Mafuta Na Mikate Mbele Za Bwana
1 Bwanaakamwambia Mose,
2 “Waagize Waisraeli wakuletee mafuta safi ya zeituni yaliyokamuliwa kwa ajili ya mwanga ili taa ziwe zinawaka daima.
3 Nje ya pazia la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, Aroni ataziwasha taa mbele zaBwanakuanzia jioni hadi asubuhi bila kuzima. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo.
4 Taa zilizo juu ya kinara cha dhahabu safi mbele zaBwanalazima zihudumiwe daima.
5 “Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efaza unga kwa kila mkate.
6 Iweke katika mistari miwili, kila mstari mikate sita, uiweke mbele zaBwanajuu ya meza iliyotengenezwa kwa dhahabu safi.
7 Kando ya kila mstari, weka uvumba safi kama sehemu ya kumbukumbu ili kuwakilisha mikate kuwa sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa kuteketezwa kwa moto.
8 Mikate hii itawekwa mbele zaBwanakila wakati, Sabato baada ya Sabato, kwa niaba ya Waisraeli, kuwa Agano la kudumu.
9 Hii ni mali ya Aroni na wanawe, watakaoila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni sehemu takatifu sana ya fungu lao la kawaida la sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa kuteketezwa kwa moto.”
Mwenye Kukufuru Apigwa Mawe
10 Basi mwana wa mama Mwisraeli na baba Mmisri alikwenda miongoni mwa Waisraeli, nayo mapigano yakatokea ndani ya kambi kati yake na Mwisraeli.
11 Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru Jina laBwanakwa kulaani; kwa hiyo wakamleta kwa Mose. (Jina la mama yake aliitwa Shelomithi binti wa Dibri, wa kabila la Dani.)
12 Nao wakamweka mahabusu mpaka mapenzi yaBwanayawe wazi kwao.
13 NdipoBwanaakamwambia Mose:
14 “Mchukue huyo aliyekufuru nje ya kambi. Wale wote waliomsikia akikufuru wataweka mikono juu ya kichwa chake, kisha kusanyiko lote litampiga mawe.
15 Waambie Waisraeli: ‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani Mungu wake, atakuwa na hatia kwa uovu wake;
16 yeyote atakayekufuru Jina laBwanani lazima auawe. Kusanyiko lote litampiga kwa mawe. Iwe ni mgeni au mzawa, atakapolikufuru Jina laBwana, ni lazima auawe.
17 “ ‘Kama mtu yeyote atamuua mtu mwingine, ni lazima auawe.
18 Mtu yeyote auaye mnyama wa mtu mwingine lazima afidie, uhai kwa uhai.
19 Ikiwa mtu yeyote atamjeruhi jirani yake, chochote alichomtenda naye atatendewa:
20 iwapo amemvunja mfupa atavunjwa mfupa, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama alivyomjeruhi mwenzake, vivyo hivyo ndivyo atakavyojeruhiwa.
21 Yeyote auaye mnyama wa mtu lazima alipe fidia, lakini yeyote auaye mtu, lazima auawe.
22 Mtakuwa na sheria iyo hiyo kwa mgeni na kwa mzawa. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.’ ”
23 Kisha Mose akasema na Waisraeli, nao wakamchukua yule aliyekufuru nje ya kambi na kumpiga mawe. Waisraeli wakafanya kamaBwanaalivyomwagiza Mose.
—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/LEV/24-f8b917f43fb3bf2f920307751a43acfa.mp3?version_id=1627—