Sala Ya Matumaini
Utenzi wa Daudi.
1 Ee Mungu, uniweke salama,
kwa maana kwako nimekimbilia.
2 NilimwambiaBwana, “Wewe ndiwe Bwana wangu;
pasipo wewe sina jambo jema.”
3 Kwa habari ya watakatifu walioko duniani,
ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao.
4 Huzuni itaongezeka kwa wale
wanaokimbilia miungu mingine.
Sitazimimina sadaka zao za damu
au kutaja majina yao midomoni mwangu.
5 Bwanaumeniwekea fungu langu na kikombe changu;
umeyafanya mambo yangu yote yawe salama.
6 Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri,
hakika nimepata urithi mzuri.
7 NitamsifuBwanaambaye hunishauri,
hata wakati wa usiku moyo wangu hunifundisha.
8 NimemwekaBwanambele yangu daima.
Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,
sitatikisika.
9 Kwa hiyo moyo wangu unafurahia, na ulimi wangu unashangilia;
mwili wangu nao utapumzika salama,
10 kwa maana hutaniacha kaburini,
wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu.
11 Umenijulisha njia ya uzima;
utanijaza na furaha mbele zako,
pamoja na furaha za milele
katika mkono wako wa kuume.
—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/16-4ccaddf1574a9e1359b06bd28e2a0236.mp3?version_id=1627—