Categories
Yeremia

Yeremia 20

Yeremia Ateswa Na Pashuri

1 Ikawa kuhani Pashuri mwana wa Imeri, mkuu wa maafisa wa Hekalu laBwana, alipomsikia Yeremia akitoa unabii juu ya mambo haya,

2 akaamuru Yeremia nabii apigwe na kufungwa kwenye mkatale katika Lango la Juu la Benyamini huko Hekaluni laBwana.

3 Siku ya pili Pashuri alipomwachia kutoka kwenye mkatale, Yeremia akamwambia, “Bwanahakukuita jina lako kuwa Pashuri bali Magor-Misabibu.

4 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwana: ‘Nitakufanya kuwa hofu kuu kwako wewe mwenyewe na rafiki zako wote, na kwa macho yako mwenyewe utawaona wakianguka kwa upanga wa adui zao. Nitawatia Yuda wote mikononi mwa mfalme wa Babeli, ambaye atawachukua na kuwapeleka Babeli, ama awaue kwa upanga.

5 Nitatia utajiri wote wa mji huu kwa adui zao: yaani mazao yao yote, vitu vyao vyote vya thamani, na hazina zote za wafalme wa Yuda. Watavitwaa kwa nyara na kuvipeleka Babeli.

6 Nawe Pashuri pamoja na wote waishio katika nyumba yako mtakwenda uhamishoni Babeli. Mtafia humo na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ”

Malalamiko Ya Yeremia

7 EeBwana, umenidanganya,

nami nikadanganyika;

wewe una nguvu kuniliko,

nawe umenishinda.

Ninadharauliwa mchana kutwa,

kila mmoja ananidhihaki.

8 Kila ninenapo, ninapiga kelele

nikitangaza ukatili na uharibifu.

Kwa hiyo neno laBwanalimeniletea matukano

na mashutumu mchana kutwa.

9 Lakini kama nikisema, “Sitamtaja

wala kusema tena kwa jina lake,”

neno lake linawaka ndani ya moyo wangu kama moto,

moto uliofungwa ndani ya mifupa yangu.

Nimechoka sana kwa kulizuia ndani mwangu;

kweli, siwezi kujizuia.

10 Ninasikia minongʼono mingi,

“Hofu iko pande zote!

Mshtakini! Twendeni tumshtaki!”

Rafiki zangu wote wananisubiri niteleze,

wakisema,

“Labda atadanganyika;

kisha tutamshinda

na kulipiza kisasi juu yake.”

11 LakiniBwanayu pamoja nami

kama shujaa mwenye nguvu;

hivyo washtaki wangu watajikwaa

na kamwe hawatashinda.

Watashindwa, nao wataaibika kabisa;

kukosa adabu kwao hakutasahauliwa.

12 EeBwanaMwenye Nguvu Zote,

wewe umjaribuye mwenye haki

na kupima moyo na nia,

hebu nione ukilipiza kisasi juu yao,

kwa maana kwako

nimeliweka shauri langu.

13 MwimbieniBwana!

MpeniBwanasifa!

Yeye huokoa uhai wa mhitaji

kutoka mikononi mwa waovu.

14 Ilaaniwe siku niliyozaliwa!

Nayo isibarikiwe ile siku

mama yangu aliyonizaa!

15 Alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari,

yule aliyemfanya afurahi sana, akisema,

“Mtoto amezaliwa kwako,

tena mtoto wa kiume!”

16 Mtu huyo na awe kama miji ile

ambayoBwanaMungu

aliiangamiza bila huruma.

Yeye na asikie maombolezo asubuhi

na kilio cha vita adhuhuri.

17 Kwa sababu hakuniua nikiwa tumboni,

hivyo mama yangu angekuwa kaburi langu,

nalo tumbo lake la uzazi

lingebaki kuwa kubwa daima.

18 Kwa nini basi nilitoka tumboni

ili kuona taabu na huzuni,

na kuzimaliza siku zangu katika aibu?

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/20-cedf2c89bb12c3fc49c923a2d0582c7b.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 21

Mungu Anakataa Ombi La Sedekia

1 Neno lilimjia Yeremia kutoka kwaBwanawakati Mfalme Sedekia alipowatuma Pashuri mwana wa Malkiya, na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwake, kusema:

2 “Tuulizie sasa kwaBwana, kwa sababu Nebukadneza mfalme wa Babeli anatushambulia. LabdaBwanaatatenda maajabu kwa ajili yetu kama nyakati zilizopita, ili Nebukadneza atuondokee.”

3 Lakini Yeremia akawajibu, “Mwambieni Sedekia,

4 ‘Hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kuwageuzia silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo mnatumia kupigana na mfalme wa Babeli na Wakaldayo ambao wako nje ya ukuta wakiwazunguka kwa jeshi. Nami nitawakusanya ndani ya mji huu.

5 Mimi mwenyewe nitapigana dhidi yenu kwa mkono wangu ulionyooshwa na mkono wa nguvu, kwa hasira na ghadhabu kali na ukali mwingi.

6 Nitawaangamiza waishio katika mji huu, watu na wanyama, nao watauawa kwa tauni ya kutisha.

7 Baada ya hayo, nitamtia Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na watu wa mji huu ambao walinusurika tauni, upanga na njaa, mkononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, na kwa adui zao wale wanaotafuta uhai wao. Atawaua kwa upanga; hatakuwa na rehema juu yao au huruma wala kuwasikitikia,’ asemaBwana.

8 “Zaidi ya hayo, waambie watu hawa, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Tazama, naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti.

9 Yeyote atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni. Lakini yeyote atakayetoka na kujisalimisha kwa Wakaldayo ambao wameuzunguka mji huu kwa jeshi, atanusurika, naye ataishi.

10 Nimekusudia kuufanyia mji huu jambo baya, wala si jema. Utatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto, asemaBwana.’

11 “Zaidi ya hayo, ambia nyumba ya mfalme ya Yuda, ‘Sikia neno laBwana,

12 Ewe nyumba ya Daudi, hili ndiloBwanaasemalo:

“ ‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi,

mwokoeni mikononi mwa mdhalimu

yeye aliyetekwa nyara,

la sivyo ghadhabu yangu italipuka

na kuwaka kama moto

kwa sababu ya uovu mlioufanya:

itawaka na hakuna wa kuizima.

13 Niko kinyume nawe, ee Yerusalemu,

wewe uishiye juu ya bonde hili

kwenye uwanda wa juu wa miamba,

asemaBwana,

wewe usemaye, “Ni nani awezaye kuja kinyume chetu?

Nani ataingia mahali pa kimbilio letu?”

14 Nitawaadhibu kama istahilivyo matendo yenu,

asemaBwana.

Nitawasha moto katika misitu yenu

ambao utateketeza kila kitu kinachowazunguka.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/21-98eb96f08aac4f2dc1e604a1079c9c98.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 22

Hukumu Dhidi Ya Wafalme Waovu

1 Hili ndilo asemaloBwana: “Shuka kwenye jumba la kifalme la mfalme wa Yuda, utangaze ujumbe huu huko:

2 ‘Sikia neno laBwana, ee mfalme wa Yuda, wewe uketiye kwenye kiti cha enzi cha Daudi: wewe, maafisa wako na watu wako mnaopitia malango haya.

3 Hili ndiloBwanaasemalo: Tenda haki na adili. Mwokoe mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane, wala usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa.

4 Kwa kuwa ukiwa mwangalifu kushika maagizo haya, ndipo wafalme watakaokalia kiti cha enzi cha Daudi watakapoingia kupitia malango ya jumba hili la kifalme, wakiwa wamepanda magari na farasi, huku wakifuatana na maafisa wao na watu wao.

5 Lakini kama hutayatii maagizo haya, asemaBwana, ninaapa kwa nafsi yangu kwamba jumba hili litakuwa gofu.’ ”

6 Kwa kuwa hili ndiloBwanaasemalo kuhusu jumba la kifalme la mfalme wa Yuda:

“Ingawa uko kama Gileadi kwangu,

kama kilele cha Lebanoni,

hakika nitakufanya uwe kama jangwa,

kama miji ambayo haijakaliwa na watu.

7 Nitawatuma waharabu dhidi yako,

kila mtu akiwa na silaha zake,

nao watazikata boriti zako nzuri za mierezi

na kuzitupa motoni.

8 “Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa niniBwanaamefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’

9 Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha agano laBwana, Mungu wao, na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ”

10 Usimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee;

badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu

yule aliyepelekwa uhamishoni,

kwa sababu kamwe hatairudia

wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa.

11 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwanakuhusu Shalumumwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “Yeye kamwe hatarudi tena.

12 Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.”

13 “Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa njia ya dhuluma,

vyumba vyake vya juu kwa udhalimu,

akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo,

bila kuwalipa kwa utumishi wao.

14 Asema, ‘Nitajijengea jumba kuu la kifalme,

na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’

Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa,

huweka kuta za mbao za mierezi,

na kuipamba kwa rangi nyekundu.

15 “Je, inakufanya kuwa mfalme

huko kuongeza idadi ya mierezi?

Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji?

Alifanya yaliyo sawa na haki,

hivyo yeye akafanikiwa katika yote.

16 Aliwatetea maskini na wahitaji,

hivyo yeye akafanikiwa katika yote.

Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?”

asemaBwana.

17 “Lakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tu

katika mapato ya udhalimu,

kwa kumwaga damu isiyo na hatia,

kwa uonevu na ukatili.”

18 Kwa hiyo hili ndilo asemaloBwanakuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:

“Hawatamwombolezea wakisema:

‘Ole, ndugu yangu! Ole, umbu langu!’

Hawatamwombolezea wakisema:

‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’

19 Atazikwa maziko ya punda:

ataburutwa na kutupwa

nje ya malango ya Yerusalemu.”

20 “Panda Lebanoni ukapige kelele,

sauti yako na isikike huko Bashani,

piga kelele toka Abarimu,

kwa kuwa wote waliojiunga nawe wameangamizwa.

21 Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama,

lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’

Hii imekuwa kawaida yako tangu ujana wako;

hujanitii mimi.

22 Upepo utawaondoa wachungaji wako wote,

na wale ulioungana nao wataenda uhamishoni.

Kisha utaaibika na kufedheheka

kwa sababu ya uovu wako wote.

23 Wewe uishiye Lebanoni,

wewe uliyetulia kwenye majengo ya mierezi,

tazama jinsi utakavyoomboleza

maumivu makali yatakapokupata,

maumivu kama yale ya mwanamke

mwenye utungu wa kuzaa!

24 “Hakika kama niishivyo,” asemaBwana, “hata kama wewe, Yekoniamwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekungʼoa hapo.

25 Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo.

26 Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko.

27 Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.”

28 Je, huyu mtu Yekonia ni chungu kilichodharauliwa,

chungu kilichovunjika,

chombo kisichotakiwa na mtu yeyote?

Kwa nini yeye na watoto wake watupwe nje kwa nguvu,

na kutupwa kwenye nchi wasioijua?

29 Ee nchi, nchi, nchi,

sikia neno laBwana!

30 Hili ndiloBwanaasemalo:

“Mwandike huyu mtu kama asiye na mtoto,

mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote,

kwa maana hakuna mtoto wake atakayefanikiwa,

wala kukaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi

wala kuendelea kutawala katika Yuda.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/22-44564e86e85d800cc764660656ea5d8f.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 23

Tawi La Haki

1 “Ole wao wachungaji wanaoharibu na kutawanya kondoo wa malisho yangu!” asemaBwana.

2 Kwa hiyo hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli, analowaambia wachungaji wanaowachunga watu wangu: “Kwa sababu mmelitawanya kundi langu na kuwafukuzia mbali, wala hamkuwatunza, basi mimi nitawaadhibu kwa ajili ya uovu mliofanya,” asemaBwana.

3 “Mimi mwenyewe nitayakusanya mabaki ya kundi langu kutoka nchi zote ambazo nimewafukuzia, nami nitawarudisha katika malisho yao, mahali ambapo watazaa na kuongezeka idadi yao.

4 Nitaweka wachungaji juu yao ambao watawachunga, nao hawataogopa tena au kutishwa, wala hatapotea hata mmoja,” asemaBwana.

5 Bwanaasema, “Siku zinakuja,

nitakapomwinulia Daudi Tawi lenye haki,

Mfalme atakayetawala kwa hekima,

na kutenda lililo haki na sawa katika nchi.

6 Katika siku zake, Yuda ataokolewa

na Israeli ataishi salama.

Hili ndilo jina atakaloitwa:

BwanaHaki Yetu.

7 “Hivyo basi, siku zinakuja, wakati ambapo watu hawatasema tena, ‘Hakika kamaBwanaaishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’

8 bali watasema, ‘Hakika kamaBwanaaishivyo, aliyewatoa wazao wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia,’ asemaBwana. Ndipo wataishi katika nchi yao wenyewe.”

Manabii Wasemao Uongo

9 Kuhusu manabii:

Moyo wangu umevunjika ndani yangu;

mifupa yangu yote inatetemeka.

Nimekuwa kama mtu aliyelewa,

kama mtu aliyelemewa na divai,

kwa sababu yaBwana

na maneno yake matakatifu.

10 Nchi imejaa wazinzi;

kwa sababu ya laana, nchi imekauka

na malisho yaliyoko nyikani yamekauka.

Mwenendo wa manabii ni mbaya

na mamlaka yao si ya haki.

11 “Nabii na kuhani wote si wacha Mungu;

hata hekaluni mwangu ninaona uovu wao,”

asemaBwana.

12 “Kwa hiyo mapito yao yatakuwa utelezi,

watafukuziwa mbali gizani

na huko wataanguka.

Nitaleta maafa juu yao

katika mwaka wa kuadhibiwa kwao,”

asemaBwana.

13 “Miongoni mwa manabii wa Samaria

nililiona jambo la kuchukiza:

Walitabiri kwa Baali

na kuwapotosha Israeli watu wangu.

14 Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemu

nimeona jambo baya sana:

Wanafanya uzinzi

na kuenenda katika uongo.

Wanatia nguvu mikono ya watenda mabaya,

kwa ajili hiyo hakuna yeyote

anayeachana na uovu wake.

Wote wako kama Sodoma kwangu;

watu na Yerusalemu wako kama Gomora.”

15 Kwa hiyo, hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo kuhusu manabii:

“Nitawafanya wale chakula kichungu

na kunywa maji yaliyotiwa sumu,

kwa sababu kutokana na manabii wa Yerusalemu

kutokumcha Mungu kumeenea katika nchi yote.”

16 Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo:

“Msisikilize wanachowatabiria manabii,

wanawajaza matumaini ya uongo.

Wanasema maono kutoka akili zao wenyewe,

hayatoki katika kinywa chaBwana.

17 Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi,

‘Bwanaasema: Mtakuwa na amani.’

Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao,

wao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’

18 Lakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama katika baraza laBwana

ili kuona au kusikia neno lake?

Ni nani aliyesikiliza

na kusikia neno lake?

19 Tazama, dhoruba yaBwana

itapasuka kwa ghadhabu,

kisulisuli kitazunguka na kuanguka

vichwani vya waovu.

20 Hasira yaBwanahaitageuka mpaka amelitimiza kusudi la moyo wake.

Siku zijazo mtalifahamu kwa wazi.

21 Mimi sikuwatuma manabii hawa,

lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao.

Mimi sikusema nao,

lakini wametabiri.

22 Lakini kama wangesimama barazani mwangu,

wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu,

nao wangewageuza kutoka njia zao mbaya

na kutoka matendo yao maovu.”

23 “Je, mimi ni Mungu aliyeko hapa karibu tu,”

Bwanaasema,

“wala si Mungu aliyeko pia mbali?

24 Je, mtu yeyote aweza kujificha

mahali pa siri ili nisiweze kumwona?”

Bwanaasema.

“Je, mimi sikuijaza mbingu na nchi?”

Bwanaasema.

25 “Nimesikia wanayoyasema manabii, hao wanaotabiri uongo kwa jina langu. Wanasema, ‘Nimeota ndoto! Nimeota ndoto!’

26 Mambo haya yataendelea mpaka lini ndani ya mioyo ya hawa manabii wa uongo, ambao hutabiri maono ya uongo ya akili zao wenyewe?

27 Wanadhani ndoto wanazoambiana wao kwa wao zitawafanya watu wangu walisahau jina langu, kama baba zao walivyolisahau jina langu kwa kumwabudu Baali.

28 Mwache nabii aliye na ndoto aseme ndoto yake, lakini yule aliye na neno langu na aliseme kwa uaminifu. Kwa maana jani kavu lina uhusiano gani na ngano?” asemaBwana.

29 “Je, neno langu si kama moto,” asemaBwana, “na kama nyundo ivunjayo mwamba vipande vipande?

30 “Kwa hiyo, niko kinyume na manabii wanaoibiana maneno kana kwamba ni yangu,” asemaBwana.

31 “Naam, mimi niko kinyume na manabii wanaotikisa ndimi zao wenyewe na kusema, ‘Bwanaasema.’

32 Kweli, niko kinyume na hao wanaotabiri ndoto za uongo,” asemaBwana. “Wanazisimulia na kuwapotosha watu wangu kwa uongo wao bila kujali, lakini sikuwatuma wala sikuwaamuru. Hawawafaidi watu hawa hata kidogo,” asemaBwana.

Maneno Ya Uongo Na Manabii Wa Uongo

33 “Wakati watu hawa, au nabii, au kuhani watakapokuuliza, ‘Mzigo waBwanani nini?’ wewe utawaambia, ‘Ninyi ndio mzigo. Nami nitawavua kama vazi, asemaBwana.’

34 Nabii, kuhani, au mtu yeyote akisema, ‘Huu ndio mzigo waBwana,’ nitamwadhibu huyo na nyumba yake.

35 Hivyo mnaambiana kila mmoja na mwenzake, au kwa mtu wa nyumba yao: ‘Bwanaamejibu nini?’ au ‘Bwanaamesema nini?’

36 Lakini kamwe msiseme tena, ‘Nina mzigo waBwana,’ kwa sababu kila neno la mtu binafsi linakuwa mzigo wake mwenyewe, na hivyo kupotosha maneno ya Mungu aliye hai,BwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wetu.

37 Hivi ndivyo utakavyoendelea kumuuliza nabii: ‘Bwanaamekujibu nini?’ au ‘Je,Bwanaamesema nini?’

38 Ingawa unadai, ‘Huu ndio mzigo waBwana,’ hili ndiloBwanaasemalo: Ulitumia maneno, ‘Huu ndio mzigo waBwana,’ hata ingawa nilikuambia kuwa kamwe usiseme, ‘Huu ni mzigo waBwana.’

39 Kwa hiyo, hakika nitakusahau na kukutupa mbali na uso wangu pamoja na mji niliowapa ninyi na baba zenu.

40 Nitaleta juu yako fedheha ya kudumu: yaani aibu ya kudumu ambayo haitasahaulika.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/23-7ce7ca3828ff1e73e6bddcedf17d0968.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 24

Vikapu Viwili Vya Tini

1 Baada ya Yekoniamwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na maafisa, mafundi stadi na wahunzi wa Yuda, kuchukuliwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli na Nebukadneza mfalme wa Babeli kwenda uhamishoni huko Babeli,Bwanaakanionyesha vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya Hekalu laBwana.

2 Kikapu kimoja kilikuwa na tini nzuri sana, kama zile za mavuno ya kwanza. Kikapu cha pili kilikuwa na tini dhaifu sana, mbovu mno zisizofaa kuliwa.

3 KishaBwanaakaniuliza, “Je, Yeremia, unaona nini?”

Nikamjibu, “Ninaona tini zile zilizo nzuri ni nzuri sana, lakini zilizo dhaifu ni mbovu mno zisizofaa kuliwa.”

4 Kisha neno laBwanalikanijia:

5 “Hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kama zilivyo hizi tini nzuri, ndivyo ninavyowaona kuwa bora watu wa uhamisho kutoka Yuda, niliowaondoa kutoka mahali hapa kwenda katika nchi ya Wakaldayo.

6 Macho yangu yatakuwa juu yao kwa ajili ya kuwapatia mema, nami nitawarudisha tena katika nchi hii. Nitawajenga wala sitawabomoa, nitawapanda wala sitawangʼoa,

7 nitawapa moyo wa kunifahamu mimi, kwamba mimi ndimiBwana. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote.

8 “ ‘Lakini kama zilivyo zile tini dhaifu, ambazo ni mbovu mno zisizofaa kuliwa,’ asemaBwana, ‘ndivyo nitakavyomtendea Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na mabaki wengine kutoka Yerusalemu, wawe wamebaki katika nchi hii, au wanaishi Misri.

9 Nitawafanya kuwa chukizo kabisa na kitu cha kulaumiwa katika mataifa yote ya dunia, watakuwa aibu na kitu cha kudharauliwa, chombo cha dhihaka na kulaaniwa, popote nitakapowafukuzia.

10 Nitautuma upanga, njaa na tauni dhidi yao hadi wawe wameangamia kutoka nchi niliyowapa wao na baba zao.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/24-470e55bc0d3f7a0e53c096330bff09fb.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 25

Miaka Sabini Ya Kuwa Mateka

1 Neno likamjia Yeremia kuhusu watu wote wa Yuda, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, ambao ulikuwa mwaka wa kwanza wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babeli.

2 Hivyo nabii Yeremia akawaambia watu wote wa Yuda na wale wote waishio Yerusalemu:

3 Kwa miaka ishirini na mitatu, kuanzia mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda, hadi siku hii ya leo, neno laBwanalimekuwa likinijia, nami nimesema nanyi mara kwa mara, lakini hamkusikiliza.

4 IngawaBwanaamewatuma watumishi wake wote hao manabii kwenu mara kwa mara, hamkusikiliza wala hamkujali.

5 Walisema, “Geukeni sasa, kila mmoja wenu kutoka njia yake mbaya na matendo yake maovu, ndipo mtaweza kukaa katika nchi ambayoBwanaaliwapa ninyi na baba zenu milele.

6 Msiifuate miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu. Msinikasirishe kwa vitu ambavyo mmevitengeneza kwa mikono yenu.”

7 “Lakini ninyi hamkunisikiliza mimi, tena mkanikasirisha kwa vitu mlivyovitengeneza kwa mikono yenu, nanyi mmejiletea madhara juu yenu wenyewe,” asemaBwana.

8 Kwa hiyoBwanaMwenye Nguvu Zote asema hivi: “Kwa sababu hamkuyasikiliza maneno yangu,

9 nitayaita mataifa yote ya kaskazini na mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli,” asemaBwana. “Nitawaleta waishambulie nchi hii na wakazi wake wote, na dhidi ya mataifa yote yanayowazunguka. Nitawaangamiza kabisa na kuwafanya kitu cha kuchukiwa na kudharauliwa, na kuwa magofu daima.

10 Nitawaondolea sauti ya shangwe na furaha, sauti ya bibi na bwana arusi, sauti ya mawe ya kusagia, na mwanga wa taa.

11 Nchi hii yote itakuwa ukiwa na isiyofaa kitu, nayo mataifa haya yatamtumikia mfalme wa Babeli kwa miaka sabini.”

12 “Lakini miaka sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na taifa lake na nchi ya Wakaldayo kwa ajili ya hatia yao,” asemaBwana. “Nitaifanya kuwa ukiwa milele.

13 Nitaleta juu ya nchi hiyo mambo yote niliyosema dhidi yake, yote yaliyoandikwa katika kitabu hiki, na kutolewa unabii na Yeremia dhidi ya mataifa yote.

14 Wao wenyewe watakuwa watumwa wa mataifa mengi na wafalme wakuu. Nitawalipizia sawasawa na matendo yao na kazi ya mikono yao.”

Kikombe Cha Ghadhabu Ya Mungu

15 Hili ndiloBwana, Mungu wa Israeli, aliloniambia: “Chukua kutoka mkononi mwangu kikombe hiki kilichojaa divai ya ghadhabu yangu, na kuyanywesha mataifa yote ambayo ninakutuma kwao.

16 Watakapoinywa, watapepesuka na kukasirika sana kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka katikati yao.”

17 Hivyo nikakichukua kikombe kutoka mkononi mwaBwana, na kuyafanya mataifa yote aliyonituma kwao kukinywa:

18 Yaani Yerusalemu na miji ya Yuda, wafalme wake na maafisa wake, kuwafanya magofu na kuwa kitu cha kuchukiza, cha dhihaka na laana, kama walivyo leo;

19 pia Farao mfalme wa Misri, watumishi wake, maafisa wake na watu wake wote,

20 pia wageni wote walioko huko; wafalme wote wa nchi ya Usi; wafalme wote wa Wafilisti (wale wa Ashkeloni, Gaza, Ekroni na watu walioachwa huko Ashdodi);

21 Edomu, Moabu na Amoni;

22 wafalme wote wa Tiro na Sidoni; wafalme wa nchi za pwani ngʼambo ya bahari;

23 Dedani, Tema, Buzi na wote walio maeneo ya mbali;

24 wafalme wote wa Arabuni na wafalme wote wa watu wageni wanaoishi katika jangwa;

25 wafalme wote wa Zimri, Elamu na Umedi;

26 na wafalme wote wa pande za kaskazini, wa karibu na wa mbali, mmoja baada ya mwingine; yaani falme zote juu ya uso wa dunia. Baada ya hao wote, mfalme wa Sheshakiatakunywa pia.

27 “Kisha uwaambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Kunyweni, mlewe na mtapike; angukeni, wala msiinuke tena kwa sababu ya upanga nitakaotuma miongoni mwenu.’

28 Lakini kama wakikataa kupokea kikombe kutoka mikononi mwako na kunywa, waambie, ‘Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: Ni lazima mnywe!

29 Tazama, nimeanza kuleta maafa juu ya mji ulio na Jina langu, na je, kweli ninyi mtaepuka kuadhibiwa? Hamwezi kuepuka kuadhibiwa, kwa maana nitaleta vita juu ya wote waishio duniani, asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.’

30 “Basi sasa toa unabii kwa maneno haya yote dhidi yao, uwaambie:

“ ‘Bwanaatanguruma kutoka juu;

atatoa sauti ya ngurumo

kutoka makao yake matakatifu

na kunguruma kwa nguvu sana

dhidi ya nchi yake.

Atapiga kelele kama wao wakanyagao zabibu,

atapiga kelele dhidi ya wote waishio duniani.

31 Ghasia zitasikika hadi miisho ya dunia,

kwa maanaBwanaataleta mashtaka dhidi ya mataifa;

ataleta hukumu juu ya wanadamu wote

na kuwaua waovu wote,’ ”

asemaBwana.

32 Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote asemalo:

“Tazama! Maafa yanaenea

kutoka taifa moja hadi jingine;

tufani kubwa inainuka

kutoka miisho ya dunia.”

33 Wakati huo, hao waliouawa naBwanawatatapakaa kila mahali, kuanzia mwisho mmoja wa dunia hadi mwisho mwingine. Hawataombolezewa wala kukusanywa au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyoenea juu ya ardhi.

34 Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji,

mgaagae mavumbini,

ninyi viongozi wa kundi.

Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia;

mtaanguka na kuvunjavunjwa

kama vyombo vizuri vya udongo.

35 Wachungaji hawatakuwa na mahali pa kukimbilia,

viongozi wa kundi hawatapata mahali pa kutorokea.

36 Sikia kilio cha wachungaji, maombolezo ya viongozi wa kundi,

kwa maanaBwanaanayaharibu malisho yao.

37 Makao yao ya amani yataharibiwa

kwa sababu ya hasira kali yaBwana.

38 Kama simba ataacha pango lake,

nchi yao itakuwa ukiwa

kwa sababu ya upanga wa mdhalimu,

na kwa sababu ya hasira kali yaBwanaMungu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/25-5c30d2d0c9b69be6b39f63c913312dd4.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 26

Yeremia Atishiwa Kuuawa

1 Mwanzoni mwa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilikuja kutoka kwaBwana:

2 “Hili ndiloBwanaasemalo: Simama katika ua wa nyumba yaBwanana useme na watu wote wa miji ya Yuda wanaokuja kuabudu katika nyumba yaBwana. Waambie kila kitu nitakachokuamuru, usipunguze neno.

3 Huenda watasikiliza, na kila mmoja akageuka kutoka njia yake mbaya. Kisha nitawahurumia na kuacha kuwaletea maafa niliyokuwa ninapanga kwa sababu ya maovu waliyofanya.

4 Waambie, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Ikiwa hamtanisikiliza na kuifuata sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu,

5 nanyi ikiwa hamtayasikiliza maneno ya watumishi wangu manabii, ambao nimewatuma kwenu tena na tena (ijapokuwa hamkuwasikiliza),

6 ndipo nitaifanya nyumba hii kama Shilo na mji huu kuwa kitu cha kulaaniwa na mataifa yote ya dunia.’ ”

7 Makuhani, manabii na watu wote wakamsikia Yeremia akiyasema maneno haya ndani ya nyumba yaBwana.

8 Lakini mara tu Yeremia alipomaliza kuwaambia watu kila kituBwanaalichomwamuru kukisema, basi makuhani, manabii na watu wote walimkamata wakisema, “Ni lazima ufe!

9 Kwa nini unatoa unabii katika jina laBwanakwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa na kuachwa tupu?” Nao watu wote wakamkusanyikia na kumzunguka Yeremia ndani ya nyumba yaBwana.

10 Maafisa wa Yuda waliposikia kuhusu mambo haya, wakapanda kutoka jumba la kifalme, wakaenda katika nyumba yaBwanana kushika nafasi zao kwenye ingilio la Lango Jipya la nyumba yaBwana.

11 Kisha makuhani na manabii wakawaambia maafisa pamoja na watu wote, “Mtu huyu anastahili ahukumiwe kifo kwa sababu ametoa unabii mbaya dhidi ya mji huu. Mmesikia kwa masikio yenu wenyewe!”

12 Kisha Yeremia akawaambia maafisa wote na watu wote: “Bwanaamenituma kutoa unabii dhidi ya nyumba hii na mji huu mambo yote mliyoyasikia.

13 Sasa tengenezeni njia zenu na matendo yenu, na kumtiiBwanaMungu wenu. NdipoBwanaatawahurumia na kuacha kuleta maafa aliyokuwa ameyatamka dhidi yenu.

14 Lakini kwa habari yangu mimi, niko mikononi mwenu, nifanyieni lolote mnaloona kuwa ni jema na la haki.

15 Hata hivyo, jueni kwa hakika, ikiwa mtaniua, mtakuwa mmejipatia dhambi kwa damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe, na juu ya mji huu na wote wanaoishi ndani yake, kwa maana ni kweliBwanaamenituma kwenu ili niseme maneno haya yote masikioni mwenu.”

16 Kisha maafisa na watu wote wakawaambia makuhani na manabii, “Mtu huyu asihukumiwe kifo! Amesema nasi katika jina laBwana, Mungu wetu.”

17 Baadhi ya wazee wa nchi wakasogea mbele, wakaliambia kusanyiko lote la watu,

18 “Mika Mmoreshethi alitoa unabii katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Akawaambia watu wote wa Yuda, ‘Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote:

“ ‘Sayuni italimwa kama shamba,

Yerusalemu itakuwa lundo la kokoto,

na kilima cha Hekalu kitakuwa kichuguu

kilichofunikwa na vichaka.’

19 Je, Hezekia mfalme wa Yuda au mtu mwingine yeyote katika Yuda alimhukumu Mika kufa? Je, Hezekia hakumchaBwanana kuhitaji msaada wake? Je,Bwanahakuwahurumia na akaacha kuleta maafa aliyokuwa ametamka dhidi yao? Tunakaribia sana kujiletea maangamizo ya kutisha sisi wenyewe!”

20 (Wakati huu, Uria mwana wa Shemaya kutoka mji wa Kiriath-Yearimu alikuwa mtu mwingine aliyetoa unabii kwa jina laBwana. Alitoa unabii juu ya mambo yaliyofanana na haya dhidi ya mji huu na nchi hii kama alivyofanya Yeremia.

21 Mfalme Yehoyakimu na wakuu wake wote na maafisa waliposikia maneno yake, mfalme alitafuta kumuua. Lakini Uria alipata habari, na kwa kuogopa akakimbilia Misri.

22 Hata hivyo, Mfalme Yehoyakimu alimtuma Elnathani mwana wa Akbori huko Misri, pamoja na watu wengine ili kwenda kumkamata Uria.

23 Wakamrudisha Uria kutoka Misri na kumpeleka kwa Mfalme Yehoyakimu, ambaye alimuua kwa upanga, na mwili wake kutupwa kwenye eneo la makaburi ya watu wasio na cheo.)

24 Zaidi ya hayo, Ahikamu mwana wa Shafani akamuunga mkono Yeremia, kwa hiyo hakutiwa tena mikononi mwa watu ili auawe.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/26-460b47dc5c6b23ac701f6aafbae52496.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 27

Yuda Kumtumikia Nebukadneza

1 Mwanzoni mwa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwaBwana:

2 Hili ndiloBwanaaliloniambia: “Tengeneza nira, ujivike shingoni mwako, uifunge kwa kamba za ngozi.

3 Kisha utume ujumbe kwa wafalme wa Edomu, Moabu, Amoni, Tiro na Sidoni kupitia wajumbe ambao wamekuja Yerusalemu kwa Sedekia mfalme wa Yuda.

4 Wape ujumbe kwa ajili ya mabwana zao na uwaambie: Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: ‘Waambieni hivi mabwana zenu:

5 Kwa uwezo wangu mkuu na kwa mkono wangu ulionyooshwa nimeumba dunia na watu wake na wanyama walioko ndani yake, nami humpa yeyote inipendezavyo.

6 Sasa nitazitia nchi zenu zote mkononi mwa mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli, na nitawafanya hata wanyama wa mwituni wamtumikie.

7 Mataifa yote yatamtumikia yeye, pamoja na mwanawe na mwana wa mwanawe, hadi wakati wa nchi yake utakapowadia, kisha mataifa mengi na wafalme wenye nguvu nyingi watamshinda.

8 “ ‘ “Lakini kama kukiwa na taifa lolote au ufalme ambao hautamtumikia Nebukadneza mfalme wa Babeli, ama kuinamisha shingo yake chini ya nira yake, nitaliadhibu taifa hilo kwa upanga, njaa na tauni, asemaBwana, mpaka nitakapoliangamiza taifa hilo kwa mkono wake.

9 Kwa hiyo msiwasikilize manabii wenu, waaguzi wenu, waota ndoto wenu, watabiri na wachawi wanaowaambia ninyi: Hamtamtumikia mfalme wa Babeli.

10 Wanawatabiria uongo ambao utawafanya ninyi mhamishwe mbali kutoka nchi yenu. Nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia.

11 Lakini ikiwa taifa lolote litainama na kuweka shingo lake katika nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitaliacha taifa hilo katika nchi yake yenyewe ili wailime na kuishi humo, asemaBwana.” ’ ”

12 Nilitoa ujumbe huo huo kwa Sedekia mfalme wa Yuda. Nilisema, “Ingiza shingo yako katika nira ya mfalme wa Babeli, umtumikie yeye na watu wake, nawe utaishi.

13 Kwa nini wewe na watu wako mfe kwa upanga, njaa na tauni, ambazoBwanaameonya juu ya taifa lolote ambalo halitamtumikia mfalme wa Babeli?

14 Msiyasikilize maneno ya manabii wanaowaambia kwamba, ‘Hamtamtumikia mfalme wa Babeli,’ kwa sababu wanawatabiria uongo.

15 ‘Sikuwatuma hao,’ asemaBwana. ‘Wanatabiri uongo kwa jina langu. Kwa hiyo, nitawafukuzia mbali, nanyi mtaangamia, ninyi pamoja na manabii wanaowatabiria.’ ”

16 Kisha nikawaambia makuhani na watu hawa wote, “Hili ndilo asemaloBwana: Msiwasikilize manabii wanaosema, ‘Hivi karibuni sana vyombo vya nyumba yaBwanavitarudishwa kutoka Babeli.’ Wanawatabiria ninyi uongo.

17 Msiwasikilize. Mtumikieni mfalme wa Babeli, nanyi mtaishi. Kwa nini mji huu uwe magofu?

18 Kama wao ni manabii na wanalo neno laBwana, basi na wamsihiBwanaMwenye Nguvu Zote ili vyombo vilivyobaki katika nyumba yaBwanana katika jumba la kifalme la mfalme wa Yuda na katika Yerusalemu visipelekwe Babeli.

19 Kwa maana hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote kuhusu zile nguzo, ile Bahari, vile vishikizo viwezavyo kuhamishika, vinara na vyombo vingine vilivyoachwa katika mji huu,

20 ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli hakuvichukua wakati alipomchukua Yekoniamwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda kwenda uhamishoni huko Babeli kutoka Yerusalemu, pamoja na wakuu wote wa Yuda na Yerusalemu.

21 Naam, hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu vitu ambavyo vimebaki ndani ya nyumba yaBwana, na ndani ya jumba la kifalme la mfalme wa Yuda, na katika Yerusalemu:

22 ‘Vitachukuliwa kupelekwa Babeli, nako huko vitabaki mpaka siku nitakayovijilia,’ asemaBwana. ‘Kisha nitavirudisha na kuvirejesha mahali hapa.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/27-22fef31aa57262e873068fe74e6163b2.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 28

Hanania Nabii Wa Uongo

1 Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba yaBwanambele ya makuhani na watu wote:

2 “Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.

3 Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba yaBwanaambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli.

4 Pia nitamrudisha mahali hapa Yekoniamwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na wote waliohamishwa kutoka Yuda ambao walikwenda Babeli,’ asemaBwana, ‘kwa kuwa nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.’ ”

5 Ndipo nabii Yeremia akamjibu nabii Hanania mbele ya makuhani na watu wote waliokuwa wamesimama ndani ya nyumba yaBwana.

6 Akasema, “Amen!Bwanana afanye hivyo!Bwanana ayatimize maneno uliyotoa unabii kwa kuvirudisha mahali hapa kutoka Babeli vyombo vya nyumba yaBwanapamoja na wote waliohamishwa.

7 Hata hivyo, nisikilize nikuambie yale nitakayoyasema masikioni mwako na masikioni mwa watu hawa wote:

8 Tangu mwanzo, manabii waliokutangulia wewe na mimi walitabiri vita, maafa na tauni dhidi ya nchi nyingi na falme kubwa.

9 Lakini nabii atakayetabiri amani atatambuliwa kuwa kweli ametumwa naBwanaikiwa unabii wake utatimia.”

10 Kisha nabii Hanania akaiondoa nira iliyokuwa shingoni mwa Yeremia na kuivunja,

11 naye akasema mbele ya watu wote, “Hili ndilo asemaloBwana: ‘Vivi hivi ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadneza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo za mataifa katika muda huu wa miaka miwili.’ ” Alipofanya hivi, nabii Yeremia akaondoka zake.

12 Kitambo kidogo baada ya nabii Hanania kuivunja nira kutoka shingo ya nabii Yeremia, neno laBwanalikamjia Yeremia:

13 “Nenda ukamwambie Hanania, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Umevunja nira ya mti, lakini badala yake utapata nira ya chuma.

14 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Nitaweka nira ya chuma kwenye shingo za mataifa haya yote ili kufanya yamtumikie Nebukadneza mfalme wa Babeli, nao watamtumikia. Nitampa kutawala hata wanyama wa mwituni.’ ”

15 Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, “Sikiliza Hanania!Bwanahajakutuma, lakini wewe umelishawishi taifa hili kuamini uongo.

16 Kwa hiyo, hili ndilo asemaloBwana: ‘Hivi karibuni nitakuondoa kutoka juu ya uso wa dunia. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi yaBwana.’ ”

17 Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/28-3413058eee3e7851ec5f1108be449b17.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 29

Barua Kwa Watu Wa Uhamisho

1 Haya ndiyo maneno ya ile barua ambayo nabii Yeremia aliituma kutoka Yerusalemu kwenda kwa wazee waliobaki miongoni mwa wale waliohamishwa, na kwa makuhani, manabii na watu wengine wote ambao Nebukadneza alikuwa amewachukua kwenda uhamishoni Babeli kutoka Yerusalemu.

2 (Hii ilikuwa ni baada ya Mfalme Yekoniana malkia mamaye, maafisa wa mahakama, viongozi wa Yuda na wa Yerusalemu, mafundi na wahunzi kwenda uhamishoni kutoka Yerusalemu.)

3 Barua ilikabidhiwa kwa Elasa mwana wa Shafani, na kwa Gemaria mwana wa Hilkia, ambao Sedekia mfalme wa Yuda aliwatuma kwa Mfalme Nebukadneza huko Babeli. Barua yenyewe ilisema:

4 Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, awaambialo wale wote niliowapeleka kutoka Yerusalemu kwenda uhamishoni Babeli:

5 “Jengeni nyumba na mstarehe, pandeni bustani na mle mazao yake.

6 Oeni wake na mzae wana na binti, waozeni wana wenu wake, nanyi watoeni binti zenu waolewe, ili nao pia wazae wana na binti. Ongezekeni idadi yenu huko, wala msipungue.

7 Pia tafuteni amani na mafanikio ya mji ambamo nimewapeleka uhamishoni. MwombeniBwanakwa ajili ya mji huo, kwa sababu ukistawi, ninyi pia mtastawi.”

8 Naam, hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Msikubali manabii na wabashiri walioko miongoni mwenu wawadanganye. Msisikilize ndoto ambazo mmewatia moyo kuota.

9 Wanawatabiria ninyi uongo kwa jina langu. Sikuwatuma,” asemaBwana.

10 Hili ndilo asemaloBwana: “Miaka sabini itakapotimia kwa ajili ya Babeli, nitakuja kwenu na kutimiza ahadi yangu ya rehema ya kuwarudisha mahali hapa.

11 Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu,” asemaBwana, “ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.

12 Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza.

13 Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

14 Nitaonekana kwenu,” asemaBwana, “nami nitawarudisha watu wenu waliotekwa. Nitawakusanya kutoka mataifa yote na mahali pote nilipokuwa nimewafukuzia, nami nitawarudisha mahali ambapo nilikuwa nimewatoa walipochukuliwa uhamishoni,” asemaBwana.

15 Mnaweza mkasema, “Bwanaameinua manabii kwa ajili yetu huku Babeli,”

16 lakini hili ndilo asemaloBwanakuhusu mfalme aketiaye kiti cha enzi cha Daudi, na watu wa kwenu wote wanaobaki katika mji huu, ndugu zenu ambao hawakwenda pamoja nanyi uhamishoni.

17 Naam, hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: “Nitatuma upanga, njaa na tauni dhidi yao, nami nitawafanya kuwa kama tini dhaifu zile ambazo ni mbovu sana zisizofaa kuliwa.

18 Nitawafukuza kwa upanga, kwa njaa na kwa tauni, nami nitawafanya kitu cha kuchukiza sana kwa falme zote za dunia, na kuwa kitu cha laana na cha kuogofya, cha dharau na kukemewa, miongoni mwa mataifa yote nitakakowafukuzia.

19 Kwa kuwa hawakuyasikiliza maneno yangu,” asemaBwana, “maneno ambayo niliwatumia tena na tena kupitia watumishi wangu manabii. Wala ninyi watu wa uhamisho hamkusikiliza pia,” asemaBwana.

20 Kwa hiyo, sikieni neno laBwana, enyi nyote mlio uhamishoni, niliowapeleka Babeli kutoka Yerusalemu.

21 Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo kuhusu Ahabu mwana wa Kolaya, na Sedekia mwana wa Maaseya, wanaowatabiria uongo kwa jina langu: “Nitawatia mikononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, naye atawaua mbele ya macho yenu hasa.

22 Kwa ajili yao, watu wote wa uhamisho kutoka Yuda walioko Babeli watatumia laana hii: ‘Bwanana akutendee kama Sedekia na Ahabu, ambao mfalme wa Babeli aliwachoma kwa moto.’

23 Kwa kuwa wamefanya mambo maovu kabisa katika Israeli, wamezini na wake za majirani zao, tena kwa Jina langu wamesema uongo, mambo ambayo sikuwaambia kuyafanya. Nami nayajua haya, na ni shahidi wa jambo hilo,” asemaBwana.

Ujumbe Kwa Shemaya

24 Mwambie Shemaya Mnehelami,

25 “Hili ndiloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: Ulituma barua kwa jina lako mwenyewe kwa watu wote wa Yerusalemu, kwa Sefania mwana wa kuhani Maaseya na kwa makuhani wengine wote. Ulimwambia Sefania,

26 ‘Bwanaamekuweka wewe uwe kuhani badala ya Yehoyada ili uwe msimamizi wa nyumba yaBwana. Unapaswa kufunga kwa mikatale na mnyororo wa shingoni mwendawazimu yeyote anayejifanya nabii.

27 Kwa nini basi hukumkemea Yeremia Mwanathothi, aliyejifanya kama nabii miongoni mwenu?

28 Ametutumia ujumbe huu huku Babeli: Mtakuwako huko muda mrefu. Kwa hiyo jengeni nyumba mkakae; pandeni mashamba na mle mazao yake.’ ”

29 Kuhani Sefania, hata hivyo, akamsomea nabii Yeremia ile barua.

30 Ndipo neno laBwanalikamjia Yeremia kusema:

31 “Tuma ujumbe huu kwa watu wote walio uhamishoni: ‘Hili ndiloBwanaasemalo kuhusu Shemaya Mnehelami: Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi, hata ingawa sikumtuma, naye amewafanya kuamini uongo,

32 hili ndiloBwanaasemalo: Hakika nitamwadhibu Shemaya Mnehelami pamoja na uzao wake. Hapatakuwa na yeyote atakayebaki miongoni mwa watu hawa, wala hataona mema nitakayowatendea watu wangu, asemaBwana, kwa sababu ametangaza uasi dhidi yangu.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/29-4dcac70fef39acfd1a41fa1b2354abbd.mp3?version_id=1627—