Baraka Za Mwenye Haki
1 MsifuniBwana.
Heri mtu yule amchayeBwana,
mtu yule apendezwaye sana na amri zake.
2 Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi,
kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.
3 Nyumbani mwake kuna mali na utajiri,
haki yake hudumu milele.
4 Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu,
yule mwenye rehema, huruma na haki.
5 Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba,
anayefanya mambo yake kwa haki.
6 Hakika hatatikisika kamwe,
mtu mwenye haki atakumbukwa milele.
7 Hataogopa habari mbaya,
moyo wake ni thabiti, ukimtegemeaBwana.
8 Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu,
mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake.
9 Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini;
haki yake hudumu milele;
pembe yake itatukuzwa kwa heshima.
10 Mtu mwovu ataona na kuchukizwa,
atasaga meno yake na kutoweka,
kutamani kwa mtu mwovu kutaishia patupu.
—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/112-9a9d1bf374d655d84427efbeb9eed1f0.mp3?version_id=1627—