Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 20

Kutekwa Kwa Raba

1 Mwanzoni mwa mwaka mpya, wakati ambapo wafalme huenda vitani, Yoabu aliliongoza jeshi. Aliangamiza nchi ya Waamoni, na akaenda Raba na kuuzingira, lakini Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu akashambulia Raba na kuuacha ukiwa magofu.

2 Daudi akachukua taji kutoka kwa kichwa cha mfalme wao, lililokuwa na uzito wa talanta moja ya dhahabu,nayo ilizungushiwa vito vya thamani. Ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Alichukua nyara nyingi kutoka mjini huo.

3 Akawatoa watu waliokuwa humo, akawaweka wafanye kazi kwa misumeno, sululu za chuma na mashoka. Daudi akafanya hivi kwa miji yote ya Waamoni. Kisha Daudi na jeshi lake lote wakarudi Yerusalemu.

Vita Na Wafilisti

4 Baada ya muda, kulitokea vita dhidi ya Wafilisti, huko Gezeri. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamuua Sipai, aliyekuwa mmoja wa wazao wa Warefai,nao Wafilisti wakashindwa.

5 Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji.

6 Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuwako na mtu mmoja mkubwa mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu: jumla vidole ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai.

7 Alipowadhihaki Israeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua.

8 Hawa walikuwa ndio wazao wa Warefai huko Gathi, nao walianguka kwa mikono ya Daudi na watu wake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/20-1c460257f920ebb5a7dbb84ca3174e9b.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 21

Daudi Ahesabu Wapiganaji

1 Shetani akainuka dhidi ya Israeli na kumshawishi Daudi ahesabu watu wa Israeli.

2 Kwa hiyo Daudi akamwambia Yoabu na majemadari wa jeshi, “Nendeni mkawahesabu Waisraeli kuanzia Beer-Sheba mpaka Dani. Kisha nileteeni taarifa ili kwamba niweze kufahamu wako wangapi.”

3 Yoabu akajibu, “Bwanana aongeze jeshi lake mara mia na zaidi. Mfalme bwana wangu, kwani hawa wote si raiya wa bwana wangu? Kwa nini bwana wangu unataka kufanya hivi? Kwa nini kuleta hatia juu ya Israeli?”

4 Hata hivyo, neno la mfalme likawa na nguvu juu ya Yoabu; kwa hiyo Yoabu akaondoka na kuzunguka Israeli yote kisha akarudi Yerusalemu.

5 Yoabu akampa Daudi jumla ya idadi ya watu wanaoweza kupigana. Katika Israeli kulikuwa na watu 1,100,000 ambao wangeweza kutumia upanga na katika Yuda watu 470,000.

6 Lakini Yoabu hakuwahesabu Walawi na Wabenyamini, kwa sababu alichukizwa sana na amri ya mfalme.

7 Amri hii ilikuwa mbaya machoni pa Mungu pia; hivyo akaiadhibu Israeli.

8 Kisha Daudi akamwambia Mungu, “Nimetenda dhambi kubwa kwa kufanya jambo hili. Sasa, ninakusihi, ondoa hatia ya mtumishi wako. Nimefanya jambo la kipumbavu sana.”

9 Bwanaakamwambia Gadi, mwonaji wa Daudi,

10 “Nenda ukamwambie Daudi, hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Ninakupa wewe uchaguzi wa mambo matatu. Nichagulie mojawapo nitakalotenda dhidi yako.’ ”

11 Kwa hiyo Gadi akamwendea Daudi akamwambia, “Hili ndiloBwanaasemalo: ‘Chagua:

12 miaka mitatu ya njaa, au miezi mitatu ya kushindwa na adui zako, ukipatwa na upanga wao, au siku tatu za upanga waBwana, yaani, siku tatu za tauni katika nchi na malaika waBwanaakiangamiza kila mahali katika Israeli.’ Sasa basi, amua jinsi nitakavyomjibu yeye aliyenituma.”

13 Daudi akamwambia Gadi, “Ninayo mahangaiko makubwa. Mimi na nianguke mikononi mwaBwanakwa maana rehema zake ni kuu mno, lakini usiniache niangukie mikononi mwa wanadamu.”

14 BasiBwanaakatuma tauni katika Israeli, watu 70,000 wa Israeli wakafa.

15 Mungu akapeleka malaika kuangamiza Yerusalemu. Lakini malaika alipokuwa akifanya hivyo,Bwanaakaona na akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anaangamiza watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika waBwanaalikuwa amesimama katika sakafu ya kupuria nafaka ya AraunaMyebusi.

16 Daudi akayainua macho yake akamwona huyo malaika waBwanaakiwa amesimama katikati ya mbingu na dunia, naye ameunyoosha upanga wake juu ya Yerusalemu tayari kuangamiza. Kisha Daudi na wazee, waliokuwa wamevaa nguo za gunia, wakaanguka kifudifudi.

17 Daudi akamwambia Mungu, “Je, si mimi ndiye niliyeamuru watu wahesabiwe? Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kukosa. Hawa ni kondoo tu. Wamefanya nini? EeBwana, Mungu wangu, mkono wako na uwe juu yangu mimi na jamaa yangu, lakini usiache tauni hii iendelee juu ya watu wako.”

18 Kisha malaika waBwanaakamwamuru Gadi amwambie Daudi apande na kumjengeaBwanamadhabahu kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Arauna Myebusi.

19 Kwa hiyo Daudi akakwea, akalitii lile neno ambalo Gadi alikuwa amelisema katika jina laBwana.

20 Arauna alipokuwa akipura ngano, akageuka akamwona yule malaika. Wanawe wanne waliokuwa pamoja naye wakajificha, yeye akaendelea kupura ngano.

21 Kisha Daudi akakaribia, Arauna alipotazama na kumwona, akaondoka kwenye uwanja wa kupuria nafaka akamsujudia Daudi akiuinamisha uso wake ardhini.

22 Daudi akamwambia, “Nipatie huu uwanja wako wa kupuria nafaka ili niweze kujenga madhabahu yaBwanatauni ipate kukomeshwa katika watu. Niuzie kwa bei yake kamili.”

23 Arauna akamwambia Daudi, “Uchukue huo uwanja. Mfalme bwana wangu na afanye lolote analopenda. Tazama, nitatoa maksai kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, vifaa vya kupuria kuwa kuni, pamoja na ngano kwa ajili ya dhabihu ya nafaka. Natoa hivi vyote.”

24 Lakini Mfalme Daudi akamjibu Arauna, “La hasha! Lakini ninasisitiza kwamba nitalipa bei yake kamili. Sitachukua kilicho chako kwa ajili yaBwanaau kutoa sadaka ya kuteketezwa ambayo hainigharimu chochote.”

25 Basi Daudi akamlipa Arauna shekeli za dhahabu 600kwa ajili ya ule uwanja.

26 Kisha Daudi akamjengeaBwanamadhabahu mahali hapo, na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. AkamwitaBwananayeBwanaakajibu maombi yake kwa moto toka mbinguni juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa.

27 KishaBwanaakanena na yule malaika, naye akarudisha upanga wake katika ala yake.

28 Wakati huo, Daudi alipoona kwambaBwanaamemjibu kule kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Arauna Myebusi, akatoa dhabihu huko.

29 Maskani yaBwanaambayo Mose aliitengeneza kule jangwani, pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa wakati huo vilikuwa viko mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni.

30 Lakini Daudi hakuthubutu kuisogelea ili kumuuliza Mungu, kwa sababu aliuogopa upanga wa yule malaika waBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/21-e96ee7b0f42df3da8e18f62f51d356e8.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 22

1 Ndipo Daudi akasema, “Nyumba yaBwanaMungu itakuwa mahali hapa, pia pamoja na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Israeli.”

Maandalizi Kwa Ajili Ya Hekalu

2 Kwa hiyo Daudi akatoa amri wakusanyike wageni wote waliokuwa wanaishi Israeli, na kutoka miongoni mwao akaweka waashi ili kuchonga mawe kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu.

3 Daudi akatoa chuma tele ili kutengenezea misumari kwa ajili ya mafungo ya malango ya nyumba na shaba tele isiyopimika.

4 Pia akatoa magogo ya mierezi yasiyohesabika, kwa kuwa Wasidoni na Watiro walikuwa wamemletea Daudi idadi kubwa ya mierezi.

5 Daudi akasema, “Mwanangu Solomoni bado ni mdogo wa umri na hana uzoefu. Nyumba itakayojengwa kwa ajili yaBwanainatakiwa iwe yenye uzuri mwingi na sifa na fahari mbele ya mataifa yote. Kwa hiyo nitaifanyia matayarisho.” Daudi akafanya matayarisho makubwa kabla ya kifo chake.

6 Kisha akamwita Solomoni mwanawe akamwagiza kujenga nyumba kwa ajili yaBwana, Mungu wa Israeli.

7 Daudi akamwambia Solomoni: “Mwanangu, nilikuwa na jambo hili ndani ya moyo wangu kujenga nyumba kwa ajili ya Jina laBwanaMungu wangu.

8 Lakini neno hili laBwanalikanijia, kusema: ‘Wewe umemwaga damu nyingi na kupigana vita vingi. Wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi juu ya nchi machoni pangu.

9 Lakini utakuwa na mwana ambaye atakuwa mtu wa amani na utulivu nami nitampa utulivu mbele ya adui zake wote pande zote. Jina lake ataitwa Solomoni, nami nitawapa Israeli amani na utulivu wakati wa utawala wake.

10 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu. Yeye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake. Nami nitakifanya imara kiti chake cha enzi cha utawala wake katika Israeli milele.’

11 “Sasa, mwanangu,Bwanaawe pamoja nawe, nawe uwe na mafanikio upate kuijenga nyumba yaBwanaMungu wako, kama alivyosema utafanya.

12 Bwanana akupe hekima na ufahamu wakati atakuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika sheria yaBwanaMungu wako.

13 Ndipo utakapofanikiwa, ikiwa utakuwa na bidii kutii amri na sheriaBwanaalizompa Mose kwa ajili ya Israeli. Uwe hodari na ushujaa. Usiogope wala usikate tamaa.

14 “Nimejitaabisha sana ili kupata mahitaji kwa ajili ya Hekalu laBwana: talanta 100,000za dhahabu, talanta 1,000,000za fedha na kiasi kisichopimika cha shaba na chuma, pia mbao na mawe. Nawe waweza kuviongeza.

15 Unao wafanyakazi wengi: Wachonga mawe, waashi na maseremala, pamoja na watu walio na ustadi katika kila kazi

16 wa kufua dhahabu, fedha, shaba na chuma, mafundi wasiohesabika. Sasa basi anza kazi hii, nayeBwanaawe pamoja nawe.”

17 Kisha Daudi akawaamuru viongozi wote wa Israeli wamsaidie Solomoni mwanawe.

18 Akawaambia, “Je,BwanaMungu wenu si yuko pamoja na ninyi? Pia si amewapa raha pande zote? Kwa maana amewatia wenyeji wa nchi mkononi mwangu, nayo nchi iko chini yaBwanana watu wake.

19 Sasa itoeni mioyo yenu na nafsi zenu katika kumtafutaBwanaMungu wenu. Anzeni kujenga Maskani yaBwanaMungu, ili mweze kulileta Sanduku la Agano laBwanana vyombo vitakatifu vya Mungu katika Hekalu litakalojengwa kwa ajili ya Jina laBwana.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/22-14fdb82cc0317ac3f353dcf4b04e6161.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 23

Jamaa Za Walawi Na Utendaji Wao

1 Daudi alipokuwa mzee aliyeshiba siku, akamfanya Solomoni mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli.

2 Pia akawakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.

3 Walawi waliokuwa na umri wa miaka thelathini au zaidi walihesabiwa, nayo hesabu ya wanaume ilikuwa 38,000.

4 Daudi akasema, “Miongoni mwa hawa, 24,000 watasimamia kazi ya Hekalu laBwanana 6,000 watakuwa maafisa na waamuzi,

5 na 4,000 watakuwa mabawabu, na wengine 4,000 watamsifuBwanakwa ala za uimbaji nilizotoa kwa ajili ya kusudi hilo.”

6 Daudi akawagawa Walawi katika makundi kufuatana na wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.

Wagershoni

7 Wana wa Wagershoni walikuwa wawili:

Ladani na Shimei.

8 Wana wa Ladani walikuwa watatu:

Yehieli wa kwanza, Zethamu na Yoeli.

9 Wana wa Shimei walikuwa watatu:

Shelomothi,Hazieli na Harani.

Hawa watatu walikuwa viongozi wa jamaa za Ladani.

10 Nao wana wa Shimei walikuwa wanne:

Yahathi, Zina,Yeushi na Beria.

11 Yahathi alikuwa wa kwanza na Ziza wa pili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; kwa hiyo walihesabiwa kama jamaa moja, wakapewa wajibu kwa pamoja.

Wakohathi

12 Wana wa Kohathi walikuwa wanne:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

13 Wana wa Amramu walikuwa:

Aroni na Mose.

Aroni waliwekwa wakfu, yeye na wazao wake milele, wawe wakiweka wakfu vitu ambavyo ni vitakatifu mno, kutoa dhabihu mbele zaBwana, kuhudumu mbele zake na kutamka baraka katika Jina laBwanamilele.

14 Wana wa Mose mtu wa Mungu walihesabiwa kama sehemu ya kabila la Lawi.

15 Wana wa Mose walikuwa:

Gershomu na Eliezeri.

16 Wazao wa Gershomu:

Shebueli alikuwa wa kwanza.

17 Wazao wa Eliezeri:

Rehabia alikuwa wa kwanza.

Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu, lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.

18 Wana wa Ishari:

Shelomithi alikuwa wa kwanza.

19 Wana wa Hebroni walikuwa:

Yeria alikuwa wa kwanza, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli, na wa nne Yekameamu.

20 Wana wa Uzieli walikuwa:

Mika wa kwanza na Ishia wa pili.

Wamerari

21 Wana wa Merari walikuwa:

Mahli na Mushi.

Wana wa Mahli walikuwa:

Eleazari na Kishi.

22 Eleazari akafa bila ya kuwa na wana: alikuwa na binti tu. Binamu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.

23 Wana wa Mushi:

Mahli, Ederi na Yeremothi; wote walikuwa watatu.

24 Hawa walikuwa wazao wa Lawi kwa jamaa zao. Wakuu wa jamaa kama walivyoandikwa kwa majina yao na kuhesabiwa kila mmoja, yaani, wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia miaka ishirini au zaidi, waliohudumu katika Hekalu laBwana.

25 Kwa maana Daudi alikuwa amesema, “Kwa vileBwana, Mungu wa Israeli amewapa watu wake raha na amekuja kuishi Yerusalemu milele,

26 Walawi hawahitaji tena kubeba Maskani wala chombo chochote cha utumishi wake.”

27 Kulingana na maagizo ya mwisho ya Daudi, Walawi waliohesabiwa ni wale wa kuanzia umri wa miaka ishirini au zaidi.

28 Wajibu wa Walawi ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aroni kuhudumu katika Hekalu laBwana: Kuwa wasimamizi wa nyua, vyumba vya pembeni, kutakasa vyombo vitakatifu na utendaji mwingine wowote katika nyumba ya Mungu.

29 Walikuwa wasimamizi wa mikate iliyowekwa mezani, unga kwa ajili ya sadaka za nafaka, mikate isiyotiwa chachu, uokaji na uchanganyaji, pamoja na vipimo vyote vya wingi na ukubwa.

30 Pia ulikuwa wajibu wao kila asubuhi kumshukuru na kumsifuBwana. Iliwapasa pia kufanya hivyo jioni

31 na wakati wowote sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwaBwanasiku za Sabato na kwenye sikukuu za Mwezi Mwandamo na katika sikukuu nyingine zilizoamriwa. Iliwapasa kuhudumu mbele zaBwanamara kwa mara kwa idadi maalum na kwa namna waliyokuwa wamepewa maelekezo.

32 Hivyo Walawi wakafanya wajibu wao katika Hema la Kukutania, katika Mahali Patakatifu chini ya uongozi wa ndugu zao wazao wa Aroni, kwa ajili ya utumishi katika Hekalu laBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/23-7402db36cf4598ea1045ca9d3f91ed49.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 24

Migawanyo Ya Makuhani

1 Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni:

Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

2 Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani.

3 Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao.

4 Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari.

5 Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.

6 Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.

7 Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu,

ya pili Yedaya,

8 ya tatu Harimu,

ya nne Seorimu,

9 ya tano Malkiya,

ya sita Miyamini,

10 ya saba Hakosi,

ya nane Abiya,

11 ya tisa Yeshua,

ya kumi Shekania,

12 ya kumi na moja Eliashibu,

ya kumi na mbili Yakimu,

13 ya kumi na tatu Hupa,

ya kumi na nne Yeshebeabu,

14 ya kumi na tano Bilga,

ya kumi na sita Imeri,

15 ya kumi na saba Heziri,

ya kumi na nane Hapisesi,

16 ya kumi na tisa Pethahia,

ya ishirini Yehezkeli,

17 ya ishirini na moja Yakini,

ya ishirini na mbili Gamuli,

18 ya ishirini na tatu Delaya,

ya ishirini na nne Maazia.

19 Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu laBwanakulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kamaBwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.

Walawi Waliobaki

20 Kuhusu wazao wa Lawi waliobaki:

Kutoka kwa wana wa Amramu: alikuwa Shubaeli;

kutoka kwa wana wa Shubaeli: alikuwa Yedeya.

21 Kwa wa Rehabia, kutoka kwa wanawe:

Ishia alikuwa wa kwanza.

22 Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomithi,

kutoka kwa wana wa Shelomithi: alikuwa Yahathi.

23 Wana wa Hebroni: Yeria alikuwa mkuu, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.

24 Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika;

kutoka kwa wana wa Mika: alikuwa Shamiri.

25 Ndugu yake Mika: alikuwa Ishia;

na kutoka kwa wana wa Ishia: alikuwa Zekaria.

26 Wana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi.

Mwana wa Yaazia: alikuwa Beno.

27 Wana wa Merari:

kutoka kwa Yaazia: ni Beno, Shohamu, Zakuri na Ibri.

28 Kutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana.

29 Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi:

alikuwa Yerameeli.

30 Nao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi.

Hawa walikuwa Walawi kulingana na jamaa zao.

31 Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/24-c345df7de7d1ae526ace055366622f52.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 25

Waimbaji

1 Daudi, pamoja na majemadari wa jeshi, wakawatenga baadhi ya wana wa Asafu, wana wa Hemani na wana wa Yeduthuni, kwa ajili ya huduma ya kutoa unabii, wakitumia vinubi, zeze na matoazi. Hii ndiyo orodha ya watu waliofanya huduma hii:

2 Kutoka kwa wana wa Asafu walikuwa:

Zakuri, Yosefu, Nethania na Asarela. Wana wa Asafu walikuwa chini ya usimamizi wa Asafu, ambaye alitoa unabii chini ya usimamizi wa mfalme.

3 Wana wa Yeduthuni walikuwa sita:

Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia, na Matithia, nao walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao Yeduthuni, wao walikuwa wakitoa unabii wakitumia vinubi, wakimshukuru na kumtukuzaBwana.

4 Wana wa Hemani walikuwa:

Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli na Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti na Romamti-Ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi.

5 Wote hawa walikuwa wana wa Hemani mwonaji wa mfalme. Aliwapata wana hawa kutokana na ahadi ya Mungu ili kumwinua. Mungu alimpa Hemani wana kumi na wanne na binti watatu.

6 Hawa wanaume wote walikuwa chini ya usimamizi wa baba yao kwa ajili ya uimbaji katika Hekalu laBwanawakitumia matoazi, zeze na vinubi, kwa ajili ya huduma katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya usimamizi wa mfalme.

7 Pamoja na ndugu zao wote walikuwa wamefundishwa na kuwa stadi wa uimbaji kwaBwana. Idadi yao walikuwa 288.

8 Vijana kwa wazee, walimu kwa wanafunzi, wote walipanga kazi zao kwa kupiga kura.

9 Kura ya kwanza, ambayo ilikuwa kwa ajili ya Asafu, ilimwangukia Yosefu,wanawe na jamaa zake, 12
Ya pili ikamwangukia Gedalia,yeye na wanawe pamoja na jamaa zake, 12
10 Ya tatu ikamwangukia Zakuri,wanawe na jamaa zake, 12
11 ya nne ikamwangukia Isri,wanawe na jamaa zake, 12
12 ya tano ikamwangukia Nethania,wanawe na jamaa zake, 12
13 ya sita ikamwangukia Bukia,wanawe na jamaa zake, 12
14 ya saba ikamwangukia Yesarela,wanawe na jamaa zake, 12
15 ya nane ikamwangukia Yeshaya,wanawe na jamaa zake, 12
16 ya tisa ikamwangukia Matania,wanawe na jamaa zake, 12
17 ya kumi ikamwangukia Shimei,wanawe na jamaa zake, 12
18 ya kumi na moja ikamwangukia Azareli,wanawe na jamaa zake, 12
19 ya kumi na mbili ikamwangukia Hashabia,wanawe na jamaa zake, 12
20 ya kumi na tatu ikamwangukia Shubaeli,wanawe na jamaa zake, 12
21 ya kumi na nne ikamwangukia Matithia,wanawe na jamaa zake, 12
22 ya kumi na tano ikamwangukia Yeremothi,wanawe na jamaa zake, 12
23 Ya kumi na sita ikamwangukia Hanania,wanawe na jamaa zake, 12
24 ya kumi na saba ikamwangukia Yoshbekasha,wanawe na jamaa zake, 12
25 ya kumi na nane ikamwangukia Hanani,wanawe na jamaa zake, 12
26 ya kumi na tisa ikamwangukia Malothi,wanawe na jamaa zake, 12
27 ya ishirini ikamwangukia Eliatha,wanawe na jamaa zake, 12
28 ya ishirini na moja ikamwangukia Hothiri,wanawe na jamaa zake, 12
29 ya ishirini na mbili ikamwangukia Gidalti,wanawe na jamaa zake, 12
30 ya ishirini na tatu ikamwangukia Mahaziothi,wanawe na jamaa zake, 12
31 ya ishirini na nne ikamwangukia Romamti-Ezeri,wanawe na jamaa zake, 12.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/25-283998d7816651ff946309de243711b7.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 26

Mabawabu

1 Hii ndiyo migawanyo ya mabawabu:

Kutoka kwa wana wa Kora alikuwa: Meshelemia mwana wa Kore, mmoja wa wana wa Asafu.

2 Meshelemia alikuwa na wana wafuatao:

Zekaria mzaliwa wa kwanza,

Yediaeli wa pili,

Zebadia wa tatu,

Yathnieli wa nne,

3 Elamu wa tano

Yehohanani wa sita

na Eliehoenai wa saba.

4 Obed-Edomu naye alikuwa na wana wafuatao:

Shemaya mzaliwa wa kwanza,

Yehozabadi wa pili,

Yoa wa tatu,

Sakari wa nne,

Nethaneli wa tano,

5 Amieli wa sita,

Isakari wa saba,

na Peulethai wa nane.

(Kwa kuwa Mungu alikuwa amembariki Obed-Edomu.)

6 Shemaya mwanawe pia alikuwa na wana, waliokuwa viongozi katika jamaa ya baba yao kwa sababu walikuwa watu wenye uwezo mkubwa.

7 Wana wa Shemaya ni: Othni, Refaeli, Obedi na Elizabadi; jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa pia watu wenye uwezo.

8 Hawa wote walikuwa wazao wa Obed-Edomu; wao na wana wao na jamaa zao walikuwa watu wenye uwezo pamoja na nguvu za kufanya kazi. Wazao wa Obed-Edomu jumla yao walikuwa sitini na wawili.

9 Meshelemia alikuwa na wana na jamaa zake, waliokuwa watu wenye uwezo: jumla yao watu kumi na wanane.

10 Hosa, Mmerari, alikuwa na wana wafuatao: Shimri alikuwa mkuu wao (baba yake alikuwa amemweka yeye kuwa mkuu ijapokuwa hakuwa mzaliwa wa kwanza),

11 Hilkia wa pili, Tabalia wa tatu na Zekaria wa nne. Wana na jamaa za Hosa jumla yao walikuwa watu kumi na watatu.

12 Hii migawanyo ya mabawabu, kupitia wakuu wao, walikuwa na zamu za kuhudumu hekaluni mwaBwanakama jamaa zao walivyokuwa nazo.

13 Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo.

14 Kura ya Lango la Mashariki ilimwangukia Shelemia.Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanawe, aliyekuwa mshauri mwenye hekima, nayo kura ya Lango la Kaskazini ikamwangukia.

15 Kura ya Lango la Kusini ikamwangukia Obed-Edomu, nayo kura ya maghala ikawaangukia wanawe.

16 Kura za Lango la Magharibi na Lango la Shalekethi kwenye barabara ya juu zikawaangukia Shupimu na Hosa.

Zamu za walinzi ziligawanywa kwa usawa:

17 Kulikuwa na Walawi sita kila siku upande wa mashariki, wanne upande wa kaskazini, wanne upande wa kusini, na wawili wawili kwa mara moja kwenye ghala.

18 Kuhusu ukumbi kuelekea magharibi, kulikuwa na wanne barabarani na wawili kwenye ukumbi wenyewe.

19 Hii ndiyo iliyokuwa migawanyo ya mabawabu waliokuwa wazao wa Kora na wa Merari.

Watunza Hazina Na Maafisa Wengine

20 Katika Walawi, Ahiya alikuwa mwangalizi wa hazina za nyumba ya Mungu na mwangalizi wa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.

21 Wazao wa Ladani, waliokuwa Wagershoni kupitia Ladani na waliokuwa viongozi wa jamaa za Ladani Mgershoni, walikuwa Yehieli,

22 wana wa Yehieli, wana wa Zethamu na wa nduguye Yoeli. Wao walikuwa waangalizi wa hazina za Hekalu laBwana.

23 Kutoka kwa wana wa Amramu, wana wa Ishari, wana wa Hebroni na wana wa Uzieli:

24 Shebueli, mzao wa Gershomu mwana wa Mose, alikuwa afisa mwangalizi wa hazina.

25 Jamaa zake kutoka kwa Eliezeri, wanawe walikuwa: Rehabia, Yeshaya, Yoramu, Zikri na Shelomithi.

26 Shelomithi na jamaa zake walikuwa waangalizi wa hazina zote za vitu vile vilivyowekwa wakfu na Mfalme Daudi, kwa viongozi wa jamaa waliokuwa majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, na kwa maafisa wengine wa jeshi.

27 Baadhi ya nyara zilizotekwa vitani waliziweka wakfu kwa ajili ya ukarabati wa Hekalu laBwana.

28 Kila kitu kilichokuwa kimewekwa wakfu na Samweli mwonaji, na Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Seruya, pamoja na vitu vingine vyote vilivyokuwa vimewekwa wakfu, vyote vilikuwa chini ya uangalizi wa Shelomithi na jamaa zake.

29 Kutoka kwa wana wa Ishari: Kenania na wanawe walipewa kazi nje ya Hekalu kama maafisa na waamuzi juu ya Israeli.

30 Kutoka kwa wana wa Hebroni: Hashabia na jamaa zake, watu 1,700 wenye uwezo, waliwajibika katika Israeli magharibi ya Yordani kwa ajili ya kazi zote zaBwanana utumishi wa mfalme.

31 Kuhusu wana wa Hebroni, Yeria alikuwa mkuu wao kufuatana na orodha ya jamaa yao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi uchunguzi ulifanyika katika kumbukumbu, nao watu wenye uwezo miongoni mwa wana wa Hebroni wakapatikana huko Yazeri katika Gileadi.

32 Yeria alikuwa na jamaa ya watu 2,700 waliokuwa watu wenye uwezo na viongozi wa jamaa, naye Mfalme Daudi akawaweka kuangalia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila Manase kuhusu kila jambo lililomhusu Mungu na shughuli za mfalme.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/26-be4a15950bc9bd7a041778b92a530266.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 27

Vikosi Vya Jeshi

1 Hii ndiyo orodha ya Waisraeli: viongozi wa jamaa, majemadari wa maelfu, majemadari wa mamia na maafisa wao, waliomtumikia mfalme kwa lolote lililohusu vikosi vya jeshi vilivyokuwa zamu mwezi baada ya mwezi katika mwaka mzima. Kila kikosi kimoja kilikuwa na watu 24,000.

2 Msimamizi wa kikosi cha kwanza kwa mwezi wa kwanza alikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Kulikuwa na watu 24,000 katika kikosi chake.

3 Yeye alikuwa mzao wa Peresi, na mkuu wa maafisa wote wa jeshi kwa mwezi wa kwanza.

4 Msimamizi wa kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai Mwahohi. Miklothi ndiye alikuwa kiongozi wa kikosi chake. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

5 Jemadari wa kikosi cha tatu kwa mwezi wa tatu alikuwa Benaya mwana wa kuhani Yehoyada. Ndiye alikuwa mkuu wa kikosi chake kilichokuwa na watu 24,000.

6 Huyu ndiye yule Benaya aliyekuwa shujaa miongoni mwa wale Thelathini na ndiye alikuwa juu yao hao Thelathini. Mwanawe Amizabadi ndiye alikuwa mkuu katika kikosi chake.

7 Jemadari wa nne kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli nduguye Yoabu, mwanawe Zebadia ndiye aliingia mahali pake kwenye uongozi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

8 Jemadari wa kikosi cha tano kwa mwezi wa tano alikuwa Shamhuthi Mwizrahi. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

9 Jemadari wa kikosi cha sita kwa mwezi wa sita alikuwa Ira, mwana wa Ikeshi Mtekoa. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

10 Jemadari wa kikosi cha saba kwa mwezi wa saba alikuwa Helesi Mpeloni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

11 Jemadari wa nane kwa mwezi wa nane, alikuwa Sibekai Mhushathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

12 Jemadari wa tisa kwa mwezi wa tisa alikuwa Abiezeri Mwanathothi wa Wabenyamini. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

13 Jemadari wa kumi kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai Mnetofathi wa Wazera. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

14 Jemadari wa kumi na moja kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaya Mpirathoni wa Waefraimu. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

15 Jemadari wa kumi na mbili kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heldai Mnetofathi kutoka jamaa ya Othnieli. Kikosi chake kilikuwa na watu 24,000.

Maafisa Wa Makabila

16 Maafisa waliokuwa wanaoongoza makabila ya Israeli walikuwa:

Kwa Wareubeni: Eliezeri mwana wa Zikri;

kwa Wasimeoni: Shefatia mwana wa Maaka;

17 kwa Walawi: Hashabia mwana wa Kemueli;

kwa Aroni: Sadoki;

18 kwa Yuda: Elihu, nduguye Daudi;

kwa Waisakari: Omri mwana wa Mikaeli;

19 kwa Wazabuloni: Ishmaya mwana wa Obadia;

kwa Wanaftali: Yeremothi mwana wa Azrieli;

20 kwa Waefraimu: Hoshea mwana wa Azazia;

kwa nusu ya kabila la Manase: Yoeli mwana wa Pedaya;

21 kwa nusu nyingine ya kabila la Manase huko Gileadi: Ido mwana wa Zekaria;

kwa Wabenyamini: Yaasieli mwana wa Abneri;

22 kwa Wadani: Azareli mwana wa Yerohamu.

Hao ndio waliokuwa maafisa wa makabila ya Israeli.

23 Daudi hakuwahesabu watu waliokuwa chini ya miaka ishirini, kwa sababuBwanaalikuwa ameahidi kuwafanya Israeli kuwa wengi kama nyota za angani.

24 Yoabu mwana wa Seruya alianza kuwahesabu watu lakini hakumaliza. Kwa sababu ya kuwahesabu watu, hasira ya Mungu iliwaka juu ya Israeli, nayo hiyo hesabu yao haikuingizwa katika kitabu cha kumbukumbu za Mfalme Daudi.

Wasimamizi Wa Mali Za Mfalme

25 Azmawethi mwana wa Adieli ndiye alikuwa msimamizi wa hazina za mfalme.

Msimamizi wa hazina katika mashamba, miji, vijiji na kwenye ngome alikuwa Yonathani mwana wa Uzia.

26 Ezri mwana wa Kelubu alikuwa msimamizi wa wafanyakazi waliolima katika mashamba.

27 Shimei Mramathi alikuwa msimamizi wa mashamba ya mizabibu.

Zabdi Mshifmi alikuwa msimamizi wa zabibu, utengenezaji na uhifadhi wa divai katika mapipa makubwa.

28 Baal-Hanani Mgederi ndiye alikuwa mwangalizi wa mashamba ya mfalme ya mizeituni na mikuyu katika tambarare za vilima vya magharibi.

Yoashi alikuwa msimamizi wa ghala za mafuta ya zeituni.

29 Shitrai Msharoni alikuwa msimamizi wa makundi ya ngʼombe waliojilisha huko Sharoni.

Shafati mwana wa Adlai alikuwa msimamizi wa yale makundi ya ngʼombe yaliyokuwa makondeni.

30 Obili Mwishmaeli alikuwa msimamizi wa ngamia.

Yedeya Mmeronothi alikuwa msimamizi wa punda.

31 Yazizi Mhagri alikuwa msimamizi wa makundi ya kondoo na mbuzi.

Hawa wote ndio waliokuwa maafisa wasimamizi wa mali alizokuwa nazo Mfalme Daudi.

32 Yonathani mjomba wa Daudi alikuwa mshauri, mtu mwenye ufahamu mkubwa na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakmoni alikuwa akiwahudumia wana wa mfalme.

33 Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme.

Hushai Mwariki alikuwa rafiki wa mfalme.

34 Baada ya Ahithofeli, Yehoyada mwana wa Benaya aliingia mahali pake kama mshauri wa mfalme pamoja na Abiathari.

Yoabu alikuwa ndiye jemadari wa majeshi ya mfalme.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/27-40052713c3a331f401cc56e641e1de08.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 28

Maandalizi Ya Daudi Ya Kujenga Hekalu

1 Daudi akawaita maafisa wote wa Israeli wakusanyike huko Yerusalemu: yaani, maafisa walio juu ya makabila, majemadari wa vikosi katika utumishi wa mfalme, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, maafisa wanaosimamia mali zote na mifugo ya mfalme na wanawe, wakiwemo maafisa wa jumba la kifalme, mashujaa na askari wote walio hodari.

2 Mfalme Daudi akainuka na kusema: “Nisikilizeni ndugu zangu nanyi watu wangu. Nilikuwa na nia ya kujenga nyumba ili iwe mahali pa kukaa Sanduku la Agano laBwanakwa ajili ya kuwa mahali pa kuwekea miguu ya Mungu wetu, nami nikafanya maandalizi ya kuijenga.

3 Lakini Mungu akaniambia, ‘Wewe hutajenga nyumba kwa Jina langu, kwa sababu wewe umepigana vita na umemwaga damu.’

4 “Hata hivyo,Bwana, Mungu wa Israeli, alinichagua mimi kutoka jamaa yangu yote niwe mfalme juu ya Israeli milele. Alimchagua Yuda kuwa kiongozi na kutoka nyumba ya Yuda akaichagua jamaa yangu na kutoka wana wa baba yangu ikampendeza kunifanya niwe mfalme juu ya Israeli yote.

5 Miongoni mwa wanangu wote, nayeBwanaamenipa wengi, amemchagua Solomoni mwanangu ili kukikalia kiti cha enzi cha ufalme waBwanajuu ya Israeli.

6 Aliniambia, ‘Solomoni mwanao ndiye atakayejenga nyumba yangu na nyua zangu, kwa maana nimemchagua yeye kuwa mwanangu, nami nitakuwa baba yake.

7 Nitaufanya imara ufalme wake milele kama akiendelea kuzishika amri zangu na sheria zangu, kama afanyavyo hivi leo.’

8 “Hivyo basi ninawaagiza mbele za Israeli yote na kusanyiko hili laBwananaye Mungu wetu akiwa anasikia: Kuweni na bidii kuzifuata amri zaBwanaMungu wenu, ili mpate kumiliki nchi hii nzuri na kuwaachia wana wenu kuwa urithi milele.

9 “Nawe Solomoni mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maanaBwanahuuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako; bali kama ukimwacha, yeye atakukataa milele.

10 Angalia basi, kwa maanaBwanaamekuchagua wewe ili ujenge Hekalu kuwa mahali patakatifu. Uwe hodari ukafanye kazi hiyo.”

11 Ndipo Daudi akampa Solomoni mwanawe kielelezo kwa ajili ya ukumbi wa Hekalu, nyumba zake, vyumba vyake vya hazina, ghorofa zake, vyumba vyake vya ndani na mahali pa kufanyia upatanisho.

12 Akampa vielelezo vya yote Roho alikuwa ameviweka moyoni mwake kwa ajili ya kumbi za Hekalu laBwanana vyumba vyote vilivyolizunguka, kwa ajili ya hazina za Hekalu la Mungu na kwa hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.

13 Mfalme pia akampa Solomoni maelekezo kwa ajili ya migawanyo ya huduma za makuhani na Walawi, pia kwa ajili ya kazi zote za huduma katika Hekalu laBwana. Akampa pia maelezo kuhusu vifaa vyote vya kutumika katika huduma ya Hekalu.

14 Akamwagizia uzito wa dhahabu kwa ajili ya vitu vyote vya dhahabu vya kutumika katika huduma mbalimbali, uzito wa fedha kwa ajili ya vitu vyote vya fedha vya kutumika katika huduma mbalimbali.

15 Uzito wa dhahabu kwa ajili ya vinara vya dhahabu na taa zake, kukiwa na uzito kwa ajili ya kila kinara na taa zake, pamoja na uzito wa fedha kwa ajili ya kila kinara cha fedha na taa zake, kulingana na matumizi ya kila kinara;

16 uzito wa dhahabu kwa ajili ya meza ya mikate iliyowekwa wakfu, uzito wa fedha kwa ajili ya meza ya fedha;

17 uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya nyuma, mabakuli ya kunyunyizia na vikombe, masinia; uzito wa dhahabu kwa ajili ya kila bakuli la dhahabu; uzito wa fedha kwa ajili ya kila bakuli la fedha;

18 na uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya madhabahu ya kufukizia uvumba. Pia alimpa kielelezo kwa ajili ya gari, yaani, wale makerubi wa dhahabu waliokunjua mbawa zao na kuweka kivuli juu ya Sanduku la Agano laBwana.

19 Daudi akasema, “Hii yote, ninayo kwa maandishi kutoka mkononi mwaBwanaulio juu yangu, naye amenipa ufahamu kwa ajili ya habari zote za kielelezo hiki.”

20 Daudi pia akamwambia Solomoni mwanawe, “Uwe hodari na moyo mkuu, ukafanye kazi hii. Usiogope wala usifadhaike, kwa maanaBwanaaliye Mungu, Mungu wangu yu pamoja nawe. Hatakuacha wala hatakupungukia mpaka kazi hii yote kwa ajili ya utumishi wa Hekalu laBwanaitakapokamilika.

21 Migawanyo ya makuhani na Walawi iko tayari kwa ajili ya kazi yote katika Hekalu la Mungu, naye kila mtu mwenye moyo wa kupenda mwenye ustadi katika aina yoyote ya ufundi atakusaidia katika kazi yote. Maafisa na watu wote watatii kila agizo lako.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/28-fb2a62e57b75a2d056b8241069adae59.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 29

Matoleo Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Hekalu

1 Ndipo Mfalme Daudi akaliambia kusanyiko lote: “Mwanangu Solomoni, yeye ambaye Mungu amemchagua, ni kijana mdogo na asiye na uzoefu. Kazi hii ni kubwa, kwa sababu Hekalu hili la fahari si kwa ajili ya mwanadamu bali ni kwa ajili yaBwana.

2 Kwa uwezo wangu wote nimetenga mali kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu: dhahabu kwa kazi za dhahabu, fedha kwa ajili ya fedha, shaba kwa kazi za shaba, chuma kwa kazi za chuma na miti kwa kazi za miti, vivyo hivyo vito vya shohamu kwa ajili ya kutia kwenye vijalizo, almasi, mawe ya rangi mbalimbali, aina zote za vito vya thamani na marmar; yote haya kwa wingi mno.

3 Zaidi ya hayo, kwa kujitolea kwangu kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, sasa ninatoa hazina zangu mwenyewe za dhahabu na fedha kwa ajili ya Hekalu la Mungu wangu, zaidi ya mali niliyotoa kwa ajili ya Hekalu hili takatifu:

4 talanta 3,000za dhahabu (dhahabu ya Ofiri) na talanta 7,000za fedha safi iliyosafishwa, kwa ajili ya kufunika kuta za Hekalu,

5 kwa kazi ya dhahabu na kazi ya fedha na kwa kazi yote itakayofanywa na mafundi. Basi, ni nani anayependa kujitoa kwaBwanaleo?”

6 Ndipo viongozi wa jamaa, maafisa wa kabila za Israeli, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia, pamoja na maafisa waliokuwa wasimamizi wa kazi za mfalme wakatoa kwa hiari yao.

7 Wakatoa kwa ajili ya kazi ya Hekalu la Mungu talanta 5,000na darkoni 10,000za dhahabu, talanta 10,000za fedha, talanta 18,000za shaba na talanta 100,000za chuma.

8 Kila mmoja aliyekuwa na vito vya thamani akavitoa katika hazina ya Hekalu laBwanachini ya uangalizi wa Yehieli Mgershoni.

9 Watu wakafurahi kwa sababu ya itikio la hiari la viongozi wao, kwa kuwa walikuwa wametoa kwa hiari na kwa moyo wote kwaBwana. Mfalme Daudi pia akafurahi sana.

Maombi Ya Daudi

10 Daudi akamhimidiBwanambele ya kusanyiko lote, akisema:

“Uhimidiwe wewe, EeBwana,

Mungu wa Israeli baba yetu,

tangu milele hata milele.

11 Ukuu na uweza, ni vyako, EeBwana,

na utukufu na enzi na uzuri,

kwa kuwa kila kilichoko mbinguni na duniani

ni chako wewe.

EeBwana, ufalme ni wako;

umetukuzwa kuwa mkuu juu ya yote.

12 Utajiri na heshima vyatoka kwako;

wewe ndiwe utawalaye vitu vyote.

Mikononi mwako kuna nguvu na uweza

ili kuinua na kuwapa wote nguvu,

13 Sasa, Mungu wetu, tunakushukuru

na kulisifu Jina lako tukufu.

14 “Lakini mimi ni nani, nao watu wangu ni nani, hata tuweze kukutolea kwa ukarimu namna hii? Vitu vyote vyatoka kwako, nasi tumekutolea tu vile vitokavyo mkononi mwako.

15 Sisi ni wageni na wapitaji machoni pako, kama walivyokuwa baba zetu wote. Siku zetu duniani ni kama kivuli, bila tumaini.

16 EeBwanaMungu wetu, kwa wingi wote huu ambao tumekutolea kwa kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina lako Takatifu, vimetoka mkononi mwako, navyo vyote ni mali yako.

17 Ninajua, Mungu wangu, kwamba wewe huujaribu moyo na unapendezwa na unyofu. Vitu hivi vyote nimetoa kwa hiari na kwa moyo mnyofu. Nami sasa nimeona kwa furaha jinsi watu wako walioko hapa kwa hiari yao walivyokutolea wewe.

18 EeBwana, Mungu wa baba zetu Abrahamu, Isaki na Israeli, weka shauku hii ndani ya mioyo ya watu wako daima na uifanye mioyo yao iwe na uaminifu kwako.

19 Nawe umpe mwanangu Solomoni kujitolea kwako kwa moyo wote ili kuzishika amri zako, masharti yako, maagizo yako na kufanya kila kitu ili kujenga Hekalu hili la fahari ambalo kwa ajili yake nimetoa.”

20 Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote, “MhimidiniBwanaMungu wenu.” Hivyo wote wakamhimidiBwana, Mungu wa baba zao. Wakasujudu na kuanguka kifudifudi mbele zaBwanana mfalme.

Solomoni Akubalika Kuwa Mfalme

21 Siku ya pili yake wakamtoleaBwanadhabihu na sadaka za kuteketezwa: mafahali 1,000, kondoo dume 1,000 na wana-kondoo dume 1,000, pamoja na sadaka za kinywaji na sadaka nyingine nyingi sana kwa ajili ya Israeli.

22 Wakala na kunywa kwa furaha kubwa mbele zaBwanasiku ile.

Wakamtawaza Solomoni mwana wa Daudi mara ya pili kuwa mfalme, wakamtia mafuta kwa ajili yaBwanaili awe mfalme na Sadoki kuwa kuhani.

23 Solomoni akaketi kwenye kiti cha enzi chaBwanakuwa mfalme mahali pa Daudi baba yake. Akafanikiwa sana na Israeli wote wakamtii.

24 Maafisa wote na mashujaa, pamoja na wana wote wa Daudi, wakaahidi kumtii Mfalme Solomoni.

25 Bwanaakamtukuza sana Solomoni mbele ya Israeli wote na kumvika fahari ya kifalme ambayo hakuna mfalme yeyote wa Israeli kabla yake aliwahi kuwa nayo.

Muhtasari Wa Utawala Wa Daudi

26 Daudi mwana wa Yese alikuwa mfalme wa Israeli yote.

27 Alitawala Israeli kwa miaka arobaini: huko Hebroni alitawala miaka saba, na katika Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.

28 Daudi akafa akiwa mzee mwenye umri mwema, akiwa ameshiba siku, utajiri na heshima. Naye Solomoni mwanawe akawa mfalme baada yake.

29 Kuhusu matukio ya utawala wa Mfalme Daudi, kuanzia mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kumbukumbu za mwonaji Samweli, na kumbukumbu za nabii Nathani na kumbukumbu za mwonaji Gadi,

30 pamoja na habari zote za utawala wake, nguvu zake na matukio yaliyompata yeye, na Israeli, na falme za nchi nyingine zote.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/29-de13ccf864afd325b146d4100815de38.mp3?version_id=1627—