Categories
Esta

Esta 8

Amri Ya Mfalme Kuhusu Wayahudi

1 Siku ile ile Mfalme Ahasuero akampa Malkia Esta shamba la Hamani, adui wa Wayahudi. Naye Mordekai akaja mbele ya mfalme, kwa kuwa Esta alikuwa amesema jinsi anavyohusiana naye.

2 Mfalme akaivua pete yake ya muhuri, ambayo alikuwa amemnyangʼanya Hamani, akampa Mordekai, naye Esta akamweka Mordekai juu ya shamba la Hamani.

3 Esta alimsihi tena mfalme, akianguka miguuni pake na kulia. Akamwomba akomeshe mpango mwovu wa Hamani Mwagagi ambao alikuwa ameupanga dhidi ya Wayahudi.

4 Kisha mfalme alimnyooshea Esta fimbo yake ya utawala ya dhahabu naye aliinuka na kusimama mbele yake.

5 Esta akasema, “Kama ikimpendeza mfalme, nami kama nikipata kibali naye akiona ni jambo lililo sawa kunitendea na kama akipendezwa nami, basi iandikwe amri ya kuzitangua barua zile Hamani mwana wa Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuandika kuangamiza Wayahudi katika majimbo yote ya mfalme.

6 Kwa maana nitawezaje kuvumilia kuona maafa yakiwapata watu wangu? Nitawezaje kuvumilia kuona maangamizi ya jamaa yangu?”

7 Mfalme Ahasuero akawajibu Malkia Esta na Mordekai Myahudi, “Kwa sababu Hamani aliwashambulia Wayahudi, nimetoa shamba la Hamani kwa Esta, naye ameangikwa kwenye mti wa kunyongea.

8 Basi andika amri nyingine kwa jina la mfalme kwa ajili ya Wayahudi kama unavyoona vyema, kisha uifunge kwa kutia muhuri kwa pete ya mfalme kwa kuwa hakuna andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa muhuri kwa pete ya mfalme linaloweza kutanguliwa.”

9 Mara moja waandishi wa mfalme wakaitwa kwenye siku ya ishirini na tatu, mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani. Wakaandika yote Mordekai aliyoamuru kwa Wayahudi, kwa majemadari, watawala na wakuu wa majimbo 127 kuanzia Bara Hindi mpaka Kushi.Maagizo haya yaliandikwa kwa maandishi ya kila jimbo na kwa lugha ya kila mtu pia kwa Wayahudi kwa maandishi yao wenyewe na lugha yao.

10 Mordekai aliandika nyaraka kwa jina la Mfalme Ahasuero, akazitia muhuri kwa pete ya mfalme na kuzipeleka kwa njia ya matarishi, ambao waliendesha farasi waendao kasi waliozalishwa maalum kwa ajili ya mfalme.

11 Waraka wa mfalme uliwaruhusu Wayahudi katika kila mji kuwa na haki ya kukusanyika na kujilinda wenyewe; kuharibu, kuua na kuangamiza jeshi lolote, taifa lolote au jimbo lile litakalowashambulia wao, wake zao, watoto wao na kuteka mali za adui zao.

12 Siku ambayo iliwekwa kwa Wayahudi kufanya hili katika majimbo yote ya Mfalme Ahasuero ilikuwa siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari.

13 Nakala ya tangazo ilikuwa itolewe kama sheria katika kila jimbo na iweze kujulikana kwa watu wa kila taifa, ili kwamba Wayahudi wawe tayari siku hiyo kulipiza kisasi kwa adui zao.

14 Matarishi, wakiwa wamepanda farasi wa kifalme, walitoka mbio wakichochewa na agizo la mfalme. Tangazo lilitolewa pia katika ngome ya mji wa Shushani.

15 Mordekai akaondoka mbele ya mfalme akiwa amevaa mavazi ya kifalme ya buluu na nyeupe, taji kubwa la dhahabu na joho la zambarau la kitani safi. Na mji wa Shushani ukasherehekea kwa furaha.

16 Kwa maana kwa Wayahudi ulikuwa wakati wa raha na furaha, shangwe na heshima.

17 Katika kila jimbo na katika kila jiji, popote waraka wa mfalme ulipofika, kulikuwepo furaha na shangwe miongoni mwa Wayahudi, pamoja na karamu na kushangilia. Na watu wengi wa mataifa mengine wakajifanya Wayahudi kwa sababu ya kuwahofu Wayahudi.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EST/8-48c9197f5672eafeecd5c0ad51ec725c.mp3?version_id=1627—

Categories
Esta

Esta 9

Ushindi Wa Wayahudi

1 Katika siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, yaani mwezi wa Adari, amri iliyoagizwa na mfalme ilikuwa itekelezwe. Siku hii adui wa Wayahudi walikuwa wametumaini kuwashinda, lakini sasa mambo yaliwageukia na Wayahudi wakawashinda wale waliokuwa wanawachukia.

2 Wayahudi walikusanyika katika miji yao, katika majimbo ya Mfalme Ahasuero kuwashambulia wale waliokuwa wanatafuta kuwaangamiza. Hakuna yeyote aliyeweza kushindana nao, kwa sababu watu wa mataifa mengine yote waliwaogopa.

3 Nao wakuu wote wa majimbo, majemadari, watawala na maafisa wa mfalme wakawasaidia Wayahudi, kwa sababu walimhofu Mordekai.

4 Mordekai alikuwa mtu mashuhuri katika jumba la mfalme; sifa zake zilienea katika majimbo yote naye alipata uwezo zaidi na zaidi.

5 Wayahudi waliwaangusha adui zao wote kwa upanga wakiwaua na kuwaangamiza, nao walifanya kile walichotaka kwa wale waliowachukia.

6 Katika ngome ya Shushani Wayahudi waliua na kuangamiza wanaume 500.

7 Pia waliwaua Parshendatha, Dalfoni, Aspatha,

8 Poratha, Adalia, Ardatha,

9 Parmashta, Arisai, Aridai na Waizatha,

10 wana kumi wa Hamani mwana wa Hamedatha, adui wa Wayahudi. Lakini hawakuchukua nyara.

11 Mfalme aliarifiwa siku iyo hiyo hesabu ya waliouawa katika ngome ya Shushani.

12 Mfalme akamwambia Malkia Esta, “Wayahudi wamewaua wanaume 500 na wana kumi wa Hamani ndani ya ngome ya Shushani. Wamefanyaje katika majimbo mengine ya mfalme yaliyobaki? Je, sasa haja yako ni nini? Nayo pia utapewa. Nalo ombi lako ni nini? Nalo utafanyiwa.”

13 Esta akajibu, “Ikimpendeza mfalme, uwape ruhusa Wayahudi walioko Shushani warudie amri ya leo kesho pia, na wana wa Hamani kumi wanyongwe mahali pa kunyongea watu.”

14 Basi mfalme akaamuru kwamba hili litendeke. Amri ilitolewa huko Shushani, nao wakawanyonga wana kumi wa Hamani.

15 Wayahudi huko Shushani wakakusanyika pamoja siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari, nao wakawaua wanaume 300 huko Shushani, lakini hawakuchukua nyara zao.

16 Wakati ule ule, Wayahudi wengine waliokuwa kwenye majimbo ya mfalme, wakakusanyika kujilinda nao wakapata nafuu kutokana na adui zao. Waliua adui zao wapatao 75,000 lakini hawakugusa nyara zao.

17 Hili lilitendeka siku ya kumi na tatu ya mwezi wa Adari na siku ya kumi na nne walipumzika na kuifanya siku ya karamu na furaha.

Kusherehekea Purimu

18 Wayahudi huko Shushani, hata hivyo, walikuwa wamekusanyika siku ya kumi na tatu na ya kumi na nne, pia siku ya kumi na tano walipumzika na kuifanya siku ya karamu na furaha.

19 Ndiyo sababu Wayahudi wanaokaa vijijini na katika miji midogo huadhimisha siku ya kumi na nne ya mwezi wa Adari kama siku ya furaha na karamu, siku ambayo wao hupeana zawadi mmoja kwa mwingine.

20 Mordekai aliandika matukio haya, naye akapeleka barua kwa Wayahudi wote walioko katika majimbo ya Mfalme Ahasuero, majimbo yaliyo mbali na karibu,

21 akiwataka kila mwaka washerehekee siku ya kumi na nne na ya kumi na tano ya mwezi wa Adari

22 kama wakati ambao Wayahudi walipata nafuu kutoka kwa adui zao na kama mwezi ambao huzuni yao iligeuzwa kuwa furaha na kuomboleza kwao kuwa siku ya kusherehekea. Aliwaandikia kushika siku hizo kama siku za karamu na za furaha na kupeana zawadi za vyakula wao kwa wao na zawadi kwa maskini.

23 Hivyo Wayahudi walikubali kuendeleza sherehe walizokuwa wamezianza, wakifanya lile Mordekai alilokuwa amewaandikia.

24 Kwa maana Hamani mwana wa Hamedatha Mwagagi, adui wa Wayahudi wote, alikuwa amepanga hila dhidi ya Wayahudi ili kuwaangamiza, na alikuwa amepigapuri(yaani kura) kwa ajili ya maangamizi na uharibifu wao.

25 Lakini wakati shauri hilo baya lilipoarifiwa kwa mfalme, alitoa amri iliyoandikwa kwamba mipango mibaya ambayo Hamani ameipanga dhidi ya Wayahudi inapasa imrudie juu ya kichwa chake mwenyewe, na kwamba yeye na wanawe waangikwe mahali pa kunyongea watu.

26 (Kwa hiyo siku hizi ziliitwa Purimu, kutokana na nenopuri.) Kwa sababu ya kila kitu kilichoandikwa kwenye barua hii na kwa sababu ya yale waliyoyaona na yale yaliyowatokea,

27 Wayahudi wakachukua na kuifanya desturi kwamba wao na wazao wao na wote ambao walijiunga nao wangefanya bila kuacha kushika siku hizi mbili kila mwaka, kwa njia ilivyoelekezwa na kwa wakati wake.

28 Siku hizi zinapasa zikumbukwe na kuadhimishwa katika kila kizazi, kila jamaa na katika kila jimbo na kila jiji. Nazo siku hizi za Purimu kamwe zisikome kusherehekewa na Wayahudi, wala kumbukumbu zake zisipotee miongoni mwa wazao wake.

29 Basi Malkia Esta binti Abihaili, pamoja na Mordekai, Myahudi, waliandika kwa mamlaka yote kuthibitisha barua hii ya pili kuhusu Purimu.

30 Naye Mordekai akatuma barua kwa Wayahudi wote katika majimbo 127 ya ufalme wa Ahasuero, barua zenye maneno ya amani na matumaini,

31 ili kuimarisha siku hizi za Purimu katika majira yake yaliyowekwa, kama Mordekai, Myahudi na Malkia Esta walivyowaamuru, na walivyojiimarisha wenyewe na wazao wao kuhusu nyakati za kufunga na kuomboleza.

32 Amri ya Esta ilithibitisha taratibu hizi kuhusu Purimu, nayo ikaandikwa katika kumbukumbu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EST/9-fccce3a4d61d0591d78cbee60d99c667.mp3?version_id=1627—

Categories
Esta

Esta 10

Ukuu Wa Mordekai

1 Mfalme Ahasuero alitoza ushuru katika ufalme wake wote hadi kwenye miambao yake ya mbali.

2 Matendo yake yote ya nguvu na uwezo, pamoja na habari zote za ukuu wa Mordekai ambao mfalme alikuwa amemkuza, je, hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu za wafalme wa Umedi na Uajemi?

3 Mordekai Myahudi alikuwa wa pili kwa cheo kutoka Mfalme Ahasuero, naye alikuwa bora kabisa miongoni mwa Wayahudi, akipandishwa katika heshima ya juu na ndugu zake Wayahudi kwa sababu aliwatendea mema watu wake, na alizungumza kwa ajili ya ustawi wa Wayahudi wote.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/EST/10-442bb7374f3ef79323e7f678cee6414b.mp3?version_id=1627—

Categories
Ayubu

Ayubu Utangulizi

Utangulizi

Kitabu cha Ayubu kimepewa jina la mhusika mkuu ambaye ni mtu mwenye haki mbele za Mungu na aliyekuwa tajiri sana. Ayubu maana yake ni “Yule anayemrudia Mungu daima.” Hata baada ya kuondokewa na vitu vyote alivyokuwa navyo na kuteseka kwa majipu hatari, Ayubu bado alikiri kumpenda Mungu. Lakini marafiki wa Ayubu walisisitiza kwamba alikuwa anateseka kwa sababu alikuwa ametenda dhambi, na kwamba hiyo ilikuwa ni adhabu yake. Ayubu alijitetea kwa kusisitiza kwamba hajafanya uovu ambao ungemsabibishia hiyo adhabu na ya kwamba yeye anamwamini Mungu. Ndipo Mungu alipozungumza na kuonyesha uwezo wake mkubwa. Mwisho wa yote Ayubu alikubali kwamba Mungu ni mkuu na wa ajabu kwetu, kiasi kwamba hatuwezi kumwelewa.

Mwandishi

Haijulikani kwa dhahiri ni nani aliyekiandika kitabu hiki, huenda ikawa ni Ayubu. Wengine hudhani ni Mose, Solomoni au Elihu.

Kusudi

Kitabu hiki kinaonyesha uweza na uaminifu wa Mungu, na pia kinathibitisha maana ya imani ya kweli ya mtu wa Mungu. Kitabu hiki kinaonyesha baraka zinazoandamana na ushindi baada ya majaribu. Kwa hiyo kazi ya majaribu ambayo Mungu anayaruhusu ni kutudhibitisha katika imani. Kitabu hiki kinazungumzia swali hili: “Ni kwa nini wenye haki huteseka?”

Mahali

Kuna uwezekano kwamba nchi ya Usi ilikuwa kaskazini mashariki mwa Palestina, karibu na jangwa iliyo katikati ya Dameski na Mto Frati.

Tarehe

Tarehe ya kuandikwa kwa kitabu hiki haijulikani; kinadhaniwa kuwa kitabu cha zamani sana, huenda kuliko vingine vyote katika Biblia. Yawezekana kuwa mambo yalioandikwa kwenye kitabu hiki yalitendeka kati ya 2000–1800 K.K.

Wahusika Wakuu

Ayubu, Elifazi Mtemani, Bildadi Mshuhi, Sofari Mnaamathi, na Elihu wa kabila la Buzi.

Wazo Kuu

Mungu ametuwekea ugo pande zote. Hivyo Shetani hawezi kutushambulia bila Mungu kujua, lakini wakati mwingine Mungu hutoa ruhusa ili kumthibitishia adui juu ya uelekevu na uadilifu wa mtu wake. Hivyo basi, kumtumaini Mungu wakati wote na katika hali zote huleta ushindi dhidi ya Shetani.

Mambo Muhimu

Kujaribiwa kwa Ayubu, mazungumzo na rafiki zake, na vile Mungu alimnenea na kumbariki baadaye na watoto na mali nyingi kushinda hapo mwanzo.

Mgawanyo

Habari za awali, na Ayubu kujaribiwa (

1:1–2:13

)

Mazungumzo ya Ayubu na rafiki zake watatu (

3:1–31:40

)

1. Mungu anahusikaje na mateso ya Ayubu? (

3:1–14:22

)

2. Je, watu waovu huwa wanateseka mara zote? (

15:1–21:34

)

3. Je, Ayubu ana hatia ya kuwa na dhambi ya siri? (

22:1–31:40

)

Elihu anamjibu Ayubu na kuwakemea marafiki zake (

32:1–37:24

)

Mungu anamjibu Ayubu (

38:1–41:34

)

Mwisho (

42:1-17

).

Categories
Ayubu

Ayubu 1

Ayubu Na Jamaa Yake

1 Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu.

2 Alikuwa na wana saba na binti watatu,

3 naye alikuwa na kondoo elfu saba, ngamia elfu tatu, jozi mia tano za maksai, na punda mia tano, tena alikuwa na idadi kubwa ya watumishi. Alikuwa mtu mkuu sana miongoni mwa watu wa Mashariki.

4 Wanawe walikuwa na desturi ya kufanya karamu katika nyumba zao kwa zamu, nao wangewaalika umbu zao watatu ili kula na kunywa pamoja nao.

5 Wakati kipindi cha karamu kilimalizika, Ayubu angetuma waitwe na kuwafanyia utakaso. Angetoa dhabihu ya sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya kila mmoja wao asubuhi na mapema, akifikiri, “Pengine wanangu wametenda dhambi na kumlaani Mungu mioyoni mwao.” Hii ilikuwa ndiyo desturi ya kawaida ya Ayubu.

Jaribu La Kwanza La Ayubu

6 Siku moja wana wa Munguwalikwenda kujionyesha mbele zaBwana. Shetaninaye akaja pamoja nao.

7 Bwanaakamwambia Shetani, “Umetoka wapi?”

Shetani akamjibuBwana, “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”

8 NdipoBwanaakamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuepukana na uovu.”

9 Shetani akamjibuBwana, “Je, Ayubu anamcha Mungu bure?

10 Je, wewe hukumjengea boma pande zote yeye na wa nyumbani mwake pamoja na kila kitu alicho nacho? Kazi za mikono yake umezibariki na hivyo makundi yake ya kondoo na mbuzi pamoja na ya wanyama yameenea katika nchi nzima.

11 Lakini nyoosha mkono wako na kupiga kila kitu alicho nacho, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.”

12 Bwanaakamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, kila kitu alicho nacho kiko mikononi mwako, lakini juu ya huyo mtu mwenyewe usimguse hata kwa kidole.”

Ndipo Shetani akatoka mbele zaBwana.

13 Siku moja watoto wa Ayubu walipokuwa wakifanya karamu wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa,

14 akaja mjumbe kwa Ayubu na kusema, “Maksai walikuwa wakilima na punda walikuwa wakilisha karibu nao,

15 Waseba wakawashambulia na kuchukua mifugo. Kisha wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!”

16 Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Moto wa Mungu ulishuka kutoka mbinguni na kuteketeza kondoo na watumishi, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!”

17 Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wakaldayo waliunda vikosi vitatu vya uvamizi na kuwaangukia ngamia wako na kuwachukua wakaondoka nao. Wakawaua watumishi kwa upanga, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari.”

18 Alipokuwa bado ananena, mjumbe mwingine akaja na kusema, “Wana wako na binti zako walipokuwa wakifanya karamu, wakila na kunywa divai katika nyumba ya ndugu yao mkubwa,

19 ghafula upepo wenye nguvu ukavuma kutoka jangwani, nao ukaipiga nyumba hiyo pembe zake nne. Ikawaangukia hao watoto nao wamekufa, nami ndimi peke yangu niliyenusurika kukuletea habari!”

20 Ndipo Ayubu akasimama, akararua joho lake na kunyoa nywele zake. Kisha akaanguka chini katika kuabudu

21 na kusema:

“Nilitoka tumboni mwa mama yangu uchi,

nami nitaondoka uchi,

Bwanaalinipa, nayeBwanaameviondoa,

jina laBwanalitukuzwe.”

22 Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi kwa kumlaumu Mungu kwa kufanya ubaya.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOB/1-f86d4ff6207168828cc8bcb99d7b9655.mp3?version_id=1627—

Categories
Ayubu

Ayubu 2

Jaribu La Pili La Ayubu

1 Siku nyingine wana wa Mungu walikuja kujionyesha mbele zaBwana. Shetani naye akaja pamoja nao kujionyesha mbele zake.

2 Bwanaakamuuliza Shetani, “Umetoka wapi?”

Shetani akamjibuBwana“Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”

3 Bwanaakamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, mtu asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Naye bado anadumisha uadilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.”

4 Shetani akamjibuBwana, “Ngozi kwa ngozi! Mwanadamu atatoa vyote alivyo navyo kwa ajili ya uhai wake.

5 Lakini nyoosha mkono wako na kuipiga nyama yake na mifupa yake, naye kwa hakika atakulaani mbele za uso wako.”

6 Bwanaakamwambia Shetani, “Vema sana, kwa hiyo, yeye yumo mikononi mwako, lakini lazima umwachie uhai wake.”

7 Basi Shetani akatoka mbele zaBwananaye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa.

8 Ndipo Ayubu akachukua kigae na kujikuna nacho huku akiketi kwenye majivu.

9 Mke wake akamwambia, “Je, bado unashikamana na uadilifu wako? Mlaani Mungu nawe ukafe!”

10 Akamjibu, “Unazungumza kama vile ambavyo mwanamke mpumbavuyeyote angenena. Je, tupokee mema mikononi mwa Mungu, nasi tusipokee na udhia?”

Katika mambo haya yote, Ayubu hakutenda dhambi katika kusema kwake.

Marafiki Watatu Wa Ayubu

11 Basi marafiki watatu wa Ayubu, ndio Elifazi Mtemani, na Bildadi Mshuhi na Sofari Mnaamathi, waliposikia juu ya taabu yote iliyompata Ayubu, wakajipanga toka manyumbani mwao, nao wakakutana pamoja kwa makubaliano kwenda kumtuliza katika taabu hiyo na kumfariji.

12 Walipomwona kwa mbali, ilikuwa vigumu kumtambua. Wakaanza kulia kwa sauti kubwa, wakayararua majoho yao na kujirushia mavumbi juu ya vichwa vyao.

13 Kisha wakaketi chini kwenye udongo pamoja na Ayubu kwa siku saba usiku na mchana. Hakuna yeyote aliyesema naye neno, kwa sababu waliona jinsi mateso yake yalivyokuwa makubwa.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOB/2-fc6d18042f3d3806c85f9523944f0fb0.mp3?version_id=1627—

Categories
Ayubu

Ayubu 3

Ayubu Anazungumza

1 Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake.

2 Kisha akasema:

3 “Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali,

nao usiku ule iliposemekana,

‘Mtoto wa kiume amezaliwa!’

4 Siku ile na iwe giza;

Mungu juu na asiiangalie;

nayo nuru isiiangazie.

5 Giza na kivuli kikuu kiikalie tena;

wingu na likae juu yake;

weusi na uifunike nuru yake.

6 Usiku ule na ushikwe na giza kuu;

usihesabiwe katika siku za mwaka,

wala usihesabiwe katika siku za mwezi wowote.

7 Usiku ule na uwe tasa;

sauti ya furaha na isisikike ndani yake.

8 Wale wazilaanio siku wailaani hiyo siku,

wale walio tayari kumwamsha Lewiathani.

9 Nyota zake za alfajiri na ziwe giza;

nao ungojee mwanga bila mafanikio,

wala usiuone mwonzi wa kwanza

wa mapambazuko,

10 kwa sababu huo usiku haukunifungia

mlango wa tumbo la mama yangu,

ili kuyaficha macho yangu

kutokana na taabu.

11 “Kwa nini sikuangamia wakati wa kuzaliwa?

Kwa nini sikufa nilipokuwa ninatoka tumboni?

12 Kwa nini pakawa na magoti ya kunipokea

na matiti ili nipate kunyonyeshwa?

13 Kwa maana sasa ningekuwa nimepumzika kwa amani.

Ningekuwa nimelala na kupumzika

14 pamoja na wafalme na washauri wa dunia,

waliojijengea mahali ambapo sasa ni magofu,

15 pamoja na watawala waliokuwa na dhahabu,

waliozijaza nyumba zao kwa fedha.

16 Au kwa nini sikufichwa ardhini kama mtoto aliyezaliwa mfu,

kama mtoto mchanga ambaye kamwe hakuuona mwanga?

17 Huko waovu huacha kusumbua

na huko waliochoka hupumzika.

18 Wafungwa nao hufurahia utulivu wao,

hawasikii tena sauti ya kukemea ya kiongozi wa watumwa.

19 Wadogo na wakubwa wamo humo,

na mtumwa ameachiwa huru kutoka kwa bwana wake.

20 “Mbona nuru inawaangazia wale walio taabuni,

na hao wenye uchungu kupewa uhai,

21 wale wanaotamani kifo ambacho hakiji,

wale watafutao kufa zaidi ya kutafuta hazina iliyofichwa,

22 ambao hujawa na furaha,

na hushangilia wafikapo kaburini?

23 Kwa nini uhai hupewa mtu

ambaye njia yake imefichika,

ambaye Mungu amemzungushia boma?

24 Kwa maana kulia kwangu kwa uchungu kwanijia badala ya chakula;

kusononeka kwangu kunamwagika kama maji.

25 Lile nililokuwa naliogopa limenijia;

lile nililokuwa ninalihofia limenipata.

26 Sina amani, wala utulivu;

sina pumziko, bali taabu tu.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOB/3-2b7b03cbd95c9324befdebee068f04d2.mp3?version_id=1627—

Categories
Ayubu

Ayubu 4

Elifazi Anazungumza: Ayubu Ametenda Dhambi

1 Ndipo Elifazi Mtemani akajibu:

2 “Kama mtu akithubutu kuzungumza nawe,

kutakukasirisha?

Lakini ni nani awezaye

kujizuia asiseme?

3 Fikiri jinsi ambavyo umewafundisha watu wengi,

jinsi ambavyo umeitia nguvu

mikono iliyokuwa dhaifu.

4 Maneno yako yamewategemeza wale waliojikwaa;

umeyatia nguvu magoti yaliyokuwa dhaifu.

5 Lakini sasa hii taabu imekujia wewe,

nawe unashuka moyo;

imekupiga wewe,

nawe unafadhaika.

6 Je, kumcha Mungu kwako hakupaswi kuwa

ndiyo matumaini yako

na njia zako kutokuwa na lawama

ndilo taraja lako?

7 “Fikiri sasa: Ni mtu yupi asiye na hatia ambaye aliwahi kuangamia?

Ni wapi wanyofu waliwahi kuangamizwa?

8 Kwa jinsi ambavyo mimi nimechunguza,

wale walimao ubaya

na wale hupanda uovu,

huvuna hayo hayo hayo.

9 Kwa pumzi ya Mungu huangamizwa;

kwa mshindo wa hasira zake huangamia.

10 Simba anaweza kunguruma na kukoroma,

lakini bado meno ya simba mkubwa huvunjika.

11 Simba anaweza kuangamia kwa kukosa mawindo,

nao wana wa simba jike hutawanyika.

12 “Neno lililetwa kwangu kwa siri,

masikio yangu yakasikia mnongʼono wake.

13 Katikati ya ndoto za kutia wasiwasi wakati wa usiku,

hapo usingizi mzito uwapatapo wanadamu,

14 hofu na kutetemeka kulinishika

na kufanya mifupa yangu yote itetemeke.

15 Kuna roho aliyepita mbele ya uso wangu,

nazo nywele za mwili wangu zikasimama.

16 Yule roho akasimama,

lakini sikuweza kutambua kilikuwa kitu gani.

Umbo fulani lilisimama mbele ya macho yangu,

kukawa na ukimya kisha nikasikia sauti:

17 ‘Je, binadamu aweza kuwa mwadilifu kuliko Mungu?

Je, mtu aweza kuwa safi kuliko Muumba wake?

18 Kama Mungu hawaamini watumishi wake,

kama yeye huwalaumu malaika zake kwa kukosea,

19 ni mara ngapi zaidi wale waishio katika nyumba

za udongo wa mfinyanzi,

ambazo misingi yake ipo mavumbini,

ambao wamepondwa kama nondo!

20 Kati ya mawio na machweo

huvunjwa vipande vipande;

bila yeyote kutambua,

huangamia milele.

21 Je, kamba za hema yao hazikungʼolewa,

hivyo hufa bila hekima?’

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOB/4-86b253121a8a1580812f68757ea04d7d.mp3?version_id=1627—

Categories
Ayubu

Ayubu 5

Elifazi Anaendelea

1 “Ita kama unataka, lakini ni nani atakayekujibu?

Ni yupi kati ya hao watakatifu utakayemgeukia?

2 Kuweka uchungu moyoni humuua mpumbavu,

nao wivu humchinja mjinga.

3 Mimi mwenyewe nimemwona mpumbavu akistawi,

lakini ghafula nyumba yake ikawa imelaaniwa.

4 Watoto wake wako mbali na usalama,

hushindwa mahakamani bila mtetezi.

5 Wenye njaa huyala mavuno yake,

wakiyatoa hata katikati ya miiba,

nao wenye kiu huitamani sana mali yake.

6 Kwa maana taabu haioti kutoka kwenye udongo,

wala udhia hauchipui kutoka ardhini.

7 Lakini mwanadamu huzaliwa ili kutaabika,

kwa hakika kama cheche za moto zirukavyo kuelekea juu.

8 “Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu,

ningeliweka shauri langu mbele zake.

9 Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa,

miujiza isiyoweza kuhesabika.

10 Yeye huipa nchi mvua,

huyapeleka maji kunyesha mashamba.

11 Huwainua juu wanyonge,

nao wale waombolezao huinuliwa wakawa salama.

12 Huipinga mipango ya wenye hila,

ili mikono yao isifikie ufanisi.

13 Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao,

nayo mipango ya wadanganyifu huifagilia mbali.

14 Giza huwapata wakati wa mchana;

wakati wa adhuhuri hupapasa kama vile usiku.

15 Humwokoa mhitaji kutokana na upanga ulioko kinywani mwao;

huwaokoa kutokana na makucha ya wenye nguvu.

16 Kwa hiyo maskini analo tarajio,

nao udhalimu hufumba kinywa chake.

17 “Heri mtu yule ambaye Mungu humrudi;

kwa hiyo usidharau adhabu yake Mwenyezi.

18 Kwa kuwa hutia jeraha, lakini pia huyafunga;

huumiza, lakini mikono yake pia huponya.

19 Kutoka majanga sita atakuokoa;

naam, hata katika saba hakuna dhara litakalokupata wewe.

20 Wakati wa njaa atakukomboa wewe na kifo,

naye katika vita atakukomboa na pigo la upanga.

21 Utalindwa kutokana na kichapo cha ulimi,

wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia.

22 Utayacheka maangamizo na njaa,

wala hutakuwa na sababu ya kuwaogopa

wanyama wakali wa mwituni.

23 Kwa kuwa utakuwa na agano na mawe ya mashamba,

nao wanyama wa mwitu watakuwa na amani nawe.

24 Utajua ya kwamba hema lako li salama;

utahesabu mali zako wala hutakuta chochote kilichopungua.

25 Utajua ya kuwa watoto wako watakuwa wengi,

nao wazao wako wengi kama majani ya nchi.

26 Utaingia kaburini ukiwa na umri wa uzee mtimilifu,

kama masuke ya ngano yakusanywapo kwa wakati wake.

27 “Tumelichunguza hili, nalo ni kweli.

Hivyo lisikie na ulitendee kazi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOB/5-6d8359bc47546ef08b10cdb0bbcfb694.mp3?version_id=1627—

Categories
Ayubu

Ayubu 6

Ayubu Anajibu: Malalamiko Yangu Ni Ya Haki

1 Kisha Ayubu akajibu:

2 “Laiti uchungu wangu ungeweza kupimwa,

nayo taabu yangu yote ingewekwa kwenye mizani!

3 Kwa kuwa hakika ingekuwa nzito kuliko mchanga wa bahari zote,

kwa hiyo si ajabu maneno yangu yamekuwa ya haraka.

4 Mishale ya Mwenyezi iko ndani yangu,

roho yangu inakunywa sumu yake;

vitisho vya Mungu vimejipanga dhidi yangu.

5 Je, punda-mwitu hulia akiwa na majani,

au ngʼombe dume hulia akiwa na chakula?

6 Je, chakula kisicho na ladha huliwa bila chumvi,

au upo utamu katika ute mweupe wa yai?

7 Ninakataa kuvigusa;

vyakula vya aina hii hunichukiza.

8 “Laiti ningepata haja yangu,

kwamba Mungu angenijalia hilo nililotarajia,

9 kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda,

kuuachia mkono wake na kunikatilia mbali!

10 Ndipo bado ningekuwa na hii faraja,

furaha yangu katika maumivu makali:

kwamba sikuwa nimeyakana maneno yake yeye Aliye Mtakatifu.

11 “Ninazo nguvu gani, hata niendelee kutumaini?

Matazamio yangu ya mbele ni nini, hata niendelee kuwa mvumilivu?

12 Je, mimi nina nguvu za jiwe?

Je, mwili wangu ni shaba?

13 Je, ninao uwezo wowote wa kujisaidia mimi mwenyewe,

wakati ambapo mafanikio yamefukuziwa mbali nami?

14 “Mtu anayekata tamaa angetazamia moyo wa kujitoa wa rafiki zake,

hata kama akiacha uchaji wa Mwenyezi.

15 Lakini ndugu zangu sio wa kutegemewa,

ni kama vijito vya msimu,

ni kama vijito ambavyo hufurika

16 wakati vimefunikwa barafu iyeyukayo,

ambavyo hujazwa na theluji inayoyeyuka,

17 lakini hukauka majira ya ukame,

na wakati wa hari hutoweka katika mikondo yake.

18 Misafara hugeuka kutoka njia zake;

hukwea kwenda kwenye nchi ya ukiwa na kuangamia.

19 Misafara ya Tema inatafuta maji,

wafanyabiashara wa Sheba wanaosafiri

hutazama kwa matarajio.

20 Wamedhikika, kwa sababu walikuwa na matumaini;

wanafika huko, lakini wanahuzunika kwa kukosa walichotarajia.

21 Sasa nanyi mmethibitika kwamba hamna msaada wowote;

mnaona jambo la kutisha, nanyi mnaogopa.

22 Je, nimewahi kusema, ‘Toeni kitu kwa ajili yangu,

au mnilipie fidia kutoka mali zenu,

23 au niokoeni mikononi mwa adui,

au nikomboeni kutoka makucha ya wasio na huruma’?

24 “Nifundisheni, nami nitanyamaza kimya;

nionyesheni nilikokosea.

25 Tazama yalivyo ya kuumiza maneno ya kweli!

Lakini mabishano yenu yanathibitisha nini?

26 Je, mna maana ya kuyasahihisha ninayosema,

na kuyafanya maneno ya mtu anayekata tamaa kama upepo?

27 Mngeweza hata kupiga kura kwa ajili ya yatima,

na kubadilishana rafiki yenu na mali.

28 “Lakini sasa kuweni na huruma mkaniangalie mimi.

Je, ningeweza kusema uongo mbele zenu?

29 Tulizeni hasira, msiwe wadhalimu;

angalieni tena, kwa maana nimehatarisha uadilifu wangu.

30 Je, pana uovu wowote midomoni mwangu?

Je, kinywa changu hakiwezi kupambanua hila?

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOB/6-a917806091f902715f12b0b700f6fcc5.mp3?version_id=1627—