Categories
Hesabu

Hesabu 20

Maji Kutoka Kwenye Mwamba

1 Katika mwezi wa kwanza jumuiya yote ya Kiisraeli ilifika kwenye Jangwa la Sini, nao wakakaa Kadeshi. Miriamu akafa huko na kuzikwa.

2 Mahali hapo hapakuwa na maji kwa ajili ya jumuiya hiyo, nao wakakusanyika ili kumpinga Mose na Aroni.

3 Watu wakagombana na Mose, na kusema, “Laiti tungelikufa wakati ndugu zetu walipoanguka na kufa mbele zaBwana!

4 Kwa nini mmeileta jumuiya yaBwanakwenye jangwa hili, ili tufe humu, sisi na mifugo yetu?

5 Kwa nini mmetupandisha kutoka Misri mpaka mahali hapa pa kutisha? Hapa hakuna nafaka wala tini, zabibu au makomamanga. Wala hapa hakuna maji ya kunywa!”

6 Mose na Aroni wakaondoka pale kwenye kusanyiko mpaka kwenye mlango wa Hema la Kukutania na kuanguka kifudifudi, nao utukufu waBwanaukawatokea.

7 Bwanaakamwambia Mose,

8 “Chukua ile fimbo, na wewe na ndugu yako Aroni mkusanye kusanyiko pamoja. Nena na ule mwamba mbele ya macho yao, nao utatoa maji yake. Utatoa maji kutoka huo mwamba kwa ajili ya jumuiya ili wao na mifugo yao waweze kunywa.”

9 Kwa hiyo Mose akaichukua hiyo fimbo kutoka pale ilipokuwa mbele zaBwanakama alivyomwagiza.

10 Mose na Aroni wakakusanya kusanyiko pamoja mbele ya huo mwamba, naye Mose akawaambia, “Sikilizeni, enyi waasi. Je, ni lazima tuwatoleeni maji kutoka mwamba huu?”

11 Ndipo Mose akainua mkono wake na kuupiga mwamba mara mbili kwa fimbo yake. Maji yakabubujika, nayo jumuiya na mifugo yao wakanywa.

12 LakiniBwanaakamwambia Mose na Aroni, “Kwa sababu hamkuniamini mimi kiasi cha kuniheshimu kama mtakatifu machoni pa Waisraeli, hamtaiingiza jumuiya hii katika nchi ninayowapa.”

13 Haya yalikuwa maji ya Meriba,mahali pale ambapo Waisraeli waligombana naBwana, naye akajionyesha mwenyewe huko kuwa mtakatifu katikati yao.

Edomu Wakatalia Israeli Kupita

14 Mose akawatuma wajumbe kutoka Kadeshi kwenda kwa mfalme wa Edomu, akisema:

“Hili ndilo ndugu yako Israeli asemalo: Wewe unafahamu juu ya taabu zote ambazo zimetupata.

15 Baba zetu walishuka Misri, nasi tumeishi huko miaka mingi. Wamisri walitutesa sisi na baba zetu,

16 lakini tulipomliliaBwana, alisikia kilio chetu na akamtuma malaika akatutoa Misri.

“Sasa tupo hapa Kadeshi, mji ulio mpakani mwa nchi yako.

17 Tafadhali turuhusu tupite katika nchi yako. Hatutapita katika shamba lolote, wala shamba la mizabibu, au kunywa maji kutoka kwenye kisima chochote. Tutasafiri kufuata njia kuu ya mfalme, na hatutageuka kulia wala kushoto mpaka tuwe tumeshapita nchi yako.”

18 Lakini mfalme wa Edomu akajibu:

“Hamtapita hapa; kama mkijaribu kupita, tutatoka na kuwashambulia kwa upanga.”

19 Waisraeli wakajibu:

“Sisi tutafuata njia kuu; tena ikiwa sisi au mifugo yetu tutakunywa tone la maji yenu, tutalilipia. Sisi tunataka tu kupita kwa miguu, wala si kitu kingine chochote.”

20 Watu wa Edomu wakajibu tena:

“Hamwezi kupita hapa.”

Ndipo watu wa Edomu wakatoka dhidi ya Waisraeli, jeshi kubwa lenye nguvu.

21 Kwa kuwa Waedomu waliwakatalia Waisraeli kupita katika nchi yao, Israeli wakageuka, wakawaacha.

Kifo Cha Aroni

22 Jumuiya yote ya Kiisraeli ikaondoka kutoka Kadeshi, wakafika kwenye Mlima Hori.

23 Kwenye Mlima Hori, karibu na mpaka wa Edomu,Bwanaakamwambia Mose na Aroni,

24 “Aroni atakusanywa pamoja na watu wake. Hataingia katika nchi ninayowapa Waisraeli, kwa sababu ninyi wawili mliasi dhidi ya agizo langu kwenye maji ya Meriba.

25 Watwae Aroni na Eleazari mwanawe, na uwapandishe juu katika Mlima wa Hori.

26 Mvue Aroni mavazi yake, na umvike Eleazari mwanawe, kwa maana Aroni atakusanywa pamoja na watu wake; atakufa huko.”

27 Mose akafanya kamaBwanaalivyomwagiza: Wakapanda Mlima Hori mbele ya macho ya jumuiya yote ya Kiisraeli.

28 Mose akamvua Aroni mavazi yake na kumvika mwanawe Eleazari mavazi hayo. Naye Aroni akafia pale juu ya mlima. Kisha Mose na Eleazari wakateremka kutoka mlimani.

29 Jumuiya yote ilipofahamu kwamba Aroni amekufa, jamaa yote ya Kiisraeli wakamwomboleza kwa siku thelathini.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/20-ce16522e521585315953f4a810315509.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 21

Nchi Ya Aradi Yaangamizwa

1 Mfalme wa Kikanaani wa Aradi aliyeishi huko Negebu aliposikia kwamba Waisraeli walikuwa wanakuja kwa njia ya Atharimu, aliwashambulia Waisraeli na kuwateka baadhi yao.

2 Ndipo Israeli akaweka nadhiri hii kwaBwana: “Ikiwa utawatia watu hawa mikononi mwetu, tutaiangamiza kabisa miji yao.”

3 Bwanaakasikiliza ombi la Waisraeli, naye akawapa ushindi juu ya Wakanaani. Wakawaangamiza kabisa na miji yao; hivyo mahali pale pakaitwa Horma.

Nyoka Wa Shaba

4 Waisraeli wakasafiri kutoka mlima Hori kupitia njia inayoelekea Bahari ya Shamu,kuizunguka Edomu. Lakini watu wakakosa uvumilivu njiani,

5 wakamnungʼunikia Mungu na Mose, wakisema, “Kwa nini umetupandisha kutoka Misri ili tufe jangwani? Hakuna mkate! Hakuna maji! Nasi tunachukia sana chakula hiki duni!”

6 NdipoBwanaakapeleka nyoka wenye sumu katikati yao; wakawauma watu, nao Waisraeli wengi wakafa.

7 Watu wakamjia Mose na kusema, “Tumetenda dhambi wakati tuliponena dhidi yaBwanana dhidi yako. MwombeBwanaili atuondolee hawa nyoka.” Hivyo Mose akawaombea hao watu.

8 Bwanaakamwambia Mose, “Tengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti; yeyote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.”

9 Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu yeyote aliumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi.

Safari Kwenda Moabu

10 Waisraeli waliendelea na safari yao na wakapiga kambi huko Obothi.

11 Kisha wakaondoka Obothi na kupiga kambi huko Iye-Abarimu, katika jangwa linalotazamana na Moabu kuelekea mawio ya jua.

12 Kutoka hapo waliendelea mbele wakapiga kambi kwenye Bonde la Zeredi.

13 Wakasafiri kutoka hapo na kupiga kambi kando ya Mto Arnoni, ambao uko katika jangwa lililoenea hadi nchi ya Waamori. Arnoni ni mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.

14 Ndiyo sababu Kitabu cha Vita vyaBwanakinasema:

“…Mji wa Wahebu nchini Seifa na mabonde

ya Arnoni,

15 na miteremko ya mabonde

inayofika hadi mji wa Ari

na huelekea mpakani mwa Moabu.”

16 Kutoka hapo waliendelea mbele hadi kisima cha Beeri; kwenye kisima ambachoBwanaalimwambia Mose, “Wakusanye watu pamoja, nami nitawapa maji.”

17 Kisha Israeli akaimba wimbo huu:

“Bubujika, ee kisima!

Imba kuhusu maji,

18 kuhusu kisima ambacho kilichimbwa na wakuu,

ambacho watu mashuhuri walikifukua,

watu mashuhuri wakiwa na fimbo za utawala na bakora.”

Kisha wakatoka jangwani kwenda Matana,

19 kutoka Matana wakafika Nahalieli, kutoka Nahalieli wakafika Bamothi,

20 na kutoka Bamothi wakafika kwenye bonde lililoko Moabu, mahali ambapo kilele cha Pisga kinatazamana na nyika.

Kushindwa Kwa Sihoni Na Ogu

21 Israeli akawatuma wajumbe kumwambia Sihoni mfalme wa Waamori:

22 “Uturuhusu tupite katika nchi yako. Hatutageuka kando kwenda katika mashamba au mashamba ya mizabibu, ama kunywa maji kutoka kisima chochote. Tutasafiri kwenye njia kuu ya mfalme hata tutakapokuwa tumekwisha kupita katika nchi yako.”

23 Lakini Sihoni hakumruhusu Israeli apite katika nchi yake. Alilikutanisha jeshi lake lote, wakaondoka kwenda jangwani ili kupigana na Israeli. Alipofika huko Yahazi, akapigana na Israeli.

24 Hata hivyo, Israeli alimshinda kwa upanga na kuiteka ardhi yake kutoka Arnoni mpaka Yaboki, lakini ni hadi kufikia nchi ya Waamoni tu, kwa sababu mipaka yake ilikuwa imezungushwa ukuta.

25 Israeli akaiteka miji yote ya Waamori na kuikalia, pamoja na Heshboni na makazi yote yanayoizunguka.

26 Heshboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa amepigana dhidi ya mfalme wa Moabu aliyetangulia na akawa amechukua ardhi yake yote mpaka Arnoni.

27 Ndiyo sababu watunga mashairi husema:

“Njoo Heshboni na ujengwe tena;

mji wa Sihoni na ufanywe upya.

28 “Moto uliwaka kutoka Heshboni,

mwali wa moto kutoka mji wa Sihoni.

Uliteketeza Ari ya Moabu,

raiya wa mahali pa Arnoni palipoinuka.

29 Ole wako, ee Moabu!

Umeharibiwa, enyi watu wa Kemoshi!

Amewatoa wanawe kuwa wakimbizi,

na binti zake kama mateka

kwa Mfalme Sihoni wa Waamori.

30 “Lakini tumewashinda;

Heshboni umeharibiwa hadi Diboni.

Tumebomoa hadi kufikia Nofa,

ulioenea hadi Medeba.”

31 Kwa hiyo Israeli akaishi katika nchi ya Waamori.

32 Baada ya Mose kutuma wapelelezi kwenda mji wa Yazeri, Waisraeli waliteka viunga vya mji huo na kuwafukuza Waamori waliokuwa wanaishi huko.

33 Kisha wakageuka na kwenda katika njia inayoelekea Bashani, naye Ogu mfalme wa Bashani pamoja na jeshi lake lote wakatoka kupigana nao huko Edrei.

34 Bwanaakamwambia Mose, “Usimwogope Ogu, kwa sababu nimeshamkabidhi mikononi mwako, pamoja na jeshi lake lote na nchi yake. Mtendee kama ulivyomtendea Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.”

35 Kwa hiyo wakamuua, pamoja na wanawe na jeshi lake lote, bila ya kumwacha hata mtu mmoja hai. Nao wakaimiliki nchi yake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/21-ac29d865b2cda095a76e01534208e4a5.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 22

Balaki Anamwita Balaamu

1 Kisha Waisraeli wakasafiri katika tambarare za Moabu na kupiga kambi kando ya Mto Yordani, ngʼambo ya Yeriko.

2 Basi Balaki mwana wa Sipori, aliona mambo yale yote ambayo Israeli aliwatendea Waamori,

3 Moabu aliogopa, kwa kuwa walikuwepo watu wengi sana. Hakika, Moabu alijawa na hofu kubwa kwa sababu ya Waisraeli.

4 Wamoabu wakawaambia wazee wa Midiani, “Umati huu wa watu unakwenda kuramba kila kitu kinachotuzunguka, kama maksai arambavyo majani ya shambani.”

Kwa hiyo Balaki mwana wa Sipori, ambaye alikuwa mfalme wa Moabu wakati huo,

5 akatuma wajumbe kwenda kumwita Balaamu mwana wa Beori, ambaye alikuwa huko Pethori, karibu na Mto Frati, katika nchi yake ya kuzaliwa. Balaki akasema:

“Taifa limekuja kutoka Misri, nao wamefunika uso wa nchi, nao wametua karibu nami.

6 Sasa uje kuwalaani watu hawa, kwa kuwa wana nguvu sana kuniliko. Kisha huenda nikaweza kuwashinda na kuwatoa nje ya nchi. Kwa kuwa ninajua kwamba, wale unaowabariki wanabarikiwa na wale unaowalaani wanalaaniwa.”

7 Wazee wa Moabu na wa Midiani wakaondoka, wakiwa wamechukua ada ya uaguzi. Walipokwenda kwa Balaamu, wakamweleza kile Balaki alikuwa amesema.

8 Balaamu akawaambia, “Mlale hapa usiku huu, nami nitawaletea jibu lileBwanaatakalonipa.” Kwa hiyo wakuu wa Moabu wakakaa naye.

9 Mungu akamjia Balaamu na kumuuliza, “Watu gani hawa walio pamoja nawe?”

10 Balaamu akamwambia Mungu, “Balaki mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, alinipelekea ujumbe huu:

11 ‘Taifa ambalo limekuja kutoka Misri limefunika uso wa nchi. Sasa uje unilaanie hao watu. Kisha huenda nitaweza kupigana nao na kuwafukuza.’ ”

12 LakiniBwanaakamwambia Balaamu, “Usiende pamoja nao. Hupaswi kulaani watu hao, kwa kuwa wamebarikiwa.”

13 Asubuhi iliyofuata Balaamu akaamka, akawaambia wakuu wa Balaki, “Rudini katika nchi yenu, kwa kuwaBwanaamenikataza nisiende pamoja nanyi.”

14 Kwa hiyo wakuu wa Moabu wakarudi kwa Balaki na kumwambia, “Balaamu amekataa kuja pamoja nasi.”

15 Kisha Balaki akatuma wakuu wengine, wengi zaidi na wanaoheshimiwa zaidi kuliko wale wa kwanza.

16 Wakafika kwa Balaamu na kumwambia:

“Balaki mwana wa Sipori amesema hivi: Usiruhusu kitu chochote kikuzuie kuja kwangu,

17 kwa sababu nitakulipa vizuri sana na kufanya lolote usemalo. Njoo unilaanie watu hawa.”

18 Lakini Balaamu akawajibu, “Hata kama Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, singeweza kufanya kitu chochote kikubwa au kidogo ili kutenda kitu nje ya agizo laBwanaMungu wangu.

19 Mlale hapa usiku huu kama wale wengine walivyofanya, nami nitatafuta ni nini kingineBwanaatakachoniambia.”

20 Usiku uleBwanaakamjia Balaamu na kumwambia, “Kwa kuwa watu hawa wamekuja kukuita wewe, nenda nao, lakini ufanye tu lile nitakalokuambia.”

Punda Wa Balaamu

21 Balaamu akaamka asubuhi, akatandika punda wake akaenda pamoja na wakuu wa Moabu.

22 Lakini Mungu alikasirika sana alipokwenda, naye malaika waBwanaakasimama barabarani kumpinga. Balaamu alikuwa amepanda punda wake, na watumishi wake wawili walikuwa pamoja naye.

23 Wakati punda alipomwona malaika waBwanaakiwa amesimama barabarani akiwa na upanga uliofutwa mkononi mwake, punda akageukia upande kuelekea shambani. Balaamu akampiga ili amrudishe barabarani.

24 Ndipo malaika waBwanaakasimama katika njia nyembamba iliyo kati ya mashamba mawili ya mizabibu, yakiwa na kuta pande zote mbili.

25 Punda alipomwona malaika waBwana, alijisukumiza karibu na ukuta, na kugandamiza mguu wa Balaamu ukutani. Ndipo Balaamu akampiga tena punda.

26 Kisha malaika waBwanaakaendelea mbele na kusimama mahali pembamba ambapo hapakuwepo nafasi ya kugeuka, upande wa kulia wala wa kushoto.

27 Punda alipomwona malaika waBwana, alilala chini Balaamu angali amempanda, naye Balaamu akakasirika na kumpiga kwa fimbo yake.

28 KishaBwanaakakifungua kinywa cha punda, akamwambia Balaamu, “Nimekutendea nini kinachokufanya unipige mara hizi tatu?”

29 Balaamu akamjibu punda, “Umenifanya mjinga! Kama ningelikuwa na upanga mkononi mwangu, ningelikuua sasa hivi.”

30 Punda akamwambia Balaamu, “Je, mimi si punda wako mwenyewe, ambaye umenipanda siku zote, hadi leo? Je, nimekuwa na tabia ya kufanya hivi kwako?”

Akajibu, “Hapana.”

31 KishaBwanaakafungua macho ya Balaamu, naye akamwona malaika waBwanaamesimama barabarani akiwa ameufuta upanga wake. Balaamu akainama, akaanguka kifudifudi.

32 Malaika waBwanaakamuuliza Balaamu, “Kwa nini umempiga punda wako mara tatu hizi? Nimekuja kukuzuia kwa sababu njia yako imepotoka mbele yangu.

33 Punda aliniona na kunikwepa mara hizi tatu. Kama punda hangenikwepa, hakika ningekuwa nimeshakuua sasa, lakini ningemwacha punda hai.”

34 Balaamu akamwambia malaika waBwana, “Nimetenda dhambi. Sikutambua kuwa umesimama barabarani kunizuia. Basi kama haikupendezi, nitarudi.”

35 Malaika waBwanaakamwambia Balaamu, “Uende na watu hao, lakini useme tu lile nikuambialo.” Kwa hiyo Balaamu akaenda na wale wakuu wa Balaki.

36 Balaki aliposikia kuwa Balaamu anakuja, akatoka kumlaki katika mji wa Moabu, katika mpaka wa Arnoni, ukingoni mwa nchi yake.

37 Balaki akamwambia Balaamu, “Je, sikukupelekea jumbe za haraka? Kwa nini hukuja kwangu? Hivi kweli mimi siwezi kukulipa?”

38 Balaamu akajibu, “Vema, sasa nimekuja kwako. Lakini kwani nina uwezo wa kusema tu chochote? Ni lazima niseme tu kile ambacho Mungu ataweka kinywani mwangu.”

39 Kisha Balaamu alikwenda na Balaki mpaka Kiriath-Husothi.

40 Balaki akatoa dhabihu ya ngʼombe na kondoo; baadhi yake akampa Balaamu na wakuu waliokuwa pamoja naye.

41 Asubuhi iliyofuata Balaki akamchukua Balaamu mpaka Bamoth-Baali, na kutoka huko Balaamu akawaona baadhi ya watu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/22-94907a16a7c2116fb8da1251a306061b.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 23

Ujumbe Wa Kwanza Wa Balaamu

1 Balaamu akasema, “Nijengee hapa madhabahu saba, mnitayarishie mafahali saba na kondoo dume saba.”

2 Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema; hao wawili kila mmoja wao akatoa fahali mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.

3 Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati mimi ninakwenda kando. HuendaBwanaatakuja kukutana nami. Lolote atakalonifunulia, nitakuambia.” Basi akaenda hata mahali peupe palipoinuka.

4 Mungu akakutana naye, kisha Balaamu akasema, “Nimekwisha kutengeneza madhabahu saba, na juu ya kila madhabahu nimetoa sadaka ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja.”

5 Bwanaakaweka ujumbe katika kinywa cha Balaamu na kusema, “Rudi kwa Balaki umpe ujumbe huu.”

6 Basi Balaamu akarudi kwa Balaki, akamkuta amesimama kando ya sadaka yake akiwa na wakuu wote wa Moabu.

7 Ndipo Balaamu akasema ujumbe wake:

“Balaki amenileta kutoka Aramu,

mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki.

Akasema, ‘Njoo, unilaanie Yakobo;

njoo unishutumie Israeli.’

8 Nitawezaje kuwalaani,

hao ambao Mungu hajawalaani?

Nitawezaje kuwashutumu

hao ambaoBwanahakuwashutumu?

9 Kutoka vilele vya miamba ninawaona,

kutoka mahali palipoinuka ninawatazama.

Ninaliona taifa ambalo wanaishi peke yao,

nao hawahesabiwi kama mojawapo ya mataifa.

10 Ni nani awezaye kuhesabu mavumbi ya Yakobo,

au kuhesabu robo ya Israeli?

Mimi na nife kifo cha mtu mwenye haki,

na mwisho wangu na uwe kama wao!”

11 Balaki akamwambia Balaamu, “Ni nini ulichonitendea? Nimekuleta ulaani adui zangu, lakini wewe badala yake umewabariki!”

12 Balaamu akajibu, “Je, hainipasi kusema kileBwanaanachoweka katika kinywa changu?”

Ujumbe Wa Pili Wa Balaamu

13 Ndipo Balaki akamwambia, “Twende pamoja mahali pengine ambapo unaweza kuwaona; utawaona baadhi tu wala si wote. Nawe kutoka huko, unilaanie hao.”

14 Basi akampeleka kwenye shamba la Sofimu, juu ya kilele cha Mlima Pisga. Pale akajenga madhabahu saba na kutoa sadaka ya fahali na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.

15 Balaamu akamwambia Balaki, “Kaa hapa kando ya sadaka yako wakati ninapokwenda kuonana na Mungu kule.”

16 Bwanaakakutana na Balaamu, akaweka ujumbe katika kinywa chake akasema, “Rudi kwa Balaki umpe ujumbe huu.”

17 Basi Balaamu akarudi kwa Balaki, akamkuta amesimama kando ya sadaka yake, akiwa na wakuu wa Moabu. Balaki akamuuliza, “Je,Bwanaamesema nini?”

18 Ndipo Balaamu akasema ujumbe wake:

“Balaki, inuka na usikilize,

nisikie mimi, wewe mwana wa Sipori.

19 Mungu si mtu, hata aseme uongo,

wala yeye si mwanadamu, hata ajute.

Je, anasema, kisha asitende?

Je, anaahidi, asitimize?

20 Nimepokea agizo kubariki;

amebariki, nami siwezi kubadilisha.

21 “Haijaonekana bahati mbaya katika Yakobo,

wala taabu katika Israeli.

Bwana, Mungu wao yu pamoja nao,

nayo sauti kuu ya Mfalme imo katikati yao.

22 Mungu aliwatoa kutoka Misri;

wao wana nguvu za nyati.

23 Hakuna uchawi dhidi ya Yakobo,

wala hakuna uaguzi dhidi ya Israeli.

Sasa itasemwa kuhusu Yakobo

na Israeli, ‘Tazama yale Mungu aliyotenda!’

24 Taifa lainuka kama simba jike;

linajiinua kama simba

ambaye hatulii mpaka amalize kurarua mawindo yake

na kunywa damu ya mawindo yake.”

25 Kisha Balaki akamwambia Balaamu, “Usiwalaani kabisa, wala usiwabariki kabisa!”

26 Balaamu akajibu, “Je, sikukuambia ni lazima nifanye lolote analosemaBwana?”

Ujumbe Wa Tatu Wa Balaamu

27 Basi Balaki akamwambia Balaamu, “Njoo, nikupeleke mahali pengine. Huenda itampendeza Mungu kukuruhusu unilaanie hao watu kutoka mahali hapo.”

28 Balaki akamchukua Balaamu juu ya Mlima Peori, unaotazamana na nyika.

29 Balaamu akasema, “Nijengee hapa madhabahu saba, uandae mafahali saba na kondoo dume saba kwa ajili yangu.”

30 Balaki akafanya kama Balaamu alivyosema, kisha akatoa sadaka ya fahali mmoja na kondoo dume mmoja juu ya kila madhabahu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/23-4c471dea8647356566b93305053ba025.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 24

1 Basi Balaamu alipoona imempendezaBwanakubariki Israeli, hakuendelea tena kutafuta uchawi kama nyakati nyingine, bali aligeuza uso wake kuelekea nyikani.

2 Balaamu alipotazama nje na kuona Israeli amepiga kambi kabila kwa kabila, Roho wa Mungu akawa juu yake,

3 naye akatoa ujumbe wake:

“Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori,

ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri;

4 ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,

ambaye huona maono kutoka kwa Mwenyezi,

ambaye huanguka kifudifudi, na ambaye macho yake yamefunguka:

5 “Tazama jinsi yalivyo mazuri mahema yako, ee Yakobo,

maskani yako, ee Israeli!

6 “Kama mabonde, yanaenea,

kama bustani kando ya mto,

kama miti ya udi iliyopandwa naBwana,

kama mierezi kando ya maji.

7 Maji yatatiririka kutoka ndoo zake;

mbegu yake itakuwa na maji tele.

“Mfalme wake atakuwa mkuu kuliko Mfalme Agagi;

ufalme wake utatukuka.

8 “Mungu alimleta kutoka Misri;

yeye ana nguvu kama nyati.

Anayararua mataifa yaliyo adui zake,

na kuvunja mifupa yao vipande vipande;

huwachoma kwa mishale yake.

9 Hujikunyata na kuvizia kama simba,

kama simba jike; nani anayethubutu kumwamsha?

“Abarikiwe kila akubarikiye,

na alaaniwe kila akulaaniye!”

10 Ndipo hasira ya Balaki ikawaka dhidi ya Balaamu. Akapiga mikono yake pamoja, akamwambia Balaamu, “Nilikuita uje kuwalaani adui zangu, lakini umewabariki mara hizi tatu.

11 Sasa ondoka upesi uende nyumbani! Mimi nilisema nitakuzawadia vizuri sana, lakiniBwanaamekuzuia usizawadiwe.”

12 Balaamu akamwambia Balaki, “Je, hukumbuki jinsi nilivyowaambia wajumbe uliowatuma kwangu? Niliwaambia hivi,

13 ‘Hata ikiwa Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, nisingeweza kufanya kitu chochote kwa matakwa yangu, kikiwa kizuri au kibaya, kwenda kinyume na agizo laBwana, nami imenipasa kusema tu kileBwanaatakachosema’?

14 Sasa ninarudi kwa watu wangu. Lakini njoo, nikuonye kuhusu kile watu hawa watakachowatenda watu wako siku zijazo.”

Ujumbe Wa Nne Wa Balaamu

15 Kisha Balaamu akatoa ujumbe wake:

“Ujumbe wa Balaamu mwana wa Beori,

ujumbe wake yeye ambaye jicho lake linaona vizuri;

16 ujumbe wake yeye ambaye husikia maneno ya Mungu,

ambaye ana maarifa kutoka kwa Aliye Juu Sana,

huona maono kutoka Mwenyezi,

ambaye huanguka kifudifudi

na ambaye macho yake yamefunguka:

17 “Namwona yeye, lakini si sasa;

namtazama yeye, lakini si karibu.

Nyota itatoka kwa Yakobo,

fimbo ya ufalme itainuka kutoka kwa Israeli.

Atawaponda Wamoabu vipaji vya nyuso

na mafuvu yote ya wana wa Shethi.

18 Edomu itamilikiwa,

Seiri, adui wake, itamilikiwa,

lakini Israeli atakuwa na nguvu.

19 Mtawala atakuja kutoka kwa Yakobo

na kuangamiza walionusurika katika mji.”

Ujumbe Wa Mwisho Wa Balaamu

20 Kisha Balaamu akawaona watu wa Amaleki, na kutoa ujumbe wake:

“Amaleki ilikuwa ya kwanza miongoni mwa mataifa,

lakini mwisho wake itaangamizwa milele.”

21 Kisha akawaona Wakeni, akatoa ujumbe wake:

“Makao yenu ni salama,

kiota chenu kiko kwenye mwamba.

22 Hata hivyo ninyi Wakeni mtaangamizwa

Ashuru atakapowachukua mateka.”

23 Ndipo akatoa ujumbe wake:

“Lo, ni nani atakayeweza kuishi wakati Mungu atakapofanya hili?

24 Meli zitakuja kutoka pwani za Kitimu,

zitaitiisha Ashuru na Eberi,

lakini nao pia wataangamizwa.”

25 Kisha Balaamu akainuka na kurudi nyumbani kwake, naye Balaki akashika njia yake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/24-8db1943ec6fa9461e30b691addbe0457.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 25

Moabu Yashawishi Israeli

1 Israeli alipokuwa akikaa Shitimu, wanaume wa Israeli walianza kuzini na wanawake wa Kimoabu,

2 ambao waliwaalika kushiriki katika kutoa kafara kwa miungu yao. Watu wakala na kusujudu mbele ya miungu hii.

3 Kwa hiyo Israeli akaungana katika kumwabudu Baali wa Peori. Hasira yaBwanaikawaka dhidi yao.

4 Bwanaakamwambia Mose, “Uwachukue viongozi wote wa watu hawa, uwaue na uwaweke hadharani mchana peupe mbele zaBwana, ili hasira kali yaBwanaiweze kuondoka kwa Israeli.”

5 Kwa hiyo Mose akawaambia waamuzi wa Israeli, “Kila mmoja wenu lazima awaue wale wanaume wenu, walioshiriki katika kumwabudu Baali wa Peori.”

6 Ndipo mwanaume wa Kiisraeli akamleta mwanamke wa Kimidiani katika jamaa yake palepale mbele ya Mose na mkutano wote wa Israeli walipokuwa wakilia kwenye lango la Hema la Kukutania.

7 Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, alipoona jambo hili, akaondoka kwenye kusanyiko, akachukua mkuki mkononi mwake,

8 akamfuata yule Mwisraeli ndani ya hema. Akawachoma mkuki wote wawili kwa pamoja, ukapenya kwenye mwili wa yule Mwisraeli na mwili wa yule mwanamke. Ndipo tauni iliyokuwepo dhidi ya Waisraeli ikakoma.

9 Lakini wale waliokufa kwa hiyo tauni walikuwa watu 24,000.

10 Bwanaakamwambia Mose,

11 “Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, amegeuza hasira yangu mbali na Waisraeli, kwa sababu alikuwa na wivu kama nilio nao kwa heshima yangu miongoni mwao, hata kwamba kwa wivu wangu sikuwaangamiza.

12 Kwa hiyo mwambie Finehasi ninafanya Agano langu la amani naye.

13 Yeye pamoja na wazao wake watakuwa na Agano la ukuhani milele, kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya heshima ya Mungu wake, na akafanya upatanisho kwa Waisraeli.”

14 Jina la Mwisraeli ambaye aliuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani ni Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa ya Simeoni.

15 Jina la mwanamke wa Kimidiani aliyeuawa ni Kozbi binti wa Suri, aliyekuwa mkuu wa kabila la jamaa ya Wamidiani.

16 Bwanaakamwambia Mose,

17 “Watendeeni Wamidiani kama adui na mwaue,

18 kwa sababu wao waliwatendea kama adui wakati waliwadanganya katika tukio la Peori na dada yao Kozbi, binti wa kiongozi wa Kimidiani, mwanamke ambaye aliuawa wakati tauni ilikuja kama matokeo ya tukio la Peori.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/25-bd2332b34b9c96b44a543da63c15ad04.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 26

Kuhesabiwa Watu Mara Ya Pili

1 Baada ya hiyo tauni,Bwanaakamwambia Mose na Eleazari mwana wa kuhani Aroni,

2 “Hesabu jumuiya yote ya Kiisraeli kwa jamaa zao, wale wote wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao wanaweza kutumika katika jeshi la Israeli.”

3 Hivyo Mose na kuhani Eleazari wakazungumza na watu kwenye nchi tambarare ya Moabu, ngʼambo ya Yordani kutokea Yeriko, wakasema,

4 “Hesabuni wanaume wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.”

Hawa ndio Waisraeli waliotoka Misri:

5 Wazao wa Reubeni, mwana mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa:

kutoka kwa Hanoki, ukoo wa Wahanoki;

kutoka kwa Palu, ukoo wa Wapalu;

6 kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni;

kutoka kwa Karmi, ukoo wa Wakarmi.

7 Hizi zilikuwa ndizo koo za Reubeni; wale waliohesabiwa walikuwa 43,730.

8 Mwana wa Palu alikuwa Eliabu,

9 nao wana wa Eliabu walikuwa Nemueli, Dathani na Abiramu. Hawa wawili Dathani na Abiramu ndio walikuwa maafisa wa jumuiya ambao walimwasi Mose na Aroni, na walikuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora wakati walimwasiBwana.

10 Ardhi ilifunua kinywa chake na kuwameza pamoja na Kora, ambaye wafuasi wake walikufa wakati moto ulipowateketeza wanaume 250. Nao walikuwa kama alama ya onyo.

11 Pamoja na hayo, hao ukoo wa Kora hawakufa.

12 Wazao wa Simeoni kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli;

kutoka kwa Yamini, ukoo wa Wayamini;

kutoka wa Yakini, ukoo wa Wayakini;

13 kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera;

kutoka kwa Shauli, ukoo wa Washauli.

14 Hizi ndizo koo za Simeoni; walikuwa 22,200.

15 Wazao wa Gadi kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Sifoni, ukoo wa Wasifoni;

kutoka kwa Hagi, ukoo wa Wahagi;

kutoka kwa Shuni, ukoo wa Washuni;

16 kutoka kwa Ozni, ukoo wa Waozni;

kutoka kwa Eri, ukoo wa Waeri;

17 kutoka kwa Arodi, ukoo wa Waarodi;

kutoka kwa Areli, ukoo wa Waareli.

18 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Gadi; wale waliohesabiwa walikuwa 40,500.

19 Eri na Onani walikuwa wana wa Yuda, lakini walifia huko Kanaani.

20 Wazao wa Yuda kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Shela, ukoo wa Washela;

kutoka kwa Peresi, ukoo wa Waperesi;

kutoka kwa Zera, ukoo wa Wazera.

21 Wazao wa Peresi walikuwa:

kutoka kwa Hesroni, ukoo wa Wahesroni;

kutoka kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.

22 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda; wale waliohesabiwa walikuwa 76,500.

23 Wazao wa Isakari kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Tola, ukoo wa Watola;

kutoka kwa Puva, ukoo wa Wapuva;

24 kutoka kwa Yashubu, ukoo wa Wayashubu;

kutoka kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.

25 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Isakari; wale waliohesabiwa walikuwa 64,300.

26 Wazao wa Zabuloni kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Seredi, ukoo wa Waseredi;

kutoka kwa Eloni, ukoo wa Waeloni;

kutoka kwa Yaleeli, ukoo wa Wayaleeli.

27 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Zabuloni, wale waliohesabiwa walikuwa 60,500.

28 Wazao wa Yosefu kwa koo zao kutoka kwa Manase na kwa Efraimu walikuwa:

29 Wazao wa Manase:

kutoka kwa Makiri, ukoo wa Wamakiri (Makiri alikuwa baba wa Gileadi);

kutoka kwa Gileadi, ukoo wa Wagileadi.

30 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Gileadi:

kutoka kwa Iezeri, ukoo wa Waiezeri;

kutoka kwa Heleki, ukoo wa Waheleki;

31 kutoka kwa Asirieli, ukoo wa Waasirieli;

kutoka kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu;

32 kutoka kwa Shemida, ukoo wa Washemida;

kutoka kwa Heferi, ukoo wa Waheferi.

33 (Selofehadi mwana wa Heferi hakuzaa wana, bali alikuwa na watoto wa kike tu, ambao majina yao yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.)

34 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Manase; wale waliohesabiwa walikuwa 52,700.

35 Hawa walikuwa wazao wa Efraimu kwa koo zao:

kutoka kwa Shuthela, ukoo wa Washuthela;

kutoka kwa Bekeri, ukoo wa Wabekeri;

kutoka kwa Tahani, ukoo wa Watahani;

36 Hawa ndio walikuwa wazao wa Shuthela:

kutoka kwa Erani, ukoo wa Waerani.

37 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa 32,500.

Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yosefu kwa koo zao.

38 Wazao wa Benyamini kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Bela, ukoo wa Wabela;

kutoka kwa Ashbeli, ukoo wa Waashbeli;

kutoka kwa Ahiramu, ukoo wa Waahiramu;

39 kutoka kwa Shufamu, ukoo wa Washufamu;

kutoka kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu.

40 Wazao wa Bela kutoka kwa Ardi na Naamani walikuwa:

kutoka kwa Ardi, ukoo wa Waardi;

kutoka kwa Naamani, ukoo wa Wanaamani.

41 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Benyamini; wale waliohesabiwa walikuwa 45,600.

42 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Dani kwa koo zao:

kutoka kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu.

Hizi ndizo zilizokuwa koo za Dani:

43 Wote walikuwa koo za Washuhamu; wale waliohesabiwa walikuwa 64,400.

44 Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Imna, ukoo wa Waimna;

kutoka kwa Ishvi, ukoo wa Waishvi;

kutoka kwa Beria, ukoo wa Waberia;

45 kutoka kwa wazao wa Beria:

kutoka kwa Heberi, ukoo wa Waheberi;

kutoka kwa Malkieli, ukoo wa Wamalkieli.

46 (Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.)

47 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa 53,400.

48 Wazao wa Naftali kwa koo zao walikuwa:

kutoka kwa Yaseeli, ukoo wa Wayaseeli;

kutoka kwa Guni, ukoo wa Waguni;

49 kutoka kwa Yeseri, ukoo wa Wayeseri;

kutoka kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu.

50 Hizi ndizo zilizokuwa koo za Naftali; wale waliohesabiwa walikuwa 45,400.

51 Jumla ya hesabu ya wanaume wa Israeli ilikuwa 601,730.

52 Bwanaakamwambia Mose,

53 “Watagawiwa nchi kama urithi kwa kulingana na hesabu ya majina.

54 Kundi kubwa zaidi lipe urithi mkubwa zaidi, na kundi dogo zaidi lipewe urithi mdogo zaidi; kila kundi litapokea urithi wake kulingana na hesabu ya wale walioorodheshwa.

55 Hakikisha kuwa nchi inagawanywa kwa kura. Kile kitakachorithiwa na kila kikundi kitakuwa kwa kulingana na majina ya kabila la babu yao.

56 Kila urithi utagawanywa kwa kura miongoni mwa makundi makubwa na madogo.”

57 Hawa walikuwa Walawi ambao walihesabiwa kwa koo zao:

kutoka kwa Gershoni, ukoo wa Wagershoni;

kutoka kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi;

kutoka kwa Merari, ukoo wa Wamerari.

58 Hizi pia zilikuwa koo za Walawi:

ukoo wa Walibni;

ukoo wa Wahebroni;

ukoo wa Wamahli;

ukoo wa Wamushi;

ukoo wa wana wa Kora.

(Kohathi alikuwa baba aliyemzaa Amramu;

59 jina la mke wa Amramu ni Yokebedi, naye pia alikuwa mzao wa Lawi, ambaye alizaliwa kwa Walawi nchini Misri. Alimzalia Amramu: Aroni, Mose na dada yao Miriamu.

60 Aroni alikuwa baba yake Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari.

61 Lakini Nadabu na Abihu walikufa wakati walitoa sadaka mbele zaBwanakwa moto usioruhusiwa.)

62 Wanaume wote wa Walawi wa umri wa mwezi mmoja na zaidi walikuwa 23,000. Wao hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine kwa sababu hawakupokea urithi miongoni mwao.

63 Hawa ndio walioorodheshwa na Mose na kuhani Eleazari wakati waliwahesabu Waisraeli kwenye nchi tambarare ya Moabu, kando ya Yordani ngʼambo ya Yeriko.

64 Hakuna hata mmoja wao aliyekuwa miongoni mwa wale waliohesabiwa na Mose na kuhani Aroni wakati waliwahesabu Waisraeli katika Jangwa la Sinai.

65 Kwa maanaBwanaalikuwa amewaambia hao Waisraeli hakika wangekufa huko jangwani, wala hakuna mmoja wao aliyeachwa, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Yoshua mwana wa Nuni.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/26-c783ac4c556bd1e9e1e21a144754f30c.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 27

Binti Wa Selofehadi

1 Binti za Selofehadi mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, walikuwa wa koo za Manase mwana wa Yosefu. Majina ya hao binti yalikuwa Mahla, Noa, Hogla, Milka na Tirsa. Walikaribia

2 ingilio la Hema la Kukutania na kusimama mbele ya Mose, kuhani Eleazari, viongozi na kusanyiko lote, wakasema,

3 “Baba yetu alikufa jangwani. Hakuwa miongoni mwa wafuasi wa Kora, ambao walifungamana pamoja dhidi yaBwana, lakini alikufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe na hakuacha wana.

4 Kwa nini jina la baba yetu lifutike kutoka ukoo wake kwa sababu hakuwa na mwana? Tupatie milki miongoni mwa ndugu za baba yetu.”

5 Kwa hiyo Mose akalileta shauri lao mbele zaBwana,

6 nayeBwanaakamwambia Mose,

7 “Wanachosema binti za Selofehadi ni sawa. Ni lazima kwa hakika uwape milki kama urithi miongoni mwa ndugu za baba yao, na kubadili urithi wa baba yao uwe wao.

8 “Waambie Waisraeli, ‘Ikiwa mtu atakufa naye hakuacha mwana, utampa binti yake urithi wake.

9 Ikiwa hana binti, wape ndugu zake wa kiume urithi wake.

10 Ikiwa hana ndugu wa kiume toa urithi wake kwa ndugu za baba yake.

11 Ikiwa baba yake hakuwa na ndugu wa kiume, toa urithi wake kwa ndugu wa karibu katika ukoo wake, ili aumiliki. Hili litakuwa dai la sheria kwa Waisraeli, kamaBwanaalivyomwamuru Mose.’ ”

Yoshua Kuchukua Nafasi Ya Mose

12 KishaBwanaakamwambia Mose, “Panda juu ya mlima huu katika kilele cha Abarimu uione nchi ambayo nimewapa Waisraeli.

13 Baada ya kuiona, wewe pia utakusanywa pamoja na watu wako kama ndugu yako Aroni alivyokusanywa,

14 kwa kuwa jumuiya ilipoasi amri yangu kwenye maji katika Jangwa la Sini, wakati jumuiya ilipogombana nami, nyote wawili mliacha kuitii amri yangu ya kuniheshimu kama mtakatifu mbele ya macho yao.” (Haya yalikuwa maji ya Meriba huko Kadeshi, katika Jangwa la Sini.)

15 Mose akamwambiaBwana,

16 “Bwana, Mungu wa roho zote za wanadamu, na amteue mtu juu ya jumuiya hii

17 ili atoke na kuingia mbele yao, atakayewaongoza katika kutoka kwao na kuingia kwao, ili watu waBwanawasiwe kama kondoo wasio na mchungaji.”

18 Kwa hiyoBwanaakamwambia Mose, “Mchukue Yoshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho yuko ndani yake, uweke mkono juu yake.

19 Msimamishe mbele ya kuhani Eleazari pamoja na kusanyiko lote, umpe maagizo mbele yao.

20 Mpe sehemu ya mamlaka yako ili jumuiya yote ya Waisraeli ipate kumtii.

21 Atasimama mbele ya kuhani Eleazari, ambaye atapokea maamuzi kwa ajili yake, kwa kuuliza mbele zaBwanakwa ile Urimu.Kwa amri yake, yeye na jumuiya yote ya Waisraeli watatoka, na kwa amri yake, wataingia.”

22 Mose akafanya kamaBwanaalivyomwagiza. Akamtwaa Yoshua na kumsimamisha mbele ya kuhani Eleazari na kusanyiko lote.

23 Kisha akaweka mikono yake juu ya kichwa cha Yoshua na kumpa maagizo, kama vileBwanaalivyoelekeza kupitia kwa Mose.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/27-24eba0022fa5a222294381f74ed8d63a.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 28

Sadaka Za Kila Siku

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Wape Waisraeli agizo hili na uwaambie: ‘Hakikisheni kwamba mnaniletea mimi kwa wakati uliowekwa chakula kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, kama harufu nzuri ya kupendeza.’

3 Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtoleaBwana: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku.

4 Andaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni,

5 kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efaya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hiniya mafuta ya zeituni.

6 Hii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa moto.

7 Sadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwaBwanamahali patakatifu.

8 Andaa yule mwana-kondoo wa pili jioni, pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kama ulivyofanya kwa ile sadaka nyingine ya asubuhi. Hii ni sadaka iliyotolewa kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

Sadaka Za Sabato

9 “ ‘Siku ya Sabato, utatoa sadaka ya wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari pamoja na sadaka yake ya kinywaji na sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu mbili za kumi za efaza unga laini uliochanganywa na mafuta.

10 Hii ni sadaka ya kuteketezwa itakayotolewa kwa ajili ya kila Sabato, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya kinywaji.

Sadaka Za Kila Mwezi

11 “ ‘Siku ya kwanza ya kila mwezi, mtamleteaBwanasadaka ya kuteketezwa ya fahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasiokuwa na dosari.

12 Pamoja na kila fahali, kutakuwa na sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa,uliochanganywa na mafuta, pamoja na kondoo dume mmoja, sadaka ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta;

13 pamoja na kila mwana-kondoo, sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta. Hii ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri, sadaka ya kuteketezwa iliyotolewa kwa moto kwaBwana.

14 Pamoja na kila fahali kutakuwa na sadaka ya kinywaji nusu ya hiniya divai; pamoja na kila kondoo dume, theluthi moja ya hini,na pamoja na kila mwana-kondoo robo hini. Hii ni sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi itakayotolewa kila mwandamo wa mwezi kwa mwaka.

15 Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwaBwanakama sadaka ya dhambi.

Pasaka

16 “ ‘Katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, itafanyika Pasaka yaBwana.

17 Katika siku ya kumi na tano ya mwezi huo itakuwa sikukuu; kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu.

18 Katika siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu, msifanye kazi za kawaida.

19 Leteni mbele zaBwanasadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo dume saba wenye umri wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

20 Pamoja na kila fahali, andaa sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa;

21 pia pamoja na kila mmoja wa wale wana-kondoo saba, andaa sehemu ya kumi ya efa.

22 Pia mtoe beberu mmoja kama sadaka ya dhambi ambaye atafanya upatanisho kwa ajili yenu.

23 Andaa hizi licha ya zile sadaka za kawaida za kuteketezwa za kila asubuhi.

24 Kwa njia hii andaa chakula cha sadaka ya kuteketezwa kila siku, kwa siku saba kama harufu nzuri impendezayoBwana. Hii itaandaliwa licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa ya kila siku pamoja na sadaka yake ya kinywaji.

25 Siku ya saba mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida.

Sikukuu Ya Majuma

26 “ ‘Siku ya malimbuko, mnapomleteaBwanasadaka ya nafaka mpya wakati wa Sikukuu ya Majuma, mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida.

27 Mlete sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na pia wana-kondoo saba wenye umri wa mwaka mmoja, kama harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

28 Pamoja na kila fahali itatolewa sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini;

29 na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba.

30 Ongeza beberu mmoja kwa kufanya upatanisho kwa ajili yenu.

31 Andaa hizi sadaka pamoja na sadaka zake za vinywaji, kuwa nyongeza ya sadaka za kawaida za kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka. Hakikisha kuwa wanyama hao hawana dosari.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/28-c47f33263bb0d321271ec9fcdcc0debe.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 29

Sikukuu Ya Tarumbeta

1 “ ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu na msifanye kazi ya kawaida. Ni siku kwa ajili yenu ya kupiga tarumbeta.

2 Mtatayarisha sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri impendezayoBwanaya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

3 Pamoja na fahali, andaeni sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume, andaa unga sehemu ya kumi mbili za efa;

4 na pamoja na wana-kondoo saba kila mmoja aandaliwe na sehemu ya kumi ya efa ya unga.

5 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi kufanya upatanisho kwa ajili yenu.

6 Hivi ni nyongeza ya sadaka za kuteketezwa kila mwezi na kila siku pamoja na sadaka zake za nafaka na sadaka za vinywaji kama ilivyoainishwa. Ni sadaka zinazotolewa kwaBwanakwa moto, harufu inayopendeza.

Siku Ya Upatanisho

7 “ ‘Kwenye siku ya kumi ya mwezi huu wa saba mtakuwa na kusanyiko takatifu. Mtajikana wenyewe na msifanye kazi.

8 Toeni sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendezaBwana.

9 Pamoja na fahali, andaeni sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini;

10 na kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba andaa sehemu ya kumi ya unga laini kwa kila mmoja.

11 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho, na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya nafaka, na sadaka zake za vinywaji.

Sikukuu Ya Vibanda

12 “ ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu, na hamtafanya kazi za kawaida. Adhimisheni sikukuu kwaBwanakwa siku saba.

13 Toeni sadaka ya kuteketezwa mafahali wachanga kumi na watatu, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari, kama harufu nzuri inayompendezaBwana.

14 Pamoja na hao mafahali kumi na watatu, kila mmoja aandaliwe na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi tatu za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; kwa kondoo dume wawili, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi mbili za efa za unga laini;

15 na kwa wana-kondoo kumi na wanne, kila mmoja aandaliwe sehemu ya kumi ya efa ya unga laini.

16 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka ya vinywaji.

17 “ ‘Katika siku ya pili andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

18 Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa.

19 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

20 “ ‘Katika siku ya tatu andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

21 Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa.

22 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

23 “ ‘Katika siku ya nne andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

24 Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa.

25 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

26 “ ‘Katika siku ya tano andaeni mafahali tisa, kondoo dume wawili na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

27 Pamoja na mafahali, kondoo dume na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za kinywaji kulingana na idadi iliyoainishwa.

28 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi katika nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka pamoja na sadaka ya kinywaji.

29 “ ‘Katika siku ya sita andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

30 Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa.

31 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

32 “ ‘Katika siku ya saba andaeni mafahali wachanga kumi na wawili, kondoo dume wawili, na wana-kondoo kumi na wanne wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

33 Pamoja na mafahali, kondoo dume, na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa.

34 Weka beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, kwa nyongeza ya kawaida ya sadaka ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka, pamoja na sadaka zao za vinywaji.

35 “ ‘Katika siku ya nane mtakuwa na kusanyiko, na msifanye kazi ya kawaida.

36 Toeni sadaka ya kuteketezwa kama harufu nzuri inayompendezaBwana, sadaka ya kuteketezwa ya fahali mmoja, kondoo dume mmoja, na wana-kondoo dume saba wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.

37 Pamoja na fahali, kondoo dume na wana-kondoo, andaeni sadaka zao za nafaka, na sadaka za vinywaji, kulingana na idadi iliyoainishwa.

38 Ongeza beberu mmoja kama sadaka ya dhambi, katika nyongeza ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, na sadaka yake ya nafaka pamoja na sadaka ya kinywaji.

39 “ ‘Zaidi ya kile unachoweka nadhiri na sadaka zenu za hiari, andaeni hizi kwa ajili yaBwanakwenye sikukuu zenu zilizoamriwa: sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za nafaka, sadaka za vinywaji, pamoja na sadaka zenu za amani.’ ”

40 Mose akawaambia Waisraeli yale yoteBwanaalimwagiza.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/29-d3ae3ab60847480027a5403b20baff68.mp3?version_id=1627—