Categories
Hesabu

Hesabu 30

Nadhiri

1 Mose akawaambia viongozi wa makabila ya Israeli: “Hili ndiloBwanaanaloagiza:

2 Mwanaume awekapo nadhiri kwaBwana, au anapoapa kujifunga kwa ahadi, kamwe asitangue neno lake, bali ni lazima afanye kila kitu alichosema.

3 “Wakati mwanamwali anayeishi bado nyumbani kwa baba yake atakapoweka nadhiri kwaBwana, ama amejifunga mwenyewe kwa ahadi,

4 na baba yake akasikia kuhusu nadhiri au ahadi yake lakini asimwambie lolote, ndipo nadhiri zake zote na kila ahadi aliyoiweka na kujifunga kwayo itathibitika.

5 Lakini kama baba yake akimkataza wakati anapoisikia, hakuna nadhiri wala ahadi yake yoyote aliyojifunga kwayo itakayosimama;Bwanaatamweka huru huyo mwanamwali kwa sababu baba yake amemkataza.

6 “Ikiwa ataolewa baada ya kuweka nadhiri au baada ya midomo yake kutamka ahadi fulani bila kufikiri akawa amejifunga hivyo,

7 na mume wake akasikia habari hiyo asimwambie neno lolote, ndipo nadhiri zake ama ahadi zake ambazo alikuwa amejifunga nazo zitathibitika.

8 Lakini ikiwa mume wake atamkataza atakaposikia kuhusu hilo, atakuwa ametangua nadhiri ambazo zilikuwa zimemfunga mkewe, ama ahadi aliyotamka pasipo kufikiri ambayo amejifunga kwayo, nayeBwanaatamweka huru yule mwanamke.

9 “Nadhiri yoyote ama patano ambalo limefanywa na mjane ama mwanamke aliyeachwa vitakuwa vimemfunga.

10 “Ikiwa mwanamke anayeishi na mumewe ataweka nadhiri ama kujifunga mwenyewe kwa ahadi chini ya kiapo,

11 na mumewe akasikia kuhusu jambo hili lakini asimwambie lolote wala hakumkataza, ndipo viapo vyake vyote au ahadi zinazomfunga zitakapothibitika.

12 Lakini ikiwa mumewe atabatilisha nadhiri hizo baada ya kuzisikia, basi hakuna nadhiri au ahadi zozote alizoziweka kwa midomo yake zitakazothibitika. Mumewe atakuwa amezibatilisha, naBwanaatamweka huru yule mwanamke.

13 Mumewe anaweza kuthibitisha au kutangua nadhiri yoyote anayoweka, au ahadi yoyote aliyoweka kwa kuapa ili kujikana mwenyewe.

14 Lakini ikiwa mumewe hasemi lolote kwake kuhusu jambo hilo siku baada ya siku, basi mumewe atakuwa amethibitisha nadhiri zote, na ahadi zote zinazomfunga mkewe. Anavithibitisha kwa kutokusema lolote kwa mkewe anapoyasikia hayo.

15 Hata hivyo, ikiwa mumewe atavibatilisha baada ya kusikia hayo, basi atawajibika kwa hatia ya mkewe.”

16 Haya ndiyo masharti ambayoBwanaalimpa Mose kuhusu mahusiano kati ya mtu na mkewe, na kati ya baba na binti yake ambaye bado anaishi nyumbani kwa baba yake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/30-7e5cf57541a5082412b8624462d26a62.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 31

Kulipiza Kisasi Juu Ya Wamidiani

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Uwalipize kisasi Wamidiani kwa ajili ya Waisraeli. Halafu baada ya hayo, utakufa.”

3 Kwa hiyo Mose akawaambia watu, “Waandaeni baadhi ya wanaume wenu waende vitani kupigana na Wamidiani ili wawalipize kisasi chaBwana.

4 Peleka wanaume 1,000 vitani kutoka kila kabila la Israeli.”

5 Kwa hiyo waliandaliwa wanaume 12,000 kwa vita, wanaume 1,000 kutoka kila kabila, walitolewa kutoka koo za Israeli.

6 Mose aliwatuma vitani, watu 1,000 kutoka kila kabila, pamoja na Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, ambaye alichukua vyombo vya mahali patakatifu na tarumbeta za kuashiria.

7 Walipigana dhidi ya Wamidiani, kamaBwanaalivyomwagiza Mose, nao waliua kila mwanaume.

8 Miongoni mwa watu waliouawa walikuwepo wafalme watano wa Midiani, nao ni Evi, Rekemu, Suri, Huri na Reba. Vilevile walimuua Balaamu mwana wa Beori kwa upanga.

9 Waisraeli waliwateka wanawake wa Kimidiani pamoja na watoto wao na walichukua makundi ya ngʼombe, kondoo na mali zao kama nyara.

10 Walichoma moto miji yote ambayo Wamidiani walikuwa wanaishi, pamoja na kambi zao zote.

11 Walichukua nyara zote na mateka, pamoja na watu na wanyama,

12 nao waliwaleta wafungwa mateka na nyara kwa Mose na kwa kuhani Eleazari, nao Waisraeli walikusanyika kwenye kambi zao katika tambarare za nchi ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko.

13 Mose, kuhani Eleazari na viongozi wote wa jumuiya wakatoka kuwalaki nje ya kambi.

14 Mose aliwakasirikia maafisa wa jeshi, yaani hao wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, ambao walirudi kutoka vitani.

15 Mose akawauliza, “Je, mmewaacha wanawake wote hai?”

16 “Wanawake hao ndio waliofuata ushauri wa Balaamu, nao ndio waliowasababisha Waisraeli wamwasiBwanakwa kile kilichotokea kule Peori, na kwa hiyo pigo liliwapata watu waBwana.

17 Sasa waue wavulana wote. Pia muue kila mwanamke ambaye alikwisha fanya tendo la ndoa,

18 lakini mwacheni hai kwa ajili yenu kila msichana ambaye kamwe hajawahi kuzini na mwanaume.

19 “Ninyi nyote ambao mmeua mtu yeyote au kumgusa mtu yeyote ambaye ameuawa, lazima mkae nje ya kambi kwa muda wa siku saba. Katika siku ya tatu na ya saba lazima mjitakase wenyewe pamoja na wafungwa wenu.

20 Takaseni kila vazi pamoja na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi, kwa singa za mbuzi au kwa mti.”

21 Kisha kuhani Eleazari aliwaambia askari waliokuwa wamekwenda vitani, “Haya ndiyo matakwa ya sheria ambayoBwanaalimpa Mose:

22 Dhahabu, fedha, shaba, chuma, bati, risasi,

23 na kitu kingine chochote ambacho kinaweza kuhimili moto lazima mkipitishe kwenye moto, kisha kitakuwa safi. Lakini ni lazima pia kitakaswe kwa maji ya utakaso. Kitu chochote kisichoweza kuhimili moto lazima kipitishwe kwenye yale maji ya utakaso.

24 Katika siku ya saba fueni nguo zenu, nanyi mtakuwa safi. Kisha mtaweza kuingia kambini.”

Kugawanya Mateka

25 Bwanaakamwambia Mose,

26 “Wewe na kuhani Eleazari pamoja na viongozi wa jamaa ya jumuiya mtahesabu watu wote na wanyama ambao walitekwa.

27 Gawanyeni hizo nyara kati ya askari ambao walishiriki katika vita na kwa jumuiya.

28 Kutoka fungu la wale waliokwenda kupigana vitani, tenga kama ushuru kwa ajili yaBwanakitu kimoja kati ya kila mia tano, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo au mbuzi.

29 Chukua ushuru huu kutoka fungu lao, umpe kuhani Eleazari kama sehemu yaBwana.

30 Kutoka fungu la Waisraeli, chukua kitu kimoja kati ya kila hamsini, ikiwa ni wanadamu, ngʼombe, punda, kondoo, mbuzi au wanyama wengine. Hivyo uwape Walawi, ambao wanawajibika kutunza Maskani yaBwana.”

31 Kwa hiyo Mose na kuhani Eleazari wakafanya kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

32 Nyara zilizobaki kutoka mateka ambayo askari walichukua ni kondoo 675,000,

33 ngʼombe 72,000,

34 punda 61,000,

35 na wanawake 32,000 ambao hawakumjua mume kwa kufanya tendo la ndoa.

36 Nusu ya fungu la wale waliokwenda kupigana vitani lilikuwa:

Kondoo 337,500

37 ambayo ushuru kwa ajili yaBwanailikuwa kondoo 675;

38 ngʼombe 36,000 ambao ushuru kwa ajili yaBwanaulikuwa ngʼombe 72;

39 punda 30,500 ambao ushuru kwa ajili yaBwanaulikuwa punda 61;

40 Watu 16,000 ambao ushuru kwa ajili yaBwanaulikuwa watu 32.

41 Mose alimpa kuhani Eleazari ushuru kama sehemu yaBwana, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

42 Ile nusu iliyokuwa ya Waisraeli, ambayo Mose aliitenga kutoka kwa ile ya watu waliokwenda vitani,

43 nusu iliyokuwa ya jumuiya, ilikuwa kondoo 337,500,

44 ngʼombe 36,000,

45 punda 30,500,

46 na wanadamu 16,000.

47 Kutoka hiyo nusu iliyokuwa ya Waisraeli, Mose alichagua moja kati ya kila hamsini ya wanadamu na wanyama, kamaBwanaalivyomwagiza, naye aliwapa Walawi, ambao waliwajibika kutunza Maskani yaBwana.

48 Kisha maafisa waliokuwa juu ya vikosi vya jeshi, wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, walimwendea Mose

49 na kumwambia, “Watumishi wako wamehesabu askari walio chini ya amri yetu na hakuna hata mmoja aliyekosekana.

50 Kwa hiyo tumeleta kama sadaka kwaBwanavyombo vya dhahabu kila mmoja wetu alivyopata, yaani vikuku, bangili, pete za muhuri, vipuli na mikufu, ili kufanya upatanisho kwa ajili yetu mbele zaBwana.”

51 Mose na kuhani Eleazari wakapokea kutoka kwao dhahabu, yaani vyombo vyote vilivyonakshiwa.

52 Dhahabu yote kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia ambavyo Mose na kuhani Eleazari walimleteaBwanakama zawadi ilikuwa shekeli 16,750

53 Kila askari alikuwa amejichukulia nyara zake binafsi.

54 Mose na kuhani Eleazari walipokea dhahabu kutoka kwa wakuu wa jeshi wa maelfu na wakuu wa jeshi wa mamia, wakazileta katika Hema la Kukutania kama ukumbusho kwa Waisraeli mbele zaBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/31-eadb759677f6f7a0016d2908c1fe3554.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 32

Makabila Ngʼambo Ya Yordani

1 Kabila la Wareubeni na Wagadi, waliokuwa na makundi makubwa ya ngʼombe, kondoo na mbuzi, waliona kuwa nchi ya Yazeri na nchi ya Gileadi ni nzuri kwa mifugo.

2 Hivyo walimjia Mose, na kuhani Eleazari na viongozi wa jumuiya, na kuwaambia,

3 “Atarothi, Diboni, Yazeri, Nimra, Heshboni, Eleale, Sebamu, Nebo na Beoni,

4 nchi ambayoBwanaameishinda mbele ya wana wa Israeli, inafaa kwa mifugo, nao watumishi wako wana mifugo.

5 Kama tumepata kibali mbele ya macho yako, nchi hii na ipewe watumishi wako kama milki yetu. Usitufanye tuvuke Yordani.”

6 Mose akawaambia Wagadi na Wareubeni, “Je, watu wa nchi yenu watakwenda vitani wakati ninyi mmeketi hapa?

7 Kwa nini mmewakatisha Waisraeli tamaa wasivuke katika nchi ambayoBwanaamewapa?

8 Hivi ndivyo baba zenu walivyofanya wakati nilipowatuma kutoka Kadesh-Barnea kuipeleleza nchi.

9 Baada ya kufika kwenye Bonde la Eshkoli na kuitazama nchi, waliwakatisha tamaa Waisraeli wasiingie katika nchi ambayoBwanaalikuwa amewapa.

10 Siku ile hasira yaBwanailiwaka naye akaapa kiapo hiki:

11 ‘Kwa kuwa hawakunifuata kwa moyo wote, hakuna mtu yeyote mwenye miaka ishirini au zaidi ambaye alikuja kutoka Misri atakayeona nchi niliyoahidi kwa kiapo kwa Abrahamu, Isaki na Yakobo;

12 hakuna hata mmoja isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni, kwa sababu walimfuataBwanakwa moyo wote.’

13 Hasira yaBwanailiwaka dhidi ya Waisraeli na akawafanya watangetange katika jangwa kwa miaka arobaini, mpaka kizazi chote cha wale waliofanya maovu mbele yake kimeangamia.

14 “Nanyi mko hapa, uzao wa wenye dhambi, mkisimamia mahali pa baba zenu na mkimfanyaBwanakuwakasirikia Waisraeli hata zaidi.

15 Kama mkigeuka na mkiacha kumfuata, atawaacha tena watu hawa wote jangwani, na mtakuwa sababu ya maangamizi yao.”

16 Ndipo wakamjia Mose na kumwambia, “Tungalitaka kujenga mazizi hapa kwa ajili ya mifugo yetu na miji kwa ajili ya wanawake wetu na watoto.

17 Lakini sisi tuko tayari kuchukua silaha zetu na kutangulia mbele ya Waisraeli mpaka tutakapowaleta mahali pao. Wakati huo wanawake wetu na watoto wataishi katika miji yenye ngome, kwa ajili ya ulinzi dhidi ya wenyeji wa nchi.

18 Hatutarudi nyumbani mwetu mpaka kila Mwisraeli apokee urithi wake.

19 Hatutapokea urithi wowote pamoja nao ngʼambo ya Yordani, kwa sababu urithi wetu umekuja kwetu upande wa mashariki ya Yordani.”

20 Kisha Mose akawaambia, “Kama mtafanya jambo hili, kama mtajivika silaha mbele zaBwanakwa ajili ya vita,

21 na kama ninyi nyote mtakwenda mmejivika silaha ngʼambo ya Yordani mbele zaBwanampaka awe amewafukuza adui zake mbele zake,

22 hadi wakati nchi itakapokuwa imeshindwa mbele zaBwana, ndipo mtaweza kurudi na kuwa huru kutoka masharti yenu kwaBwanana Israeli. Nayo nchi hii itakuwa milki yenu mbele zaBwana.

23 “Lakini mkishindwa kufanya hili, mtakuwa mnatenda dhambi dhidi yaBwana; nanyi kuweni na hakika kuwa dhambi yenu itawapata.

24 Jengeni miji kwa ajili ya wanawake na watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya mbuzi na kondoo zenu, lakini fanyeni yale mliyoahidi.”

25 Wagadi na Wareubeni wakamwambia Mose, “Sisi watumishi wako tutafanya kama bwana wetu anavyotuagiza.

26 Watoto na wake zetu, makundi ya mbuzi na kondoo, na makundi ya ngʼombe zetu, watabaki hapa katika miji ya Gileadi.

27 Lakini watumishi wenu, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, watavuka ngʼambo kupigana mbele zaBwana, sawa kama bwana wetu anavyosema.”

28 Kisha Mose akatoa amri kuhusu wao kwa kuhani Eleazari, na Yoshua mwana wa Nuni na viongozi wa jamaa za makabila ya Waisraeli.

29 Mose akawaambia, “Ikiwa Wagadi na Wareubeni, kila mwanaume aliyevaa silaha za vita, atavuka Yordani pamoja nanyi mbele zaBwana, basi wakati mtakapoishinda nchi iliyoko mbele yenu, wapeni nchi ya Gileadi kama milki yao.

30 Lakini kama hawatavuka pamoja nanyi wakiwa wamevaa silaha za vita, lazima wakubali kupokea milki yao pamoja nanyi katika nchi ya Kanaani.”

31 Wagadi na Wareubeni wakajibu, “Watumishi wako watafanya lileBwanaalilosema.

32 Tutavuka mbele zaBwanakuingia Kanaani tukiwa tumevaa silaha za vita, lakini mali tutakayoirithi itakuwa ngʼambo hii ya Yordani.”

33 Kisha Mose akawapa Wagadi, Wareubeni, na nusu ya kabila la Manase mwana wa Yosefu ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, nchi yote pamoja na miji yake, na nchi inayowazunguka.

34 Wagadi wakajenga Diboni, Atarothi, Aroeri,

35 Atroth-Shofani, Yazeri, Yogbeha,

36 Beth-Nimra na Beth-Harani kama miji iliyozungushiwa ngome, tena wakajenga mazizi kwa ajili ya makundi yao ya mbuzi na kondoo.

37 Nao Wareubeni wakajenga upya miji ya Heshboni, Eleale na Kiriathaimu,

38 pia Nebo na Baal-Meoni (majina ya hiyo miji yalibadilishwa) na Sibma. Miji waliyoijenga upya waliipa majina.

39 Wazao wa Makiri mwana wa Manase walikwenda Gileadi, wakaiteka nchi na kuwafukuza Waamori waliokuwa huko.

40 Kwa hiyo Mose akawapa Wamakiri, wazao wa Manase, nchi ya Gileadi, nao wakakaa huko.

41 Yairi, mzao wa Manase, akateka makao yao, akayaita Hawoth-Yairi.

42 Naye Noba akateka Kenathi na makao yaliyoizunguka, akayaita Noba kwa jina lake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/32-b0d63069369cd0d9cd5355dbd4b2c2b8.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 33

Vituo Katika Safari Ya Waisraeli

1 Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Mose na Aroni.

2 Kwa agizo laBwana, Mose aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao:

3 Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote,

4 waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambaoBwanaalikuwa amewaua katikati yao, kwa kuwaBwanaalikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.

5 Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.

6 Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.

7 Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki ya Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.

8 Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.

9 Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.

10 Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.

11 Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.

12 Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.

13 Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.

14 Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.

15 Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.

16 Wakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava.

17 Wakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi.

18 Wakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma.

19 Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi.

20 Wakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna.

21 Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa.

22 Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha.

23 Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi.

24 Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada.

25 Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi.

26 Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi.

27 Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera.

28 Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka.

29 Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona.

30 Wakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi.

31 Wakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yakani.

32 Wakaondoka Bene-Yakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi.

33 Wakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha.

34 Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi huko Abrona.

35 Wakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi.

36 Wakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini.

37 Wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu.

38 Kwa amri yaBwana, kuhani Aroni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri.

39 Aroni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka 123.

40 Mfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja.

41 Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona.

42 Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni.

43 Wakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi.

44 Wakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu.

45 Wakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi.

46 Wakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu.

47 Wakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo.

48 Wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko.

49 Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi mpaka Abel-Shitimu.

50 Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani kuvukia Yeriko,Bwanaakamwambia Mose,

51 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani,

52 wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kuyeyusha chuma, na kupabomoa mahali pao pa ibada.

53 Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki.

54 Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu.

55 “ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi.

56 Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/33-dbbc214f858652d3e7b638193b45b9ad.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 34

Mipaka Ya Kanaani

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Waamuru Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia nchi ya Kanaani, nchi ambayo itagawanywa kwenu kama urithi itakuwa na mipaka ifuatayo:

3 “ ‘Upande wenu wa kusini utajumuisha sehemu ya Jangwa la Sini kufuata mpaka wa Edomu. Upande wa mashariki mpaka wenu wa kusini utaanzia mwisho wa Bahari ya Chumvi,

4 katiza kusini mwa Pito la Akrabimu, endelea mpaka Sini na kwenda kusini ya Kadesh-Barnea. Kisha mpaka huo utaenda hadi Hasar-Adari hadi Azmoni,

5 mahali ambapo utapinda, na kuunganika na Kijito cha Misri na kumalizikia kwenye Bahari ya Kati.

6 “ ‘Mpaka wenu wa magharibi utakuwa Bahari ya Kati. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa magharibi.

7 “ ‘Kwa mpaka wenu wa kaskazini, wekeni alama kuanzia Bahari ya Kati hadi mlima Hori,

8 na kutoka mlima Hori hadi Pito la Hamathi. Kisha mpaka utaenda hadi Sedadi,

9 kuendelea hadi Zifroni, na kuishia Hasar-Enani. Huu utakuwa mpaka wenu upande wa kaskazini.

10 “ ‘Kwa mpaka wenu wa mashariki, wekeni alama kuanzia Hasar-Enani hadi Shefamu.

11 Mpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye miteremko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi.

12 Kisha mpaka utashuka kuelekea Mto Yordani na kuishia katika Bahari ya Chumvi.

“ ‘Hii itakuwa nchi yenu, ikiwa na mipaka yake kila upande.’ ”

13 Mose akawaamuru Waisraeli: “Gawanyeni nchi hii kwa kura kama urithi.Bwanaameagiza kwamba itolewe kwa yale makabila tisa na nusu,

14 kwa sababu jamaa ya kabila la Reubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase wamekwishapokea urithi wao.

15 Haya makabila mawili na nusu wamekwishapokea urithi wao upande wa mashariki wa Yordani ngʼambo ya Yeriko, kuelekea mawio ya jua.”

16 Bwanaakamwambia Mose,

17 “Haya ndiyo majina ya watu ambao watakusaidia kugawanya nchi kama urithi: Eleazari kuhani na Yoshua mwana wa Nuni.

18 Tena uteue kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia kuigawanya nchi.

19 Haya ndiyo majina yao:

“Kalebu mwana wa Yefune,

kutoka kabila la Yuda;

20 Shemueli mwana wa Amihudi,

kutoka kabila la Simeoni;

21 Elidadi mwana wa Kisloni,

kutoka kabila la Benyamini;

22 Buki mwana wa Yogli,

kiongozi kutoka kabila la Dani;

23 Hanieli mwana wa Efodi,

kiongozi kutoka kabila la Manase mwana wa Yosefu;

24 Kemueli mwana wa Shiftani,

kiongozi kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yosefu;

25 Elisafani mwana wa Parnaki,

kiongozi kutoka kabila la Zabuloni;

26 Paltieli mwana wa Azani,

kiongozi kutoka kabila la Isakari;

27 Ahihudi mwana wa Shelomi,

kiongozi kutoka kabila la Asheri;

28 Pedaheli mwana wa Amihudi,

kiongozi kutoka kabila la Naftali.”

29 Hawa ndio watu ambaoBwanaaliamuru wagawanye urithi kwa Waisraeli katika nchi ya Kanaani.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/34-7acd76436f7b19c89a484215882d0836.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 35

Miji Kwa Ajili Ya Walawi

1 Bwanaakamwambia Mose katika nchi tambarare ya Moabu, kando ya Mto Yordani kuvukia Yeriko,

2 “Waagize Waisraeli kuwapa Walawi miji ya kuishi kutoka urithi ambao Waisraeli wataumiliki. Wape maeneo ya malisho kuzunguka hiyo miji.

3 Kisha watakuwa na miji ya kuishi na maeneo ya malisho kwa ajili ya ngʼombe zao, mbuzi, kondoo na mifugo yao mingine yote.

4 “Maeneo ya malisho kuzunguka miji hiyo ambayo mtawapa Walawi yataenea mita 450 kutoka kwenye ukuta wa miji.

5 Nje ya mji, pima mita 900 upande wa mashariki, upande wa kusini mita 900, upande wa magharibi mita 900, na upande wa kaskazini mita 900, na mji utakuwa katikati. Eneo hili litakuwa lao kwa ajili ya malisho.

Miji Ya Makimbilio

6 “Miji sita mtakayowapa Walawi itakuwa ya makimbilio, ambayo mtu anayemuua mwenzake aweza kukimbilia humo. Zaidi ya hiyo, wapeni miji mingine arobaini na miwili.

7 Kwa jumla inawapasa kuwapa Walawi miji arobaini na minane, pamoja na maeneo ya malisho yao.

8 Miji ambayo mtawapa Walawi kutoka nchi ambayo Waisraeli wanamiliki itatolewa kwa uwiano wa urithi wa kila kabila. Chukua miji mingi kutoka lile kabila lenye miji mingi, lakini uchukue miji michache kutoka kwa kabila lile lenye miji michache.”

9 KishaBwanaakamwambia Mose:

10 “Sema na Waisraeli, uwaambie: ‘Mtakapovuka Yordani kuingia Kanaani,

11 chagueni baadhi ya miji iwe miji yenu ya makimbilio, ambayo mtu ambaye ameua mwenzake bila kukusudia aweza kukimbilia humo.

12 Itakuwa mahali pa kukimbilia kutoka mlipiza kisasi, ili kwamba mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji asife kabla ya kujitetea mbele ya mkutano.

13 Miji hii sita mtakayoitoa itakuwa miji yenu ya makimbilio.

14 Mtatoa miji mitatu ngʼambo hii ya Yordani na miji mingine mitatu upande wa Kanaani kama miji ya makimbilio.

15 Miji hii sita itakuwa mahali pa makimbilio kwa ajili ya Waisraeli, wageni na watu wengine wanaoishi katikati yenu, ili kwamba mtu yeyote ambaye ameua mtu mwingine pasipo kukusudia aweze kukimbilia humo.

16 “ ‘Kama mtu akimpiga mwenzake kwa chuma naye mtu huyo akafa, mtu huyo ni muuaji; muuaji sharti atauawa.

17 Au kama mtu analo jiwe mkononi mwake ambalo laweza kuua, naye akampiga mwenzake akafa, yeye ni muuaji; muuaji huyo sharti atauawa.

18 Au kama mtu ana chombo cha mti mkononi mwake ambacho chaweza kuua, naye akampiga mwenzake akafa, yeye ni muuaji; muuaji huyo sharti atauawa.

19 Mlipiza kisasi cha damu atamuua muuaji; wakati akikutana naye, atamuua.

20 Ikiwa mtu ana chuki ya siku nyingi na mwenzake akamsukuma au akamtupia kitu kwa kukusudia naye akafa,

21 au ikiwa katika uadui akampiga ngumi naye akafa, mtu yule sharti atauawa; yeye ni muuaji. Mlipiza kisasi cha damu atamuua muuaji atakapokutana naye.

22 “ ‘Lakini kama mtu akimsukuma mwenziwe ghafula pasipo chuki, au kumtupia kitu pasipo kukusudia,

23 au, pasipo kumwona, akimwangushia jiwe ambalo laweza kumuua naye akafa, basi kwa kuwa hakuwa adui yake naye hakukusudia kumuumiza,

24 kusanyiko lazima liamue kati yake na mlipiza kisasi wa damu kufuatana na sheria hizi.

25 Kusanyiko ni lazima limlinde yule anayeshtakiwa kuua kutoka kwa mlipiza kisasi wa damu, na kumrudisha katika mji wa makimbilio alikokuwa amekimbilia. Lazima akae humo mpaka atakapokufa kuhani mkuu ambaye alikuwa amepakwa mafuta matakatifu.

26 “ ‘Lakini kama mshtakiwa atatoka nje ya mipaka ya mji wa makimbilio ambao amekimbilia,

27 na mlipiza kisasi wa damu akamkuta nje ya mji, mlipiza kisasi wa damu anaweza kumuua mshtakiwa huyo bila kuwa na hatia ya kuua.

28 Mshtakiwa lazima akae katika mji wake wa makimbilio mpaka atakapokufa kuhani mkuu; atarudi tu kwenye mali yake baada ya kifo cha kuhani mkuu.

29 “ ‘Hizi ndizo kanuni za sheria zitakazohitajiwa kwenu na katika vizazi vyenu vijavyo, popote mtakapoishi.

30 “ ‘Yeyote anayeua mtu atauawa kama muuaji ikiwa tu kuna ushuhuda wa mashahidi. Lakini hakuna mtu atakayeuawa kwa ushuhuda wa shahidi mmoja tu.

31 “ ‘Usikubali fidia yoyote ya kuokoa uhai wa muuaji ambaye anastahili kufa. Mtu huyo hakika lazima auawe.

32 “ ‘Usikubali fidia ya mtu yeyote ambaye amekimbilia katika mji wa makimbilio na kumruhusu kurudi kuishi katika nchi yake kabla ya kifo cha kuhani mkuu.

33 “ ‘Msiinajisi nchi mnayoishi. Umwagaji damu hunajisi nchi, na upatanisho hauwezekani kufanyika katika nchi ambayo damu imemwagwa, isipokuwa tu kwa damu ya yule aliyeimwaga damu.

34 Msiinajisi nchi mnayoishi, ambayo nami ninakaa, kwa kuwa Mimi,Bwana, ninakaa katikati ya Waisraeli.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/35-6325f346d85f830fac09ac893a1b97e7.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 36

Urithi Wa Binti Za Selofehadi

1 Viongozi wa jamaa ya ukoo wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase, waliokuwa wametoka katika koo za wazao wa Yosefu, walikuja na kuzungumza mbele ya Mose na viongozi, wakuu wa jamaa ya Waisraeli.

2 Wakasema, “Bwanaalipomwamuru bwana wangu kuwapa Waisraeli nchi kama urithi kwa kura, alikuamuru kutoa urithi wa ndugu yetu Selofehadi kwa binti zake.

3 Sasa ikiwa wataolewa na watu wa makabila mengine ya Kiisraeli, itakuwa kwamba urithi wao utaondolewa kutoka urithi wa mababu zetu na kuongezwa katika urithi wa kabila ambalo dada hao wameolewa. Kwa hiyo sehemu ya urithi tuliyogawiwa itachukuliwa kutoka kwetu.

4 Wakati mwaka wa Yubile kwa Waisraeli utafika, urithi wao utaongezwa kwa lile kabila ambalo wameolewa, na mali yao itaondolewa kutoka urithi wa kabila la mababu zetu.”

5 Ndipo kwa agizo laBwanaMose akatoa amri ifuatayo kwa Waisraeli: “Kile wazao wa kabila la Yosefu wanachosema ni kweli.

6 Hivi ndivyoBwanaanavyoamuru kwa binti za Selofehadi: Wanaweza kuolewa na mtu yeyote wampendaye, mradi tu waolewe miongoni mwa koo za kabila za baba yao.

7 Hakuna urithi katika Israeli utakaohamishwa kutoka kabila moja kwenda kabila jingine, kwa kuwa kila Mwisraeli atatunza ardhi ya kabila lake aliyoirithi kutoka kwa baba zake.

8 Kila binti atakayerithi ardhi katika kabila lolote la Israeli ni lazima aolewe na mtu kutoka kabila na ukoo wa baba yake, ili kila Mwisraeli amiliki urithi wa baba zake.

9 Hakuna urithi uwezao kuhamishwa kutoka kabila moja kwenda kabila jingine, kwa kuwa kila kabila la Israeli litatunza nchi linayorithi.”

10 Kwa hiyo binti za Selofehadi wakafanya kamaBwanaalivyomwamuru Mose.

11 Binti za Selofehadi, ambao ni Mahla, Tirsa, Hogla, Milka na Noa, wakaolewa na waume, wana wa ndugu za baba yao.

12 Waliolewa ndani ya koo za wazao wa Manase mwana wa Yosefu, na urithi wao ukabaki katika ukoo na kabila la baba yao.

13 Haya ndiyo maagizo na masharti ambayoBwanaaliwapa Waisraeli kupitia Mose katika tambarare za Moabu, karibu na Yordani ngʼambo ya Yeriko.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/36-97526d7e64ebf4cf2fca720d17228cb7.mp3?version_id=1627—