Categories
Kumbukumbu

Kumbukumbu 23

Kutengwa Na Mkutano

1 Asiingie mtu yeyote aliyehasiwa kwa kupondwa makende au kwa kukatwa uume wake katika kusanyiko laBwana.

2 Mtu yeyote ambaye amezaliwa kwenye ndoa isiyo halali au wazao wake wasiingie kwenye kusanyiko laBwana, hata mpaka kizazi cha kumi.

3 Hapatakuwa na Mwamoni au Mmoabu au yeyote wa wazao wao atakayeruhusiwa kuingia katika kusanyiko laBwana, hata mpaka kizazi cha kumi.

4 Kwa kuwa hawakuja kuwalaki wakiwa na mkate na maji mlipokuwa njiani mlipotoka Misri, tena walimwajiri Balaamu mwana wa Beori kutoka Pethori iliyoko Aramu-Naharaimuili kuwalaani ninyi.

5 Hata hivyo,BwanaMungu wenu hakumsikiliza Balaamu bali aligeuza laana kuwa baraka kwenu kwa sababuBwanaMungu wenu anawapenda.

6 Msitafute mapatano ya urafiki nao maisha yenu yote.

7 Usimchukie Mwedomu, kwa kuwa yeye ni ndugu yako. Usimchukie Mmisri, kwa sababu uliishi kama mgeni katika nchi yake.

8 Kizazi cha tatu cha watoto watakaozaliwa nao wanaweza kuingia katika kusanyiko laBwana.

Unajisi Katika Kambi

9 Unapokuwa umepiga kambi dhidi ya adui zako, jitenge na kitu chochote kisicho safi.

10 Ikiwa mtu amechafuka kwa sababu ya kutokwa na shahawa usiku, inampasa atoke nje ya kambi na kukaa huko.

11 Lakini jioni ikikaribia ataoga, na baada ya jua kuzama ataingia tena kambini.

12 Tengeni mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda kujisaidia.

13 Kama sehemu ya vifaa vyenu kuweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho.

14 Kwa kuwaBwanaMungu wenu hutembea katika kambi yenu ili kuwalinda na kuwaweka adui zenu mikononi mwenu. Kambi yenu ni lazima iwe takatifu, ili asione kitu chochote miongoni mwenu kilicho kichafu akageuka na kuwaacha.

Sheria Mbalimbali

15 Ikiwa mtumwa amekimbilia kwako, usimrudishe kwa bwana wake.

16 Mwache aishi miongoni mwenu mahali popote anapopapenda na katika mji wowote anaochagua. Usimwonee.

17 Asiwepo Mwisraeli mwanamke kahaba au mwanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.

18 Kamwe usilete mapato ya ukahaba ikiwa ni ya mwanamke au ni ya mwanaume katika nyumba yaBwanaMungu wako kwa ajili ya nadhiri yoyote, kwa sababuBwanaMungu wako anachukizwa na yote mawili.

19 Usimtoze ndugu yako riba, iwe ni fedha ama chakula ama kitu kingine chochote ambacho waweza kupata riba juu yake.

20 Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili kwambaBwanaMungu wako akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoingia kuimiliki.

21 Ukiweka nadhiri kwaBwanaMungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwaBwanaMungu wako atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi.

22 Lakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia.

23 Chochote kitakachotamkwa kwa midomo yako ni lazima uhakikishe umekifanya, kwa sababu uliweka nadhiri yako kwa hiari mbele zaBwanaMungu wako kwa kinywa chako mwenyewe.

24 Kama ukiingia katika shamba la mizabibu la jirani yako, unaweza kula zabibu kadiri utakavyo, lakini usiweke chochote kwenye kikapu chako.

25 Kama ukiingia katika shamba la nafaka la jirani yako, unaweza kukwanyua kwa mikono yako, lakini usikate kwa mundu nafaka iliyosimama.

—https://api-cdn.youversionapi.com/audio-bible-youversionapi/337/32k/DEU/23-53383c563ac1f5e66e79b39871b3173e.mp3?version_id=1627—

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *