Categories
Mhubiri

Mhubiri Utangulizi

Utangulizi

Neno la Kiyunani “Ecclesiastes” limetafsiriwa kutoka kwa neno la Kiebrania “Qoheleth.” Maana yake ni “Mhubiri” au “Yeye ahutubiaye kusanyiko.” Maadamu mwandishi anajitaja mwenyewe mara nyingi kuwa ndiye “Mhubiri.” Jina hili “Mhubiri” linaonekana kuwa ndilo linalofaa kukitambulisha kitabu hiki. Neno “Mwalimu” lililotumika katika tafsiri ya Agano la Kale ya Kiyunani “Septuagint” ndilo linalofanana na hili. Kitabu cha Mhubiri kinachunguza maana ya maisha.

Mwandishi

Solomoni.

Kusudi

Kusudi la kitabu hiki ni kuchunguza maisha kwa ujumla wake na kufundisha kwamba upembuzi wa mwisho unaonyesha kuwa maisha hayana maana, yaani ni ubatili, bila kumheshimu na kumcha Mungu kikamilifu.

Mahali

Yerusalemu.

Tarehe

Kama mwaka wa 935 K.K.

Wahusika Wakuu

Solomoni.

Wazo Kuu

Ili kuelewa maisha na kufanya uamuzi ulio sawa, binadamu anahitaji hekima ambayo inapatikana kwa kumjua Mungu pekee.

Mambo Muhimu

Kuonyesha jinsi kufuata starehe maishani kunaweza kuleta udanganyifu wa dhambi na kutukosesha utoshelevu na furaha. Chanzo cha furaha, mafanikio na utoshelevu ni kumcha Mungu na kuzishika amri zake. Kama mtu yeyote ataishi na Mungu daima, basi kumtii Mungu ndio njia pekee ya kufanikiwa katika maisha ya hapa duniani.

Mgawanyo

Maisha ni ubatili kabisa (

1:1-11

)

Kikomo cha hekima (

1:12–2:26

)

Wakati kwa kila jambo (

3:1-22

)

Ugumu wa maisha na kumcha Mungu (

4:1–5:20

)

Maudhi na kutosheka (

6:1–8:17

)

Maisha ni lazima yatawaliwe na hekima (

9:1–10:20

)

Hekima ya kweli ni kumcha Mungu (

11:1–12:14

).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *