Categories
2 Wathesalonike

2 Wathesalonike Utangulizi

Utangulizi

Waraka huu uliandikwa miezi michache tu baada ya ule wa kwanza. Baadhi ya watu walikuwa wamemwelewa vibaya Paulo, au waraka mwingine wa bandia uliosemekana kuwa ulitoka kwa Paulo ulikuwa umewafadhaisha Wathesalonike kuhusu kurudi kwa Yesu. Paulo aliandika waraka huu ili kuwakumbusha yale aliyokuwa ametangulia kuwafundisha, akiwahakikishia waumini kuwa Kristo atarudi kuwafariji waliomwamini na kuwaadhibu wale waliokuwa wakiwatesa. Aliwaambia kwamba siku ya Bwana, yaani siku ya hukumu, haitawafikia mara moja, bali itatanguliwa na matukio mbalimbali. Wakifahamu kuwa hakika Kristo atarudi, basi iliwapasa waumini kuishi maisha matakatifu yasiyo na lawama.

Mwandishi

Mtume Paulo.

Kusudi

Kuondoa mkanganyiko kuhusu kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili.

Mahali

Korintho.

Tarehe

Kati ya 51-52 B.K.

Wahusika Wakuu

Paulo, Silvano, na Timotheo.

Wazo Kuu

Kuwafariji Wathesalonike kwa ajili ya mateso, na kuwahimiza waishi maisha ya kumtukuza Mungu.

Mambo Muhimu

Kuja kwa Yesu Kristo mara ya pili, na kuwaonya waumini wasiache kufanya kazi.

Mgawanyo

Faraja kutokana na kurudi kwa Kristo (

1:1-12

)

Matukio kabla ya kuja kwa siku ya Bwana (

2:1-12

)

Maagizo zaidi na maonyo (

2:13–3:5

)

Mausia ya Kikristo, na kuwatakia heri (

3:6-18

).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *