Categories
Zaburi

Zaburi 111

Sifa Za Bwana Kwa Matendo Ya Ajabu

1 MsifuniBwana.

NitamtukuzaBwanakwa moyo wangu wote,

katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.

2 Kazi zaBwanani kuu,

wote wanaopendezwa nazo huzitafakari.

3 Kazi zake zimejaa fahari na utukufu,

haki yake hudumu daima.

4 Amefanya maajabu yake yakumbukwe,

Bwanani mwenye neema na huruma.

5 Huwapa chakula wale wanaomcha,

hulikumbuka agano lake milele.

6 Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake,

akiwapa nchi za mataifa mengine.

7 Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki,

mausia yake yote ni ya kuaminika.

8 Zinadumu milele na milele,

zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.

9 Aliwapa watu wake ukombozi,

aliamuru agano lake milele:

jina lake ni takatifu na la kuogopwa.

10 KumchaBwanandicho chanzo cha hekima,

wote wanaozifuata amri zake wana busara.

Sifa zake zadumu milele.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/PSA/111-fcbaf92f4ba0a7f3ecc7034f23b9cdb2.mp3?version_id=1627—

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *