Sifa Kwa Yerusalemu
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.
1 Nilishangilia pamoja na wale walioniambia,
“Twende nyumbani yaBwana.”
2 Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama
malangoni mwako.
3 Yerusalemu imejengwa vyema kama mji
ambao umeshikamanishwa pamoja.
4 Huko ndiko makabila hukwea,
makabila yaBwana,
kulisifu jina laBwanakulingana na maagizo
waliopewa Israeli.
5 Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa,
viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.
6 Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu:
“Wote wakupendao na wawe salama.
7 Amani na iwepo ndani ya kuta zako
na usalama ndani ya ngome zako.”
8 Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki,
nitasema, “Amani iwe ndani yako.”
9 Kwa ajili ya nyumba yaBwanaMungu wetu,
nitatafuta mafanikio yako.
—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/122-e9675173996f9bd2375b6b4776caf398.mp3?version_id=1627—