Categories
Zaburi

Zaburi 24

Mfalme Mkuu

Zaburi ya Daudi.

1 Dunia ni mali yaBwana, na vyote vilivyomo ndani yake,

ulimwengu, na wote waishio ndani yake,

2 maana aliiwekea misingi yake baharini

na kuifanya imara juu ya maji.

3 Nani awezaye kuupanda mlima waBwana?

Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?

4 Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe,

yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake

au kuapa kwa kitu cha uongo.

5 Huyo atapokea baraka kutoka kwaBwana,

na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.

6 Hiki ndicho kizazi cha wale wamtafutao,

wale wautafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.

7 Inueni vichwa vyenu, enyi malango,

inukeni enyi milango ya kale,

ili mfalme wa utukufu apate kuingia.

8 Ni nani huyu Mfalme wa utukufu?

NiBwanaaliye na nguvu na uweza,

niBwanaaliye hodari katika vita.

9 Inueni vichwa vyenu, enyi malango,

viinueni juu enyi milango ya kale,

ili Mfalme wa utukufu apate kuingia.

10 Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu?

NiBwanaMwenye Nguvu Zote;

yeye ndiye Mfalme wa utukufu.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/24-91c40c17d34778b02a40e9bd38202f5a.mp3?version_id=1627—

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *