Categories
Walawi

Walawi 23

Sikukuu Zilizoamriwa

1 Bwanaakamwambia Mose,

2 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Hizi ndizo sikukuu zangu zilizoamriwa, sikukuu zilizoamriwa zaBwana, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu.

Sabato

3 “ ‘Kuna siku sita mnazoweza kufanya kazi, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika, siku ya kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi yoyote. Popote mnapoishi, ni Sabato kwaBwana.

Pasaka Na Mikate Isiyotiwa Chachu

4 “ ‘Hizi ni sikukuu zaBwanazilizoamriwa, makusanyiko matakatifu mtakayoyatangaza kwa nyakati zilizoamriwa:

5 Pasaka yaBwanahuanza jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.

6 Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa kwanza, Sikukuu yaBwanaya Mikate Isiyotiwa Chachu huanza; kwa siku saba, mtakula mikate isiyotiwa chachu.

7 Katika siku ya kwanza, mtakuwa na kusanyiko takatifu, na msifanye kazi zenu za kawaida.

8 Kwa siku saba mtamleteaBwanasadaka ya kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku hiyo ya saba mtafanya kusanyiko takatifu, na msifanye kazi zenu za kawaida.’ ”

Malimbuko

9 Bwanaakamwambia Mose,

10 “Sema na Waisraeli na uwaambie: ‘Mtakapoingia katika nchi nitakayowapa na kuvuna mazao ya nchi hiyo, leteni kwa kuhani mganda wa nafaka ya kwanza mtakayovuna.

11 Naye atauinua huo mganda mbele zaBwanaili ukubaliwe kwa niaba yenu; kuhani ataupunga siku inayofuata Sabato.

12 Siku hiyo mtakapoinua huo mganda, lazima mtoe kwaBwanadhabihu ya kuteketezwa kwa moto ya mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiye na dosari,

13 pamoja na sadaka yake ya nafaka ya sehemu mbili za kumi za efaza unga laini uliochanganywa na mafuta, sadaka iliyotolewa kwaBwanakwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kupendeza, na sadaka yake ya kinywaji ya robo ya hiniya divai.

14 Kamwe msile mkate wowote, au nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya, mpaka siku ile mtakayomletea Mungu wenu sadaka hii. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mnapoishi.

Sikukuu Ya Majuma

15 “ ‘Tangu siku ile iliyofuata Sabato, siku mliyotoa sadaka ya mganda wa kuinuliwa, hesabuni majuma saba kamili.

16 Mtahesabu siku hamsini mpaka siku inayofuata Sabato ya saba, ndipo mtatoa sadaka ya nafaka mpya kwaBwana.

17 Kutoka popote mnapoishi, mtaleta mikate miwili ya unga laini, sehemu mbili za kumi za efa, uliookwa kwa chachu, kuwa sadaka ya kuinuliwa ya malimbuko kwaBwana.

18 Toeni pamoja na hiyo mikate wana-kondoo saba, kila mmoja wa mwaka mmoja asiye na dosari, na fahali mchanga, na kondoo dume wawili. Watakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto iliyotolewa kwaBwana, pamoja na sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji, sadaka iliyotolewa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendezaBwana.

19 Kisha toeni dhabihu ya mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi, na wana-kondoo wawili, kila mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya amani.

20 Kuhani atawainua hao wana-kondoo wawili mbele zaBwanakuwa sadaka ya kuinuliwa, pamoja na mkate wa malimbuko. Ni sadaka takatifu kwaBwanakwa ajili ya kuhani.

21 Siku iyo hiyo mtatangaza kusanyiko takatifu, na msifanye kazi zenu za kawaida. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mnapoishi.

22 “ ‘Mnapovuna mavuno ya ardhi yenu, msivune hadi mpakani mwa shamba lenu, au kukusanya masazo ya mavuno yenu. Hayo utayaacha kwa ajili ya maskini na mgeni. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.’ ”

Sikukuu Ya Tarumbeta

23 Bwanaakamwambia Mose,

24 “Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na siku ya mapumziko, kusanyiko takatifu la ukumbusho litakaloadhimishwa kwa kupiga tarumbeta.

25 Msifanye kazi zenu zozote za kawaida, lakini toeni sadaka kwaBwanailiyoteketezwa kwa moto.’ ”

Siku Ya Upatanisho

26 Bwanaakamwambia Mose,

27 “Siku ya kumi ya mwezi huu wa saba ni Siku ya Upatanisho. Mtafanya kusanyiko takatifu, mfunge, nanyi mtoe sadaka kwaBwanaya kuteketezwa kwa moto.

28 Msifanye kazi siku hiyo, kwa sababu ni Siku ya Upatanisho, ambapo upatanisho unafanyika kwa ajili yenu mbele zaBwanaMungu wenu.

29 Mtu yeyote ambaye hatafunga siku hiyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

30 Mtu yeyote atakayefanya kazi siku hiyo nitamwangamiza kutoka miongoni mwa watu wake.

31 Hamtafanya kazi kamwe. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo popote mnapoishi.

32 Ni Sabato ya mapumziko kwenu ninyi, na lazima mfunge. Tangu jioni ya siku ya tisa ya mwezi hadi jioni inayofuata, mtaishika Sabato yenu.”

Sikukuu Ya Vibanda

33 Bwanaakamwambia Mose,

34 “Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, Sikukuu yaBwanaya vibanda itaanza, nayo itaadhimishwa kwa siku saba.

35 Siku ya kwanza ni kusanyiko takatifu, msifanye kazi zenu za kawaida.

36 Kwa siku saba toeni sadaka kwaBwanaza kuteketezwa kwa moto. Kwenye siku ya nane fanyeni kusanyiko takatifu, na mtoe sadaka kwaBwanaya kuteketezwa kwa moto. Ni kusanyiko la mwisho, msifanye kazi zenu za kawaida.

37 (“ ‘Hizi ni sikukuu zaBwanazilizoamriwa, ambazo mtazitangaza kuwa makusanyiko matakatifu kwa kuleta sadaka kwaBwanaza kuteketeza kwa moto: sadaka za kuteketezwa na sadaka za nafaka, dhabihu na sadaka za vinywaji zitahitajika kila siku.

38 Sadaka hizi ni nyongeza ya zile mnazozitoa katika Sabato zaBwana, na pia ni nyongeza ya matoleo yenu ya chochote mlichoweka nadhiri, na sadaka zenu zote za hiari mnazozitoa kwaBwana.)

39 “ ‘Basi kuanzia siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, baada ya kuvuna mazao yote ya nchi, mtaadhimisha sikukuu kwaBwanakwa siku saba; siku ya kwanza ni mapumziko, pia siku ya nane ni mapumziko.

40 Siku ya kwanza mtachukua matunda mazuri ya miti, matawi ya mitende, matawi yenye majani mengi, na matawi ya mirebi, nanyi mtashangilia mbele zaBwanaMungu wenu kwa siku saba.

41 Mtaadhimisha siku hii kuwa sikukuu kwaBwanakwa siku saba kila mwaka. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo; iadhimisheni mwezi wa saba.

42 Mtaishi katika vibanda kwa siku saba: Wazawa wote wa Waisraeli wataishi katika vibanda,

43 ili wazao wenu wajue kuwa niliwafanya Waisraeli waishi kwenye vibanda nilipowatoa Misri. Mimi ndimiBwanaMungu wenu.’ ”

44 Kwa hiyo Mose akawatangazia Waisraeli sikukuu zilizoamriwa naBwana.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/LEV/23-09161edba0f1f306b2a1c438e35cbfed.mp3?version_id=1627—

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *