Categories
Isaya

Isaya 30

Ole Wa Taifa Kaidi

1 Bwanaasema,

“Ole kwa watoto wakaidi,

kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu,

wakifanya makubaliano, lakini si kwa Roho wangu,

wakilundika dhambi juu ya dhambi,

2 wale washukao kwenda Misri

bila kutaka shauri langu,

wanaotafuta msaada wa ulinzi wa Farao,

watafutao kivuli cha Misri kwa ajili ya kimbilio.

3 Lakini ulinzi wa Farao utakuwa kwa aibu yenu,

kivuli cha Misri kitawaletea fedheha.

4 Ingawa wana maafisa katika Soani

na wajumbe wamewasili katika Hanesi,

5 kila mmoja ataaibishwa

kwa sababu ya taifa lisilowafaa kitu,

ambalo haliwaletei msaada wala faida,

bali aibu tu na fedheha.”

6 Neno kuhusu wanyama wa Negebu:

Katika nchi ya taabu na shida,

ya simba za dume na jike,

ya nyoka mwenye sumu kali na nyoka warukao,

wajumbe huchukua utajiri wao juu ya migongo ya punda,

hazina zao juu ya nundu za ngamia,

kwa lile taifa lisilokuwa na faida,

7 kuvipeleka Misri,

ambaye msaada wake haufai kabisa.

Kwa hiyo nimemwita “Rahabu Asiyefanya Chochote.”

8 Nenda sasa, liandike neno hili juu ya kibao kwa ajili yao,

liandike kwenye kitabu,

ili liweze kuwa shahidi milele

kwa ajili ya siku zijazo.

9 Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu,

watoto ambao hawataki kusikiliza mafundisho yaBwana.

10 Wanawaambia waonaji,

“Msione maono tena!”

Nako kwa manabii wanasema,

“Msiendelee kutupatia maono

ambayo ni ya kweli!

Tuambieni mambo ya kupendeza,

tabirini mambo ya uongo.

11 Acheni njia hii,

ondokeni katika mapito haya,

nanyi acheni kutukabili pamoja

na yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!”

12 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:

“Kwa sababu mmekataa ujumbe huu,

mkategemea uonevu na kutumainia udanganyifu,

13 dhambi hii itakuwa kwenu

kama ukuta mrefu,

wenye ufa na wenye kubetuka,

ambao unaanguka ghafula,

mara moja.

14 Utavunjika vipande vipande kama chombo cha udongo

ukipasuka pasipo huruma

ambapo katika vipande vyake

hakuna kipande kitakachopatikana

kwa kuukulia makaa kutoka jikoni

au kuchotea maji kisimani.”

15 Hili ndiloBwanaMwenyezi, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, asemalo:

“Katika kutubu na kupumzika ndio wokovu wenu,

katika kutulia na kutumaini ndizo nguvu zenu,

lakini hamkutaka.

16 Mlisema, ‘Hapana, tutakimbia kwa farasi.’

Kwa hiyo mtakimbia!

Mlisema, ‘Tutakimbia kwa farasi waendao kasi.’

Kwa hiyo wanaowafukuza watakwenda kasi!

17 Watu 1,000 watakimbia

kwa ajili ya kitisho cha mtu mmoja,

kwa vitishio vya watu watano

wote mtakimbia,

hadi mtakapoachwa kama mlingoti wa bendera

juu ya kilele cha mlima,

kama bendera juu ya kilima.”

18 Hata hivyoBwanaanatamani kutupatia neema,

anainuka ili kuwaonyesha huruma.

Kwa kuwaBwanani Mungu wa haki.

Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!

19 Enyi watu wa Sayuni, mnaoishi Yerusalemu, hamtalia tena. Tazameni jinsi atakavyokuwa na huruma mtakapolia kwa kumwomba msaada! Mara asikiapo, atawajibu.

20 Ingawa Bwana huwapa chakula cha shida na maji ya taabu, walimu wenu hawatafichwa tena, kwa macho yenu wenyewe mtawaona.

21 Mkigeuka kuume au kushoto, masikio yenu yatasikia sauti nyuma yenu ikisema, “Hii ndiyo njia, ifuateni.”

22 Kisha mtanajisi sanamu zenu zilizofunikwa kwa fedha, na vinyago vyenu vilivyofunikwa kwa dhahabu. Mtazitupilia mbali kama vitambaa vya wakati wa hedhi na kuziambia, “Haya, tokeni hapa!”

23 Pia atawapa mvua kwa ajili ya mbegu mnazootesha ardhini, chakula kinachotoka ardhini kitakuwa kizuri sana, tena tele. Katika siku ile, ngʼombe wenu watalisha katika shamba pana la majani.

24 Maksai na punda walimao watakula majani makavu na vyakula vilivyotengenezwa, vinavyotandazwa kwa uma na sepeto.

25 Katika siku ile ya mauaji makuu, wakati minara itakapoanguka, vijito vya maji vitatiririka juu ya kila mlima mrefu na kila kilima kilichoinuka sana.

26 Mwezi utaangaza kama jua, nao mwanga wa jua utangʼaa mara saba zaidi, kama nuru ya siku saba, wakatiBwanaatakapoyafunga majeraha ya watu wake na kuwaponya vidonda alivyowatia.

27 Tazama, Jina laBwanalinakuja kutoka mbali,

likiwa na hasira kali inayowaka

pamoja na wingu zito la moshi,

midomo yake imejaa ghadhabu

na ulimi wake ni moto ulao.

28 Pumzi yake ni kama mkondo wa maji yaendayo kasi,

yakipanda hadi shingoni.

Hutikisa mataifa katika chekecheke ya uharibifu,

huweka lijamu katika mataya ya mataifa

ambayo huwaongoza upotevuni.

29 Nanyi mtaimba kama usiku ule mnaadhimisha

sikukuu takatifu.

Mioyo yenu itashangilia

kama vile watu wanapokwea na filimbi

kwenye mlima waBwana,

kwa Mwamba wa Israeli.

30 Bwanaatawasababisha watu waisikie sauti yake ya utukufu,

naye atawafanya wauone mkono wake ukishuka

pamoja na hasira yake kali na moto ulao,

kukiwa na tufani ya mvua,

ngurumo za radi na mvua ya mawe.

31 Sauti yaBwanaitaivunjavunja Ashuru,

kwa fimbo yake ya utawala atawapiga.

32 Kila pigoBwanaatakaloliweka juu yao

kwa fimbo yake ya kuadhibu,

litakuwa kwa wimbo wa matari na vinubi,

anapopigana nao katika vita

kwa mapigo ya mkono wake.

33 Tofethi imeandaliwa toka zamani,

imewekwa tayari kwa ajili ya mfalme.

Shimo lake la moto limetengenezwa kwa kina kirefu

na kwa upana mkubwa,

likiwa na moto na kuni tele;

pumzi yaBwana,

kama kijito cha kiberiti,

huuwasha moto.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/30-0fdc42da734d063b43738287f9512bc2.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 31

Ole Wa Wale Wanaotegemea Misri

1 Ole wao wale washukao Misri kwa ajili ya msaada,

wale wategemeao farasi,

wanaoweka tumaini katika wingi wa magari yao ya vita,

na katika nguvu nyingi za wapanda farasi,

lakini hawamwangalii yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,

wala hawatafuti msaada kwaBwana.

2 Hata hivyo yeye pia ana hekima na anaweza kuleta maafa,

wala hayatangui maneno yake.

Yeye atainuka dhidi ya nyumba ya mwovu,

dhidi ya wale ambao huwasaidia watenda mabaya.

3 Lakini Wamisri ni wanadamu, wala si Mungu,

farasi wao ni nyama, wala si roho.

WakatiBwanaatakaponyoosha Mkono wake,

yeye anayesaidia atajikwaa,

naye anayesaidiwa ataanguka,

wote wawili wataangamia pamoja.

4 Hili ndiloBwanaanaloniambia:

“Kama vile simba angurumavyo,

simba mkubwa juu ya mawindo yake:

hata ingawa kundi lote la wachunga mifugo

huitwa pamoja dhidi yake,

hatiwi hofu na kelele zao

wala kusumbuliwa na ghasia zao;

ndivyoBwanaMwenye Nguvu Zote atakavyoshuka

kufanya vita juu ya Mlima Sayuni

na juu ya vilele vyake.

5 Kama ndege warukao,

BwanaMwenye Nguvu Zote ataukinga Yerusalemu;

ataukinga na kuuokoa,

atapita juu yake na kuufanya salama.”

6 Mrudieni yeye ambaye nyumba ya Israeli imemwasi sana.

7 Kwa kuwa katika siku ile kila mmoja wenu atazikataa sanamu za fedha na za dhahabu zilizotengenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi.

8 “Ashuru itaanguka kwa upanga ambao si wa mwanadamu;

upanga usio wa kibinadamu utawaangamiza.

Watakimbia mbele ya upanga

na vijana wao wa kiume watafanyizwa kazi kwa lazima.

9 Ngome zao zitaanguka kwa sababu ya hofu;

kwa kuona bendera ya vita,

majemadari wao watashikwa na hofu ya ghafula,”

asemaBwana,

ambaye moto wake uko Sayuni,

nayo tanuru yake iko Yerusalemu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/31-5cfb50d7e1913a2e11ccab7e3b674f51.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 32

Ufalme Wa Haki

1 Tazama, mfalme atatawala kwa uadilifu

na watawala watatawala kwa haki.

2 Kila mtu atakuwa kama kivuli cha kujificha kutokana na upepo

na kimbilio kutokana na dhoruba,

kama vijito vya maji jangwani

na kivuli cha mwamba mkubwa katika ardhi yenye kiu.

3 Ndipo macho ya wale wanaoona hayatafumbwa tena,

nayo masikio ya wale wanaosikia yatasikiliza.

4 Moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu na kuelewa,

nao ulimi wenye kigugumizi utanena kwa ufasaha.

5 Mpumbavu hataitwa tena muungwana,

wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu.

6 Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu,

moyo wake hushughulika na uovu:

Hutenda mambo yasiyo ya kumcha Mungu,

na hueneza habari za makosa kuhusuBwana;

yeye huwaacha wenye njaa bila kitu,

na wenye kiu huwanyima maji.

7 Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu,

hufanya mipango miovu

ili kumwangamiza maskini kwa uongo,

hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki.

8 Lakini mtu muungwana hufanya mipango ya kiungwana,

na kwa matendo ya kiungwana yeye hufanikiwa.

Wanawake Wa Yerusalemu

9 Enyi wanawake wenye kuridhika sana,

amkeni na mnisikilize.

Enyi binti mnaojisikia kuwa salama,

sikieni lile ninalotaka kuwaambia!

10 Muda zaidi kidogo ya mwaka mmoja,

ninyi mnaojisikia salama mtatetemeka,

mavuno ya zabibu yatakoma

na mavuno ya matunda hayatakuwepo.

11 Tetemekeni, enyi wanawake wenye kuridhika,

tetemekeni kwa hofu, enyi binti mnaojisikia salama!

Vueni nguo zenu,

vaeni nguo ya gunia viunoni mwenu.

12 Pigeni matiti yenu kwa ajili ya mashamba mazuri,

kwa ajili ya mizabibu iliyozaa vizuri

13 na kwa ajili ya nchi ya watu wangu,

nchi ambayo miiba na michongoma imemea:

naam, ombolezeni kwa ajili ya nyumba zote za furaha

na kwa ajili ya mji huu wenye kufanya sherehe.

14 Ngome itaachwa,

mji wenye kelele nyingi utahamwa,

ngome ndani ya mji na mnara wa ulinzi vitakuwa ukiwa milele,

mahali pazuri pa punda na malisho ya makundi ya kondoo,

15 mpaka Roho amwagwe juu yetu kutoka juu,

nalo jangwa kuwa shamba lenye rutuba,

na shamba lenye rutuba kuwa kama msitu.

16 Haki itakaa katika jangwa,

na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba.

17 Matunda ya haki yatakuwa amani,

matokeo ya haki yatakuwa utulivu

na matumaini milele.

18 Watu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani,

katika nyumba zilizo salama,

katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu.

19 Hata kama mvua ya mawe iangushe msitu

na mji ubomolewe kabisa,

20 tazama jinsi utakavyobarikiwa,

ukipanda mbegu yako katika kila kijito,

na kuwaacha ngʼombe wako

na punda wajilishe kwa uhuru.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/32-3621b8ccce0d1fe34d61cabc87da26c8.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 33

Taabu Na Msaada

1 Ole wako wewe, ee mharabu,

wewe ambaye hukuharibiwa!

Ole wako, ee msaliti,

wewe ambaye hukusalitiwa!

Utakapokwisha kuharibu,

utaharibiwa;

utakapokwisha kusaliti,

utasalitiwa.

2 EeBwana, uturehemu,

tunakutamani.

Uwe nguvu yetu kila asubuhi

na wokovu wetu wakati wa taabu.

3 Kwa ngurumo ya sauti yako, mataifa yanakimbia;

unapoinuka, mataifa hutawanyika.

4 Mateka yenu, enyi mataifa, yamevunwa kama vile wafanyavyo madumadu,

kama kundi la nzige watu huvamia juu yake.

5 Bwanaametukuka, kwa kuwa anakaa mahali palipoinuka,

ataijaza Sayuni kwa haki na uadilifu.

6 Atakuwa msingi ulio imara kwa wakati wenu,

ghala za wokovu tele, hekima na maarifa;

kumchaBwanani ufunguo wa hazina hii.

7 Angalia, watu wake mashujaa wanapiga kelele kwa nguvu barabarani,

wajumbe wa amani wanalia kwa uchungu.

8 Njia kuu zimeachwa,

hakuna wasafiri barabarani.

Mkataba umevunjika,

mashahidi wake wamedharauliwa,

hakuna yeyote anayeheshimiwa.

9 Ardhi inaombolezana kuchakaa,

Lebanoni imeaibika na kunyauka,

Sharoni ni kama Araba,

nayo Bashani na Karmeli

wanapukutisha majani yao.

10 “Sasa nitainuka,” asemaBwana.

“Sasa nitatukuzwa;

sasa nitainuliwa juu.

11 Mlichukua mimba ya makapi,

mkazaa mabua,

pumzi yenu ni moto uwateketezao.

12 Mataifa yatachomwa kama ichomwavyo chokaa,

kama vichaka vya miiba vilivyokatwa ndivyo watakavyochomwa.”

13 Ninyi mlio mbali sana, sikieni lile nililofanya;

ninyi mlio karibu, tambueni uweza wangu!

14 Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu,

kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu:

“Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao?

Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?”

15 Yeye aendaye kwa uadilifu

na kusema lililo haki,

yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma

na kuizuia mikono yake isipokee rushwa,

yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji,

na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu:

16 huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu,

ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani.

Atapewa mkate wake,

na maji yake hayatakoma.

17 Macho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake

na kuiona nchi inayoenea mbali.

18 Katika mawazo yenu mtaifikiria hofu iliyopita:

“Yuko wapi yule afisa mkuu?

Yuko wapi yule aliyechukua ushuru?

Yuko wapi afisa msimamizi wa minara?”

19 Hutawaona tena wale watu wenye kiburi,

wale watu wenye usemi wa mafumbo,

wenye lugha ngeni, isiyoeleweka.

20 Mtazame Sayuni, mji wa sikukuu zetu;

macho yenu yatauona Yerusalemu,

mahali pa amani pa kuishi, hema ambalo halitaondolewa,

nguzo zake hazitangʼolewa kamwe,

wala hakuna kamba yake yoyote itakayokatika.

21 HukoBwanaatakuwa Mwenye Nguvu wetu.

Patakuwa kama mahali pa mito mipana na vijito.

Hakuna jahazi lenye makasia litakalopita huko,

wala hakuna meli yenye nguvu itakayopita huko.

22 Kwa kuwaBwanani mwamuzi wetu,

Bwanandiye mtoa sheria wetu,

Bwanani mfalme wetu,

yeye ndiye atakayetuokoa.

23 Kamba zenu za merikebu zimelegea:

Mlingoti haukusimama imara,

nalo tanga halikukunjuliwa.

Wingi wa mateka yatagawanywa,

hata yeye aliye mlemavu atachukua nyara.

24 Hakuna yeyote aishiye Sayuni atakayesema, “Mimi ni mgonjwa”;

nazo dhambi za wale waishio humo zitasamehewa.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/33-266cf71af09405eec759a6e358662e17.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 34

Hukumu Dhidi Ya Mataifa

1 Njooni karibu, enyi mataifa, nanyi msikilize;

sikilizeni kwa makini,

enyi kabila za watu!

Dunia na isikie, navyo vyote vilivyo ndani yake,

ulimwengu na vyote vitokavyo ndani yake!

2 Bwanaameyakasirikia mataifa yote;

ghadhabu yake ni juu ya majeshi yao yote.

Atawaangamiza kabisa,

atawatia mikononi mwa wachinjaji.

3 Waliouawa watatupwa nje,

maiti zao zitatoa uvundo,

milima itatota kwa damu zao.

4 Nyota zote za mbinguni zitayeyuka

na anga litasokotwa kama kitabu,

jeshi lote la angani litaanguka

kama majani yaliyonyauka kutoka kwenye mzabibu,

kama tini iliyonyauka kutoka kwenye mtini.

5 Upanga wangu umekunywa na kushiba huko mbinguni,

tazama, unashuka katika hukumu juu ya Edomu,

wale watu ambao nimeshawahukumu,

kuwaangamiza kabisa.

6 Upanga waBwanaumeoga katika damu,

umefunikwa na mafuta ya nyama:

damu ya kondoo na mbuzi,

mafuta kutoka figo za kondoo dume.

Kwa maanaBwanaana dhabihu huko Bosra,

na machinjo makuu huko Edomu.

7 Nyati wataanguka pamoja nao,

ndama waume na mafahali wakubwa.

Nchi yao italowana kwa damu,

nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama.

8 Kwa sababuBwanaanayo siku ya kulipiza kisasi,

mwaka wa malipo,

siku ya kushindania shauri la Sayuni.

9 Vijito vya Edomu vitageuka kuwa lami,

mavumbi yake yatakuwa kiberiti kiunguzacho,

nchi yake itakuwa lami iwakayo!

10 Haitazimishwa usiku wala mchana,

moshi wake utapaa juu milele.

Kutoka kizazi hadi kizazi itakuwa ukiwa,

hakuna mtu yeyote atakayepita huko tena.

11 Bundi wa jangwani na bundi mwenye sauti nyembamba wataimiliki,

bundi wakubwa na kunguru wataweka viota humo.

Mungu atanyoosha juu ya Edomu

kamba ya kupimia ya machafuko matupu,

na timazi ya ukiwa.

12 Watu wake wa kuheshimiwa hawatakuwa na chochote

kitakachoitwa ufalme huko,

nao wakuu wao wote watatoweka.

13 Miiba itaenea katika ngome za ndani,

viwawi na michongoma itaota

kwenye ngome zake.

Itakuwa maskani ya mbweha,

makao ya bundi.

14 Viumbe vya jangwani vitakutana na fisi,

nao mbuzi-mwitu watalia wakiitana;

huko viumbe vya usiku vitastarehe pia

na kujitafutia mahali pa kupumzika.

15 Bundi wataweka viota huko na kutaga mayai,

atayaangua na kutunza makinda yake

chini ya uvuli wa mabawa yake;

pia huko vipanga watakusanyika,

kila mmoja na mwenzi wake.

16 Angalieni katika gombo laBwanana msome:

Hakuna hata mmoja katika hawa atakayekosekana,

hakuna hata mmoja atakayemkosa mwenzi wake.

Kwa kuwa ni kinywa chake Mungu kimeagiza,

na Roho wake atawakusanya pamoja.

17 Huwagawia sehemu zao,

mkono wake huwagawanyia kwa kipimo.

Wataimiliki hata milele

na kuishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/34-c881929f04f8be4b62c70e56bce73c70.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 35

Furaha Ya Waliokombolewa

1 Jangwa na nchi kame vitafurahi;

nyika itashangilia na kuchanua maua.

Kama waridi,

2 litachanua maua,

litashangilia sana na kupaza sauti kwa furaha.

Litapewa utukufu wa Lebanoni,

fahari ya Karmeli na Sharoni;

wataona utukufu waBwana,

fahari ya Mungu wetu.

3 Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu,

yafanyeni imara magoti yaliyolegea,

4 waambieni wale wenye mioyo ya hofu,

“Kuweni hodari, msiogope;

tazama, Mungu wenu atakuja,

pamoja na malipo ya Mungu,

atakuja na kuwaokoa ninyi.”

5 Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa

na masikio ya viziwi yatazibuliwa.

6 Ndipo kilema atarukaruka kama kulungu,

nao ulimi wa aliye bubu utapaza sauti kwa shangwe.

Maji yatatiririka kwa kasi katika nyika,

na vijito katika jangwa.

7 Mchanga wa moto utakuwa bwawa la maji,

ardhi yenye kiu itabubujika chemchemi.

Maskani ya mbweha walikolala hapo awali

patamea majani, matete na mafunjo.

8 Nako kutakuwa na njia kuu,

nayo itaitwa Njia ya Utakatifu.

Wasio safi hawatapita juu yake;

itakuwa ya wale watembeao katika Njia ile;

yeye asafiriye juu yake,

ajapokuwa mjinga, hatapotea.

9 Huko hakutakuwepo na simba,

wala mnyama mkali hatapita njia hiyo,

wala hawatapatikana humo.

Ila waliokombolewa tu ndio watakaopita huko,

10 waliokombolewa naBwanawatarudi.

Wataingia Sayuni wakiimba;

furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao.

Watapata furaha na shangwe;

huzuni na majonzi vitakimbia.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/35-96b8b13a1ac9d2d57620cc3bb28ea101.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 36

Senakeribu Atishia Yerusalemu

1 Katika mwaka wa kumi na nne wa utawala wa Mfalme Hezekia, Senakeribu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote ya Yuda yenye ngome na kuiteka.

2 Kisha mfalme wa Ashuru akamtuma jemadari wa jeshi pamoja na jeshi kubwa kutoka Lakishi hadi kwa Mfalme Hezekia huko Yerusalemu. Jemadari wa jeshi akasimama kwenye mfereji wa Bwawa la Juu, lililojengwa katika barabara iendayo kwenye Uwanja wa Dobi.

3 Eliakimu mwana wa Hilkia aliyekuwa msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna aliyekuwa katibu, na Yoa mwana wa Asafu mwandishi wakamwendea.

4 Jemadari wa jeshi akawaambia, “Mwambieni Hezekia,

“ ‘Hili ndilo asemalo mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru: Ni wapi unapoweka hili tumaini lako?

5 Unasema mnayo mikakati na nguvu za kijeshi, lakini unasema maneno matupu tu. Je, wewe unamtegemea nani, hata ukaniasi mimi?

6 Tazama sasa, unaitegemea Misri, fimbo ile ya mwanzi uliopasuka, ambayo huuchoma na kuujeruhi mkono wa mtu akiiegemea! Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri, kwa wote wanaomtegemea.

7 Nawe kama ukiniambia, “TunamtumainiaBwanaMungu wetu”: je, siyo yeye ambaye Hezekia aliondoa mahali pake pa juu pa kuabudia miungu na madhabahu zake, akiwaambia Yuda na Yerusalemu, “Ni lazima mwabudu mbele ya madhabahu haya”?

8 “ ‘Njooni sasa, fanyeni mapatano na bwana wangu, mfalme wa Ashuru: Nitakupa farasi elfu mbili, kama unaweza kuwapandisha waendesha farasi juu yao!

9 Utawezaje kumzuia hata afisa mmoja aliye mdogo kati ya maafisa wa bwana wangu, ijapo unategemea Misri kwa magari ya vita na wapanda farasi?

10 Zaidi ya hayo, je, nimekuja kushambulia na kuangamiza nchi hii bilaBwana?Bwanamwenyewe ndiye aliniambia niishambulie nchi hii na kuiangamiza.’ ”

11 Ndipo Eliakimu, Shebna na Yoa wakamwambia yule jemadari wa jeshi, “Tafadhali zungumza na watumishi wako kwa lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaifahamu. Usiseme nasi kwa Kiebrania watu walioko juu ya ukuta wakiwa wanasikia.”

12 Lakini yule jemadari wa jeshi akajibu, “Je, bwana wangu amenituma kutoa ujumbe huu kwa bwana wenu na kwenu tu? Je, hakunituma pia kwa watu walioketi ukutani, ambao, kama ninyi, itawabidi kula mavi yao na kunywa mikojo yao wenyewe?”

13 Kisha yule jemadari wa jeshi akasimama na kuita kwa lugha ya Kiebrania, akasema: “Sikieni maneno ya mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru!

14 Hili ndilo asemalo mfalme: Msikubali Hezekia awadanganye. Hawezi kuwaokoa!

15 Msikubali Hezekia awashawishi kumtumainiBwanakwa kuwaambia, ‘HakikaBwanaatatuokoa. Mji huu hautaangukia mikononi mwa mfalme wa Ashuru.’

16 “Msimsikilize Hezekia. Hili ndilo mfalme wa Ashuru asemalo: Fanyeni amani nami na mje kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka kwa mzabibu wake na mtini wake mwenyewe, na kunywa maji kutoka kisima chake mwenyewe,

17 mpaka nije nikawapeleke katika nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai mpya, nchi ya mkate na ya mashamba ya mizabibu.

18 “Msikubali Hezekia awapotoshe asemapo, ‘Bwanaatatuokoa.’ Je, yuko mungu wa taifa lolote aliyewahi kuokoa nchi yake kutoka mkononi mwa mfalme wa Ashuru?

19 Iko wapi miungu ya Hamathi na ya Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu? Je, imeokoa Samaria kutoka mkononi mwangu?

20 Ni yupi miongoni mwa miungu yote ya nchi hizi ameweza kuokoa nchi yake mkononi mwangu? Inawezekanaje basiBwanaaiokoe Yerusalemu mkononi mwangu?”

21 Lakini wale watu wakakaa kimya, wala hawakujibu lolote, kwa kuwa mfalme alikuwa amewaamuru, “Msimjibu lolote.”

22 Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia msimamizi wa jumba la kifalme, Shebna katibu, na Yoa mwana wa Asafu, mwandishi wakamwendea Hezekia, nguo zao zikiwa zimeraruliwa, na kumwambia yale jemadari wa jeshi aliyoyasema.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/36-86f666f221ff9e6fa78ee36635bd0d1b.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 37

Kuokolewa Kwa Yerusalemu Kunatabiriwa

1 Mfalme Hezekia aliposikia haya, akararua nguo zake na kuvaa nguo ya gunia, naye akaenda katika Hekalu laBwana.

2 Akawatuma Eliakimu msimamizi wa nyumba ya mfalme, Shebna mwandishi, na viongozi wa makuhani, wote wakiwa wamevaa nguo za magunia, waende kwa nabii Isaya mwana wa Amozi.

3 Wakamwambia, “Hili ndilo asemalo Hezekia: Siku hii ni siku ya dhiki, ya kukaripiwa na ya aibu, kama wakati watoto wanapofikia karibu kuzaliwa na kumbe hakuna nguvu ya kuwazaa.

4 YamkiniBwana, Mungu wako atayasikia maneno ya jemadari wa jeshi, ambaye bwana wake, mfalme wa Ashuru, amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, tena kwamba atamkemea kwa maneno ambayoBwana, Mungu wako ameyasikia. Kwa hiyo omba kwa ajili ya mabaki ambao bado wako.”

5 Maafisa wa Mfalme Hezekia walipofika kwa Isaya,

6 Isaya akawaambia, “Mwambieni bwana wenu, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Usiogope kwa hayo uliyoyasikia, yale maneno ambayo watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana nayo.

7 Sikiliza! Nitatia roho fulani ndani yake ili kwamba atakaposikia taarifa fulani, atarudi nchi yake mwenyewe, nami huko nitafanya auawe kwa upanga.’ ”

8 Jemadari wa jeshi aliposikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi, alirudi, akamkuta mfalme akipigana na Libna.

9 Basi Senakeribu akapata taarifa kwamba Tirhaka, Mkushi mfalme wa Misri, alikuwa anaenda kupigana naye. Aliposikia jambo hili akatuma wajumbe kwa Hezekia na neno hili:

10 “Mwambieni Hezekia mfalme wa Yuda: Usikubali huyo Mungu unayemtumainia akudanganye wakati anaposema, ‘Yerusalemu haitatiwa mkononi mwa mfalme wa Ashuru.’

11 Hakika umesikia yale ambayo wafalme wa Ashuru wametenda kwa nchi zote, wakiwaangamiza kabisa. Je, wewe utaokolewa?

12 Je, miungu ya mataifa ambayo yaliangamizwa na baba zangu iliweza kuwaokoa? Yaani miungu ya Gozani, Harani, Resefu, na ya watu wa Edeni waliokuwa Telasari?

13 Yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme wa Arpadi, mfalme wa mji wa Sefarvaimu, au wa Hena au wa Iva?”

Maombi Ya Hezekia

14 Hezekia akapokea barua kutoka kwa wale wajumbe naye akaisoma. Kisha akapanda katika Hekalu laBwana, akaikunjua mbele zaBwana.

15 Naye Hezekia akamwombaBwanaakisema:

16 “EeBwanaMwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya kiti cha enzi kati ya makerubi, wewe peke yako ndiwe Mungu juu ya falme zote za dunia. Wewe umeumba mbingu na nchi.

17 Tega sikio, EeBwana, usikie; fungua macho yako, EeBwana, uone; sikiliza maneno yote ambayo Senakeribu ametuma kumtukana Mungu aliye hai.

18 “Ni kweli, EeBwana, kwamba wafalme wa Ashuru wameyaangamiza mataifa haya yote pamoja na nchi zao.

19 Wameitupa miungu yao kwenye moto na kuiangamiza, kwa kuwa haikuwa miungu, bali miti na mawe tu, iliyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.

20 Sasa basi, EeBwanaMungu wetu, tuokoe kutoka mkononi mwake, ili kwamba falme zote duniani zipate kujua kwamba wewe peke yako, EeBwana, ndiwe Mungu.”

Kuanguka Kwa Senakeribu

21 Kisha Isaya mwana wa Amozi akapeleka ujumbe kwa Hezekia, akasema: “Hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa Israeli: Kwa sababu umeniomba kuhusu Senakeribu mfalme wa Ashuru,

22 hili ndilo neno ambaloBwanaamelisema dhidi yake:

“Bikira binti Sayuni anakudharau na kukudhihaki.

Binti Yerusalemu anatikisa kichwa chake unapokimbia.

23 Ni nani uliyemtukana na kumkufuru?

Ni nani uliyeinua sauti yako dhidi yake,

na kumwinulia macho yako kwa kiburi?

Ni dhidi ya yule Aliye Mtakatifu wa Israeli!

24 Kupitia kwa wajumbe wako

umelundika matukano juu ya Bwana.

Nawe umesema,

‘Kwa magari yangu mengi ya vita,

nimepanda juu ya vilele vya milima,

vilele vya juu sana katika Lebanoni.

Nami nimeiangusha mierezi yake mirefu,

misunobari yake iliyo bora sana.

Nimefikia sehemu zake zilizoinuka juu sana,

misitu yake iliyo mizuri sana.

25 Nimechimba visima katika nchi za kigeni

na kunywa maji yake.

Kwa nyayo za miguu yangu

nimekausha vijito vyote vya Misri.’

26 “Je, hujasikia?

Zamani sana niliamuru hili.

Siku za kale nilipanga hili;

sasa nimelifanya litokee,

kwamba umegeuza miji yenye ngome

kuwa malundo ya mawe.

27 Watu wa miji hiyo wameishiwa nguvu,

wanavunjika mioyo na kuaibishwa.

Wao ni kama mimea katika shamba,

kama machipukizi mororo ya kijani,

kama majani yachipuayo juu ya paa la nyumba,

ambayo hukauka kabla ya kukua.

28 “Lakini ninajua mahali ukaapo,

kutoka kwako na kuingia kwako,

na jinsi unavyoghadhibika dhidi yangu.

29 Kwa sababu unaghadhibika na ufidhuli dhidi yangu,

na kwa sababu ufidhuli wako umefika masikioni mwangu,

nitaweka ndoana yangu puani mwako

na hatamu yangu kinywani mwako,

nami nitakufanya urudi kwa njia ile uliyoijia.

30 “Hii ndiyo itakuwa ishara kwako, ee Hezekia:

“Mwaka huu utakula kile kiotacho chenyewe,

na mwaka wa pili utakula kutoka machipukizi yake.

Lakini katika mwaka wa tatu panda na uvune,

panda mashamba ya mizabibu na ule matunda yake.

31 Mara nyingine tena mabaki ya nyumba ya Yuda

wataeneza mizizi chini na kuzaa matunda juu.

32 Kwa kuwa kutoka Yerusalemu watakuja mabaki,

na kutoka Mlima Sayuni kundi la walionusurika.

Wivu waBwanaMwenye Nguvu Zote,

ndio utatimiza jambo hili.

33 “Kwa hiyo hili ndilo asemaloBwanakuhusu mfalme wa Ashuru:

“Hataingia katika mji huu

wala hatapiga mshale hapa.

Hatakuja mbele yake na ngao

wala kupanga majeshi kuuzingira.

34 Kwa njia ile aliyoijia ndiyo atakayorudi;

hataingia katika mji huu,”

asemaBwana.

35 “Nitaulinda mji huu na kuuokoa,

kwa ajili yangu mwenyewe,

na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu!”

36 Ndipo malaika waBwanaakaenda, akawaua wanajeshi 185,000 katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali!

37 Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akavunja kambi na kuondoka. Akarudi Ninawi na kukaa huko.

38 Siku moja, alipokuwa akiabudu katika hekalu la mungu wake Nisroki, wanawe Adrameleki na Shareza wakamuua kwa upanga, nao wakakimbilia nchi ya Ararati. Naye Esar-Hadoni mwanawe akawa mfalme badala yake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/37-d4d0dc7573517cdf553c345d2888fe39.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 38

Kuugua Kwa Mfalme Hezekia

1 Katika siku hizo Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemaloBwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”

2 Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwombaBwana:

3 “EeBwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Naye Hezekia akalia kwa uchungu.

4 Ndipo neno laBwanalikamjia Isaya, kusema:

5 “Nenda ukamwambie Hezekia, ‘Hili ndilo asemaloBwana, Mungu wa baba yako Daudi: Nimeyasikia maombi yako na nimeona machozi yako. Nitakuongezea miaka kumi na mitano katika maisha yako.

6 Nami nitakuokoa wewe pamoja na mji huu mkononi mwa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu.

7 “ ‘Hii ndiyo ishara yaBwanakwako ya kwambaBwanaatafanya kile alichoahidi:

8 Nitafanya kivuli cha jua kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi kirudi nyuma madaraja kumi.’ ” Hivyo jua likarudi nyuma madaraja kumi ambayo lilikuwa limeshuka.

9 Maandiko ya Hezekia mfalme wa Yuda baada ya kuugua kwake na kupona:

10 Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu,

je, ni lazima nipite katika malango ya mauti,

na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?”

11 Nilisema, “Sitamwona tenaBwana,

Bwanakatika nchi ya walio hai,

wala sitamtazama tena mwanadamu,

wala kuwa na wale ambao sasa wanakaa katika ulimwengu huu.

12 Kama hema la mchunga mifugo,

nyumba yangu imebomolewa na kutwaliwa kutoka kwangu.

Kama mfumaji nimevingirisha maisha yangu,

naye amenikatilia mbali kutoka kitanda cha mfumi.

Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

13 Nilingoja kwa uvumilivu hadi mapambazuko,

lakini alivunja mifupa yangu yote kama simba.

Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

14 Nililia kama mbayuwayu au korongo,

niliomboleza kama hua aombolezaye.

Macho yangu yalififia nilipotazama mbinguni.

Ee Bwana, ninataabika, njoo unisaidie!”

15 Lakini niseme nini?

Amesema nami, naye yeye mwenyewe amelitenda hili.

Nitatembea kwa unyenyekevu

katika miaka yangu yote

kwa sababu ya haya maumivu makali

ya nafsi yangu.

16 Bwana, kwa mambo kama haya watu huishi,

nayo roho yangu hupata uzima katika hayo pia.

Uliniponya

na kuniacha niishi.

17 Hakika ilikuwa ya faida yangu

ndiyo maana nikapata maumivu makali.

Katika upendo wako ukaniokoa

kutoka shimo la uharibifu;

umeziweka dhambi zangu zote

nyuma yako.

18 Kwa maana kaburihaliwezi kukusifu,

mauti haiwezi kuimba sifa zako;

wale washukao chini shimoni

hawawezi kuutarajia uaminifu wako.

19 Walio hai, walio hai: hao wanakusifu,

kama ninavyofanya leo.

Baba huwaambia watoto wao

habari za uaminifu wako.

20 Bwanaataniokoa,

nasi tutaimba kwa vyombo vya nyuzi

siku zote za maisha yetu

katika Hekalu laBwana.

21 Isaya alikuwa amesema, “Tengenezeni dawa ya kubandika ya tini, mweke juu ya jipu, naye atapona.”

22 Hezekia alikuwa ameuliza, “Kutakuwa na ishara gani kwamba nitapanda kwenda Hekalu laBwana?”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/38-e25042c08218db7f0aab76070ad3053b.mp3?version_id=1627—

Categories
Isaya

Isaya 39

Wajumbe Kutoka Babeli

1 Wakati huo Merodaki-Baladani, mwana wa Baladani mfalme wa Babeli, akamtumia Hezekia barua na zawadi, kwa sababu alikuwa amesikia habari za kuugua na kupona kwake.

2 Hezekia akawapokea wale wajumbe kwa furaha na kuwaonyesha vitu vile vilivyokuwa katika ghala zake: yaani fedha, dhahabu, vikolezo na mafuta safi, ghala la silaha lote, na kila kitu kilichokuwa katika hazina zake. Hapakuwa na kitu chochote katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonyesha.

3 Ndipo nabii Isaya akaenda kwa Mfalme Hezekia na kumuuliza, “Watu hao walisema nini, na wametoka wapi?”

Hezekia akamjibu, “Wametoka nchi ya mbali. Walikuja kwangu kutoka Babeli.”

4 Nabii akauliza, “Waliona nini katika jumba lako la kifalme?”

Hezekia akajibu, “Waliona kila kitu katika jumba langu la kifalme. Hakuna kitu chochote katika hazina yangu ambacho sikuwaonyesha.”

5 Ndipo Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno laBwanaMwenye Nguvu Zote:

6 Hakika wakati unakuja ambapo vitu vyote katika jumba lako la kifalme, na vyote ambavyo baba zako waliweka akiba mpaka siku hii, vitachukuliwa kwenda Babeli. Hakuna chochote kitakachosalia, asemaBwana.

7 Nao baadhi ya wazao wako, nyama yako na damu yako mwenyewe watakaozaliwa kwako, watachukuliwa mbali, nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli.”

8 Hezekia akamjibu Isaya, “Neno laBwanaulilosema ni jema.” Kwa kuwa alifikiri, “Patakuwepo amani na usalama wakati wa uhai wangu.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/39-e218a60b2018a0ff6536e76ed482bc99.mp3?version_id=1627—