Categories
Yoshua

Yoshua 23

Yoshua Anawaaga Viongozi

1 Baada ya muda mrefu kupita, nayeBwanaakawa amewapa Israeli pumziko mbele ya adui zao wote waliowazunguka, Yoshua, wakati huo akiwa mzee na umri ukiwa umeendelea sana,

2 akawaita Israeli wote, wazee wao, viongozi, waamuzi na maafisa Yoshua akawaambia: “Mimi ni mzee na umri wangu umeendelea sana.

3 Ninyi wenyewe mmeona kila kituBwanaMungu wenu, alichowatendea mataifa haya yote kwa ajili yenu. Ilikuwa niBwanaMungu wenu aliyewapigania.

4 Kumbukeni jinsi nilivyowagawia kama urithi kwa makabila yenu yote nchi ya mataifa yaliyobaki, yaani mataifa niliyowashinda, kati ya Mto Yordani na Bahari kuu upande wa magharibi.

5 BwanaMungu wenu mwenyewe atawaondoa watoke mbele yenu. Atawafukuza mbele yenu, nanyi mtamiliki nchi yao, kama vileBwanaMungu wenu alivyowaahidi.

6 “Kuweni hodari sana, kuweni waangalifu kutii yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Sheria ya Mose, pasipo kugeuka upande wa kuume au kushoto.

7 Msishirikiane na mataifa yaliyobakia katikati yenu, wala msiombe kwa majina ya miungu yao au kuapa kwayo. Msiitumikie wala kuisujudia.

8 Bali mtashikamana kwa uthabiti naBwana, Mungu wenu, kama vile ambavyo mmefanya mpaka sasa.

9 “Bwanaamewafukuza mbele yenu mataifa makubwa na yenye nguvu, mpaka siku ya leo hakuna yeyote aliyeweza kusimama mbele yenu.

10 Mtu mmoja miongoni mwenu anafukuza watu elfu, kwa kuwaBwanaMungu wenu anawapigania, kama alivyoahidi.

11 Kwa hiyo kuweni waangalifu sana kumpendaBwanaMungu wenu.

12 “Lakini ikiwa mtageuka na kushikamana na mabaki ya mataifa haya yaliyosalia katikati yenu na kama mtaoana na kushirikiana nao,

13 basi mwe na hakika kuwaBwanaMungu wenu hatawafukuza tena mataifa hayo mbele yenu. Badala yake, watakuwa tanzi na mitego kwenu, mijeledi migongoni mwenu, na miiba machoni mwenu, mpaka mwangamie kutoka nchi hii nzuri, ambayoBwanaMungu wenu amewapa.

14 “Sasa mimi ninakaribia kwenda katika njia ya watu wote wa dunia. Mnajua kwa mioyo yenu na roho zenu kwamba hakuna ahadi zozote njemaBwanaMungu wenu alizowaahidia, ambazo hazikutimia. Kila ahadi imetimizwa, hakuna hata moja ambayo haikutimia.

15 Lakini kama vile kila ahadi njema yaBwanaMungu wenu imekuwa kweli, vivyo hivyoBwanaataleta maovu yote kama alivyo onya, mpaka awe amewaangamiza kutoka nchi hii nzuri aliyowapa.

16 Kama mkilivunja agano laBwanaMungu wenu, ambalo aliwaamuru ninyi, mkaenda na kuitumikia miungu mingine na kuisujudia, hasira yaBwanaitawaka dhidi yenu, nanyi mtaangamia kutoka nchi nzuri aliyowapa ninyi.”

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JOS/23-66bad3d200ae96492b40ac9253ae7665.mp3?version_id=1627—

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *