Categories
1 Nyakati

1 Nyakati Utangulizi

Utangulizi

Jina hili la kitabu “Mambo ya Nyakati” linaweza likafuatiliwa hadi kwa Yerome ambaye alilitumia katika tafsiri ya Kilatini ya Neno la Mungu, yaani “Vulgate.” Jina la kitabu hiki katika Kiyunani, “Mambo Yaliyorukwa,” linaonyesha ile hali ya watafsiri wa Agano la Kale katika “Septuagint” kwamba mambo yaliyomo katika vitabu hivi kimsingi yalikuwa mambo ya nyongeza yaliyokuwa yameachwa na vitabu vya Samweli na Wafalme.

Vitabu vya 1 na 2 Mambo ya Nyakati viliandikwa kwa ajili ya watu waliorudi Israeli kutoka utumwani, baada ya kutekwa na kupelekwa Babeli, ili kuwakumbusha kwamba walikuwa wa ukoo wa ufalme wa Daudi, na kwamba wao walikuwa watu wateule wa Mungu.

Mwandishi

Mapokeo ya Kiyahudi husema ni Ezra.

Kusudi

Kuunganisha watu wa Mungu, kufuatilia ukoo wa Daudi, na kufundisha watu sala iliyo ya kweli ambayo ndiyo hitaji kubwa katika maisha ya mtu binafsi na taifa pia.

Mahali

Yerusalemu, na katika Hekalu.

Tarehe

Kama mwaka wa 430 K.K.

Wahusika Wakuu

Daudi na Solomoni.

Wazo Kuu

Kitabu cha 1 Mambo ya Nyakati kinaelezea kwa kifupi historia na koo za Waisraeli tangu Adamu hadi kifo cha Mfalme Sauli. Sehemu ya kitabu iliyobaki inaeleza habari za Mfalme Daudi.

Mambo Muhimu

Kuelezea historia ya vizazi vya Israeli, na habari kumhusu Mfalme Daudi na uhusiano wake na Mungu, na kuletwa kwa Sanduku la Agano huko Yerusalemu kama chanzo cha sala ya kweli.

Mgawanyo

ORODHA YA VIZAZI (

1:1–9:44

)

1. Orodha ya nasaba za mababa wa taifa

2. Makabila ya Israeli

3. Kurudi kutoka utumwa Babeli.

UTAWALA WA DAUDI (

10:1–29:30

)

1. Daudi afanyika mfalme juu ya Israeli yote

2. Daudi alirudisha Sanduku la

Bwana

Yerusalemu

3. Majeshi ya Daudi yajinufaisha

4. Daudi aandaa kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu.

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 1

Kumbukumbu Za Historia Kuanzia Adamu Hadi Abrahamu

Adamu Hadi Wana Wa Noa

1 Adamu, Sethi, Enoshi,

2 Kenani, Mahalaleli, Yaredi,

3 Enoki, Methusela, Lameki, Noa.

4 Wana wa Noa walikuwa:

Shemu, Hamu na Yafethi.

Wana Wa Yafethi

5 Wana wa Yafethi walikuwa:

Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

6 Wana wa Gomeri walikuwa:

Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

7 Wana wa Yavani walikuwa:

Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.

Wana Wa Hamu

8 Wana wa Hamu walikuwa:

Kushi, Misraimu,Putu na Kanaani.

9 Wana wa Kushi walikuwa:

Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka.

Wana wa Raama walikuwa:

Sheba na Dedani.

10 Kushi akamzaa

Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi.

11 Misraimu akawazaa:

Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,

12 Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.

13 Wana wa Kanaani walikuwa:

Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi,

14 Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,

15 Wahivi, Waariki, Wasini,

16 Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.

Wana Wa Shemu

17 Wana wa Shemu walikuwa:

Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu.

Wana wa Aramu walikuwa:

Usi, Huli, Getheri na Mesheki.

18 Arfaksadi akamzaa Shela,

Shela akamzaa Eberi.

19 Eberi alipata wana wawili:

Mmoja wao aliitwa Pelegi,kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani.

20 Wana wa Yoktani walikuwa:

Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,

21 Hadoramu, Uzali, Dikla,

22 Obali, Abimaeli, Sheba,

23 Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani.

24 Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela,

25 Eberi, Pelegi, Reu,

26 Serugi, Nahori, Tera,

27 Tera akamzaa Abramu (yaani, Abrahamu).

Jamaa Ya Abrahamu

28 Abrahamu alikuwa na wana wawili:

Isaki na Ishmaeli.

Wazao Wa Hagari

29 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Hagari:

Nebayothi mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Kedari, Adbeeli, Mibsamu,

30 Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema,

31 Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.

Wazao Wa Ketura

32 Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa:

Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.

Wana wa Yokshani walikuwa:

Sheba na Dedani.

33 Wana wa Midiani walikuwa:

Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa.

Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura.

Wazao Wa Sara

34 Abrahamu alikuwa baba wa Isaki.

Wana wa Isaki walikuwa:

Esau na Israeli.

Wana Wa Esau

35 Wana wa Esau walikuwa:

Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora.

36 Wana wa Elifazi walikuwa:

Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi;

Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki.

37 Wana wa Reueli walikuwa:

Nahathi, Zera, Shama na Miza.

Watu Wa Seiri Waliokuwa Edomu

38 Wana wa Seiri walikuwa:

Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani.

39 Wana wa Lotani walikuwa wawili:

Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna.

40 Wana wa Shobali walikuwa:

Alvani,Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.

Wana wa Sibeoni walikuwa:

Aiya na Ana.

41 Mwana wa Ana alikuwa:

Dishoni.

Nao wana wa Dishoni walikuwa:

Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.

42 Wana wa Eseri walikuwa:

Bilhani, Zaavani na Akani.

Wana wa Dishani walikuwa:

Usi na Arani.

Watawala Wa Edomu

43 Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli:

Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba.

44 Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.

45 Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.

46 Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.

47 Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.

48 Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake.

49 Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.

50 Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.

51 Naye Hadadi pia akafa.

Wakuu wa Edomu walikuwa:

Timna, Alva, Yethethi,

52 Oholibama, Ela, Pinoni,

53 Kenazi, Temani, Mibsari,

54 Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/1-f4c06fda4cc22e1527f752ad96ef473c.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 2

Wana Wa Israeli

1 Hawa ndio waliokuwa wana wa Israeli:

Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zabuloni,

2 Dani, Yosefu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri.

Yuda

Hadi Wana Wa Hesroni

3 Wana wa Yuda walikuwa:

Eri, Onani na Shela. Hawa watatu walizaliwa kwake na mkewe Mkanaani, binti wa Shua. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu machoni paBwana, kwa hiyoBwanaalimuua.

4 Tamari, mkwewe Yuda, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Yuda alikuwa na jumla ya wana watano.

5 Wana wa Peresi walikuwa:

Hesroni na Hamuli.

6 Wana wa Zera walikuwa:

Zimri, Ethani, Hemani, Kalkoli na Dara. Jumla ya wana wa Zera walikuwa watano.

7 Mwana wa Karmi alikuwa:

Akari,ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutokuchukua vitu vilivyokuwa vimewekwa wakfu.

8 Mwana wa Ethani alikuwa:

Azariya.

9 Wana wa Hesroni walikuwa:

Yerameeli, Ramu na Kalebu.

Kuanzia Ramu Mwana Wa Hesroni

10 Ramu alimzaa

Aminadabu, na Aminadabu akamzaa Nashoni, kiongozi wa kabila la Yuda.

11 Nashoni akamzaa Salmoni, Salmoni akamzaa Boazi,

12 Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese.

13 Yese akawazaa

Eliabu mwanawe wa kwanza; wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea,

14 wa nne Nethaneli, wa tano Radai,

15 wa sita Osemu, na wa saba Daudi.

16 Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli.

17 Abigaili alikuwa mama yake Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.

Kalebu Mwana Wa Hesroni

18 Kalebu mwana wa Hesroni akazaa wana na mkewe Azuba (na pia na Yeriothi). Hawa ndio wana Azuba aliomzalia Kalebu: Yesheri, Shobabu na Ardoni.

19 Azuba alipofariki, Kalebu akamwoa Efrathi, ambaye alimzalia Huri.

20 Huri akamzaa Uri, Uri akamzaa Bezaleli.

21 Hatimaye, Hesroni akakutana kimwili na binti wa Makiri babaye Gileadi (ambaye alimwoa alipokuwa na umri wa miaka sitini), naye akamzaa Segubu.

22 Segubu akamzaa Yairi, ambaye alitawala miji ishirini na mitatu katika Gileadi.

23 (Lakini Geshuri na Aramu wakateka miji ya Hawoth-Yairi, pamoja na Kenathi na viunga vyake; jumla ilikuwa miji sitini.) Wote hawa walikuwa wazao wa Makiri babaye Gileadi.

24 Baada ya Hesroni kufa huko Efrathi, Abiya mjane wa Hesroni akamzalia Ashuru, aliye baba wa Tekoa.

Yerameeli Mwana Wa Hesroni

25 Wana wa Yerameeli mzaliwa wa kwanza wa Hesroni walikuwa:

Ramu mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya.

26 Yerameeli alikuwa na mke mwingine, aliyeitwa Atara, aliyekuwa mama yake Onamu.

27 Wana wa Ramu mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli walikuwa:

Maasi, Yamini na Ekeri.

28 Wana wa Onamu walikuwa:

Shamai na Yada.

Wana wa Shamai walikuwa:

Nadabu na Abishuri.

29 Mke wa Abishuri aliitwa Abihaili, ambaye alimzalia Abani na Molidi.

30 Wana wa Nadabu walikuwa

Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa bila kuzaa watoto.

31 Apaimu akamzaa:

Ishi ambaye alikuwa baba wa Sheshani.

Sheshani akamzaa Alai.

32 Wana wa Yada, nduguye Shamai walikuwa:

Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa bila kuzaa watoto.

33 Wana wa Yonathani walikuwa:

Pelethi na Zaza.

Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yerameeli.

34 Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, ila wasichana tu.

Alikuwa na mtumishi Mmisri aliyeitwa Yarha.

35 Sheshani akamwoza huyu mtumishi wake Yarha binti yake, akamzalia mwana jina lake Atai.

36 Atai akamzaa Nathani,

Nathani akamzaa Zabadi,

37 Zabadi akamzaa Eflali,

Eflali akamzaa Obedi,

38 Obedi akamzaa Yehu,

Yehu akamzaa Azaria,

39 Azaria akamzaa Helesi,

Helesi akamzaa Eleasa,

40 Eleasa akamzaa Sismai,

Sismai akamzaa Shalumu,

41 Shalumu akamzaa Yekamia,

naye Yekamia akamzaa Elishama.

Koo Za Kalebu

42 Wana wa Kalebu nduguye Yerameeli walikuwa:

Mesha mzaliwa wake wa kwanza alimzaa Zifu, naye mwanawe Maresha akamzaa Hebroni.

43 Hebroni alikuwa na wana wanne:

Kora, Tapua, Rekemu na Shema.

44 Shema alikuwa baba yake Rahamu na Rahamu alikuwa baba wa Yorkeamu na Rekemu alikuwa baba wa Shamai.

45 Shamai akamzaa Maoni na Maoni akamzaa Beth-Suri.

46 Efa, suria wa Kalebu alikuwa mamaye Harani, Mosa na Gazezi. Harani alikuwa baba wa Gazezi.

47 Wana wa Yadai walikuwa:

Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu.

48 Maaka suria wa Kalebu alikuwa mamaye Sheberi na Tirhana.

49 Pia Maaka akamzaa Shaafu babaye Madmana, na Sheva babaye Makbena na Gibea. Kalebu alikuwa na binti jina lake Aksa.

50 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Kalebu.

Wana wa Huri, mzaliwa mkuu wao wa Efrathi, walikuwa:

Shobali akamzaa Kiriath-Yearimu,

51 Salma akamzaa Bethlehemu, naye Harefu akamzaa Beth-Gaderi.

52 Wazao wa Shobali, baba yake Kiriath-Yearimu, walikuwa:

Haroe, nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi,

53 pamoja na koo za Kiriath-Yearimu ambazo ni: Waithiri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. Kutokana na watu hawa walizaliwa Wasorathi na Waeshtaoli.

54 Wazao wa Salma walikuwa:

Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, nusu ya Wamanahathi, Wasori,

55 pamoja na koo za waandishi zilizoishi katika mji wa Yabesi: yaani Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Hawa ndio Wakeni waliotokana na Hamathi, baba wa nyumba ya Rekabu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/2-a1dde605f23315c89d40233f2faf3c77.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 3

Wana Wa Daudi

1 Hawa ndio waliokuwa wana wa Daudi waliozaliwa huko Hebroni:

Mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni ambaye mama yake aliitwa Ahinoamu wa Yezreeli;

wa pili, Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili wa Karmeli;

2 wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, binti Talmai mfalme wa Geshuri;

wa nne, Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi;

3 wa tano alikuwa Shefatia ambaye mama yake alikuwa Abitali;

wa sita alikuwa Ithreamu, aliyezaliwa na mke wake Egla.

4 Hawa sita walizaliwa huko Hebroni ambako Daudi alitawala kwa miaka saba na miezi sita.

Daudi alitawala Yerusalemu kwa miaka thelathini na mitatu,

5 nao hawa ndio watoto wa Daudi waliozaliwa huko Yerusalemu:

mkewe Bathsheba, binti Amieli, alimzalia Shamua,Shobabu, Nathani na Solomoni.

6 Pia kulikuwa na wana wengine: Ibihari, Elishua, Elifeleti,

7 Noga, Nefegi, Yafia,

8 Elishama, Eliada na Elifeleti; wote walikuwa tisa.

9 Hawa wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wana waliozaliwa na masuria. Naye Tamari alikuwa dada yao.

Wafalme Wa Yuda

10 Mwana wa Solomoni alikuwa Rehoboamu,

mwanawe huyo alikuwa Abiya,

mwanawe huyo alikuwa Yehoshafati,

mwanawe huyo alikuwa Asa,

11 mwanawe huyo alikuwa Yehoramu,

mwanawe huyo alikuwa Ahazia,

mwanawe huyo alikuwa Yoashi,

12 mwanawe huyo alikuwa Amazia,

mwanawe huyo alikuwa Azaria,

mwanawe huyo alikuwa Yothamu,

13 mwanawe huyo alikuwa Ahazi,

mwanawe huyo alikuwa Hezekia,

mwanawe huyo alikuwa Manase,

14 mwanawe huyo alikuwa Amoni

na mwanawe huyo alikuwa Yosia.

15 Wana wa Yosia walikuwa:

Yohanani mzaliwa wake wa kwanza,

Yehoyakimu mwanawe wa pili,

wa tatu Sedekia,

wa nne Shalumu.

16 Walioingia mahali pa Yehoyakimu kama wafalme ni:

Yekonia mwanawe,

na Sedekia.

Ukoo Wa Kifalme Baada Ya Uhamisho

17 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yekonia aliyekuwa mateka:

Shealtieli mwanawe,

18 Malkiramu, Pedaya, Shenasari, Yekamia, Hoshama na Nedabia.

19 Wana wa Pedaya walikuwa:

Zerubabeli na Shimei.

Wana wa Zerubabeli walikuwa:

Meshulamu na Hanania.

Shelomithi alikuwa dada yao.

20 Pia walikuwepo wengine watano:

Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-Hesedi.

21 Wazao wa Hanania walikuwa:

Pelatia na Yeshaya, na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.

22 Wazao wa Shekania:

Shemaya na wanawe:

Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati; jumla yao walikuwa sita.

23 Wana wa Nearia walikuwa:

Elioenai, Hizkia na Azrikamu; jumla yao watatu.

24 Wana wa Elioenai walikuwa:

Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani; jumla yao wote saba.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/3-63383f6fd4d3a50103c8a68bec68b895.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 4

Koo Nyingine Za Yuda

1 Wana wa Yuda walikuwa:

Peresi, Hesroni, Karmi, Huri na Shobali.

2 Reaya mwana wa Shobali akamzaa Yahathi, Yahathi akawazaa Ahumai na Lahadi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Wasorathi.

3 Hawa ndio waliokuwa wana wa Etamu:

Yezreeli, Ishma na Idbashi. Dada yao aliitwa Haselelponi.

4 Penueli akamzaa Gedori, naye Ezeri akamzaa Husha.

Hawa walikuwa wazao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, na baba yake Bethlehemu.

5 Ashuri baba yake Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.

6 Hawa walikuwa wazao wa Naara: Ahuzamu, Heferi, Temeni na Haahashtari.

7 Wana wa Hela walikuwa:

Serethi, Sohari, Ethnani,

8 na Kosi ambaye aliwazaa Anubi, Sobeba na jamaa zote za Aharheli mwana wa Harumu.

9 Yabesi aliheshimiwa kuliko ndugu zake. Mama yake alimwita Yabesi, akisema, “Nilimzaa kwa huzuni.”

10 Yabesi akamlilia Mungu wa Israeli akisema, “Ee Mungu, laiti ungenibariki kweli kweli na kuipanua mipaka yangu! Mkono wako na uwe pamoja nami, uniepushe na uovu ili nisidhurike!” Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.

11 Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, naye Mehiri akamzaa Eshtoni.

12 Eshtoni akawazaa Beth-Rafa, Pasea na Tehina. Tehina alikuwa baba wa Iri-Nahashi. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Reka.

13 Wana wa Kenazi walikuwa:

Othnieli na Seraya.

Wana wa Othnieli walikuwa:

Hathathi na Meonathai.

14 Meonathai akamzaa Ofra.

Seraya akamzaa Yoabu,

baba wa Ge-Harashimu.Liliitwa hivyo kwa sababu watu walioishi humo walikuwa mafundi.

15 Kalebu mwana wa Yefune alikuwa na wana watatu:

Iru, Ela na Naamu.

Naye mwana wa Ela alikuwa:

Kenazi.

16 Wana wa Yahaleleli walikuwa:

Zifu, Zifa, Tiria na Asareli.

17 Wana wa Ezra walikuwa:

Yetheri, Meredi, Eferi na Yaloni. Mmojawapo wa wake zake Meredi aliwazaa: Miriamu, Shamai na Ishba aliyekuwa baba yake Eshtemoa.

18 Meredi alikuwa na mke mwingine Myahudi ambaye aliwazaa: Yeredi baba wa Gedori, Heberi baba wa Soko na Yekuthieli baba wa Zanoa. Hawa walikuwa watoto wa Bithia binti Farao, ambaye Meredi alikuwa amemwoa.

19 Wana wa mke wa Hodia aliyekuwa dada yake Nahamu walikuwa:

baba yake Keila, Mgarmi na Eshtemoa, Mmaakathi.

20 Wana wa Shimoni walikuwa:

Amnoni, Rina, Ben-Hanani na Tiloni.

Wazao wa Ishi walikuwa:

Zohethi na Ben-Zohethi.

21 Wana wa Shela, mwana wa Yuda, walikuwa:

Eri baba yake Leka, Laada baba yake Maresha na jamaa za wafumaji nguo za kitani safi waliokuwa wakiishi huko Beth-Ashbea,

22 Yokimu, watu walioishi Kozeba, Yoashi na Sarafi waliotawala huko Moabu na Yashubi-Lehemu. (Taarifa hizi ni za zamani sana.)

23 Hawa walikuwa wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera; waliishi huko wakimtumikia mfalme.

Simeoni

24 Wazao wa Simeoni walikuwa:

Nemueli, Yamini, Yaribu, Zera na Shauli.

25 Mwana wa Shauli alikuwa Shalumu, Shalumu akamzaa Mibsamu, na Mibsamu akamzaa Mishma.

26 Wazao wa Mishma walikuwa:

Hamueli aliyemzaa Zakuri, Zakuri akamzaa Shimei.

27 Shimei alikuwa na wana kumi na sita, na binti sita, lakini ndugu zake hawakuwa na watoto wengi, hivyo ukoo wao wote haukuwa na watu wengi kama ukoo wa Yuda.

28 Waliishi Beer-Sheba, Molada, Hasar-Shuali,

29 Bilha, Esemu, Toladi,

30 Bethueli, Horma, Siklagi,

31 Beth-Markabothi, Hasar-Susimu, Beth-Biri na Shaaraimu. Hii ilikuwa miji yao mpaka wakati wa utawala wa Daudi.

32 Vijiji vilivyoizunguka vilikuwa Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani; jumla miji mitano:

33 pamoja na vijiji vyote kuizunguka hii miji hadi huko Baali. Haya yalikuwa makao yao, nao waliweka kumbukumbu ya ukoo wao.

34 Meshobabu, Yamleki, Yosha mwana wa Amazia,

35 Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli.

36 Pia Elioenai, Yaakoba, Yeshohaya, Asaya, Adieli, Yesimieli, Benaya,

37 Ziza mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya.

38 Watu hawa walioorodheshwa hapa juu kwa majina walikuwa viongozi wa koo zao. Jamaa zao ziliongezeka sana,

39 wakaenea mpaka kwenye viunga vya Gedori kuelekea mashariki mwa bonde wakitafuta malisho kwa ajili ya mifugo yao.

40 Huko walipata malisho mengi mazuri, nayo nchi ilikuwa na nafasi kubwa, yenye amani na utulivu. Baadhi ya Wahamu waliishi huko zamani.

41 Watu walioorodheshwa majina walikuja katika nchi hiyo wakati wa Hezekia mfalme wa Yuda. Akawashambulia Wahamu katika makao yao pamoja na Wameuni ambao walikuwako huko nao wakawaangamiza kabisa, kama ilivyo dhahiri hadi leo. Kisha wakafanya makazi yao huko kwa sababu kulikuwa na malisho mazuri kwa ajili ya mifugo yao.

42 Watu wa kabila la wa Simeoni wapatao mia tano, wakiongozwa na Pelatia, Nearia, Refaya na Uzieli wana wa Ishi, wakavamia nchi ya vilima ya Seiri.

43 Wakawaua Waamaleki waliobaki, waliokuwa wamenusurika, nao wanaishi huko hadi leo.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/4-6eb0fdddf0ca8f310fb8cf2047399897.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 5

Wana Wa Reubeni

1 Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli (yeye alikuwa mzaliwa wa kwanza, lakini kwa kuwa alikinajisi kitanda cha baba yake, haki zake za mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yosefu mwana wa Israeli. Hivyo hakuorodheshwa kwenye orodha ya ukoo wao kulingana na haki yake ya kuzaliwa.

2 Na ingawa Yuda alikuwa na nguvu zaidi ya ndugu zake wote, na mtawala alitoka kwake, haki za mzaliwa wa kwanza zilikuwa za Yosefu.)

3 Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli walikuwa:

Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi.

4 Wazao wa Yoeli walikuwa:

Shemaya mwanawe, Gogu mwanawe;

Shimei mwanawe,

5 Mika mwanawe,

Reaya mwanawe, Baali mwanawe,

6 na Beera mwanawe, ambaye Tiglath-Pileseri mfalme wa Ashuru alimchukua kwenda uhamishoni. Beera alikuwa kiongozi wa Wareubeni.

7 Jamaa zao kulingana na koo zao, walioorodheshwa kwa kufuata koo zao kama ifuatavyo:

Yeieli aliyekuwa mkuu wao, Zekaria,

8 Bela mwana wa Azazi, mwana wa Shema, mwana wa Yoeli. Hao waliishi katika eneo kuanzia Aroeri mpaka Nebo na Baal-Meoni.

9 Kwa upande wa mashariki walienea hadi pembeni mwa jangwa linaloenea mpaka kwenye Mto Frati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka huko Gileadi.

10 Wakati wa utawala wa Mfalme Sauli, walipigana vita dhidi ya Wahagari, wakaanguka kwa mikono yao, kisha wakaishi katika mahema ya Wahagari katika eneo lote la mashariki ya Gileadi.

Wana Wa Gadi

11 Wagadi waliishi jirani nao katika nchi ya Bashani, mpaka Saleka.

12 Yoeli ndiye alikuwa mkuu wao, Shafamu wa pili, na wakafuata Yanai na Shafati, huko Bashani.

13 Ndugu zao kulingana na koo zao walikuwa saba:

Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, Zia na Eberi.

14 Hawa walikuwa ndio wana wa Abihaili mwana wa Huri, mwana wa Yaroa, mwana wa Gileadi, mwana wa Mikaeli, mwana wa Yeshishai, mwana wa Yahdo, mwana wa Buzi.

15 Ahi mwana wa Abdieli, mwana wa Guni, alikuwa ndiye kiongozi wa jamaa yao.

16 Wagadi waliishi Gileadi, huko Bashani pamoja na vijiji vilivyoizunguka, pia katika nchi yote ya malisho ya Sharoni kote walikoenea.

17 Yote haya yaliwekwa katika kumbukumbu za ukoo wao wakati wa utawala wa Yothamu, mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli.

18 Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase walikuwa na watu mashujaa 44,760 waliokuwa wameandaliwa kwa ajili ya vita: watu wenye nguvu, hodari wa kutumia ngao na upanga, mashujaa wa kutumia upinde, waliokuwa tayari kwa ajili ya kazi hiyo.

19 Walipigana vita dhidi ya Wahagari, Yeturi, Nafishi na Nodabu.

20 Walisaidiwa katika kupigana nao, Mungu akawatia Wahagari pamoja na wote walioungana nao mikononi mwao, kwa sababu walimlilia Mungu wakati wa vita. Alijibu maombi yao, kwa sababu walimtegemea.

21 Walitwaa mifugo ya Wahagari: ngamia 50,000, kondoo 250,000, punda 2,000. Pia wakateka watu 100,000,

22 na wengine wengi waliuawa kwa sababu vita vilikuwa ni vya Mungu. Nao waliendelea kuikalia nchi hiyo mpaka wakati wa uhamisho.

Nusu Ya Kabila La Manase

23 Idadi ya nusu ya kabila la Manase walikuwa wengi sana, Wakakaa kuanzia Bashani hadi Baal-Hermoni, yaani mpaka Seniri na mlima Hermoni.

24 Hawa ndio waliokuwa viongozi wa jamaa za kabila hilo: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia na Yahdieli. Walikuwa askari shujaa watu maarufu, viongozi wa jamaa zao.

25 Lakini hawakuwa waaminifu kwa Mungu wa baba zao, nao wakafanya ukahaba kwa miungu ya mataifa, ambayo Mungu alikuwa ameyaangamiza mbele yao.

26 Kwa hiyo Mungu wa Israeli akaiamsha roho ya Pulu, mfalme wa Ashuru (ambaye pia alijulikana kama Tiglath-Pileseri), ambaye aliwachukua Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase kwenda uhamishoni. Akawapeleka huko Hala, Habori, Hara na mto Gozani, ambako wamekaa mpaka leo.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/5-7f92016b21d1f3baee614f26c685965c.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 6

Wana Wa Lawi

1 Wana wa Lawi walikuwa:

Gershoni, Kohathi na Merari.

2 Wana wa Kohathi walikuwa:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

3 Amramu alikuwa na wana:

Aroni, Mose, na Miriamu.

Aroni alikuwa na wana:

Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

4 Eleazari akamzaa Finehasi,

Finehasi akamzaa Abishua,

5 Abishua akamzaa Buki,

Buki akamzaa Uzi,

6 Uzi akamzaa Zerahia,

Zerahia akamzaa Merayothi,

7 Merayothi akamzaa Amaria,

Amaria akamzaa Ahitubu,

8 Ahitubu akamzaa Sadoki,

Sadoki akamzaa Ahimaasi,

9 Ahimaasi akamzaa Azaria,

Azaria akamzaa Yohanani,

10 Yohanani akamzaa Azaria (ndiye alifanya kazi ya ukuhani katika Hekalu alilojenga Mfalme Solomoni huko Yerusalemu),

11 Azaria akamzaa Amaria,

Amaria akamzaa Ahitubu,

12 Ahitubu akamzaa Sadoki,

Sadoki akamzaa Shalumu,

13 Shalumu akamzaa Hilkia,

Hilkia akamzaa Azaria,

14 Azaria akamzaa Seraya,

Seraya akamzaa Yehosadaki.

15 Yehosadaki alihamishwa wakatiBwanaaliwapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Mfalme Nebukadneza.

16 Wana wa Lawi walikuwa:

Gershoni, Kohathi na Merari.

17 Haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni:

Libni na Shimei.

18 Wana wa Kohathi walikuwa:

Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.

19 Wana wa Merari walikuwa:

Mahli na Mushi.

Zifuatazo ni koo za Walawi zilizoorodheshwa kufuatana na baba zao:

20 Wazao wa Gershoni:

Gershoni akamzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi,

Yahathi akamzaa Zima,

21 Zima akamzaa Yoa,

Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera,

Zera akamzaa Yeatherai.

22 Wazao wa Kohathi:

Kohathi akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora,

Kora akamzaa Asiri,

23 Asiri akamzaa Elikana,

Elikana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri,

24 Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli,

Urieli akamzaa Uzia, Uzia akamzaa Shauli.

25 Wazao wa Elikana walikuwa:

Amasai na Ahimothi,

26 Ahimothi akamzaa Elikana, Elikana akamzaa Sofai,

Sofai akamzaa Nahathi,

27 Nahathi akamzaa Eliabu,

Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elikana,

Elikana akamzaa Samweli.

28 Wana wa Samweli walikuwa:

Yoeli mzaliwa wake wa kwanza,

na Abiya mwanawe wa pili.

29 Wafuatao ndio wazao wa Merari:

Merari akamzaa Mahli, Mahli akamzaa Libni,

Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza,

30 Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia,

Hagia akamzaa Asaya.

Waimbaji Wa Hekalu

31 Hawa ndio watu ambao Daudi aliwaweka kuwa viongozi wa uimbaji katika nyumba yaBwana, baada ya Sanduku la Agano kuletwa ili kukaa huko.

32 Walihudumu kwa kuimba mbele ya Maskani, Hema la Kukutania, mpaka hapo Mfalme Solomoni alipojenga Hekalu laBwanahuko Yerusalemu. Walitimiza wajibu wao kulingana na taratibu walizokuwa wamewekewa.

33 Wafuatao ni watu waliohudumu pamoja na wana wao:

Kutoka ukoo wa Kohathi walikuwa:

Hemani, mpiga kinanda,

alikuwa mwana wa Yoeli, mwana wa Samweli,

34 mwana wa Elikana, mwana wa Yerohamu,

mwana wa Elieli, mwana wa Toa,

35 mwana wa Sufu, mwana wa Elikana,

mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai,

36 mwana wa Elikana, mwana wa Yoeli,

mwana wa Azaria, mwana wa Sefania,

37 mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri,

mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora,

38 mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi,

mwana wa Lawi, mwana wa Israeli;

39 na msaidizi wa Hemani alikuwa Asafu, aliyesimama mkono wa kuume:

Asafu mwana wa Berekia, mwana wa Shimea,

40 mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya,

mwana wa Malkiya,

41 mwana wa Ethni,

mwana wa Zera, mwana wa Adaya,

42 mwana wa Ethani, mwana wa Zima,

mwana wa Shimei,

43 mwana wa Yahathi,

mwana wa Gershoni, mwana wa Lawi.

44 Na kutoka kwa walioshirikiana nao, Wamerari, mkono wake wa kushoto:

Ethani mwana wa Kishi, mwana wa Abdi,

mwana wa Maluki,

45 mwana wa Hashabia,

mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia,

46 mwana wa Amsi, mwana wa Bani,

mwana wa Shemeri,

47 mwana wa Mahli,

mwana wa Mushi, mwana wa Merari,

mwana wa Lawi.

48 Ndugu zao wengine Walawi walipewa huduma nyingine za kuhudumia hema takatifu, nyumba ya Mungu.

49 Lakini Aroni na uzao wake ndio waliokuwa na wajibu wa kutoa sadaka katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na kwenye madhabahu ya kufukizia uvumba pamoja na yote yaliyofanyika pa Patakatifu, wakifanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, sawasawa na yale yote aliyoagiza Mose mtumishi wa Mungu.

50 Hawa ndio waliokuwa wazao wa Aroni:

Aroni akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi,

Finehasi akamzaa Abishua,

51 Abishua akamzaa Buki,

Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Zerahia,

52 Zerahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria,

Amaria akamzaa Ahitubu,

53 Ahitubu akamzaa Sadoki,

Sadoki akamzaa Ahimaasi.

54 Zifuatazo ni sehemu walizopewa ziwe nchi yao kwa ajili ya makazi yao (walipewa wazao wa Aroni waliotoka katika ukoo wa Wakohathi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia):

55 Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda pamoja na sehemu ya malisho inayouzunguka.

56 Lakini mashamba pamoja na vijiji vilivyouzunguka mji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.

57 Kwa hiyo wazao wa Aroni walipewa miji ifuatayo pamoja na eneo la malisho: Hebroni (mji wa makimbilio), Libna, Yatiri, Eshtemoa,

58 Hileni, Debiri,

59 Ashani, Yuta na Beth-Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho.

60 Kutoka kabila la Benyamini walipewa Gibeoni, Geba, Alemethi na Anathothi, pamoja na maeneo yake ya malisho.

Miji hii kumi na mitatu iligawanywa miongoni mwa koo za Wakohathi.

61 Wazao waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za nusu ya kabila la Manase.

62 Wazao wa Gershoni, ukoo kwa ukoo, walipewa miji kumi na mitatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri na Naftali kutoka sehemu ya kabila la Manase huko Bashani.

63 Wazao wa Merari, ukoo kwa ukoo walipewa miji kumi na miwili kutoka makabila ya Reubeni, Gadi na Zabuloni.

64 Kwa hiyo Waisraeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yake ya malisho.

65 Kutoka makabila ya Yuda, Simeoni na Benyamini walipewa miji iliyotajwa hapo juu.

66 Baadhi ya koo za Wakohathi walipewa kama nchi yao miji kutoka kabila la Efraimu.

67 Katika nchi ya vilima ya Efraimu walipewa Shekemu (mji wa makimbilio) na Gezeri,

68 Yokmeamu, Beth-Horoni,

69 Aiyaloni na Gath-Rimoni, pamoja na maeneo yake ya malisho.

70 Kutoka nusu ya kabila la Manase, Waisraeli waliwapa koo za Wakohathi waliobaki miji ya Aneri na Bileamu pamoja na maeneo yake ya malisho.

71 Wagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho:

Katika nusu ya kabila la Manase:

walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.

72 Kutoka kabila la Isakari

walipokea Kedeshi, Daberathi,

73 Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho.

74 Kutoka kabila la Asheri

walipokea Mashali, Abdoni,

75 Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho.

76 Kutoka kabila la Naftali

walipokea Kedeshi katika Galilaya, Hamoni na Kiriathaimu pamoja na maeneo yake ya malisho.

77 Wamerari (Walawi waliobakia) walipokea miji ifuatayo:

kutoka kabila la Zabuloni

walipokea Yokneamu, Karta, Rimoni na Tabori pamoja na maeneo yake ya malisho.

78 Kutoka kabila la Reubeni, ngʼambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko

walipokea Bezeri ulioko jangwani, Yahasa,

79 Kedemothi na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.

80 Na kutoka kabila la Gadi

walipokea Ramothi huko Gileadi, Mahanaimu,

81 Heshboni na Yazeri, pamoja na maeneo yake ya malisho.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/6-be4a48d34bb471def64fcf4a8a0a6e97.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 7

Wana Wa Isakari

1 Wana wa Isakari walikuwa:

Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne.

2 Wana wa Tola walikuwa:

Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600.

3 Mwana wa Uzi alikuwa:

Izrahia.

Wana wa Izrahia walikuwa:

Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao.

4 Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu hodari wa vita wapatao 36,000, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi.

5 Jamaa ya watu waliokuwa wapiganaji hodari kutoka koo zote za Isakari, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, jumla yao walikuwa 87,000.

Wana Wa Benyamini

6 Wana watatu wa Benyamini walikuwa:

Bela, Bekeri na Yediaeli.

7 Wana wa Bela walikuwa:

Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Watu wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa 22,034.

8 Wana wa Bekeri walikuwa:

Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elioenai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri.

9 Orodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji 20,200.

10 Mwana wa Yediaeli alikuwa:

Bilhani.

Wana wa Bilhani walikuwa:

Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari.

11 Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwako wanaume wapiganaji 17,200 waliokuwa tayari kwenda vitani.

12 Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri.

Wana Wa Naftali

13 Wana wa Naftali walikuwa:

Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha.

Wana Wa Manase

14 Wana wa Manase walikuwa:

Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake wa Kiaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi.

15 Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake aliitwa Maaka.

Mwana wa pili wa Makiri aliitwa Selofehadi, ambaye alikuwa na wasichana tu.

16 Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu.

17 Mwana wa Ulamu alikuwa:

Bedani.

Hawa ndio waliokuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase.

18 Dada yake aliyeitwa Hamolekethi aliwazaa Ish-Hodi, Abiezeri na Mahla.

19 Wana wa Shemida walikuwa:

Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu.

Wana Wa Efraimu

20 Wana wa Efraimu walikuwa:

Shuthela, ambaye alimzaa Beredi,

Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada,

Eleada akamzaa Tahathi,

21 Tahathi akamzaa Zabadi,

na Zabadi akamzaa Shuthela.

Ezeri na Eleadi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wamekwenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao.

22 Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji.

23 Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake.

24 Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera.

25 Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu,

Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani,

26 Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi,

Amihudi akamzaa Elishama,

27 Elishama akamzaa Nuni,

Nuni akamzaa Yoshua.

28 Nchi zao na makazi yao yalijumuisha Betheli na vijiji vilivyouzunguka, Naarani ilikuwa upande wa mashariki, Gezeri pamoja na vijiji vyake upande wa magharibi, pia Shekemu na vijiji vyake hadi kufikia Aya na vijiji vyake.

29 Katika mipaka ya Manase walikuwepo Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wana wa Yosefu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii.

Wana Wa Asheri

30 Wana wa Asheri walikuwa:

Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera.

31 Wana wa Beria walikuwa:

Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.

32 Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao.

33 Wana wa Yafleti walikuwa:

Pasaki, Bimhali na Ashvathi.

Hawa walikuwa wana wa Yafleti.

34 Wana wa Shemeri walikuwa:

Ahi, Roga, Yehuba na Aramu.

35 Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa:

Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.

36 Wana wa Sofa walikuwa:

Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra,

37 Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithranina Beera.

38 Wana wa Yetheri walikuwa:

Yefune, Pispa na Ara.

39 Wana wa Ula walikuwa:

Ara, Hanieli na Risia.

40 Hawa wote ndio waliokuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa walio hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa tayari kwa vita, kama ilivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa 26,000.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/7-a955d51240c25438619d34e26d9a6df2.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 8

Ukoo Wa Sauli Mbenyamini

1 Benyamini akamzaa: Bela mzaliwa wake wa kwanza,

Ashbeli mwanawe wa pili, Ahara mwanawe wa tatu,

2 Noha mwanawe wa nne na Rafa mwanawe wa tano.

3 Wana wa Bela walikuwa:

Adari, Gera, Abihudi,

4 Abishua, Naamani, Ahoa,

5 Gera, Shefufani na Huramu.

6 Hawa ndio wazao wa Ehudi, waliokuwa viongozi wa jamaa za wale walioishi huko Geba na ambao walihamishiwa Manahathi:

7 Naamani, Ahiya na Gera. Gera alikuwa baba yao Uza na Ahihudi na ndiye aliwaongoza kwenda uhamishoni.

8 Shaharaimu aliwazaa wana katika nchi ya Moabu baada ya kuwapa talaka wake zake wawili yaani, Hushimu na Baara.

9 Kwa mkewe Hodeshi, akawazaa wana saba: Yobabu, Sibia, Mesha, Malkamu,

10 Yeuzi, Sakia na Mirma. Hawa ndio waliokuwa wanawe, viongozi wa jamaa zao.

11 Hushimu alimzalia: Abitubu na Elpaali.

12 Wana wa Elpaali walikuwa:

Eberi, Mishamu, Shemedi (aliyeijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji vilivyoizunguka),

13 na Beria na Shema, waliokuwa viongozi wa zile jamaa zilizokuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na ambao waliwafukuza wenyeji wa Gathi.

14 Wana wa Beria walikuwa Ahio, Shashaki, Yeremothi,

15 Zebadia, Aradi, Ederi,

16 Mikaeli, Ishpa, na Yoha.

17 Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi,

18 Ishmerai, Izlia na Yobabu ndio waliokuwa wana wa Elpaali.

19 Yakimu, Zikri, Zabdi,

20 Elienai, Silethai, Elieli,

21 Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wana wa Shimei.

22 Wana wa Shashaki walikuwa Ishpani, Eberi, Elieli,

23 Abdoni, Zikri, Hanani,

24 Hanania, Elamu, Anthothiya,

25 Ifdeya na Penueli.

26 Shamsherai, Sheharia, Athalia,

27 Yaareshia, Eliya na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.

28 Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao wakuu, kama ilivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.

29 Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni.

Mke wake aliitwa Maaka.

30 Mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu,

31 Gedori, Ahio, Zekeri,

32 na Miklothi ambaye alikuwa baba yake Shimea. Hawa pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.

33 Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli, Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.

34 Yonathani akamzaa:

Merib-Baali,naye Merib-Baali akamzaa Mika.

35 Wana wa Mika walikuwa:

Pithoni, Meleki, Tarea na Ahazi.

36 Ahazi akamzaa Yehoada. Naye Yehoada akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa.

37 Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Rafa, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli.

38 Aseli alikuwa na wana sita; haya ndiyo majina yao:

Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa wote ndio waliokuwa wana wa Aseli.

39 Wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa:

Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti.

40 Wana wa Ulamu walikuwa mashujaa hodari walioweza kutumia upinde. Alikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla yao 150.

Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Benyamini.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/8-8fac8885233ff6a0f615f14f44815b0d.mp3?version_id=1627—

Categories
1 Nyakati

1 Nyakati 9

1 Waisraeli wote waliorodheshwa katika koo zilizoandikwa kwenye kitabu cha wafalme wa Israeli.

Watu Katika Yerusalemu

Watu wa Yuda walichukuliwa mateka kwenda Babeli kwa sababu ya kukosa uaminifu kwa Mungu.

2 Basi watu wa kwanza kurudi kukaa kwenye milki zao katika miji yao walikuwa baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi na watumishi wa Hekalu.

3 Wale waliotoka Yuda, Benyamini, Efraimu na Manase ambao waliishi Yerusalemu walikuwa:

Jamaa Za Yuda

4 Uthai mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imri, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda.

5 Wazao wa Washiloni waliorudi ni:

Asaya mzaliwa wa kwanza na wanawe.

6 Kwa wana wa Zera:

Yeueli.

Watu wa Yuda jumla yao walikuwa watu 690.

Jamaa Za Benyamini

7 Kwa Benyamini walikuwa:

Salu mwana wa Meshulamu, mwana wa Hodavia, mwana wa Hasenua;

8 Ibneya mwana wa Yerohamu, Ela mwana wa Uzi, mwana wa Mikri; na Meshulamu mwana wa Shefatia, mwana wa Reueli, mwana wa Ibniya.

9 Watu kutoka Benyamini kama walivyoorodheshwa katika koo zao jumla yao ni 956. Watu hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa zao.

Jamaa Za Makuhani

10 Wa jamaa za makuhani walikuwa:

Yedaya, Yehoyaribu na Yakini;

11 Azaria mwana wa Hilkia, mwana wa Meshulamu, mwana wa Sadoki, mwana wa Merayothi, mwana wa Ahitubu aliyekuwa afisa kiongozi wa nyumba ya Mungu.

12 Adaya mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya; Maasai, mwana wa Adieli, mwana wa Yahzera, mwana wa Meshulamu, mwana wa Meshilemithi, mwana wa Imeri.

13 Makuhani waliokuwa viongozi wa jamaa zao walikuwa 1,760. Walikuwa watu wenye uwezo, waliowajibika kuhudumu katika nyumba ya Mungu.

Jamaa Za Walawi

14 Jamaa za Walawi walikuwa:

Shemaya, mwana wa Hashubu, mwana wa Azrikamu, mwana wa Hashabia, wa wana wa Merari.

15 Bakbakari, Hereshi, Galali na Matania mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu.

16 Obadia mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni. Berekia mwana wa Asa, mwana wa Elikana, ambao waliishi katika vijiji vya Wanetofathi.

Jamaa Za Mabawabu

17 Mabawabu katika Hekalu laBwanawaliorudi walikuwa:

Shalumu, Akubu, Talmoni, Ahimani na ndugu zao. Shalumu alikuwa mlinzi wao mkuu.

18 Walikuwa wamewekwa katika lango la mfalme lililokuwa upande wa mashariki, mpaka wakati huu. Hawa walikuwa mabawabu wa kutoka kwenye kambi ya Walawi.

19 Shalumu mwana wa Kore, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, pamoja na mabawabu wenzake kutoka jamaa yake ya Kora waliwajibika kulinda malango ya Hema, kama vile baba zao walivyokuwa wamewajibika kulinda ingilio la Maskani yaBwana.

20 Hapo zamani Finehasi mwana wa Eleazari alikuwa kiongozi wa mabawabu, nayeBwanaalikuwa pamoja naye:

21 Zekaria mwana wa Meshelemia alikuwa bawabu katika ingilio la Hema la Kukutania.

22 Jumla ya waliochaguliwa kuwa mabawabu katika sakafu za kupuria nafaka walikuwa watu 212. Waliandikishwa kwa koo zao kwenye vijiji vyao. Mabawabu hawa waliwekwa katika nafasi zao za kuaminiwa na Daudi pamoja na mwonaji Samweli.

23 Wao na wazao wao walikuwa viongozi wa kulinda malango ya nyumba yaBwana, nyumba iliyoitwa Hema.

24 Mabawabu walikuwa pande zote nne: mashariki, magharibi, kaskazini na kusini.

25 Ndugu zao katika vijiji vyao walikuwa wakija mara kwa mara na kuwasaidia katika kazi zao kwa vipindi mbalimbali vya siku saba.

26 Lakini mabawabu wanne wakuu, waliokuwa Walawi, walikabidhiwa wajibu kwa ajili ya vyumba na hazina katika nyumba ya Mungu.

27 Walikesha mahali walipowekwa kuizunguka nyumba ya Mungu, kwa sababu iliwapasa kuilinda. Pia walitunza funguo kwa ajili ya kufungua mlango kila siku asubuhi.

28 Baadhi yao walikuwa viongozi wa kutunza vifaa vilivyotumika katika huduma ndani ya Hekalu; walivihesabu kila vilipoingizwa ndani na kila vilipotolewa.

29 Wengine walipangiwa kutunza mapambo na vifaa vingine vya patakatifu, pamoja na unga, divai, mafuta, uvumba na vikolezo.

30 Lakini baadhi ya makuhani walifanya kazi ya kuchanganya vikolezo.

31 Mlawi aliyeitwa Matithia, mwana mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, wa ukoo wa Kora, alikabidhiwa wajibu kwa ajili ya kuoka mikate ya sadaka.

32 Baadhi ya ndugu zao wa ukoo wa Kohathi walikuwa viongozi wa kuandaa mikate ya Wonyesho kwa ajili ya kila Sabato, mikate iliyokuwa inawekwa mezani.

33 Wale waliokuwa waimbaji, viongozi wa jamaa za Walawi, waliishi katika vyumba vya Hekalu, nao hawakufanya shughuli nyingine yoyote kwa sababu iliwapasa kuwajibika kwa kazi hiyo usiku na mchana.

34 Hawa wote walikuwa viongozi wa jamaa za Walawi, wakuu kama walivyoorodheshwa katika koo zao, nao waliishi Yerusalemu.

Ukoo Wa Sauli

35 Yeieli alikuwa baba yake Gibeoni naye aliishi huko Gibeoni. Mke wake aliitwa Maaka,

36 mwanawe mzaliwa wa kwanza alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Suri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu,

37 Gedori, Ahio, Zekaria na Miklothi.

38 Miklothi akamzaa Shimeamu. Wao pia waliishi karibu na jamaa zao huko Yerusalemu.

39 Neri akamzaa Kishi, Kishi akamzaa Sauli. Sauli akamzaa Yonathani, Malki-Shua, Abinadabu na Esh-Baali.

40 Yonathani akamzaa Merib-Baali,

naye Merib-Baali akamzaa Mika.

41 Wana wa Mika walikuwa:

Pithoni, Meleki, Tarea, na Ahazi.

42 Ahazi akamzaa Yara, Yara akawazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri, naye Zimri akamzaa Mosa.

43 Mosa akamzaa Binea, Binea akamzaa Refaya, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli.

44 Aseli alikuwa na wana sita, na haya ndiyo majina yao:

Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Hawa ndio waliokuwa wana wa Aseli.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/1CH/9-23730e5a91ce4fd7639fa341ab386d04.mp3?version_id=1627—