Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 5

Amri Kumi

1 Mose akawaita Israeli wote, akawaambia:

Ee Israeli, sikilizeni amri na sheria ninazowatangazia leo. Jifunzeni, na mwe na hakika kuzifuata.

2 BwanaMungu wetu alifanya Agano nasi katika mlima wa Horebu.

3 Si kwambaBwanaalifanya Agano na baba zetu, bali alifanya nasi, nasi sote ambao tuko hai hapa leo.

4 Bwanaalisema nanyi uso kwa uso kutoka moto juu ya mlima.

5 (Wakati huo nilisimama kati yaBwanana ninyi kuwatangazia neno laBwana, kwa sababu mliogopa ule moto, nanyi hamkupanda mlimani.) Naye Mungu alisema:

6 “Mimi ndimiBwanaMungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.

7 Usiwe na miungu mingine ila mimi.

8 Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji.

9 Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi,BwanaMungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,

10 lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu.

11 Usilitaje bure jina laBwanaMungu wako, kwa kuwaBwanahataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure.

12 Adhimisha siku ya Sabato na kuiweka takatifu, kamaBwanaMungu wako alivyokuagiza.

13 Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote.

14 Lakini siku ya Saba ni Sabato kwaBwana, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au mtumishi wa kike, wala ngʼombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliyeko malangoni mwako, ili kwamba mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe.

15 Kumbuka mlikuwa watumwa huko Misri, naBwanaMungu wenu aliwatoa huko kwa mkono wenye nguvu na kwa mkono ulionyooshwa. Kwa hiyoBwanaMungu wako amekuagiza kuiadhimisha siku ya Sabato.

16 Waheshimu baba yako na mama yako, kamaBwanaMungu wako alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchiBwanaMungu wako anayokupa.

17 Usiue.

18 Usizini.

19 Usiibe.

20 Usimshuhudie jirani yako uongo.

21 Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ngʼombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.”

22 Hizi ndizo amri alizozitangazaBwanakwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenu lote huko mlimani kutoka kwenye moto, wingu na giza nene, wala hakuongeza chochote zaidi. Kisha akaziandika juu ya vibao viwili vya mawe, naye akanipa mimi.

Woga Wa Watu Mlimani

23 Mliposikia sauti kutoka kwenye giza, mlima ulipokuwa ukiwaka moto, viongozi wenu wote wa makabila yenu na wazee wenu walinijia mimi.

24 Nanyi mkasema, “BwanaMungu wetu ametuonyesha utukufu na enzi yake, nasi tumesikia sauti yake kutoka kwenye moto. Leo tumeona kwamba mwanadamu anaweza kuishi hata kama Mungu akizungumza naye.

25 Lakini sasa, kwa nini tufe? Moto huu mkubwa utatuteketeza sisi na tutakufa kama tukiendelea kusikia sauti yaBwanaMungu wetu zaidi.

26 Ni mtu yupi mwenye mwili ambaye amewahi kuisikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza kutoka kwenye moto, kama sisi tulivyoisikia, naye akaishi?

27 Sogea karibu usikie yale yote asemayoBwanaMungu wetu. Kisha utuambie chochote kile ambachoBwanaMungu wetu anakuambia. Tutasikiliza na kutii.”

28 Bwanaaliwasikia wakati mlipozungumza nami, naBwanaakaniambia, “Nimesikia kile hawa watu walichokuambia. Kila kitu walichokisema ni kizuri.

29 Laiti kama mioyo yao ingekuwa na mwelekeo wa kuniogopa na kuzishika amri zangu zote daima, ili kwamba wafanikiwe wao pamoja na watoto wao milele!

30 “Nenda uwaambie warudi kwenye mahema yao.

31 Lakini wewe baki hapa pamoja nami ili niweze kukupa maagizo yote, amri na sheria ambazo utawafundisha wazifuate katika nchi ninayokwenda kuwapa waimiliki.”

32 Hivyo kuweni waangalifu kuyafanya yaleBwanaMungu wenu aliyowaagiza; msigeuke upande wa kuume wala wa kushoto.

33 Fuateni yale yote ambayoBwanaMungu wenu aliwaagiza, ili mpate kuishi, kustawi na kuziongeza siku zenu katika nchi mtakayoimiliki.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/5-334568423215b2ac8113821ad2320506.mp3?version_id=1627—

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *