Categories
Ezekieli

Ezekieli 30

Maombolezo Kwa Ajili Ya Misri

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Ombolezeni ninyi na mseme,

“Ole wa siku ile!”

3 Kwa kuwa siku ile imekaribia,

siku yaBwanaimekaribia,

siku ya mawingu,

siku ya maangamizi kwa mataifa.

4 Upanga utakuja dhidi ya Misri,

nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia.

Mauaji yatakapoangukia Misri,

utajiri wake utachukuliwa

na misingi yake itabomolewa.

5 Kushina Putu, Ludi na Arabia yote, Libyana watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.

6 “ ‘Hili ndiloBwanaasemalo:

“ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka

na kiburi cha nguvu zake kitashindwa.

Kutoka Migdoli hadi Aswani,

watauawa ndani yake kwa upanga,

asemaBwanaMwenyezi.

7 “ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa

miongoni mwa nchi zilizo ukiwa,

nayo miji yao itakuwa magofu

miongoni mwa miji iliyo magofu.

8 Ndipo watakapojua kwamba mimi ndimiBwana,

nitakapoiwasha Misri moto

na wote wamsaidiao watapondwa.

9 “ ‘Siku hiyo wajumbe watatoka kwangu kwa merikebu, ili kuwatia hofu Ethiopia, wakiwa katika hali yao ya kuridhika. Maumivu makali yatawapata siku ya maangamizi ya Misri, kwa kuwa hakika itakuja.

10 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Nitakomesha makundi ya wajeuri ya Misri

kwa mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli.

11 Yeye na jeshi lake, taifa lililo katili kuliko mataifa yote,

litaletwa ili kuangamiza nchi.

Watafuta panga zao dhidi ya Misri

na kuijaza nchi kwa waliouawa.

12 Nitakausha vijito vya Naili

na nitaiuza nchi kwa watu waovu,

kwa mkono wa wageni,

nitaifanya nchi ukiwa na kila kitu

kilichomo ndani yake.

MimiBwananimenena haya.

13 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Nitaangamiza sanamu

na kukomesha vinyago katika Memfisi

Hapatakuwepo tena na mkuu katika nchi ya Misri,

nami nitaeneza hofu katika nchi nzima.

14 Nitaifanya Pathrosikuwa ukiwa

na kuitia moto Soani,

nami nitaipiga kwa adhabu Thebesi

15 Nitaimwaga ghadhabu yangu juu ya Pelusiumu,

ngome ya Misri,

nami nitakatilia mbali

makundi ya wajeuri wa Thebesi.

16 Nitaitia moto nchi ya Misri;

Pelusiumu itagaagaa kwa maumivu makuu.

Thebesi itachukuliwa na tufani,

Memfisi itakuwa katika taabu daima.

17 Wanaume vijana wa Onina wa Pi-Besethi

wataanguka kwa upanga

nayo hiyo miji itatekwa.

18 Huko Tahpanhesi mchana utatiwa giza

nitakapovunja kongwa la Misri;

hapo kiburi cha nguvu zake kitakoma.

Atafunikwa na mawingu

na vijiji vyake vitatekwa.

19 Kwa hiyo nitaipiga Misri kwa adhabu,

nao watajua kuwa Mimi ndimiBwana.’ ”

20 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa kwanza, siku ya saba, neno laBwanalikanijia kusema:

21 “Mwanadamu, nimevunja mkono wa Farao mfalme wa Misri. Haukufungwa ili upone au kuwekewa kipande cha ubao ili upate nguvu za kuweza kuchukua upanga.

22 Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na Farao mfalme wa Misri. Nitavunja mikono yake yote miwili, ule mkono ulio mzima pia na ule uliovunjika na kuufanya upanga uanguke toka mkononi mwake.

23 Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi zote.

24 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli na kuutia upanga wangu mkononi mwake, lakini nitavunja mikono ya Farao, naye atalia kwa huzuni mbele yake kama mtu aliyetiwa jeraha la kumfisha.

25 Nitaitia nguvu mikono ya mfalme wa Babeli, lakini mikono ya Farao italegea. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwana, nitakapoutia upanga wangu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye ataunyoosha dhidi ya Misri.

26 Nitawatawanya Wamisri miongoni mwa mataifa na kuwafukuza huku na huko katika nchi mbalimbali. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwana.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/30-1df7d03bab06f06833e454751ecfd504.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 31

Mwerezi Katika Lebanoni

1 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa tatu, siku ya kwanza, neno laBwanalikanijia, kusema:

2 “Mwanadamu, mwambie Farao mfalme wa Misri na makundi yake ya wajeuri:

“ ‘Je, ni nani awezaye kulinganishwa

na wewe katika fahari.

3 Angalia Ashuru, wakati fulani ilikuwa mwerezi huko Lebanoni,

ukiwa na matawi mazuri ukitia msitu kivuli;

ulikuwa mrefu sana,

kilele chake kilipita majani ya miti yote.

4 Maji mengi yaliustawisha,

chemchemi zenye maji mengi ziliufanya urefuke;

vijito vyake vilitiririka pale

ulipoota pande zote

na kupeleka mifereji yake

kwenye miti yote ya shambani.

5 Hivyo ukarefuka

kupita miti yote ya shambani;

vitawi vyake viliongezeka

na matawi yake yakawa marefu,

yakitanda kwa sababu ya wingi wa maji.

6 Ndege wote wa angani

wakaweka viota kwenye vitawi vyake,

wanyama wote wa shambani

wakazaana chini ya matawi yake,

mataifa makubwa yote

yaliishi chini ya kivuli chake.

7 Ulikuwa na fahari katika uzuri,

ukiwa na matawi yaliyotanda,

kwa kuwa mizizi yake ilikwenda chini

mpaka kwenye maji mengi.

8 Mierezi katika bustani ya Mungu

haikuweza kushindana nao,

wala misunobari haikuweza

kulingana na vitawi vyake,

wala miaramoni

haikulinganishwa na matawi yake,

wala hakukuwa na mti katika bustani ya Mungu

wa kulinganisha na uzuri wake.

9 Niliufanya kuwa mzuri

ukiwa na matawi mengi,

ulionewa wivu na miti yote ya Edeni

katika bustani ya Mungu.

10 “ ‘Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa sababu ulikuwa mrefu sana, kilele chake kikiwa juu ya majani manene ya miti na kwa sababu ulikuwa na kiburi cha urefu wake,

11 niliutia mikononi mwa mtawala wa mataifa, ili yeye aushughulikie sawasawa na uovu wake. Nikaukatilia mbali,

12 nayo mataifa mageni yaliyo makatili sana yaliukata huo mti na kuuacha. Matawi yake yalianguka juu ya milima na kwenye mabonde yote, vitawi vyake vikavunjika na kusambaa katika makorongo yote ya nchi. Mataifa yote ya duniani yakaondoka kutoka kwenye kivuli chake na kuuacha.

13 Ndege wote wa angani wakakaa kwenye ule mti ulioanguka na wanyama pori wote wakakaa katikati ya vitawi vyake.

14 Kamwe hakutakuwa na miti mingine kando ya hayo maji itakayorefuka zaidi ya huo, vilele vyake vikiwa juu ya majani yote ya miti. Hakuna miti mingine, hata kama imekunywa maji vizuri namna gani, itakayofikia urefu huo. Yote mwisho wake ni kifo, na kuingia ardhini, kama vile ilivyo kwa wanadamu, pamoja na wale waendao shimoni.

15 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Katika siku ile mwerezi uliposhushwa chini kaburininilizifunika chemchemi zenye maji mengi kwa maombolezo: Nilivizuia vijito vyake na wingi wa maji yake nikauzuia. Kwa sababu yake niliivika Lebanoni huzuni, nayo miti yote ya shambani ikanyauka.

16 Niliyafanya mataifa yatetemeke kwa kishindo cha kuanguka kwake wakati nilipoushusha chini kaburini pamoja na wale washukao shimoni. Ndipo miti yote ya Edeni, miti iliyo bora kuliko yote na iliyo mizuri sana ya Lebanoni, miti yote ile iliyokunywa maji vizuri, ilifarijika hapa duniani.

17 Wale walioishi katika kivuli chake, wale walioungana naye miongoni mwa mataifa, nao pia walikuwa wamezikwa pamoja naye, wakiungana na wale waliouawa kwa upanga.

18 “ ‘Ni miti ipi ya Edeni inayoweza kulinganishwa nawe kwa fahari na utukufu? Hata hivyo, wewe pia, utashushwa chini pamoja na miti ya Edeni mpaka kuzimu, utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.

“ ‘Huyu ni Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/31-2981f288694f100387272388ec45df59.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 32

Maombolezo Kwa Ajili Ya Farao

1 Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, neno laBwanalikanijia, kusema:

2 “Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Farao mfalme wa Misri na umwambie:

“ ‘Wewe ni kama simba miongoni mwa mataifa,

wewe ni kama joka kubwa baharini,

unayevuruga maji kwa miguu yako

na kuchafua vijito.

3 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Nikiwa pamoja na wingi mkubwa wa watu

nitautupa wavu wangu juu yako,

nao watakukokota katika wavu wangu.

4 Nitakutupa nchi kavu

na kukuvurumisha uwanjani.

Nitawafanya ndege wote wa angani watue juu yako

na wanyama wote wa nchi

watajishibisha nyama yako.

5 Nitatawanya nyama yako juu ya milima

na kujaza mabonde kwa mabaki yako.

6 Nitailowanisha nchi kwa damu yako inayotiririka

njia yote hadi milimani,

nayo mabonde yatajazwa na nyama yako.

7 Nitakapokuzimisha, nitafunika mbingu

na kuzitia nyota zake giza;

nitalifunika jua kwa wingu,

nao mwezi hautatoa nuru yake.

8 Mianga yote itoayo nuru angani

nitaitia giza juu yako;

nitaleta giza juu ya nchi yako,

asemaBwanaMwenyezi.

9 Nitaifadhaisha mioyo ya mataifa mengi

nitakapokuangamiza miongoni mwa mataifa,

nikikuleta uhamishoni miongoni mwa nchi

ambazo haujapata kuzijua.

10 Nitayafanya mataifa mengi wakustaajabie,

wafalme wao watatetemeka

kwa hofu kwa ajili yako

nitakapotikisa upanga wangu mbele yao.

Siku ya anguko lako

kila mmoja wao atatetemeka

kila dakika kwa ajili ya maisha yake.

11 “ ‘Kwa kuwa hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo:

“ ‘Upanga wa mfalme wa Babeli

utakuja dhidi yako.

12 Nitafanya makundi yako ya wajeuri kuanguka

kwa panga za watu mashujaa,

taifa katili kuliko mataifa yote.

Watakivunjavunja kiburi cha Misri,

nayo makundi yake yote

ya wajeuri yatashindwa.

13 Nitaangamiza mifugo yake yote

wanaojilisha kando ya maji mengi,

hayatavurugwa tena kwa mguu wa mwanadamu

wala kwato za mnyama

hazitayachafua tena.

14 Kisha nitafanya maji yake yatulie

na kufanya vijito vyake

vitiririke kama mafuta,

asemaBwanaMwenyezi.

15 Nitakapoifanya Misri kuwa ukiwa

na kuiondolea nchi kila kitu

kilichomo ndani yake,

nitakapowapiga wote waishio humo,

ndipo watakapojua kuwa

Mimi ndimiBwana.’

16 “Hili ndilo ombolezo watakalomwimbia. Binti za mataifa wataliimba, kwa kuwa Misri na makundi yake yote ya wajeuri wataliimba, asemaBwanaMwenyezi.”

17 Katika mwaka wa kumi na mbili, mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi, neno laBwanalikanijia kusema:

18 “Mwanadamu, omboleza kwa ajili ya makundi ya wajeuri wa Misri na uwatupe kuzimu yeye na binti za mataifa yenye nguvu, waende huko pamoja nao washukao shimoni.

19 Je, ninyi mnamzidi nani kwa uzuri? Shukeni chini! Nanyi mkalazwe pamoja na hao wasiotahiriwa!

20 Wataanguka miongoni mwa wale waliouawa kwa upanga. Upanga umefutwa, mwache aburutwe mbali pamoja na hao wajeuri wake wote.

21 Kutoka kuzimu viongozi hodari watanena kuhusu Misri pamoja na wale walioungana nao, ‘Wameshuka chini, nao wamelala kimya pamoja na hao wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.’

22 “Ashuru yuko huko pamoja na jeshi lake lote, amezungukwa na makaburi ya watu wake wote waliouawa, wale wote walioanguka kwa upanga.

23 Makaburi yao yako kwenye kina cha chini cha shimo na jeshi lake limelala kulizunguka kaburi lake. Wote waliokuwa wameeneza hofu kuu katika nchi ya walio hai wameuawa, wameanguka kwa upanga.

24 “Elamu yuko huko, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote wameuawa, wameanguka kwa upanga. Wote waliokuwa wameeneza hofu katika nchi ya walio hai walishuka kuzimu bila kutahiriwa. Wanaichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni.

25 Kitanda kimetandikwa kwa ajili yake miongoni mwa waliouawa, pamoja na makundi yake yote ya wajeuri wakiwa wamelizunguka kaburi lake. Wote ni watu wasiotahiriwa, wameuawa kwa upanga. Kwa sababu vitisho vyao vilienea katika nchi ya walio hai, wameichukua aibu yao pamoja na wale washukao shimoni, nao wamewekwa miongoni mwa waliouawa.

26 “Mesheki na Tubali wako humo, pamoja na makundi yao ya wajeuri wakiwa wameyazunguka makaburi yao. Wote hawakutahiriwa, wameuawa kwa upanga kwa sababu walieneza vitisho vyao katika nchi ya walio hai.

27 Je, hawakulala na mashujaa wengine wasiotahiriwa waliouawa, ambao wameshuka kaburini wakiwa na silaha zao za vita, ambao panga zao ziliwekwa chini ya vichwa vyao na uovu wao juu ya mifupa yao? Adhabu kwa ajili ya dhambi zao ilikuwa juu ya mifupa yao, ingawa vitisho vya mashujaa hawa vilikuwa vimeenea hadi kwenye nchi ya walio hai.

28 “Wewe pia, ee Farao, utavunjwa nawe utalala miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.

29 “Edomu yuko humo, wafalme wake wote na wakuu wake wote, ambao ijapokuwa wana nguvu, wamelazwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga. Wamelala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale washukao shimoni.

30 “Wakuu wote wa kaskazini na Wasidoni wote wako huko, wameshuka chini pamoja na waliouawa kwa aibu ijapokuwa kuna vitisho vilivyosababishwa na nguvu zao. Wamelala bila kutahiriwa pamoja na wale waliouawa kwa upanga na kuchukua aibu yao pamoja na wale washukao chini shimoni.

31 “Farao, yeye pamoja na jeshi lake lote, atakapowaona atafarijiwa kwa ajili ya makundi yake yote ya wajeuri, wale waliouawa kwa upanga, asemaBwanaMwenyezi.

32 Ingawa nilimfanya Farao aeneze vitisho vyake katika nchi ya walio hai, Farao pamoja na makundi yake yote ya wajeuri watalazwa miongoni mwa wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga, asemaBwanaMwenyezi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/32-f004430cd7113fc65cb6929eca50cbac.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 33

Wajibu Wa Ezekieli Kuwa Mlinzi Kwa Watu Wake

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, sema na watu wako uwaambie, ‘Nitakapoleta upanga dhidi ya nchi, nao watu wa nchi wakamchagua mmoja wa watu wao na kumfanya awe mlinzi wao,

3 naye auonapo upanga unakuja dhidi ya nchi na kupiga tarumbeta kuonya watu,

4 kama mtu yeyote asikiapo sauti ya tarumbeta hakukubali kuonywa, basi upanga ujapo na kuutoa uhai wake, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.

5 Kwa kuwa alisikia sauti ya tarumbeta lakini hakukubali maonyo, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe. Kama angekubali maonyo, angelijiokoa mwenyewe.

6 Lakini kama mlinzi akiona upanga unakuja na asipige tarumbeta kuonya watu na upanga ukija na kutoa uhai wa mmoja wao, yule mtu ataondolewa kwa sababu ya dhambi yake, lakini damu yake nitaitaka mkononi mwa mlinzi huyo.’

7 “Mwanadamu, nimekufanya wewe kuwa mlinzi kwa ajili ya nyumba ya Israeli, kwa hiyo sikia neno nisemalo na uwape maonyo kutoka kwangu.

8 Nimwambiapo mtu mwovu, ‘Ewe mtu mwovu, hakika utakufa,’ nawe hukusema neno la kumwonya ili atoke katika njia zake, yule mtu mwovu atakufa kwa ajili ya dhambi yake, mimi nitaitaka damu yake mkononi mwako.

9 Lakini kama utamwonya huyo mtu mwovu aache njia zake mbaya naye hafanyi hivyo, atakufa kwa ajili ya dhambi yake, lakini utakuwa umejiokoa mwenyewe.

10 “Mwanadamu, sema na nyumba ya Israeli uwaambie, ‘Hili ndilo mnalosema: “Makosa yetu na dhambi zetu zimetulemea, nasi tunadhoofika kwa sababu ya hayo. Tutawezaje basi kuishi?” ’

11 Waambie, ‘Hakika kama mimi niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, sifurahii kifo cha watu waovu, bali kwamba wageuke kutoka njia zao mbaya wapate kuishi. Geukeni! Geukeni kutoka njia zenu mbaya! Kwa nini mkafe, ee nyumba ya Israeli?’

12 “Kwa hiyo, mwanadamu, waambie watu wako, ‘Haki ya mtu mwenye haki haitamwokoa wakati anapoacha kutii, wala uovu wa mtu mwovu hautamsababisha yeye kuanguka anapotubu na kuacha uovu. Mtu mwenye haki, kama akitenda dhambi, hataishi kwa sababu ya uadilifu wake wa awali.’

13 Kama nikimwambia mtu mwenye haki kwamba hakika utaishi, lakini akategemea hiyo haki yake na kutenda uovu, hakuna tendo lolote la haki alilotenda litakalokumbukwa, atakufa kwa ajili ya uovu alioutenda.

14 Nami kama nikimwambia mtu mwovu, ‘Hakika utakufa,’ kisha akageuka kutoka dhambi yake na kufanya lile lililo haki na sawa,

15 kama akirudisha kile alichochukua rehani kwa ajili ya deni, akarudisha alichoiba na kufuata amri zile ziletazo uzima, wala hafanyi uovu, hakika ataishi, hatakufa.

16 Hakuna dhambi yoyote aliyoitenda itakayokumbukwa juu yake. Ametenda lile lililo haki na sawa, hakika ataishi.

17 “Lakini watu wako wanasema, ‘Njia ya Bwana si sawa.’ Lakini ni njia zao ambazo si sawa.

18 Kama mtu mwenye haki akigeuka kutoka uadilifu wake na kufanya uovu, atakufa kwa ajili ya huo uovu.

19 Naye mtu mwovu kama akigeuka kutoka uovu wake na kufanya lile lililo haki na sawa, kwa kufanya hivyo ataishi.

20 Lakini, ee nyumba ya Israeli, unasema, ‘Njia ya Bwana si sawa.’ Lakini nitamhukumu kila mmoja wenu sawasawa na njia zake mwenyewe.”

Anguko La Yerusalemu Laelezewa

21 Mwaka wa kumi na mbili wa uhamisho wetu, mwezi wa kumi, siku ya tano, mtu aliyekuwa ametoroka kutoka Yerusalemu akanijia na kusema, “Mji wa Yerusalemu umeanguka!”

22 Basi jioni kabla mtu huyo hajaja, mkono waBwana, ulikuwa juu yangu, naye alifungua kinywa changu kabla ya mtu yule aliyenijia asubuhi hajafika. Basi kinywa changu kilifunguliwa na sikuweza tena kunyamaza.

23 Ndipo neno laBwanalikanijia kusema:

24 “Mwanadamu, watu wanaoishi katika magofu hayo katika nchi ya Israeli wanasema hivi, ‘Abrahamu alikuwa mtu mmoja tu, hata hivyo akaimiliki nchi. Lakini sisi ni wengi, hakika tumepewa nchi kuwa milki yetu.’

25 Kwa hiyo waambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa kuwa mnakula nyama pamoja na damu na kuinulia sanamu zenu macho na kumwaga damu, je, mtaimiliki nchi?

26 Mnategemea panga zenu, mnafanya mambo ya machukizo na kila mmoja wenu humtia unajisi mke wa jirani yake. Je, mtaimiliki nchi?’

27 “Waambie hivi: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, wale waliobaki katika magofu wataanguka kwa upanga, wale walio nje mashambani nitawatoa wararuliwe na wanyama pori, nao wale walio katika ngome na kwenye mapango watakufa kwa tauni.

28 Nitaifanya nchi kuwa ukiwa na utupu na kiburi cha nguvu zake zitafikia mwisho, nayo milima ya Israeli itakuwa ukiwa ili mtu yeyote asipite huko.

29 Kisha watajua kuwa Mimi ndimiBwana, nitakapokuwa nimeifanya nchi kuwa ukiwa na utupu kwa sababu ya mambo yote ya machukizo waliyotenda.’

30 “Kwa habari yako wewe, mwanadamu, watu wako wanaongea habari zako wakiwa karibu na kuta na kwenye milango ya nyumba, wakiambiana kila mmoja na mwenzake, ‘Njooni msikie ujumbe ule utokao kwaBwana.’

31 Watu wangu wanakujia, kama wafanyavyo, nao wanaketi mbele yako kama watu wangu na kusikiliza maneno yako, lakini hawayatendi. Kwa maana udanganyifu u katika midomo yao, lakini mioyo yao ina tamaa ya faida isiyo halali.

32 Naam, mbele yao umekuwa tu kama yeye aimbaye nyimbo za mapenzi kwa sauti nzuri za kuvutia na kupiga vyombo kwa ustadi, kwa kuwa wanasikia maneno yako lakini hawayatendi.

33 “Wakati mambo haya yote yatakapotimia, kwa kuwa hakika yatatokea, ndipo watakapojua kwamba nabii amekuwepo miongoni mwao.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/33-27a165227a9aa7e31b9ae8a128143a53.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 34

Wachungaji Na Kondoo

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, tabiri juu ya wachungaji wa Israeli, tabiri na uwaambie: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ole wa wachungaji wa Israeli ambao hujitunza wenyewe tu! Je, haiwapasi wachungaji kutunza kundi la kondoo?

3 Mnakula mafuta ya wanyama, mnavaa mavazi ya sufu na kuchinja kondoo walionona, lakini hamlitunzi kundi.

4 Hamkuwatia nguvu walio dhaifu wala hamkuwaganga wenye maradhi wala kuwafunga waliojeruhiwa. Hamkuwarudisha waliotangatanga wala kuwatafuta wale waliopotea. Badala yake mmewatawala kwa ukali na kwa ukatili.

5 Hivyo walitawanyika kwa sababu hapakuwepo mchungaji, nao walipotawanyika, wakawa chakula cha wanyama wa mwitu wote.

6 Kondoo wangu walitawanyika, wakatangatanga kwenye milima yote na kwenye kila kilima kirefu. Kondoo wangu walitawanyika juu ya uso wa dunia yote bila kuwa na yeyote wa kuwaulizia wala wa kuwatafuta.

7 “ ‘Kwa hiyo, ninyi wachungaji, lisikieni neno laBwana:

8 Kwa hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, kwa sababu kondoo zangu wamekosa mchungaji na hivyo wametekwa nyara na kuwa chakula cha wanyama wote wa mwituni na kwa sababu wachungaji wangu, hawakuwatafuta kondoo zangu, bali wachungaji wamejitunza wenyewe, nao hawakuwalisha kondoo zangu,

9 kwa hiyo enyi wachungaji, sikieni neno laBwana:

10 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume na wachungaji nami nitawadai kondoo zangu mikononi mwao. Nitawafukuza kutoka kwenye kuchunga kundi langu, ili wachungaji wasiendelee kujitunza wenyewe. Nitaokoa kondoo zangu kutoka kwenye vinywa vyao, nao kondoo hawatakuwa tena chakula chao.

11 “ ‘Kwa kuwa hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitawaulizia kondoo wangu na kuwatafuta.

12 Kama vile mchungaji atafutavyo kundi lake lililotawanyika wakati akiwa pamoja nalo, hivyo ndivyo nitakavyowatafuta kondoo wangu. Nitawaokoa kutoka mahali pote walipokuwa wametawanyikia katika siku ya mawingu na giza nene.

13 Nitawatoa katika mataifa na kuwakusanya kutoka nchi mbalimbali, nami nitawaleta katika nchi yao wenyewe. Nitawalisha kwenye milima ya Israeli, katika mabonde na mahali pote panapokalika katika nchi.

14 Nitawachunga kwenye malisho mazuri na miinuko ya mlima wa Israeli patakuwa mahali pao pa malisho. Huko watajipumzisha kwa amani katika nchi ya malisho mazuri, nao watajilisha huko katika malisho tele katika milima ya Israeli.

15 Mimi mwenyewe nitawachunga kondoo zangu na kuwafanya wapumzike, asemaBwanaMwenyezi.

16 Nitawaulizia kondoo waliopotea na kuwaleta waliotangatanga. Nitawafunga waliojeruhiwa na kuwatia nguvu walio dhaifu lakini wale waliojikinai na wenye nguvu nitawaangamiza. Nitalichunga kundi kwa haki.

17 “ ‘Kwa habari yenu, enyi kundi langu, hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitahukumu kati ya kondoo na kondoo, kati ya kondoo dume na mbuzi.

18 Je, haiwatoshi ninyi kujilisha kwenye malisho mazuri? Je, ni lazima ninyi kuyakanyaga pia malisho yenu yaliyobaki kwa miguu yenu? Je, haiwatoshi ninyi kunywa maji safi? Je, ni lazima kuyachafua maji mengine kwa miguu yenu?

19 Je, ni lazima kundi langu wajilishe kwa yale mliyoyakanyaga na kunywa maji mliyoyachafua kwa miguu yenu?

20 “ ‘Kwa hiyo, hili ndiloBwanaMwenyezi awaambialo: Tazama, mimi mwenyewe nitahukumu kati ya kondoo wanono na waliokonda.

21 Kwa sababu mmewapiga kikumbo na kuwapiga kwa pembe zenu kondoo wote walio dhaifu mpaka wakawafukuza,

22 nitaliokoa kundi langu na hawatatekwa nyara tena. Nitahukumu kati ya kondoo na kondoo.

23 Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi, naye atawachunga, atawachunga na kuwa mchungaji wao.

24 MimiBwananitakuwa Mungu wao, naye mtumishi wangu Daudi atakuwa mkuu miongoni mwao. MimiBwananimenena.

25 “ ‘Nitafanya nao Agano la amani na kuwaondoa wanyama wa mwitu kutoka nchi yao ili kondoo wangu waweze kupumzika nyikani na msituni kwa salama.

26 Nitawabariki wao pamoja na maeneo yanayozunguka kilima changu. Nitawanyeshea mvua kwa majira yake, kutakuwepo mvua za baraka.

27 Miti ya shambani itatoa matunda yake na ardhi itatoa mazao yake, watu watakaa salama katika nchi yao. Watajua kuwa Mimi ndimiBwana, nitakapovunja vifungo vya nira zao na kuwaokoa kutoka mikono ya wale waliowafanya watumwa.

28 Hawatatekwa tena nyara na mataifa, wala wanyama pori hawatawala tena. Wataishi kwa salama, wala hakuna yeyote atakayewatia hofu.

29 Nitawapa nchi yenye sifa kutokana na mazao yake, hawatapatwa na njaa katika nchi tena wala hawatadharauliwa na mataifa.

30 Ndipo watakapojua kuwa Mimi,Bwana, Mungu wao, niko pamoja nao, na kwamba wao, nyumba ya Israeli, ni watu wangu, asemaBwanaMwenyezi.

31 Ninyi ni kondoo wangu, kondoo wa malisho yangu, ninyi ni watu wangu, nami ni Mungu wenu, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/34-a98c9cb75bb1932db4fb679e55fc9d16.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 35

Unabii Dhidi Ya Edomu

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya mlima Seiri, utabiri dhidi yake

3 na useme: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume nawe, ee mlima Seiri, nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yako na kukufanya ukiwa na usiyekaliwa na watu wala kulimika.

4 Nitaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa ukiwa. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.

5 “ ‘Kwa sababu ulificha moyoni uadui wa siku nyingi nawe ukawatoa Waisraeli wauawe kwa upanga wakati wa maafa yao, wakati adhabu yake ilipofikia kilele chake,

6 kwa hiyo hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, nitakutia katika umwagaji damu nao utakufuatia. Kwa kuwa hakuchukia kumwaga damu, kumwaga damu kutakufuatia.

7 Nitaufanya Mlima Seiri ukiwa na usiokaliwa na watu wala kulimika na kuukatilia mbali na wote wanaokuja na wanaokwenda.

8 Nitaijaza milima yenu kwa watu wake waliouawa, wale waliouawa kwa upanga wataanguka juu ya vilima vyako na katika mabonde yako na katika makorongo yako yote.

9 Nitakufanya ukiwa milele, watu hawataishi katika miji yako. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.

10 “ ‘Kwa sababu umesema, “Mataifa haya mawili na nchi hizi zitakuwa zetu nasi tutazimiliki,” ingawa hata mimiBwananilikuwa huko,

11 kwa hiyo hakika kama niishivyo, asemaBwanaMwenyezi, nitakutenda kwa kadiri ya hasira na wivu uliouonyesha katika chuki yako juu yao nami nitafanya nijulikane miongoni mwao wakati nitakapokuhukumu.

12 Ndipo utakapojua kuwa MimiBwananimesikia mambo yote ya dharau uliyosema dhidi ya milima ya Israeli. Ulisema, “Wamefanyika ukiwa na kutiwa mikononi mwetu tuwararue.”

13 Ulijigamba dhidi yangu na kusema maneno dhidi yangu bila kujizuia, nami nikayasikia.

14 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Wakati dunia yote inashangilia nitakufanya ukiwa.

15 Kwa sababu ulishangilia wakati urithi wa nyumba ya Israeli ulipofanyika ukiwa, hivyo ndivyo nitakavyokutendea. Utakuwa ukiwa, ee mlima Seiri, wewe na Edomu yote. Kisha ndipo watajua kuwa Mimi ndimiBwana.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/35-2c943a2013a3831088f73f89b74d7af3.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 36

Unabii Kwa Milima Ya Israeli

1 “Mwanadamu, itabirie milima ya Israeli na useme, ‘Ee milima ya Israeli, sikieni neno laBwana.

2 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa sababu adui wanasema juu yako, “Aha! Mahali palipoinuka pa zamani pamekuwa milki yetu.” ’

3 Kwa hiyo tabiri na useme, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa sababu wamewafanya ukiwa na kuwagandamiza kila upande ili mpate kuwa milki ya mataifa mengine na kuwa kitu cha kusimangwa na kudhihakiwa miongoni mwa watu,

4 kwa hiyo, ee milima ya Israeli, sikieni neno laBwanaMwenyezi: Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo kwa milima na vilima, kwa makorongo na mabonde, kwa mahame yaliyo ukiwa, miji iliyoachwa ambayo imetekwa nyara na kudharauliwa na mataifa mengine yanayowazunguka,

5 hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Katika wivu wangu uwakao nimenena dhidi ya mataifa mengine na dhidi ya Edomu yote, kwa maana kwa furaha na hila katika mioyo yao waliifanya nchi yangu kuwa milki yao ili wapate kuteka nyara sehemu yake ya malisho.’

6 Kwa hiyo tabiri kuhusu nchi ya Israeli na uiambie milima na vilima, makorongo na vijito na mabonde: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ninanena katika wivu wa ghadhabu yangu kwa sababu mmedharauliwa na mataifa.

7 Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ninaapa kwa mkono wangu ulioinuliwa kwamba mataifa wanaowazunguka nao pia watadharauliwa.

8 “ ‘Lakini ninyi, ee milima ya Israeli, mtatoa matawi na matunda kwa ajili ya watu wangu Israeli, kwa sababu hivi karibuni watakuja nyumbani.

9 Mimi ninawajibika nanyi na nitawaangalia kwa upendeleo, mtalimwa na kupandwa mbegu,

10 nami nitaizidisha idadi ya watu kwenu, naam, nyumba yote ya Israeli. Miji itakaliwa na watu na magofu yatajengwa upya.

11 Nitaongeza idadi ya watu na wanyama juu yenu, nao watazaana sana na kuwa wengi mno. Nitawakalisha watu ndani yenu kama ilivyokuwa wakati uliopita, nami nitawafanya mfanikiwe kuliko hapo kwanza. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.

12 Nitawafanya watu, watu wangu Israeli, kutembea juu yenu. Watawamiliki ninyi, nanyi mtakuwa urithi wao, kamwe hamtawaondolea tena watoto wao.

13 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Kwa sababu watu wanakuambia, “Unawala watu na kuliondolea taifa lako watoto wake,”

14 kwa hiyo hutakula tena watu wala kulifanya tena taifa lako lisiwe na watoto, asemaBwanaMwenyezi.

15 Sitakufanya tena usikie dhihaka za mataifa, wala kudharauliwa na kabila za watu, wala kulifanya taifa lako lianguke, asemaBwanaMwenyezi.’ ”

16 Neno laBwanalikanijia tena, kusema:

17 “Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokuwa wakiishi katika nchi yao wenyewe, waliinajisi kwa mwenendo wao na matendo yao. Mwenendo wao mbele zangu ulikuwa kama mwanamke aliye katika hedhi.

18 Hivyo nilimwaga ghadhabu yangu juu yao kwa sababu walikuwa wamemwaga damu katika nchi na kwa sababu walikuwa wameitia nchi unajisi kwa sanamu zao.

19 Nikawatawanya miongoni mwa mataifa, nao wakaenda huku na huko katika nchi mbalimbali, nikawahukumu sawasawa na mwenendo wao na matendo yao.

20 Tena popote walipokwenda miongoni mwa mataifa walilitia unajisi Jina langu takatifu, kwa kuwa watu walisema kuwahusu, ‘Hawa ndio watu waBwana, lakini imewapasa kuondoka katika nchi yake.’

21 Lakini niliwahurumia kwa ajili ya Jina langu takatifu, ambalo nyumba ya Israeli imelitia unajisi miongoni mwa mataifa huko walikokwenda.

22 “Kwa hiyo iambie nyumba ya Israeli, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Si kwa ajili yako, ee nyumba ya Israeli, kwamba ninafanya mambo haya, bali ni kwa ajili ya Jina langu takatifu, ambalo mmelitia unajisi miongoni mwa mataifa mliyoyaendea.

23 Nitauonyesha utakatifu wa Jina langu kuu, ambalo limetiwa unajisi miongoni mwa mataifa, jina ambalo limetiwa unajisi miongoni mwao. Ndipo mataifa watakapojua kuwa Mimi ndimiBwana, asemaBwanaMwenyezi, nitakapojionyesha mwenyewe kuwa mtakatifu kwa kuwapitia ninyi mbele ya macho yao.

24 “ ‘Kwa kuwa nitawaondoa ninyi toka mataifa, nitawakusanya kutoka nchi zote na kuwarudisha kwenye nchi yenu wenyewe.

25 Nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi, nitawatakasa kutoka uchafu wenu wote na kutoka sanamu zenu zote.

26 Nitawapa moyo mpya na kuweka roho mpya ndani yenu, nitaondoa ndani yenu moyo wenu wa jiwe na kuwapa moyo wa nyama.

27 Nami nitaweka Roho yangu ndani yenu na kuwafanya ninyi mfuate amri zangu na kuwafanya kuwa waangalifu kuzishika sheria zangu.

28 Mtaishi katika nchi niliyowapa baba zenu, ninyi mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu.

29 Nitawaokoa ninyi kutoka unajisi wenu wote. Nitaiita nafaka na kuiongeza iwe nyingi sana nami sitaleta njaa juu yenu.

30 Nitaongeza matunda ya miti na mazao ya mashamba, ili kwamba msipate tena aibu miongoni mwa mataifa kwa ajili ya njaa.

31 Ndipo mtakapozikumbuka njia zenu za uovu na matendo yenu maovu, nanyi mtajichukia wenyewe kwa ajili ya dhambi zote na matendo yenu ya kuchukiza.

32 Ninataka ninyi mjue kwamba sifanyi hili kwa ajili yenu, asemaBwanaMwenyezi. Oneni aibu na mkatahayari kwa ajili ya mwenendo wenu, ee nyumba ya Israeli!

33 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Siku ile nitakapowasafisha kutoka dhambi zenu zote, nitarudisha watu waishi katika miji yenu na magofu yatajengwa upya.

34 Nchi iliyokuwa ukiwa italimwa badala ya kukaa ukiwa machoni mwa wale wote wanaopita ndani yake.

35 Watasema, “Hii nchi iliyokuwa imeachwa ukiwa sasa imekuwa kama bustani ya Edeni, miji ile iliyokuwa magofu, ukiwa na kuangamizwa, sasa imejengewa ngome na kukaliwa na watu.”

36 Ndipo mataifa yanayowazunguka yaliyobakia watakapojua kuwa MimiBwananimejenga tena kile kilichoharibiwa na nimepanda tena kile kilichokuwa ukiwa. MimiBwananimenena, nami nitalifanya.’

37 “Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Mara nyingine tena nitasikia maombi ya nyumba ya Israeli na kuwatendea jambo hili: Nitawafanya watu wake kuwa wengi kama kondoo,

38 kuwa wengi kama kundi la kondoo kwa ajili ya dhabihu huko Yerusalemu wakati wa sikukuu zao za wakati ulioamriwa. Hivyo ndivyo miji iliyokuwa magofu itajazwa na makundi ya watu. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/36-f2bbfde741697b3c05db37b4b8908a58.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 37

Bonde La Mifupa Mikavu

1 Mkono waBwanaulikuwa juu yangu, naye akanitoa nje kwa Roho waBwanana kuniweka katikati ya bonde lililokuwa limejaa mifupa tele.

2 Akanipitisha pande zote kwenye hiyo mifupa, nami nikaona mifupa mingi sana ndani ya lile bonde, mifupa iliyokuwa imekauka sana.

3 Akaniuliza, “Mwanadamu, mifupa hii yaweza kuishi?”

Nikajibu, “EeBwanaMwenyezi, wewe peke yako wajua.”

4 Ndipo akaniambia, “Itabirie mifupa hii na uiambie, ‘Enyi mifupa mikavu, sikieni neno laBwana!

5 Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo kwa hii mifupa: Nitatia pumzindani yenu, nanyi mtaishi.

6 Nitawawekea mishipa, nami nitaifanya nyama ije juu yenu na kuwafunika kwa ngozi. Nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtakuwa hai. Ndipo mtakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.’ ”

7 Basi nikatabiri kama nilivyoamriwa. Wakati nilipokuwa ninatabiri, kukawa na sauti, sauti ya kugongana, nayo mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe.

8 Nikatazama, mishipa na nyama vikatokea juu ya mifupa na ngozi ikaifunika, lakini hapakuwepo pumzi ndani yake.

9 Ndipo aliponiambia, “Utabirie upepo, tabiri, mwanadamu na uuambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Njoo kutoka pande nne, ee pumzi, nawe upulizie pumzi ndani ya hawa waliouawa, ili wapate kuishi.’ ”

10 Hivyo nikatabiri kama alivyoniamuru, nayo pumzi ikawaingia, wakawa hai na wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno.

11 Ndipo akaniambia: “Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli. Nao wanasema, ‘Mifupa yetu imekauka na tumaini letu limetoweka, tumekatiliwa mbali.’

12 Hivyo watabirie na uwaambie: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Enyi watu wangu, nitayafunua makaburi yenu na kuwatoa ndani yake, nami nitawarudisha tena katika nchi ya Israeli.

13 Ndipo ninyi watu wangu, mtakapojua kuwa Mimi ndimiBwana, nitakapoyafunua makaburi yenu na kuwatoa humo.

14 Nitatia Roho yangu ndani yenu nanyi mtaishi, nami nitawakalisha katika nchi yenu wenyewe. Ndipo mtakapojua kwamba MimiBwananimenena, nami nitalitenda, asemaBwana!’ ”

Taifa Moja Chini Ya Mfalme Mmoja

15 Neno laBwanalikanijia kusema:

16 “Mwanadamu, chukua fimbo na uandike juu yake, ‘Hii ni kwa ajili ya Yuda na Waisraeli waliofungamana naye.’ Kisha chukua fimbo nyingine, uandike juu yake, ‘Fimbo ya Efraimu, ni kwa ajili ya Yosefu na nyumba yote ya Israeli wanaofungamana naye.’

17 Ziunganishe pamoja kuwa fimbo moja ili kwamba ziwe fimbo moja katika mkono wako.

18 “Watu wako watakapokuuliza, ‘Je, hutatuambia ni nini maana ya jambo hili?’

19 Waambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitaichukua fimbo ya Yosefu, iliyoko mikononi mwa Efraimu na ya makabila ya Israeli yanayofungamana naye na kuiunganisha na fimbo ya Yuda, nikizifanya kuwa fimbo moja, nao watakuwa wamoja katika mkono wangu.’

20 Inua mbele ya macho yao zile fimbo ulizoziandika

21 kisha waambie, ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Nitawatoa Waisraeli katika mataifa walikokuwa wamekwenda. Nitawakusanya popote walipo na kuwarudisha katika nchi yao wenyewe.

22 Nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi, katika milima ya Israeli. Patakuwa na mfalme mmoja juu yao wote na kamwe hawatagawanyika tena kuwa mataifa mawili au kugawanyika katika falme mbili.

23 Hawatajitia tena unajisi kwa sanamu zao na vinyago vyao visivyo na maana wala kwa makosa yao yoyote, kwa maana nitawaokoa kutoka dhambi zao zote zilizowarudisha nyuma, nami nitawatakasa. Wao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.

24 “ ‘Mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja. Watafuata sheria zangu na kuzishika amri zangu kwa uangalifu.

25 Wataishi katika nchi niliyompa mtumishi wangu Yakobo, nchi ambamo baba zenu waliishi. Wao na watoto wao na watoto wa watoto wao wataishi humo milele, naye Daudi mtumishi wangu atakuwa mkuu wao milele.

26 Nitafanya nao Agano la amani, litakuwa Agano la milele. Nitawafanya imara na kuongeza idadi yao, nami nitaweka mahali patakatifu pangu miongoni mwao milele.

27 Maskani yangu yatakuwa pamoja nao, nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.

28 Ndipo mataifa watakapojua kwamba MimiBwanandiye ninayeifanya Israeli kuwa takatifu, wakati mahali patakatifu pangu patakapokuwa miongoni mwao milele.’ ”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/37-777a713afed8989a30f0fb84e36039ab.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 38

Unabii Dhidi Ya Gogu

1 Neno laBwanalikanijia kusema:

2 “Mwanadamu, kaza uso wako dhidi ya Gogu, katika nchi ya Magogu, mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali, tabiri dhidi yake

3 na useme: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ee Gogu, mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali.

4 Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukutia ndoana kwenye mataya yako na kukutoa nje wewe pamoja na jeshi lako lote, yaani, farasi wako, wapanda farasi wako waliojiandaa tayari kwa vita, pamoja na kundi kubwa la wajeuri wakiwa na ngao na vigao, wote wakipunga panga zao.

5 Uajemi, Kushina Putu watakuwa pamoja nao, wote wakiwa na ngao na kofia za chuma,

6 pia Gomeri pamoja na vikosi vyake vyote, na Beth-Togarma kutoka kaskazini ya mbali pamoja na vikosi vyake vyote, mataifa mengi wakiwa pamoja nawe.

7 “ ‘Jiandae, uwe tayari, wewe na makundi yako yote ya wajeuri yaliyokusanyika pamoja nawe, nawe waamrishe.

8 Baada ya siku nyingi utaitwa vitani. Katika miaka ijayo, utaivamia nchi ile ambayo imepona kutoka vita, ambayo watu wake walikusanywa kutoka mataifa mengi kuja katika milima ya Israeli, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa imeachwa ukiwa. Wameletwa kutoka mataifa na sasa wote wanaishi katika hali ya salama.

9 Wewe na vikosi vyako vyote na mataifa mengi yaliyo pamoja nawe mtapanda juu, mtawazoa kama tufani na kuifunika nchi kama wingu.

10 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Katika siku ile mawazo yataingia moyoni mwako nawe utapanga mipango mibaya.

11 Utasema, “Nitapigana vita na nchi ambayo vijiji vyake havina maboma. Nitawashambulia watu wanaoishi kwa amani na wasiotarajia vita: wote wanaishi bila maboma na bila malango na makomeo.

12 Nitateka mateka na kuchukua nyara mali za wale waliorudi kuishi katika mahame na wale watu waliokusanywa kutoka kwa mataifa, ambao sasa wana mifugo na mali nyingi, wanaoishi katikati ya nchi.”

13 Sheba na Dedani pamoja na wafanyabiashara wa Tarshishi na vijiji vyake vyote watakuambia, “Je, umekuja kuteka mateka? Je, umekusanya makundi yako ya wajeuri ili kuchukua nyara mali, kutwaa fedha na dhahabu, kutunyangʼanya mifugo na mali na kuteka nyara nyingi zaidi?” ’

14 “Kwa hiyo, mwanadamu, tabiri na umwambie Gogu: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Katika siku ile, watu wangu Israeli watakapokuwa wanaishi salama, Je, wewe mwenyewe hutalijua hilo?

15 Utakuja kutoka kwako huko kaskazini ya mbali, ukiwa pamoja na mataifa mengi, wote wakiwa wamepanda farasi, kundi kubwa, jeshi kuu.

16 Utakuja dhidi ya watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Siku zijazo, ee Gogu, nitakuleta wewe dhidi ya nchi yangu, ili kwamba mataifa wapate kunijua Mimi nitakapojionyesha mtakatifu kwa kukupitia wewe mbele ya macho yao.

17 “ ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Je, wewe si yule niliyenena juu yako katika siku za zamani kwa kupitia kwa watumishi wangu manabii wa Israeli? Wakati ule walitabiri kwa miaka mingi kwamba ningekuleta upigane nao.

18 Hili ndilo litakalotokea katika siku ile: Gogu atakaposhambulia nchi ya Israeli, hasira yangu kali itaamka, asemaBwanaMwenyezi.

19 Katika wivu wangu na ghadhabu yangu kali ninasema kuwa wakati ule patakuwepo tetemeko kuu katika nchi ya Israeli.

20 Samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kondeni, kila kiumbe kitambaacho ardhini, na watu wote walio juu ya uso wa nchi watatetemeka mbele zangu. Milima itapinduka, majabali yatapasuka na kila ukuta utaanguka chini.

21 Nitaita upanga vita dhidi ya Gogu juu ya milima yangu yote, asemaBwanaMwenyezi. Upanga wa kila mtu utakuwa dhidi ya ndugu yake.

22 Nitatekeleza hukumu juu yake kwa tauni na kwa umwagaji wa damu. Nitaifanya mvua ya mafuriko kunyesha, mvua ya mawe na moto wa kiberiti juu yake na juu ya vikosi vyake na juu ya mataifa mengi walio pamoja naye.

23 Nami hivyo ndivyo nitakavyoonyesha ukuu wangu na utakatifu wangu, nami nitajijulisha mbele ya macho ya mataifa mengi. Ndipo watakapojua kuwa Mimi ndimiBwana.’

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/38-fc3385726f85b950cab532550c9ec505.mp3?version_id=1627—

Categories
Ezekieli

Ezekieli 39

Majeshi Ya Gogu Yataangamizwa

1 “Mwanadamu, tabiri dhidi ya Gogu useme: ‘Hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ee Gogu mimi ni kinyume nawe, mtawala mkuu wa Roshi, Mesheki na Tubali.

2 Nitakugeuza kuelekea ulikotoka na kukuburuta. Nitakuleta kutoka kaskazini ya mbali na kukupeleka wewe dhidi ya milima ya Israeli.

3 Kisha nitaupiga upinde wako kutoka mkono wako wa kushoto na kuifanya mishale ianguke kutoka mkono wako wa kuume.

4 Utaanguka kwenye milima ya Israeli, wewe pamoja na vikosi vyako vyote na yale mataifa yaliyo pamoja nawe. Nitakutoa uwe chakula cha ndege wa aina zote walao nyama na cha wanyama wa mwituni.

5 Utaanguka katika uwanja, kwa kuwa nimenena, asemaBwanaMwenyezi.

6 Nitatuma moto juu ya Magogu na kwa wale wanaoishi kwa salama huko pwani, nao watajua kwamba Mimi ndimiBwana.

7 “ ‘Nitalifanya Jina langu takatifu lijulikane miongoni mwa watu wangu Israeli. Sitaliacha tena Jina langu takatifu litiwe unajisi, nayo mataifa watajua kuwa MimiBwanandimi Aliye Mtakatifu wa Israeli.

8 Hili jambo linakuja! Hakika litatokea, asemaBwanaMwenyezi. Hii ndiyo siku ile niliyosema habari zake.

9 “ ‘Ndipo wale wanaoishi katika miji ya Israeli watakapotoka na kutumia hizo silaha kuwashia moto na kuziteketeza, yaani, kigao na ngao, pinde na mishale, rungu za vita na mikuki. Kwa miaka saba watavitumia kama kuni.

10 Hawatahitaji kukusanya kuni kutoka mashambani wala kukata kuni kutoka kwenye misitu, kwa sababu watatumia silaha kuwa kuni. Nao watawateka mateka wale waliowateka na kuchukua nyara mali za wale waliochukua mali zao nyara, asemaBwanaMwenyezi.

11 “ ‘Siku ile nitampa Gogu mahali pa kuzikia katika Israeli, katika bonde la wale wasafirio upande wa mashariki kuelekea baharini. Jambo hili litazuia njia ya wasafiri kwa sababu Gogu na makundi yake yote ya wajeuri watazikwa huko. Kwa hiyo litaitwa Bonde la Hamon-Gogu.

12 “ ‘Kwa miezi saba nyumba ya Israeli itakuwa ikiwazika ili kuisafisha nchi.

13 Watu wote wa nchi watawazika, nayo siku nitakayotukuzwa itakuwa siku ya kumbukumbu kwa ajili yao, asemaBwanaMwenyezi.

14 “ ‘Watu wataajiriwa mara kwa mara kuisafisha nchi. Baadhi yao watapita nchini kote na zaidi yao hao wengine, watawazika wale waliosalia juu ya uso wa nchi. Mwisho wa hiyo miezi saba wataanza upekuzi wao.

15 Wakati wanapopita nchini kote na mmoja wao akaona mfupa wa mwanadamu, ataweka alama kando yake mpaka wachimba kaburi wawe wameuzika katika Bonde la Hamon-Gogu.

16 (Pia mji uitwao Hamonautakuwa humo.) Hivyo ndivyo watakavyoisafisha nchi.’

17 “Mwanadamu, hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Ita kila aina ya ndege na wanyama wote wa mwituni, waambie: ‘Kusanyikeni mje pamoja kutoka pande zote kwa ajili ya dhabihu ninayowaandalia, dhabihu kuu katika milima ya Israeli. Huko mtakula nyama na kunywa damu.

18 Mtakula nyama za watu mashujaa na kunywa damu za wakuu wa dunia kana kwamba ni za kondoo dume na kondoo wake, mbuzi na mafahali, wote walionona kutoka Bashani.

19 Katika dhabihu ninayoandaa kwa ajili yenu, mtakula mafuta mpaka mkinai na kunywa damu mpaka mlewe.

20 Kwenye meza yangu watajishibisha kwa farasi na wapanda farasi, watu mashujaa na askari wa kila aina,’ asemaBwanaMwenyezi.

21 “Nitauonyesha utukufu wangu miongoni mwa mataifa, nayo mataifa yote wataiona adhabu nitakayotoa na mkono wangu nitakaouweka juu yao.

22 Kuanzia siku ile na kuendelea nyumba ya Israeli itajua kuwa Mimi ndimiBwana, Mungu wao.

23 Na mataifa watajua kuwa nyumba ya Israeli walikwenda utumwani kwa ajili ya dhambi yao, kwa sababu hawakuwa waaminifu kwangu. Hivyo niliwaficha uso wangu na kuwatia mikononi mwa adui zao, nao wote wakaanguka kwa upanga.

24 Niliwatendea sawasawa na uchafu wao na makosa yao, nami nikawaficha uso wangu.

25 “Kwa hiyo hili ndiloBwanaMwenyezi asemalo: Sasa nitamrudisha Yakobo kutoka utumwani, nami nitawahurumia watu wote wa Israeli, nami nitakuwa na wivu kwa ajili ya Jina langu takatifu.

26 Wataisahau aibu yao na jinsi walivyoonyesha kutokuwa waaminifu kwangu mimi wakati waliishi salama katika nchi yao, bila kuwa na mtu yeyote wa kuwatia hofu.

27 Nitakapokuwa nimewarudisha kutoka mataifa na kuwakusanya kutoka nchi za adui zao, mimi nitajionyesha kuwa mtakatifu kwa kupitia kwao machoni mwa mataifa mengi.

28 Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimiBwana, Mungu wao, ingawa niliwapeleka uhamishoni miongoni mwa mataifa, nitawakusanya tena katika nchi yao wenyewe, bila kumwacha yeyote nyuma.

29 Sitawaficha tena uso wangu, kwa maana nitamimina Roho wangu juu ya nyumba ya Israeli, asemaBwanaMwenyezi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EZK/39-3cfd7071071499b75c0e88a3f4b42451.mp3?version_id=1627—