Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 3

Kushindwa Kwa Ogu Mfalme Wa Bashani

1 Kisha tukageuka tukakwea kufuata njia iliyoelekea Bashani, Ogu mfalme wa Bashani akaondoka na jeshi lake lote kupigana na sisi huko Edrei.

2 Bwanaakaniambia, “Usimwogope kwa kuwa nimekwisha mkabidhi mikononi mwako pamoja na jeshi lake lote na nchi yake. Umfanyie sawasawa na ulivyomfanyia Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.”

3 HivyoBwanaMungu wetu pia akamweka Ogu mfalme wa Bashani pamoja na jeshi lake lote mikononi mwetu. Tuliwaangamiza wote, hakubakia hata mmoja.

4 Wakati huo tuliteka miji yake yote. Hakuna mji hata mmoja kati ya ile sitini ambao hatukuuteka, yaani eneo lote la Argobu, utawala wa Mfalme Ogu katika Bashani.

5 Miji yote hii ilijengewa ngome zenye kuta ndefu zenye malango na makomeo, pia kulikuwako na vijiji vingi ambavyo havikujengewa kuta.

6 Tuliwaangamiza kabisa, kama tulivyomfanyia Sihoni mfalme wa Heshboni, tukiangamiza kila mji, yaani wanaume, wanawake na watoto.

7 Lakini wanyama wote wa kufuga pamoja na nyara kutoka kwenye miji yao tulichukua vikawa vyetu.

8 Hivyo kwa wakati huo tukachukua kutoka kwa wafalme hawa wawili wa Waamori nchi ya mashariki ya Yordani, kutoka Bonde la Arnoni mpaka kufika kwenye Mlima Hermoni.

9 (Wasidoni huuita mlima huo Sirioni, nao Waamori huuita Seniri.)

10 Tuliteka miji yote kwenye uwanda wa juu, Gileadi yote, Bashani yote mpaka kufika Saleka na Edrei, miji ya utawala wa Ogu huko Bashani.

11 (Mfalme Ogu wa Bashani ndiye peke yake aliyesalia miongoni mwa mabaki ya Warefai. Kitanda chake kilikuwa cha chuma chenye urefu wa dhiraa tisana upana wa dhiraa nne.Mpaka sasa kinaweza kuonekana katika mji wa Waamoni wa Raba.)

Mgawanyo Wa Nchi Mashariki Ya Yordani

12 Katika nchi tuliyoiteka wakati ule, niliwapa kabila la Reubeni na Gadi eneo lililoko kaskazini la Aroeri kando ya Bonde la Arnoni, na nusu ya eneo la milima ya Gileadi, pamoja na miji yake.

13 Kisha nusu ya kabila la Manase niliwapa sehemu ya Gileadi iliyobaki pamoja na Bashani yote, ambayo ilikuwa utawala wa Ogu. (Eneo lote la Argobu katika Bashani lilikuwa linajulikana kama nchi ya Warefai.

14 Yairi, mzao wa kabila la Manase, alichukua eneo lote la nchi ya Argobu hadi kufikia mpaka wa Wageshuri na Wamaaka, ukaitwa kwa jina lake; kwa hiyo mpaka leo hii Bashani inaitwa Hawoth-Yairi.)

15 Nikampa Makiri nchi ya Gileadi.

16 Lakini niliwapa Wareubeni na Wagadi eneo kuanzia Gileadi hadi Bonde la Arnoni (katikati ya bonde ulikuwa ndio mpaka), kuelekea mpaka Mto Yaboki, ambao ndio mpaka wa Waamoni.

17 Kwa upande wa magharibi mpaka wao ulikuwa Yordani katika Araba, toka ziwa Galilaya hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi), kwenye miteremko ya Pisga upande wa mashariki.

18 Wakati huo nilikuamuru: “BwanaMungu wako amekupa nchi hii uimiliki. Lakini ni lazima wanaume wenu wote wenye uwezo, wakiwa wamejiandaa tayari kwa vita, wavuke ngʼambo wakiwatangulia ndugu zako Waisraeli.

19 Lakini wake zenu, watoto wenu na mifugo yenu (kwani najua mnayo mifugo mingi) wanaweza kukaa katika miji niliyowapa,

20 mpaka hapoBwanaatakapowapa ndugu zenu kupumzika kama alivyowapa ninyi, wao pia wamiliki ile nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa, ngʼambo ya Yordani. Baada ya hapo, kila mmoja wenu anaweza kurudi kwenye milki niliyowapa.”

Mose Akatazwa Kuvuka Yordani

21 Wakati huo nilimwamuru Yoshua, “Umejionea kwa macho yako mwenyewe yale yote ambayoBwanaMungu wenu amewafanyia wafalme hawa wawili.Bwanaatazifanyia falme zote huko mnakokwenda vivyo hivyo.

22 Msiwaogope,BwanaMungu wenu atapigana kwa ajili yenu.”

23 Wakati huo nilimsihiBwana:

24 “EeBwanaMwenyezi, umemwonyesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza. Kwa kuwa ni mungu yupi aliye mbinguni au duniani anayeweza kufanya kazi na matendo makuu kama ufanyayo wewe?

25 Acha niende nikaione hiyo nchi nzuri ngʼambo ya Yordani, ile nchi nzuri ya vilima na Lebanoni.”

26 Lakini kwa sababu yenuBwanaalinikasirikia na hakutaka kunisikiliza.Bwanaaliniambia, “Hilo latosha; usiseme nami jambo hili tena.

27 Kwea juu ya kilele cha Pisga uangalie magharibi, kaskazini, kusini na mashariki. Iangalie hiyo nchi kwa macho yako, kwa vile wewe hutavuka Yordani.

28 Lakini mwagize Yoshua, mtie moyo na umtie nguvu, kwa kuwa yeye atawaongoza watu hawa hadi ngʼambo na kuwarithisha nchi utakayoiona.”

29 Kwa hiyo tulikaa kwenye bonde karibu na Beth-Peori.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/3-4bb1beab748da21a6f301a0d7d9f9f21.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 4

Waamriwa Utii

1 Sikia sasa, ee Israeli, amri na sheria nitakazokufundisha wewe. Zifuate ili upate kuishi na uingie kuimiliki nchi ambayoBwana, Mungu wa baba zako anawapa.

2 Usiongeze wala usipunguze chochote ninachowaamuru ninyi, ila myashike maagizo yaBwanaMungu wenu ambayo nawapa.

3 Mliona kwa macho yenu wenyewe kileBwanaalichokifanya kule Baal-Peori.BwanaMungu wenu aliwaangamiza kutoka miongoni mwenu kila mmoja aliyemfuata Baali wa Peori,

4 lakini ninyi nyote mlioshikamana naBwanakwa uthabiti, Mungu wenu, mko hai mpaka leo.

5 Tazama, nimewafundisha amri na sheria kamaBwanaMungu wangu alivyoniamuru mimi, ili mzifuate katika nchi mnayoiingia kuimiliki.

6 Zishikeni kwa uangalifu, kwa kuwa hii itaonyesha hekima na ufahamu wenu kwa mataifa, ambayo yatasikia kuhusu amri zote hizi, nao watasema, “Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na ufahamu.”

7 Ni taifa gani jingine lililo kubwa kiasi cha kuwa na miungu yao iliyo karibu nao kamaBwanaMungu wetu alivyo karibu nasi wakati wowote tunapomwomba?

8 Nalo ni taifa gani jingine lililo kubwa hivi lenye kuwa na amri na sheria za haki kama hizi ninazoweka mbele yenu leo?

9 Mwe waangalifu, na makini ili msije mkasahau mambo ambayo mliyaona kwa macho yenu, wala kuyaacha yaondoke moyoni mwenu siku zote za uhai wenu. Mwafundishe hayo watoto wenu na watoto wao baada yao.

10 Kumbuka siku uliyosimama mbele zaBwanaMungu wako kule Horebu, wakati aliponiambia, “Wakutanishe watu mbele yangu wasikie maneno yangu ili kwamba waweze kujifunza kuniheshimu kwa muda wote watakaoishi katika nchi, nao waweze kuwafundisha watoto wao maneno hayo.”

11 Mlisogea karibu na mkasimama chini ya mlima wakati ulipowaka moto mpaka mbinguni juu, pamoja na mawingu meusi na giza nene.

12 NdipoBwanaalipozungumza nanyi kutoka moto. Mkasikia sauti ya maneno lakini hamkuona umbo, kulikuwa na sauti tu.

13 Aliwatangazia Agano lake na Amri Kumi, ambazo aliwaamuru mzifuate, kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe.

14 NayeBwanaalinielekeza wakati huo kuwafundisha ninyi sheria na amri ambazo mnapaswa kuzifuata katika nchi ambayo mnavuka Yordani kuimiliki.

Kuabudu Sanamu Kwakatazwa

15 Hamkuona umbo la aina yoyote siku ambayoBwanaalizungumza nanyi kule Horebu kutoka kwenye moto. Kwa hiyo mjihadhari kwa uangalifu sana,

16 ili msije mkajichafua na kujitengenezea sanamu au kinyago chenye umbo lolote kama la mwanaume au mwanamke,

17 au kama mnyama aliye juu ya nchi au ndege yeyote arukaye angani,

18 au kama kiumbe kitambaacho juu ya ardhi au samaki yeyote aliye ndani ya maji.

19 Na utazamapo juu angani na ukaliona jua, mwezi na nyota na vyote vinavyoipamba mbingu, usije ukashawishiwa kuviinamia na kuviabudu vile ambavyoBwanaMungu wenu alivyogawia mataifa yote chini ya mbingu.

20 Lakini kwenu ninyi,Bwanaamewatoa kutoka kwenye tanuru ya kuyeyushia chuma, katika Misri kuwa watu wa urithi wake kama mlivyo sasa.

21 Bwanaalinikasirikia kwa sababu yenu na akaapa kwamba sitavuka Yordani kuingia katika nchi nzuriBwanaMungu wenu anayowapa kuwa urithi wenu.

22 Nitakufa katika nchi hii; sitavuka Yordani, lakini ninyi ni karibu mvuke mkaimiliki ile nchi nzuri.

23 Jihadharini msilisahau Agano laBwanaMungu wenu lile alilofanya nanyi; msijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote ambachoBwanaMungu wenu amewakataza.

24 Kwa kuwaBwanaMungu wenu ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.

25 Baada ya kuwa na watoto na wajukuu na kuishi katika nchi hiyo siku nyingi, tena kama mkijichafua na kutengeneza sanamu ya aina yoyote, mkifanya maovu machoni paBwanaMungu wenu na kumfanya awe na hasira,

26 ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yenu siku hii kwamba mtaangamia mara moja kutoka nchi ile ambayo mnavuka Yordani kuimiliki. Hamtaishi kule kwa muda mrefu bali kwa hakika mtaangamizwa.

27 Bwanaatawatawanya miongoni mwa mataifa, na ni wachache wenu tu watakaosalia miongoni mwa mataifa hayo ambayoBwanaatawafukuzia.

28 Huko mtaabudu miungu ya miti na mawe iliyotengenezwa na watu, ambayo haiwezi kuona au kusikia wala kula au kunusa.

29 Lakini kama mtamtafutaBwanaMungu wenu, mtampata; kama mtamtafuta kwa moyo wenu wote na kwa roho yote.

30 Wakati mnapokuwa katika dhiki, nayo mambo haya yote yamewatokea siku hizo, ndipo mtamrudiaBwanaMungu wenu na kumtii.

31 Kwa maanaBwanaMungu wenu ni Mungu mwenye huruma, hatawaacha au kuwaangamiza wala kusahau Agano alilofanya na baba zenu, alilowathibitishia kwa kiapo.

Bwana Ndiye Mungu

32 Sasa uliza kuhusu siku za zamani, zamani kabla ya wakati wako, tangu siku ile Mungu alipomuumba mtu juu ya nchi, uliza kutoka mwisho mmoja wa mbingu mpaka mwisho mwingine wa mbingu. Je, kumepata kutokea jambo jingine lililo kubwa kama hili, au kuna jambo jingine kama hilo limepata kusikiwa?

33 Je, kuna watu wengine wowote waliosikia sauti ya Mungu ikizungumza kwenye moto, kama mlivyosikia, nao wakaishi?

34 Je, kuna mungu yeyote amepata kujaribu mwenyewe kuchukua taifa moja kutoka taifa lingine, kwa mapigo, kwa ishara za miujiza na maajabu, kwa vita, kwa mkono wenye nguvu na mkono ulionyooshwa au kwa matendo makuu ya kutisha, kama yale ambayoBwanaMungu wenu aliyofanya kwa ajili yenu huko Misri mbele ya macho yenu?

35 Mlionyeshwa mambo haya ili mpate kujua kuwaBwanandiye Mungu; hakuna mwingine ila yeye.

36 Kutoka mbinguni amewasikizisha sauti yake ili kuwaadilisha. Hapa duniani aliwaonyesha moto wake mkubwa, nanyi mlisikia maneno yake kutoka kwenye ule moto.

37 Kwa sababu aliwapenda baba zenu na alichagua wazao wao baada yao, aliwatoa katika nchi ya Misri kwa Uwepo wake na kwa uwezo wake mkuu,

38 aliwafukuza mbele yenu mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko ninyi na kuwaleta ninyi katika nchi yao na akawapa ninyi kuwa urithi wenu, kama ilivyo leo.

39 Kubalini na mweke moyoni leo kuwaBwanandiye Mungu mbinguni juu na duniani chini. Hakuna mwingine.

40 Mshike amri na maagizo yake ninayowapa leo, ili mpate kufanikiwa ninyi na watoto wenu baada yenu, na mpate kuishi maisha marefu katika nchi awapayoBwanaMungu wenu siku zote.

Miji Ya Makimbilio

41 Kisha Mose akatenga miji mitatu mashariki ya Yordani,

42 ambayo mtu yeyote aliyemuua mtu angeweza kukimbilia ikiwa amemuua jirani yake bila kukusudia na bila kuwa na chuki naye siku zilizopita. Angeweza kukimbilia katika mmojawapo ya miji hii na kuokoa maisha yake.

43 Miji hiyo ilikuwa: Bezeri katika tambarare ya jangwa kwa ajili ya Wareubeni; Ramothi katika nchi ya Gileadi kwa ajili ya Wagadi; nao mji wa Golani katika nchi ya Bashani kwa ajili ya Wamanase.

Utangulizi Wa Sheria

44 Hii ndiyo sheria Mose aliyoweka mbele ya Waisraeli.

45 Haya ndiyo masharti, amri na sheria Mose aliyowapa wana wa Israeli wakati walitoka Misri,

46 nao walikuwa katika bonde karibu na Beth-Peori mashariki ya Yordani, katika nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala Heshboni, naye alishindwa na Mose na Waisraeli walipokuja toka Misri.

47 Waliimiliki nchi yake na nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, wafalme wawili Waamori waliotawala mashariki ya Yordani.

48 Nchi hii ilienea kutoka Aroeri ukingoni mwa Bonde la Arnoni mpaka Mlima Sioni (yaani Hermoni),

49 pamoja na eneo lote la Araba mashariki ya Yordani, na kuenea mpaka Bahari ya Araba kwenye miteremko ya Pisga.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/4-e54feee2029e3988abaff35b8a4b587e.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 5

Amri Kumi

1 Mose akawaita Israeli wote, akawaambia:

Ee Israeli, sikilizeni amri na sheria ninazowatangazia leo. Jifunzeni, na mwe na hakika kuzifuata.

2 BwanaMungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu.

3 Si kwambaBwanaalifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo.

4 Bwanaalisema nanyi uso kwa uso kutoka moto juu ya mlima.

5 (Wakati huo nilisimama kati yaBwanana ninyi kuwatangazia neno laBwana, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema:

6 “Mimi ndimiBwanaMungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.

7 Usiwe na miungu mingine ila mimi.

8 Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji.

9 Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi,BwanaMungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

10 lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.

11 Usilitaje bure jina laBwanaMungu wako, kwa kuwaBwanahataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.

12 Adhimisha siku ya Sabato na kuiweka takatifu, kamaBwanaMungu wako alivyokuagiza.

13 Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote.

14 Lakini siku ya Saba ni Sabato kwaBwana, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au mtumishi wa kike, wala ngʼombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliyeko malangoni mwako, ili kwamba mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe.

15 Kumbuka mlikuwa watumwa huko Misri, naBwanaMungu wenu aliwatoa huko kwa mkono wenye nguvu na kwa mkono ulionyooshwa. Kwa hiyoBwanaMungu wako amekuagiza kuiadhimisha siku ya Sabato.

16 Waheshimu baba yako na mama yako, kamaBwanaMungu wako alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchiBwanaMungu wako anayokupa.

17 Usiue.

18 Usizini.

19 Usiibe.

20 Usimshuhudie jirani yako uongo.

21 Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ngʼombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.”

22 Hizi ndizo amri alizozitangazaBwanakwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenu lote huko mlimani kutoka kwenye moto, wingu na giza nene, wala hakuongeza chochote zaidi. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, naye akanipa mimi.

Woga Wa Watu Mlimani

23 Mliposikia sauti kutoka kwenye giza, mlima ulipokuwa ukiwaka moto, viongozi wenu wote wa makabila yenu na wazee wenu walinijia mimi.

24 Nanyi mkasema, “BwanaMungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye.

25 Lakini sasa, kwa nini tufe? Moto huu mkubwa utatuteketeza sisi na tutakufa kama tukiendelea kusikia sauti yaBwanaMungu wetu zaidi.

26 Ni mtu yupi mwenye mwili ambaye amewahi kuisikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza kutoka kwenye moto, kama sisi tulivyoisikia, naye akaishi?

27 Sogea karibu usikie yale yote asemayoBwanaMungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambachoBwanaMungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.”

28 Bwanaaliwasikia wakati mlipozungumza nami, naBwanaakaniambia, “Nimesikia kile hawa watu walichokuambia. Kila kitu walichokisema ni kizuri.

29 Laiti kama mioyo yao ingekuwa na mwelekeo wa kuniogopa na kuzishika amri zangu zote daima, ili kwamba wafanikiwe wao pamoja na watoto wao milele!

30 “Nenda uwaambie warudi kwenye mahema yao.

31 Lakini wewe baki hapa pamoja nami ili niweze kukupa maagizo yote, amri na sheria ambazo utawafundisha wazifuate katika nchi ninayokwenda kuwapa waimiliki.”

32 Hivyo kuweni waangalifu kuyafanya yaleBwanaMungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto.

33 Fuateni yale yote ambayoBwanaMungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/5-334568423215b2ac8113821ad2320506.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 6

Mpende Bwana Mungu Wako

1 Haya ndiyo maagizo, amri na sheria ambazoBwanaMungu wenu aliniagiza niwafundishe ninyi ili mpate kuyashika katika nchi ambayo ninyi mnavuka Yordani kuimiliki,

2 ili kwamba ninyi, watoto wenu na watoto wao baada yao wamcheBwanaMungu wenu siku zote kwa kushika amri na maagizo yake yote ninayowapa, ili mweze kuyafurahia maisha marefu.

3 Sikia, ee Israeli, nawe uwe mwangalifu kutii ili upate kufanikiwa na kuongezeka sana katika nchi itiririkayo maziwa na asali, kamaBwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi ninyi.

4 Sikia, ee Israeli:BwanaMungu wako,Bwanani mmoja.

5 MpendeBwanaMungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote.

6 Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako.

7 Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.

8 Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako.

9 Ziandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako.

10 WakatiBwanaMungu wako atakapokuleta katika nchi aliyowaapia baba zako, Abrahamu, Isaki na Yakobo, kukupa wewe, nchi kubwa, ina miji inayopendeza ambayo hukuijenga,

11 nyumba zilizojaa vitu vizuri vya aina nyingi ambavyo hukuvijaza, visima ambavyo hukuchimba, na mashamba ya mizabibu na mizeituni ambayo hukupanda wewe, basi, utakapokula na kushiba,

12 jihadhari usije ukamwachaBwana, aliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.

13 UtamchaBwanaMungu wako, na umtumikie yeye peke yake na kuapa kwa jina lake.

14 Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka;

15 kwa kuwaBwanaMungu wako, ambaye yuko katikati yako, ni Mungu mwenye wivu na hasira yake itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza kutoka uso wa nchi.

16 UsimjaribuBwanaMungu wako kama ulivyofanya huko Masa.

17 Utayashika maagizo yaBwanaMungu wako kwa bidii, na masharti na amri alizokupa.

18 Fanya lililo haki na jema mbele zaBwana, ili upate kufanikiwa, uweze kuingia na kuimiliki nchi nzuri ambayoBwanaaliahidi kwa kiapo kwa baba zako,

19 kuwafukuza kwa nguvu adui zako mbele yako kamaBwanaalivyosema.

20 Siku zijazo, mtoto wako atakapokuuliza, “Ni nini maana ya masharti haya, amri na sheria hizi ambazoBwanaMungu wako alikuagiza wewe?”

21 Mwambie: “Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri, lakiniBwanaalitutoa sisi kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu.

22 Bwanaakapeleka mbele yetu ishara za miujiza na maajabu makubwa na ya kutisha mno juu ya Misri na Farao pamoja na nyumba yake yote.

23 Lakini Mungu akatutoa huko, akatuleta na kutupa nchi hii ambayo aliwaahidi baba zetu kwa kiapo.

24 Bwanaakatuagiza tutii amri hizi zote na kumchaBwanaMungu wetu, ili tupate kustawi na kuendelea kuwa hai kama ilivyo leo.

25 Kama tukizitii kwa bidii amri hizi zote mbele zaBwanaMungu wetu, kama alivyotuamuru sisi, hiyo itakuwa haki yetu.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/6-bc5311edec2b518759d98228f23fe746.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 7

Kuyafukuza Mataifa

1 BwanaMungu wako akuletapo katika nchi unayoingia kuimiliki, na awafukuzapo mbele yako mataifa mengi, yaani Wahiti, Wagirgashi, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi, mataifa saba makubwa tena yenye nguvu kuliko wewe,

2 piaBwanaMungu wako atakapowatia mkononi mwako na ukawashinda, basi ni lazima uwaangamize wote kabisa. Usifanye agano nao, wala usiwahurumie.

3 Usioane nao. Usimtoe binti yako kuolewa na mwanawe, au kumchukua binti yake aolewe na mwanao.

4 Kwa maana watamgeuza mwanao aache kunifuata, ili aitumikia miungu mingine, nayo hasira yaBwanaitawaka dhidi yako, naye atakuangamiza ghafula.

5 Hili ndilo utakalowafanyia: Vunja madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia, katakata nguzo zao za Ashera na kuchoma sanamu zao kwa moto.

6 Kwa kuwa wewe ni taifa takatifu kwaBwanaMungu wako.BwanaMungu wako amekuchagua wewe kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia kuwa watu wake, hazina yake ya thamani.

7 Bwanahakuweka upendo wake juu yenu na kuwachagua kwa sababu mlikuwa wengi mno kuliko watu wengine, kwa maana ninyi ndio mliokuwa wachache sana kuliko mataifa yote.

8 Lakini ni kwa sababuBwanaaliwapenda ninyi na kutunza kiapo alichowaapia babu zenu kwamba atawatoa ninyi kwa mkono wenye nguvu na kuwakomboa kutoka nchi ya utumwa, kutoka nguvu za Farao mfalme wa Misri.

9 Basi ujue kwambaBwanaMungu wako ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayetunza Agano la upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanaompenda na kuzishika amri zake.

10 Lakini

kwa wale wanaomchukia

atawalipiza kwenye nyuso zao

kwa maangamizi;

hatachelewa kuwalipiza kwenye nyuso zao

wale wamchukiao.

11 Kwa hiyo, kuweni waangalifu kufuata maagizo, amri na sheria ninazowapa leo.

Baraka Za Utiifu

12 Kama mkizingatia sheria hizi na kuzifuata kwa uangalifu, basiBwanaMungu wenu atatunza Agano lake la upendo nanyi, kama alivyowaapia baba zenu.

13 Atawapenda ninyi na kuwabariki na kuongeza idadi yenu. Atabariki uzao wa tumbo lenu, mazao ya nchi yenu, nafaka, divai mpya na mafuta, ndama za ngʼombe wa makundi yenu, na kondoo za makundi yenu katika nchi ile aliyoapa kuwapa baba zenu.

14 Mtabarikiwa kuliko mataifa mengine yote, hakuna wanaume wala wanawake kwenu watakaokosa watoto, wala mifugo yenu haitakuwa tasa.

15 Bwanaatawakinga na kila ugonjwa. Mungu hatatia juu yenu ugonjwa wowote mbaya mlioufahamu huko Misri, lakini atatia ugonjwa juu ya wale wote wanaokuchukia.

16 Ni lazima mwangamize watu wote ambaoBwanaMungu wenu atawatia mikononi mwenu. Msiwatazame kwa kuwahurumia na msiitumikie miungu yao, kwa kuwa itakuwa mtego kwenu.

17 Mnaweza kujiuliza wenyewe “Mataifa haya ni yenye nguvu kuliko sisi. Tutawezaje kuwafukuza?”

18 Lakini msiwaogope. Kumbukeni vyema jinsiBwanaMungu wenu alivyofanya kwa Farao na kwa wote huko Misri.

19 Mliona kwa macho yenu wenyewe majaribu makubwa, ishara za miujiza na maajabu, mkono wenye nguvu na ulionyooshwa, ambao kwa huoBwanaMungu wenu aliwatoa mtoke Misri.BwanaMungu wenu atawafanyia hivyo watu wote ambao mnawaogopa sasa.

20 Zaidi ya hayo,BwanaMungu wenu atatuma manyigu miongoni mwao hadi yale mabaki watakaojificha waangamie.

21 Msiingiwe na hofu kwa sababu yao, kwa kuwaBwanaMungu wenu, ambaye yupo miongoni mwenu ni mkuu naye ni Mungu wa kutisha.

22 BwanaMungu wenu atawafukuza mataifa hayo mbele yenu kidogo kidogo. Hamtaruhusiwa kuwaondoa wote kwa mara moja, la sivyo wanyama mwitu wataongezeka na kuwa karibu nanyi.

23 LakiniBwanaMungu wenu atawatia watu hao mikononi mwenu, akiwatia katika kuchanganyikiwa kukubwa mpaka wawe wameangamizwa.

24 Atawatia wafalme wao mikononi mwenu, nanyi mtayafuta majina yao chini ya mbingu. Hakuna hata mmoja atakayeweza kusimama dhidi yenu bali mtawaangamiza.

25 Vinyago vya miungu yao mtavichoma moto. Msitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala msizichukue kwa ajili yenu, la sivyo mtakuwa mmetekwa navyo. Kwa kuwa ni chukizo kwaBwanaMungu wenu.

26 Msilete vitu vya machukizo katika nyumba zenu kwani ninyi, mtatengwa kama vitu hivyo kwa maangamizo. Ukichukie kabisa kitu hicho kwa kuwa kimetengwa kwa maangamizo.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/7-fadc45cb5701ff3fb9ac1fe8a4a350b9.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 8

Usimsahau Bwana

1 Uwe mwangalifu kufuata kila agizo ninalokupa wewe leo, ili mweze kuishi, kuongezeka na mweze kuingia mkamiliki nchi ambayoBwanaaliahidi kwa kiapo kwa baba zenu.

2 Kumbuka jinsiBwanaMungu wenu alivyowaongoza katika njia yote katika jangwa kwa miaka hii arobaini, kukunyenyekeza na kukujaribu ili ajue lililoko moyoni mwako, kwamba utayashika maagizo yake au la.

3 Alikudhili na kukufanya uone njaa kisha akulishe kwa mana, ambayo wewe wala baba zako hamkuijua, awafundishe kuwa mwanadamu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa chaBwana.

4 Nguo zenu hazikuchakaa wala miguu yenu haikuvimba kwa miaka hii arobaini.

5 Mjue basi ndani ya mioyo yenu kama mtu anavyomwadibisha mwanawe, ndivyoBwanaMungu wako atawaadibisha ninyi.

6 Shikeni maagizo yaBwanaMungu wenu mtembee katika njia zake na kumheshimu.

7 Kwa kuwaBwanaMungu wenu anawaleta katika nchi nzuri, nchi yenye vijito na mabwawa ya maji, yenye chemchemi zinazotiririka mabondeni na katika vilima;

8 nchi yenye ngano na shayiri, mizabibu na mitini, mikomamanga, mafuta ya zeituni na asali;

9 nchi ambayo chakula hakitapungua na hamtakosa chochote; nchi ambayo miamba yake ni chuma na mnaweza kuchimba shaba kutoka kwenye vilima.

10 Wakati mtakapokwisha kula na kushiba, msifuniBwanaMungu wenu kwa ajili ya nchi nzuri aliyowapa.

11 Jihadharini msimsahauBwanaMungu wenu, mkashindwa kushika maagizo yake, sheria na amri zake ambazo ninawapa leo.

12 Angalia wakati mtakapokuwa mmekula na kushiba, mkajenga nyumba nzuri na kukaa humo,

13 na wakati makundi yenu ya ngʼombe na mbuzi na kondoo yatakapoongezeka na fedha na dhahabu yenu itakapoongezeka na vyote mlivyo navyo vitakapozidishwa,

14 basi mioyo yenu isiwe na kiburi mkamsahauBwanaMungu wenu aliyewatoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.

15 Aliwaongoza kupitia jangwa lile kubwa na la kutisha, nchi ile ya kiu isiyo na maji, yenye nyoka wa sumu na nge. Aliwatolea maji kutoka kwenye mwamba mgumu.

16 Aliwapa mana ya kula jangwani, kitu ambacho baba zenu hawakukijua, ili kuwanyenyekesha na kuwajaribu ninyi ili mwishoni apate kuwatendea mema.

17 Mnaweza kusema, “Uwezo wangu na nguvu za mikono yangu ndizo zilizonipatia utajiri huu.”

18 Lakini kumbukeniBwanaMungu wenu, ndiye ambaye huwapa uwezo wa kupata utajiri, na hivyo kulithibitisha Agano lake, ambalo aliwaapia baba zenu, kama ilivyo leo.

19 Ikiwa mtamsahauBwanaMungu wenu, mkaifuata miungu mingine, mkaiabudu na kuisujudia, ninashuhudia dhidi yenu leo kwamba hakika mtaangamizwa.

20 Kama mataifaBwanaaliyoyaangamiza mbele yenu, ndivyo ninyi mtakavyoangamizwa kwa kutokumtiiBwanaMungu wenu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/8-8aca7ac071be4b88ae744c88841996b7.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 9

Si Kwa Sababu Ya Haki Ya Waisraeli

1 Sikiliza, ee Israeli. Sasa mnakaribia kuvuka Yordani mwingie na kuwafukuza mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko ninyi pamoja na miji mikubwa yenye kuta zilizofika juu angani.

2 Watu ni wenye nguvu na warefu, ni wana wa Waanaki! Mnafahamu habari zao na mmesikia inavyosemekana: “Ni nani awezaye kusimama dhidi ya Waanaki?”

3 Kuweni na hakika leo kwambaBwanaMungu wenu ndiye atakayetangulia kuvuka mbele yenu kama moto uteketezao. Atawaangamiza; atawatiisha mbele yenu. Nanyi mtawafukuza na kuwaangamiza mara moja, kamaBwanaalivyowaahidi.

4 Baada yaBwanaMungu wenu kuwafukuza mbele yenu, msiseme mioyoni mwenu, “Bwanaametuleta hapa kuimiliki nchi hii kwa sababu ya haki yetu.” La, ni kwa sababu ya uovu wa mataifa haya ndiyoBwanaanawafukuza mbele yenu.

5 Si kwa sababu ya haki yenu wala uadilifu wenu kwamba mtaimiliki nchi yao; lakini kwa sababu ya uovu wa mataifa haya,BwanaMungu wenu atawafukuza mbele yenu, ili kutimiza lile alilowaapia baba zenu Abrahamu, Isaki na Yakobo.

6 Basi mjue, si kwa sababu ya haki yenuBwanaMungu wenu anawapa nchi hii nzuri kuimiliki, kwa kuwa ninyi ni taifa lenye shingo ngumu.

Ndama Ya Dhahabu

7 Kumbukeni hili, kamwe msisahau jinsi mlivyomkasirishaBwanaMungu wenu kwa hasira huko jangwani. Tangu siku mlipotoka Misri mpaka mlipofika hapa, mmekuwa waasi dhidi yaBwana.

8 Kule Horebu mliamsha ghadhabu yaBwana, kwa hiyo alikasirika vya kutosha hata akataka kuwaangamiza.

9 Nilipopanda mlimani kupokea mbao za mawe, mbao za Agano lileBwanaalilofanya nanyi, nilikaa mlimani siku arobaini usiku na mchana, sikula mkate wala sikunywa maji.

10 Bwanaalinipa mbao mbili za mawe zilizoandikwa kwa kidole cha Mungu. Juu ya mbao hizo kulikuwepo amri zote ambazoBwanaaliwatangazia kule mlimani kwa njia ya moto, siku ya kusanyiko.

11 Mwisho wa siku arobaini usiku na mchana,Bwanaalinipa mbao mbili za mawe, mbao za Agano.

12 KishaBwanaakaniambia, “Shuka chini mara moja, kwa sababu watu wako ambao umewatoa katika nchi ya Misri wamepotoka. Wamegeukia mbali haraka kutoka lile nililowaagiza, wamejitengenezea sanamu ya kusubu.”

13 NayeBwanaakaniambia, “Nimewaona watu hawa nao ni watu wenye shingo ngumu sana!

14 Niache, ili nipate kuwaangamiza na kufuta jina lao kutoka chini ya mbingu. Nami nitakufanya kuwa taifa lenye nguvu zaidi na kuwa wengi kuliko wao.”

15 Kwa hiyo niligeuka na kuteremka kutoka mlimani kwani mlima ulikuwa ukiwaka moto. Pia vibao vile viwili vya Agano vilikuwa mikononi mwangu.

16 Nilipotazama, niliona kuwa mmefanya dhambi dhidi yaBwanaMungu wenu; mmejifanyia sanamu ya kusubu katika umbo la ndama. Mmegeuka upesi kutoka njia ileBwanaaliyowaagiza.

17 Kwa hiyo nilichukua vibao vile viwili nikavitupa na kuvipasua vipande vipande mbele ya macho yenu.

18 Ndipo tena nikasujudu mbele zaBwanakwa siku arobaini usiku na mchana. Sikula mkate wala sikunywa maji, kwa sababu ya dhambi yote mliyoifanya, mkifanya lile lililo ovu mbele zaBwanana kumkasirisha.

19 Niliogopa hasira na ghadhabu yaBwana, kwa kuwa aliwakasirikia vya kutosha na kutaka kuwaangamiza. LakiniBwanaalinisikiliza tena.

20 Bali yeye alimkasirikia Aroni kiasi cha kutaka kumwangamiza, nami wakati huo nilimwombea Aroni pia.

21 Kisha nikachukua ile sanamu ya ndama mliyoitengeneza na kuichoma kwenye moto. Nikaiponda na kuisaga ikawa unga laini kama vumbi, nikatupa lile vumbi kwenye kijito kilichotiririka toka mlimani.

22 Pia mlimkasirishaBwanahuko Tabera, Masa na Kibroth-Hataava.

23 Vilevile wakatiBwanaalipowatuma kutoka Kadesh-Barnea, alisema, “Kweeni, mkaimiliki nchi ambayo nimewapa.” Lakini mliasi dhidi ya agizo laBwanaMungu wenu. Hamkumtegemea wala kumtii.

24 Mmekuwa waasi dhidi yaBwanatangu nilipowajua ninyi.

25 Nilianguka kifudifudi mbele zaBwanakwa zile siku arobaini usiku na mchana kwa sababuBwanaalikuwa amesema angewaangamiza ninyi.

26 NilimwombaBwanana kusema, “EeBwanaMwenyezi, usiangamize watu wako, urithi wako mwenyewe ule ulioukomboa kwa uweza wako mkuu na kuwatoa katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu.

27 Wakumbuke watumishi wako Abrahamu, Isaki na Yakobo. Usiangalie ukaidi wa watu hawa, uovu wao wala dhambi yao.

28 Watu wa nchi ile uliyotutoa sisi wasije wakasema, ‘Ni kwa sababuBwanahakuweza kuwachukua mpaka nchi aliyokuwa amewaahidia, kwa sababu aliwachukia, akawaleta ili aje kuwaua jangwani.’

29 Bali wao ni watu wako, urithi wako ule ulioutoa Misri kwa uweza wako mkuu na kwa mkono wako ulionyooka.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/9-f6f1a5dcfb89326722970806253438ff.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 10

Vibao Vingine Vya Amri Kumi

1 Wakati uleBwanaaliniambia, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza uje kwangu juu mlimani. Pia utengeneze Sanduku la mbao.

2 Nitaandika juu ya vibao maneno yaliyokuwa katika vile vibao vya kwanza, ambavyo ulivivunja. Kisha utaviweka ndani ya Sanduku.”

3 Hivyo nikatengeneza Sanduku kwa mti wa mshita, nikachonga pia vibao vya mawe kama vile vya kwanza, kisha nikakwea mlimani nikiwa na vibao viwili mikononi mwangu.

4 Bwanaakaandika juu ya hivi vibao kile alichokuwa amekiandika kabla, Amri Kumi alizokuwa amewatangazia juu mlimani, kutoka kwenye moto siku ile ya kusanyiko.Bwanaakanikabidhi.

5 Kisha nikashuka kutoka mlimani na kuweka vibao ndani ya Sanduku nililokuwa nimelitengeneza, kamaBwanaalivyoniagiza, navyo viko huko sasa.

6 (Waisraeli walisafiri kutoka visima vya Yaakani hadi Mosera. Huko Aroni alifariki na kuzikwa, naye Eleazari mwanawe akachukua nafasi yake kama kuhani.

7 Kutoka pale, walisafiri hadi Gudgoda wakaendelea mpaka Yotbatha, nchi yenye vijito vya maji.

8 Wakati huoBwanaaliteua kabila la Lawi kulibeba Sanduku la Agano laBwana, kusimama mbele zaBwanaili kutoa huduma, na kutangaza baraka kwa Jina lake, kama wanavyofanya mpaka leo.

9 Hiyo ndiyo sababu ya Walawi kutokuwa na sehemu wala urithi miongoni mwa ndugu zao;Bwanandiye urithi wao, kamaBwanaMungu wao alivyowaambia.)

10 Basi nilikaa mlimani kwa siku arobaini usiku na mchana, kama nilivyofanya mara ya kwanza, piaBwanaalinisikiliza hata wakati huu. Haikuwa nia yake kuwaangamiza.

11 Bwanaakaniambia, “Nenda, ukawaongoze watu katika njia yao ili kwamba waweze kuingia na kuimiliki nchi ile niliyowaapia baba zao kuwapa.”

Mche Bwana

12 Na sasa, ee Israeli,BwanaMungu wako anataka nini kwako ila kumchaBwanaMungu wako, kwenda katika njia zake, kumpenda na kumtumikiaBwanaMungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote,

13 na kuyashika maagizo yaBwanana amri zake ninazokupa leo kwa mafanikio yako mwenyewe?

14 Mbingu, hata mbingu za juu sana, dunia na kila kitu kilichomo ndani yake, ni mali yaBwanaMungu wako.

15 Hata hivyoBwanaalikuwa na shauku na baba zako, akawapenda na akawachagua ninyi, wazao wao, kuliko mataifa yote, kama ilivyo leo.

16 Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena.

17 Kwa kuwaBwanaMungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa.

18 Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.

19 Nanyi wapendeni wageni, kwa kuwa ninyi wenyewe mlikuwa wageni huko Misri.

20 McheBwanaMungu wako na umtumikie yeye. Shikamana naye kwa uthabiti na kuapa kwa jina lake.

21 Yeye ni sifa yako; yeye ni Mungu wako, ambaye alikutendea yale maajabu makubwa na ya kutisha uliyoyaona kwa macho yako mwenyewe.

22 Baba zako walioshuka kwenda Misri jumla yao walikuwa sabini, na sasaBwanaMungu wako amekufanya wengi kama nyota za angani.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/10-ef0829b15dd02672c90a099b6e3f50fb.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 11

Mpende Na Umtii Bwana

1 MpendeBwanaMungu wako na kushika masharti yake, amri zake, sheria zake na maagizo yake siku zote.

2 Kumbuka hivi leo kwamba sio watoto wako walioona na kujua adhabu yaBwanaMungu wako: utukufu wake, mkono wake wenye nguvu, mkono wake ulionyooshwa;

3 ishara alizozifanya na mambo aliyoyafanya katikati ya Misri, kwa Farao mfalme wa Misri na kwa nchi yake yote;

4 lile alilolifanyia jeshi la Wamisri, farasi na magari yake, jinsi alivyowafurikisha na maji ya Bahari ya Shamu walipokuwa wakiwafuatilia ninyi, na jinsiBwanaalivyowaletea angamizo la kudumu juu yao.

5 Sio watoto wenu walioyaona yale Mungu aliyowafanyia huko jangwani mpaka mkafika mahali hapa,

6 wala lile Mungu alilowafanyia Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu wa kabila la Reubeni, wakati ardhi ilipofungua kinywa chake katikati ya Israeli yote, ikawameza pamoja na walio nyumbani mwao, hema zao na kila kitu kilichokuwa hai ambacho kilikuwa mali yao.

7 Bali ilikuwa ni macho yenu wenyewe ambayo yaliyaona mambo haya yote makuuBwanaaliyoyatenda.

8 Kwa hiyo fuateni maagizo yote ninayowapa leo, ili mpate kuwa na nguvu za kuingia na kuiteka nchi ile ambayo mnavuka Yordani kuimiliki,

9 ili mpate kuishi siku nyingi katika nchi ile ambayoBwanaaliapa kuwapa baba zenu na wazao wao, nchi itiririkayo maziwa na asali.

10 Nchi mnayoiingia kuimiliki haifanani na nchi ya Misri mlikotoka ambako mlipanda mbegu yenu na kuinywesha, kama bustani ya mboga.

11 Lakini nchi mnayovuka Yordani kuimiliki ni nchi ya milima na mabonde inywayo mvua kutoka mbinguni.

12 Ni nchi ambayoBwanaMungu wenu anaitunza; macho yaBwanaMungu wenu yanaitazama daima kutoka mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka.

13 Hivyo kama mkiyatii maagizo yangu ninayowapa leo kwa uaminifu, yaani kwa kumpendaBwanaMungu wenu, na kumtumikia kwa moyo wako wote na kwa roho yenu yote,

14 ndipo atawanyweshea mvua katika nchi yenu kwa majira yake, mvua ya masika na ya vuli, ili mpate kuvuna nafaka zenu, divai mpya na mafuta.

15 Nitawapa majani kwa ajili ya ngʼombe wenu, nanyi mtakula na kushiba.

16 Jihadharini, la sivyo mtashawishika kugeuka na kuabudu miungu mingine na kuisujudia.

17 Ndipo hasira yaBwanaitawaka dhidi yenu, naye atafunga mbingu ili mvua isinyeshe nayo ardhi haitatoa mazao, nanyi mtaangamia mara katika nchi nzuri ambayoBwanaanawapa.

18 Yawekeni haya maneno yangu katika mioyo yenu na akili zenu, yafungeni kama alama juu ya mikono yenu na kwenye paji za nyuso zenu.

19 Wafundisheni watoto wenu, yazungumzeni wakati mketipo nyumbani na wakati mtembeapo njiani, wakati mlalapo na wakati mwamkapo.

20 Yaandikeni juu ya miimo ya nyumba zenu na juu ya malango yenu,

21 ili kwamba siku zenu na siku za watoto wenu zipate kuwa nyingi katika nchi ileBwanaaliyoapa kuwapa baba zenu, kama zilivyo nyingi siku za mbingu juu ya nchi.

22 Kama mkishika kwa makini maagizo haya yote ninayowapa kuyafuata, ya kumpendaBwanaMungu wenu, kuenenda katika njia zake zote na kushikamana naye kwa uthabiti,

23 ndipoBwanaatawafukuza mataifa haya yote mbele yako, nawe utawafukuza mataifa yaliyo makubwa na yenye nguvu kukuliko wewe.

24 Kila mahali mtakapoweka mguu wenu patakuwa penu: Nchi yenu itaenea kutoka jangwa la Lebanoni, na kutoka mto wa Frati hadi bahari ya magharibi

25 Hapatakuwa na mtu atakayeweza kusimama dhidi yenu.BwanaMungu wenu, kama alivyoahidi, ataweka juu ya nchi yote utisho na hofu kwa ajili yenu popote mwendako.

26 Tazama, leo ninaweka mbele yenu baraka na laana:

27 baraka kama mtatii maagizo yaBwanaMungu wenu, ambayo ninawapa leo;

28 laana kama hamtatii maagizo yaBwanaMungu wenu na kuacha njia ambayo ninawaamuru leo kwa kufuata miungu mingine, ambayo hamkuijua.

29 WakatiBwanaMungu wenu atakapokuwa amewaleta katika nchi mnayoiingia kuimiliki, mtatangaza baraka kutoka Mlima Gerizimu, na kutangaza laana kutoka Mlima Ebali.

30 Kama mnavyofahamu, milima hii ipo ngʼambo ya Yordani, magharibi ya barabara, kuelekea machweo ya jua, karibu na miti mikubwa ya More, katika nchi ya wale Wakanaani wanaoishi Araba, jirani na Gilgali.

31 Karibu mvuke ngʼambo ya Yordani kuingia na kuimiliki nchi ambayoBwanaMungu wenu anawapa. Wakati mtakapokuwa mmeichukua na mnaishi humo,

32 hakikisheni kwamba mnatii amri na sheria zote ninazoziweka mbele yenu leo.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/11-0c440b75a351e17e19fce5f90e126964.mp3?version_id=1627—

Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 12

Mahali Pekee Pa Kuabudia

1 Hizi ndizo amri na sheria ambazo ni lazima mwe waangalifu kuzifuata katika nchi ambayoBwana, Mungu wa baba zenu, amewapa kumiliki, kwa muda wote mtakaoishi katika nchi.

2 Haribuni kabisa kila mahali pao pa kuabudia kwenye milima mirefu, vilima na chini ya kila mti mkubwa ambamo mataifa haya mnayokwenda kuchukua ardhi yao huabudia miungu yao.

3 Bomoeni madhabahu zao, vunjeni yale mawe wanayoabudu, chomeni moto nguzo zao za Ashera; katilieni mbali sanamu za miungu yao na mfute majina yao mahali hapo.

4 Kamwe msimwabuduBwanaMungu wenu kama wanavyoabudu wao.

5 Bali mtatafuta mahaliBwanaMungu wenu atakapopachagua katika makabila yenu yote ili aliweke jina lake huko kuwa makao yake. Mahali hapo ndipo iwapasapo kwenda;

6 hapo ndipo mtakapoleta sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo zenu, kile ulichoweka nadhiri kutoa, sadaka zenu za hiari na malimbuko ya makundi yenu ya ngʼombe pamoja na mbuzi na kondoo.

7 Hapo, katika uwepo waBwanaMungu wenu, ninyi pamoja na jamaa zenu, mtakula na kufurahia kila kitu ambacho mmegusa kwa mikono yenu, kwa sababuBwanaMungu wenu amewabariki.

8 Msifanye kama tunavyofanya hapa leo, kila mtu anavyopenda mwenyewe,

9 kwa kuwa bado hamjafikia mahali pa mapumziko na urithi ambaoBwanaMungu wenu anawapa.

10 Lakini mtavuka Yordani na kuishi katika nchiBwanaMungu wenu anayowapa kama urithi, naye atawapa pumziko kutokana na adui zenu wote wanaowazunguka ili ninyi mpate kuishi kwa salama.

11 Kisha kuhusu mahaliBwanaMungu wenu atakapopachagua kuwa mahali pa makao ya Jina lake, hapo ndipo inapowapasa kuleta kila kitu ninachowaamuru: sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo, pamoja na vitu vyote vyenye thamani ambavyo mmeweka nadhiri kumtoleaBwana.

12 Hapo furahini mbele zaBwanaMungu wenu, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, pamoja na Walawi kutoka miji yenu ambao hawana mgawo wala urithi wao wenyewe.

13 Kuweni waangalifu, msitoe dhabihu zenu za kuteketezwa mahali popote mnapopapenda.

14 Mtazitoa tu mahali pale ambapoBwanaatachagua katika mojawapo ya makabila yenu, nanyi hapo zingatieni kila jambo ninalowaamuru.

15 Hata hivyo, mnaweza kuwachinja wanyama wenu katika miji yenu yoyote ile na kula nyama nyingi mpendavyo kama vile mmemchinja paa au kulungu, kulingana na baraka mtakazojaliwa naBwanaMungu wenu. Watu walio najisi au walio safi wanaweza kula.

16 Lakini kamwe usinywe damu; imwage juu ya ardhi kama maji.

17 Hamruhusiwi kula katika miji yenu zaka yenu ya nafaka, ya divai mpya na ya mafuta, au mzaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ngʼombe na makundi yenu ya mbuzi na kondoo, wala chochote ambacho mmeweka nadhiri kukitoa, au sadaka zako za hiari, wala matoleo maalum.

18 Badala yake, mtakula vitu hivyo katika uwepo waBwanaMungu wenu mahali ambapoBwanaMungu wenu atapachagua: wewe, wana wako na binti zako, watumishi wako wa kiume na wa kike, na Walawi kutoka miji yenu. Mnatakiwa mfurahi mbele zaBwanaMungu wenu kwa kula kitu mtakachoweka mikono yenu.

19 Mwe waangalifu msiwapuuze Walawi kwa muda wote mnaoishi katika nchi yenu.

20 BwanaMungu wenu atakapokuwa ameongeza nchi yenu kama alivyowaahidi, nanyi mkitamani nyama na mkisema, “Ningependa nyama,” hapo unaweza kula nyingi upendavyo.

21 Kama mahali ambapoBwanaMungu wenu atapachagua kuweka Jina lake ni mbali sana kutoka kwenu, unaweza kuchinja wanyama kutoka makundi yenu ya ngʼombe, ya mbuzi na ya kondoo ambayoBwanaamewapa, kama nilivyokuamuru, na mkiwa katika miji yenu wenyewe mnaweza kula nyingi mtakavyo.

22 Mle kama vile mngekula paa na kulungu. Wote walio najisi kiibada na walio safi mwaweza kula.

23 Lakini hakikisheni kwamba hamkunywa damu, kwa sababu damu ni uhai, kamwe msile uhai pamoja na nyama.

24 Hamruhusiwi kamwe kunywa damu; imwageni juu ya ardhi kama maji.

25 Msinywe damu, ili mweze kufanikiwa ninyi pamoja na watoto wenu baada yenu, kwa sababu mtakuwa mkifanya lililo haki machoni paBwana.

26 Lakini vichukueni vitu vyenu vilivyowekwa wakfu pamoja na vile mlivyoweka nadhiri, mwende mahali paleBwanaatakapopachagua.

27 Leteni sadaka zenu za kuteketezwa juu ya madhabahu yaBwanaMungu wenu, vyote nyama na damu. Damu ya dhabihu zenu lazima imiminwe kando ya madhabahu yaBwanaMungu wenu, lakini nyama mnaweza kula.

28 Mwe waangalifu kutii masharti haya yote ninayowapa, ili kwamba siku zote mweze kufanikiwa, ninyi pamoja na watoto wenu baada yenu, kwa sababu mtakuwa mkifanya lililo jema na sahihi mbele za macho yaBwanaMungu wenu.

29 BwanaMungu wenu atayakatilia mbali mbele yenu mataifa ambayo punde kidogo mtayavamia na kuyaondoa. Lakini mtakapokuwa mmeyafukuza na kuishi katika nchi yao,

30 na baada ya kuangamizwa mbele yenu, mwe waangalifu msijiingize katika tanzi kwa kuuliza habari za miungu yao, mkisema, “Je, mataifa haya hutumikiaje miungu yao? Nasi tutafanya vivyo hivyo.”

31 Kamwe msimwabuduBwanaMungu wenu kwa njia wanayoabudu miungu yao, kwa sababu katika kuabudu miungu yao, wanafanya aina zote za machukizo anayoyachukiaBwana. Hata huwateketeza wana wao na binti zao kwa moto kama kafara kwa miungu yao.

32 Angalieni kwamba mnafanya yote niliyowaamuru; msiongeze kitu wala msipunguze kitu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/12-d19b23d00de47ca8635847849612199c.mp3?version_id=1627—