Mungu Mfalme Mkuu
1 MwimbieniBwanawimbo mpya;
mwimbieniBwanadunia yote.
2 MwimbieniBwana, lisifuni jina lake;
tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
3 Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa,
matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.
4 Kwa kuwaBwanani mkuu mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote;
yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.
5 Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu,
lakiniBwanaaliziumba mbingu.
6 Fahari na enzi viko mbele yake;
nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.
7 MpeniBwana, enyi jamaa za mataifa,
mpeniBwanautukufu na nguvu.
8 MpeniBwanautukufu unaostahili jina lake;
leteni sadaka na mje katika nyua zake.
9 MwabuduniBwanakatika uzuri wa utakatifu wake;
dunia yote na itetemeke mbele zake.
10 Katikati ya mataifa semeni, “Bwanaanatawala.”
Ulimwengu ameuweka imara, hauwezi kusogezwa;
atawahukumu watu kwa uadilifu.
11 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi;
bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake;
12 mashamba na yashangilie,
pamoja na vyote vilivyomo ndani yake.
Kisha miti yote ya msituni itaimba kwa furaha;
13 itaimba mbele zaBwanakwa maana anakuja,
anakuja kuihukumu dunia.
Ataihukumu dunia kwa haki,
na mataifa katika kweli yake.
—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/96-a54c28136746e51ea86d1c4f8707af2d.mp3?version_id=1627—