Categories
Isaya

Isaya 61

Mwaka Wa Upendeleo Wa Bwana

1 Roho waBwanaMwenyezi yu juu yangu,

kwa sababuBwanaamenitia mafuta

kuwahubiria maskini habari njema.

Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo,

kuwatangazia mateka uhuru wao,

na hao waliofungwa

habari za kufunguliwa kwao;

2 kutangaza mwaka waBwanauliokubaliwa,

na siku ya kisasi ya Mungu wetu,

kuwafariji wote waombolezao,

3 na kuwapa mahitaji

wale wanaohuzunika katika Sayuni,

ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu,

mafuta ya furaha badala ya maombolezo,

vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa.

Nao wataitwa mialoni ya haki,

pando laBwana,

ili kuonyesha utukufu wake.

4 Watajenga upya magofu ya zamani

na kupatengeneza mahali palipoachwa ukiwa zamani;

watafanya upya miji iliyoharibiwa,

iliyoachwa ukiwa kwa vizazi vingi.

5 Wageni watayachunga makundi yenu,

wageni watafanya kazi katika mashamba yenu,

na kutunza mashamba yenu ya mizabibu.

6 Nanyi mtaitwa makuhani waBwana,

mtaitwa watumishi wa Mungu wetu.

Mtakula utajiri wa mataifa,

nanyi katika utajiri wao mtajisifu.

7 Badala ya aibu yao

watu wangu watapokea sehemu maradufu,

na badala ya fedheha

watafurahia katika urithi wao;

hivyo watarithi sehemu maradufu katika nchi yao,

nayo furaha ya milele itakuwa yao.

8 “Kwa maana Mimi,Bwana, napenda haki,

na ninachukia unyangʼanyi na uovu.

Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao

na kufanya agano la milele nao.

9 Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa,

na uzao wao miongoni mwa kabila za watu.

Wale wote watakaowaona watatambua

kuwa ni taifa ambaloBwanaamelibariki.”

10 Ninafurahia sana katikaBwana,

nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu.

Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu,

na kunipamba kwa joho la haki,

kama vile bwana arusi apambavyo

kichwa chake kama kuhani,

na kama bibi arusi ajipambavyo

kwa vito vyake vya thamani.

11 Kwa maana kama vile ardhi ifanyavyo chipukizi kuota,

na bustani isababishavyo mbegu kuota,

ndivyoBwanaMwenyezi atafanya haki na sifa

zichipuke mbele ya mataifa yote.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/ISA/61-97beb3b5258f8abd70a3e59639a345a3.mp3?version_id=1627—

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *