Categories
Zaburi

Zaburi 74

Maombi Kwa Ajili Ya Taifa Kuokolewa

Utenzi wa Asafu.

1 Ee Mungu, mbona umetukataa milele?

Mbona hasira yako inatoka moshi

juu ya kondoo wa malisho yako?

2 Kumbuka watu uliowanunua zamani,

kabila la urithi wako, ambao uliwakomboa:

Mlima Sayuni, ambamo uliishi.

3 Geuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu,

uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu.

4 Adui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi,

wanaweka bendera zao kama alama.

5 Walifanya kama watu wanaotumia mashoka

kukata kichaka cha miti.

6 Walivunjavunja milango yote iliyonakshiwa

kwa mashoka na vishoka vyao.

7 Waliteketeza kabisa mahali pako patakatifu,

wakayanajisi makao ya Jina lako.

8 Walisema mioyoni mwao,

“Tutawaponda kabisa!”

Walichoma kila mahali ambapo Mungu

aliabudiwa katika nchi.

9 Hatukupewa ishara za miujiza;

hakuna manabii waliobaki,

hakuna yeyote kati yetu ajuaye

hali hii itachukua muda gani.

10 Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini?

Je, adui watalitukana jina lako milele?

11 Kwa nini unazuia mkono wako,

mkono wako wa kuume?

Uutoe kutoka makunjo ya vazi lako

na uwaangamize!

12 Lakini wewe, Ee Mungu, ni mfalme wangu tangu zamani,

unaleta wokovu duniani.

13 Ni wewe uliyeigawanya bahari kwa uweza wako;

ulivunja vichwa vya wanyama wakubwa wa kutisha katika maji.

14 Ni wewe uliyeponda vichwa vya Lewiathani

nawe ukamtoa kama chakula

kwa viumbe vya jangwani.

15 Ni wewe uliyefungua chemchemi na vijito,

ulikausha mito ambayo ilikuwa ikitiririka daima.

16 Mchana ni wako, nao usiku ni wako pia,

uliziweka jua na mwezi.

17 Ni wewe uliyeiweka mipaka yote ya dunia,

ulifanya kiangazi na masika.

18 EeBwana, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki,

jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako.

19 Usiukabidhi uhai wa njiwa wako kwa wanyama wakali wa mwitu;

usisahau kabisa uhai wa watu wako wanaoteseka milele.

20 Likumbuke agano lako,

maana mara kwa mara mambo ya jeuri

yamejaa katika sehemu za giza nchini.

21 Usiruhusu walioonewa warudi nyuma kwa aibu;

maskini na wahitaji hebu walisifu jina lako.

22 Inuka, Ee Mungu, ujitetee;

kumbuka jinsi wapumbavu

wanavyokudhihaki mchana kutwa.

23 Usipuuze makelele ya watesi wako,

ghasia za adui zako, zinazoinuka mfululizo.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/74-ecd31c4f04e9b5de7d636b79495e0199.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 75

Mungu Ni Mwamuzi

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Zaburi ya Asafu. Wimbo.

1 Ee Mungu, tunakushukuru,

tunakushukuru wewe,

kwa kuwa jina lako li karibu;

watu husimulia matendo yako ya ajabu.

2 Unasema, “Ninachagua wakati maalum;

ni mimi nihukumuye kwa haki.

3 Wakati dunia na watu wake wote inapotetemeka,

ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.

4 Kwa wale wenye majivuno ninasema,

‘Msijisifu tena,’

kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.

5 Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu;

msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ”

6 Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi

au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.

7 Bali Mungu ndiye ahukumuye:

Humshusha huyu na kumkweza mwingine.

8 Mkononi mwaBwanakuna kikombe

kilichojaa mvinyo unaotoka povu

uliochanganywa na vikolezo;

huumimina, nao waovu wote wa dunia

hunywa mpaka tone la mwisho.

9 Bali mimi, nitatangaza hili milele;

nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.

10 Nitazikatilia mbali pembe za waovu wote,

bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/75-7aff16755558c333f90a5afc2d18b118.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 76

Mungu Wa Israeli Ni Mhukumu Wa Dunia Yote

Kwa mwimbishaji. Kwa ala za nyuzi za muziki. Zaburi ya Asafu. Wimbo.

1 Katika Yuda, Mungu anajulikana,

jina lake ni kuu katika Israeli.

2 Hema lake liko Salemu,

makao yake katika Sayuni.

3 Huko alivunja mishale imetametayo,

ngao na panga, silaha za vita.

4 Wewe unangʼaa kwa mwanga,

mwenye fahari zaidi ya milima yenye utajiri wa wanyama pori.

5 Mashujaa hulala wametekwa nyara,

hulala usingizi wao wa mwisho;

hakuna hata mmoja wa watu wa vita

anayeweza kuinua mikono yake.

6 Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo,

farasi na gari la vita vilikaa kimya.

7 Wewe peke yako ndiye wa kuogopwa.

Ni nani awezaye kusimama mbele yako unapokasirika?

8 Kutoka mbinguni ulitamka hukumu,

nayo nchi ikaogopa, ikawa kimya:

9 wakati wewe, Ee Mungu, ulipoinuka kuhukumu,

kuwaokoa wote walioonewa katika nchi.

10 Hakika ghadhabu yako dhidi ya wanadamu inakuletea sifa,

na masalia ya ghadhabu yako unajifunga mshipi.

11 Wekeni nadhiri kwaBwanaMungu wenu na kuzitimiza;

nchi zote za jirani na walete zawadi

kwa Yule astahiliye kuogopwa.

12 Huvunja roho za watawala;

anaogopwa na wafalme wa dunia.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/76-0310f348750f1c41b2c81d2903b2e953.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 77

Matendo Makuu Ya Mungu Yanakumbukwa

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Asafu.

1 Nilimlilia Mungu ili anisaidie,

nilimlilia Mungu ili anisikie.

2 Nilipokuwa katika taabu, nilimtafuta Bwana,

usiku nilinyoosha mikono bila kuchoka

na nafsi yangu ilikataa kufarijika.

3 Ee Mungu, nilikukumbuka wewe, nikalia kwa huzuni;

nikatafakari, roho yangu ikadhoofika.

4 Ulizuia macho yangu kufumba;

nilikuwa nasumbuka, nikashindwa kusema.

5 Nilitafakari juu ya siku zilizopita,

miaka mingi iliyopita,

6 nilikumbuka nilivyoimba nyimbo usiku.

Moyo wangu ulitafakari

na roho yangu ikauliza:

7 “Je, Bwana atakataa milele?

Je, hatatenda mema tena?

8 Je, upendo wake usio na mwisho umetoweka milele?

Je, ahadi yake imekoma nyakati zote?

9 Je, Mungu amesahau kuwa na huruma?

Je, katika hasira amezuia huruma yake?”

10 Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu:

lakini nitakumbuka

miaka ya mkono wa kuume

wa Aliye Juu Sana.”

11 Nitayakumbuka matendo yaBwana;

naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani.

12 Nitazitafakari kazi zako zote

na kuyawaza matendo yako makuu.

13 Ee Mungu, njia zako ni takatifu.

Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu?

14 Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza,

umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa.

15 Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako,

uzao wa Yakobo na Yosefu.

16 Maji yalikuona, Ee Mungu,

maji yalikuona yakakimbia,

vilindi vilitetemeka.

17 Mawingu yalimwaga maji,

mbingu zikatoa ngurumo kwa radi,

mishale yako ikametameta huku na huko.

18 Ngurumo yako ilisikika katika upepo wa kisulisuli,

umeme wako wa radi ukaangaza dunia,

nchi ikatetemeka na kutikisika.

19 Njia yako ilipita baharini,

mapito yako kwenye maji makuu,

ingawa nyayo zako hazikuonekana.

20 Uliongoza watu wako kama kundi

kwa mkono wa Mose na Aroni.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/77-92567aad6c2595bb9449a6d396229bf2.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 78

Mungu Na Watu Wake

Utenzi wa Asafu.

1 Enyi watu wangu, sikieni mafundisho yangu,

sikilizeni maneno ya kinywa changu.

2 Nitafungua kinywa changu kwa mafumbo,

nitazungumza mambo yaliyofichika, mambo ya kale:

3 yale ambayo tuliyasikia na kuyajua,

yale ambayo baba zetu walituambia.

4 Hatutayaficha kwa watoto wao;

tutakiambia kizazi kijacho

matendo yastahiliyo sifa yaBwana,

uweza wake, na maajabu aliyoyafanya.

5 Aliagiza amri kwa Yakobo

na akaweka sheria katika Israeli,

ambazo aliwaamuru baba zetu

wawafundishe watoto wao,

6 ili kizazi kijacho kizijue,

pamoja na watoto ambao watazaliwa,

nao pia wapate kuwaeleza watoto wao.

7 Ndipo wangeweka tumaini lao kwa Mungu,

nao wasingesahau matendo yake,

bali wangalizishika amri zake.

8 Ili wasifanane na baba zao,

waliokuwa kizazi cha ukaidi na uasi,

ambao roho zao hazikuwa na uaminifu kwake,

ambao roho zao hazikumwamini.

9 Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde,

walikimbia siku ya vita.

10 Hawakulishika agano la Mungu

na walikataa kuishi kwa sheria yake.

11 Walisahau aliyokuwa ameyatenda,

maajabu aliyokuwa amewaonyesha.

12 Alitenda miujiza machoni mwa baba zao,

huko Soani, katika nchi ya Misri.

13 Aliigawanya bahari akawapitisha,

alifanya maji yasimame imara kama ukuta.

14 Aliwaongoza kwa wingu mchana

na kwa nuru kutoka kwenye moto usiku kucha.

15 Alipasua miamba jangwani

na akawapa maji tele kama bahari,

16 alitoa vijito kutoka kwenye jabali lililochongoka,

akayafanya maji yatiririke kama mito.

17 Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake,

wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana.

18 Kwa makusudi walimjaribu Mungu,

wakidai vyakula walivyovitamani.

19 Walinena dhidi ya Mungu, wakisema,

“Je, Mungu aweza kuandaa meza jangwani?

20 Alipopiga mwamba, maji yalitoka kwa nguvu,

vijito vikatiririka maji mengi.

Lakini je, aweza kutupa chakula pia?

Je, anaweza kuwapa watu wake nyama?”

21 Bwanaalipowasikia, alikasirika sana,

moto wake ukawa dhidi ya Yakobo,

na ghadhabu yake ikawaka dhidi ya Israeli,

22 kwa kuwa hawakumwamini Mungu,

wala kuutumainia ukombozi wake.

23 Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu

na kufungua milango ya mbingu,

24 akawanyeshea mana ili watu wale;

aliwapa nafaka ya mbinguni.

25 Watu walikula mkate wa malaika,

akawatumia chakula chote ambacho wangeliweza kula.

26 Aliachia upepo wa mashariki kutoka kwenye mbingu

na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake.

27 Aliwanyeshea nyama kama mavumbi,

ndege warukao kama mchanga wa pwani.

28 Aliwafanya washuke ndani ya kambi yao,

kuzunguka mahema yao yote.

29 Walikula na kusaza,

kwa maana alikuwa amewapa kile walichotamani.

30 Kabla hawajamaliza kula walichokitamani,

hata kilipokuwa kingali bado vinywani mwao,

31 hasira ya Mungu ikawaka juu yao,

akawaua wale waliokuwa na nguvu zaidi miongoni mwao,

akiwaangusha vijana wa Israeli.

32 Licha ya haya yote, waliendelea kutenda dhambi,

licha ya maajabu yake, hawakuamini.

33 Kwa hiyo akamaliza siku zao katika ubatili

na miaka yao katika vitisho.

34 Kila mara Mungu alipowaua baadhi yao,

waliosalia walimtafuta,

walimgeukia tena kwa shauku.

35 Walikumbuka kwamba Mungu alikuwa Mwamba wao,

kwamba Mungu Aliye Juu Sana alikuwa Mkombozi wao.

36 Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao,

wakisema uongo kwa ndimi zao,

37 mioyo yao haikuwa thabiti kwake,

wala hawakuwa waaminifu katika agano lake.

38 Hata hivyo alikuwa na huruma,

alisamehe maovu yao

na hakuwaangamiza.

Mara kwa mara alizuia hasira yake,

wala hakuchochea ghadhabu yake yote.

39 Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu,

upepo upitao ambao haurudi.

40 Mara ngapi walimwasi jangwani

na kumhuzunisha nyikani!

41 Walimjaribu Mungu mara kwa mara,

wakamkasirisha yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

42 Hawakukumbuka uwezo wake,

siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi,

43 siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri,

maajabu yake huko Soani.

44 Aligeuza mito yao kuwa damu,

hawakuweza kunywa maji kutoka vijito vyao.

45 Aliwapelekea makundi ya mainzi yakawala,

na vyura wakawaharibu.

46 Aliruhusu tunutu kuharibu mimea yao,

mazao yao kwa nzige.

47 Aliharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe

na mikuyu yao kwa mvua iliyochangamana na theluji.

48 Aliwaachia mifugo yao mvua ya mawe,

akayapiga makundi ya wanyama wao kwa radi.

49 Aliwafungulia hasira yake kali,

ghadhabu yake, hasira na uadui,

na kundi la malaika wa kuharibu.

50 Aliitengenezea njia hasira yake,

hakuwaepusha na kifo,

bali aliwaachia tauni.

51 Aliwapiga wazaliwa wote wa kwanza wa Misri,

matunda ya kwanza ya ujana katika mahema ya Hamu.

52 Lakini aliwatoa watu wake kama kundi,

akawaongoza kama kondoo kupitia jangwani.

53 Aliwaongoza salama, wala hawakuogopa,

bali bahari iliwameza adui zao.

54 Hivyo akawaleta hadi kwenye mpaka wa nchi yake takatifu,

hadi nchi ya vilima ambayo mkono wake wa kuume ulikuwa umeitwaa.

55 Aliyafukuza mataifa mbele yao,

na kuwagawia nchi zao kama urithi,

aliwakalisha makabila ya Israeli katika makao yao.

56 Lakini wao walimjaribu Mungu,

na kuasi dhidi ya Yeye Aliye Juu Sana,

wala hawakuzishika sheria zake.

57 Kama baba zao, hawakuwa thabiti wala waaminifu,

wakawa wasioweza kutegemewa

kama upinde wenye kasoro.

58 Wakamkasirisha Mungu kwa mahali pao pa juu pa kuabudia miungu,

wakachochea wivu wake kwa sanamu zao.

59 Wakati Mungu alipowasikia, alikasirika sana,

akamkataa Israeli kabisa.

60 Akaiacha hema ya Shilo,

hema aliyokuwa ameiweka katikati ya wanadamu.

61 Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani,

utukufu wake mikononi mwa adui.

62 Aliachia watu wake wauawe kwa upanga,

akaukasirikia sana urithi wake.

63 Moto uliwaangamiza vijana wao,

na wanawali wao hawakuimbiwa nyimbo za arusi,

64 makuhani wao waliuawa kwa upanga,

wala wajane wao hawakuweza kulia.

65 Ndipo Bwana alipoamka kama vile kuamka usingizini,

kama vile mtu aamkavyo kutoka kwenye bumbuazi la mvinyo.

66 Aliwapiga na kuwashinda adui zake,

akawatia katika aibu ya milele.

67 Ndipo alipozikataa hema za Yosefu,

hakulichagua kabila la Efraimu,

68 lakini alilichagua kabila la Yuda,

Mlima Sayuni, ambao aliupenda.

69 Alijenga patakatifu pake kama vilele,

kama dunia ambayo aliimarisha milele.

70 Akamchagua Daudi mtumishi wake

na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo.

71 Kutoka kuchunga kondoo alimleta

kuwa mchungaji wa watu wake Yakobo,

wa Israeli urithi wake.

72 Naye Daudi aliwachunga kwa uadilifu wa moyo,

kwa mikono ya ustadi aliwaongoza.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/78-1189d6dae5fa0f6dc31378469c577047.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 79

Maombi Kwa Ajili Ya Wokovu Wa Taifa

Zaburi ya Asafu.

1 Ee Mungu, mataifa yameuvamia urithi wako,

wamelinajisi Hekalu lako takatifu,

wameifanya Yerusalemu kuwa magofu.

2 Wametoa maiti za watumishi

kuwa chakula cha ndege wa angani

na nyama ya watakatifu wako

kwa wanyama wa nchi.

3 Wamemwaga damu kama maji

kuzunguka Yerusalemu yote,

wala hakuna yeyote wa kuwazika.

4 Tumekuwa kitu cha aibu kwa jirani zetu,

cha dharau na mzaha kwa wale wanaotuzunguka.

5 Hata lini, EeBwana? Je, wewe utakasirika milele?

Wivu wako utawaka kama moto hadi lini?

6 Mwaga ghadhabu yako kwa mataifa yasiyokukubali,

juu ya falme za hao wasioliitia jina lako,

7 kwa maana wamemrarua Yakobo

na kuharibu nchi ya makao yake.

8 Usituhesabie dhambi za baba zetu,

huruma yako na itujie hima,

kwa maana tu wahitaji mno.

9 Ee Mungu Mwokozi wetu, utusaidie,

kwa ajili ya utukufu wa jina lako;

tuokoe na kutusamehe dhambi zetu

kwa ajili ya jina lako.

10 Kwa nini mataifa waseme,

“Yuko wapi Mungu wenu?”

Mbele ya macho yetu,

dhihirisha kati ya mataifa

kwamba unalipiza kisasi damu iliyomwagwa

ya watumishi wako.

11 Kilio cha huzuni cha wafungwa kifike mbele zako;

kwa nguvu za mkono wako

hifadhi wale waliohukumiwa kufa.

12 Walipize jirani zetu mara saba vifuani mwao

aibu walizovurumisha juu yako, EeBwana.

13 Ndipo sisi watu wako, kondoo wa malisho yako,

tutakusifu milele;

toka kizazi hadi kizazi

tutasimulia sifa zako.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/79-be3042ef5e97803f3fb6e99253d7d312.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 80

Maombi Kwa Ajili Ya Kuponywa Kwa Taifa

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi za Agano.” Zaburi ya Asafu.

1 Ee Mchungaji wa Israeli tusikie,

wewe umwongozaye Yosefu kama kundi;

wewe uketiye katika kiti cha enzi

katikati ya makerubi, angaza

2 mbele ya Efraimu, Benyamini na Manase.

Uamshe nguvu zako,

uje utuokoe.

3 Ee Mungu, uturejeshe,

utuangazie uso wako,

ili tuweze kuokolewa.

4 EeBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote,

hata lini hasira yako itawaka na kufoka moshi

dhidi ya maombi ya watu wako?

5 Umewalisha kwa mkate wa machozi,

umewafanya wanywe machozi bakuli tele.

6 Tumekuwa chanzo cha ugomvi kwa jirani zetu,

na adui zetu wanatudhihaki.

7 Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;

utuangazie uso wako,

nasi tuweze kuokolewa.

8 Ulileta mzabibu kutoka Misri,

ukawafukuza mataifa, ukaupanda.

9 Uliandaa shamba kwa ajili yake,

mizizi ikawa imara, ukajaza nchi.

10 Milima ilifunikwa kwa kivuli chake,

matawi yake yakafunika mierezi mikubwa.

11 Matawi yake yalienea mpaka Baharini,

machipukizi yake mpaka kwenye Mto.

12 Mbona umebomoa kuta zake

ili wote wapitao karibu

wazichume zabibu zake?

13 Nguruwe mwitu wanauharibu

na wanyama wa kondeni hujilisha humo.

14 Turudie, Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote!

Tazama chini kutoka mbinguni na uone!

Linda mzabibu huu,

15 mche ulioupanda kwa mkono wako wa kuume,

mwana uliyemlea

kwa ajili yako mwenyewe.

16 Mzabibu wako umekatwa, umechomwa moto,

unapowakemea, watu wako huangamia.

17 Mkono wako na utulie juu ya mtu aliyeko mkono wako wa kuume,

mwana wa mtu uliyemlea kwa ajili yako mwenyewe.

18 Ndipo hatutakuacha tena,

utuhuishe, nasi tutaliitia jina lako.

19 EeBwanaMungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe;

utuangazie uso wako,

ili tuweze kuokolewa.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/80-e66411dc1eba208e8eb0c3030a5e0c2d.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 81

Wimbo Wa Sikukuu

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Asafu.

1 Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu;

mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo!

2 Anzeni wimbo, pigeni matari,

pigeni kinubi na zeze kwa sauti nzuri.

3 Pigeni baragumu za pembe za kondoo dume

wakati wa Mwandamo wa Mwezi,

na wakati wa mwezi mpevu,

katika siku ya Sikukuu yetu;

4 hii ni amri kwa Israeli,

agizo la Mungu wa Yakobo.

5 Aliiweka iwe kama sheria kwa Yosefu

alipotoka dhidi ya Misri,

huko tulikosikia lugha ambayo hatukuielewa.

6 Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao;

mikono yao iliwekwa huru kutoka kwenye kikapu.

7 Katika shida yako uliniita nami nikakuokoa,

nilikujibu katika mawingu yenye ngurumo;

nilikujaribu katika maji ya Meriba.

8 “Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya:

laiti kama mngenisikiliza, ee Israeli!

9 Hamtakuwa na mungu mgeni miongoni mwenu;

msimsujudie mungu wa kigeni.

10 Mimi niBwanaMungu wako,

niliyekutoa nchi ya Misri.

Panua sana kinywa chako

nami nitakijaza.

11 “Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza;

Israeli hakutaka kunitii.

12 Basi niliwaacha katika ukaidi wa mioyo yao

wafuate mashauri yao wenyewe.

13 “Laiti kama watu wangu wangalinisikiliza,

kama Israeli wangalifuata njia zangu,

14 ningaliwatiisha adui zao kwa haraka,

na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao!

15 Wale wanaomchukiaBwanawangalinyenyekea mbele zake,

na adhabu yao ingedumu milele.

16 Bali ninyi mngalilishwa ngano iliyo bora,

na kuwatosheleza kwa asali itokayo kwenye mwamba.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/81-e87653961eb08b44308f749c8a325e06.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 82

Maombi Kwa Ajili Ya Kutaka Haki

Zaburi ya Asafu.

1 Mungu anaongoza kusanyiko kuu,

anatoa hukumu miongoni mwa “miungu”:

2 “Hata lini utaendelea kuwatetea wasio haki

na kuonyesha upendeleo kwa waovu?

3 Teteeni wanyonge na yatima,

tunzeni haki za maskini na walioonewa.

4 Mwokoeni mnyonge na mhitaji,

wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.

5 “Hawajui lolote, hawaelewi lolote.

Wanatembea gizani;

misingi yote ya dunia imetikisika.

6 “Nilisema, ‘Ninyi ni “miungu”;

ninyi nyote ni wana wa Aliye Juu Sana.’

7 Lakini mtakufa kama wanadamu wa kawaida;

mtaanguka kama mtawala mwingine yeyote.”

8 Ee Mungu, inuka uihukumu nchi,

kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/82-60692687af86ed7e0cf29b48afb24c48.mp3?version_id=1627—

Categories
Zaburi

Zaburi 83

Maombi Kwa Ajili Ya Kushindwa Kwa Adui Wa Israeli

Wimbo. Zaburi ya Asafu.

1 Ee Mungu, usinyamaze kimya,

usinyamaze, Ee Mungu, usitulie.

2 Tazama watesi wako wanafanya fujo,

jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao.

3 Kwa hila, wanafanya shauri dhidi ya watu wako,

wanafanya shauri baya dhidi ya wale unaowapenda.

4 Wanasema, “Njooni, tuwaangamize kama taifa,

ili jina la Israeli lisikumbukwe tena.”

5 Kwa nia moja wanapanga mashauri mabaya pamoja,

wanafanya muungano dhidi yako,

6 mahema ya Edomu na Waishmaeli,

ya Wamoabu na Wahagari,

7 Gebali,Amoni na Amaleki,

Ufilisti, pamoja na watu wa Tiro.

8 Hata Ashuru wameungana nao

kuwapa nguvu wazao wa Loti.

9 Uwatendee kama vile ulivyowatendea Midiani,

na kama vile ulivyowatendea Sisera na Yabini

hapo kijito cha Kishoni,

10 ambao waliangamia huko Endori

na wakawa kama takataka juu ya nchi.

11 Wafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu,

watawala wao kama Zeba na Salmuna,

12 ambao walisema, “Na tumiliki nchi

ya malisho ya Mungu.”

13 Ee Mungu wangu, wapeperushe kama mavumbi ya kisulisuli,

kama makapi yapeperushwayo na upepo.

14 Kama vile moto uteketezavyo msitu

au mwali wa moto unavyounguza milima,

15 wafuatilie kwa tufani yako

na kuwafadhaisha kwa dhoruba yako.

16 Funika nyuso zao kwa aibu

ili watu walitafute jina lako, EeBwana.

17 Wao na waaibishwe na kufadhaishwa milele,

na waangamie kwa aibu.

18 Hebu wajue kwamba wewe, ambaye jina lako niBwana,

kwamba wewe peke yako ndiwe Uliye Juu Sana ya dunia yote.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/83-34518efc42844b96fe74402423a0cd6a.mp3?version_id=1627—