Categories
Hesabu

Hesabu 10

Tarumbeta Za Fedha

1 Bwanaakamwambia Mose:

2 “Tengeneza tarumbeta mbili za fedha ya kufua, uzitumie kwa kuita jumuiya pamoja na wakati wa kuvunja makambi ili kuondoka.

3 Tarumbeta zote mbili zikipigwa, jumuiya yote itakusanyika mbele yako katika ingilio la Hema la Kukutania.

4 Kama tarumbeta moja tu ikipigwa, viongozi, yaani wakuu wa koo za Israeli, ndio watakaokusanyika mbele yako.

5 Wakati mlio wa kujulisha hatari ukipigwa, makabila yaliyo na makambi upande wa mashariki yataondoka.

6 Ukisikika mlio wa pili wa jinsi hiyo, walioko kwenye makambi ya kusini wataondoka. Mlio huo wa kujulisha hatari utakuwa ishara ya kuondoka.

7 Ili kukusanya kusanyiko, piga tarumbeta zote, lakini siyo kwa mlio wa kujulisha hatari.

8 “Wana wa Aroni, makuhani, ndio watakaopiga hizo tarumbeta. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu na kwa vizazi vijavyo.

9 Wakati mtakapopigana vita katika nchi yenu wenyewe dhidi ya adui anayewaonea, piga tarumbeta kwa mlio wa kujulisha hatari. Ndipo utakumbukwa naBwanaMungu wenu na kuokolewa kutoka kwa adui zenu.

10 Pia nyakati za furaha yenu, yaani sikukuu zenu zilizoamriwa na sikukuu za Mwezi Mwandamo, mtapiga tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za amani, nazo zitakuwa ukumbusho kwa ajili yenu mbele za Mungu wenu. Mimi ndimiBwana, Mungu wenu.”

Waisraeli Waondoka Sinai

11 Katika siku ya ishirini ya mwezi wa pili wa mwaka wa pili, wingu liliinuka kutoka juu ya maskani ya Ushuhuda.

12 Ndipo Waisraeli wakaondoka kutoka Jangwa la Sinai wakasafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine mpaka wingu lilipotua katika Jangwa la Parani.

13 Waliondoka kwa mara ya kwanza kwa agizo laBwanakupitia kwa Mose.

14 Vikosi vya kambi ya Yuda vilitangulia kwanza chini ya alama yao. Nashoni mwana wa Aminadabu alikuwa kiongozi wao.

15 Nethaneli mwana wa Suari alikuwa kiongozi wa kabila la Isakari,

16 naye Eliabu mwana wa Heloni alikuwa kiongozi wa kabila la Zabuloni.

17 Ndipo Maskani iliposhushwa, nao wana wa Gershoni na wana wa Merari ambao waliibeba wakaondoka.

18 Vikosi vya kambi ya Reubeni vilifuata, chini ya alama yao. Elisuri mwana wa Shedeuri alikuwa kiongozi wao.

19 Shelumieli mwana wa Surishadai aliongoza kikosi cha kabila la Simeoni,

20 naye Eliasafu mwana wa Deueli aliongoza kikosi cha kabila la Gadi.

21 Kisha Wakohathi wakaondoka, wakichukua vitu vitakatifu. Maskani ilikuwa isimamishwe kabla wao hawajafika.

22 Vikosi vya kambi ya Efraimu vilifuata, chini ya alama yao. Elishama mwana wa Amihudi alikuwa kiongozi wao.

23 Gamalieli mwana wa Pedasuri aliongoza kikosi cha kabila la Manase,

24 naye Abidani mwana wa Gideoni alikuwa kiongozi wa kikosi cha kabila la Benyamini.

25 Mwishowe, kama kikosi cha nyuma cha ulinzi wa vikosi vyote, vikosi vya kambi ya Dani viliondoka chini ya alama yao. Ahiezeri mwana wa Amishadai alikuwa kiongozi wao.

26 Pagieli mwana wa Okrani aliongoza kikosi cha kabila la Asheri,

27 naye Ahira mwana wa Enani aliongoza kikosi cha kabila la Naftali.

28 Huu ndio ulikuwa utaratibu wa kuondoka wa vikosi vya Waisraeli walipokuwa wanaondoka.

29 Basi Mose akamwambia Hobabu mwana wa Reueli, Mmidiani, mkwewe Mose, “Tunaondoka kwenda mahali ambapoBwanaamesema ‘Nitawapa ninyi mahali hapo.’ Twende pamoja nasi tutakutendea mema, kwa maanaBwanaameahidi mambo mema kwa Israeli.”

30 Akajibu, “Hapana, sitakwenda; nitarudi kwenye nchi yangu mwenyewe na watu wangu mwenyewe.”

31 Lakini Mose akasema, “Tafadhali usituache. Wewe unajua mahali ambapo yatupasa kupiga kambi jangwani, nawe unaweza kuwa macho yetu.

32 Ikiwa utafuatana nasi, tutashirikiana nawe mema yoyote tutakayopewa naBwana.”

33 Hivyo waliondoka kutoka mlima waBwana, nao wakasafiri kwa siku tatu. Sanduku la Agano laBwanaliliwatangulia kwa zile siku tatu ili kuwatafutia mahali pa kupumzika.

34 Wingu laBwanalilikuwa juu yao wakati wa mchana walipoondoka kambini.

35 Wakati wowote Sanduku lilipoondoka, Mose alisema,

“EeBwana, inuka!

Watesi wako na watawanyike;

adui zako na wakimbie mbele zako.”

36 Wakati wowote Sanduku liliposimama, alisema,

“EeBwana, rudi,

kwa maelfu ya Waisraeli wasiohesabika.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/10-d7a0b35e516f26690d4d8c62f3451e7b.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 11

Moto Kutoka Kwa Bwana

1 Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwaBwana, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwaBwanaukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi.

2 Watu walipomlilia Mose, akamwombaBwana, nao moto ukazimika.

3 Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera,kwa sababu moto kutoka kwaBwanauliwaka miongoni mwao.

Kware Kutoka Kwa Bwana

4 Umati wa watu wenye zogo waliokuwa miongoni mwao walitamani sana chakula kingine, Waisraeli wakaanza kulia tena na kusema, “Laiti tungekuwa na nyama tule!

5 Tunakumbuka wale samaki tuliokula huko Misri bila gharama, pia yale matango, matikitimaji, mboga, vitunguu, na vitunguu saumu.

6 Lakini sasa tumepoteza hamu ya chakula; hatuoni kitu kingine chochote isipokuwa hii mana!”

7 Mana ilifanana kama mbegu za giligilani, nayo ilikuwa na rangi ya manjano iliyopauka.

8 Hao watu walikwenda kukusanya, kisha waliisaga kwa mawe ya kusagia ya mkono au kuitwanga kwenye vinu. Waliipika vyunguni au kutengeneza maandazi. Ladha yake ilikuwa kama kitu kilichotengenezwa kwa mafuta ya zeituni.

9 Umande ulipoanguka kambini wakati wa usiku, pia mana ilianguka pamoja nao.

10 Mose akasikia watu wa kila jamaa wakilia, kila mmoja kwenye mlango wa hema lake.Bwanaakakasirika mno, naye Mose akafadhaika.

11 AkamuulizaBwana, “Kwa nini umeleta taabu hii juu ya mtumishi wako? Nimekufanyia nini cha kukuchukiza hata ukaweka mzigo huu wa watu hawa wote juu yangu?

12 Je, watu hawa wote mimi ndiye niliyewatungisha mimba? Je, ni mimi niliyewazaa? Kwa nini unaniambia niwachukue mikononi mwangu, kama vile mlezi abebavyo mtoto mchanga, hadi kwenye nchi uliyowaahidi baba zao?

13 Nitapata wapi nyama kwa ajili ya watu wote hawa? Wanaendelea kunililia wakisema, ‘Tupe nyama tule!’

14 Mimi siwezi kuwabeba watu hawa wote peke yangu, mzigo ni mzito sana kwangu.

15 Kama hivi ndivyo unavyonitendea, uniue sasa hivi, yaani kama nimepata kibali machoni pako, wala usiniache nione maangamizi yangu mwenyewe.”

16 Bwanaakamwambia Mose: “Niletee wazee sabini wa Israeli, unaowafahamu kama viongozi na maafisa miongoni mwa watu. Walete katika Hema la Kukutania, ili waweze kusimama huko pamoja nawe.

17 Nami nitashuka na kusema nawe huko. Nami nitachukua sehemu ya Roho iliyo juu yako na kuiweka juu yao. Watakusaidia kubeba mzigo wa watu hao ili usije ukaubeba peke yako.

18 “Waambie hao watu: ‘Jiwekeni wakfu wenyewe kwa ajili ya kesho, wakati mtakapokula nyama.Bwanaaliwasikia mlipolia, mkisema, “Laiti tungekuwa na nyama tule! Tulikuwa na hali nzuri zaidi katika nchi ya Misri!” SasaBwanaatawapa nyama, nanyi mtaila.

19 Hamtaila kwa siku moja tu, au siku mbili, au tano, kumi au siku ishirini,

20 bali kwa mwezi mzima mpaka iwatokee puani, nanyi mtaichukia kabisa, kwa kuwa mmemkataaBwana, ambaye yupo miongoni mwenu, nanyi mmelia mbele zake, mkisema, “Hivi kwa nini tulitoka Misri?” ’ ”

21 Lakini Mose alisema, “Mimi niko hapa miongoni mwa watu 600,000 wanaotembea kwa miguu, nawe umesema, ‘Nitawapa nyama ya kula kwa mwezi mzima!’

22 Je, wangeweza kupata nyama ya kuwatosha hata kama makundi ya kondoo na ya ngʼombe yangechinjwa kwa ajili yao? Je, wangetosheka hata kama samaki wote wa baharini wangevuliwa kwa ajili yao?”

23 Bwanaakamjibu Mose, “Je, mkono waBwanani mfupi sana? Sasa utaona kama jambo nililolisema litatimizwa kwa ajili yako au la.”

24 Kwa hiyo Mose akatoka na kuwaambia watu lile ambaloBwanaalikuwa amesema. Akawakusanya wazee wao sabini, akawasimamisha kuzunguka Hema.

25 KishaBwanaakashuka katika wingu na kunena na Mose, naye akachukua sehemu ya Roho iliyokuwa juu ya Mose na kuiweka juu ya wale wazee sabini. Roho aliposhuka juu yao, wakatoa unabii, lakini hawakufanya hivyo tena.

26 Lakini, watu wawili, ambao majina yao ni Eldadi na Medadi, walibaki kambini. Walikuwa wameorodheshwa miongoni mwa wale wazee sabini, lakini hawakutoka kwenda kwenye Hema. Lakini Roho pia alishuka juu yao, nao wakatabiri huko kambini.

27 Mwanaume mmoja kijana alikimbia na kumwambia Mose, “Eldadi na Medadi wanatoa unabii kambini.”

28 Yoshua mwana wa Nuni, ambaye alikuwa msaidizi wa Mose tangu ujana wake, akajibu akasema, “Mose bwana wangu, wanyamazishe!”

29 Lakini Mose akajibu, “Je, unaona wivu kwa ajili yangu? Ningetamani watu wote waBwanawangekuwa manabii na kwambaBwanaangeweka Roho yake juu yao!”

30 Ndipo Mose na wale wazee wa Israeli wakarudi kambini.

31 Kisha ukatokea upepo kutoka kwaBwana, nao ukawaletea kware kutoka baharini. Ukawaangusha kwenye eneo lote linalozunguka kambi na kujaa ardhini kimo cha mita moja hivi kutoka ardhini kwenye eneo la umbali wa mwendo wa siku moja kila upande.

32 Mchana kutwa na usiku kucha pamoja na siku nzima iliyofuata watu walitoka kwenda kuokota kware. Hakuna mtu yeyote aliyekusanya chini ya homeri kumi.Kisha wakazianika kuzunguka kambi yote.

33 Lakini walipokuwa wakila nyama, ilipokuwa ingali kati ya meno yao na kabla hawajamaliza kula, hasira yaBwanaikawaka dhidi ya watu, naye akawapiga kwa tauni.

34 Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Kibroth-Hataava,kwa sababu huko ndiko walipowazika watu ambao walitamani sana chakula kingine.

35 Kutoka Kibroth-Hataava watu wakasafiri mpaka Haserothi na kukaa huko.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/11-58a1d45624f44c87cc2c9f6eeef0d02d.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 12

Miriamu Na Aroni Wampinga Mose

1 Miriamu na Aroni walianza kuzungumza dhidi ya Mose kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi.

2 Waliuliza, “Je,Bwanaamesema kupitia Mose peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?” NayeBwanaakasikia hili.

3 (Basi Mose alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine yeyote katika uso wa dunia.)

4 GhafulaBwanaakawaambia Mose, Aroni na Miriamu, “Njooni katika Hema la Kukutania, ninyi nyote watatu.” Kwa hiyo wote watatu wakaenda.

5 KishaBwanaakashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye ingilio la Hema, akawaita Aroni na Miriamu. Wakati wote wawili waliposogea mbele,

6 Bwanaakasema, “Sikilizeni maneno yangu:

“Akiwapo nabii waBwanamiongoni mwenu,

nitajifunua kwake kwa maono,

nitanena naye katika ndoto.

7 Lakini sivyo kwa mtumishi wangu Mose;

yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.

8 Kwake nitanena naye uso kwa uso,

waziwazi wala si kwa mafumbo;

yeye ataona umbo laBwana.

Kwa nini basi ninyi hamkuogopa

kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Mose?”

9 Hasira yaBwanaikawaka dhidi yao, akawaacha.

10 Wakati hilo wingu liliinuka kutoka juu ya Hema, Miriamu akawa tayari ana ukoma, mweupe kama theluji. Aroni akamgeukia, akaona ana ukoma.

11 Kisha Aroni akamwambia Mose, “Tafadhali, bwana wangu, usituhesabie dhambi hii ambayo tumeifanya kwa upumbavu.

12 Usimwache awe kama mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa mfu, ambaye nusu ya mwili wake imeharibika hapo atokapo katika tumbo la mama yake.”

13 Hivyo Mose akamliliaBwanaakisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!”

14 Bwanaakamjibu Mose, “Je, kama baba yake angemtemea usoni, asingeona aibu kwa siku saba? Mfungie nje ya kambi kwa siku saba; baada ya hapo anaweza kurudishwa kambini.”

15 Kwa hiyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba, nao watu hawakuendelea na safari mpaka aliporudishwa kambini.

16 Baada ya hayo, watu waliondoka Haserothi, wakapiga kambi katika Jangwa la Parani.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/12-ca41a1439e1a5ac5eca1313dc61c6e01.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 13

Kupeleleza Kanaani

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Watume baadhi ya watu wakaipeleleze nchi ya Kanaani, ambayo ninawapa Waisraeli. Kutoka kwa kila kabila la baba zao, tuma mmoja wa viongozi wao.”

3 Hivyo kwa agizo laBwanaMose akawatuma kutoka Jangwa la Parani. Wote walikuwa viongozi wa Waisraeli.

4 Haya ndiyo majina yao:

kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;

5 kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;

6 kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;

7 kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu;

8 kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;

9 kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu;

10 kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi,

11 kutoka kabila la Manase (kabila la Yosefu), Gadi mwana wa Susi;

12 kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali;

13 kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli;

14 kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi;

15 kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki.

16 Haya ndiyo majina ya watu ambao Mose aliwatuma kuipeleleza nchi. (Mose akampa Hoshea mwana wa Nuni jina Yoshua.)

17 Mose alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, “Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya vilima.

18 Mwone nchi ni ya namna gani, na kama watu waishio humo wana nguvu au ni wadhaifu, iwapo ni wachache au wengi.

19 Wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome?

20 Ardhi iko aje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadiri mwezavyo kuleta baadhi ya matunda ya nchi.” (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.)

21 Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo-Hamathi.

22 Wakapanda kupitia Negebu hadi wakafika Hebroni, mahali ambapo Ahimani, Sheshai na Talmai, wazao wa Anaki, waliishi. (Hebroni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya mji wa Soani ulioko Misri.)

23 Walipofika katika Bonde la Eshkoli, walivunja tawi lililokuwa na kishada kimoja cha zabibu. Wawili wao wakalichukua lile tawi kwenye mti, pamoja na komamanga na tini.

24 Eneo lile likaitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya kile kishada cha zabibu ambacho Waisraeli walikikata huko.

25 Mwishoni mwa siku arobaini wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.

Taarifa Juu Ya Upelelezi

26 Wakarudi kwa Mose, Aroni na jumuiya yote ya Waisraeli huko Kadeshi kwenye Jangwa la Parani. Hapo ndipo walipotoa habari kwao na kwa kusanyiko lote na kuwaonyesha matunda ya hiyo nchi.

27 Wakampa Mose taarifa hii: “Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo inatiririka maziwa na asali! Hili hapa tunda lake.

28 Lakini watu wanaoishi huko ni wenye nguvu, na miji yao ina ngome na ni mikubwa sana. Huko tuliona hata wazao wa Anaki.

29 Waamaleki wanaishi Negebu; Wahiti, Wayebusi na Waamori wanaishi katika nchi ya vilima; nao Wakanaani wanaishi karibu na bahari na kando ya Yordani.”

30 Kisha Kalebu akawanyamazisha watu mbele ya Mose na kusema, “Imetupasa kupanda na kuimiliki nchi, kwa maana hakika tunaweza kufanya hivyo.”

31 Lakini watu waliokuwa wamepanda pamoja naye wakasema, “Hatuwezi kuwashambulia wale watu; wana nguvu kutuliko sisi.”

32 Wakaeneza taarifa mbaya miongoni mwa Waisraeli kuhusu nchi waliyoipeleleza. Wakasema, “Nchi tuliyoipeleleza hula watu waishio ndani yake. Watu wote tuliowaona huko ni majitu.

33 Tuliwaona Wanefili huko (wazao wa Anaki wanatokana na Wanefili.) Tulijiona kama panzi machoni petu wenyewe, nao ndivyo walivyotuona.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/13-08507c2a8a2cf8b620a0a47e1763ca28.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 14

Watu Wanaasi

1 Usiku ule watu wote wa jumuiya walipaza sauti zao na kulia kwa sauti kuu.

2 Waisraeli wote wakanungʼunika dhidi ya Mose na Aroni, nalo kusanyiko lote wakawaambia, “Laiti tungekuwa tumefia humo nchi ya Misri! Au humu kwenye hili jangwa!

3 Kwa niniBwanaanatuleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watachukuliwa kama nyara. Je, isingekuwa bora kwetu kurudi Misri?”

4 Wakasemezana wao kwa wao, “Inatupasa kumchagua kiongozi na kurudi Misri.”

5 Ndipo Mose na Aroni wakaanguka kifudifudi mbele ya kusanyiko lote la Kiisraeli lililokusanyika hapo.

6 Yoshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwa watu wale waliokwenda kuipeleleza nchi, wakararua nguo zao,

7 wakasema na kusanyiko lote la Kiisraeli, wakawaambia, “Nchi tuliyopita katikati yake na kuipeleleza ni nzuri sana sana.

8 IkiwaBwanaanapendezwa nasi, atatuongoza kuingia katika nchi ile, nchi itiririkayo maziwa na asali, naye atatupa nchi hiyo.

9 Ila tu msimwasiBwana. Wala msiwaogope watu wa nchi hiyo, kwa sababu tutawameza. Ulinzi wao umeondoka, lakiniBwanayupo pamoja nasi. Msiwaogope.”

10 Lakini kusanyiko lote likazungumza juu ya kuwapiga kwa mawe. Ndipo utukufu waBwanaukaonekana katika Hema la Kukutania kwa Waisraeli wote.

11 Bwanaakamwambia Mose, “Watu hawa watanidharau mpaka lini? Wataendelea kukataa kuniamini mimi mpaka lini, ingawa nimetenda ishara za miujiza miongoni mwao?

12 Nitawapiga kwa tauni na kuwaangamiza, lakini nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa lenye nguvu kuliko wao.”

13 Mose akamwambiaBwana, “Ndipo Wamisri watasikia juu ya jambo hili! Kwa uweza wako uliwapandisha watu hawa kutoka miongoni mwao.

14 Nao watawaambia wenyeji wa nchi hii jambo hili. Wao tayari wameshasikia kwamba wewe, EeBwana, upo pamoja na watu hawa, na kuwa wewe, EeBwana, umeonekana uso kwa uso, nalo wingu lako hukaa juu yao. Tena wewe unawatangulia kwa nguzo ya wingu mchana na kwa nguzo ya moto usiku.

15 Ikiwa utawaua watu hawa wote mara moja, mataifa ambayo yamesikia taarifa hii kukuhusu wewe watasema,

16 ‘Bwanaalishindwa kuwaingiza watu hawa katika nchi aliyowaahidi kwa kiapo; hivyo akawaua jangwani.’

17 “Basi sasa nguvu za Bwana na zionekane, sawasawa na vile ulivyosema:

18 ‘Bwanasi mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo na mwenye kusamehe dhambi na uasi. Lakini haachi kumwadhibu mwenye hatia, huadhibu watoto kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne.’

19 Kwa kadiri ya upendo wako mkuu, usamehe dhambi ya watu hawa, kama vile ulivyowasamehe tangu wakati walitoka Misri mpaka sasa.”

20 Bwanaakajibu, “Nimewasamehe kama ulivyoomba.

21 Hata hivyo, kwa hakika kama niishivyo, na kwa hakika kama utukufu waBwanauijazavyo dunia yote,

22 hakuna hata mmoja wa watu hawa ambao waliuona utukufu wangu na ishara za miujiza niliyotenda huko Misri na huko jangwani, lakini ambaye hakunitii na akanijaribu mara hizi kumi,

23 hakuna hata mmoja wao atakayeona nchi niliyowaahidi baba zao kwa kiapo. Hakuna hata mmoja ambaye amenidharau atakayeiona.

24 Lakini kwa sababu mtumishi wangu Kalebu ana roho ya tofauti na ananifuata kwa moyo wote, nitamwingiza katika nchi aliyoiendea, nao wazao wake watairithi.

25 Kwa kuwa Waamaleki na Wakanaani wanaishi katika mabonde, kesho geukeni mwelekee jangwani kwa kufuata njia iendayo Bahari ya Shamu.”

26 Bwanaakamwambia Mose na Aroni:

27 “Jumuiya hii ovu itanungʼunika dhidi yangu hadi lini? Nimesikia malalamiko ya hawa Waisraeli wanaonungʼunika.

28 Hivyo waambie, ‘Hakika kama niishivyo, asemaBwana, nitawafanyia vitu vilevile nilivyosikia mkisema:

29 Kila mmoja wenu mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi ambaye alihesabiwa na amenungʼunika dhidi yangu, miili yenu itaanguka katika jangwa hili.

30 Hakuna hata mmoja wenu atakayeingia katika nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kuwa makao yenu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.

31 Lakini watoto wenu ambao mlisema watachukuliwa kama mateka, nitawaingiza humo ili waifurahie nchi ambayo ninyi mmeikataa.

32 Lakini ninyi, miili yenu itaanguka katika jangwa hili.

33 Watoto wenu watakuwa wachungaji wa mifugo hapa kwa miaka arobaini, wakiteseka kwa ajili ya kukosa uaminifu kwenu, hadi mwili wa mtu wenu wa mwisho ulale katika jangwa hili.

34 Kwa miaka arobaini, mwaka mmoja kwa kila siku katika zile siku arobaini mlizoipeleleza nchi, mtateseka kwa ajili ya dhambi zenu, na kujua jinsi ilivyo vibaya kunifanya mimi kuwa adui yenu.’

35 MimiBwananimesema, na hakika nitafanya mambo haya kwa jumuiya hii yote ovu, ambayo imefungamana pamoja dhidi yangu. Watakutana na mwisho wao katika jangwa hili; hapa ndipo watafia.”

36 Hivyo watu wale ambao Mose alikuwa amewatuma kuipeleleza nchi, waliorudi na kuifanya jumuiya nzima kunungʼunika dhidi ya Mose kwa kueneza taarifa mbaya kuhusu hiyo nchi:

37 watu hawa waliohusika kueneza taarifa mbaya kuhusu hiyo nchi walipigwa na kuanguka kwa tauni mbele zaBwana.

38 Miongoni mwa watu waliokwenda kuipeleleza hiyo nchi, ni Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune peke yao waliosalia.

39 Mose alipotoa taarifa hii kwa Waisraeli wote, waliomboleza kwa uchungu.

40 Mapema asubuhi siku iliyofuata walipanda juu kuelekea kwenye nchi ya vilima virefu, wakasema, “Tumetenda dhambi. Tutakwea mpaka mahaliBwanaalipotuahidi.”

41 Lakini Mose akasema, “Kwa nini hamtii amri yaBwana? Jambo hili halitafanikiwa!

42 Msipande juu, kwa kuwaBwanahayupo pamoja nanyi. Mtashindwa na adui zenu,

43 kwa kuwa Waamaleki na Wakanaani watapambana nanyi huko. Kwa sababu mmemwachaBwana, hatakuwa pamoja nanyi, ninyi mtaanguka kwa upanga.”

44 Hata hivyo, kwa kiburi chao walipanda juu kuelekea nchi ya vilima virefu, ijapokuwa Mose hakutoka kambini wala Sanduku la Agano laBwana.

45 Ndipo Waamaleki na Wakanaani walioishi katika hiyo nchi ya vilima wakateremka na kuwashambulia, wakawapiga njia yote hadi Horma.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/14-63bb5135a58486d93ccd99ed8ecc6bce.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 15

Sadaka Za Nyongeza

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Baada ya ninyi kuingia katika nchi ninayowapa kama nyumbani,

3 nanyi mkitoa sadaka za kuteketezwa kwa moto, kutoka makundi ya ngʼombe au kondoo, kama harufu nzuri inayompendezaBwana, ikiwa ni sadaka za kuteketezwa au dhabihu, kwa ajili ya nadhiri maalum ama sadaka ya hiari au sadaka ya sikukuu zenu,

4 ndipo yeye aletaye sadaka yake ataiweka mbele zaBwanasadaka ya nafaka, sehemu ya kumi ya efaya unga laini uliochanganywa na robo ya hiniya mafuta.

5 Pamoja na kila mwana-kondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, andaa robo ya hini ya divai kwa sadaka ya kinywaji.

6 “ ‘Pamoja na kondoo dume andaa sadaka ya nafaka ya sehemu mbili za kumi za efaza unga laini uliochanganywa na theluthi mojaya hini ya mafuta,

7 na theluthi moja ya hini ya divai kama sadaka ya kinywaji. Vitoe kama harufu nzuri inayompendezaBwana.

8 “ ‘Unapoandaa fahali mchanga kama sadaka ya kuteketezwa au dhabihu, kwa ajili ya nadhiri maalum au sadaka ya amani kwaBwana,

9 leta pamoja na huyo fahali sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efauliochanganywa na nusu ya hiniya mafuta.

10 Pia utaleta nusu ya hini ya divai kama sadaka ya kinywaji. Itakuwa sadaka iliyoteketezwa kwa moto, harufu nzuri inayompendezaBwana.

11 Kila fahali au kondoo dume, kila mwana-kondoo au mbuzi mchanga, atatayarishwa kwa njia hii.

12 Fanyeni hivi kwa ajili ya kila mmoja, kwa kadiri ya wingi wa mtakavyoandaa.

13 “ ‘Kila mmoja ambaye ni mzawa ni lazima afanye vitu hivi kwa njia hii hapo aletapo sadaka ya kuteketezwa kwa moto kama harufu nzuri inayompendezaBwana.

14 Kwa vizazi vijavyo, wakati wowote mgeni au mtu mwingine yeyote anayeishi miongoni mwenu aletapo sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu nzuri ya kumpendezaBwana, ni lazima afanye sawasawa kabisa na jinsi mnavyofanya ninyi.

15 Jumuiya itakuwa na sheria hizo hizo kwenu na kwa mgeni aishiye miongoni mwenu; hii ni amri ya kudumu kwa vizazi vijavyo. Ninyi na mgeni mtakuwa sawa mbele zaBwana:

16 Sheria hizo hizo na masharti hayo hayo hayo, yatawahusu ninyi na mgeni aishiye miongoni mwenu.’ ”

17 Bwanaakamwambia Mose,

18 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi ninayowapeleka

19 nanyi mkala chakula cha nchi hiyo, toeni sehemu ya chakula hicho kama sadaka kwaBwana.

20 Toeni andazi kutoka kwa malimbuko ya chakula chenu kitokacho katika ardhi, na mkitoe kama sadaka kutoka sakafu ya kupuria nafaka.

21 Kwa vizazi vyote vijavyo hamna budi kutoa sadaka hii kwaBwanakutoka kwa malimbuko ya unga wenu.

Sadaka Kwa Ajili Ya Dhambi Isiyo Ya Makusudi

22 “ ‘Basi kama pasipo kukusudia umeshindwa kushika mojawapo katika amri hizi ambazoBwanaalimpa Mose,

23 amri yoyote yaBwanakwenu kupitia Mose, tangu siku ileBwanaalipowapa na inaendelea hadi vizazi vyote vijavyo;

24 ikiwa hili limefanyika pasipo kukusudia bila jumuiya kuwa na habari nalo, basi jumuiya yote itatoa fahali mchanga kuwa sadaka ya kuteketezwa ikiwa harufu nzuri inayompendezaBwana, pamoja na sadaka ya nafaka na ya kinywaji zilizoamriwa kwayo, na mbuzi dume kwa ajili ya sadaka ya dhambi.

25 Kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya jumuiya yote ya Kiisraeli, nao watasamehewa, kwa kuwa haikuwa makusudi nao wamemleteaBwanasadaka iliyoteketezwa kwa moto na sadaka ya dhambi kwa ajili ya kosa lao.

26 Jumuiya yote ya Kiisraeli pamoja na wageni waishio miongoni mwao watasamehewa, kwa sababu watu wote walihusika katika kosa lile lisilokusudiwa.

27 “ ‘Lakini kama mtu mmoja peke yake akitenda dhambi pasipo kukusudia, ni lazima alete mbuzi mke wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi.

28 Kuhani atafanya upatanisho mbele zaBwanakwa ajili ya yule aliyekosa kwa kufanya dhambi pasipo kukusudia, upatanisho utakapofanywa kwa ajili yake, atasamehewa.

29 Sheria hiyo moja itamhusu kila mmoja ambaye ametenda dhambi pasipo kukusudia, awe Mwisraeli mzawa ama mgeni.

30 “ ‘Lakini yeyote ambaye amefanya dhambi kwa dharau awe mzawa au mgeni, anamkufuruBwana, naye mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

31 Kwa sababu amelidharau neno laBwanana kuvunja amri zake, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali; hatia yake inabaki juu yake.’ ”

Mvunja Sabato Auawe

32 Waisraeli walipokuwa jangwani, mtu mmoja alikutwa akikusanya kuni siku ya Sabato.

33 Wale waliomkuta akikusanya kuni wakamleta kwa Mose, Aroni na kusanyiko lote,

34 nao wakamweka kifungoni, kwa sababu haikufahamika kwa wazi kwamba afanyiwe nini.

35 NdipoBwanaakamwambia Mose, “Huyo mtu ni lazima afe. Kusanyiko lote lazima limpige mawe nje ya kambi.”

36 Hivyo kusanyiko likamtoa nje ya kambi na kumpiga mawe hadi akafa, kamaBwanaalivyomwamuru Mose.

Vifundo Kwenye Mavazi

37 Bwanaakamwambia Mose,

38 “Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Kwa vizazi vyote vijavyo jifanyieni vifundo katika pindo za mavazi yenu vikiwa na uzi wa buluu kwenye kila kifundo.

39 Mtakuwa mkivitazama vifundo hivyo ili mpate kukumbuka amri zote zaBwana, ili mpate kuzitii msije mkajitia uzinzi wenyewe kwa kuzifuata tamaa za mioyo yenu na za macho yenu.

40 Ndipo mtakumbuka kuzitii amri zangu zote nanyi mtawekwa wakfu kwa Mungu wenu.

41 Mimi NdimiBwanaMungu wenu, niliyewatoa Misri niwe Mungu wenu. Mimi NdimiBwanaMungu wenu.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/15-0376ac97d713814f2a543c9e91896b18.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 16

Kora, Dathani Na Abiramu

1 Kora mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, pamoja na baadhi ya Wareubeni, yaani Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni mwana wa Pelethi, wakachukua baadhi ya watu,

2 wakainuka dhidi ya Mose. Pamoja nao walikuwepo wanaume wa Kiisraeli 250, watu waliojulikana, viongozi wa jumuiya waliokuwa wameteuliwa kuwa wakuu wa kusanyiko.

3 Wakaja kama kikundi kuwapinga Mose na Aroni, wakawaambia, “Ninyi mmejitukuza sana! Kusanyiko hili lote ni takatifu, kila mmoja wao, nayeBwanayu pamoja nao. Kwa nini basi mmejitukuza wenyewe juu ya kusanyiko laBwana?”

4 Mose aliposikia jambo hili, akaanguka kifudifudi.

5 Kisha akamwambia Kora na wafuasi wake wote: “AsubuhiBwanaataonyesha ni nani aliye wake na ni nani aliye mtakatifu, tena atamtaka mtu huyo aje kwake. Mtu yule ambaye atamchagua atamfanya kuja karibu naye.

6 Wewe Kora na wafuasi wako wote mtafanya hivi: Chukueni vyetezo,

7 kesho wekeni moto na uvumba kwenye hivyo vyetezo mbele zaBwana. Mtu ambayeBwanaatamchagua atakuwa ndiye mtakatifu. Ninyi Walawi mmejitukuza sana!”

8 Pia Mose akamwambia Kora, “Enyi Walawi! Sasa nisikilizeni.

9 Haiwatoshi ninyi kwamba Mungu wa Israeli amewateua ninyi kutoka kusanyiko lote la Kiisraeli, na kuwaleta karibu naye mpate kufanya kazi kwenye Maskani yaBwana, na kusimama mbele ya kusanyiko ili kuwahudumia?

10 Amekuleta wewe na ndugu zako Walawi mwe karibu naye, lakini sasa unajaribu kupata na ukuhani pia.

11 Wewe na wafuasi wako wote mmekusanyika pamoja kinyume chaBwana. Aroni ni nani kwamba ninyi mnungʼunike dhidi yake?”

12 Kisha Mose akawaita Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu. Lakini wao wakasema, “Sisi hatuji!

13 Haitoshi tu kwamba wewe umetuleta kutoka nchi itiririkayo maziwa na asali ili kutuua sisi jangwani? Nawe sasa pia unataka kuwa mkuu juu yetu?

14 Zaidi ya hayo, hujatuingiza katika nchi inayotiririka maziwa na asali, wala hujatupa urithi wa mashamba na mashamba ya mizabibu. Je, utayangʼoa macho ya watu hawa? Hapana, sisi hatuji!”

15 Ndipo Mose akakasirika sana na kumwambiaBwana, “Usiikubali sadaka yao. Mimi sikuchukua chochote, hata punda kutoka kwao, wala sijamkosea hata mmoja wao.”

16 Mose akamwambia Kora, “Wewe na wafuasi wako wote kesho mtatokea mbele zaBwana: yaani wewe na hao wenzako, pamoja na Aroni.

17 Kila mtu atachukua chetezo chake na kuweka uvumba ndani yake, vyetezo 250 kwa jumla, na kukileta mbele zaBwana. Wewe na Aroni mtaleta vyetezo vyenu pia.”

18 Kwa hiyo kila mtu akachukua chetezo chake, akaweka moto na uvumba ndani yake, na kusimama pamoja na Mose na Aroni kwenye mlango wa Hema la Kukutania.

19 Kora alipokuwa amekusanya wafuasi wake wote kuwapinga Mose na Aroni kwenye mlango wa Hema la Kukutania, utukufu waBwanaukatokea kwa kusanyiko lote.

20 Bwanaakamwambia Mose na Aroni,

21 “Jitengeni kutoka kwenye kusanyiko hili ili nipate kuwaangamiza mara moja.”

22 Lakini Mose na Aroni wakaanguka kufudifudi na kulia kwa sauti, wakasema, “Ee Mungu, Mungu wa roho za wanadamu wote, utakuwa na hasira na kusanyiko lote wakati ni mtu mmoja tu ametenda dhambi?”

23 NdipoBwanaakamwambia Mose,

24 “Liambie kusanyiko, ‘Ondokeni hapo karibu na mahema ya Kora, Dathani na Abiramu.’ ”

25 Mose akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu, nao wazee wa Israeli wakafuatana naye.

26 Mose akalionya kusanyiko, “Sogeeni nyuma mbali na mahema ya hawa watu waovu! Msiguse kitu chochote kilicho mali yao, la sivyo mtafagiliwa mbali kwa sababu ya dhambi zao zote.”

27 Hivyo wakaondoka karibu na mahema ya Kora, Dathani na Abiramu. Dathani na Abiramu walikuwa wametoka nje, nao walikuwa wamesimama pamoja na wake zao, watoto wao na wale wanyonyao kwenye mlango wa mahema yao.

28 Ndipo Mose akasema, “Hivi ndivyo mtakavyojua kuwaBwanaamenituma kufanya mambo haya, na kwamba halikuwa wazo langu.

29 Ikiwa watu hawa watakufa kifo cha kawaida na kupatwa na yale ya kawaida yanayowapata wanadamu, basiBwanahakunituma mimi.

30 Lakini ikiwaBwanaataleta jambo jipya kabisa, ardhi ikifunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na kila kitu kilicho mali yao, nao washuke chini kaburiniwakiwa hai, ndipo mtafahamu kuwa watu hawa wamemdharauBwana.”

31 Mara Mose alipomaliza kusema haya yote, ardhi iliyokuwa chini yao ikapasuka,

32 nchi ikafunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na jamaa zao, na watu wote wa Kora na mali zao zote.

33 Wakashuka chini kaburini wakiwa hai, pamoja na kila kitu walichokuwa nacho; nchi ikajifunika juu yao, nao wakaangamia wakatoweka kutoka kusanyiko.

34 Kutoka kilio chao, Waisraeli wote waliowazunguka walikimbia, wakipaza sauti, “Nchi inatumeza na sisi pia!”

35 Moto ukaja kutoka kwaBwana, ukawateketeza wale watu 250 waliokuwa wakifukiza uvumba.

36 Bwanaakamwambia Mose,

37 “Mwambie Eleazari mwana wa kuhani Aroni, atoe vyetezo kwenye mabaki ya moto na kutawanya makaa mbali kiasi, kwa maana vyetezo ni vitakatifu:

38 vyetezo vya watu waliofanya dhambi iliyowagharimu maisha yao. Fua vyetezo hivyo kuwa bamba ili kufunika madhabahu, kwa maana vimeletwa mbele zaBwanana vimekuwa vitakatifu. Navyo viwe ishara kwa Waisraeli.”

39 Hivyo kuhani Eleazari akavikusanya vile vyetezo vya shaba vilivyoletwa na wale waliokuwa wameteketezwa kwa moto, naye akavifua kufunika madhabahu,

40 kama vileBwanaalivyomwelekeza kupitia Mose. Hili lilikuwa kuwakumbusha Waisraeli kwamba hakuna mtu hata mmoja, isipokuwa mzao wa Aroni, awezaye kuja kufukiza uvumba mbele zaBwana, la sivyo, angekuwa kama Kora na wafuasi wake.

41 Siku iliyofuata jumuiya yote ya Kiisraeli wakanungʼunika dhidi ya Mose na Aroni, wakisema, “Mmewaua watu waBwana.”

42 Lakini wakati kusanyiko lilipokusanyika kupingana na Mose na Aroni, nalo likageuka kuelekea Hema la Kukutania, ghafula wingu likafunika Hema, nao utukufu waBwanaukatokea.

43 Ndipo Mose na Aroni wakaenda mbele ya Hema la Kukutania,

44 nayeBwanaakamwambia Mose,

45 “Jitenge mbali na kusanyiko hili ili niweze kuwaangamiza mara moja.” Wakaanguka chini kifudifudi.

46 Kisha Mose akamwambia Aroni, “Chukua chetezo chako na uweke uvumba ndani yake, pamoja na moto kutoka madhabahuni, nawe uende haraka kwenye kusanyiko ili kufanya upatanisho kwa ajili yao. Ghadhabu imekuja kutoka kwaBwana, na tauni imeanza.”

47 Hivyo Aroni akafanya kama Mose alivyosema, akakimbilia katikati ya kusanyiko. Tauni ilikuwa tayari imeanza miongoni mwa watu, lakini Aroni akafukiza uvumba na kufanya upatanisho kwa ajili yao.

48 Aroni akasimama kati ya waliokuwa hai na waliokufa, nayo tauni ikakoma.

49 Lakini walikufa watu 14,700 kutokana na tauni hiyo, licha ya wale waliokuwa wamekufa kwa sababu ya Kora.

50 Ndipo Aroni akamrudia Mose kwenye mlango wa Hema la Kukutania, kwa maana tauni ilikuwa imekoma.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/16-25a319c4b0ffc78f9cdba0660a14b15b.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 17

Kuchipuka Kwa Fimbo Ya Aroni

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Waisraeli, na ujipatie fimbo kumi na mbili kutoka kwao, moja kutoka kwa kila mmoja wa viongozi wa kabila za baba zao. Andika jina la kila mtu kwenye fimbo yake.

3 Kwenye fimbo ya Lawi andika jina la Aroni, kwa maana ni lazima iwepo fimbo moja kwa kila kiongozi kwa ajili ya kila kabila la baba zao.

4 Ziweke hizo fimbo ndani ya Hema la Kukutania mbele ya Sanduku la Ushuhuda, mahali nikutanapo nawe.

5 Fimbo ya mtu nitakayemchagua itachipuka, nami mwenyewe nitayakomesha haya manungʼuniko ya mara kwa mara ya Waisraeli dhidi yako.”

6 Hivyo Mose akasema na Waisraeli, nao viongozi wao wakampa fimbo kumi na mbili, fimbo moja kwa ajili ya kila kabila la baba zao, nayo fimbo ya Aroni ikiwa miongoni mwa hizo.

7 Mose akaziweka hizo fimbo mbele zaBwanandani ya Hema la Ushuhuda.

8 Siku iliyofuata Mose aliingia kwenye Hema la Ushuhuda akaona ile fimbo ya Aroni ambayo iliwakilisha jamaa ya Lawi haikuwa tu imechipuka, bali pia ilikuwa imetoa machipukizi, kuchanua maua na kuzaa malozi.

9 Ndipo Mose akaleta zile fimbo zote kwa Waisraeli wote kutoka mbele zaBwana. Wakaziangalia, na kila mtu akaichukua fimbo yake mwenyewe.

10 Bwanaakamwambia Mose, “Rudisha fimbo ya Aroni mbele ya Sanduku la Ushuhuda, ili ihifadhiwe kama alama kwa waasi. Hili litakomesha manungʼuniko yao dhidi yangu, ili kwamba wasife.”

11 Mose akafanya kamaBwanaalivyomwamuru.

12 Waisraeli wakamwambia Mose, “Tutakufa! Tumepotea, sote tumepotea!

13 Yeyote akaribiaye Maskani yaBwanaatakufa. Je, sisi sote tutakufa?”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/17-c6ca6c7397bf70c33aa11c7392aaf9de.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 18

Wajibu Wa Makuhani Na Walawi

1 Bwanaakamwambia Aroni, “Wewe, wanao na jamaa ya baba yako mtawajibika kwa makosa dhidi ya mahali patakatifu, na wewe na wanao peke yenu ndio mtakaowajibika kwa makosa dhidi ya ukuhani.

2 Walete Walawi wenzako kutoka kabila la baba zako ili waungane nanyi na kuwasaidia wakati wewe na wanao mnapohudumu mbele ya Hema la Ushuhuda.

3 Watawajibika kwenu na watafanya kazi zote za Hema, lakini kamwe wasisogelee vifaa vya patakatifu au madhabahu, la sivyo wao na ninyi mtakufa.

4 Watajiunga nanyi na watawajibika kwa utunzaji wa Hema la Kukutania, yaani kazi zote kwenye Hema, wala hakuna mtu mwingine yeyote atakayeweza kusogea karibu hapo mlipo.

5 “Mtawajibika katika utunzaji wa mahali patakatifu na madhabahu, ili kwamba ghadhabu isiwaangukie Waisraeli tena.

6 Mimi mwenyewe nimewachagua Walawi wenzenu kutoka miongoni mwa Waisraeli kama zawadi kwenu, waliowekwa wakfu kwaBwanaili kufanya kazi katika Hema la Kukutania.

7 Lakini ni wewe tu na wanao mtakaoweza kutumika kama makuhani kuhusiana na kila kitu kwenye madhabahu na ndani ya pazia. Ninawapa utumishi wa ukuhani kama zawadi. Mtu mwingine yeyote atakayekaribia mahali patakatifu ni lazima auawe.”

Sadaka Kwa Ajili Ya Makuhani Na Walawi

8 KishaBwanaakamwambia Aroni, “Mimi mwenyewe nimekuweka kuwa mwangalizi wa sadaka zote zitakazotolewa kwangu; matoleo yote matakatifu Waisraeli wanayonipa ninakupa wewe na wanao kama sehemu yenu na fungu lenu la kawaida.

9 Mtachukua sehemu ya yale matoleo matakatifu sana ambayo hayateketezwi kwa moto. Kutoka kwa matoleo yote wanayoniletea kama sadaka takatifu sana, ziwe za nafaka, au za dhambi, au za makosa, sehemu ile itakuwa yako na wanao.

10 Mtaila kama kitu kilicho kitakatifu sana; kila mwanaume ataila. Ni lazima mtaiheshimu kama takatifu.

11 “Hiki pia ni chako: chochote kilichotengwa kutoka kwenye matoleo yote ya sadaka za kuinuliwa za Waisraeli. Ninakupa wewe haya, wana na binti zako kama sehemu yenu ya kawaida. Kila mmoja wa nyumba yako ambaye ni safi kwa taratibu za ibada anaweza kuyala.

12 “Ninawapa mafuta ya zeituni yaliyo bora kuliko yote, na divai mpya iliyo bora kuliko zote na nafaka wanazompaBwanakama malimbuko katika mavuno yao.

13 Malimbuko yote ya nchi ambayo wanamleteaBwanayatakuwa yenu. Kila mmoja nyumbani kwako ambaye ni safi kwa taratibu za Ibada anaweza kula.

14 “Kila kitu katika Israeli ambacho kimetolewa kwaBwanani chenu.

15 Kila mzaliwa wa kwanza wa mwanadamu na wa mnyama, ambaye ametolewa kwaBwanani wenu. Lakini ni lazima mtamkomboa kila mwana mzaliwa wa kwanza na kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa wanyama wasio safi.

16 Watakapokuwa na umri wa mwezi mmoja, ni lazima mtawakomboa kwa bei ya ukombozi iliyowekwa, kwa shekeli tanoza fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, yenye uzito wa gera ishirini.

17 “Lakini kamwe usimkomboe mzaliwa wa kwanza wa maksai, kondoo au mbuzi; hawa ni watakatifu. Nyunyizia damu yao juu ya madhabahu na uchome mafuta yao kama sadaka itolewayo kwa moto, harufu nzuri inayompendezaBwana.

18 Nyama zao zitakuwa chakula chenu, kama ilivyokuwa kidari cha kuinuliwa na paja la mguu wa kulia.

19 Chochote kitakachotengwa kutoka sadaka takatifu ambazo Waisraeli wanamtoleaBwana, ninakupa wewe, wanao na binti zako kama fungu lenu la kawaida. Ni Agano la milele la chumvi mbele zaBwanakwako na watoto wako.”

20 Bwanaakamwambia Aroni, “Hutakuwa na urithi wowote katika nchi yao, wala hutakuwa na sehemu miongoni mwao; Mimi ni fungu lako na urithi wako miongoni mwa Waisraeli.

21 “Ninawapa Walawi zaka yote katika Israeli kama urithi wao kuwa kama malipo kwa kazi wanayoifanya wakati wanapohudumu katika Hema la Kukutania.

22 Kuanzia sasa, kamwe Waisraeli wasisogelee karibu na Hema la Kukutania, la sivyo watabeba matokeo ya dhambi zao, nao watakufa.

23 Ni Walawi watakaofanya kazi katika Hema la Kukutania na kubeba wajibu wa makosa dhidi yake. Hili ni agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo. Hawatapokea urithi wowote miongoni mwa Waisraeli.

24 Badala yake, ninawapa Walawi zaka zote zinazotolewa na Waisraeli kama sadaka kwaBwanakuwa urithi wao. Hiyo ndiyo sababu nimesema hivi kuhusu wao: ‘Hawatakuwa na urithi miongoni mwa Waisraeli.’ ”

25 Bwanaakamwambia Mose,

26 “Sema na Walawi na uwaambie: ‘Mtakapopokea zaka kutoka kwa Waisraeli ambayo ninawapa kama urithi wenu kutoka kwao, ni lazima mtoe sehemu ya kumi ya hiyo zaka kama sadaka kwaBwana, iwe zaka ya hiyo zaka.

27 Sadaka yenu itahesabiwa kwenu kama nafaka kutoka sakafu ya kupuria, au divai kutoka kwenye shinikizo la kukamulia zabibu.

28 Kwa njia hii, ninyi pia mtatoa sadaka kwaBwanakutoka zaka zote mtakazopokea kutoka kwa Waisraeli. Kutoka kwenye zaka hizi, ni lazima mtoe sehemu yaBwanakwa Aroni, kuhani.

29 Ni lazima mtoe kama sehemu yaBwanailiyo nzuri sana tena ile sehemu iliyo takatifu sana kuliko zote ya kile kitu mlichopewa.’

30 “Waambie Walawi: ‘Mtakapotoa sehemu zilizo bora sana, itahesabiwa kwenu kama mazao ya sakafu ya kupuria nafaka, au ya shinikizo la kukamulia zabibu.

31 Ninyi na watu wa nyumbani mwenu mnaweza kula sehemu iliyobaki mahali popote, kwani ndio ujira wenu kwa ajili ya kazi yenu katika Hema la Kukutania.

32 Kwa kutoa sehemu zake zilizo bora sana, hamtakuwa na hatia katika jambo hili; ndipo hamtatia unajisi sadaka takatifu za Waisraeli, nanyi hamtakufa.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/18-1d73cb0709c314b39800c9b6fb141162.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 19

Maji Ya Utakaso

1 Bwanaakamwambia Mose na Aroni:

2 “Hivi ndivyo sheria ambayoBwanaameagiza itakavyo: Waambie Waisraeli wakuletee mtamba mwekundu asiye na dosari wala waa, na ambaye hajapata kufungwa nira.

3 Mpeni kuhani Eleazari huyo mtamba; naye atatolewa nje ya kambi na kuchinjwa mbele yake huyo kuhani.

4 Kisha kuhani Eleazari atachukua baadhi ya damu yake kwenye kidole chake na kuinyunyiza mara saba kuelekea upande wa mbele ya Hema la Kukutania.

5 Wakati angali akitazama, mtamba huyo atateketezwa: ngozi yake, nyama yake, damu na sehemu zake za ndani.

6 Kuhani atachukua kuni za mti wa mwerezi, hisopo na sufu nyekundu, na kuvitupa kwenye huyo mtamba anayeungua.

7 Baada ya hayo, kuhani lazima afue nguo zake, na aoge mwili wake kwa maji. Kisha anaweza kurudi kambini, lakini atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada mpaka jioni.

8 Mtu amchomaye huyo mtamba lazima naye pia afue nguo zake na kuoga kwa maji, naye pia atakuwa najisi mpaka jioni.

9 “Mtu ambaye ni safi atakusanya majivu ya mtamba huyo na kuyaweka mahali ambapo ni safi nje ya kambi kwa taratibu za kiibada. Yatahifadhiwa na jumuiya ya Kiisraeli kwa matumizi katika maji ya utakaso; ni kwa ajili ya kutakasa kutoka dhambini.

10 Mtu akusanyaye majivu ya huyo mtamba ni lazima pia afue nguo zake, kadhalika naye pia atakuwa najisi hadi jioni. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa Waisraeli na kwa wageni wanaoishi miongoni mwao.

11 “Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote atakuwa najisi kwa siku saba.

12 Ni lazima ajitakase mwenyewe kwa maji katika siku ya tatu na siku ya saba, ndipo atakuwa safi. Lakini kama hatajitakasa mwenyewe katika siku ya tatu na ya saba, hatakuwa safi.

13 Mtu yeyote agusaye maiti ya mtu yeyote na kushindwa kujitakasa mwenyewe hunajisi Maskani yaBwana. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na Israeli. Kwa sababu hajanyunyiziwa maji ya utakaso, yeye ni najisi; unajisi wake unabaki juu yake.

14 “Hii ndiyo sheria itumikayo wakati mtu amekufa ndani ya hema: Yeyote aingiaye ndani ya hema hilo na yeyote aliye ndani yake watakuwa najisi kwa muda wa siku saba,

15 nacho kila chombo kisicho na kifuniko juu yake kitakuwa najisi.

16 “Mtu yeyote aliyeko nje mahali pa wazi agusaye mtu aliyeuawa kwa upanga au mtu aliyekufa kwa kifo cha kawaida, au mtu yeyote agusaye mfupa wa mtu aliyekufa au kaburi, atakuwa najisi kwa siku saba.

17 “Kwa mtu aliye najisi, weka majivu ya sadaka ya utakaso wa dhambi ndani ya chombo, umimine maji safi juu yao.

18 Kisha mtu aliye safi kwa kawaida za kiibada atachukua hisopo, achovye ndani ya maji, na kunyunyizia hema na vifaa vyote pamoja na watu ambao walikuwamo. Pia ni lazima amnyunyizie mtu yeyote ambaye amegusa mfupa wa mtu aliyekufa, au kaburi, au mtu ambaye ameuawa, au mtu ambaye amekufa kifo cha kawaida.

19 Mtu ambaye ni safi ndiye atakayemnyunyizia yeyote ambaye ni najisi siku ya tatu na siku ya saba, na katika siku ya saba atamtakasa mtu huyo. Mtu ambaye ametakaswa lazima afue nguo zake na kuoga kwa maji, na jioni ile atakuwa safi.

20 Lakini ikiwa mtu ambaye ni najisi hakujitakasa mwenyewe, ni lazima akatiliwe mbali na jumuiya, kwa sababu ameinajisi Maskani yaBwana. Maji ya utakaso hayajanyunyizwa juu yake, naye ni najisi.

21 Hii ni sheria ya kudumu kwao.

“Mtu yeyote ambaye ananyunyiza yale maji ya utakaso lazima pia afue nguo zake, na yeyote ambaye hugusa maji ya utakaso atakuwa najisi mpaka jioni.

22 Kitu chochote anachogusa mtu aliye najisi kitakuwa najisi, na yeyote akigusaye huwa najisi mpaka jioni.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/19-0ce88076d3419b9d06406d7a26ef8714.mp3?version_id=1627—