Categories
Nehemia

Nehemia Utangulizi

Utangulizi

Vitabu vya Ezra na Nehemia vinakwenda sambamba na vitabu vya Mambo ya Nyakati, vikisimulia habari zinazofuata matukio ya Mambo ya Nyakati. Kitabu cha Nehemia kimepewa jina la mhusika wake mkuu ambaye ni Nehemia. Katika andiko la Kiebrania, kitabu hiki ni sehemu ya kitabu cha Ezra. Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba katika kipindi hiki nabii Malaki alikuwa akihudumu.

Mwandishi

Kuna uwezekano mkubwa kwamba Nehemia au Ezra, au wote wawili ndio walioandika kitabu hiki, kwani mwanzoni Ezra na Nehemia vilikuwa kitabu kimoja.

Kusudi

Habari za kurudi kwa Wayahudi kutoka uhamishoni, na kujengwa kwa ukuta wa Yerusalemu.

Mahali

Yerusalemu.

Tarehe

Kuna uwezekano hiki kitabu kiliandikwa miaka ya 445–432 K.K.

Wahusika Wakuu

Nehemia, Ezra, Tobia na Sanbalati.

Wazo Kuu

Kitabu hiki kinaonyesha kutimizwa kwa unabii wa Zekaria na Danieli kuhusu kujengwa upya kuta za Yerusalemu.

Mambo Muhimu

Kujengwa kwa ukuta wa Yerusalemu, na kurejezwa kwa utaratibu wa ibada.

Mgawanyo

Nehemia anazijenga kuta (

1:1–7:3

)

Mabadiliko chini ya Ezra (

7:4–10:39

)

Mipango ya Nehemia (

11:1–13:31

).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *