Categories
Hosea

Hosea Utangulizi

Utangulizi

Hosea mwana wa Beeri alikuwa mzaliwa wa Ufalme wa Kaskazini, yaani, Israeli, ambao pia anauita Efraimu. Maana ya jina lake ni “Wokovu.” Inawezekana alianza huduma yake kabla ya kifo cha Mfalme Yeroboamu wa Pili mwaka wa 753 K.K. Huduma ya Hosea kwa Ufalme wa Kaskazini ilikaribiana sana na ile ya Amosi. Hawa wawili ndio manabii pekee wa Agano la Kale ambao vitabu vyao vilihusu Ufalme wa Kaskazini na maangamizi yake.

Hosea alipoanza huduma yake katika miaka ya baadaye ya utawala wa Yeroboamu wa Pili, Israeli ilikuwa inafurahia ustawi mkubwa wa kiuchumi na amani ya kisiasa iliyosababisha kuwepo kwa usalama pande zote. Mara baada ya kufa kwa Yeroboamu wa Pili mwaka 753 K.K., taifa lilianza kuharibika kwa haraka, na hatimaye likaangamia, nao Waisraeli wakapelekwa utumwani na Waashuru mwaka 722 K.K.

Mwandishi

Hosea mwana wa Beeri.

Kusudi

Kiini cha ujumbe wa Hosea ni kuonyesha upendo wa Mungu kwa watu wa Israeli waliogeuka na kumwacha Bwana.

Mahali

Ufalme wa Kaskazini (Israeli), ambao nabii anauita Efraimu.

Tarehe

715 K.K.

Wahusika Wakuu

Hosea, Gomeri, na watoto wao.

Wazo Kuu

Uhusiano wa Mungu na Israeli uliokuwa umefifia.

Mambo Muhimu

Hosea anaelezea hali ya taifa la Israeli akitumia hali iliyojitokeza katika maisha ya kila siku. Mungu anafananishwa na: mume, baba, simba, chui, dubu, umande, mvua, nondo, n.k. Israeli inafananishwa na: mke aliyekosa uaminifu kwa mumewe, mtu mgonjwa, mzabibu, mzeituni, mwanamke anayejifungua, jiko la kuokea, ukungu wa asubuhi, makapi, moshi, n.k.

Mgawanyo

Maisha ya Hosea katika familia (

1:1–3:5

)

Hali ya dhambi ya Israeli (

4:1–6:3

)

Adhabu kwa ajili ya Israeli (

6:4–10:15

)

Hukumu ya Mungu na rehema zake (

11:1–14:9

).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *