Kuomba Msaada
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Maombi.
1 Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa;
EeBwana, njoo hima unisaidie.
2 Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu.
3 Wale waniambiao, “Aha! Aha!”
warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
4 Lakini wote wakutafutao
washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,
“Mungu na atukuzwe!”
5 Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;
Ee Mungu, unijie haraka.
Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;
EeBwana, usikawie.
—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/70-098f2b592afdfeb0c290fdafa03c8c88.mp3?version_id=1627—