Categories
Hesabu

Hesabu Utangulizi

Utangulizi

Kitabu cha Hesabu kimepewa jina hili kutokana na matukio mawili ya kuwahesabu wana wa Israeli: La kwanza huko Sinai katika mwaka wa pili baada ya kutoka Misri (Hes 1), na la pili huko Yordani katika mwaka wa arobaini (Hes 26). Jina la kitabu hiki kwa Kiebrania ni “Bemidbar,” ambalo maana yake ni “Huko jangwani,” jina linaloelekea kueleza zaidi yale yaliyomo.

Kitabu hiki kinatoa maelezo ya safari ya Waisraeli ya miaka 38 wakati walikuwa wanatangatanga jangwani baada ya kuanzishwa kwa Agano la Mungu katika Mlima Sinai. Kitabu cha Hesabu kinagusia safari ya Waisraeli kutoka Mlima Sinai hadi nchi tambarare ya Moabu katika mpaka wa Kanaani. Kitabu hiki kinaelezea vile Waisraeli walivyonungʼunika na kumwasi Mungu, na hukumu iliyofuata baadaye. Watu wazima waliotoka Misri walikosa nafasi ya kuingia katika Nchi ya Ahadi, isipokuwa watoto wao.

Mwandishi

Mose.

Kusudi

Kuelezea jinsi Waisraeli walivyojitayarisha kuingia katika Nchi ya Ahadi, na walivyoasi na kuhukumiwa.

Mahali

Kitabu hiki kiliandikwa wakati Waisraeli walikuwa wanatangatanga jangwani, mahali fulani katika Ghuba ya Sinai.

Tarehe

Kati ya 1450–1410 K.K.

Wahusika Wakuu

Mose, Aroni, Miriamu, Yoshua, Kalebu, Eleazari, Kora, Balaamu na Balaki.

Wazo Kuu

Kitabu hiki kinaeleza juu ya utunzaji na uongozi wa Mungu, uvumilivu wake, na uasi wa watu wa Mungu na matokeo yake. Jambo moja lililokuwa dhahiri na ambalo limerudiwa mara kwa mara katika kitabu chote ni jinsi mkono wa Mungu ulivyokuwa pamoja na wana wa Israeli saa zote ili kuwahudumia na kuwapa mahitaji yao.

Mambo Muhimu

Kuhesabiwa kwa Waisraeli, uasi dhidi ya Mungu, na hukumu ya Waisraeli ya kutangatanga jangwani.

Mgawanyo

Maelezo ya Hema la Kukutania, na kuendelea na safari (

1:1–10:10

)

Kutoka Sinai hadi nchi tambarare ya Moabu (

10:11–21:35

)

Balaamu, Balaki na Israeli (

22:1–25:18

)

Maelekezo juu ya kuishinda na kuitwaa nchi ya Kanaani (

26:1–36:13

).

Categories
Hesabu

Hesabu 1

Watu Wahesabiwa Kwa Mara Ya Kwanza

1 Bwanaalisema na Mose katika Jangwa la Sinai, katika Hema la Kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Akamwambia,

2 “Hesabu watu wa jumuiya yote ya Waisraeli kwa kufuata koo zao na jamaa zao, ukiorodhesha kila mwanaume kwa jina lake, mmoja mmoja.

3 Wewe na Aroni mtawahesabu kwa migawanyo yao wanaume wote katika Israeli wenye miaka ishirini na kuendelea ambao wanaweza kutumika katika jeshi.

4 Mwanaume mmoja kutoka kila kabila, kila aliye kiongozi wa jamaa yake, atawasaidia.

5 Haya ndiyo majina ya wanaume watakaowasaidia:

“kutoka Reubeni, ni Elisuri mwana wa Shedeuri;

6 kutoka Simeoni, ni Shelumieli mwana wa Surishadai;

7 kutoka Yuda, ni Nashoni mwana wa Aminadabu;

8 kutoka Isakari, ni Nethaneli mwana wa Suari;

9 kutoka Zabuloni, ni Eliabu mwana wa Heloni;

10 kutoka wana wa Yosefu:

kutoka Efraimu, ni Elishama mwana wa Amihudi;

kutoka Manase, ni Gamalieli mwana wa Pedasuri;

11 kutoka Benyamini, ni Abidani mwana wa Gideoni;

12 kutoka Dani, ni Ahiezeri mwana wa Amishadai;

13 kutoka Asheri, ni Pagieli mwana wa Okrani;

14 kutoka Gadi, ni Eliasafu mwana wa Deueli;

15 kutoka Naftali, ni Ahira mwana wa Enani.”

16 Hawa walikuwa wanaume walioteuliwa kutoka jumuiya, viongozi wa makabila ya baba zao. Walikuwa wakuu wa koo za Israeli.

17 Mose na Aroni wakawachukua wanaume hao waliokuwa wamepewa majina yao,

18 wakaita jumuiya yote pamoja katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Watu wakaonyesha nasaba zao kwa koo zao na jamaa zao, nao wanaume waliokuwa na miaka ishirini au zaidi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja,

19 kamaBwanaalivyomwagiza Mose. Hivyo aliwahesabu katika Jangwa la Sinai:

20 Kutoka wazao wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

21 Idadi kutoka kabila la Reubeni ilikuwa watu 46,500.

22 Kutoka wazao wa Simeoni:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi walihesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

23 Idadi kutoka kabila la Simeoni walikuwa watu 59,300.

24 Kutoka wazao wa Gadi:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

25 Idadi kutoka kabila la Gadi walikuwa watu 45,650.

26 Kutoka wazao wa Yuda:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

27 Idadi kutoka kabila la Yuda walikuwa watu 74,600.

28 Kutoka wazao wa Isakari:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

29 Idadi kutoka kabila la Isakari walikuwa watu 54,400.

30 Kutoka wazao wa Zabuloni:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

31 Idadi kutoka kabila la Zabuloni walikuwa watu 57,400.

32 Kutoka wana wa Yosefu:

Kutoka wazao wa Efraimu:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

33 Idadi kutoka kabila la Efraimu walikuwa watu 40,500.

34 Kutoka wazao wa Manase:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

35 Idadi kutoka kabila la Manase walikuwa watu 32,200.

36 Kutoka wazao wa Benyamini:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

37 Idadi kutoka kabila la Benyamini walikuwa watu 35,400.

38 Kutoka wazao wa Dani:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

39 Idadi kutoka kabila la Dani walikuwa watu 62,700.

40 Kutoka wazao wa Asheri:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

41 Idadi kutoka kabila la Asheri walikuwa watu 41,500.

42 Kutoka wazao wa Naftali:

Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

43 Idadi kutoka kabila la Naftali walikuwa watu 53,400.

44 Hawa walikuwa wanaume waliohesabiwa na Mose, Aroni na viongozi kumi na wawili wa Israeli, kila mmoja akiwakilisha jamaa yake.

45 Wanaume wote Waisraeli waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi la Israeli walihesabiwa kufuatana na jamaa zao.

46 Jumla ya hesabu yao ilikuwa watu 603,550.

47 Hata hivyo, jamaa ya kabila la Lawi hawakuhesabiwa pamoja na wengine.

48 Bwanaalikuwa amemwambia Mose:

49 “Kamwe usihesabu kabila la Lawi wala kuwaweka pamoja katika hesabu ya Waisraeli wengine.

50 Badala yake, waweke Walawi kuwa viongozi wa Maskani ya Ushuhuda, juu ya samani zake na kila kitu kilichomo ndani yake. Wao watabeba Maskani na samani zake zote; wataitunza na kupiga kambi kuizunguka.

51 Wakati wowote Maskani inapohamishwa, Walawi wataifungua, na wakati wowote maskani inapotakiwa kusimamishwa, Walawi watafanya kazi hiyo. Mtu yeyote mwingine ambaye atasogea karibu nayo atauawa.

52 Waisraeli watapiga mahema yao kwa makundi makundi, kila mwanaume katika kambi yake mwenyewe chini ya bendera yake.

53 Hata hivyo, Walawi watapiga mahema yao kuzunguka Maskani ya Ushuhuda ili ghadhabu isiipate jumuiya ya Waisraeli. Walawi watawajibika kwa utunzaji wa Maskani ya Ushuhuda.”

54 Waisraeli walifanya yote haya sawasawa kamaBwanaalivyomwamuru Mose.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/1-4dd2702063645dbc088512caaee4e489.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 2

Mpangilio Wa Kambi Za Makabila

1 Bwanaaliwaambia Mose na Aroni:

2 “Waisraeli watapiga kambi zao kuzunguka Hema la Kukutania kwa umbali fulani kutoka kwenye hema, kila mwanaume chini ya alama yake pamoja na bendera ya jamaa yake.”

3 Kwa upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua, kambi ya makundi ya Yuda watapiga kambi chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Yuda ni Nashoni mwana wa Aminadabu.

4 Kundi lake lina watu 74,600.

5 Kabila la Isakari watapiga kambi karibu na Yuda. Kiongozi wa watu wa Isakari ni Nethaneli mwana wa Suari.

6 Kundi lake lina watu 54,400.

7 Kabila la Zabuloni litafuata. Kiongozi wa watu wa Zabuloni ni Eliabu mwana wa Heloni.

8 Kundi lake lina watu 57,400.

9 Wanaume wote walio katika kambi ya Yuda, kufuatana na makundi yao, ni 186,400. Wao watatangulia kuondoka.

10 Kwa upande wa kusini kutakuwa kambi ya makundi ya Reubeni chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Reubeni ni Elisuri mwana wa Shedeuri.

11 Kundi lake lina watu 46,500.

12 Kabila la Simeoni watapiga kambi karibu na Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Surishadai.

13 Kundi lake lina watu 59,300.

14 Kabila la Gadi litafuata. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deueli.

15 Kundi lake lina watu 45,650.

16 Wanaume wote walio katika kambi ya Reubeni, kufuatana na makundi yao, ni 151,450. Nao watakuwa nafasi ya pili kuondoka.

17 Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya alama yake.

18 Upande wa magharibi kutakuwepo na kambi ya makundi ya Efraimu chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi.

19 Kundi lake lina watu 40,500.

20 Kabila la Manase litafuata baada ya Efraimu. Kiongozi wa watu wa Manase ni Gamalieli mwana wa Pedasuri.

21 Kundi lake lina watu 32,200.

22 Kabila la Benyamini litafuata baada ya Manase. Kiongozi wa watu wa Benyamini ni Abidani mwana wa Gideoni.

23 Kundi lake lina watu 35,400.

24 Wanaume wote walio katika kambi ya Efraimu kufuatana na makundi yao ni 108,100. Nao watakuwa nafasi ya tatu kuondoka.

25 Upande wa kaskazini kutakuwa na makundi ya kambi ya Dani, chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.

26 Kundi lake lina watu 62,700.

27 Kabila la Asheri watapiga kambi karibu na Dani. Kiongozi wa watu wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okrani.

28 Kundi lake lina watu 41,500.

29 Kabila la Naftali litafuata. Kiongozi wa watu wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani.

30 Kundi lake lina watu 53,400.

31 Wanaume wote walio katika kambi ya Dani ni 157,600. Wao watakuwa wa mwisho kuondoka chini ya alama yao.

32 Hawa ndio Waisraeli, wakiwa wamehesabiwa kufuatana na jamaa zao. Wote walio kambini kwa makundi yao ni watu 603,550.

33 Hata hivyo, Walawi hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine, kamaBwanaalivyomwagiza Mose.

34 Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kila kituBwanaalichomwamuru Mose. Hivyo ndivyo walivyopiga kambi chini ya alama zao, pia hivyo ndivyo walivyoondoka, kila mmoja akiwa na ukoo wake na jamaa yake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/2-9826c94294424bf79a970f89ee9a4019.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 3

Walawi

1 Hii ni hesabu ya jamaa ya Aroni na Mose kwa wakati ambaoBwanaalizungumza na Mose katika Mlima Sinai.

2 Majina ya wana wa Aroni yalikuwa: Nadabu mzaliwa wa kwanza na Abihu, Eleazari na Ithamari.

3 Hayo yalikuwa majina ya wana wa Aroni, makuhani wapakwa mafuta, waliokuwa wamesimikwa kuhudumu kama makuhani.

4 Hata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele zaBwanawalipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari walihudumu peke yao kama makuhani wakati wote wa maisha ya Aroni baba yao.

5 Bwanaakamwambia Mose,

6 “Walete watu wa kabila la Lawi mbele ya Aroni kuhani ili wamsaidie.

7 Watafanya huduma kwa ajili yake na kwa jumuiya yote katika Hema la Kukutania kwa kufanya kazi za Maskani.

8 Watatunza samani zote za Hema la Kukutania, wakitimiza wajibu wa kuhudumia Waisraeli kwa kufanya kazi ya Maskani.

9 Wakabidhi Walawi kwa Aroni na wanawe; hao ndio Waisraeli ambao wanakabidhiwa kwake kabisa.

10 Waweke Aroni na wanawe kuhudumu kama makuhani; mtu mwingine yeyote atakayesogea mahali patakatifu ni lazima auawe.”

11 Bwanaakamwambia Mose,

12 “Nimewatwaa Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli badala ya mzaliwa wa kwanza wa kiume wa kila mwanamke wa Mwisraeli. Walawi ni wangu,

13 kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza ni wangu. Nilipowaua wazaliwa wa kwanza huko Misri, nilimtenga kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli awe wangu, akiwa mwanadamu au mnyama. Watakuwa wangu. Mimi ndimiBwana.”

14 Bwanaakamwambia Mose katika Jangwa la Sinai,

15 “Wahesabu Walawi kwa jamaa zao na koo zao. Mhesabu kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi.”

16 Kwa hiyo Mose akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno laBwana.

17 Haya yalikuwa majina ya wana wa Lawi:

Gershoni, Kohathi na Merari.

18 Haya ndiyo yaliyokuwa majina ya koo za Wagershoni:

Libni na Shimei.

19 Koo za Wakohathi zilikuwa ni:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

20 Koo za Wamerari zilikuwa ni:

Mahli na Mushi.

Hizi ndizo zilizokuwa koo za Walawi, kufuatana na jamaa zao.

21 Kulikuwa na koo za Walibni na Washimei kwa Gershoni; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wagershoni.

22 Idadi ya waume wote waliokuwa na mwezi mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 7,500.

23 Ukoo wa Wagershoni walitakiwa kuweka kambi zao upande wa magharibi, nyuma ya Maskani.

24 Kiongozi wa jamaa za Wagershoni alikuwa Eliasafu mwana wa Laeli.

25 Katika Hema la Kukutania, Wagershoni walikuwa na wajibu wa kutunza Maskani na hema, vifuniko vyake, pazia katika mlango wa kuingilia ndani ya Hema la Kukutania,

26 mapazia ya ua, pazia katika ingilio la ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pamoja na kamba, na kila kinachohusika kwa matumizi yake.

27 Kwa Kohathi kulikuwepo koo za Waamramu, Waishari, Wahebroni na Wauzieli; hizi ndizo zilizokuwa koo za Wakohathi.

28 Hesabu ya waume wote wenye mwezi mmoja au zaidi ilikuwa watu 8,600. Wakohathi waliwajibika kutunza mahali patakatifu.

29 Koo za Wakohathi zilitakiwa kuweka kambi zao upande wa kusini wa Maskani.

30 Kiongozi wa jamaa za koo za Wakohathi alikuwa Elisafani mwana wa Uzieli.

31 Waliwajibika kutunza Sanduku la Agano, meza, kinara cha taa, madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu vinavyotumika kuhudumu, pazia, na kila kitu kinachohusika na matumizi yake.

32 Kiongozi mkuu wa Walawi alikuwa Eleazari mwana wa kuhani, Aroni. Aliwekwa juu ya wale waliowajibika kutunza mahali patakatifu.

33 Kwa Merari kulikuwa na koo za Wamahli na Wamushi; hizi zilikuwa koo za Merari.

34 Hesabu ya waume wote wenye umri wa mwaka mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa 6,200.

35 Kiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili; hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani.

36 Wamerari waliwekwa kutunza miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo, vitako na vifaa vyake vyote na kila kitu kilichohusika na matumizi yake,

37 na pia nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema na kamba zake.

38 Mose, na Aroni na wanawe walitakiwa kuweka kambi zao mashariki mwa Maskani, kuelekea mawio ya jua, mbele ya Hema la Kukutania. Wao walihusika na utunzaji wa mahali patakatifu kwa niaba ya Waisraeli. Mtu mwingine yeyote aliyepasogelea mahali patakatifu angeuawa.

39 Jumla ya hesabu ya Walawi waliohesabiwa na Mose na Aroni kwa amri yaBwana, kufuatana na koo, pamoja na kila mume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walikuwa 22,000.

40 Bwanaakamwambia Mose, “Wahesabu wazaliwa wa kwanza wa kiume wote wa Waisraeli wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi na uorodheshe majina yao.

41 Nitwalie Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya wazaliwa wa mifugo ya Waisraeli. Mimi ndimiBwana.”

42 Hivyo Mose akawahesabu wazaliwa wa kwanza wote wa Waisraeli, kamaBwanaalivyomwamuru.

43 Jumla ya hesabu ya wazaliwa wa kwanza waume wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walioorodheshwa kwa majina, walikuwa 22,273.

44 Bwanaakamwambia Mose,

45 “Watwae Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya mifugo yao. Walawi watakuwa wangu. Mimi ndimiBwana.

46 Ili kukomboa wazao wa kwanza 273 wa Waisraeli ambao wamezidi hesabu ya Walawi,

47 kusanya shekeli tanokwa kila mmoja, kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.

48 Mpe Aroni na wanawe hizo fedha kwa ajili ya ukombozi wa idadi ya Waisraeli waliozidi.”

49 Kwa hiyo Mose akakusanya fedha za ukombozi kutoka kwa wale ambao hesabu yao ilizidi wale waliokombolewa na Walawi.

50 Kutokana na wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli alikusanya fedha yenye uzito wa shekeli 1,365kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu.

51 Mose akampa Aroni na wanawe ile fedha ya ukombozi, kama alivyoamriwa na neno laBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/3-e86f3cb2b11f7d6ad28c7b04ad5715bb.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 4

Wakohathi

1 Bwanaakawaambia Mose na Aroni,

2 “Wahesabu Wakohathi walio sehemu ya Walawi kwa koo zao na jamaa zao.

3 Wahesabu wanaume wote wenye umri wa miaka thelathini hadi hamsini wanaokuja kutumika katika kazi ya Hema la Kukutania.

4 “Hii ndiyo kazi ya Wakohathi katika Hema la Kukutania: Watatunza vitu vilivyo vitakatifu sana.

5 Wakati kambi inapohamishwa, Aroni na wanawe wataingia ndani na kushusha lile pazia la kuzuilia na kufunika nalo Sanduku la Ushuhuda.

6 Kisha watafunika juu yake na ngozi za pomboo,na kutandaza juu yake kitambaa cha rangi ya buluu iliyokolea na kuingiza mipiko mahali pake.

7 “Juu ya meza ya mikate ya Wonyesho watatandaza kitambaa cha buluu na waweke sahani juu yake, masinia, bakuli na magudulia kwa ajili ya sadaka za kinywaji; mkate ule ambao upo hapa daima utabaki juu yake.

8 Juu ya hivyo vitu watatandaza kitambaa chekundu na kufunika kwa ngozi za pomboo na kuweka mipiko yake mahali pake.

9 “Watachukua kitambaa cha buluu na kufunika kinara cha taa kilicho kwa ajili ya nuru, pamoja na taa zake, mikasi yake, sinia zake, magudulia yake yote yaliyotumika kuwekea mafuta.

10 Kisha watakisokotea pamoja na vifaa vyake vyote katika ngozi za pomboo na kukiweka kwenye jukwaa lake.

11 “Juu ya madhabahu ya dhahabu watatandaza kitambaa cha buluu na kukifunika kwa ngozi za pomboo na kuweka mipiko yake mahali pake.

12 “Watavichukua vyombo vyote vinavyotumika kuhudumia mahali patakatifu, watavisokotea kwenye kitambaa cha buluu na kufunika kwa ngozi za pomboo, na kuviweka juu ya miti ya kuchukulia.

13 “Wataondoa majivu kutoka madhabahu ya shaba na kutandaza kitambaa cha zambarau juu yake.

14 Kisha wataweka vyombo vyote juu yake vinavyotumika kwa kuhudumia madhabahuni pamoja na vyombo vya kutolea moto, nyuma, miiko na mabakuli ya kunyunyizia. Juu yake watatandaza ngozi za pomboo ya kufunika, na kuweka mipiko mahali pake.

15 “Baada ya Aroni na wanawe kumaliza kazi ya kufunika samani takatifu na vyombo vyake vyote, watu watakapokuwa tayari kungʼoa kambi, Wakohathi watakuja kufanya kazi ya kubeba. Lakini wasije wakagusa vitu vitakatifu la sivyo watakufa. Wakohathi ndio watakaobeba vile vitu vilivyomo katika Hema la Kukutania.

16 “Eleazari mwana wa Aroni, kuhani, ndiye atakayesimamia mafuta kwa ajili ya taa, uvumba wenye harufu nzuri, sadaka za kila siku za nafaka na mafuta ya upako. Ndiye atakayekuwa msimamizi wa maskani yote yaBwanana kila kitu kilichomo ndani mwake pamoja na samani takatifu na vyombo vyake.”

17 Bwanaakawaambia Mose na Aroni,

18 “Hakikisheni kwamba koo za kabila la Wakohathi hawatengwi kutoka Walawi.

19 Ili wapate kuishi wala wasife wanapokaribia vitu vitakatifu sana, uwafanyie hivi: Aroni na wanawe watakwenda mahali patakatifu na kumgawia kila mtu kazi yake, na kwamba ni nini atakachochukua.

20 Lakini Wakohathi hawaruhusiwi kuingia ndani ili kuangalia vitu vitakatifu, hata kwa kitambo kidogo, la sivyo watakufa.”

Wagershoni

21 Bwanaakamwambia Mose,

22 “Wahesabu pia Wagershoni kwa jamaa zao na koo zao.

23 Wahesabu wanaume wote wenye umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao huja kutumika katika Hema la Kukutania.

24 “Hii ndiyo huduma ya koo za Wagershoni wakati wanapofanya kazi na kubeba mizigo.

25 Watabeba mapazia ya maskani. Hema la Kukutania, kifuniko chake na kifuniko cha nje cha ngozi za pomboo, mapazia ya maingilio ya Hema la Kukutania,

26 mapazia ya ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pazia la maingilio, kamba na vifaa vyote vinavyotumika katika huduma yake. Wagershoni watafanya yote yatakiwayo kufanyika na vitu hivi.

27 Utumishi wao wote ukiwa ni kuchukua au wa kufanya kazi nyingine, utafanyika chini ya maelekezo ya Aroni na wanawe. Mtawapangia kama wajibu wao yote watakayoyafanya.

28 Hii ndiyo huduma ya koo za Wagershoni katika Hema la Kukutania. Wajibu wao utakuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani Aroni.

Wamerari

29 “Wahesabu Wamerari kwa koo zao na jamaa zao.

30 Wahesabu wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao watakuja kutumika katika Hema la Kukutania.

31 Huu ndio wajibu wao wanapofanya huduma katika Hema la Kukutania: kubeba miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo na vitako,

32 nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema, kamba, vifaa vyake vyote na kila kitu kinachohusiana na matumizi yake. Kila mtu mpangie vitu maalum vya kubeba.

33 Huu ndio utumishi wa koo za Merari kama watakavyofanya kazi katika Hema la Kukutania, chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Aroni.”

Kuhesabiwa Kwa Koo Za Walawi

34 Mose, Aroni na viongozi wa jumuiya wakawahesabu Wakohathi kwa koo zao na jamaa zao.

35 Wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania,

36 waliohesabiwa kwa koo zao, walikuwa 2,750.

37 Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wote wale wa koo za Wakohathi ambao walitumika katika Hema la Kukutania. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatana na amri yaBwanakupitia kwa Mose.

38 Wagershoni walihesabiwa kwa koo zao na jamaa zao.

39 Watu wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania,

40 waliohesabiwa kwa koo zao na jamaa zao, walikuwa 2,630.

41 Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wale wa koo za Gershoni ambao walitumika katika Hema la Kukutania. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatana na amri yaBwana.

42 Wamerari walihesabiwa kwa koo zao na jamaa zao.

43 Wanaume wote kuanzia umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini ambao walikuja kutumika katika Hema la Kukutania,

44 waliohesabiwa kwa koo zao, walikuwa 3,200.

45 Hii ilikuwa ndiyo jumla ya wale wa koo za Wamerari. Mose na Aroni waliwahesabu kufuatia amri yaBwanakupitia kwa Mose.

46 Hivyo Mose, Aroni na viongozi wa Israeli waliwahesabu Walawi wote kwa koo zao na jamaa zao.

47 Wanaume wote wenye umri kuanzia miaka thelathini hadi hamsini waliokuja kufanya kazi ya kuhudumu na kubeba Hema la Kukutania

48 walikuwa watu 8,580.

49 Kwa amri yaBwanakupitia Mose, kila mmoja aligawiwa kazi yake na kuambiwa kitu cha kubeba.

Hivyo ndivyo walivyohesabiwa kamaBwanaalivyomwamuru Mose.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/4-76d36a970fda3a08e0fb98d54ca1fdd7.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 5

Utakaso Wa Kambi

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Waamuru Waisraeli kumtoa nje ya kambi mtu yeyote ambaye ana ugonjwa wa ngozi uambukizao,au anayetokwa na majimaji ya aina yoyote, au ambaye ni najisi kwa utaratibu wa ibada kwa sababu ya maiti.

3 Hii itakuwa ni kwa wote, yaani, wanaume na wanawake; watoeni nje ya kambi ili wasije wakanajisi kambi yao, ambamo ninaishi miongoni mwao.”

4 Waisraeli wakafanya hivyo; wakawatoa nje ya kambi. Wakafanya kama vileBwanaalivyokuwa amemwelekeza Mose.

Malipo Kwa Ajili Ya Makosa

5 Bwanaakamwambia Mose,

6 “Waambie Waisraeli, ‘Wakati mwanaume au mwanamke akimkosea mwenzake kwa njia yoyote, na kwa hivyo akawa si mwaminifu kwaBwana, mtu huyo ana hatia,

7 na ni lazima atubu dhambi aliyoifanya. Ni lazima atoe malipo kamili kwa ajili ya kosa lake, aongeze sehemu ya tano juu ya malipo hayo na kutoa yote kwa mtu aliyemkosea.

8 Lakini ikiwa mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye malipo yanaweza kufanywa kwa ajili ya kosa, malipo yatakuwa mali yaBwana, nayo ni lazima apewe kuhani, pamoja na kondoo dume ambaye anatumika kufanyia upatanisho kwa ajili yake.

9 Matoleo yote matakatifu ya Waisraeli wanayoleta kwa kuhani yatakuwa yake.

10 Kila kitu cha mtu kilichowekwa wakfu ni chake mwenyewe, lakini kile atoacho kwa kuhani kitakuwa cha kuhani.’ ”

Jaribio Kwa Ajili Ya Mke Asiye Mwaminifu

11 KishaBwanaakamwambia Mose,

12 “Nena na Waisraeli uwaambie: ‘Ikiwa mke wa mtu amepotoka na si mwaminifu kwa mumewe,

13 kwa kukutana kimwili na mwanaume mwingine, tendo hili likafichika kwa mumewe na unajisi wake usigundulike (kwa kuwa hakuna ushahidi dhidi yake, naye hakukamatwa katika tendo hilo),

14 nazo hisia za wivu zikamjia mumewe na kumshuku mkewe, naye mke yule ni najisi, au mumewe ana wivu na akamshuku ingawa si najisi,

15 basi atampeleka mkewe kwa kuhani. Huyo mume itampasa apeleke pia sadaka ya unga wa shayiri kiasi cha sehemu ya kumi ya efakwa niaba ya mkewe. Huyo mwanaume kamwe asimimine mafuta juu ya huo unga wala asiweke uvumba juu yake, kwa sababu ni sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu, sadaka ya ukumbusho ili kukumbushia uovu.

16 “ ‘Kuhani atamleta huyo mwanamke na kumsimamisha mbele zaBwana.

17 Kisha kuhani atachukua sehemu ya maji matakatifu ndani ya gudulia la udongo na kuchanganya na baadhi ya vumbi kutoka sakafu ya Maskani.

18 Baada ya kuhani kumsimamisha huyo mwanamke mbele zaBwana, atazifungua nywele za huyo mwanamke na kuweka sadaka ya ukumbusho mikononi mwake, ile sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu, huku kuhani mwenyewe akishikilia yale maji machungu yaletayo laana.

19 Kisha kuhani atamwapiza huyo mwanamke, akimwambia, “Ikiwa hakuna mwanaume mwingine aliyekutana kimwili nawe, wala hujapotoka na kuwa najisi wakati ukiwa umeolewa na mumeo, maji haya machungu yaletayo laana na yasikudhuru.

20 Lakini ikiwa umepotoka wakati ukiwa umeolewa na mume wako na umejinajisi mwenyewe kwa kukutana kimwili na mwanaume mwingine asiyekuwa mumeo”;

21 hapa kuhani atamweka huyo mwanamke chini ya laana ya kiapo akisema: “Bwanana awafanye watu wako wakulaani na kukukataa, wakatiBwanaatakapolifanya paja lako kupooza na tumbo lako kuvimba.

22 Maji haya yaletayo laana na yaingie ndani ya mwili wako ili tumbo lako livimbe na paja lako lipooze.”

“ ‘Kisha mwanamke atasema, “Amen. Iwe hivyo.”

23 “ ‘Kuhani ataandika laana hizi kwenye kitabu, kisha atazioshea laana hizo kwenye yale maji machungu.

24 Kuhani atamnywesha yule mwanamke yale maji machungu yaletayo laana, nayo maji haya yatamwingia na kumsababishia maumivu makali.

25 Kuhani atachukua sadaka ya nafaka kwa ajili ya wivu kutoka mikononi mwa huyo mwanamke, naye ataipunga mbele zaBwanana kuileta madhabahuni.

26 Kisha kuhani atachota sadaka ya nafaka mkono uliojaa kama sehemu ya kumbukumbu na kuiteketeza juu ya madhabahu, baada ya hayo, atamtaka huyo mwanamke anywe yale maji.

27 Kama amejitia unajisi na kukosa uaminifu kwa mumewe, wakati anapotakiwa anywe maji yale yaletayo laana, yatamwingia na kusababisha maumivu makali; tumbo lake litavimba na paja lake litapooza, naye atakuwa amelaaniwa miongoni mwa watu wake.

28 Hata hivyo, ikiwa huyo mwanamke hakujitia unajisi, naye ni safi, atasafishwa hatia na ataweza kuzaa watoto.

29 “ ‘Basi, hii ndiyo sheria ya wivu mwanamke anapopotoka na kujitia unajisi akiwa ameolewa na mumewe,

30 au hisia za wivu zinapomjia mwanaume kwa sababu ya kumshuku mkewe. Kuhani atamfanya huyo mwanamke kusimama mbele zaBwanana atatumia sheria hii yote kwa huyo mwanamke.

31 Mume atakuwa hana hatia ya kosa lolote, bali mwanamke atayachukua matokeo ya dhambi yake.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/5-67c5a126272d4a1a35b1946bc2c3f693.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 6

Mnadhiri

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Ikiwa mwanaume au mwanamke anataka kuweka nadhiri maalum, nadhiri ya kutengwa kwa ajili yaBwanakama Mnadhiri,

3 ni lazima ajitenge na mvinyo na kinywaji kingine chochote chenye chachu, na kamwe asinywe siki itokanayo na mvinyo au itokanayo na kinywaji kingine chenye chachu. Kamwe asinywe maji ya zabibu wala kula zabibu mbichi au kavu.

4 Kwa muda wote atakaokuwa Mnadhiri, kamwe hatakula chochote kitokanacho na mzabibu, sio mbegu wala maganda.

5 “ ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili yaBwana, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu mpaka kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili yaBwanakiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke.

6 Kwa kipindi chochote cha kujitenga kwa ajili yaBwanahatakaribia maiti.

7 Hata kama baba yake mwenyewe au mama au kaka au dada akifa, hatajinajisi mwenyewe kwa taratibu za ibada kwa ajili yao, kwa sababu ishara ya kujiweka wakfu kwake kwa Mungu ipo katika kichwa chake.

8 Kwa kipindi chote cha kujitenga kwake yeye ni wakfu kwaBwana.

9 “ ‘Kama mtu yeyote akifa ghafula karibu naye, atakuwa ametiwa unajisi nywele zake alizoziweka wakfu, hivyo ni lazima anyoe nywele zake siku ya utakaso wake, yaani siku ya saba.

10 Kisha siku ya nane ni lazima alete hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa kuhani katika mlango wa Hema la Kukutania.

11 Kuhani atatoa mmoja kama sadaka ya dhambi, na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa ili kufanya upatanisho kwa ajili yake kwa sababu ametenda dhambi kwa kuwepo mbele ya maiti. Siku iyo hiyo atakiweka wakfu kichwa chake.

12 Ni lazima ajitoe kabisa kwaBwanakwa kipindi cha kujitenga kwake, na ni lazima atoe mwana-kondoo wa mwaka mmoja kama sadaka ya hatia. Siku zilizopita hazitahesabiwa kwa sababu alijitia unajisi katika siku zake za kujitenga.

13 “ ‘Basi hii ndiyo sheria kwa ajili ya Mnadhiri baada ya kipindi chake cha kujitenga kupita. Ataletwa kwenye ingilio la Hema la Kukutania.

14 Hapo atatoa sadaka zake kwaBwana: yaani, mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kondoo mke wa mwaka mmoja asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume asiye na waa kwa ajili ya sadaka ya amani,

15 pamoja na sadaka zake za nafaka na za vinywaji, na kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, yaani maandazi yaliyotengenezwa kwa unga laini uliochanganywa na mafuta, na mikate myembamba iliyopakwa mafuta.

16 “ ‘Kuhani atavileta vitu hivyo mbele zaBwanana kufanya sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa.

17 Ataleta pia kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, na atatoa dhabihu kondoo dume kama sadaka ya amani kwaBwana, pamoja na sadaka yake ya nafaka na sadaka ya kinywaji.

18 “ ‘Kisha kwenye ingilio la Hema la Kukutania, Mnadhiri ni lazima anyoe nywele zake ambazo alikuwa ameziweka wakfu. Atazichukua hizo nywele na kuziweka ndani ya moto ulio chini ya dhabihu ya sadaka ya amani.

19 “ ‘Baada ya Mnadhiri kunyoa hizo nywele zake za kujitenga kwake, kuhani atampa mikononi mwake bega la kondoo dume lililochemshwa, na pia andazi na mkate mwembamba kutoka kwenye kikapu, vyote vikiwa vimetengenezwa bila kuwekwa chachu.

20 Kisha kuhani ataviinua mbele zaBwanakama sadaka ya kuinua; ni vitakatifu na ni mali ya kuhani, pamoja na kile kidari kilichoinuliwa na lile paja lililotolewa. Baada ya hayo, Mnadhiri anaweza kunywa divai.

21 “ ‘Hii ndiyo sheria ya Mnadhiri ambaye anaweka nadhiri kwa matoleo yake kwaBwanakufuatana na kujitenga kwake, zaidi ya chochote kile anachoweza kupata. Ni lazima atimize nadhiri aliyoiweka kufuatana na sheria ya Mnadhiri.’ ”

Baraka Ya Kikuhani

22 Bwanaakamwambia Mose,

23 “Mwambie Aroni na wanawe, ‘Hivi ndivyo mtakavyowabariki Waisraeli. Waambieni:

24 “ ‘ “Bwanaakubariki

na kukulinda;

25 Bwanaakuangazie nuru ya uso wake

na kukufadhili;

26 Bwanaakugeuzie uso wake

na kukupa amani.” ’

27 “Hivyo wataliweka Jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/6-9851c137e30f5a4ecb9302071f22f373.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 7

Sadaka Wakati Wa Kuweka Wakfu Maskani Ya Bwana

1 Mose alipomaliza kuisimamisha Maskani, aliitia mafuta na kuiweka wakfu pamoja na samani zake zote. Pia alitia madhabahu mafuta na kuiweka wakfu, pamoja na vyombo vyake vyote.

2 Ndipo viongozi wa Israeli, wale wakuu wa jamaa waliokuwa viongozi wa kabila wasimamizi wa wale waliohesabiwa, wakatoa sadaka.

3 Walizileta kama matoleo yao mbele zaBwana: magari sita ya kukokotwa yaliyofunikwa, pamoja na maksai kumi na wawili; yaani maksai mmoja kutoka kwa kila kiongozi, na gari moja la kukokotwa kutoka kwa kila viongozi wawili. Haya waliyaleta mbele ya Maskani.

4 Bwanaakamwambia Mose,

5 “Vikubali vitu hivi kutoka kwao, ili viweze kutumika katika kazi kwenye Hema la Kukutania. Wapatie Walawi kama kazi ya kila mtu itakavyohitaji.”

6 Hivyo Mose akachukua yale magari ya kukokotwa pamoja na maksai, na kuwapa Walawi.

7 Aliwapa Wagershoni magari mawili ya kukokotwa na maksai wanne, kama walivyohitaji kwa kazi yao,

8 na pia aliwapa Wamerari magari manne ya kukokotwa na maksai wanane, kama kazi yao ilivyohitaji. Wote walikuwa chini ya maelekezo ya Ithamari mwana wa kuhani, Aroni.

9 Lakini Mose hakuwapa Wakohathi chochote kati ya hivyo, kwa sababu walitakiwa kubeba vitu vitakatifu mabegani mwao, vile walikuwa wanawajibika.

10 Wakati madhabahu yalitiwa mafuta, viongozi walileta sadaka zao kwa ajili ya kule kuwekwa wakfu kwake na kuziweka mbele ya madhabahu.

11 Kwa maanaBwanaalikuwa amemwambia Mose, “Kila siku kiongozi mmoja ataleta sadaka yake ili kuwekwa wakfu madhabahu.”

12 Yule ambaye alileta sadaka yake siku ya kwanza alikuwa Nashoni, mwana wa Aminadabu, wa kabila la Yuda.

13 Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130,na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini,vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

14 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi,likiwa limejazwa uvumba;

15 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

16 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

17 maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.

18 Siku ya pili yake Nethaneli mwana wa Suari, kiongozi wa kabila la Isakari, alileta sadaka yake.

19 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

20 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

21 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

22 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

23 maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Nethaneli mwana wa Suari.

24 Siku ya tatu Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa kabila la Zabuloni, alileta sadaka yake.

25 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

26 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

27 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

28 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

29 maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Eliabu mwana wa Heloni.

30 Siku ya nne Elisuri mwana wa Shedeuri, kiongozi wa kabila la Reubeni, alileta sadaka yake.

31 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

32 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

33 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

34 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

35 maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Elisuri mwana wa Shedeuri.

36 Siku ya tano Shelumieli mwana wa Surishadai, kiongozi wa watu wa Simeoni, alileta sadaka yake.

37 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

38 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

39 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

40 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

41 maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Shelumieli mwana wa Surishadai.

42 Siku ya sita Eliasafu mwana wa Deueli, kiongozi wa watu wa Gadi, alileta sadaka yake.

43 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

44 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

45 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

46 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

47 maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Eliasafu mwana wa Deueli.

48 Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa watu wa Efraimu, alileta sadaka yake.

49 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

50 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

51 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

52 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

53 maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Elishama mwana wa Amihudi.

54 Siku ya nane Gamalieli mwana wa Pedasuri, kiongozi wa watu wa Manase, alileta sadaka yake.

55 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

56 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

57 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

58 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

59 maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Gamalieli mwana wa Pedasuri.

60 Siku ya tisa Abidani mwana wa Gideoni, kiongozi wa watu wa Benyamini, alileta sadaka yake.

61 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

62 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

63 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

64 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

65 maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Abidani mwana wa Gideoni.

66 Siku ya kumi Ahiezeri mwana wa Amishadai, kiongozi wa watu wa Dani, alileta sadaka yake.

67 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

68 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

69 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

70 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

71 maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Ahiezeri mwana wa Amishadai.

72 Siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, kiongozi wa watu wa Asheri, alileta sadaka yake.

73 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

74 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

75 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

76 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

77 maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani.

78 Siku ya kumi na mbili Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa watu wa Naftali, alileta sadaka yake.

79 Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

80 sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

81 fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

82 mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

83 maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Ahira mwana wa Enani.

84 Hizi ndizo zilikuwa sadaka za viongozi wa Israeli madhabahu yalipowekwa wakfu, wakati yalitiwa mafuta: sahani kumi na mbili za fedha, bakuli kumi na mbili za fedha za kunyunyizia, na masinia kumi na mawili ya dhahabu.

85 Kila sahani ya fedha ilikuwa na uzito wa shekeli 130, na kila bakuli la fedha la kunyunyizia lilikuwa na uzito wa shekeli sabini. Masinia yote kumi na mawili yalikuwa na uzito wa shekeli 2,400kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.

86 Sahani kumi na mbili za dhahabu zilizojazwa uvumba zilikuwa na uzito wa shekeli kumi kila moja, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Kwa jumla, sahani za dhahabu zilikuwa na uzito wa shekeli 120.

87 Jumla ya wanyama waliotolewa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa walikuwa fahali kumi na wawili wachanga, kondoo dume kumi na wawili na wana-kondoo dume kumi na wawili wa mwaka mmoja, pamoja na sadaka zao za nafaka. Mbuzi waume kumi na wawili walitolewa kwa ajili ya sadaka za dhambi.

88 Jumla ya wanyama kwa ajili ya dhabihu ya sadaka ya amani walikuwa maksai ishirini na wanne, kondoo dume sitini, mbuzi dume wa mwaka mmoja sitini na wana-kondoo dume wa mwaka mmoja sitini. Hizi ndizo zilikuwa sadaka zilizoletwa kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu baada ya kutiwa mafuta.

89 Mose alipoingia kwenye Hema la Kukutania kuzungumza naBwana, alisikia sauti ikisema naye kutoka kati ya wale makerubi wawili waliokuwa juu ya kile kiti cha rehema, juu ya Sanduku la Ushuhuda. Mose akazungumza naye.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/7-ed01d157c4698a513d1d7d46ca969b24.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 8

Kuwekwa Kwa Taa

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Aroni umwambie, ‘Wakati utakapoziweka zile taa saba, zinatakiwa kuangaza eneo lililo mbele ya kinara cha taa.’ ”

3 Aroni akafanya hivyo; akaziweka zile taa ili zielekee mbele kwenye kinara cha taa, kama vileBwanaalivyomwamuru Mose.

4 Hivi ndivyo kinara cha taa kilivyotengenezwa: Kilitengenezwa kwa dhahabu iliyofuliwa, kuanzia kwenye kitako chake hadi kwenye maua yake. Kinara cha taa kilitengenezwa sawasawa kabisa na kielelezo ambachoBwanaalikuwa amemwonyesha Mose.

Kutengwa Kwa Walawi Kwa Ajili Ya Bwana

5 Bwanaakamwambia Mose:

6 “Watwae Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli wengine na uwatakase kwa kawaida ya ibada.

7 Ili kuwatakasa fanya hivi: Nyunyizia maji ya utakaso juu yao; kisha uwaambie wanyoe nywele kwenye mwili mzima, wafue nguo zao na hivyo wajitakase wenyewe.

8 Waambie wamchukue fahali mchanga pamoja na sadaka yake ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta; kisha utamchukua fahali mchanga wa pili kwa ajili ya sadaka ya dhambi.

9 Walete Walawi mbele ya Hema la Kukutania na ukusanye jumuiya yote ya Waisraeli.

10 Utawaleta Walawi mbele zaBwana, na Waisraeli wataweka mikono yao juu ya Walawi.

11 Aroni atawaweka Walawi mbele zaBwanakama sadaka ya kuinua kutoka kwa Waisraeli, ili kwamba wawe tayari kuifanya kazi yaBwana.

12 “Baada ya Walawi kuweka mikono yao juu ya vichwa vya hao mafahali wawili, tumia mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi kwaBwana, na mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Walawi.

13 Waambie hao Walawi wasimame mbele ya Aroni na wanawe, kisha wawatoe kama sadaka ya kuinuliwa kwaBwana.

14 Kwa njia hii utakuwa umewatenga Walawi kutoka kwa Waisraeli wengine, nao Walawi watakuwa wangu.

15 “Utakapokuwa umekwisha kuwatakasa Walawi na kuwatoa kama sadaka ya kuinuliwa, watakuja kufanya kazi yao katika Hema la Kukutania.

16 Wao ndio Waisraeli ambao watatolewa kabisa kwangu. Nimewatwaa kama mali yangu mwenyewe badala ya mzaliwa wa kwanza, mzaliwa wa kwanza wa kiume kutoka kwa kila mwanamke wa Kiisraeli.

17 Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume katika Israeli, awe wa mwanadamu au mnyama, ni wangu. Wakati nilipowaua wazaliwa wote wa kwanza huko Misri, niliwatenga kwa ajili yangu mwenyewe.

18 Nami nimewatwaa Walawi badala ya wazaliwa wote wa kwanza wa kiume katika Israeli.

19 Kati ya Waisraeli wote, nimempa Aroni na wanawe Walawi kama zawadi ili wafanye kazi katika Hema la Kukutania kwa niaba ya Waisraeli, na kufanya upatanisho kwa ajili yao ili pasiwepo na pigo lolote litakalowapata Waisraeli wakati watakapokaribia mahali patakatifu.”

20 Mose, Aroni na jumuiya yote ya Waisraeli wakawafanyia Walawi kamaBwanaalivyomwamuru Mose.

21 Walawi wakajitakasa wenyewe na wakafua nguo zao. Kisha Aroni akawasogeza mbele zaBwanakuwa sadaka ya kuinuliwa, na kufanya upatanisho kwa ajili yao ili kuwatakasa.

22 Baada ya hayo, Walawi walikuja kufanya kazi yao katika Hema la Kukutania chini ya usimamizi wa Aroni na wanawe. Waliwafanyia Walawi kama vileBwanaalivyomwamuru Mose.

23 Bwanaakamwambia Mose,

24 “Hili linawahusu Walawi: Wanaume wenye umri wa miaka ishirini na mitano au zaidi watakuja kushiriki katika kazi kwenye Hema la Kukutania,

25 lakini watakapofika umri wa miaka hamsini, ni lazima waache kazi zao za kawaida wala wasiendelee.

26 Wanaweza kuwasaidia ndugu zao kufanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, lakini wao wenyewe kamwe hawatafanya hiyo kazi. Basi, hivi ndivyo utakavyogawa wajibu kwa Walawi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/8-9c3b2beda352a25ba9fadd06a50575b1.mp3?version_id=1627—

Categories
Hesabu

Hesabu 9

Pasaka Huko Sinai

1 Bwanaakasema na Mose katika Jangwa la Sinai katika mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka Misri. Akasema,

2 “Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamriwa.

3 Adhimisheni wakati ulioamriwa, yaani wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi huu, kufuatana na desturi zake zote na masharti yake.”

4 Hivyo Mose akawaambia Waisraeli waiadhimishe Pasaka,

5 nao wakafanya hivyo kwenye Jangwa la Sinai wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Waisraeli wakafanya kila kitu kama vileBwanaalivyomwamuru Mose.

6 Lakini baadhi yao hawakuweza kuadhimisha Pasaka siku ile kwa sababu walikuwa najisi kwa taratibu za kiibada kwa ajili ya kugusa maiti. Kwa hiyo wakamwendea Mose na Aroni siku ile ile,

7 wakamwambia Mose, “Tumekuwa najisi kwa sababu tumegusa maiti, lakini kwa nini tuzuiliwe kumtoleaBwanasadaka yake pamoja na Waisraeli wengine katika wakati ulioamriwa?”

8 Mose akawajibu, “Ngojeni mpaka nitafute kileBwanaanachoagiza kuwahusu ninyi.”

9 NdipoBwanaakamwambia Mose,

10 “Waambie Waisraeli: ‘Wakati mmoja wenu au wazao wenu wanapokuwa najisi kwa sababu ya maiti au wakiwa safarini, hata hivyo wanaweza kuadhimisha Pasaka yaBwana.

11 Wataiadhimisha wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Watamla mwana-kondoo, pamoja na mkate usiotiwa chachu, na mboga chungu.

12 Wasibakize chochote hadi asubuhi wala wasivunje mifupa ya mwana-kondoo. Wakati wanapoadhimisha Pasaka, hawana budi kufuata masharti yote.

13 Lakini kama mtu ni safi kwa taratibu za kiibada naye hayuko safarini, asipoadhimisha Pasaka, mtu huyo hana budi kukatiliwa mbali na watu wake kwa sababu hakutoa sadaka yaBwanakwa wakati ulioamriwa. Mtu huyo atawajibika kubeba matokeo ya dhambi yake.

14 “ ‘Mgeni anayeishi miongoni mwenu ambaye anataka kuadhimisha Pasaka yaBwana, lazima afanye hivyo kwa kufuata desturi na masharti. Lazima masharti yawe sawasawa kwa mgeni na mzawa.’ ”

Wingu La Moto Juu Ya Maskani

15 Katika siku hiyo ambayo Maskani, Hema la Ushuhuda, iliposimamishwa, wingu liliifunika. Kuanzia jioni mpaka asubuhi wingu lililokuwa juu ya Maskani lilionekana kama moto.

16 Hivyo ndivyo lilivyoendelea kuwa; wingu liliifunika wakati wa mchana, na usiku lilionekana kama moto.

17 Wakati wowote wingu lilipoinuka kutoka juu ya Hema, nao Waisraeli waliondoka; mahali popote wingu liliposimama, Waisraeli walipiga kambi.

18 Kwa amri yaBwanaWaisraeli waliondoka, na kwa amri yake walipiga kambi. Kwa muda wote wingu liliposimama juu ya Maskani, Waisraeli walibaki wamepiga kambi.

19 Wakati wingu lilipobaki juu ya Maskani kwa muda mrefu, Waisraeli walitii amri yaBwananao hawakuondoka.

20 Wakati mwingine wingu lilikuwa juu ya Maskani kwa siku chache tu; kwa amri yaBwanawangelipiga kambi na kisha kwa amri yake wangeliondoka.

21 Wakati mwingine wingu lilikuwepo kuanzia jioni mpaka asubuhi tu, na lilipoinuka asubuhi, nao waliondoka. Ikiwa ni mchana au usiku, wakati wowote wingu lilipoinuka, waliondoka.

22 Ikiwa wingu lilikaa juu ya Maskani kwa siku mbili au mwezi au mwaka, Waisraeli wangebaki wamepiga kambi na hawakuondoka; lakini lilipoinuka, wangeondoka.

23 Kwa amri yaBwanawalipiga kambi, na kwa amri yaBwanawaliondoka. Walitii amri yaBwana, kufuatana na agizo lake kupitia Mose.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/NUM/9-befe803cce6de1a5d4676487a0b545ea.mp3?version_id=1627—