Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 13

Kuabudu Miungu Mingine

1 Kama nabii, au yule anayetabiri kwa njia ya ndoto, akijitokeza miongoni mwenu na akawatangazia ishara ya miujiza na ajabu,

2 ikiwa ishara au ajabu ya aliyozungumza ikatokea, naye akasema, “Na tufuate miungu mingine” (miungu ambayo hamjaifahamu) “na tuiabudu,”

3 kamwe msiyasikilize maneno ya nabii wala mwota ndoto huyo.BwanaMungu wenu anawajaribu kuangalia kama mnampenda kwa moyo wenu wote na kwa roho yenu yote.

4 NiBwanaMungu wenu ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.

5 Huyo nabii au mwota ndoto lazima auawe, kwa sababu amehubiri uasi dhidi yaBwanaMungu wenu, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa; amejaribu kuwageuza kutoka njia ambayoBwanaMungu wenu aliwaagiza mfuate. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.

6 Kama ndugu yako hasa, au mwanao au binti yako, au mke umpendaye, au rafiki yako wa karibu sana akikushawishi kwa siri, akisema, “Na twende tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo ninyi wala baba zenu hamkuifahamu,

7 miungu ya watu wanaowazunguka, ikiwa karibu au mbali, kutoka mwisho mmoja wa nchi mpaka mwingine),

8 usikubali wala usimsikilize. Usimhurumie! Usimwache wala usimkinge.

9 Hakika ni lazima auawe. Ni lazima mkono wako uwe wa kwanza katika kumuua kisha mikono ya watu wengine wote.

10 Mpigeni kwa mawe mpaka afe, kwa sababu alijaribu kuwageuza mtoke kwaBwanaMungu wenu ambaye aliwatoa Misri, kutoka nchi ya utumwa.

11 Kisha Israeli wote watasikia na kuogopa, wala hakuna mmoja miongoni mwenu atakayefanya uovu tena.

12 Kama mkisikia ikisemwa kwamba moja ya miji ambayoBwanaMungu wenu anawapa mkae ndani yake

13 kuna wanaume waovu wameinuka miongoni mwenu na wamewapotosha watu wa mji, wakisema, “Twendeni tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo hamkuifahamu),

14 ndipo itakubidi kuuliza, kupima na kuchunguza kwa makini. Kama ni kweli, tena ikihakikishwa kwamba jambo hili lichukizalo limefanyika miongoni mwenu,

15 kwa hakika ni lazima mwaue kwa upanga wale wote wanaoishi katika mji ule. Uharibuni kabisa, pamoja na watu wake na mifugo yake.

16 Kusanyeni nyara zote za mji katika uwanja wa wazi na kuuchoma mji kabisa pamoja na nyara zake zote kama sadaka ya kuteketezwa kwaBwanaMungu wenu. Utabaki kuwa magofu milele na hautajengwa tena.

17 Hakuna kimoja kati ya vitu vilivyolaaniwa kitakachokutwa mikononi mwenu, iliBwanaageuze hasira yake kali. Atawahurumia na kuwa na rehema kwenu pia kuongeza idadi yenu, kama alivyowaahidi baba zenu,

18 kwa sababu mnamtiiBwanaMungu wenu, mkizishika amri zake zote zile ninazowapa leo na kufanya lile lililo jema machoni pake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/13-aa3d692f62a1ad31f67c25e05d49d35b.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 14

Vyakula Vilivyo Najisi Na Vilivyo Safi

1 Ninyi ni watoto waBwanaMungu wenu. Msijichanje ama kujinyoa upara kwenye paji la uso kwa ajili ya aliyekufa,

2 kwa maana ninyi ni taifa takatifu kwaBwanaMungu wenu.Bwanaamewachagua ninyi kuwa taifa la kipekee kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia, mwe tunu yake.

3 Msile kitu chochote ambacho ni machukizo.

4 Hawa ndio wanyama mtakaokula: ngʼombe, kondoo, mbuzi,

5 kulungu, paa, kongoni, paa mweupe, mbuzi-mwitu, pofu na kondoo wa mlimani.

6 Mnaweza kumla mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika mara mbili, pia yule anayecheua.

7 Hata hivyo, miongoni mwa wale wanaocheua au wale walio na kwato zilizogawanyika kamwe msile ngamia, sungura na pelele. Iwapo wanacheua, lakini hawana kwato zilizogawanyika; ni najisi kwenu kwa taratibu za kiibada.

8 Nguruwe pia ni najisi; ingawa ana kwato zilizogawanyika, hacheui. Msile nyama yake wala kugusa mzoga wake.

9 Katika viumbe hai vyote viishivyo kwenye maji, mnaweza kula yeyote aliye na mapezi na magamba.

10 Lakini chochote kisicho na mapezi na magamba msile; kwenu ni najisi.

11 Mnaweza kula ndege yeyote aliye safi.

12 Lakini wafuatao msiwale: tai, furukombe, kipungu,

13 kengewa mwekundu, kengewa mweusi, mwewe wa aina yoyote,

14 kunguru wa aina yoyote,

15 mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga wa aina yoyote,

16 bundi, mumbi, bundi mkubwa,

17 mwari, nderi, mnandi,

18 korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo.

19 Wadudu wote warukao kwa makundi ni najisi kwenu, msiwale.

20 Lakini viumbe vyote vyenye mabawa vilivyo safi mwaweza kula.

21 Msile kitu chochote mtakachokuta kimekufa. Mnaweza kumpa mgeni yeyote anayeishi katika mojawapo ya miji yenu, naye anaweza kula au mnaweza kumuuzia mtu wa nchi nyingine. Lakini ninyi ni watu watakatifu kwaBwanaMungu wenu.

Msitokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.

Zaka

22 Hakikisheni mmetenga sehemu ya kumi ya mazao yote ya mashamba yenu kila mwaka.

23 Mtakula zaka za nafaka yenu, divai mpya, mafuta na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ngʼombe na ya kondoo na mbuzi mbele zaBwanaMungu wenu pale mahali atakapopachagua kama maskani kwa ajili ya Jina lake, ili kwamba mpate kujifunza kumheshimuBwanaMungu wenu daima.

24 Lakini ikiwa mahali pale ni mbali sana nanyi mmebarikiwa naBwanaMungu wenu na hamwezi kubeba zaka yenu (kwa sababu mahali paleBwanaatakapopachagua kuliweka Jina lake ni mbali sana),

25 basi badilisheni zaka yenu kuwa fedha, mkaichukue hiyo fedha mwende nayo mahaliBwanaMungu wenu atakapopachagua.

26 Tumieni hiyo fedha kununua chochote ukitakacho: ngʼombe, kondoo, divai au kinywaji chochote chenye chachu au chochote mnachotaka. Kisha ninyi na wa nyumbani mwenu mtaila mbele zaBwanaMungu wenu na kufurahi.

27 Msiache kuwajali Walawi waishio katika miji yenu, kwa kuwa hao hawana shamba wala urithi wao wenyewe.

28 Mwishoni mwa kila mwaka wa tatu, leteni zaka zote za mazao ya miaka ile na uyahifadhi kwenye miji yenu,

29 ili Walawi (ambao hawana mashamba wala urithi wao wenyewe) na wageni, yatima na wajane wanaoishi kwenye miji yenu wapate kuja kula na kushiba, iliBwanaMungu wenu apate kuwabariki ninyi katika kazi zote za mikono yenu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/14-3ccbf53850fb3f6d71aa3430deb33540.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 15

Mwaka Wa Kufuta Madeni

1 Kila mwisho wa miaka saba ni lazima mfute madeni.

2 Hivi ndivyo itakavyofanyika: Kila mkopeshaji atafuta mkopo aliomkopesha Mwisraeli mwenzake. Hatamtaka Mwisraeli mwenzake au ndugu yake amlipe hilo deni, kwa sababu wakati waBwanawa kufuta madeni umetangazwa.

3 Unaweza kudai malipo kwa mgeni, lakini lazima ufute kila deni ambalo unamdai ndugu yako.

4 Hata hivyo, hapatakuwepo maskini miongoni mwenu, kwa kuwa katika nchiBwanaMungu wenu anayowapa kuimiliki kama urithi wenu, atawabariki sana,

5 ikiwa tutamtiiBwanaMungu wenu kikamilifu na kuwa waangalifu kuyafuata maagizo haya yote ninayowapa leo.

6 Kwa kuwaBwanaMungu wenu atawabariki kama alivyoahidi, nanyi mtawakopesha mataifa mengi lakini hamtakopa kwa yeyote. Mtatawala mataifa mengi lakini hakuna taifa litakalowatawala ninyi.

7 Ikiwa kuna mtu maskini miongoni mwa ndugu zenu, katika mji wowote wa hiyo nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa, msiwe na moyo mgumu wala usimfumbie mkono ndugu yako aliye maskini.

8 Afadhali fungua mikono yako na umkopeshe kwa hiari chochote anachohitaji.

9 Jihadhari usijiwekee wazo hili ovu: “Mwaka wa saba, mwaka wa kufuta madeni umekaribia,” usije ukaonyesha nia mbaya kwa ndugu yako mhitaji na ukaacha kumpa chochote. Anaweza kumlalamikiaBwanadhidi yako nawe utakuwa umepatikana na hatia ya dhambi.

10 Mpe kwa ukarimu na ufanye hivyo bila kinyongo moyoni, ndipo kwa sababu ya hiliBwanaMungu wenu atakubariki katika kazi zako zote na kwa kila kitu utakachokiwekea mkono wako.

11 Siku zote watakuwepo watu maskini katika nchi. Kwa hiyo ninawaamuru mwe na mikono iliyokunjuliwa kuwaelekea ndugu zenu, kuwaelekea maskini na wahitaji katika nchi yenu.

Kuwaacha Huru Watumwa

12 Kama Mwebrania mwenzako, mwanaume au mwanamke, akijiuza kwako na kukutumikia miaka sita, katika mwaka wa saba ni lazima umwache aende zake akiwa huru.

13 Nawe wakati utakapomwachia usimwache aende mikono mitupu.

14 Mpe kwa uhuru kutoka zizi lako la kondoo na mbuzi, kutoka sakafu yako ya kupuria nafaka na kutoka mashinikizo yako ya kukamulia divai. Mpe kama vile ambavyoBwanaMungu wako alivyokubariki.

15 Kumbukeni kuwa ninyi mlikuwa watumwa huko Misri nayeBwanaMungu wenu aliwakomboa. Ndiyo sababu nimewapa agizo hili leo.

16 Lakini mtumishi wako akikuambia, “Sitaki kukuacha,” kwa sababu anakupenda wewe na jamaa yako naye anaridhika nawe,

17 ndipo utachukua chuma kidogo utoboe sikio lake mpaka hicho chuma kiingie kwenye ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako wa maisha. Ufanye vivyo hivyo kwa mtumishi wa kike.

18 Usifikiri kuwa kuna ugumu kumwacha mtumishi wako huru, kwa sababu utumishi wake kwako kwa miaka hii sita umekuwa wa thamani mara mbili ya ujira wa mtumishi wa kuajiriwa. NayeBwanaMungu wenu atakubarikia kwa kila kitu utakachofanya.

Wazaliwa Wa Kwanza Wa Wanyama

19 Wekeni wakfu kwaBwanaMungu wenu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa makundi yenu ya ngʼombe na ya mbuzi na kondoo. Maksai walio wazaliwa wa kwanza msiwafanyize kazi, wala msinyoe manyoya ya wazaliwa wa kwanza wa kondoo.

20 Kila mwaka ninyi na jamaa zenu mtapaswa kuwala mbele zaBwanaMungu wenu pale mahali atakapopachagua.

21 Kama mnyama ana dosari, akiwa ni kilema au kipofu au kama ana kilema kibaya, kamwe usimtoe dhabihu kwaBwanaMungu wenu.

22 Itawapasa kumla ninyi wenyewe katika miji yenu. Wote wasio safi na walio safi kwa desturi za kiibada mwaweza kula kama vile mnavyokula paa au kulungu.

23 Lakini kamwe msinywe damu; imwageni ardhini kama maji.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/15-02e56bd2cdd9be518a80ccea690ec933.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 16

Pasaka

1 Shikeni mwezi wa Abibu, na kuiadhimisha Pasaka yaBwanaMungu wenu, kwa sababu katika mwezi wa Abibu, Mungu aliwatoa Misri usiku.

2 Mtatoa dhabihu ya Pasaka ya mnyama kwaBwanaMungu wenu kutoka kundi lenu la mbuzi na kondoo au la ngʼombe, mahali pale ambapoBwanaatapachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake.

3 Msile nyama hiyo pamoja na mikate iliyotiwa chachu, lakini kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, mikate ya kujitesa, kwa sababu mliondoka Misri kwa haraka, ili kwamba siku zote za maisha yenu mpate kukumbuka wakati wenu wa kuondoka Misri.

4 Chachu isionekane katika mali zenu katika nchi yenu yote kwa siku saba. Nyama yoyote ya dhabihu mtakayotoa jioni ya siku ya kwanza isibakizwe mpaka asubuhi.

5 Kamwe msitoe dhabihu ya Pasaka katika mji wowote ambaoBwanaMungu wenu amewapa,

6 isipokuwa mahali atakapopachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake. Hapo ndipo lazima mtoe dhabihu ya Pasaka jioni, jua litakapotua, iwe kumbukumbu yenu ya kutoka Misri.

7 Okeni na mle mahali pale ambapoBwanaMungu wenu atakapopachagua, kisha asubuhi mrudi kwenye mahema yenu.

8 Kwa siku sita mtakula mikate isiyotiwa chachu na siku ya saba fanyeni kusanyiko kwa ajili yaBwanaMungu wenu na msifanye kazi.

Sikukuu Ya Mavuno

9 Mhesabu majuma saba tangu wakati mnapoanza kuchukua mundu kuvuna nafaka.

10 Kisha msherehekee Sikukuu ya Majuma kwaBwanaMungu wenu kwa kutoa sadaka ya hiari kwa kadiri ya baraka ambayoBwanaMungu wenu amewapa.

11 Shangilieni mbele zaBwanaMungu wenu mahali atakapopachagua kama makao ya Jina lake, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi walio katika miji yenu, na wageni, yatima na wajane waishio miongoni mwenu.

12 Kumbukeni kwamba mlikuwa watumwa kule Misri na mfuate amri hizi kwa uangalifu.

Sikukuu Ya Vibanda

13 Adhimisheni sikukuu ya vibanda kwa siku saba baada ya kukusanya mazao yenu ya nafaka na kukamua zabibu.

14 Mfurahie sikukuu yenu, ninyi, wana wenu, binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi, wageni, yatima na wajane ambao wanaishi katika miji yenu.

15 Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu yaBwanaMungu wenu katika mahali atakapopachaguaBwana. Kwa kuwaBwanaMungu wenu atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.

16 Wanaume wenu wote lazima wajitokeze mara tatu kwa mwaka mbele zaBwanaMungu wenu mahali atakapopachagua: kwa ajili ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma, na Sikukuu ya Vibanda. Hakuna mtu atakayejitokeza mbele zaBwanamikono mitupu:

17 Kila mmoja wenu ni lazima alete zawadi kulingana na jinsi ambavyoBwanaMungu wenu alivyowabariki.

Waamuzi

18 Wateue waamuzi na maafisa kwa kila kabila lenu katika kila mji ambaoBwanaMungu wenu anawapa, nao watawaamua watu kwa usawa.

19 Msipotoshe haki wala msifanye upendeleo. Msikubali rushwa kwa sababu rushwa hupofusha macho ya wenye busara na kugeuza maneno ya wenye haki.

20 Mfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa.

Kuabudu Miungu Mingine

21 Msisimamishe nguzo yoyote ya Ashera kando ya madhabahu mliyomjengeaBwanaMungu wenu,

22 wala msisimamishe jiwe la kuabudu, kwa maanaBwanaMungu wenu anavichukia vitu hivi.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/16-d4f6f98e5664fa92f4ef6cd7f524d45f.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 17

1 MsimtoleeBwanaMungu wenu dhabihu ya maksai au kondoo ambaye ana dosari yoyote au hitilafu ndani yake, kwa kuwa hilo litakuwa chukizo kwake.

2 Ikiwa mwanaume au mwanamke anayeishi kati ya mojawapo ya miji akupayoBwana, anakutwa anafanya uovu mbele zaBwanaMungu wenu, kwa kuvunja Agano lake,

3 naye amekwenda kinyume na agizo langu kuabudu miungu mingine na kuisujudia, kama vile jua, mwezi au nyota za angani,

4 hili likiwa limeletwa mbele yenu, ni lazima kulichunguza kikamilifu. Ikiwa ni kweli na kuwa limehakikishwa kwamba hili ni chukizo lililofanyika katika Israeli,

5 mchukueni huyo mwanaume au mwanamke ambaye amelifanya tendo hili ovu kwenye lango la mji wenu na kumpiga mawe mtu huyo mpaka afe.

6 Kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu mtu huyo atauawa, bali hakuna mtu atakayeuawa kwa ushuhuda wa shahidi mmoja tu.

7 Ni lazima kwanza mikono ya mashahidi itangulie kumuua huyo mtu, kisha mikono ya watu wote. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.

Mahakama Za Sheria

8 Kama mashauri yanaletwa katika mahakama zenu ambayo ni magumu zaidi kwenu kuyaamua, ikiwa ni umwagaji wa damu, madai au mashambulio, yapelekeni mahali ambapoBwanaMungu wenu atapachagua.

9 Nendeni kwa makuhani, ambao ni Walawi, na kwa mwamuzi ambaye atakuwa kazini wakati huo. Ulizeni kwao nao watawapa maamuzi.

10 Ni lazima mtende sawasawa na maamuzi watakayowapa mahaliBwanaatakapopachagua. Kuweni waangalifu kufanya kila kitu watakachowaongoza kufanya.

11 Fanyeni sawasawa na sheria wanayowafundisha na maamuzi wanayowapa. Msigeuke mkono wa kuume au kushoto kuacha kufanya yale wanayowaambia.

12 Mwanaume atakayeonyesha dharau kwa mwamuzi au kwa kuhani ambaye amewekwa kumtumikiaBwanaMungu wenu lazima auawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli.

13 Watu wote watasikia na kuogopa, nao hawatakuwa wenye kudharau tena.

Mfalme

14 Wakati utakapoingia katika nchi anayowapaBwanaMungu wenu kuimiliki na kukaa humo, nanyi mkasema, “Na tumweke mfalme juu yetu kama mataifa yanayotuzunguka,”

15 kuweni na uhakika wa kumweka mfalme juu yenu ambayeBwanaMungu wenu atamchagua. Ni lazima atoke miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msimweke mgeni juu yenu ambaye si ndugu wa Kiisraeli.

16 Hata hivyo, kamwe mfalme asijipatie hesabu kubwa ya farasi kwa ajili yake mwenyewe, au kuwafanya watu warudi Misri ili kupata farasi zaidi, kwa maanaBwanaamekuambia, “Hamtairudia njia ile tena.”

17 Kamwe asioe wake wengi, la sivyo moyo wake utapotoka. Kamwe asijilimbikizie kiasi kikubwa cha fedha na dhahabu.

18 Atakapokuwa amekalia kiti cha ufalme wake, ajiandikie kwenye kitabu nakala ya sheria kwa ajili yake mwenyewe kutoka zile sheria za makuhani ambao ni Walawi.

19 Atakuwa na nakala hiyo, naye ataisoma siku zote za maisha yake ili kwamba ajifunze kumheshimuBwanaMungu wake na kufuata kwa uangalifu maneno yote ya sheria hii na amri hizi,

20 naye asijifikirie kuwa ni bora kuliko ndugu zake na kuipotosha sheria. Ndipo yeye na wazao wake watatawala katika ufalme wake kwa muda mrefu katika Israeli.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/17-f2aa0ced8133fbbedcb2219aab4b0e7d.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 18

Sadaka Kwa Makuhani Na Walawi

1 Makuhani ambao ni Walawi, yaani kabila lote la Lawi, hawatakuwa na mgawo wala urithi pamoja na Israeli. Wataishi kwa sadaka zitolewazo kwa ajili yaBwanaza kuteketezwa kwa moto, kwa maana huo ndio urithi wao.

2 Hawatakuwa na urithi miongoni mwa ndugu zao;Bwanandiye urithi wao, kama alivyowaahidi.

3 Hili ndilo fungu la makuhani kutoka kwa watu watakaotoa dhabihu ya fahali au kondoo: mguu wa mbele, mataya na matumbo.

4 Mtawapa malimbuko ya nafaka zenu, divai mpya, mafuta na sufu ya kwanza kutoka manyoya ya kondoo zenu,

5 kwa kuwaBwanaMungu wenu amewachagua pamoja na wazao wao kutoka makabila yenu kusimama na kuhudumu katika jina laBwanasiku zote.

6 Ikiwa Mlawi atahama kutoka mmojawapo ya miji yenu popote katika Israeli ambapo anaishi, akaja kwa moyo wote mahali ambapoBwanaatapachagua,

7 anaweza akahudumu katika jina laBwanaMungu wake kama Walawi wenzake wote wanaohudumu hapo mbele zaBwana.

8 Atashiriki sawa katika mafao yao, hata kama amepokea fedha kutoka mauzo ya mali ya jamaa yake.

Matendo Ya Machukizo

9 Wakati mtakapoingia katika nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa, msijifunze kuiga njia za machukizo za mataifa ya huko.

10 Asionekane mtu yeyote miongoni mwenu ampitishaye mwanawe au binti yake katika moto, atakayefanya uaguzi, ulozi, anayetabiri nyakati, anayejishughulisha na uchawi,

11 wala arogaye kwa kupiga mafundo, wala mwaguzi au anayeabudu mizimu, wala awaombaye wafu.

12 Mtu yeyote afanyaye mambo haya ni chukizo kwaBwana, tena ni kwa sababu ya matendo haya ya kuchukiza wayafanyayo ndiyo maanaBwanaMungu wenu atayafukuza mataifa hayo mbele yenu.

13 Kamwe msilaumiwe mbele zaBwanaMungu wenu.

Nabii

14 Mataifa mtakayowafukuza husikiliza wale wafanyao ulozi na uaguzi. Lakini kwenu ninyi,BwanaMungu wenu hajawaruhusu kufanya hivyo.

15 BwanaMungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msikilizeni yeye.

16 Kwa kuwa hivi ndivyo mlivyomwombaBwanaMungu wenu kule Horebu siku ile ya kusanyiko, wakati mliposema, “Na tusiisikie sauti yaBwanaMungu wetu, wala kuuona moto huu mkubwa tena, ama sivyo tutakufa.”

17 Bwanaakaniambia: “Wanachosema ni vyema.

18 Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zao; nitaweka maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia kila kitu nitakachomwamuru.

19 Kama mtu yeyote hatasikiliza maneno yangu ambayo huyo nabii atayasema kwa Jina langu, mimi mwenyewe nitamwajibisha.

20 Lakini nabii ambaye atathubutu kusema kwa Jina langu kitu chochote ambacho sikumwamuru akiseme, au nabii ambaye husema kwa jina la miungu mingine ni lazima auawe.”

21 Mnaweza kuulizana wenyewe, “Tutawezaje kujua wakati ujumbe haukusemwa naBwana?”

22 Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina laBwanahakikutokea au kutimia, huo ni ujumbe ambaoBwanahakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/18-c2b66949ba184d38da65476c92845154.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 19

Miji Ya Makimbilio

1 WakatiBwanaMungu wenu atakapokuwa amewaangamiza mataifa ambayo nchi yao anawapa ninyi, wakati mtakapokuwa mmewafukuza na kuishi katika miji yao na nyumba zao,

2 ndipo mtenge miji mitatu iliyopo katikati ya nchi kwa ajili yenu, katika nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa kuimiliki.

3 Jengeni barabara katika miji hiyo na kuigawa mara tatu, nchi anayowapaBwanaMungu wenu kama urithi, ili kwamba yeyote amuuaye mtu aweze kukimbilia humo.

4 Hii ndiyo kanuni kuhusu mtu amuuaye mwingine na kukimbilia humo kuokoa maisha yake, yaani, yeye amuuaye jirani yake bila kukusudia, wala hakumchukia kabla ya hapo.

5 Kwa mfano, mtu aweza kwenda msituni na jirani yake kukata miti, naye anapozungusha shoka kuangusha mti, shoka linaweza kuchomoka kutoka kwenye mpini na kumpiga jirani yake na kumuua. Yule mtu anaweza kukimbilia katika mmojawapo ya miji hii na kuokoa maisha yake.

6 Kama sivyo, mlipiza kisasi cha damu anaweza kumfuatilia kwa hasira kali, naye akamkamata na kumuua kama umbali ni mrefu sana hata ingawa hastahili kifo, kwa sababu amemuua jirani yake bila kukusudia.

7 Hii ndiyo sababu nimewaagiza ninyi kutenga miji mitatu ya makimbilio kwa ajili yenu.

8 KamaBwanaMungu wenu akipanua nchi yenu, kama alivyoahidi kwa kiapo kwa baba zenu na kuwapa nchi yote aliyowaahidi,

9 kwa sababu mmefuata kwa uangalifu sheria zote ninazowaamuru leo, kumpendaBwanaMungu wenu na kuenenda siku zote katika njia zake, ndipo mtenge miji mingine, mitatu zaidi.

10 Fanyeni hivi ili damu isiyo na hatia isimwagwe katika nchi yenu, ambayoBwanaMungu wenu anawapa kama urithi wenu, ili kwamba msije mkawa na hatia ya kumwaga damu.

11 Lakini kama mtu anamchukia ndugu yake, akamvizia, akamshambulia na kumuua, kisha akakimbilia katika mmojawapo ya miji hii,

12 wazee wa mji wake watatuma ujumbe kwake, kumleta kutoka mji ule na kumkabidhi mlipiza kisasi cha damu kumuua.

13 Msimwonee huruma. Lazima mwondoe katika Israeli hatia ya umwagaji damu isiyo na hatia ili kwamba mpate kufanikiwa.

14 Usisogeze jiwe la mpaka wa jirani yako ambao uliwekwa na wale waliokutangulia katika urithi upokeao katika nchiBwanaMungu wako anayowapa kuimiliki.

Mashahidi

15 Shahidi mmoja hatoshi kumtia hatiani mtu kwa uhalifu au kosa lolote ambalo anaweza kuwa amelitenda. Lazima shauri lolote lithibitishwe kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.

16 Kama shahidi mwenye nia ya kumdhuru mwingine akisimama kumshtaki mtu kwa uhalifu,

17 watu wawili wanaohusika katika mabishano lazima wasimame mbele zaBwanana mbele ya makuhani na waamuzi ambao wako kazini wakati huo.

18 Waamuzi lazima wafanye uchunguzi kwa makini na shahidi akionekana kuwa ni mwongo, akitoa ushuhuda wa uongo dhidi ya ndugu yake,

19 basi mtende kama alivyotaka kumtendea ndugu yake. Ni lazima mwondoe uovu miongoni mwenu.

20 Watu watakaosalia watasikia hili na kuogopa, uovu kama huo kamwe hautatendeka tena miongoni mwenu.

21 Msionyeshe huruma, uhai kwa uhai, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/19-17631560fea3017c87fda7a33e32af0f.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 20

Kwenda Vitani

1 Mtakapokwenda vitani kupigana na adui zenu na mkaona farasi na magari ya vita na jeshi kubwa kuliko lenu, msiwaogope, kwa sababuBwanaMungu wenu aliyewatoa kutoka Misri, atakuwa pamoja nanyi.

2 Wakati mtakapokaribia kwenda vitani, kuhani atakuja mbele na kuhutubia jeshi.

3 Atasema: “Sikia, ee Israeli, leo unakwenda vitani kupigana na adui zako. Usife moyo wala usiogope, usitishwe wala usitiwe hofu mbele yao.

4 Kwa kuwaBwanaMungu wenu ndiye huenda pamoja nanyi kuwapigania dhidi ya adui zenu na kuwapatia ushindi.”

5 Maafisa wataliambia jeshi: “Je, kuna yeyote aliyejenga nyumba mpya ambayo haijawekwa wakfu? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akaiweka wakfu.

6 Je, kuna yeyote aliyepanda shamba la mizabibu na hajaanza kulifurahia? Yeye na arudi nyumbani, au sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akalifurahia.

7 Je, kuna yeyote aliyeposa mwanamke na hajamwoa? Yeye na arudi nyumbani, ama sivyo anaweza kufa vitani na mtu mwingine akamwoa.”

8 Kisha maafisa wataongeza haya, “Je, kuna mtu anayeogopa ama kufa moyo? Yeye na arudi nyumbani ili ndugu zake nao wasije wakafa moyo pia.”

9 Wakati maafisa watakapomaliza kuzungumza na jeshi, watawateua wakuu wa vikosi.

10 Wakati mtakapokwenda kushambulia mji, wapeni watu wake masharti ya amani.

11 Wakikubali na kuwafungulia malango yao, watu wake wote watawatumikia kwa kufanya kazi ngumu na watawatumikia.

12 Ikiwa watakataa kufanya mapatano ya amani na wakiwaingiza katika vita, basi mtauzunguka mji huo kwa vita.

13 WakatiBwanaMungu wenu atakapouweka mji huo mkononi mwenu, waueni kwa upanga wanaume wote waliomo ndani yake.

14 Kwa upande wa wanawake, watoto, mifugo na kila kitu kingine chochote ndani ya huo mji, mnaweza kuvichukua kama nyara kwa ajili yenu. Nanyi mnaweza kuzitumia hizo nyara ambazoBwanaMungu wenu amewapa kutoka kwa adui zenu.

15 Hivi ndivyo mtakavyofanya kwa miji yote ambayo iko mbali nanyi, ambayo haimilikiwi na mataifa ya karibu.

16 Hata hivyo, katika miji ya mataifa ambayoBwanaMungu wenu anawapa kama urithi, msiache kitu chochote hai kinachopumua.

17 Waangamizeni kabisa Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, kamaBwanaMungu wenu alivyowaamuru.

18 La sivyo, watawafundisha kufuata mambo yote ya machukizo wanayofanya wakiabudu miungu yao, nanyi mtatenda dhambi dhidi yaBwanaMungu wenu.

19 Wakati mtakapouzunguka mji kwa vita kwa muda mrefu, mkipigana dhidi yake ili kuuteka, msiharibu miti yake kwa kuikata kwa shoka, kwa sababu mtaweza kula matunda yake. Hivyo msiikate. Je, miti hiyo ya mashambani ni watu, hata muizingire?

20 Hata hivyo, mnaweza kuikata miti ambayo sio miti ya matunda na kuitumia kujenga ngome, mpaka mji ulio katika vita na ninyi utakapoanguka.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/20-3a4de4468fde17501e21364fee187822.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 21

Upatanisho Kuhusu Mauaji

1 Kama mtu akikutwa ameuawa, naye amelala kwenye shamba katika nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa kuimiliki, wala haijulikani ni nani aliyemuua,

2 wazee wenu na waamuzi watatoka na kupima umbali kutoka maiti alipolala mpaka kwenye miji ya jirani.

3 Kisha wazee wa ule mji ulio karibu zaidi na yule maiti watamchukua mtamba ambaye hajapata kufanyishwa kazi na ambaye hajafungwa nira,

4 na kumpeleka kwenye bonde ambalo halijapata kulimwa au kupandwa mazao na ambapo kuna chemchemi itiririkayo. Huko kwenye hilo bonde, wazee watamvunja yule mtamba shingo.

5 Makuhani, hao wana wa Lawi, watasogea mbele, kwa kuwaBwanaMungu wenu, amewachagua kuhudumu na kutoa baraka katika jina laBwana, na kuamua mashauri yote ya mabishano na mashambulio.

6 Ndipo wazee wote wa mji ulio karibu zaidi na huyo maiti watanawa mikono yao juu ya huyo mtamba ambaye shingo yake imevunjwa huko kwenye bonde,

7 nao watatangaza: “Mikono yetu haikumwaga damu hii, wala macho yetu hayakuona likifanyika.

8 EeBwana, ukubali upatanisho kwa watu wako Israeli, ambao umewakomboa, wala usiwahesabie watu wako hatia ya damu ya mtu asiyekuwa na hatia.” Nayo damu iliyomwagika itakuwa imefanyiwa upatanisho.

9 Hivyo mtakuwa mmejitakasa wenyewe kutoka hatia ya kumwaga damu isiyokuwa na hatia, kwa kuwa mmefanya lile lililo sawa mbele za macho yaBwana.

Kuoa Mwanamke Mateka

10 Mkienda vitani kupigana na adui zenu nayeBwanaMungu wenu akawatia adui mikononi mwenu, nanyi mkachukua mateka,

11 kama ukiona miongoni mwa mateka mwanamke mzuri wa sura nawe wavutwa naye, waweza kumwoa akawa mke wako.

12 Mlete nyumbani mwako, anyoe nywele na kukata kucha zake,

13 avue nguo alizokuwa amevaa alipotekwa. Baada ya kuishi nyumbani mwako na kumwombolezea baba yake na mama yake kwa mwezi mzima, ndipo utakapoweza kumwendea na kuwa mume wake naye atakuwa mke wako.

14 Lakini kama hutaendelea kupendezwa naye, mwache aende popote anapotaka. Kamwe huwezi kumuuza au kumtendea kama mtumwa, kwa sababu utakuwa umemvunjia heshima.

Haki Ya Mzaliwa Wa Kwanza

15 Kama mwanaume ana wake wawili, naye anampenda mmoja na mwingine hampendi na wote wawili wamemzalia wana wa kiume, lakini mwana mzaliwa wa kwanza ni wa yule mke asiyempenda,

16 wakati anapotoa wosia wa mali yake kwa wanawe, kamwe asitoe haki za mzaliwa wa kwanza kwa mwana wa mke ampendaye kwa upendeleo, badala ya mzaliwa hasa wa kwanza, ambaye ni mwana wa mke ambaye hampendi.

17 Ni lazima amkubali mwana wa mke asiyempenda kama mzaliwa wa kwanza kwa kumpa sehemu ya vile vyote alivyo navyo maradufu. Mwana huyo ni ishara ya kwanza ya nguvu za baba yake. Haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye.

Mwana Mwasi

18 Kama mtu ana mwana mkaidi na mwasi ambaye hamtii baba yake na mama yake, na hasikii wazazi wanapomrudi,

19 baba yake na mama yake watamleta kwa wazee kwenye lango la mji wake.

20 Watawaambia wazee, “Huyu mwanetu ni mkaidi na mwasi. Hatutii sisi, yeye ni mpotovu na mlevi.”

21 Kisha wanaume wote wa mjini mwake watampiga kwa mawe mpaka afe. Ndivyo imewapasa kuondoa maovu kati yenu. Israeli yote itasikia hili na kuogopa.

Sheria Mbalimbali

22 Kama mtu ana hatia ya kosa linalompasa kuuawa naye akauawa, mwili wake utaangikwa mtini,

23 kamwe msiuache mwili wake mtini usiku kucha. Hakikisheni mnauzika mwili wake siku ile ile, kwa sababu kila mtu anayeangikwa mtini yupo chini ya laana ya Mungu. Msiinajisi nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa kama urithi wenu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/21-c7d6cd2392c23cd0f166dbea026bbcb9.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 22

1 Kama ukimwona ngʼombe au kondoo wa ndugu yako anapotea, usipuuze, bali uhakikishe unamrudisha kwa mwenyewe.

2 Ikiwa huyo ndugu haishi karibu nawe au kama hufahamu yeye ni nani, mchukue nyumbani kwako huyo mnyama umweke mpaka mwenyewe aje kumtafuta. Ndipo umrudishie.

3 Fanya vivyo hivyo ukimkuta punda wa nduguyo au joho lake au chochote alichopoteza. Usipuuze jambo hilo.

4 Kama ukimwona punda wa nduguyo au ngʼombe wake ameanguka barabarani, usipuuze jambo hilo. Msaidie asimame kwa miguu yake.

5 Haimpasi mwanamke kuvaa nguo za kiume wala mwanaume kuvaa nguo za kike, kwa maanaBwanaMungu wenu anachukia yeyote ambaye hufanya hivi.

6 Kama ukikuta kiota cha ndege kando ya barabara, iwe juu ya mti au chini, naye ndege amelala juu ya makinda au mayai, usimchukue huyo ndege pamoja na makinda yake.

7 Waweza kuchukua makinda, lakini uwe na hakika ya kumwacha huyo ndege, ili upate kufanikiwa na uweze kuishi maisha marefu.

8 Wakati unapojenga nyumba mpya, fanya ukuta wa kuzuia kandokando ya dari ili usijiletee hatia ya kumwaga damu juu ya nyumba yako ikiwa yeyote ataanguka kutoka humo.

9 Usipande aina mbili za mbegu katika shamba lako la mizabibu; ikiwa utafanya hivyo, si mazao utakayopanda tu yatakuwa najisi, bali nayo matunda ya shamba la mizabibu pia.

10 Usilime kwa maksai aliyefungwa nira pamoja na punda.

11 Usivae nguo za sufu na kitani zilizofumwa pamoja.

12 Fanya vishada kwenye pembe nne za joho unalovaa.

Kukiuka Taratibu Za Ndoa

13 Ikiwa mtu atamwoa mke na, baada ya kufanya naye tendo la ndoa, akamchukia,

14 akimsingizia na kumwita jina baya, akisema, “Nilimwoa mwanamke huyu, lakini nilipomkaribia sikupata uthibitisho wa ubikira wake”

15 ndipo baba na mama wa msichana wataleta uthibitisho kwamba alikuwa bikira kwa wazee wa mji kwenye lango.

16 Baba wa msichana atawaambia wazee, “Nilimwoza binti yangu kwa huyu mwanaume, lakini hampendi.

17 Sasa amemsingizia na kusema, ‘Sikumkuta huyu binti akiwa bikira.’ Lakini hapa kuna uthibitisho wa ubikira wa binti yangu.” Kisha wazazi wake wataonyesha nguo zake kwa wazee wa mji,

18 nao wazee watamchukua huyo mwanaume na kumwadhibu.

19 Watamtoza shekeli mia mojaza fedha na kupewa wazazi wa msichana, kwa sababu mwanaume huyu amempa bikira wa Kiisraeli jina baya. Ataendelea kuwa mke wake; kamwe hawezi kumpa talaka siku zote za maisha yake.

20 Hata hivyo, kama shtaka ni la kweli na hakuna uthibitisho juu ya ubikira wa huyo msichana ulioweza kupatikana,

21 huyo msichana ataletwa kwenye mlango wa nyumba ya baba yake, na hapo watu wa mji wake watampiga kwa mawe hadi afe. Amefanya kitu cha aibu katika Israeli kwa kufanya ukahaba akiwa nyumbani kwa babaye. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.

22 Ikiwa mwanaume atakutwa akizini na mke wa mtu mwingine, wote wawili, mwanaume na mwanamke aliyezini naye, lazima wauawe. Lazima mwondoe uovu katika Israeli.

23 Ikiwa mwanaume atakutana na bikira mjini ambaye ameposwa na mtu akazini naye,

24 utawachukua wote wawili kwenye lango la mji na kuwapiga kwa mawe mpaka wafe; yule msichana kwa kuwa alikuwa mjini na hakupiga kelele kuomba msaada, na yule mwanaume kwa sababu amemtenda jeuri mke wa mtu mwingine. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.

25 Lakini ikiwa itatokea mwanaume akakutana na msichana aliyeposwa huko mashambani, akambaka, mwanaume aliyefanya hivi peke yake ndiye atakayeuawa.

26 Usimtendee msichana yule jambo lolote; hajafanya dhambi inayostahili kifo. Shauri hili ni kama lile la yeyote ambaye anamshambulia na kumuua kwa makusudi jirani yake,

27 kwa maana mwanaume huyo alimkuta msichana huko mashambani, na ingawa msichana aliyeposwa alipiga kelele, hapakuwa na mtu wa kumwokoa.

28 Ikiwa itatokea mwanaume akutane na bikira ambaye hajaposwa na kumbaka nao wakakutwa,

29 mwanaume atamlipa baba wa msichana shekeli hamsiniza fedha. Ni lazima amwoe huyo msichana, kwa maana amemfanyia jeuri. Kamwe hawezi kumpa talaka siku zote za maisha yake.

30 Mwanaume asimwoe mke wa baba yake; kamwe asidhalilishe kitanda cha baba yake.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/22-a5dbdccab002c86593a6a6accc4bd6b4.mp3?version_id=1627—