Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 10

Sauli Ajiua

1 Basi Wafilisti wakapigana na Israeli. Waisraeli wakawakimbia, na wengi wakauawa katika mlima Gilboa.

2 Wafilisti wakawafuatia kwa bidii Sauli na wanawe, wakawaua Yonathani, Abinadabu na Malki-Shua.

3 Mapigano yakawa makali kumzunguka Sauli na wakati wapiga mishale walipompata, wakamjeruhi.

4 Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome nao, la sivyo hawa watu wasiotahiriwa watakuja na kunidhalilisha.”

Lakini mbeba silaha wake akaogopa sana wala hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo Sauli akachukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia.

5 Mbeba silaha wake alipoona kwamba Sauli amekufa, naye pia akauangukia upanga wake akafa.

6 Kwa hiyo Sauli na wanawe watatu wakafa, pamoja na nyumba yake yote.

7 Waisraeli wote waliokuwa bondeni walipoona kwamba jeshi limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, waliacha miji yao wakakimbia. Nao Wafilisti wakaja na kukaa humo.

8 Kesho yake Wafilisti walipokuja kuwavua maiti silaha, walimkuta Sauli na wanawe wameanguka katika Mlima Gilboa.

9 Wakamvua mavazi, wakachukua kichwa chake pamoja na silaha zake, wakawatuma wajumbe katika nchi yote ya Wafilisti kutangaza habari hizi miongoni mwa sanamu zao na watu wao.

10 Waliweka silaha zake katika hekalu la miungu yao, wakatundika kichwa chake katika hekalu la Dagoni.

11 Wakazi wote wa Yabeshi-Gileadi waliposikia yote Wafilisti waliyomtendea Sauli,

12 mashujaa wao wote wakaondoka, wakautwaa mwili wa Sauli na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mti mkubwa huko Yabeshi, nao wakafunga kwa siku saba.

13 Sauli alikufa kwa sababu hakuwa mwaminifu kwaBwana. Hakulishika neno laBwana, hata akataka shauri kwa mwaguzi kwa ajili ya uongozi,

14 hakumuulizaBwana. Kwa hiyoBwanaalimuua, na ufalme akampa Daudi mwana wa Yese.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/10-1a39b4ad164adaf0fd0257b0571cbe90.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 11

Daudi Atiwa Mafuta Kuwa Mfalme Wa Israeli

1 Israeli yote walimjia Daudi kwa pamoja huko Hebroni wakamwambia, “Sisi ni nyama yako na damu yako.

2 Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, nayeBwanaMungu wako alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ”

3 Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele zaBwana, nao wakamtia Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa naBwanaalivyoahidi kupitia kwa Samweli.

Daudi Ateka Yerusalemu

4 Daudi na Waisraeli wote wakaenda Yerusalemu (ndio Yebusi). Nao Wayebusi walioishi humo

5 wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu.” Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi.

6 Daudi alikuwa amesema, “Yeyote aongozaye mashambulizi dhidi ya Wayebusi, atakuwa jemadari mkuu.” Yoabu mwana wa Seruya akawa wa kwanza kukwea, naye akawa mkuu.

7 Daudi akafanya makao yake kwenye ngome, hivyo ukaitwa Mji wa Daudi.

8 Akajenga mji pande zote, kuanzia kwenye mito hadi kwenye ukuta kuzunguka, wakati huo huo Yoabu akajenga sehemu zingine zilizobaki za Yerusalemu.

9 Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababuBwanaMwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye.

Mashujaa Wa Daudi

10 Hawa ndio waliokuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Israeli wote wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, kamaBwanaalivyoahidi.

11 Hii ndio orodha ya mashujaa wa Daudi:

Yashobeamu, Mhakmoni, alikuwa mkuu wa maafisa; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua katika pambano moja.

12 Aliyefuata alikuwa Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu.

13 Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walikusanyika huko kwa ajili ya vita. Huko ambapo kulikuwa na shamba lililokuwa limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti.

14 Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. NayeBwanaakawapa ushindi mkubwa.

15 Wakuu watatu miongoni mwa wale thelathini, walimwendea Daudi katika mwamba huko kwenye pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai.

16 Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu.

17 Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilichoko karibu na lango la Bethlehemu!”

18 Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele zaBwana.

19 Akasema, “Mungu apishie mbali kwamba nifanye hivi! Je kweli, niinywe damu ya watu hawa waliohatarisha maisha yao?” Kwa sababu walihatarisha maisha yao kuyaleta yale maji, Daudi hakukubali kuyanywa.

Huo ndio uliokuwa ujasiri wa wale mashujaa watatu.

20 Abishai, ndugu yake Yoabu ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu.

21 Alitunukiwa heshima maradufu ya wale Watatu, akawa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao.

22 Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba.

23 Alimuua Mmisri aliyekuwa na urefu kama dhiraa tano.Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi mwake, Benaya alimwendea na rungu. Akamnyangʼanya Mmisri mkuki wake na kumuua nao.

24 Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu.

25 Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu: Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake.

26 Wale watu mashujaa walikuwa:

Asaheli nduguye Yoabu,

Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,

27 Shamothi Mharori,

Helesi Mpeloni,

28 Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa,

Abiezeri kutoka Anathothi,

29 Sibekai Mhushathi,

Ilai Mwahohi,

30 Maharai Mnetofathi,

Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi,

31 Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini,

Benaya Mpirathoni,

32 Hurai kutoka mabonde ya Gaashi,

Abieli Mwaribathi,

33 Azmawethi Mbaharumi,

Eliaba Mshaalboni,

34 wana wa Hashemu Mgiloni,

Yonathani mwana wa Shagee Mharari,

35 Ahiamu mwana wa Sakari Mharari,

Elifale mwana wa Uru,

36 Heferi Mmekerathi,

Ahiya Mpeloni,

37 Hezro Mkarmeli,

Naarai mwana wa Ezbai,

38 Yoeli nduguye Nathani,

Mibhari mwana wa Hagri,

39 Seleki Mwamoni,

Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,

40 Ira Mwithiri,

Garebu Mwithiri,

41 Uria Mhiti,

Zabadi mwana wa Alai,

42 Adina mwana wa Shiza Mreubeni, ambaye alikuwa mkuu wa Wareubeni, akiwa pamoja na watu thelathini,

43 Hanani mwana wa Maaka,

Yoshafati Mmithni,

44 Uzia Mwashterathi,

Shama na Yeieli wana wa Hothamu Mwaroeri,

45 Yediaeli mwana wa Shimri,

nduguye Yoha Mtizi,

46 Elieli Mmahawi,

Yeribai na Yoshavia wana wa Elnaamu,

Ithma Mmoabu,

47 Elieli, na Obedi na Yaasieli Mmesobai.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/11-3761b931983b4e0a41b3d8fda616b2cd.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 12

Mashujaa Waungana Na Daudi

1 Hawa ndio watu waliomjia Daudi huko Siklagi, wakati alikuwa amefukuzwa mbele ya Sauli mwana wa Kishi (walikuwa miongoni mwa mashujaa waliomsaidia Daudi vitani,

2 walikuwa na pinde na walikuwa na uwezo wa kupiga mishale au kutupa mawe kwa kombeo wakitumia mkono wa kushoto au wa kulia; hawa walikuwa ndugu zake Sauli kutoka kabila la Benyamini):

3 Mkuu wao alikuwa Ahiezeri, na wa pili Yoashi, wote wana wa Shemaa Mgibeathi; pia Yezieli na Peleti wana wa Azmawethi; Beraka, Yehu Mwanathothi,

4 na Ishmaya Mgibeoni, shujaa miongoni mwa wale Thelathini, ambaye alikuwa kiongozi wa wale Thelathini; Yeremia, Yahazieli, Yohanani, Yozabadi, Mgederathi,

5 Eluzai, Yeremothi, Bealia, Shemaria, Shefatia, Mharufi;

6 Elikana, Ishia, Azareli, Yoezeri na Yashobeamu, wana wa Kora;

7 Yoela na Zebadia, wana wa Yerohamu, kutoka Gedori.

8 Baadhi ya Wagadi wakajitenga na kujiunga na Daudi katika ngome yake huko jangwani. Walikuwa mashujaa hodari, waliokuwa tayari kwa vita na wenye uwezo wa kutumia ngao na mkuki. Nyuso zao zilikuwa nyuso za simba na walikuwa na wepesi kama paa milimani.

9 Ezeri alikuwa mkuu wao,

Obadia alikuwa wa pili katika uongozi, Eliabu wa tatu,

10 Mishmana wa nne, Yeremia wa tano,

11 Atai wa sita, Elieli wa saba,

12 Yohanani wa nane, Elzabadi wa tisa,

13 Yeremia wa kumi, na Makbanai wa kumi na moja.

14 Hawa Wagadi walikuwa majemadari. Aliyekuwa wa mwisho kuliko wote aliweza kuongoza askari 100, na aliyekuwa na uweza zaidi ya wote aliongoza 1,000.

15 Wao ndio walivuka Mto Yordani katika mwezi wa kwanza ukiwa umefurika hadi kwenye kingo zake zote na kusababisha watu wote waliokuwa wanaishi kwenye mabonde kukimbilia mashariki na wengine magharibi.

16 Wabenyamini wengine na baadhi ya watu kutoka Yuda pia walikuja kwa Daudi katika ngome yake.

17 Daudi akatoka nje kuwalaki na akawaambia, “Kama mmekuja kwangu kwa amani, kunisaidia, mimi niko tayari kuwaruhusu ninyi kuungana nami. Lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu wakati mimi mikono yangu haina hatia, basi Mungu wa baba zetu aone na awahukumu.”

18 Kisha Roho akaja juu ya Amasai, mkuu wa wale Thelathini, naye akasema:

“Sisi tu watu wako, ee Daudi!

Nasi tuko pamoja na wewe, ee mwana wa Yese!

Ushindi, naam, ushindi uwe kwako,

pia ushindi kwa wale walio upande wako,

kwa kuwa Mungu wako atakusaidia.”

Kwa hiyo Daudi akawapokea na kuwafanya viongozi wa vikosi vyake vya uvamizi.

19 Baadhi ya watu kutoka kabila la Manase wakajiunga na Daudi wakati alikwenda pamoja na Wafilisti, kupigana na Sauli. (Daudi na watu wake hawakuwasaidia Wafilisti kwa sababu, baada ya ushauri, watawala wao walimrudisha. Wakasema, “Itatugharimu vichwa vyetu kama Daudi atatuasi na kurudi kwa Sauli bwana wake.”)

20 Daudi alipokwenda Siklagi, hawa ndio watu wa kabila la Manase waliojiunga naye: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai, viongozi wa vikosi vya watu 1,000 katika kabila la Manase.

21 Walimsaidia Daudi dhidi ya makundi ya uvamizi, kwa kuwa wote walikuwa mashujaa hodari na walikuwa majemadari katika jeshi lake.

22 Siku baada ya siku watu walikuja kumsaidia Daudi, mpaka akawa na jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.

Wengine Waungana Na Daudi Huko Hebroni

23 Hawa ndio watu waliojiandaa kwa ajili ya vita waliokuja kwa Daudi huko Hebroni ili kumtwalia ufalme kutoka kwa Sauli, kamaBwanaalivyokuwa amesema:

24 watu wa Yuda, wanaochukua ngao na mikuki walikuwa 6,800 wote wakiwa tayari kwa vita.

25 Watu wa Simeoni, mashujaa waliokuwa tayari kwa vita walikuwa 7,100.

26 Watu wa Lawi walikuwa 4,600,

27 pamoja na Yehoyada, kiongozi wa jamaa ya Aroni, aliyekuwa pamoja na watu 3,700,

28 na Sadoki, kijana shujaa na hodari, aliyekuwa pamoja na maafisa ishirini na wawili kutoka jamaa yake.

29 Watu wa Benyamini, ndugu zake Sauli, walikuwa 3,000; wengi wao walikuwa wameendelea kuwa waaminifu kwa Sauli mpaka wakati huo.

30 Watu wa Efraimu, mashujaa hodari 20,800, watu waliokuwa maarufu katika koo zao.

31 Watu wa nusu ya kabila la Manase, waliotajwa kwa majina ili waje kumweka Daudi kuwa mfalme, watu 18,000.

32 Watu wa Isakari, waliofahamu majira na kujua kile ambacho Israeli inapasa kufanya, walikuwa viongozi 200, pamoja na jamaa zao wote chini ya uongozi wao.

33 Watu wa Zabuloni, askari wenye uzoefu mkubwa walioandaliwa tayari kwa vita wakiwa na silaha za kila aina, ili kumsaidia Daudi kwa uaminifu thabiti, walikuwa 50,000.

34 Watu wa Naftali, maafisa 1,000, pamoja na watu 37,000 waliochukua ngao na mikuki.

35 Watu wa Dani 28,600 waliokuwa tayari kwa vita.

36 Watu wa Asheri, askari 40,000 wenye uzoefu mkubwa waliondaliwa kwa ajili ya vita.

37 Na pia watu kutoka mashariki ya Yordani, watu wa Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, wakiwa na kila aina ya silaha, watu 120,000.

38 Wote hawa walikuwa watu wapiganaji waliojitolea kutumika katika safu zao. Walikuja Hebroni wakiwa wameamua kikamilifu kumfanya Daudi mfalme juu ya Israeli yote. Waisraeli wengine wote walikuwa pia na nia hiyo moja ya kumfanya Daudi kuwa mfalme.

39 Watu hawa wakakaa huko na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa sababu jamaa zao zilikuwa zimewapatia mahitaji yao.

40 Pia, majirani zao hata wale walio mbali hadi Isakari, Zabuloni na Naftali, walikuja wakiwaletea vyakula walivyovibeba kwa punda, ngamia, nyumbu na maksai. Kulikuwepo na wingi wa unga, maandazi ya tini, maandazi ya zabibu kavu, divai, mafuta, ngʼombe na kondoo, kwa maana kulikuwa na furaha katika Israeli.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/12-4d127e797f17cab415ee7100a65991fb.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 13

Kurudishwa Kwa Sanduku La Mungu

1 Daudi alishauriana na kila afisa wake, majemadari wa maelfu na majemadari wa mamia.

2 Ndipo Daudi akaliambia kusanyiko lote la Israeli, “Kama mkiona ni vyema, na kama ni mapenzi yaBwanaMungu wetu, tupeleke ujumbe kwa ndugu zetu wengine walio mbali na walio karibu katika nchi yote ya Israeli, pia kwa makuhani na Walawi walio pamoja nao katika miji yao na katika sehemu zao za malisho yao, waje waungane na sisi.

3 Sisi na tulirudishe Sanduku la Mungu wetu kwetu kwa maana hatukujali wakati wa utawala wa Sauli.”

4 Kusanyiko lote likakubaliana kufanya hivyo, kwa sababu ilionekana vyema kwa watu wote.

5 Basi Daudi akawakusanya Waisraeli wote, kuanzia Mto Shihori ulioko Misri hadi Lebo-Hamathi, ili kulileta Sanduku la Mungu kutoka Kiriath-Yearimu.

6 Daudi akiwa pamoja na Waisraeli wote wakaenda Baala ya Yuda (yaani Kiriath-Yearimu) kulipandisha Sanduku la MunguBwana, yeye anayeketi katika kiti cha enzi kati ya makerubi: Sanduku linaloitwa kwa Jina lake, kutoka huko.

7 Wakalisafirisha Sanduku la Mungu kwa gari jipya la kukokotwa na maksai kutoka nyumba ya Abinadabu, Uza na Ahio wakiliongoza gari hilo.

8 Daudi pamoja na Waisraeli wote walikuwa wanasifu kwa nguvu zao zote mbele za Mungu, kwa nyimbo na kwa vinubi, zeze, matari, matoazi na tarumbeta.

9 Walipofika kwenye uwanja wa kupuria nafaka wa Kidoni, Uza akaunyoosha mkono wake ili kulizuia Sanduku, kwa sababu maksai walijikwaa.

10 Hasira yaBwanaikawaka dhidi ya Uza, akampiga kwa sababu aliuweka mkono wake kwenye Sanduku. Kwa hiyo akafa pale mbele za Mungu.

11 Ndipo Daudi akakasirika kwa sababu ghadhabu yaBwanailifurika dhidi ya Uza, mahali pale pakaitwa Peres-Uzahadi leo.

12 Siku ile Daudi akamwogopa Mungu naye akauliza. “Nitawezaje kulichukua Sanduku la Mungu kwangu?”

13 Hakulichukua hilo Sanduku akae nalo katika Mji wa Daudi. Badala yake, akalipeleka nyumbani kwa Obed-Edomu, Mgiti.

14 Sanduku la Mungu likabaki pamoja na jamaa ya Obed-Edomu, nyumbani kwake kwa miezi mitatu, nayeBwanaakaibariki nyumba yake pamoja na kila kitu alichokuwa nacho.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/13-5cf1499fe7c8907d81dec27a0aec1bf1.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 14

Nyumba Ya Daudi Na Jamaa Yake

1 Basi Hiramu mfalme wa Tiro akawatuma wajumbe kwa Daudi, wakiwa na magogo ya mierezi, waashi na maseremala ili kumjengea jumba la kifalme.

2 Naye Daudi akatambua kwambaBwanaamemwimarisha kuwa mfalme juu ya Israeli na kwamba ufalme wake umetukuzwa kwa ajili ya Israeli, watu wake.

3 Huko Yerusalemu Daudi akaoa wake wengine zaidi na akawa baba wa wana na mabinti wengi.

4 Haya ndiyo majina ya watoto waliozaliwa kwake huko: Shamua, Shobabu, Nathani, Solomoni,

5 Ibihari, Elishua, Elpeleti,

6 Noga, Nefegi, Yafia,

7 Elishama, Beeliada na Elifeleti.

Daudi Awashinda Wafilisti

8 Wafilisti waliposikia kuwa Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli yote, wakapanda na jeshi lao lote kwenda kumsaka, lakini Daudi akapata habari hizo, naye akatoka ili kwenda kukabiliana nao.

9 Basi Wafilisti walikuwa wameingia na kushambulia Bonde la Warefai,

10 Hivyo Daudi akamuuliza Mungu: “Je, niende kuwashambulia hao Wafilisti? Je, utawatia mikononi mwangu?”

Bwanaakamjibu, “Nenda, nitawatia mikononi mwako.”

11 Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu,akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu.

12 Wafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto.

13 Kwa mara nyingine Wafilisti wakavamia lile bonde;

14 hivyo Daudi akamuuliza Mungu tena, naye Mungu akamjibu, “Usiwapandie moja kwa moja, bali wazungukie na uwashambulie kutoka mbele ya hiyo miti ya miforosadi.

15 Mara usikiapo sauti ya kwenda juu ya hiyo miti ya miforosadi, hapo ndipo utoke upigane vita, kwa sababu hiyo itaonyesha kwamba Mungu amekutangulia ili kupiga jeshi la Wafilisti.”

16 Kwa hiyo Daudi akafanya kama alivyoagizwa na Mungu, wakalipiga jeshi la Wafilisti kuanzia Gibeoni hadi Gezeri.

17 Hivyo umaarufu wa Daudi ukaenea katika kila nchi, nayeBwanaakayafanya mataifa yote kumwogopa Daudi.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/14-dc122d5963e0c4dd89dc7fe55c35c6c2.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 15

Sanduku La Agano Laletwa Yerusalemu

1 Baada ya Daudi kujijengea nyumba zake katika Mji wa Daudi, akatengeneza sehemu kwa ajili ya Sanduku la Mungu, kisha akasimamisha hema kwa ajili yake.

2 Kisha Daudi akasema, “Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kulibeba Sanduku la Mungu isipokuwa Walawi peke yao, kwa sababuBwanaaliwachagua kulibeba Sanduku laBwanana kuhudumu mbele zake milele.”

3 Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu ili kulipandisha Sanduku laBwanana kulileta hadi kwenye sehemu aliyokuwa ametengeneza kwa ajili yake.

4 Kisha Daudi akawakusanya pamoja wazao wa Aroni na Walawi:

5 Kutoka wazao wa Kohathi,

Urieli kiongozi na ndugu zake 120,

6 Kutoka wazao wa Merari,

Asaya kiongozi na ndugu zake 220.

7 Kutoka wazao wa Gershoni,

Yoeli kiongozi na ndugu zake 130.

8 Kutoka wazao wa Elisafani,

Shemaya kiongozi na ndugu zake 200.

9 Kutoka wazao wa Hebroni,

Elieli kiongozi na ndugu zake 80.

10 Kutoka wazao wa Uzieli,

Aminadabu kiongozi na ndugu zake 112.

11 Kisha Daudi akawaita makuhani Sadoki na Abiathari, pamoja na Walawi Urieli, Asaya, Yoeli, Shemaya, Elieli na Aminadabu.

12 Akawaambia, “Ninyi ndio viongozi wa jamaa za Walawi. Ninyi pamoja na Walawi wenzenu inawapasa mjitakase na kulipandisha Sanduku laBwana, Mungu wa Israeli hadi mahali ambapo nimetengeneza kwa ajili yake.

13 Ilikuwa ni kwa sababu hii, ninyi Walawi, hamkulipandisha Sanduku laBwanamara ya kwanza, hata ikasababishaBwanaMungu wetu kuwaka hasira dhidi yetu. Hatukumuuliza jinsi ya kufanya ili tupate kulileta jinsi alivyoagiza.”

14 Kwa hiyo makuhani pamoja na Walawi wakajitakasa ili kulipandisha Sanduku laBwana, Mungu wa Israeli.

15 Nao Walawi wakalichukua Sanduku la Mungu mabegani mwao wakitumia mipiko, kama vile Mose alivyoamuru sawasawa na neno laBwana.

16 Daudi akawaambia viongozi wa Walawi kuwaweka ndugu zao waimbaji ili waimbe nyimbo za shangwe, wakiwa na vyombo vya uimbaji: zeze, vinubi na matoazi.

17 Basi Walawi wakawaweka Hemani mwana wa Yoeli; kutoka miongoni mwa ndugu zake, Asafu mwana wa Berekia; kutoka miongoni mwa ndugu zao Wamerari, Ethani mwana wa Kushaiya;

18 hawa ndio waliochaguliwa kuwa wasaidizi wao: Zekaria, Yaazieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Benaya, Maaseya, Matithia, Elifelehu, Mikneya, pamoja na mabawabu Obed-Edomu na Yehieli.

19 Waimbaji Hemani, Asafu na Ethani walichaguliwa kupiga matoazi ya shaba;

20 Zekaria, Azieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Maaseya na Benaya walikuwa wapiga zeze kufuatana na sauti yaalamothi,

21 na Matithia, Elifelehu, Mikneya, Obed-Edomu, Yehieli na Azazia walikuwa wapiga vinubi, wakiongozwa kwa kufuata sauti yasheminithi.

22 Kenania kiongozi wa Walawi alikuwa msimamizi wa uimbaji; huu ndio uliokuwa wajibu wake kwa sababu alikuwa stadi katika hilo.

23 Berekia na Elikana walikuwa mabawabu kwa ajili ya Sanduku.

24 Shebania, Yoshafati, Nethaneli, Amasai, Zekaria, Benaya na Eliezeri, makuhani, walikuwa wapiga tarumbeta mbele ya Sanduku la Mungu. Obed-Edomu na Yehiya waliwekwa pia kuwa mabawabu wa Sanduku.

25 Basi Daudi pamoja na wazee wa Israeli na majemadari wa vikosi vya elfu wakaenda ili kulipandisha Sanduku la Agano laBwanakutoka nyumba ya Obed-Edomu kwa shangwe.

26 Kwa sababu Mungu alikuwa amewasaidia Walawi waliokuwa wanalichukua Sanduku la Agano laBwana, mafahali saba na kondoo dume saba walitolewa dhabihu.

27 Basi Daudi alikuwa amevaa joho la kitani safi, kama walivyokuwa wamevaa Walawi wote waliokuwa wanalichukua lile Sanduku, waimbaji nao walivaa vivyo hivyo, pamoja na Kenania aliyekuwa anaongoza nyimbo za waimbaji. Daudi alivaa pia kisibau cha kitani safi.

28 Hivyo Israeli wote wakalipandisha Sanduku la Agano laBwanakwa shangwe, wakipiga pembe za kondoo dume, tarumbeta, matoazi, wakipiga zeze na vinubi.

29 Sanduku la Agano laBwanalilipokuwa linaingia katika Mji wa Daudi, Mikali binti Sauli akachungulia dirishani. Naye alipomwona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea, akamdharau moyoni mwake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/15-1792d8650495241ae7c7876ca5bfc071.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 16

Sanduku Lawekwa Ndani Ya Hema

1 Wakaleta Sanduku la Mungu na kuliweka ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, na wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu.

2 Baada ya Daudi kumaliza kutoa hizo sadaka za kuteketezwa na hizo sadaka za amani, akawabariki watu katika jina laBwana.

3 Kisha akamgawia kila Mwisraeli mwanaume na mwanamke mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu.

4 Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku laBwanakufanya maombi, kumshukuru na kumsifuBwana, Mungu wa Israeli:

5 Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi,

6 nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio wangepiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu.

Zaburi Ya Daudi Ya Shukrani

7 Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwaBwana:

8 MshukuruniBwana, liitieni jina lake;

wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.

9 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa;

waambieni matendo yake yote ya ajabu.

10 Lishangilieni jina lake takatifu;

mioyo ya wale wamtafutaoBwanana ifurahi.

11 MtafuteniBwanana nguvu zake;

utafuteni uso wake siku zote.

12 Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,

miujiza yake na hukumu alizozitamka,

13 enyi wazao wa Israeli mtumishi wake,

enyi wana wa Yakobo, wateule wake.

14 Yeye ndiyeBwanaMungu wetu;

hukumu zake zimo duniani pote.

15 Hulikumbuka agano lake milele,

neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,

16 agano alilolifanya na Abrahamu,

kiapo alichomwapia Isaki.

17 Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,

kwa Israeli liwe agano la milele:

18 “Nitakupa wewe nchi ya Kanaani

kuwa sehemu utakayoirithi.”

19 Walipokuwa wachache kwa idadi,

wachache sana na wageni ndani yake,

20 walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,

kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.

21 Hakuruhusu mtu yeyote awaonee;

kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:

22 “Msiwaguse niliowatia mafuta;

msiwadhuru manabii wangu.”

23 MwimbieniBwanadunia yote;

tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.

24 Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,

matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

25 Kwa kuwaBwanani mkuu,

mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote;

yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.

26 Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,

lakiniBwanaaliziumba mbingu.

27 Fahari na enzi viko mbele yake;

nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.

28 MpeniBwana, enyi jamaa za mataifa,

mpeniBwanautukufu na nguvu,

29 mpeniBwanautukufu

unaostahili jina lake.

Leteni sadaka na mje katika nyua zake;

mwabuduniBwanakatika uzuri wa utakatifu wake.

30 Dunia yote na itetemeke mbele zake!

Ulimwengu ameuweka imara; hauwezi kusogezwa.

31 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;

semeni katikati ya mataifa, “Bwanaanatawala!”

32 Bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;

mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo ndani yake.

33 Kisha miti ya msituni itaimba,

itaimba kwa furaha mbele zaBwana,

kwa maana anakuja kuihukumu dunia.

34 MshukuruniBwanakwa kuwa ni mwema;

upendo wake wadumu milele.

35 Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe.

Tukusanye tena na utukomboe kutoka kwa mataifa,

ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu,

na kushangilia katika sifa zako.”

36 AtukuzweBwana, Mungu wa Israeli,

tangu milele na hata milele.

Nao watu wote wakasema, “Amen,” na “MsifuniBwana.”

37 Daudi akamwacha Asafu na wenzake mbele ya Sanduku la Agano laBwanaili wahudumu humo mara kwa mara, kulingana na mahitaji ya kila siku.

38 Pia akamwacha Obed-Edomu pamoja na wenzake sitini na wanane wahudumu pamoja nao. Obed-Edomu mwana wa Yeduthuni na pia Hosa walikuwa mabawabu wa lango.

39 Daudi akamwacha kuhani Sadoki pamoja na makuhani wenzake mbele ya hema ya ibada yaBwanakatika mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni

40 ili kutoa sadaka za kuteketezwa kwaBwanakwenye madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mara kwa mara, asubuhi na jioni, sawasawa na kila kitu kilichoandikwa katika sheria yaBwanaambayo alikuwa amempa Israeli.

41 Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpaBwanashukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.”

42 Hemani na Yeduthuni walikuwa na wajibu wa kupiga tarumbeta, matoazi na kutumia vyombo vingine kwa ajili ya nyimbo za sifa kwa Mungu. Wana wa Yeduthuni waliwekwa langoni.

43 Kisha watu wote wakaondoka, kila mmoja akarudi nyumbani kwake, naye Daudi akarudi nyumbani kuibariki jamaa yake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/16-157fff63e48fccd5acea57599db47d28.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 17

Ahadi Ya Mungu Kwa Daudi

1 Baada ya Daudi kuingia rasmi katika jumba lake la kifalme, akamwambia nabii Nathani, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mierezi, wakati Sanduku la Agano laBwanaliko ndani ya hema.”

2 Nathani akamjibu Daudi, “Lolote ulilo nalo moyoni mwako litende, kwa maana Mungu yu pamoja nawe.”

3 Usiku ule neno la Mungu likamjia Nathani, kusema:

4 “Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemaloBwana: Wewe hutanijengea mimi nyumba ili nikae humo.

5 Mimi sijakaa ndani ya nyumba tangu siku ile niliyowatoa Israeli kutoka Misri mpaka leo. Nimehama kutoka hema moja hadi jingine na kutoka mahali pamoja hadi pengine.

6 Je, popote nilipokwenda pamoja na Waisraeli wote, wakati wowote nilimwambia kiongozi yeyote niliyemwagiza kuwachunga watu wangu, kwa nini hujanijengea nyumba ya mierezi?’

7 “Sasa basi, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo asemaloBwanaMwenye Nguvu Zote: Nilikuchukua machungani na kutoka kuandama kondoo ili uwatawale watu wangu Israeli.

8 Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda, nami nimekuondolea mbali adui zako wote mbele yako. Basi nitalifanya jina lako kuwa kuu kama majina ya watu walio wakuu sana duniani.

9 Nami nitawapatia watu wangu Israeli mahali na nitawapa ili wawe na mahali pao wenyewe pa kuishi na wasisumbuliwe tena. Watu waovu hawatawaonea tena, kama walivyofanya mwanzoni,

10 na ambavyo wamefanya siku zote tangu nilipowachagua viongozi kwa ajili ya watu wangu Israeli. Pia nitawatiisha adui zenu wote.

“ ‘Pamoja na hayo ninakuambia kwambaBwanaatakujengea nyumba:

11 Wakati wako utakapokuwa umekwisha, nawe ukawa umekwenda kukaa na baba zako, nitamwinua mzao wako aingie mahali pako kuwa mfalme, mmoja wa wana wako mwenyewe, nami nitaufanya imara ufalme wake.

12 Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili yangu, nami nitakifanya imara kiti cha ufalme wake milele.

13 Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Kamwe sitaondoa upendo wangu kwake, kama nilivyouondoa kwa yeye aliyekutangulia.

14 Nitamweka juu ya nyumba yangu na ufalme wangu milele; kiti chake cha enzi nitakifanya imara milele.’ ”

15 Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya.

Maombi Ya Daudi

16 Ndipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele zaBwana, akasema:

“Mimi ni nani, EeBwanaMungu, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo?

17 Kana kwamba hili halitoshi machoni pako, Ee Mungu, umenena pia kuhusu siku zijazo za nyumba ya mtumishi wako. Umeniangalia kama mtu aliyetukuka kuliko watu wote, EeBwanaMungu.

18 “Daudi aweza kukuambia nini zaidi kuhusu kumheshimu mtumishi wako? Kwa maana wewe unamjua mtumishi wako,

19 EeBwanaMungu. Kwa ajili ya mtumishi wako, tena sawasawa na mapenzi yako, umefanya jambo hili kubwa sana na kujulisha ahadi hizi zote zilizo kubwa sana.

20 “Hakuna aliye kama wewe, EeBwanaMungu, wala hakuna Mungu ila wewe, kama vile tulivyosikia kwa masikio yetu wenyewe.

21 Naye ni nani aliye kama watu wako Israeli: taifa pekee duniani ambalo Mungu wake alitoka kwenda kulikomboa kwa ajili yake mwenyewe na kujifanyia jina kwa ajili yake mwenyewe, kwa kufanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa kuwafukuza mataifa mbele ya watu wako, ambao uliwakomboa kutoka Misri?

22 Uliwafanya watu wako Israeli kuwa watu wako wewe mwenyewe milele, nawe, EeBwanaMungu, umekuwa Mungu wao.

23 “Sasa basi,Bwanaahadi uliyoweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake na uithibitishe milele. Fanya kama ulivyoahidi,

24 ili ithibitike na jina lako litakuwa kuu milele. Kisha watu watasema, ‘BwanaMungu Mwenye Nguvu Zote, Mungu aliye juu ya Israeli, ndiye Mungu wa Israeli.’ Nayo nyumba ya mtumishi wako Daudi itafanywa imara mbele zako.

25 “Wewe, Mungu wangu, umemfunulia mtumishi wako Daudi kwamba utamjengea yeye nyumba. Hivyo mtumishi wako amekuwa na ujasiri wa kukuomba maombi haya.

26 EeBwana, wewe ndiwe Mungu! Umemwahidi mtumishi wako mambo haya mazuri.

27 Basi imekupendeza kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili idumu milele machoni pako; kwa ajili yako, EeBwana, umeibariki, nayo itabarikiwa milele.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/17-52d2e7b2e6461151dcb51c5728205bb9.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 18

Ushindi Wa Daudi

1 Baada ya muda, Daudi akawashinda Wafilisti na kuwatiisha, naye akautwaa Gathi pamoja na vijiji vinavyouzunguka kutoka utawala wa Wafilisti.

2 Pia Daudi akawashinda Wamoabu, wakawa watumishi wake, nao wakawa wanamletea ushuru.

3 Zaidi ya hayo, Daudi akapigana na Hadadezeri mfalme wa Soba, hadi Hamathi, wakati alikwenda kuimarisha utawala wake katika Mto Frati.

4 Daudi akateka magari ya vita 1,000 miongoni mwa magari yake, waendesha hayo magari ya kukokotwa na farasi 7,000 na askari wa miguu 20,000. Daudi akakata mishipa ya miguu ya nyuma ya farasi wote wakokotao magari, ila akabakiza 100.

5 Waaramu wa Dameski, walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi akawashambulia na kuwaua 22,000 miongoni mwao.

6 Daudi akaweka askari walinzi katika ufalme wa Waaramu huko Dameski. Basi Waaramu wakawa watumwa wa Daudi, na kumlipa ushuru.Bwanaakampa Daudi ushindi kote alipokwenda.

7 Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizokuwa za maafisa wa Hadadezeri na kuzileta Yerusalemu.

8 Kutoka miji ya Tibhathi na Kuni, iliyokuwa miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi sana, ambayo Solomoni aliitumia kutengenezea ile Bahari ya shaba, zile nguzo na vifaa mbalimbali vya shaba.

9 Tou mfalme wa Hamathi aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri mfalme wa Soba,

10 akamtuma mwanawe, Hadoramu kwa Mfalme Daudi ili kumsalimu na kumpongeza kwa ushindi wake katika vita dhidi ya Mfalme Hadadezeri, kwa kuwa alikuwa amepigana vita mara nyingi na Tou. Hadoramu akamletea Daudi vifaa mbalimbali vya dhahabu, fedha na shaba.

11 Mfalme Daudi akaviweka vifaa hivi wakfu kwaBwanakama vile alivyokuwa amefanya kwa fedha na dhahabu aliyokuwa ameitwaa katika mataifa yote haya: Edomu na Moabu, Waamoni, Wafilisti na Waamaleki.

12 Abishai mwana wa Seruya akawaua Waedomu 18,000 katika Bonde la Chumvi.

13 Akaweka kambi za askari walinzi huko Edomu, nao Waedomu wote wakawa watumishi wa Daudi.Bwanaakampa Daudi ushindi kila alipokwenda.

Maafisa Wa Daudi

14 Daudi akatawala Israeli yote, akitenda lililo haki na sawa kwa watu wake wote.

15 Yoabu mwana wa Seruya alikuwa jemadari wa jeshi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mweka kumbukumbu;

16 Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; Shausha alikuwa mwandishi;

17 naye Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa msimamizi wa Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi walikuwa maafisa wakuu katika utumishi wa mfalme.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/18-ad664989e284da66c3799c403fb625f0.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 19

Vita Dhidi Ya Waamoni

1 Baada ya muda, Nahashi mfalme wa Waamoni akafa, mwanawe akaingia mahali pake.

2 Daudi akawaza, “Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kwa sababu baba yake alinitendea wema.”

Hivyo Daudi akatuma wajumbe ili kumfariji Hanuni kwa ajili ya kifo cha baba yake. Watu wa Daudi walipofika kwa Hanuni katika nchi ya Waamoni ili kumfariji,

3 wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, “Hivi unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kuwatuma wajumbe kukufariji? Je, hawa watu hawakuja kuipeleleza na kuidadisi nchi ili waishinde?”

4 Kwa hiyo Hanuni akawakamata watu wa Daudi, akawanyoa ndevu akakata nguo zao katikati kwenye matako, akawaacha waende zao.

5 Mtu mmoja alipofika na kumpasha Daudi habari za watu hawa, akawatuma wajumbe wengine kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko mpaka ndevu zenu ziote, ndipo mje.”

6 Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni wakatuma talanta 1,000za fedha ili kukodisha magari ya vita pamoja na waendeshaji wa hayo magari ya kukokotwa na farasi, kutoka Aramu-Naharaimu,Aramu-Maaka na Soba.

7 Wakakodisha magari ya vita 32,000 yakiwa na waendeshaji wake, pamoja na mfalme wa Maaka na vikosi vyake, wakaja na kupiga kambi karibu na Medeba. Waamoni nao wakakusanyika toka miji yao, wakatoka ili kupigana vita.

8 Daudi aliposikia jambo hili, akamtuma Yoabu na jeshi lote la wapiganaji.

9 Waamoni wakatoka wakajipanga wakiwa tayari kwa vita langoni la mji wao, wakati wale wafalme wengine waliokuja nao walijipanga kwa vita uwanjani.

10 Yoabu akaona kuwa mbele yake na nyuma yake kumepangwa vita; kwa hiyo akachagua baadhi ya vikosi vilivyo bora sana katika Israeli akavipanga dhidi ya Waaramu.

11 Akawaweka wale wanajeshi wengine waliobaki chini ya amri ya Abishai ndugu yake, nao wakapangwa ili wakabiliane na Waamoni.

12 Yoabu akasema, “Kama Waaramu watanizidi nguvu, basi itakupasa wewe unisaidie; lakini kama Waamoni watakuzidi nguvu, basi mimi nitakusaidia.

13 Uwe hodari na tupigane kwa ujasiri kwa ajili ya watu wetu na miji ya Mungu wetu.Bwanaatafanya lile lililo jema machoni pake.”

14 Basi Yoabu na vikosi vyake wakasonga mbele kupigana na Waaramu, nao Waaramu wakakimbia mbele yake.

15 Waamoni walipoona Waaramu wanakimbia, nao pia wakakimbia mbele ya nduguye Abishai na kuingia ndani ya mji. Basi Yoabu akarudi Yerusalemu.

16 Baada ya Waaramu kuona kwamba wameshindwa na Israeli, wakapeleka wajumbe na kuwataka Waaramu wengine kutoka ngʼambo ya Mto Frati, wakiongozwa na Shofaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri.

17 Daudi alipoambiwa haya, akawakusanya Israeli wote na kuvuka Yordani. Akasonga mbele dhidi yao na akajipanga kuwakabili. Daudi akapanga vita ili kupigana na Waaramu, nao wakapigana dhidi yake.

18 Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari 7,000 na askari wao wa miguu 40,000. Pia akamuua Shofaki, jemadari wa jeshi lao.

19 Raiya wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, wakafanya mapatano ya amani na Daudi, wakawa watumishi wake.

Hivyo Waaramu hawakukubali kuwasaidia Waamoni tena.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/19-c41b9e3074e3918643b971793a543252.mp3?version_id=1627—