Categories
Yeremia

Yeremia Utangulizi

Utangulizi

Kitabu hiki kimepewa jina la Yeremia, mwana wa kuhani, aliyezaliwa katika kijiji cha Anathothi. Kitabu hiki kinatoa taarifa kwa kina na mtazamo wa kidini, na hali ya kisiasa katika Yuda kwenye kipindi cha miaka arobaini kabla ya kuharibiwa kwa Yerusalemu. Mengi yanajulikana kuhusu historia binafsi ya Yeremia kuliko nabii mwingine yeyote katika Agano la Kale. Yeremia, kama Isaya, alikuwa kijana ambaye aliitwa na Mungu kuionya Yuda juu ya uovu wake.

Kwa miaka 21 ya mwanzo ya huduma ya Yeremia, Yuda, chini ya utawala wa Yosia, walipata mwamko wa kisiasa na uamsho wa kiroho; wakati huo dola ya Waashuru ilikuwa inadidimia. Yeremia alipoanza huduma yake ya unabii 627 K.K., alipata miaka mizuri ya huduma yake hadi Yosia alipouawa mnamo 609 K.K.

Baada ya Yosia kufa, Yeremia alikuwa katika hatari kubwa kutoka kwa viongozi wa dini na wa kisiasa ambao walikasirishwa na ujumbe wake. Ingawa Yeremia alishauri Wayahudi wajitolee kwa Wababeli, wao waliasi. Hivyo mnamo mwaka wa 586 K.K., mji wa Yerusalemu pamoja na Hekalu lake vikaharibiwa, naye Yeremia akachukuliwa kwa nguvu na watu wa Yuda, wakaenda naye Misri.

Mwandishi

Nabii Yeremia.

Kusudi

Yeremia anawaita watu wa Mungu kugeuka kutoka dhambi zao na kumrudia Mungu.

Mahali

Yerusalemu.

Tarehe

627–586 K.K.

Wahusika Wakuu

Wafalme wa Yuda: Yosia, Yehoahazi, Yehoyakimu, Yehoyakini na Sedekia; Yeremia, Baruku, Ebed-Meleki, Mfalme Nebukadneza, Warekabi.

Wazo Kuu

Uovu usipotubiwa husababisha taifa, jamii, au mtu binafsi kuangamia.

Mambo Muhimu

Yeremia aliorodhesha dhambi za Yuda zote na kutoa unabii wa hukumu ya Mungu, na pia kuwaita watu watubu. Lakini watu waliendelea na maisha yao ya ubinafsi na kuabudu sanamu. Pia viongozi wote walikataa sheria ya Mungu, wakakubaliana na manabii wa uongo. Yerusalemu iliharibiwa, Hekalu likaachwa likiwa magofu, nao watu wakatekwa na kupelekwa uhamishoni Babeli. Ilipasa watu waajibike kwa ajili ya uharibifu na utekwaji huu uliosababishwa na wao kutosikia na kutotii ujumbe wa Mungu.

Mgawanyo

Wito wa Yeremia (

1:1-9

)

Hali ya dhambi ya Yuda (

2:1–6:30

)

Hekalu, sheria na agano (

7:1–12:17

)

Uhakika wa kutekwa (

13:1–18:23

)

Yeremia anakumbana na viongozi (

19:1–29:32

)

Ahadi ya kufanywa upya (

30:1–33:26

)

Ufalme unasambaratika (

34:1–39:18

)

Safari ya kwenda Misri (

40:1–45:5

)

Jumbe kuhusu mataifa ya kigeni (

46:1–51:64

)

Kuanguka kwa Yerusalemu (

52:1-34

).

Categories
Yeremia

Yeremia 1

1 Maneno ya Yeremia mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani katika mji wa Anathothi, katika nchi ya Benyamini.

2 Neno laBwanalilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda,

3 na pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa uhamishoni.

Wito Wa Yeremia

4 Neno laBwanalilinijia, kusema,

5 “Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua;

kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum;

nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.”

6 Nami nikasema, “Aa,BwanaMwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.”

7 LakiniBwanaakaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza.

8 Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asemaBwana.

9 KishaBwanaakaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako.

10 Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.”

11 Neno laBwanalikanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?”

Nami nikajibu, “Naona tawi la mti wa mlozi.”

12 Bwanaakaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba limetimizwa.”

13 Neno laBwanalikanijia tena, “Unaona nini?”

Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.”

14 Bwanaakaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote waishio katika nchi.

15 Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asemaBwana.

“Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya enzi

katika maingilio ya malango ya Yerusalemu,

watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka,

na dhidi ya miji yote ya Yuda.

16 Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu

kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi,

kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine

na kuabudu kile ambacho mikono yao imekitengeneza.

17 “Jiandae! Simama useme chochote nitakachokuamuru. Usiwaogope, la sivyo nitakufanya uwaogope wao.

18 Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma, na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo.

19 Watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa kuwa niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,” asemaBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/1-95955986344391729205a4da72b0ed63.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 2

Israeli Amwacha Mungu

1 Neno laBwanalilinijia kusema,

2 “Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu:

“ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako,

jinsi ulivyonipenda kama bibi arusi

na kunifuata katika jangwa lile lote,

katika nchi isiyopandwa mbegu.

3 Israeli alikuwa mtakatifu kwaBwana,

kama malimbuko ya kwanza ya mavuno yake;

wote waliowaangamiza walihesabiwa kuwa na hatia,

nayo maafa yaliwakumba,’ ”

asemaBwana.

4 Sikia neno laBwana, ee nyumba ya Yakobo,

nanyi nyote jamaa za nyumba ya Israeli.

5 Hivi ndivyo asemavyoBwana:

“Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu,

hata wakatangatanga mbali nami hivyo?

Walifuata sanamu zisizofaa,

nao wenyewe wakawa hawafai.

6 Hawakuuliza, ‘Yuko wapiBwana,

aliyetupandisha kutoka Misri

na kutuongoza kupitia nyika kame,

kupitia nchi ya majangwa na mabonde,

nchi ya ukame na giza,

nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake

wala hakuna mtu aishiye humo?’

7 Niliwaleta katika nchi yenye wingi wa vitu

ili mpate kula matunda yake

na utajiri wa mazao yake.

Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu,

na kuufanya urithi wangu chukizo.

8 Makuhani hawakuuliza,

‘Yuko wapiBwana?’

Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi;

viongozi waliasi dhidi yangu.

Manabii walitabiri kwa jina la Baali,

wakifuata sanamu zisizofaa.

9 “Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,”

asemaBwana.

“Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako.

10 Vuka, nenda ngʼambo mpaka pwani ya Kitimunawe uangalie,

tuma watu waende Kedari, wachunguze kwa makini,

uone kama kumekuwepo kitu kama hiki.

11 Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote?

(Hata ingawa hao si miungu kamwe.)

Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao

kwa sanamu zisizofaa kitu.

12 Shangaeni katika hili, ee mbingu,

nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,”

asemaBwana.

13 “Watu wangu wametenda dhambi mbili:

Wameniacha mimi,

niliye chemchemi ya maji yaliyo hai,

nao wamejichimbia visima vyao wenyewe,

visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji.

14 Je, Israeli ni mtumishi, yaani mtumwa kwa kuzaliwa?

Kwa nini basi amekuwa mateka?

15 Simba wamenguruma;

wamemngurumia.

Wameifanya nchi yake kuwa ukiwa;

miji yake imeteketezwa, nayo imeachwa haina watu.

16 Pia watu wa Memfisina Tahpanhesi

wamevunja taji ya kichwa chako.

17 Je, hukujiletea hili wewe mwenyewe

kwa kumwachaBwana, Mungu wako

alipowaongoza njiani?

18 Sasa kwa nini uende Misri

kunywa maji ya Shihori?

Nawe kwa nini kwenda Ashuru

kunywa maji ya Mto Frati?

19 Uovu wako utakuadhibu;

kurudi nyuma kwako kutakukemea.

Basi kumbuka, utambue

jinsi lilivyo ovu na chungu kwako

unapomwachaBwanaMungu wako

na kutokuwa na hofu yangu,”

asema Bwana,BwanaMwenye Nguvu Zote.

20 “Zamani nilivunja nira yako

na kukatilia mbali vifungo vyako;

ukasema, ‘Sitakutumikia!’

Naam kweli, kwenye kila kilima kirefu

na chini ya kila mti uliotanda matawi yake

ulijilaza kama kahaba.

21 Nilikupanda ukiwa mzabibu ulio bora sana,

mkamilifu na wa mbegu nzuri.

Ilikuwaje basi ukawa kinyume nami,

ukaharibika na kuwa mzabibu mwitu?

22 Hata ujisafishe kwa magadi

na kutumia sabuni nyingi,

bado doa la hatia yako liko mbele zangu,”

asemaBwanaMwenyezi.

23 “Wawezaje kusema, ‘Mimi si najisi,

sijawafuata Mabaali’?

Kumbuka jinsi ulivyotenda kule bondeni;

fikiri uliyoyafanya.

Wewe ni ngamia jike mwenye mbio

ukikimbia hapa na pale,

24 punda-mwitu aliyezoea jangwa,

anayenusa upepo katika tamaa yake kubwa:

katika wakati wake wa kuhitaji mbegu

ni nani awezaye kumzuia?

Madume yoyote yanayomfuatilia

hayana haja ya kujichosha;

wakati wa kupandwa kwake watampata tu.

25 Usikimbie hadi miguu yako iwe haina viatu,

na koo lako liwe limekauka.

Lakini ulisema, ‘Haina maana!

Ninaipenda miungu ya kigeni,

nami lazima niifuatie.’

26 “Kama vile mwizi aaibikavyo wakati amekamatwa,

hivyo ndivyo nyumba ya Israeli inavyoaibishwa:

wao wenyewe, wafalme wao na maafisa wao,

makuhani wao na manabii wao.

27 Wanaiambia miti, ‘Wewe ndiwe baba yangu,’

nalo jiwe, ‘Wewe ndiwe uliyenizaa.’

Wamenipa visogo vyao

wala hawakunigeuzia nyuso zao;

lakini wakiwa katika taabu, wanasema,

‘Njoo utuokoe!’

28 Iko wapi basi ile miungu mliyojitengenezea?

Yenyewe na ije kama inaweza kuwaokoa

wakati mko katika taabu!

Kwa maana mna miungu mingi

kama mlivyo na miji, ee Yuda.

29 “Kwa nini mnaleta mashtaka dhidi yangu?

Ninyi nyote mmeniasi,”

asemaBwana.

30 “Nimeadhibu watu wako bure tu,

hawakujirekebisha.

Upanga wako umewala manabii wako

kama simba mwenye njaa.

31 “Enyi wa kizazi hiki, tafakarini neno laBwana:

“Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli

au nchi ya giza kuu?

Kwa nini watu wangu wanasema, ‘Sisi tuko huru kuzurura,

hatutarudi kwako tena’?

32 Je, mwanamwali husahau vito vyake,

au bibi arusi mapambo yake ya arusi?

Lakini watu wangu wamenisahau mimi,

tena kwa siku zisizo na hesabu.

33 Je, wewe una ustadi kiasi gani katika kufuatia mapenzi!

Hata wale wanawake wabaya kuliko wote

wanaweza kujifunza kutokana na njia zako.

34 Katika nguo zako watu huona

damu ya uhai ya maskini wasio na hatia,

ingawa hukuwakamata wakivunja nyumba.

Lakini katika haya yote

35 unasema, ‘Sina hatia;

Mungu hajanikasirikia.’

Lakini nitakuhukumu kwa sababu unasema,

‘Mimi sijatenda dhambi.’

36 Kwa nini unatangatanga sana,

kubadili njia zako?

Utakatishwa tamaa na Misri

kama ulivyokatishwa na Ashuru.

37 Pia utaondoka mahali hapo

ukiwa umeweka mikono kichwani,

kwa kuwaBwanaamewakataa wale unaowatumainia;

hutasaidiwa nao.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/2-25231161dca39d00a279a7a85285a98f.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 3

Israeli Asiye Mwaminifu

1 “Kama mtu akimpa talaka mkewe,

naye akamwacha na akaolewa na mtu mwingine,

je, huyo mume aweza kumrudia tena?

Je, hiyo nchi haitanajisika kabisa?

Lakini umeishi kama kahaba na wapenzi wengi:

je, sasa utanirudia tena?”

asemaBwana.

2 “Inua macho utazame miinuko iliyo kame na uone.

Je, pana mahali ambapo hawajalala nawe?

Uliketi kando ya barabara ukiwasubiri wapenzi,

ukakaa kama yeye ahamahamaye jangwani.

Umeinajisi nchi

kwa ukahaba wako na uovu wako.

3 Kwa hiyo mvua imezuiliwa,

nazo mvua za vuli hazikunyesha.

Hata hivyo, una uso usio na haya kama wa kahaba;

unakataa kutahayari kwa aibu.

4 Je, wewe hujaniita hivi punde tu:

‘Baba yangu, rafiki yangu tangu ujana wangu,

5 je, utakasirika siku zote?

Je, ghadhabu yako itaendelea milele?’

Hivi ndivyo unavyozungumza,

lakini unafanya maovu yote uwezayo.”

Wito Kwa Ajili Ya Toba

6 Wakati wa utawala wa Mfalme Yosia,Bwanaaliniambia, “Umeona kile Israeli asiye mwaminifu amekifanya? Amepanda juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti uliotanda na amefanya uzinzi huko.

7 Mimi nilifikiri kuwa baada ya kuyafanya yote haya angelinirudia, lakini hakurudi, naye dada yake Yuda mdanganyifu aliona hili.

8 Nilimpa Israeli asiye mwaminifu hati yake ya talaka, na kumfukuza kwa ajili ya uzinzi wake wote. Hata hivyo nikaona kuwa Yuda dada yake mdanganyifu hakuogopa. Yeye pia alitoka na kufanya uzinzi.

9 Kwa sababu uasherati wa Israeli haukuwa kitu kwake, Yuda aliinajisi nchi kwa kuzini na mawe na miti.

10 Pamoja na hayo yote, Yuda dada yake mdanganyifu hakunirudia kwa moyo wake wote, bali kwa kujifanya tu,” asemaBwana.

11 Bwanaakaniambia, “Israeli asiye mwaminifu ana haki kuliko Yuda mdanganyifu.

12 Nenda, ukatangaze ujumbe huu kuelekea kaskazini:

“ ‘Rudi, Israeli usiye mwaminifu,’ asemaBwana,

‘sitakutazama tena kwa uso uliokunjamana,

kwa kuwa mimi ni mwenye huruma,’ asemaBwana,

‘Sitashika hasira yangu milele.

13 Ungama dhambi zako tu:

kwamba umemwasiBwanaMungu wako,

umetapanya wema wako kwa miungu ya kigeni

chini ya kila mti unaotanda,

nawe hukunitii mimi,’ ”

asemaBwana.

14 “Rudini, enyi watu msio waaminifu, kwa kuwa mimi ni mume wenu,” asemaBwana. “Nitawachagua ninyi, mmoja kutoka kwenye mji, na wawili kutoka kwenye ukoo, nami nitawaleta Sayuni.

15 Kisha nitawapeni wachungaji wanipendezao moyo wangu, ambao watawaongoza kwa maarifa na ufahamu.

16 Katika siku hizo, idadi yenu itakapokuwa imeongezeka sana katika nchi, watu hawatasema tena, ‘Sanduku la Agano laBwana,’ ” asemaBwana. “Halitaingia tena kwenye mawazo yao wala kukumbukwa, hawatalihitaji wala halitatengenezwa jingine.

17 Wakati huo, wataita Yerusalemu kuwa Kiti cha Enzi chaBwana, nayo mataifa yote watakusanyika Yerusalemu kuliheshimu jina laBwana. Hawatafuata tena ukaidi wa mioyo yao miovu.

18 Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaungana na nyumba ya Israeli, wao kwa pamoja watakuja kutoka nchi ya kaskazini hadi nchi niliyowapa baba zenu kama urithi.

19 “Mimi mwenyewe nilisema,

“ ‘Tazama jinsi nitakavyowatunza kwa furaha kama wana

na kuwapa nchi nzuri,

urithi ulio mzuri kuliko wa taifa jingine lolote.’

Nilidhani mngeniita ‘Baba,’

na msingegeuka, mkaacha kunifuata.

20 Lakini kama mwanamke asiye mwaminifu kwa mumewe,

vivyo hivyo mmekosa uaminifu kwangu pia, ee nyumba ya Israeli,”

asemaBwana.

21 Kilio kinasikika juu ya miinuko iliyo kame,

kulia na kuomboleza kwa watu wa Israeli,

kwa sababu wamepotoka katika njia zao

na wamemsahauBwanaMungu wao.

22 “Rudini, enyi watu msio waaminifu,

nami nitawaponya ukengeufu wenu.”

“Naam, tutakuja kwako,

kwa maana wewe niBwanaMungu wetu.

23 Hakika zile ghasia za kuabudu sanamu kwenye vilima

na milimani ni udanganyifu;

hakika katikaBwana, Mungu wetu,

uko wokovu wa Israeli.

24 Tangu ujana wetu miungu ya aibu imeyala

matunda ya kazi za baba zetu:

makundi yao ya kondoo na ngʼombe,

wana wao na binti zao.

25 Sisi na tulale chini katika aibu yetu,

na fedheha yetu itufunike.

Tumetenda dhambi dhidi yaBwanaMungu wetu,

sisi na mababa zetu;

tangu ujana wetu hadi leo

hatukumtiiBwanaMungu wetu.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/3-917b6ea650bc5f87169f2d50b31289b1.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 4

1 “Ikiwa utataka kurudi, ee Israeli,

nirudie mimi,”

asemaBwana.

“Ikiwa utaondoa sanamu zako za kuchukiza mbele ya macho yangu

na usiendelee kutangatanga,

2 ikiwa kwa kweli, kwa haki na kwa unyofu utaapa,

‘Kwa hakika kama vileBwanaaishivyo,’

ndipo mataifa yatakapobarikiwa naye

na katika yeye watajitukuza.”

3 Hili ndilo asemaloBwanakwa watu wa Yuda na kwa Yerusalemu:

“Vunjeni mabonge kwenye mashamba yenu,

wala msipande katikati ya miiba.

4 Jitahirini katikaBwana,

tahirini mioyo yenu,

enyi wanaume wa Yuda

na watu wa Yerusalemu,

la sivyo ghadhabu yangu itatoka kwa nguvu

na kuwaka kama moto

kwa sababu ya uovu mliotenda,

ikiwaka pasipo wa kuizima.

Maafa Kutoka Kaskazini

5 “Tangaza katika Yuda na upige mbiu katika Yerusalemu na kusema:

‘Piga tarumbeta katika nchi yote!’

Piga kelele na kusema:

‘Kusanyikeni pamoja!

Tukimbilie katika miji yenye maboma!’

6 Onyesheni ishara ili kwenda Sayuni!

Kimbilieni usalama pasipo kuchelewa!

Kwa kuwa ninaleta maafa kutoka kaskazini,

maangamizi ya kutisha.”

7 Simba ametoka nje ya pango lake,

mharabu wa mataifa amejipanga.

Ametoka mahali pake

ili aangamize nchi yenu.

Miji yenu itakuwa magofu

pasipo mtu wa kuishi humo.

8 Hivyo vaeni nguo za magunia,

ombolezeni na kulia kwa huzuni,

kwa kuwa hasira kali yaBwana

haijaondolewa kwetu.

9 “Katika siku ile,” asemaBwana

“mfalme na maafisa watakata tamaa,

makuhani watafadhaika,

na manabii watashangazwa mno.”

10 Ndipo niliposema, “Aa,BwanaMwenyezi, umewadanganyaje kabisa watu hawa na Yerusalemu kwa kusema, ‘Mtakuwa na amani,’ wakati upanga uko kwenye koo zetu!”

11 Wakati huo watu hawa na Yerusalemu wataambiwa, “Upepo wa moto kutoka miinuko iliyo kame katika jangwa unavuma kuelekea watu wangu, lakini sio kupepeta au kutakasa,

12 upepo wenye nguvu sana kuliko wa kupepeta na kutakasa utakuja kwa amri yangu. Sasa natangaza hukumu zangu dhidi yao.”

13 Tazama! Anakuja kama mawingu,

magari yake yanakuja kama upepo wa kisulisuli,

farasi wake wana mbio kuliko tai.

Ole wetu! Tunaangamia!

14 Ee Yerusalemu, usafishe uovu kutoka moyoni mwako na uokolewe.

Utaendelea kuficha mawazo mapotovu mpaka lini?

15 Sauti inatangaza kutoka Dani,

ikipiga mbiu ya maafa kutoka vilima vya Efraimu.

16 “Waambie mataifa jambo hili,

piga mbiu hii dhidi ya Yerusalemu:

‘Jeshi la kuzingira linakuja kutoka nchi ya mbali,

likipiga kelele ya vita dhidi ya miji ya Yuda.

17 Wamemzunguka kama watu walindao shamba,

kwa sababu amefanya uasi dhidi yangu,’ ”

asemaBwana.

18 “Mwenendo wako na matendo yako mwenyewe

yameleta haya juu yako.

Hii ndiyo adhabu yako.

Tazama jinsi ilivyo chungu!

Tazama jinsi inavyochoma moyo!”

19 Ee mtima wangu, mtima wangu!

Ninagaagaa kwa maumivu.

Ee maumivu makuu ya moyo wangu!

Moyo wangu umefadhaika ndani yangu,

siwezi kunyamaza.

Kwa sababu nimesikia sauti ya tarumbeta,

nimesikia kelele ya vita.

20 Maafa baada ya maafa,

nchi yote imekuwa magofu.

Kwa ghafula mahema yangu yameangamizwa,

makazi yangu kwa muda mfupi.

21 Hata lini nitaendelea kuona bendera ya vita

na kusikia sauti za tarumbeta?

22 “Watu wangu ni wapumbavu,

hawanijui mimi.

Ni watoto wasio na akili,

hawana ufahamu.

Ni hodari kutenda mabaya,

hawajui kutenda yaliyo mema.”

23 Niliitazama dunia,

nayo haikuwa na umbo tena ni tupu;

niliziangalia mbingu,

mianga ilikuwa imetoweka.

24 Niliitazama milima, nayo ilikuwa ikitetemeka,

vilima vyote vilikuwa vikiyumbayumba.

25 Nilitazama, wala watu hawakuwepo;

kila ndege wa angani alikuwa ameruka zake.

26 Nilitazama, hata nchi iliyokuwa imestawi vizuri imekuwa jangwa,

miji yake yote ilikuwa magofu

mbele zaBwana,

mbele ya hasira yake kali.

27 Hivi ndivyoBwanaasemavyo:

“Nchi yote itaharibiwa,

ingawa sitaiangamiza kabisa.

28 Kwa hiyo dunia itaomboleza

na mbingu zilizo juu zitakuwa giza,

kwa sababu nimesema nami sitarudi nyuma,

nimeamua na wala sitageuka.”

29 Kwa sauti ya wapanda farasi na wapiga upinde

kila mji unakimbia.

Baadhi wanakimbilia vichakani,

baadhi wanapanda juu ya miamba.

Miji yote imeachwa,

hakuna aishiye ndani yake.

30 Unafanya nini, ewe uliyeharibiwa?

Kwa nini unajivika vazi jekundu

na kuvaa vito vya dhahabu?

Kwa nini unapaka macho yako rangi?

Unajipamba bure.

Wapenzi wako wanakudharau,

wanautafuta uhai wako.

31 Nasikia kilio kama cha mwanamke

katika utungu wa kuzaa,

kilio cha uchungu kama cha anayemzaa

mtoto wake wa kwanza:

kilio cha Binti Sayuni akitweta ili aweze kupumua,

akiinua mikono yake, akisema,

“Ole wangu! Ninazimia;

maisha yangu yamekabidhiwa kwa wauaji.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/4-d6b16d9a29c1139a2216bc13a082d78a.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 5

Hakuna Hata Mmoja Aliye Mkamilifu

1 “Pandeni na kushuka katika mitaa ya Yerusalemu,

tazameni pande zote na mtafakari,

tafuteni katika viwanja vyake.

Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja tu

atendaye kwa uaminifu na kutafuta kweli,

nitausamehe mji huu.

2 Ingawa wanasema, ‘Kwa hakika kamaBwanaaishivyo,’

bado wanaapa kwa uongo.”

3 EeBwana, je, macho yako hayaitafuti kweli?

Uliwapiga, lakini hawakusikia maumivu,

uliwapondaponda, lakini walikataa maonyo.

Walifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko jiwe

nao walikataa kutubu.

4 Ndipo nikasema, “Hawa ni maskini tu;

wao ni wapumbavu,

kwa maana hawaijui njia yaBwana,

sheria ya Mungu wao.

5 Kwa hiyo nitakwenda kwa viongozi

na kuzungumza nao,

hakika wao wanaijua njia yaBwana,

sheria ya Mungu wao.”

Lakini kwa nia moja nao pia walikuwa wameivunja nira

na kuvivunja vifungo.

6 Kwa hiyo simba kutoka mwituni atawashambulia,

mbwa mwitu kutoka jangwani atawaangamiza,

chui atawavizia karibu na miji yao,

ili kumrarua vipande vipande yeyote atakayethubutu kutoka nje,

kwa maana maasi yao ni makubwa,

na kukengeuka kwao kumekuwa ni kwingi.

7 “Kwa nini niwasamehe?

Watoto wenu wameniacha na kuapa kwa miungu ambayo si miungu.

Niliwapatia mahitaji yao yote,

lakini bado wamefanya uzinzi na kusongana katika nyumba za makahaba.

8 Wamelishwa vizuri, kama farasi waume wenye tamaa nyingi,

kila mmoja akimlilia mke wa mwanaume mwingine.

9 Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?”

asemaBwana.

“Je, nisijilipizie kisasi

juu ya taifa kama hili?

10 “Piteni katika mashamba yake ya mizabibu na kuyaharibu,

lakini msiangamize kabisa.

Pogoeni matawi yake,

kwa kuwa watu hawa sio waBwana.

11 Nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda

wamekuwa si waaminifu kwangu kamwe,”

asemaBwana.

12 Wamedanganya kuhusuBwana.

Wamesema, “Yeye hatafanya jambo lolote!

Hakuna dhara litakalotupata;

kamwe hatutaona upanga wala njaa.

13 Manabii ni upepo tu, wala neno halimo ndani yao,

kwa hiyo hayo wayasemayo na yatendeke kwao.”

14 Kwa hiyo hili ndilo asemaloBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote:

“Kwa sababu watu hawa wamesema maneno haya,

nitayafanya maneno yangu vinywani mwenu kuwa moto,

na watu hawa wawe kuni

zinazoliwa na huo moto.

15 Ee nyumba ya Israeli,” asemaBwana,

“Ninaleta taifa toka mbali dhidi yako,

taifa la kale na linaloendelea kudumu,

taifa ambalo lugha yao huijui,

wala msemo wao huwezi kuuelewa.

16 Podo zao ni kama kaburi lililo wazi,

wote ni mashujaa hodari wa vita.

17 Watayaangamiza mazao yenu na chakula chenu,

wataangamiza wana wenu na mabinti zenu;

wataangamiza makundi yenu ya kondoo na ya ngʼombe,

wataangamiza mizabibu yenu na mitini yenu.

Kwa upanga wataangamiza

miji yenye maboma mliyoitumainia.

18 “Hata hivyo katika siku hizo, sitakuangamiza kabisa,” asemaBwana.

19 “Nao watu watakapouliza, ‘Kwa niniBwana, Mungu wetu ametufanyia mambo haya yote?’ utawaambia, ‘Kama vile mlivyoniacha mimi na kutumikia miungu migeni katika nchi yenu wenyewe, ndivyo sasa mtakavyowatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.’

20 “Itangazie nyumba ya Yakobo hili

na ulipigie mbiu katika Yuda:

21 Sikieni hili, enyi watu wapumbavu, msio na akili,

mlio na macho lakini hamwoni,

mlio na masikio lakini hamsikii:

22 Je, haiwapasi kuniogopa mimi?” asemaBwana.

“Je, haiwapasi kutetemeka mbele zangu?

Niliufanya mchanga kuwa mpaka wa bahari,

kizuizi cha milele ambacho haiwezi kupita.

Mawimbi yanaweza kuumuka, lakini hayawezi kuupita;

yanaweza kunguruma, lakini hayawezi kuuvuka.

23 Lakini watu hawa wana mioyo ya ukaidi na ya uasi,

wamegeukia mbali na kwenda zao.

24 Wao hawaambiani wenyewe,

‘Sisi na tumwogopeBwanaMungu wetu,

anayetupatia mvua za masika na za vuli kwa majira yake,

anayetuhakikishia majuma ya mavuno kwa utaratibu.’

25 Matendo yenu mabaya yamezuia haya yote,

dhambi zenu zimewazuia msipate mema.

26 “Miongoni mwa watu wangu wamo walio waovu

wanaovizia kama watu wanaotega ndege,

na kama wale wanaoweka mitego

kuwakamata watu.

27 Kama vitundu vilivyojaa ndege,

nyumba zao zimejaa udanganyifu;

wamekuwa matajiri na wenye nguvu,

28 wamenenepa na kunawiri.

Matendo yao maovu hayana kikomo;

hawatetei mashauri ya yatima wapate kushinda,

hawatetei haki za maskini.

29 Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?”

asemaBwana.

“Je, nisijilipizie kisasi

juu ya taifa kama hili?

30 “Jambo la kutisha na kushtusha

limetokea katika nchi hii:

31 Manabii wanatabiri uongo,

makuhani wanatawala kwa mamlaka yao wenyewe,

nao watu wangu wanapenda hivyo.

Lakini mtafanya nini mwisho wake?

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/5-db89a177e08909e60b4f558336801058.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 6

Yerusalemu Imezingirwa Na Jeshi

1 “Kimbieni kwa usalama wenu, enyi watu wa Benyamini!

Kimbieni kutoka Yerusalemu!

Pigeni tarumbeta katika Tekoa!

Inueni ishara juu ya Beth-Hakeremu!

Kwa kuwa maafa yanaonekana yakitoka kaskazini,

na uharibifu wa kutisha.

2 Nitamwangamiza Binti Sayuni,

aliye mzuri sana na mwororo.

3 Wachungaji pamoja na makundi yao

watakuja dhidi yake;

watapiga mahema yao kumzunguka,

kila mmoja akichunga kundi lake mwenyewe.”

4 “Jiandaeni kwa vita dhidi yake!

Inukeni tumshambulie mchana!

Lakini, ole wetu, mchana unaisha,

na vivuli vya jioni vinazidi kuwa virefu.

5 Kwa hiyo inukeni, tufanye mashambulizi usiku,

na kuharibu ngome zake!”

6 Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote:

“Kateni miti mjenge boma

kuzunguka Yerusalemu.

Mji huu ni lazima uadhibiwe,

umejazwa na uonevu.

7 Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake,

ndivyo anavyomwaga uovu wake.

Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake,

ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima.

8 Pokea onyo, ee Yerusalemu,

la sivyo nitageukia mbali nawe

na kuifanya nchi yako kuwa ukiwa,

asiweze mtu kuishi ndani yake.”

9 Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote:

“Wao na wayakusanye mabaki ya Israeli

kwa uangalifu kama kwenye mzabibu;

pitisha mkono wako kwenye matawi tena,

kama yeye avunaye zabibu.”

10 Niseme na nani na kumpa onyo?

Ni nani atakayenisikiliza mimi?

Masikio yao yameziba,

kwa hiyo hawawezi kusikia.

Neno laBwanani chukizo kwao,

hawalifurahii.

11 Lakini nimejaa ghadhabu yaBwana,

nami siwezi kuizuia.

“Wamwagie watoto walioko barabarani,

na juu ya vijana waume waliokusanyika;

mume na mke watakumbwa pamoja ndani yake,

hata nao wazee waliolemewa na miaka.

12 Nyumba zao zitapewa watu wengine,

pamoja na mashamba yao na wake zao,

nitakapounyoosha mkono wangu

dhidi ya wale waishio katika nchi,”

asemaBwana.

13 “Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,

wote wana tamaa ya kupata faida zaidi;

manabii na makuhani wanafanana,

wote wanafanya udanganyifu.

14 Wanafunga majeraha ya watu wangu

bila uangalifu.

Wanasema, ‘Amani, amani,’

wakati hakuna amani.

15 Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao

inayochukiza mno?

Hapana, hawana aibu hata kidogo;

hawajui hata kuona haya.

Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka,

watashushwa chini nitakapowaadhibu,”

asemaBwana.

16 Hivi ndivyo asemavyoBwana:

“Simama kwenye njia panda utazame,

ulizia mapito ya zamani,

ulizia wapi ilipo njia nzuri, uifuate hiyo,

nanyi mtapata raha nafsini mwenu.

Lakini ninyi mlisema, ‘Hatutaipita hiyo.’

17 Niliweka walinzi juu yenu na kusema,

‘Sikieni sauti ya tarumbeta!’

Lakini mkasema, ‘Hatutasikiliza.’

18 Kwa hiyo sikilizeni, enyi mataifa,

angalieni, enyi mashahidi,

lile litakalowatokea.

19 Sikia, ee nchi:

Ninaleta maafa juu ya watu hawa,

matunda ya mipango yao,

kwa sababu hawakusikiliza maneno yangu

na wameikataa sheria yangu.

20 Unanifaa nini uvumba kutoka Sheba,

au udi wa harufu nzuri kutoka nchi ya mbali?

Sadaka zako za kuteketezwa hazikubaliki,

dhabihu zako hazinifurahishi mimi.”

21 Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyoBwana:

“Nitaweka vikwazo mbele ya watu hawa.

Baba na wana wao watajikwaa juu yake,

majirani na marafiki wataangamia.”

22 Hivi ndivyo asemavyoBwana:

“Tazama, jeshi linakuja

kutoka nchi ya kaskazini,

taifa kubwa linaamshwa

kutoka miisho ya dunia.

23 Wamejifunga pinde na mkuki,

ni wakatili na hawana huruma.

Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma

wanapoendesha farasi zao.

Wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita

ili kukushambulia, ee Binti Sayuni.”

24 Tumesikia taarifa zao,

nayo mikono yetu imelegea.

Uchungu umetushika,

maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.

25 Usitoke kwenda mashambani

au kutembea barabarani,

kwa kuwa adui ana upanga,

na kuna vitisho kila upande.

26 Enyi watu wangu, vaeni magunia

mjivingirishe kwenye majivu,

ombolezeni kwa kilio cha uchungu

kama amliliaye mwana pekee,

kwa maana ghafula

mharabu atatujia.

27 “Nimekufanya wewe kuwa kitu cha kujaribu chuma,

nao watu wangu kama mawe yenye madini,

ili upate kuzijua na kuzijaribu njia zao.

28 Wote ni waasi sugu,

wakienda huku na huko kusengenya.

Wao ni shaba na chuma,

wote wanatenda upotovu.

29 Mivuo inavuma kwa nguvu,

kinachoungua kwa huo moto ni risasi,

lakini pamoja na kusafisha kote huku ni bure;

waovu hawaondolewi.

30 Wanaitwa fedha iliyokataliwa,

kwa sababuBwanaamewakataa.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/6-e49680ec34ceddf994d47cedcf5c68f0.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 7

Dini Za Uongo Hazina Maana

1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwaBwana:

2 “Simama kwenye lango la nyumba yaBwana, na huko upige mbiu ya ujumbe huu:

“ ‘Sikieni neno laBwana, enyi watu wote wa Yuda mliokuja kupitia malango haya ili kumwabuduBwana.

3 Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Tengenezeni njia zenu na matendo yenu, nami nitawaacha mkae mahali hapa.

4 Msitumainie maneno ya udanganyifu na kusema, “Hili ni Hekalu laBwana, Hekalu laBwana, Hekalu laBwana!”

5 Kama kweli mkibadili njia zenu na matendo yenu, mkatendeana haki kila mmoja na mwenzake,

6 kama msipomwonea mgeni, yatima wala mjane, na kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa, nanyi kama msipofuata miungu mingine kwa madhara yenu wenyewe,

7 ndipo nitawaacha mkae mahali hapa, katika nchi niliyowapa baba zenu milele na milele.

8 Lakini tazama, mnatumainia maneno ya udanganyifu yasiyo na maana.

9 “ ‘Je, mtaiba na kuua, mtazini na kuapa kwa uongo, na kufukiza uvumba kwa Baali, na kufuata miungu mingine ambayo hamkuijua,

10 kisha mje na kusimama mbele yangu katika nyumba hii inayoitwa kwa Jina langu, mkisema, “Tuko salama.” Salama kwa kufanya mambo haya yote ya kuchukiza?

11 Je, nyumba hii, iitwayo kwa Jina langu, imekuwa pango la wanyangʼanyi kwenu? Lakini nimekuwa nikiona yanayotendeka! asemaBwana.

12 “ ‘Nendeni sasa mahali pangu palipokuwa huko Shilo, mahali ambapo nilipafanya pa kwanza kuwa makao ya Jina langu, nanyi mwone lile nililopafanyia kwa ajili ya uovu wa watu wangu Israeli.

13 Mlipokuwa mnafanya yote haya, asemaBwana, nilisema nanyi tena na tena, lakini hamkusikiliza; niliwaita, lakini hamkujibu.

14 Kwa hiyo, nililolifanyia Shilo, nitalifanya sasa kwa nyumba hii iitwayo kwa Jina langu, Hekalu mnalolitumainia, mahali nilipowapa ninyi na baba zenu.

15 Nitawafukuza mbele yangu, kama nilivyowafanyia ndugu zenu, watu wa Efraimu.’

16 “Kwa hiyo usiombe kwa ajili ya watu hawa, wala usinililie, na usifanye maombi kwa ajili yao; usinisihi, kwa sababu sitakusikiliza.

17 Je, huyaoni hayo wanayoyatenda katika miji ya Yuda na katika barabara za Yerusalemu?

18 Watoto wanakusanya kuni, baba zao wanawasha moto, na wanawake wanakanda unga na kuoka mikate kwa ajili ya Malkia wa Mbinguni. Wanamimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha.

19 Lakini je, mimi ndiye wanayenikasirisha? asemaBwana. Je, hawajiumizi wenyewe na kujiaibisha?

20 “ ‘Kwa hiyo hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenyezi: Hasira yangu na ghadhabu yangu itamwagwa mahali hapa, juu ya mwanadamu na mnyama, juu ya miti ya shambani na juu ya matunda ya ardhini, nayo itaungua pasipo kuzimwa.

21 “ ‘Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Endeleeni, ongezeni sadaka zenu za kuteketezwa juu ya dhabihu zenu nyingine, mle nyama hiyo wenyewe!

22 Kwa kuwa nilipowaleta baba zenu kutoka Misri na kusema nao, sikuwapa amri kuhusu sadaka za kuteketezwa na dhabihu tu,

23 lakini niliwapa amri hii nikisema: Nitiini mimi, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Enendeni katika njia zote ninazowaamuru ili mpate kufanikiwa.

24 Lakini hawakusikiliza wala kujali. Badala yake, walifuata ukaidi wa mioyo yao miovu. Walirudi nyuma badala ya kusonga mbele.

25 Tangu wakati ule baba zenu walipotoka Misri hadi sasa, siku baada ya siku, tena na tena nimewatumia watumishi wangu manabii.

26 Lakini hawakunisikiliza wala hawakujali. Walikuwa na shingo ngumu na kufanya maovu kuliko baba zao.’

27 “Utakapowaambia haya yote, hawatakusikiliza; utakapowaita, hawatajibu.

28 Kwa hiyo waambie, ‘Hili ni taifa ambalo halimtiiBwana, Mungu wao, wala kukubali maonyo. Kweli imekufa, imetoweka midomoni mwao.

29 Nyoeni nywele zenu na kuzitupa, ombolezeni katika miinuko iliyo kame, kwa kuwaBwanaamekikataa na kukiacha kizazi hiki kilichomkasirisha.

Bonde La Machinjo

30 “ ‘Watu wa Yuda wamefanya maovu machoni pangu, asemaBwana. Wameziweka sanamu zao za machukizo ndani ya nyumba iitwayo kwa Jina langu, na wameitia unajisi.

31 Wamejenga mahali pa juu pa kuabudia sanamu pa Tofethi kwenye Bonde la Ben-Hinomu ili kuwateketeza wana wao na binti zao kwenye moto, kitu ambacho sikuamuru, wala hakikuingia akilini mwangu.

32 Kwa hiyo mjihadhari, siku zinakuja, asemaBwana, wakati watu watakapokuwa hawapaiti Tofethi au Bonde la Ben-Hinomu, lakini watapaita Bonde la Machinjo, kwa sababu watawazika wafu huko Tofethi mpaka pasiwe tena nafasi.

33 Ndipo mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwepo na yeyote wa kuwafukuza.

34 Nitazikomesha sauti za shangwe na furaha, na sauti za bwana arusi na bibi arusi katikati ya miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu, kwa sababu nchi itakuwa ukiwa.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/7-33a1b99e0bdfada4376ac4250541752a.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 8

1 “ ‘Wakati huo, asemaBwana, mifupa ya wafalme na maafisa wa Yuda, mifupa ya makuhani na manabii, na mifupa ya watu wa Yerusalemu itaondolewa kutoka makaburi yao.

2 Itawekwa wazi kwa jua, na mwezi, na nyota zote za mbingu, ambazo walizipenda na kuzitumikia, na ambazo wamezifuata kutafuta ushauri na kuziabudu. Hawatakusanywa pamoja au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyotapakaa juu ya ardhi.

3 Popote nitakapowafukuzia, mabaki wote wa kizazi hiki kiovu watatamani kufa kuliko kuishi, asemaBwanaMwenye Nguvu Zote.’

Dhambi Na Adhabu

4 “Waambie, ‘Hivi ndivyo asemavyoBwana:

“ ‘Je, watu wanapoanguka hawainuki?

Je, mtu anapopotea harudi?

5 Kwa nini basi watu hawa walipotea?

Kwa nini Yerusalemu inapotea kila mara?

Wanangʼangʼania udanganyifu

na wanakataa kurudi.

6 Nimewasikiliza kwa makini,

lakini hawataki kusema lililo sawa.

Hakuna anayetubia makosa yake

akisema, “Nimefanya nini?”

Kila mmoja hufuata njia yake mwenyewe

kama farasi anayekwenda vitani.

7 Hata korongo aliyeko angani

anayajua majira yake yaliyoamriwa,

nao njiwa, mbayuwayu na koikoi

hufuata majira yao ya kurudi.

Lakini watu wangu hawajui

Bwanaanachotaka kwao.

8 “ ‘Mwawezaje kusema, “Sisi tuna busara

kwa sababu tunayo sheria yaBwana,”

wakati ambapo kwa hakika kalamu ya uongo ya waandishi

imeandika kwa udanganyifu?

9 Wenye hekima wataaibika,

watafadhaika na kunaswa.

Kwa kuwa wamelikataa neno laBwana,

hiyo hekima waliyo nayo ni ya namna gani?

10 Kwa hiyo nitawapa watu wengine wake zao,

na mashamba yao kwa wamiliki wengine.

Kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkubwa kabisa,

wote wana tamaa ya kupata zaidi;

manabii na makuhani wanafanana,

wote wanafanya udanganyifu.

11 Wanafunga majeraha ya watu wangu

bila uangalifu.

Wanasema, “Amani, amani,”

wakati hakuna amani.

12 Je, wanaona aibu kwa ajili ya tabia yao inayochukiza mno?

Hapana, hawana aibu hata kidogo,

hawajui hata kuona haya.

Kwa hiyo wataanguka miongoni mwa hao walioanguka,

watashushwa chini watakapoadhibiwa,

asemaBwana.

13 “ ‘Nitayaondoa mavuno yao,

asemaBwana.

Hapatakuwepo zabibu kwenye mzabibu.

Hapatakuwepo na tini kwenye mtini,

majani yake yatanyauka.

Kile nilichowapa

watanyangʼanywa.’ ”

14 “Kwa nini tunaketi hapa?

Kusanyikeni pamoja!

Tukimbilie kwenye miji yenye maboma,

tukaangamie huko!

Kwa kuwaBwana, Mungu wetu

ametuhukumu kuangamia,

na kutupa maji yenye sumu tunywe,

kwa sababu tumemtenda dhambi.

15 Tulitegemea amani,

lakini hakuna jema lililokuja,

tulitegemea wakati wa kupona,

lakini kulikuwa hofu tu.

16 Mkoromo wa farasi za adui

umesikika kuanzia Dani,

kwa mlio wa madume yao ya farasi,

nchi yote inatetemeka.

Wamekuja kuangamiza nchi na vyote vilivyomo,

mji na wote waishio ndani yake.”

17 “Tazama, nitatuma nyoka wenye sumu kali katikati yenu,

fira ambao hawawezi kulogwa,

nao watawauma,”

asemaBwana.

18 Ee Mfariji wangu katika huzuni,

moyo wangu umezimia ndani yangu.

19 Sikia kilio cha watu wangu

kutoka nchi ya mbali:

“Je,Bwanahayuko Sayuni?

Je, Mfalme wake hayuko tena huko?”

“Kwa nini wamenikasirisha kwa vinyago vyao,

kwa sanamu zao za kigeni zisizofaa?”

20 “Mavuno yamepita,

kiangazi kimekwisha,

nasi hatujaokolewa.”

21 Kwa kuwa watu wangu wamepondwa, nami nimepondeka pia;

ninaomboleza, nayo hofu kuu imenishika.

22 Je, hakuna zeri ya kuponya katika Gileadi?

Je, hakuna tabibu huko?

Kwa nini basi hakuna uponyaji

wa majeraha ya watu wangu?

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/8-e933fd5efcea2bc05863648d23243122.mp3?version_id=1627—

Categories
Yeremia

Yeremia 9

1 Laiti kichwa changu kingekuwa chemchemi ya maji

na macho yangu yangekuwa kisima cha machozi!

Ningelia usiku na mchana

kwa kuuawa kwa watu wangu.

2 Laiti ningekuwa na nyumba

ya kukaa wasafiri jangwani,

ningewaacha watu wangu

na kwenda mbali nao,

kwa kuwa wote ni wazinzi,

kundi la watu wadanganyifu.

3 “Huweka tayari ndimi zao kama upinde,

ili kurusha uongo;

wamekuwa na nguvu katika nchi

lakini si katika ukweli.

Wanatoka dhambi moja hadi nyingine,

hawanitambui mimi,”

asemaBwana.

4 “Jihadhari na rafiki zako;

usiwaamini ndugu zako.

Kwa kuwa kila ndugu ni mdanganyifu,

na kila rafiki ni msingiziaji.

5 Rafiki humdanganya rafiki,

hakuna yeyote asemaye kweli.

Wamefundisha ndimi zao kudanganya,

wanajichosha wenyewe katika kutenda dhambi.

6 Unakaa katikati ya udanganyifu;

katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,”

asemaBwana.

7 Kwa hiyo hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote:

“Tazama, nitawasafisha na kuwajaribu,

kwani ni nini kingine niwezacho kufanya

kwa sababu ya dhambi ya watu wangu?

8 Ndimi zao ni mshale wenye sumu,

hunena kwa udanganyifu.

Kwa kinywa chake kila mmoja huzungumza maneno mazuri na jirani yake,

lakini moyoni mwake humtegea mtego.

9 Je, nisiwaadhibu kwa ajili ya jambo hili?”

asemaBwana.

“Je, nisijilipizie kisasi

kwa taifa kama hili?”

10 Nitalia na kuomboleza kwa ajili ya milima

na kuomboleza kuhusu malisho ya jangwani.

Yamekuwa ukiwa, wala hakuna apitaye humo,

milio ya ngʼombe haisikiki.

Ndege wa angani wametoroka

na wanyama wamekimbia.

11 “Nitaifanya Yerusalemu lundo la magofu,

makao ya mbweha;

nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa

ili asiwepo atakayeishi humo.”

12 Ni mtu yupi aliye na hekima ya kutosha ayaelewe haya? Ni nani aliyefundishwa naBwanaawezaye kuyaeleza haya? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa ukiwa kama jangwa ambapo hakuna awezaye kupita?

13 Bwanaakasema, “Ni kwa sababu wameiacha sheria yangu, niliyoiweka mbele yao: hawajaniheshimu mimi wala kufuata sheria yangu.

14 Badala yake wamefuata ukaidi wa mioyo yao, wamefuata Mabaali, kama vile baba zao walivyowafundisha.”

15 Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: “Tazama, nitawafanya watu hawa wale chakula kichungu na kunywa maji yenye sumu.

16 Nitawatawanya katika mataifa ambayo wao wala baba zao hawakuwajua, nikiwafuata kwa upanga mpaka niwe nimewaangamiza kabisa.”

17 Hivi ndivyo asemavyoBwanaMwenye Nguvu Zote:

“Fikiri sasa! Waite wanawake waombolezao waje,

waite wale walio na ustadi kuliko wote.

18 Nao waje upesi

na kutuombolezea,

mpaka macho yetu yafurike machozi

na vijito vya maji vitoke kwenye kope zetu.

19 Sauti ya kuomboleza imesikika kutoka Sayuni:

‘Tazama jinsi tulivyoangamizwa!

Tazama jinsi aibu yetu ilivyo kubwa!

Ni lazima tuihame nchi yetu

kwa sababu nyumba zetu zimekuwa magofu.’ ”

20 Basi, enyi wanawake, sikieni neno laBwana;

fungueni masikio yenu msikie maneno ya kinywa chake.

Wafundisheni binti zenu kuomboleza;

fundishaneni kila mmoja na mwenzake maombolezo.

21 Mauti imeingia ndani kupitia madirishani,

imeingia kwenye majumba yetu ya fahari;

imewakatilia mbali watoto katika barabara

na vijana waume kutoka viwanja vya miji.

22 Sema, “Hili ndilo asemaloBwana:

“ ‘Maiti za wanaume zitalala

kama mavi katika mashamba,

kama malundo ya nafaka nyuma ya mvunaji,

wala hakuna anayekusanya.’ ”

23 Hili ndilo asemaloBwana:

“Mwenye hekima asijisifu katika hekima yake,

au mwenye nguvu ajisifu katika nguvu zake,

wala tajiri ajisifu katika utajiri wake,

24 lakini yeye ajisifuye, na ajisifu kwa sababu hili:

kwamba ananifahamu na kunijua mimi,

kwamba mimi ndimiBwana, nitendaye wema,

hukumu na haki duniani,

kwa kuwa napendezwa na haya,”

asemaBwana.

25 “Siku zinakuja, nitakapowaadhibu wale wote ambao wametahiriwa kimwili tu, asemaBwana,

26 yaani Misri, Yuda, Edomu, Amoni, Moabu na wote wanaoishi jangwani sehemu za mbali. Kwa maana mataifa haya yote hayakutahiriwa mioyo yao, nayo nyumba yote ya Israeli haikutahiriwa.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/9-2849268e2ce5e5921009817933f8b1bf.mp3?version_id=1627—