminia sadaka zetu za kinywaji kama vile sisi na baba zetu, wafalme wetu na maafisa wetu tulivyofanya katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu. Wakati ule tulikuwa na chakula tele, tulikuwa matajiri wala hatukupata dhara lolote.

18 Lakini tangu tulipoacha kumfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka za kinywaji, hatupati chochote, na tumekuwa tukiangamizwa kwa upanga na njaa.”

19 Wanawake wakaongeza kusema, “Wakati tulipomfukizia uvumba Malkia wa Mbinguni na kummiminia sadaka zetu za kinywaji, je, waume zetu hawakujua kwamba tulikuwa tukitengeneza maandazi kwa mfano wake, na kummiminia yeye sadaka za kinywaji?”

20 Ndipo Yeremia akawaambia watu wote, wanaume na wanawake waliokuwa wakimjibu,

21 “Je,Bwanahakukumbuka na kufikiri juu ya uvumba uliofukizwa katika miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu na ninyi pamoja na baba zenu, wafalme wenu, maafisa wenu na watu wa nchi?

22 Bwanaalipokuwa hawezi kuendelea kuvumilia matendo yenu maovu na mambo ya machukizo mliyoyafanya, nchi yenu ilikuwa kitu cha kulaania na kuachwa ukiwa pasipo wakazi, kama ilivyo leo.

23 Kwa sababu mmefukiza uvumba na kufanya dhambi dhidi yaBwana, nanyi hamkumtii wala kufuata sheria yake au amri zake au maagizo yake, maafa haya yamekuja juu yenu, kama mnavyoona sasa.”

24 Kisha Yeremia akawaambia watu wote, pamoja na wanawake, “Sikieni neno laBwana, enyi watu wote wa Yuda mlioko Misri.

25 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Ninyi na wake zenu mmeonyesha kwa matendo yenu kile mlichoahidi mliposema, ‘Hakika tutatimiza nadhiri tulizoziweka za kumfukizia uvumba na kummiminia sadaka za kinywaji Malkia wa Mbinguni.’

“Endeleeni basi, fanyeni yale mliyoahidi! Timizeni nadhiri zenu!

26 Lakini sikieni neno laBwana, enyi Wayahudi wote mnaoishi Misri: ‘Ninaapa kwa Jina langu lililo kuu,’ asemaBwana, ‘kwamba hakuna hata mmoja atokaye Yuda anayeishi popote Misri ambaye kamwe ataomba tena kwa Jina langu au kuapa, akisema, “Hakika kamaBwanaMwenyezi aishivyo.”

27 Kwa maana ninawaangalia kwa ajili ya madhara, wala sio kwa mema. Wayahudi walioko Misri wataangamia kwa upanga na njaa, hadi wote watakapoangamizwa.

28 Wale watakaonusurika upanga na kurudi katika nchi ya Yuda kutoka Misri watakuwa wachache sana. Ndipo mabaki wote wa Yuda waliokuja kuishi Misri watakapojua ni neno la nani litakalosimama, kwamba ni langu au lao.

29 “ ‘Hii itakuwa ndiyo ishara kwenu kwamba nitawaadhibu mahali hapa, asemaBwana, ili mpate kujua kuwa onyo langu la madhara dhidi yenu hakika litatimizwa.’

30 Hili ndilo asemaloBwana: ‘Nitamtia Farao Hofra mfalme wa Misri mikononi mwa adui zake wanaoutafuta uhai wake, kama vile nilivyomtia Sedekia mfalme wa Yuda mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, adui aliyekuwa akiutafuta uhai wake.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/44-ff193ecfab339583c2c87581a0c564c8.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 45

Ujumbe Kwa Baruku

1 Hili ndilo nabii Yeremia alilomwambia Baruku mwana wa Neria katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, baada ya Baruku kuandika katika kitabu maneno ambayo yalitoka kinywani mwa Yeremia wakati ule:

2 “Hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli, akuambialo wewe Baruku:

3 Ulisema, ‘Ole wangu!Bwanaameongeza huzuni juu ya maumivu yangu, nimechoka kwa kulia kwa uchungu wala sipati pumziko.’ ”

4 Bwanaakasema, “Mwambie hivi: ‘Hili ndilo asemaloBwana: Nitakibomoa kile nilichokijenga, na kungʼoa kile nilichokipanda katika nchi yote.

5 Je, utajitafutia mambo makubwa kwa ajili yako mwenyewe? Usiyatafute hayo. Kwa kuwa nitaleta maangamizi juu ya watu wote, asemaBwana, lakini popote utakapokwenda, nitayaokoa maisha yako.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/45-ec89824bdbfc3cb8636fd7a64eb5df53.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 46

Ujumbe Kuhusu Misri

1 Hili ni neno laBwanalililomjia nabii Yeremia kuhusu mataifa:

2 Kuhusu Misri:

Huu ni ujumbe dhidi ya jeshi la Farao Neko mfalme wa Misri, lililoshindwa huko Karkemishi kwenye Mto Frati na Nebukadneza mfalme wa Babeli, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:

3 “Wekeni tayari ngao zenu, kubwa na ndogo,

mtoke kwa ajili ya vita!

4 Fungieni farasi lijamu,

pandeni farasi!

Shikeni nafasi zenu

mkiwa mmevaa chapeo!

Isugueni mikuki yenu,

vaeni dirii vifuani!

5 Je, ninaona nini?

Wametiwa hofu,

wanarudi nyuma,

askari wao wameshindwa.

Wanakimbia kwa haraka

pasipo kutazama nyuma,

tena kuna hofu kuu kila upande,”

asemaBwana.

6 Walio wepesi na wenye mbio hawawezi kukimbia,

wala wenye nguvu hawawezi kutoroka.

Kaskazini, kando ya Mto Frati,

wanajikwaa na kuanguka.

7 “Ni nani huyu ajiinuaye kama Mto Naili,

kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi?

8 Misri hujiinua kama Mto Naili,

kama mito yenye maji yanayofanya mawimbi.

Husema, ‘Nitainuka na kufunika dunia,

nitaiangamiza miji na watu wake.’

9 Songeni mbele, enyi farasi!

Endesheni kwa ukali, enyi magari ya farasi,

Endeleeni mbele, enyi mashujaa:

watu wa Kushina Putuwachukuao ngao,

watu wa Ludiwavutao upinde.

10 Lakini ile siku ni ya Bwana,BwanaMwenye Nguvu Zote,

siku ya kulipiza kisasi,

kisasi juu ya adui zake.

Upanga utakula hata utakapotosheka,

hadi utakapozima kiu yake kwa damu.

Kwa maana Bwana,BwanaMwenye Nguvu Zote, atatoa dhabihu

kwenye nchi ya kaskazini, kando ya Mto Frati.

11 “Panda hadi Gileadi ukapate zeri,

ee Bikira Binti wa Misri.

Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio;

huwezi kupona.

12 Mataifa yatasikia juu ya aibu yako,

kilio chako kitaijaza dunia.

Shujaa mmoja atajikwaa juu ya mwingine,

nao wataanguka chini pamoja.”

13 Huu ndio ujumbeBwanaaliomwambia nabii Yeremia kuhusu kuja kwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ili kuishambulia Misri:

14 “Tangaza hili katika Misri, nawe ulihubiri katika Migdoli,

hubiri pia katika Memfisina Tahpanhesi:

‘Shikeni nafasi zenu na mwe tayari,

kwa kuwa upanga unawala wale wanaokuzunguka.’

15 Kwa nini mashujaa wako wamesombwa

na kupelekwa mbali?

Hawawezi kusimama, kwa maanaBwana

atawasukuma awaangushe chini.

16 Watajikwaa mara kwa mara,

wataangukiana wao kwa wao.

Watasema, ‘Amka, turudi

kwa watu wetu na nchi yetu,

mbali na upanga wa mtesi.’

17 Huko watatangaza,

‘Farao mfalme wa Misri ni makelele tu,

amekosa wasaa wake.’

18 “Kwa hakika kama niishivyo,” asema Mfalme,

ambaye jina lake niBwanaMwenye Nguvu Zote,

“mmoja atakuja ambaye ni kama Tabori miongoni mwa milima,

kama Karmeli kando ya bahari.

19 Funga mizigo yako kwenda uhamishoni,

wewe ukaaye Misri,

kwa kuwa Memfisi utaangamizwa

na kuwa magofu pasipo mkazi.

20 “Misri ni mtamba mzuri,

lakini kipanga anakuja dhidi yake kutoka kaskazini.

21 Askari wake waliokodiwa katika safu zake

wako kama ndama walionenepeshwa.

Wao pia watageuka na kukimbia pamoja,

hawataweza kuhimili vita,

kwa maana siku ya msiba inakuja juu yao,

wakati wao wa kuadhibiwa.

22 Misri atatoa sauti kama ya nyoka anayekimbia

kadiri adui anavyowasogelea na majeshi,

watakuja dhidi yake wakiwa na mashoka,

kama watu wakatao miti.

23 Wataufyeka msitu wake,”

asemaBwana,

“hata kama umesongamana kiasi gani.

Ni wengi kuliko nzige,

hawawezi kuhesabika.

24 Binti wa Misri ataaibishwa,

atatiwa mikononi mwa watu wa kaskazini.”

25 BwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asema: “Nakaribia kuleta adhabu juu ya Amoni mungu wa Thebesi,na juu ya Farao, Misri na miungu yake, na wafalme wake, pamoja na wale wanaomtegemea Farao.

26 Nitawatia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wao, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na maafisa wake. Hatimaye, hata hivyo, Misri itakaliwa kama nyakati zilizopita,” asemaBwana.

27 “Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,

usifadhaike, ee Israeli.

Hakika nitakuokoa kutoka nchi za mbali,

uzao wako kutoka nchi ya uhamisho wao.

Yakobo atakuwa tena na amani na salama,

wala hakuna hata mmoja atakayewatia hofu.

28 Usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu,

kwa maana mimi niko pamoja nawe,”

asemaBwana.

“Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote

ambayo miongoni mwake nimekutawanya,

sitakuangamiza wewe kabisa.

Nitakurudi, lakini kwa haki tu,

wala sitakuacha kabisa bila kukuadhibu.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/46-0482eba6ec303002e91d40b4bb6f9d80.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 47

Ujumbe Kuhusu Wafilisti

1 Hili ndilo neno laBwanalililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaishambulia Gaza:

2 Hili ndilo asemaloBwana:

“Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini,

yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana.

Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyomo ndani yake,

miji na wale waishio ndani yake.

Watu watapiga kelele;

wote waishio katika nchi wataomboleza

3 kwa sauti ya kwato za farasi waendao mbio,

kwa sauti ya magari ya adui

na mngurumo wa magurudumu yake.

Baba hawatageuka kuwasaidia watoto wao,

mikono yao italegea.

4 Kwa maana siku imewadia

kuwaangamiza Wafilisti wote

na kuwakatilia mbali walionusurika wote

ambao wangeweza kusaidia Tiro na Sidoni.

Bwanaanakaribia kuwaangamiza Wafilisti,

mabaki toka pwani za Kaftori.

5 Gaza atanyoa kichwa chake katika kuomboleza,

Ashkeloni atanyamazishwa.

Enyi mabaki kwenye tambarare,

mtajikatakata wenyewe mpaka lini?

6 “Mnalia, ‘Aa, upanga waBwana,

utaendelea mpaka lini ndipo upumzike?

Rudi ndani ya ala yako;

acha na utulie.’

7 Lakini upanga utatuliaje

wakatiBwanaameuamuru,

wakati ameuagiza kuishambulia Ashkeloni

pamoja na pwani yake?”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/47-c3edb0f62bd1412519000f571c8e9abe.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 48

Ujumbe Kuhusu Moabu

1 Kuhusu Moabu:

Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo:

“Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa.

Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa;

Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa.

2 Moabu haitasifiwa tena;

huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake:

‘Njooni na tuangamize taifa lile.’

Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa;

upanga utakufuatia.

3 Sikiliza kilio kutoka Horonaimu,

kilio cha maangamizi makuu na uharibifu.

4 Moabu utavunjwa,

wadogo wake watapiga kelele.

5 Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi,

wakilia kwa uchungu wanapotembea,

kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu,

kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika.

6 Kimbieni! Okoeni maisha yenu,

kuweni kama kichaka jangwani.

7 Kwa kuwa mmetumainia matendo yenu na mali zenu,

ninyi pia mtachukuliwa mateka,

naye Kemoshiatakwenda uhamishoni,

pamoja na makuhani wake na maafisa wake.

8 Mharabu atakuja dhidi ya kila mji,

wala hakuna mji utakaookoka.

Bonde litaangamizwa na uwanda utaharibiwa,

kwa sababuBwanaamesema.

9 Wekeni chumvi kwa ajili ya Moabu,

kwa kuwa ataangamizwa;

miji yake itakuwa ukiwa,

pasipo kuwa na mtu atakayeishi ndani yake.

10 “Alaaniwe yeye afanyaye kazi yaBwanakwa hila!

Alaaniwe yeye auzuiaye upanga wake usimwage damu!

11 “Moabu amestarehe tangu ujana wake,

kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake,

haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine,

hajaenda uhamishoni.

Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo,

nayo harufu yake haijabadilika.

12 Lakini siku zinakuja,”

asemaBwana,

“nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia,

nao watamimina;

wataacha magudulia yake yakiwa matupu

na kuvunja mitungi yake.

13 Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi,

kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu

walipotegemea mungu wa Betheli.

14 “Mwawezaje kusema, ‘Sisi ni mashujaa,

watu jasiri katika vita’?

15 Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa,

vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,”

asema Mfalme, ambaye jina lake

niBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote.

16 “Kuanguka kwa Moabu kumekaribia,

janga kubwa litamjia kwa haraka.

17 Ombolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaomzunguka,

ninyi nyote mnaojua sifa zake,

semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika fimbo ya kifalme yenye nguvu,

tazama jinsi ilivyovunjika fimbo iliyotukuka!’

18 “Shuka kutoka fahari yako

na uketi katika ardhi iliyokauka,

enyi wenyeji wa Binti wa Diboni,

kwa maana yeye aangamizaye Moabu atakuja dhidi yako,

na kuangamiza miji yako iliyozungushiwa maboma.

19 Simama kando ya barabara na utazame,

wewe unayeishi Aroeri.

Muulize mwanaume anayekimbia

na mwanamke anayetoroka,

waulize, ‘Kumetokea nini?’

20 Moabu amefedheheshwa, kwa kuwa amevunjavunjwa.

Lieni kwa huzuni na kupiga kelele!

Tangazeni kando ya Arnoni

kwamba Moabu ameangamizwa.

21 Hukumu imefika kwenye uwanda wa juu:

katika Holoni, Yahasa na Mefaathi,

22 katika Diboni, Nebo

na Beth-Diblathaimu,

23 katika Kiriathaimu, Beth-Gamuli

na Beth-Meoni,

24 katika Keriothi na Bosra;

kwa miji yote ya Moabu,

iliyoko mbali na karibu.

25 Pembeya Moabu imekatwa,

mkono wake umevunjwa,”

asemaBwana.

26 “Mlevye,

kwa kuwa amemdharauBwana.

Moabu na agaegae katika matapishi yake,

yeye na awe kitu cha dhihaka.

27 Je, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa?

Je, alikamatwa miongoni mwa wezi,

kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharau

kila mara unapozungumza juu yake?

28 Ondokeni kwenye miji yenu, mkaishi katikati ya miamba,

enyi mnaoishi Moabu.

Kuweni kama huwa ambaye hutengeneza kiota chake

kwenye mdomo wa pango.

29 “Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu:

kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno,

kiburi chake na ufidhuli wake,

na kujivuna kwa moyo wake.

30 Ninaujua ujeuri wake, lakini ni bure,”

asemaBwana,

“nako kujisifu kwake hakumsaidii chochote.

31 Kwa hiyo namlilia Moabu,

kwa ajili ya Moabu yote ninalia,

ninaomboleza kwa ajili

ya watu wa Kir-Haresethi.

32 Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo,

enyi mizabibu ya Sibma.

Matawi yako yameenea hadi baharini;

yamefika hadi bahari ya Yazeri.

Mharabu ameyaangukia matunda yako yaliyoiva

na mizabibu yako iliyoiva.

33 Shangwe na furaha vimetoweka

kutoka bustani na mashamba ya Moabu.

Nimekomesha kutiririka kwa divai kutoka mashinikizo;

hakuna hata mmoja ayakanyagaye kwa kelele za shangwe.

Ingawa kuna kelele,

sio kelele za shangwe.

34 “Sauti ya kilio chao inapanda

kutoka Heshboni hadi Eleale na Yahazi,

kutoka Soari hadi Horonaimu na Eglath-Shelishiya,

kwa kuwa hata maji ya Nimrimu yamekauka.

35 Nitakomesha wale wote katika Moabu

watoao sadaka mahali pa juu,

na kufukiza uvumba kwa miungu yao,”

asemaBwana.

36 “Kwa hiyo moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama filimbi;

unaomboleza kama filimbi kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi.

Utajiri waliojipatia umetoweka.

37 Kila kichwa kimenyolewa

na kila mwenye ndevu zimekatwa;

kila mkono umekatwa

na kila kiuno kimefunikwa kwa nguo ya gunia.

38 Juu ya mapaa yote katika Moabu

na katika viwanja

hakuna kitu chochote isipokuwa maombolezo,

kwa kuwa nimemvunja Moabu

kama gudulia ambalo hakuna mtu yeyote anayelitaka,”

asemaBwana.

39 “Tazama jinsi alivyovunjikavunjika!

Jinsi wanavyolia kwa huzuni!

Tazama jinsi Moabu anavyogeuka kwa aibu!

Moabu amekuwa kitu cha kudhihakiwa,

kitu cha kutisha kwa wale wote

wanaomzunguka.”

40 Hili ndilo asemaloBwana:

“Tazama! Tai anashuka chini,

akitanda mabawa yake juu ya Moabu.

41 Miji itatekwa na ngome zake

zitatwaliwa.

Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Moabu

itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa.

42 Moabu ataangamizwa kama taifa

kwa sababu amemdharauBwana.

43 Hofu kuu, shimo na mtego vinawangojea,

enyi watu wa Moabu,”

asemaBwana.

44 “Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu

ataanguka ndani ya shimo,

yeyote atakayepanda kutoka shimoni,

atanaswa katika mtego,

kwa sababu nitaletea Moabu

mwaka wa adhabu yake,”

asemaBwana.

45 “Katika kivuli cha Heshboni,

wakimbizi wamesimama pasipo msaada,

kwa kuwa moto umezimika huko Heshboni,

mwali wa moto kutoka katikati ya Sihoni;

unaunguza vipaji vya nyuso za Moabu,

mafuvu yao wenye kujivuna kwa kelele.

46 Ole wako, ee Moabu!

Watu wa Kemoshi wameangamizwa;

wana wako wamepelekwa uhamishoni

na binti zako wamechukuliwa mateka.

47 “Lakini nitarudisha mateka wa Moabu,

katika siku zijazo,”

asemaBwana.

Huu ndio mwisho wa hukumu juu ya Moabu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/48-f4cb2d105b31349f0d5963d492217cd1.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 49

Ujumbe Kuhusu Amoni

1 Kuhusu Waamoni:

Hili ndilo asemaloBwana:

“Je, Israeli hana wana?

Je, hana warithi?

Kwa nini basi Moleki amechukua milki ya Gadi?

Kwa nini watu wake wanaishi katika miji yake?

2 Lakini siku zinakuja,”

asemaBwana,

“nitakapopiga kelele ya vita

dhidi ya Raba mji wa Waamoni;

utakuwa kilima cha magofu,

navyo vijiji vinavyouzunguka

vitateketezwa kwa moto.

Kisha Israeli atawafukuza

wale waliomfukuza,”

asemaBwana.

3 “Lia kwa huzuni, ee Heshboni, kwa kuwa Ai umeangamizwa!

Pigeni kelele, enyi wakazi wa Raba!

Vaeni nguo za gunia na kuomboleza,

kimbieni hapa na pale ndani ya kuta,

kwa kuwa Moleki atakwenda uhamishoni,

yeye pamoja na makuhani na maafisa wake.

4 Kwa nini unajivunia mabonde yako,

kujivunia mabonde yako yaliyozaa sana?

Ee binti usiye mwaminifu, unayeutumainia utajiri wako na kusema,

‘Ni nani atakayenishambulia?’

5 Nitaleta hofu kuu juu yako

kutoka kwa wale wote wanaokuzunguka,”

asema Bwana,BwanaMwenye Nguvu Zote.

“Kila mmoja wenu ataondolewa,

wala hakuna hata mmoja atakayekusanya wakimbizi.

6 “Lakini hatimaye,

nitarudisha mateka wa Waamoni,”

asemaBwana.

Ujumbe Kuhusu Edomu

7 Kuhusu Edomu:

Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote:

“Je, hakuna tena hekima katika Temani?

Je, shauri limewapotea wenye busara?

Je, hekima yao imechakaa?

8 Geuka na ukimbie, jifiche katika mapango marefu kabisa,

wewe uishiye Dedani,

kwa kuwa nitaleta maafa juu ya Esau

wakati nitakapomwadhibu.

9 Je, kama wachuma zabibu wangekuja kwako,

wasingebakiza zabibu chache?

Kama wezi wangekujia usiku,

je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji?

10 Lakini nitamvua Esau nguo abaki uchi,

nitayafunua maficho yake,

ili asiweze kujificha.

Watoto wake, jamaa na majirani wataangamia,

naye hatakuwepo tena.

11 Waache yatima wako; nitayalinda maisha yao.

Wajane wako pia

wanaweza kunitumaini mimi.”

12 Hili ndilo asemaloBwana: “Kama wale wasiostahili kukinywea kikombe ni lazima wakinywe, kwa nini wewe usiadhibiwe? Hutakwepa kuadhibiwa, ni lazima ukinywe.

13 Ninaapa kwa nafsi yangu,” asemaBwana, “kwamba Bosra utakuwa magofu na kitu cha kutisha, cha aibu na cha kulaania; miji yake yote itakuwa magofu milele.”

14 Nimesikia ujumbe kutoka kwaBwana:

Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema,

“Jikusanyeni ili kuushambulia!

Inukeni kwa ajili ya vita!”

15 “Sasa nitakufanya uwe mdogo miongoni mwa mataifa,

aliyedharauliwa miongoni mwa watu.

16 Vitisho vyako na kiburi cha moyo wako

vimekudanganya,

wewe unayeishi katika majabali ya miamba,

wewe unayedumu katika miinuko ya kilima.

Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai,

nitakushusha chini kutoka huko,”

asemaBwana.

17 “Edomu atakuwa kitu cha kuogofya;

wote wapitao karibu

watashangaa na kuzomea

kwa sababu ya majeraha yake yote.

18 Kama vile Sodoma na Gomora zilivyoangamizwa,

pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,”

asemaBwana,

“vivyo hivyo hakuna mtu yeyote atakayeishi humo.

Naam, hakuna mtu yeyote atakayekaa humo.

19 “Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani

kuja kwenye nchi ya malisho mengi,

ndivyo nitamfukuza Edomu kutoka nchi yake ghafula.

Ni nani aliye mteule nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili?

Ni nani aliye kama mimi,

na ni nani awezaye kunipinga?

Tena ni mchungaji yupi awezaye

kusimama kinyume nami?”

20 Kwa hiyo, sikia kileBwanaalichokipanga dhidi ya Edomu,

kile alichokusudia dhidi ya wale waishio Temani:

Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali;

yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.

21 Kwa sauti ya anguko lao, dunia itatetemeka.

Kilio chao kitasikika hadi Bahari ya Shamu.

22 Tazama! Tai atapaa juu angani na kuruka chini kwa ghafula,

akitandaza mabawa yake juu ya Bosra.

Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Edomu

itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa.

Ujumbe Kuhusu Dameski

23 Kuhusu Dameski:

“Hamathi na Arpadi imetahayarika,

kwa kuwa wamesikia habari mbaya.

Wamevunjika moyo na wametaabika

kama bahari iliyochafuka.

24 Dameski amedhoofika,

amegeuka na kukimbia,

hofu ya ghafula imemkamata sana;

amepatwa na uchungu na maumivu,

maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.

25 Kwa nini mji ambao unajulikana haujaachwa,

mji ambao ninaupenda?

26 Hakika, vijana wake wanaume wataanguka barabarani;

askari wake wote watanyamazishwa siku hiyo,”

asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.

27 “Nitatia moto kuta za Dameski;

utaangamiza ngome za Ben-Hadadi.”

Ujumbe Kuhusu Kedari Na Hazori

28 Kuhusu Kedari na falme za Hazori, ambazo Nebukadneza mfalme wa Babeli alizishambulia:

Hili ndilo asemaloBwana:

“Inuka, ushambulie Kedari

na kuwaangamiza watu wa mashariki.

29 Hema zao na makundi yao ya kondoo yatachukuliwa;

vibanda vyao vitatwaliwa

pamoja na mali zao zote na ngamia zao.

Watu watawapigia kelele,

‘Hofu kuu iko kila upande!’

30 “Kimbieni haraka!

Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mkaao Hazori,”

asemaBwana.

“Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga shauri baya dhidi yenu;

amebuni hila dhidi yenu.

31 “Inuka na ulishambulie taifa lililo starehe,

linaloishi kwa kujiamini,”

asemaBwana,

“taifa lisilo na malango wala makomeo;

watu wake huishi peke yao.

32 Ngamia wao watakuwa nyara,

nayo makundi yao makubwa ya ngʼombe yatatekwa.

Wale walio maeneo ya mbali

nitawatawanya pande zote,

nami nitaleta maafa juu yao

kutoka kila upande,”

asemaBwana.

33 “Hazori itakuwa makao ya mbweha,

mahali pa ukiwa milele.

Hakuna yeyote atakayeishi humo;

hakuna mtu atakayekaa ndani yake.”

Ujumbe Kuhusu Elamu

34 Hili ndilo neno laBwanalililomjia nabii Yeremia kuhusu Elamu, mapema katika utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda:

35 Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo:

“Tazama, nitavunja upinde wa Elamu,

ulio tegemeo la nguvu zao.

36 Nitaleta pepo nne dhidi ya Elamu

toka pande nne za mbingu,

nitawatawanya katika hizo pande nne,

wala hapatakuwa na taifa

ambalo watu wa Elamu waliofukuzwa

hawatakwenda.

37 Nitamfadhaisha Elamu mbele ya adui zao,

mbele yao wale wanaotafuta uhai wao;

nitaleta maafa juu yao,

naam, hasira yangu kali,”

asemaBwana.

“Nitawafuatia kwa upanga

mpaka nitakapowamaliza.

38 Nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu

na kumwangamiza mfalme wake na maafisa wake,”

asemaBwana.

39 “Lakini nitarudisha mateka wa Elamu

katika siku zijazo,”

asemaBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/49-b499d4b1d5b8ec8b7770b9dfae75750a.mp3?version_id=1627—