Categories
Ayubu

Ayubu 40

1 Bwanaakamwambia Ayubu:

2 “Je, mwenye kushindana na Mwenyezi aweza kumsahihisha?

Mwenye kumlaumu Mungu na ajibu.”

3 Ndipo Ayubu akamjibuBwana:

4 “Mimi sistahili kabisa: ninawezaje kukujibu wewe?

Nauweka mkono wangu juu ya kinywa changu.

5 Nimesema mara moja, lakini sina jibu;

naam, nimesema mara mbili,

lakini sitasema tena.”

6 NdipoBwanaakasema na Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli:

7 “Jikaze kama mwanaume;

nitakuuliza maswali, nawe yakupasa unijibu.

8 “Je, utabatilisha hukumu yangu?

Utanilaumu mimi ili kujihesabia haki mwenyewe?

9 Je, una mkono kama wa Mungu,

nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake?

10 Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari,

nawe uvae heshima na enzi.

11 Fungulia ukali wa ghadhabu yako,

mtafute kila mwenye kiburi umshushe,

12 mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze,

waponde waovu mahali wasimamapo.

13 Wazike wote mavumbini pamoja;

wafunge nyuso zao kaburini.

14 Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia

kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.

15 “Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi,

niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe,

anayekula majani kama ngʼombe.

16 Tazama basi nguvu alizo nazo kwenye viuno vyake,

uwezo alio nao kwenye misuli ya tumbo lake!

17 Mkia wake hutikisika kama mwerezi;

mishipa ya mapaja yake imesukwa pamoja.

18 Mifupa yake ni bomba za shaba,

maungo yake ni kama fito za chuma.

19 Yeye ni wa kwanza miongoni mwa kazi za Mungu,

lakini Muumba wake anaweza kumsogelea kwa upanga wake.

20 Vilima humletea yeye mazao yake,

nao wanyama wote wa porini hucheza karibu naye.

21 Hulala chini ya mimea ya yungiyungi,

katika maficho ya matete kwenye matope.

22 Hiyo mimea ya yungiyungi humficha kwenye vivuli vyake;

miti mirefu karibu na kijito humzunguka.

23 Wakati mto ufurikapo, yeye hapati mshtuko wa hofu;

yeye yu salama, hata kama Yordani ingefurika hadi kwenye kinywa chake.

24 Je, mtu yeyote anaweza kumkamata yeye akiwa macho,

au kumnasa kwa mtego na kutoboa pua yake?

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOB/40-9a82a235af97c35ef4e9bdfbd9bb1399.mp3?version_id=1627—

Categories
Ayubu

Ayubu 41

1 “Je, waweza kumvua Lewiathanikwa ndoano ya samaki,

au kufunga ulimi wake kwa kamba?

2 Waweza kupitisha kamba puani mwake,

au kutoboa taya lake kwa kulabu?

3 Je, ataendelea kukuomba umhurumie?

Atasema nawe maneno ya upole?

4 Je, atafanya agano nawe ili umtwae

awe mtumishi wako maisha yake yote?

5 Je, utamfuga na kumfanya rafiki kama ndege,

au kumfunga kamba kwa ajili ya wasichana wako?

6 Je, wafanyabiashara watabadilishana bidhaa kwa ajili yake?

Watamgawanya miongoni mwa wafanyao biashara?

7 Je, waweza kuijaza ngozi yake kwa vyuma vyenye ncha kali,

au kichwa chake kwa mkuki wa kuvulia samaki?

8 Kama ukiweka mkono wako juu yake,

utavikumbuka hivyo vita na kamwe hutarudia tena!

9 Tumaini lolote la kumtiisha ni kujidanganya;

kule kumwona tu kunamwangusha mtu chini.

10 Hakuna yeyote aliye mkali athubutuye kumchokoza.

Ni nani basi awezaye kusimama dhidi yangu?

11 Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa?

Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu.

12 “Sitashindwa kunena juu ya maungo yake,

nguvu zake na umbo lake zuri.

13 Ni nani awezaye kumvua gamba lake la nje?

Ni nani awezaye kumsogelea na lijamu?

14 Nani athubutuye kuufungua mlango wa kinywa chake,

kilichozungukwa na meno yake ya kutisha pande zote?

15 Mgongo wake una safu za ngao

zilizoshikamanishwa imara pamoja;

16 kila moja iko karibu sana na mwenzake,

wala hakuna hewa iwezayo kupita kati yake.

17 Zimeunganishwa imara kila moja na nyingine;

zimengʼangʼaniana pamoja wala haziwezi kutenganishwa.

18 Akipiga chafya mwanga humetameta;

macho yake ni kama mionzi ya mapambazuko.

19 Mienge iwakayo humiminika kutoka kinywani mwake;

cheche za moto huruka nje.

20 Moshi hufuka kutoka puani mwake,

kama kutoka kwenye chungu kinachotokota kwa moto wa matete.

21 Pumzi yake huwasha makaa ya mawe,

nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake.

22 Nguvu hukaa katika shingo yake;

utisho hutangulia mbele yake.

23 Mikunjo ya nyama yake imeshikamana imara pamoja;

iko imara na haiwezi kuondolewa.

24 Kifua chake ni kigumu kama mwamba,

kigumu kama jiwe la chini la kusagia.

25 Ainukapo, mashujaa wanaogopa;

hurudi nyuma mbele yake anapokwenda kwa kishindo.

26 Upanga unaomfikia haumdhuru,

wala mkuki au mshale wala fumo.

27 Chuma hukiona kama unyasi,

na shaba kama mti uliooza.

28 Mishale haimfanyi yeye akimbie;

mawe ya kombeo kwake ni kama makapi.

29 Rungu kwake huwa kama kipande cha jani kavu;

hucheka sauti za kugongana kwa mkuki.

30 Sehemu zake za chini kwenye tumbo

zina menomeno na mapengo kama vigae vya chungu,

zikiacha mburuzo kwenye matope

kama chombo chenye meno cha kupuria.

31 Huvisukasuka vilindi kama sufuria kubwa ichemkayo,

na kukoroga bahari kama chungu cha marhamu.

32 Anapopita nyuma yake huacha mkondo unaometameta;

mtu angedhani vilindi vilikuwa na mvi.

33 Hakuna chochote duniani kinacholingana naye:

yeye ni kiumbe kisicho na woga.

34 Yeye huwatazama chini wale wote wenye kujivuna;

yeye ni mfalme juu ya wote wenye kiburi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOB/41-b80ee188812911100ed0a7552396d5a7.mp3?version_id=1627—

Categories
Ayubu

Ayubu 42

Ayubu Anamjibu Bwana

1 Ndipo Ayubu akamjibuBwana:

2 “Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote,

wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.

3 Uliuliza, ‘Ni nani huyu afichaye mashauri yangu bila maarifa?’

Hakika nilisema juu ya mambo niliyokuwa siyaelewi,

mambo ya ajabu mno kwangu mimi kuyajua.

4 “Ulisema, ‘Sikiliza sasa, nami nitanena;

nitakuuliza swali, nawe yakupasa kunijibu.’

5 Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako,

lakini sasa macho yangu yamekuona.

6 Kwa hiyo najidharau mwenyewe,

na kutubu katika mavumbi na majivu.”

Mwisho: Marafiki Wa Ayubu Wanafedheheshwa

7 Baada yaBwanakusema mambo haya yote na Ayubu, akamwambia Elifazi Mtemani, “Nina hasira juu yako na juu ya rafiki zako wawili, kwa sababu hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.

8 Basi sasa chukueni mafahali saba na kondoo dume saba mkamwendee mtumishi wangu Ayubu nanyi mkatoe sadaka za kuteketezwa kwa ajili yenu wenyewe. Mtumishi wangu Ayubu ataomba kwa ajili yenu, nami nitayakubali maombi yake ili nisiwatendee sawasawa na upumbavu wenu. Ninyi hamkusema yaliyo sawa kwa habari yangu, kama alivyosema mtumishi wangu Ayubu.”

9 Kwa hiyo Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, na Sofari Mnaamathi wakafanya kamaBwanaalivyowaambia; nayeBwanaakayakubali maombi ya Ayubu.

10 Baada ya Ayubu kuwaombea rafiki zake,Bwanaakamwondoa kwenye uteka, akamfanikisha tena naye akampa mara mbili ya vile alivyokuwa navyo hapo mwanzoni.

11 Ndipo ndugu zake wote waume kwa wake na kila mtu aliyemfahamu mwanzoni, wakaja wakala pamoja naye katika nyumba yake. Wakamfariji na kumtuliza moyo juu ya taabu yoteBwanaaliyoileta juu yake, nao kila mmoja akampa kipande cha fedha na pete ya dhahabu.

12 Bwanaakaibariki sehemu ya mwisho ya maisha ya Ayubu kuliko ile ya kwanza. Alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, ngamia elfu sita, jozi za mafahali elfu moja, na punda wa kike elfu moja.

13 Tena alikuwa na wana saba na binti watatu.

14 Binti wa kwanza aliitwa Yemima, wa pili Kesia na wa tatu Keren-Hapuki.

15 Hapakuwepo mahali popote katika nchi ile yote palipopatikana wanawake wazuri kama binti za Ayubu; naye baba yao akawapa urithi pamoja na ndugu zao.

16 Baada ya hili Ayubu akaishi miaka 140; akawaona wanawe na wana wa wanawe hata kizazi cha nne.

17 Hivyo Ayubu akafa, akiwa mzee aliyekuwa ameshiba siku.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOB/42-f4f15620604b73cc5f955b360bb8d163.mp3?version_id=1627—