Categories
Yeremia

Yeremia 12

Lalamiko La Yeremia

1 Wewe daima u mwenye haki, EeBwana,

niletapo mashtaka mbele yako.

Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako:

Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa?

Kwa nini wasio waaminifu

wote wanaishi kwa raha?

2 Umewapanda, nao wameota,

wanakua na kuzaa matunda.

Daima u midomoni mwao,

lakini mbali na mioyo yao.

3 Hata hivyo unanijua mimi, EeBwana;

unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe.

Wakokote kama kondoo wanaokwenda kuchinjwa!

Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa!

4 Je, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza mpaka lini,

na majani katika kila shamba kunyauka?

Kwa sababu wale waishio ndani yake ni waovu,

wanyama na ndege wameangamia.

Zaidi ya hayo, watu wanasema,

“Bwanahataona yatakayotupata sisi.”

Jibu La Mungu

5 “Ikiwa umeshindana mbio na watu kwa mguu na wakakushinda,

unawezaje kushindana na farasi?

Ikiwa unajikwaa kwenye nchi ambayo ni salama,

utawezaje kwenye vichaka kando ya Yordani?

6 Ndugu zako, watu wa jamaa yako mwenyewe:

hata wao wamekusaliti;

wameinua kilio kikubwa dhidi yako.

Usiwaamini, ingawa wanazungumza

mema juu yako.

7 “Nitaiacha nyumba yangu,

nitupe urithi wangu;

nitamtia yeye nimpendaye

mikononi mwa adui zake.

8 Urithi wangu umekuwa kwangu

kama simba wa msituni.

Huningurumia mimi,

kwa hiyo ninamchukia.

9 Je, urithi wangu haukuwa

kama ndege wa mawindo wa madoadoa

ambaye ndege wengine wawindao

humzunguka na kumshambulia?

Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni;

walete ili wale.

10 Wachungaji wengi wataliharibu shamba langu la mizabibu

na kulikanyaga shamba langu;

watalifanya shamba langu zuri

kuwa jangwa la ukiwa.

11 Litafanywa kuwa jangwa,

lililokauka na kuachwa ukiwa mbele zangu;

nchi yote itafanywa jangwa

kwa sababu hakuna hata mmoja anayejali.

12 Juu ya miinuko yote ilivyo kama jangwani

mharabu atajaa,

kwa maana upanga waBwanautawala,

kuanzia ncha moja ya nchi hadi nyingine;

hakuna hata mmoja atakayekuwa salama.

13 Watapanda ngano lakini watavuna miiba;

watajitaabisha lakini hawatafaidi chochote.

Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako

kwa sababu ya hasira kali yaBwanaMungu.”

14 Hili ndilo asemaloBwana: “Kwa habari ya majirani zangu wote wabaya wanaonyangʼanya urithi ambao ninawapa watu wangu Israeli, nitawangʼoa kutoka nchi zao, nami nitaingʼoa nyumba ya Yuda kutoka katikati yao.

15 Lakini baada ya kuwangʼoa, nitawahurumia tena na kumrudisha kila mmoja wao kwenye urithi wake mwenyewe na kwenye nchi yake mwenyewe.

16 Ikiwa watajifunza vyema njia za watu wangu na kuapa kwa Jina langu, wakisema, ‘Hakika kamaBwanaaishivyo,’ hata kama wakati fulani walifundisha watu wangu kuapa kwa Baali, ndipo watakapofanywa imara katikati ya watu wangu.

17 Lakini kama taifa lolote halitasikiliza na kutii, nitalingʼoa kabisa na kuliangamiza,” asemaBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/12-65b0859db929909aeaabd9cd5a5d88c2.mp3?version_id=1627—

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *