Kitu Mungu Anachotaka
Zaburi ya Daudi.
1 Bwana, ni nani awezaye kukaa
katika Hekalu lako?
Nani awezaye kuishi
katika mlima wako mtakatifu?
2 Ni yule aendaye pasipo mawaa,
atendaye yaliyo haki,
asemaye kweli toka moyoni mwake,
3 na hana masingizio ulimini mwake,
asiyemtenda jirani yake vibaya,
na asiyemsingizia mwenzake,
4 ambaye humdharau mtu mbaya,
lakini huwaheshimu wale wamwogopaoBwana,
yule atunzaye kiapo chake
hata kama anaumia.
5 Yeye akopeshaye fedha yake bila riba,
na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia.
Mtu afanyaye haya
kamwe hatatikisika.
—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/15-12ac0bb687ff8678dd16cf5435ddfab1.mp3?version_id=1627—