Categories
Obadia

Obadia Utangulizi

Utangulizi

Maana ya jina Obadia ni “Mtumishi wa Yehova.” Hakuna habari zinazojulikana kuhusu huyu nabii isipokuwa mambo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Obadia alitoa unabii kuhusu hukumu ya Mungu dhidi ya taifa la Edomu, kukomeshwa na kuangamizwa kwalo lisiwepo tena ulimwenguni. Waedomu, waliokuwa uzao wa Esau, walijivunia usalama katika ngome zao zilizokuwa Mlima Seiri, kusini mwa Bahari ya Chumvi. Waliwatazama watu wa Yuda walipopatwa na mikasa mikononi mwa wavamizi bila kuwasaidia. Mwanzoni mwa karne ya tisa Waedomu wenyewe walishiriki zaidi ya mara nne kuiteka nyara Yerusalemu.

Mwandishi

Obadia.

Kusudi

Kuonyesha kwamba Mungu anawahukumu wale wanaowadhuru watu wake.

Mahali

Yerusalemu.

Tarehe

Kati ya 605–586 K.K.

Wahusika Wakuu

Waedomu.

Wazo Kuu

Obadia alitangaza hukumu ya Mungu dhidi ya Waedomu, na akatabiri kuangamizwa kwao na kufutwa kwa kumbukumbu lao katika uso wa dunia. Wale wanaopigana na watu walioitwa na Mungu, yeye hupigana nao na kufuta kumbukumbu lao duniani wasipotubu.

Mambo Muhimu

Hukumu ya Mungu, na kuangamizwa kwa taifa la Waedomu.

Mgawanyo

Maangamizi ya Edomu (

1-14

)

Kurejezwa kwa Israeli (

15-21

).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *