Categories
Zaburi

Zaburi 141

Maombi Ya Kuhifadhiwa Dhidi Ya Uovu

Zaburi ya Daudi.

1 EeBwana, ninakuita wewe, uje kwangu hima.

Sikia sauti yangu ninapokuita.

2 Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba;

kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni.

3 EeBwana, weka mlinzi kinywani mwangu,

weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu.

4 Usiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya,

nisije nikashiriki katika matendo maovu

pamoja na watu watendao mabaya,

wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa.

5 Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma;

na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu.

Kichwa changu hakitalikataa.

Hata hivyo, maombi yangu daima

ni kinyume cha watenda mabaya,

6 watawala wao watatupwa chini

kutoka kwenye majabali,

waovu watajifunza kwamba maneno yangu

yalikuwa kweli.

7 Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi,

ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.”

8 Lakini nimekaza macho yangu kwako, EeBwanaMwenyezi,

ndani yako nimekimbilia, usiniache nife.

9 Niepushe na mitego waliyonitegea,

kutokana na mitego iliyotegwa na watenda mabaya.

10 Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe,

wakati mimi ninapita salama.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/141-2e78f72da3c85efe3c132cabfafda772.mp3?version_id=1627—

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *