Categories
Zaburi

Zaburi 94

Mungu Mlipiza Kisasi Kwa Ajili Ya Wenye Haki

1 EeBwana, ulipizaye kisasi,

Ee Mungu ulipizaye kisasi, uangaze sasa.

2 Ee Mhukumu wa dunia, inuka,

uwalipize wenye kiburi kama wanavyostahili.

3 Hata lini, waovu, EeBwana,

hata lini waovu watashangilia?

4 Wanamimina maneno ya kiburi,

watenda mabaya wote wamejaa majivuno.

5 EeBwana, wanawaponda watu wako,

wanawaonea urithi wako.

6 Wanamchinja mjane na mgeni,

na kuwaua yatima.

7 Nao husema, “Bwanahaoni,

Mungu wa Yakobo hafahamu.”

8 Sikizeni, enyi wajinga miongoni mwa watu;

enyi wapumbavu, lini mtakuwa na hekima?

9 Je, aliyeweka sikio asisikie?

Aliyeumba jicho asione?

10 Je, anayeadhibisha mataifa asiadhibu?

Je, awafundishaye wanadamu asiwe na maarifa?

11 Bwanaanajua mawazo ya mwanadamu;

anajua kwamba ni ubatili.

12 EeBwana, heri mtu anayeadhibishwa na wewe,

mtu unayemfundisha kwa sheria yako,

13 unampa utulivu siku za shida,

mpaka shimo litakapokuwa limechimbwa

kwa ajili ya mwovu.

14 Kwa kuwaBwanahatawakataa watu wake,

hatauacha urithi wake.

15 Hukumu itasimamishwa tena kwenye haki,

wote walio na mioyo minyofu wataifuata.

16 Ni nani atakayeinuka dhidi ya mwovu kwa ajili yangu?

Ni nani atakayenikinga dhidi ya watenda maovu?

17 KamaBwanaasingelinisaidia upesi,

ningelikuwa ninaishi katika ukimya wa kifo.

18 Niliposema, “Mguu wangu unateleza,”

EeBwana, upendo wako ulinishikilia.

19 Wakati wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu,

faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu.

20 Je, kiti cha utawala wa udhalimu kitajiunga nawe,

ule utawala uletao taabu kutokana na sheria zake?

21 Huungana kuwashambulia wenye haki,

kuwahukumu kufa wasio na hatia.

22 LakiniBwanaamekuwa ngome yangu,

na Mungu wangu amekuwa mwamba ninaoukimbilia.

23 Yeye atawalipa kwa ajili ya dhambi zao

na atawaangamiza kwa ajili ya maovu yao;

BwanaMungu wetu atawaangamiza.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/94-46bff0cdadad6fa6cc848420a248fdf9.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 95

Wimbo Wa Kumsifu Mungu

1 Njooni, tumwimbieBwanakwa furaha;

tumfanyie kelele za shangwe

Mwamba wa wokovu wetu.

2 Tuje mbele zake kwa shukrani,

tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.

3 Kwa kuwaBwanani Mungu mkuu,

mfalme mkuu juu ya miungu yote.

4 Mkononi mwake mna vilindi vya dunia,

na vilele vya milima ni mali yake.

5 Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya,

na mikono yake iliumba nchi kavu.

6 Njooni, tusujudu, tumwabudu,

tupige magoti mbele zaBwanaMuumba wetu,

7 kwa maana yeye ndiye Mungu wetu,

na sisi ni watu wa malisho yake,

kondoo chini ya utunzaji wake.

Kama mkiisikia sauti yake leo,

8 msiifanye mioyo yenu migumu

kama mlivyofanya kule Meriba,

kama mlivyofanya siku ile

kule Masajangwani,

9 ambapo baba zenu walinijaribu na kunipima,

ingawa walikuwa wameyaona matendo yangu.

10 Kwa miaka arobaini nilikasirikia kizazi kile,

nikasema, “Hawa ni taifa ambalo mioyo yao imepotoka,

nao hawajazijua njia zangu.”

11 Hivyo nikatangaza kwa kiapo katika hasira yangu,

“Kamwe hawataingia rahani mwangu.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/95-8b88b1c01eacb1139a02594f1d7bf3b8.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 96

Mungu Mfalme Mkuu

1 MwimbieniBwanawimbo mpya;

mwimbieniBwanadunia yote.

2 MwimbieniBwana, lisifuni jina lake;

tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.

3 Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,

matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.

4 Kwa kuwaBwanani mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote;

yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.

5 Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,

lakiniBwanaaliziumba mbingu.

6 Fahari na enzi viko mbele yake;

nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.

7 MpeniBwana, enyi jamaa za mataifa,

mpeniBwanautukufu na nguvu.

8 MpeniBwanautukufu unaostahili jina lake;

leteni sadaka na mje katika nyua zake.

9 MwabuduniBwanakatika uzuri wa utakatifu wake;

dunia yote na itetemeke mbele zake.

10 Katikati ya mataifa semeni, “Bwanaanatawala.”

Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa;

atawahukumu watu kwa uadilifu.

11 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;

bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;

12 mashamba na yashangilie,

pamoja na vyote vilivyomo ndani yake.

Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha;

13 itaimba mbele zaBwanakwa maana anakuja,

anakuja kuihukumu dunia.

Ataihukumu dunia kwa haki,

na mataifa katika kweli yake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/96-a54c28136746e51ea86d1c4f8707af2d.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 97

Mungu Mtawala Mkuu

1 Bwanaanatawala, nchi na ifurahi,

visiwa vyote vishangilie.

2 Mawingu na giza nene vinamzunguka,

haki na hukumu ndio msingi wa kiti chake cha enzi.

3 Moto hutangulia mbele zake

na huteketeza adui zake pande zote.

4 Umeme wake wa radi humulika dunia,

nchi huona na kutetemeka.

5 Milima huyeyuka kama nta mbele zaBwana,

mbele za Bwana wa dunia yote.

6 Mbingu zinatangaza haki yake,

na mataifa yote huona utukufu wake.

7 Wote waabuduo sanamu waaibishwa,

wale wajisifiao sanamu:

mwabuduni yeye, enyi miungu yote!

8 Sayuni husikia na kushangilia,

vijiji vya Yuda vinafurahi

kwa sababu ya hukumu zako, EeBwana.

9 Kwa kuwa wewe, EeBwana, ndiwe Uliye Juu Sana kuliko dunia yote;

umetukuka sana juu ya miungu yote.

10 Wale wanaompendaBwanana wauchukie uovu,

kwa maana yeye hulinda maisha ya waaminifu wake

na kuwaokoa kutoka mkononi mwa mwovu.

11 Nuru huangaza wenye haki

na furaha kwa watu wanyofu wa moyo.

12 Furahini katikaBwana, ninyi mlio wenye haki,

lisifuni jina lake takatifu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/97-31c80bbda1a8cd4bd7bfb2719c9c1c1c.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 98

Mungu Mtawala Wa Dunia

Zaburi.

1 MwimbieniBwanawimbo mpya,

kwa maana ametenda mambo ya ajabu;

kitanga chake cha kuume na mkono wake mtakatifu

umemfanyia wokovu.

2 Bwanaameufanya wokovu wake ujulikane

na amedhihirisha haki yake kwa mataifa.

3 Ameukumbuka upendo wake

na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli;

miisho yote ya dunia imeuona

wokovu wa Mungu wetu.

4 MpigieniBwanakelele za shangwe, dunia yote,

ipaze sauti kwa nyimbo za shangwe na vinanda;

5 mwimbieniBwanakwa kinubi,

kwa kinubi na sauti za kuimba,

6 kwa tarumbeta na mvumo wa baragumu za pembe za kondoo dume:

shangilieni kwa furaha mbele zaBwana, aliye Mfalme.

7 Bahari na ivume na kila kiliomo ndani yake,

dunia na wote wakaao ndani yake.

8 Mito na ipige makofi,

milima na iimbe pamoja kwa furaha,

9 vyote na viimbe mbele zaBwana,

kwa maana yuaja kuhukumu dunia.

Atahukumu dunia kwa haki

na mataifa kwa haki.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/98-7163a39f7828c4519ba46a2a4ee3a38a.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 99

Mungu Mfalme Mkuu

1 Bwanaanatawala,

mataifa na yatetemeke;

anakalia kiti cha enzi katikati ya makerubi,

dunia na itikisike.

2 Bwanani mkuu katika Sayuni;

ametukuzwa juu ya mataifa yote.

3 Wanalisifu jina lako ambalo ni kuu na la kuogopwa:

yeye ni mtakatifu!

4 Mfalme ni mwenye nguvu na hupenda haki,

wewe umethibitisha adili;

katika Yakobo umefanya

yaliyo haki na sawa.

5 MtukuzeniBwanaMungu wetu,

na mkaabudu katika mahali pa kuwekea miguu yake;

yeye ni mtakatifu.

6 Mose na Aroni walikuwa miongoni mwa makuhani wake,

Samweli alikuwa miongoni mwa walioliitia jina lake;

walimwitaBwana,

naye aliwajibu.

7 Alizungumza nao kutoka nguzo ya wingu;

walizishika sheria zake na amri alizowapa.

8 EeBwana, wetu,

ndiwe uliyewajibu,

kwa Israeli ulikuwa Mungu mwenye kusamehe,

ingawa uliadhibu matendo yao mabaya.

9 MtukuzeniBwanaMungu wetu,

mwabuduni kwenye mlima wake mtakatifu,

kwa maanaBwanaMungu wetu ni mtakatifu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/99-11d9d4ae955a940aed5492da831339ad.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 100

Dunia Yote Yaitwa Kumsifu Mungu

Zaburi ya shukrani.

1 MpigieniBwanakelele za shangwe, dunia yote.

2 MwabuduniBwanakwa furaha;

njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.

3 Jueni kwambaBwanandiye Mungu.

Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;

sisi tu watu wake,

kondoo wa malisho yake.

4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani

na katika nyua zake kwa kusifu,

mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.

5 Kwa maanaBwanani mwema

na upendo wake wadumu milele;

uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/100-eff14a40452cabadf74ec057d9d8d961.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 101

Ahadi Ya Kuishi Kwa Uadilifu Na Kwa Haki

Zaburi ya Daudi.

1 Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako;

kwako wewe, EeBwana, nitaimba sifa.

2 Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama:

utakuja kwangu lini?

Nitatembea nyumbani mwangu

kwa moyo usio na lawama.

3 Sitaweka mbele ya macho yangu

kitu kiovu.

Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani;

hawatashikamana nami.

4 Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami;

nitajitenga na kila ubaya.

5 Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri,

huyo nitamnyamazisha;

mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi

huyo sitamvumilia.

6 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,

ili waweze kuishi pamoja nami;

yeye ambaye moyo wake hauna lawama

atanitumikia.

7 Mdanganyifu hatakaa

nyumbani mwangu,

yeye asemaye kwa uongo

hatasimama mbele yangu.

8 Kila asubuhi nitawanyamazisha

waovu wote katika nchi;

nitamkatilia mbali kila mtenda mabaya

kutoka mji waBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/101-94c837dab923fee4400aad2840d4c3c4.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 102

Maombi Ya Mtu Mwenye Taabu

Maombi ya mtu aliyechoka. Anapoteseka na kumimina malalamiko yake kwa

Bwana

.

1 EeBwana, usikie maombi yangu,

kilio changu cha kuomba msaada kikufikie.

2 Usinifiche uso wako

ninapokuwa katika shida.

Unitegee sikio lako,

ninapoita, unijibu kwa upesi.

3 Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi,

mifupa yangu inaungua kama kaa la moto.

4 Moyo wangu umefifia na kunyauka kama jani,

ninasahau kula chakula changu.

5 Kwa sababu ya kusononeka kwangu kwa uchungu,

nimebakia ngozi na mifupa.

6 Nimekuwa kama bundi wa jangwani,

kama bundi kwenye magofu.

7 Nilalapo sipati usingizi,

nimekuwa kama ndege mpweke

kwenye paa la nyumba.

8 Mchana kutwa adui zangu hunidhihaki,

wale wanaonizunguka hutumia jina langu kama laana.

9 Ninakula majivu kama chakula changu

na nimechanganya kinywaji changu na machozi

10 kwa sababu ya ghadhabu yako kuu,

kwa maana umeniinua na kunitupa kando.

11 Siku zangu ni kama kivuli cha jioni,

ninanyauka kama jani.

12 Lakini wewe, EeBwana, umeketi katika kiti chako cha enzi milele,

sifa zako za ukuu zaendelea vizazi vyote.

13 Utainuka na kuihurumia Sayuni,

kwa maana ni wakati wa kumwonyesha wema;

wakati uliokubalika umewadia.

14 Kwa maana mawe yake ni ya thamani kwa watumishi wako,

vumbi lake lenyewe hulionea huruma.

15 Mataifa wataogopa jina laBwana,

wafalme wote wa dunia watauheshimu utukufu wako.

16 Kwa maanaBwanaataijenga tena Sayuni

na kutokea katika utukufu wake.

17 Ataitikia maombi ya mtu mkiwa,

wala hatadharau hoja yao.

18 Hili na liandikwe kwa ajili ya kizazi kijacho,

ili taifa litakaloumbwa baadaye waweze kumsifuBwana:

19 “Bwanaalitazama chini kutoka patakatifu pake palipo juu,

kutoka mbinguni alitazama dunia,

20 kusikiliza vilio vya uchungu vya wafungwa

na kuwaweka huru wale waliohukumiwa kufa.”

21 Kwa hiyo jina laBwanalatangazwa huko Sayuni

na sifa zake katika Yerusalemu,

22 wakati mataifa na falme zitakapokusanyika

ili kumwabuduBwana.

23 Katika kuishi kwangu alivunja nguvu zangu,

akafupisha siku zangu.

24 Ndipo niliposema:

“Ee Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu;

miaka yako inaendelea vizazi vyote.

25 Hapo mwanzo uliweka misingi ya dunia,

nazo mbingu ni kazi ya mikono yako.

26 Hizi zitatoweka, lakini wewe utadumu,

zote zitachakaa kama vazi.

Utazibadilisha kama nguo

nazo zitaondoshwa.

27 Lakini wewe, U yeye yule,

nayo miaka yako haikomi kamwe.

28 Watoto wa watumishi wako wataishi mbele zako;

wazao wao wataimarishwa mbele zako.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/102-dc2ab09e05dc7cba3ad9c246c7c4d214.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 103

Upendo Wa Mungu

Zaburi ya Daudi.

1 Ee nafsi yangu, umhimidiBwana.

Vyote vilivyomo ndani yangu

vilihimidi jina lake takatifu.

2 Ee nafsi yangu, umhimidiBwana,

wala usisahau wema wake wote,

3 akusamehe dhambi zako zote,

akuponya magonjwa yako yote,

4 aukomboa uhai wako na kaburi,

akuvika taji ya upendo na huruma,

5 atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema,

ili ujana wako uhuishwe kama wa tai.

6 Bwanahutenda haki,

naye huwapa hukumu ya haki wote wanaoonewa.

7 Alijulisha Mose njia zake,

na wana wa Israeli matendo yake.

8 Bwanani mwingi wa huruma na mwenye neema;

si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.

9 Yeye hatalaumu siku zote,

wala haweki hasira yake milele,

10 yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu

wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.

11 Kama vile mbingu zilivyo juu ya dunia sana,

ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha;

12 kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,

ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.

13 Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake,

ndivyoBwanaanavyowahurumia wale wanaomcha;

14 kwa kuwa anajua tulivyoumbwa,

anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi.

15 Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani,

anachanua kama ua la shambani;

16 upepo huvuma juu yake nalo hutoweka,

mahali pake hapalikumbuki tena.

17 Lakini kutoka milele hata milele

upendo waBwanauko kwa wale wamchao,

nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:

18 kwa wale walishikao agano lake

na kukumbuka kuyatii mausia yake.

19 Bwanaameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni,

ufalme wake unatawala juu ya vyote.

20 MhimidiniBwana, enyi malaika zake,

ninyi mlio mashujaa mnaozitii amri zake,

ninyi mnaotii neno lake.

21 MhimidiniBwana, ninyi jeshi lake lote la mbinguni,

ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake.

22 MhimidiniBwana, kazi zake zote

kila mahali katika milki yake.

Ee nafsi yangu, umhimidiBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/103-27ce97ceb3011e92f6a21ca1ee3d567b.mp3?version_id=1627—