Categories
Zaburi

Zaburi 30

Maombi Ya Shukrani

Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi.

1 Nitakutukuza wewe, EeBwana,

kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi,

na hukuacha adui zangu

washangilie juu yangu.

2 EeBwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie

na wewe umeniponya.

3 EeBwana, umenitoa Kuzimu,

umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.

4 MwimbieniBwana, enyi watakatifu wake;

lisifuni jina lake takatifu.

5 Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,

bali upendo wake hudumu siku zote.

Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,

lakini asubuhi kukawa na furaha.

6 Nilipofanikiwa nilisema,

“Sitatikiswa kamwe.”

7 EeBwana, uliponijalia,

uliuimarisha mlima wangu,

lakini ulipouficha uso wako

nilifadhaika.

8 Kwako wewe, EeBwana, niliita,

kwa Bwana niliomba rehema:

9 “Kuna faida gani katika kuangamia kwangu?

Katika kushuka kwangu shimoni?

Je, mavumbi yatakusifu?

Je, yatatangaza uaminifu wako?

10 EeBwana, unisikie na kunihurumia,

EeBwana, uwe msaada wangu.”

11 Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza,

ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,

12 ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya.

EeBwanaMungu wangu, nitakushukuru milele.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/30-445301d403cecad780d7e1817451227b.mp3?version_id=1627—

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *