Categories
Yeremia

Yeremia 20

Yeremia Ateswa Na Pashuri

1 Ikawa kuhani Pashuri mwana wa Imeri, mkuu wa maafisa wa Hekalu laBwana, alipomsikia Yeremia akitoa unabii juu ya mambo haya,

2 akaamuru Yeremia nabii apigwe na kufungwa kwenye mkatale katika Lango la Juu la Benyamini huko Hekaluni laBwana.

3 Siku ya pili Pashuri alipomwachia kutoka kwenye mkatale, Yeremia akamwambia, “Bwanahakukuita jina lako kuwa Pashuri bali Magor-Misabibu.

4 Kwa kuwa hili ndilo asemaloBwana: ‘Nitakufanya kuwa hofu kuu kwako wewe mwenyewe na rafiki zako wote, na kwa macho yako mwenyewe utawaona wakianguka kwa upanga wa adui zao. Nitawatia Yuda wote mikononi mwa mfalme wa Babeli, ambaye atawachukua na kuwapeleka Babeli, ama awaue kwa upanga.

5 Nitatia utajiri wote wa mji huu kwa adui zao: yaani mazao yao yote, vitu vyao vyote vya thamani, na hazina zote za wafalme wa Yuda. Watavitwaa kwa nyara na kuvipeleka Babeli.

6 Nawe Pashuri pamoja na wote waishio katika nyumba yako mtakwenda uhamishoni Babeli. Mtafia humo na kuzikwa, wewe na rafiki zako wote ambao umewatabiria uongo.’ ”

Malalamiko Ya Yeremia

7 EeBwana, umenidanganya,

nami nikadanganyika;

wewe una nguvu kuniliko,

nawe umenishinda.

Ninadharauliwa mchana kutwa,

kila mmoja ananidhihaki.

8 Kila ninenapo, ninapiga kelele

nikitangaza ukatili na uharibifu.

Kwa hiyo neno laBwanalimeniletea matukano

na mashutumu mchana kutwa.

9 Lakini kama nikisema, “Sitamtaja

wala kusema tena kwa jina lake,”

neno lake linawaka ndani ya moyo wangu kama moto,

moto uliofungwa ndani ya mifupa yangu.

Nimechoka sana kwa kulizuia ndani mwangu;

kweli, siwezi kujizuia.

10 Ninasikia minongʼono mingi,

“Hofu iko pande zote!

Mshtakini! Twendeni tumshtaki!”

Rafiki zangu wote wananisubiri niteleze,

wakisema,

“Labda atadanganyika;

kisha tutamshinda

na kulipiza kisasi juu yake.”

11 LakiniBwanayu pamoja nami

kama shujaa mwenye nguvu;

hivyo washtaki wangu watajikwaa

na kamwe hawatashinda.

Watashindwa, nao wataaibika kabisa;

kukosa adabu kwao hakutasahauliwa.

12 EeBwanaMwenye Nguvu Zote,

wewe umjaribuye mwenye haki

na kupima moyo na nia,

hebu nione ukilipiza kisasi juu yao,

kwa maana kwako

nimeliweka shauri langu.

13 MwimbieniBwana!

MpeniBwanasifa!

Yeye huokoa uhai wa mhitaji

kutoka mikononi mwa waovu.

14 Ilaaniwe siku niliyozaliwa!

Nayo isibarikiwe ile siku

mama yangu aliyonizaa!

15 Alaaniwe mtu yule aliyemletea baba yangu habari,

yule aliyemfanya afurahi sana, akisema,

“Mtoto amezaliwa kwako,

tena mtoto wa kiume!”

16 Mtu huyo na awe kama miji ile

ambayoBwanaMungu

aliiangamiza bila huruma.

Yeye na asikie maombolezo asubuhi

na kilio cha vita adhuhuri.

17 Kwa sababu hakuniua nikiwa tumboni,

hivyo mama yangu angekuwa kaburi langu,

nalo tumbo lake la uzazi

lingebaki kuwa kubwa daima.

18 Kwa nini basi nilitoka tumboni

ili kuona taabu na huzuni,

na kuzimaliza siku zangu katika aibu?

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/20-cedf2c89bb12c3fc49c923a2d0582c7b.mp3?version_id=1627—

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *