Categories
Yeremia

Yeremia 1

1 Maneno ya Yeremia mwana wa Hilkia, mmoja wa makuhani katika mji wa Anathothi, katika nchi ya Benyamini.

2 Neno laBwanalilimjia katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda,

3 na pia wakati wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipopelekwa uhamishoni.

Wito Wa Yeremia

4 Neno laBwanalilinijia, kusema,

5 “Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua;

kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum;

nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.”

6 Nami nikasema, “Aa,BwanaMwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.”

7 LakiniBwanaakaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza.

8 Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asemaBwana.

9 KishaBwanaakaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako.

10 Tazama, leo nimekuweka juu ya mataifa na falme ili kungʼoa na kubomoa, kuharibu na kuangamiza, kujenga na kupanda.”

11 Neno laBwanalikanijia kusema, “Je, Yeremia unaona nini?”

Nami nikajibu, “Naona tawi la mti wa mlozi.”

12 Bwanaakaniambia, “Umeona vyema kwa maana ninaliangalia neno langu ili kuona kwamba limetimizwa.”

13 Neno laBwanalikanijia tena, “Unaona nini?”

Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.”

14 Bwanaakaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote waishio katika nchi.

15 Nitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asemaBwana.

“Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya enzi

katika maingilio ya malango ya Yerusalemu,

watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka,

na dhidi ya miji yote ya Yuda.

16 Nitatoa hukumu zangu kwa watu wangu

kwa sababu ya uovu wao wa kuniacha mimi,

kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine

na kuabudu kile ambacho mikono yao imekitengeneza.

17 “Jiandae! Simama useme chochote nitakachokuamuru. Usiwaogope, la sivyo nitakufanya uwaogope wao.

18 Leo nimekufanya mji wenye ngome, nguzo ya chuma, na ukuta wa shaba ili kusimama dhidi ya nchi yote: dhidi ya wafalme wa Yuda, maafisa wake, makuhani wake na watu wa nchi hiyo.

19 Watapigana nawe lakini hawatakushinda, kwa kuwa niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,” asemaBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/JER/1-95955986344391729205a4da72b0ed63.mp3?version_id=1627—

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *